Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

KAMISHNA MKUU WA TRA ATEMBELEWA NA BALOZI WA SERIKALI YA JAMHURI YA KOREA KUSINI NCHINI TANZANIA

$
0
0
Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Bw. Song Geum - Young (wa pili kushoto) akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (kulia) alipomtembelea Kamishna huyo ofsini kwake mapema leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kodi katika uwekezaji na biashara. Kulia ni Bw. Tiger Lee (Seung - Hoon) kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (kulia) akizungumza na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Bw. Song Geum - Young (wa pili kushoto) alipomtembelea Kamishna huyo ofsini kwake mapema leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kodi katika uwekezaji na biashara. Kulia ni Bw. Tiger Lee (Seung - Hoon) kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania.
Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Bw. Song Geum - Young akimkabidhi zawadi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere alipomtembelea Kamishna huyo ofsini kwake mapema leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kodi katika uwekezaji na biashara. Wa kwanza kushoto ni Bw. Tiger Lee (Seung - Hoon) kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania na wa kwanza kulia ni Bw. Said Athumani, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango wa TRA.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania Bw. Song Geum - Young wakipeana mikono baada ya kumaliza mazungumzo wakati Balozi huyo alipomtembelea Kamishna Mkuu ofsini kwake mapema leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya kodi katika uwekezaji na biashara. Wa kwanza kulia ni Bw. Said Athumani, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango wa TRA. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO). 

WIZARA YA AFYA YAMWAGA AJIRA 8,000 SEKTA YA AFYA NCHINI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
                                                                                            
  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali cha Ajira kwa sekta ya afya nchini cha kuwaajiri wataalam wa kada mbalimbali za Afya wapatao 8,000.

Hayo ya mesemwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.

Dkt. Mpoki amesema wamepata kibali hicho kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kuongeza kwamba Wizara yake inalo jukumu la kuwapangia vituo vya kazi waombaji wenye sifa kwa mujibu wa waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Umma Namba 1 wa mwaka 2009 kuhusu miundo ya utumishi wa kada za afya chini ya Wizara ya Afya.

Aidha, alisema kibali hicho chenye aina mbili za mwajiri ikiwepo nafasi 6,180 ambazo zimeenda Hospitali zilizo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati. Nafasi 1,820 zimeenda Hospitali zilizo chini ya Wizara ya Afya, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Wizara zingine na Taasisi za Umma pamoja na Hospitali ya Mlongazila na Benjamini Mkapa.

Alitaja sifa za waombaji wa nafasi hizo kuwa, awe raia wa Tanzania, umri usiozidi miaka 45, asiwe mwajiri wa Serikali au mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali na asiwe ameshawahi kufanya kazi Serikalini na kuacha kazi.Hata hivyo, Dkt. Mpoki amewakumbusha wataalam hasa wale wanaosajiliwa na mabaraza ya kitaaluma kuambatanisha nakala za usajili au leseni ya kufanya kazi ya taaluma husika wakati wa maombi hayo.

Katibu Mkuu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na kueleza kuwa nafasi hizi 8,000 ni juhudi za Serikali za kupunguza uhaba wa rasilimali watu katika sekta ya afya. 

Imetolewa na : 
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya 
11/5/2018

BALOZI WA KUWAIT AZINDUA KISIMA CHA MAJI KATIKA SHULE YA IBNU JAZAR

$
0
0
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem amezindua kisima cha maji safi na salama katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar iliyopo Vikindu Mkoa wa Pwani. Katika hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Picha ya Ndege Mjini Nassoro Ruhulo, Diwani Mstaafu wa Vikindu Al-Hajj Abdalla Bofu pamoja na walimu na wanafunzi wa Shule hiyo.

Katika hotuba yake fupi mara baada ya ufunguzi wa kisima hicho Mhe. Balozi amesema kuwa kisima hicho ni cha 62 tangu Ubalozi uzindue mradi uliopewa jina la "KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE.

Pia Balozi Al-Najem alikagua madarasa ya Shule, maabara ya Fizia na kituo cha Kompyuta katika Shule ya Ibnu Jazar ambapo aliahidi kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili Shule ikiwa ni hatua ya kuunga mkono sera za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Magufuli katika sekta ya elimu nchini. Shule ya Ibnu Jazar ina idadi ya wanafunzi zaidi ya 800.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al-Najem akizindua kisima cha  safi na salama katika Shule Ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar iliyopo Vikindu Mkoa wa Pwani.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al-Najem akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule Ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar mara baada ya kuzindua kisima cha  safi na salama shuleni hapo
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al-Najem akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kisima cha  safi na salama katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar iliyopo Vikindu Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar wakimsikiliza Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem alipofika shuleni hapo kuzindua  kisima cha  safi na salama shuleni hapo.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al-Najem akikagua maabara ya Fizia na kituo cha Kompyuta kwenye Shule ya Ibnu Jazar iliyopo mkoani Pwani.

MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2

$
0
0
Na Octavian Kimario
Mapato yanayotokana na utalii yameongezela kutoka Dola za Marekani Bil. 1.7 mwaka 2012 hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 2.2 mwaka 2017 ambapo ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka 1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,327,143 mwaka 2017.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi A. Kigwangalla alipokuwa akifungua Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018.

" Wote tunaelewa ya kuwa Utalii ni moja wapo ya sekta zinazokua kwa kasi na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kupunguza umasikini wa kipato. Sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni (foreign exchange earnings)," alisema Dkt. Kigwangalla.

Aidha amesema, mafanikio ya Sekta ya Utalii yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 na juhudi za Serikali  kutekeleza Sera hiyo kwa ushirikiano na wadau katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za utalii, utangazaji katika masoko mbalimbali ya utalii duniani na mazingira bora ya uwekezaji.

Dkt. Kigwangalla ametaja masuala ambayo yametiliwa mkazo katika  Sera hiyo kuwa ni pamoja na Serikali kuendelea kushirikiana na wadau wote wa utalii katika kuhifadhi rasilimali za utalii, kuendeleza rasilimali watu, kuimairisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa,  kuimarisha mnyororo wa thamani katika mazao ya utalii pamoja na kuongeza wigo wa mazao ya utalii (kama vile kuendeleza utalii wa fukwe na utalii wa mikutano).

Vile vile kuweka mkazo katika kutangaza Tanzania kama kituo bora cha utalii kimataifa,  kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji,  pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani na kuendelea kusimamia viwango vya ubora wa huduma za malazi nchini.

" Mtakubaliana nami kuwa, leo tunayo kazi kubwa iliyopo mbele yetu, hivyo ni vema kuweka mawazo yetu kwa pamoja katika kipindi cha masaa machache yajayo na kuibuka na maboresho kwa ajili ya rasimu hii ya Sera kwa mustakabali wa sekta ya Utalii nchini," alifafanua Dkt. Kigwangalla.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mej. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza na Washiriki wa warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Warsha hiyo leo Jijini Dodoma.
  Waziri wa Maliaasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Washiriki wa warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 wakati alipofungua Warsha hiyo leo Jijini Dodoma.
  Washiriki wa warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 wakimsikiliza Waziri wa Maliaasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (hayupo pichani) alipofungua Warsha hiyo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliaasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara, Wadau wa Sekta ya Utalii na Washiriki wa Warsha ya Kitaifa ya Mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 2018 wakati alipofungua Warsha hiyo leo Jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MSHANA AILEZA MAHAKAMA ALIVYOSHTUKA ALIPOPOKEA TAARIFA YA BV1 ILIYODAI TBC IMEWASABABISHIA HASARA

$
0
0
*Ni katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC Tido Mhando

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana  ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, alishtuka alipopokea taarifa ya usuluhishi(notice of arbitration) kutoka Channel 2 Group Corporation (BV1) iliyopo Uingereza wakidai TBC imewasababishia hasara.

Mshana amedai taarifa hiyo ilimshtua kwa kuwa waliwaahidi kuwapatia kazi ya kuhamisha urushaji wa matangazo ya televisheni  kutoka mfumo wa analojia kwenda digitali.

leo, mbele ya Hakimu Huruma Shaidi wa Mahakama hiyo wakati akitoa ushahidi wake kama shahidi watatu wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Tido

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887.1.

Akizungumza na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, Mshana amedai kuwa, Mei 28 mwaka 2012 walipokea madai ya usuluhishi (Notice of arbitration) yanayohusisha kampuni kudaiwa  pesa nyingi na walipewa siku 28 ty lazima TBC iwe imejibu madai hayo.

Alidai aliwasiliana na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TBC kuuliza kama wanajua juu ya taarifa hiyo au kama waliwahi kupitisha suala hilo lakini naye alionekana hakufahamu mkataba huo  ulioingiwa na Tido na  Channel 2 Group Corporation (BV1) .

Mshana aliendelea kudai Mwenyekiti wa bodi alielekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo aandikiwe barua pengine analifahamu suala hilo la mkataba ambapo alidai kuwa Wizara hiyo ya Habari ilimwandikia mwanasheria wa Serikali  (AG) kuliangalia hilo suala na kutoa ushauri wa kisheria na maelekezo.

"Nakumbuka Wizara ikitoa maelekezo kwa bodi ya wakurugenzi ya TBC  iitishe kikao na kujali na kutoa mapendekezo na kwamba Wizara ilitaka kujua zaidi huo mkataba,"amedai.

Alidai kuwa kulikuwepo na Mawasiliano kati ya TBC, Mwanasheria Mkuu(AG) na Wizara kwa sababu unapotakiwa kuingia mkataba ni lazima ipate ridhaa ya AG. Alidai kuwa Msajili wa Hazina naye alifahamishwa kwa sababu yeye ndiyo amepewa dhamana na mali ya shirika pamoja na Wizara ya fedha ambayo ni mtoa fedha.
Aliendelea kutoa ushahidi Katika kesi huyo Mshana alidai kuwa AG aliagiza ateuliwe mwanasheria aliyepo nchini Uingereza kusimamia suala hilo la usuluhishi kwa niaba ya Serikali na ikateuliwa kampuni ya uwakili ya Freshfield Bruckhaus Derringer us  LLP .
Kampuni hiyo gharama zao zilikuwa zikilipwa kwa muda ambapo walilipwa zaidi ya Sh 887 milioni.
Alibainisha kuwa kutokana na mchakato huo TBC ilipata hasara kwa kulazimika kulipa kiasi hicho cha fedha kwa kampuni hiyo ya uwakili walioitetea TBC fedha ambayo ingeweza kutumika katika kuleta maendeleo mengine
Kwani imewasababishia kukosa faida ambayo wangeipata iwapo wangewekeza katika kuhamisha urushaji wa matangazo ya Televisheni kutoka mfumo wa analojia kwenda digital.

Kesi imeahirishwa hadi Mei 18,2018. Katika kesi hiyo Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali  hasara ya ya 887,122,219.19.

OFISA MAUZO KAMPUNI YA AGGREY &CLIPFORD KORTINI KWA TUHUMA ZA TAARIFA ZA UCHOCHEZI KUPITIA MTANDAO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
OFISA Mauzo wa Kampuni ya Aggrey&Clipford, Razack Hamad (26) amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kijubu shtaka  la kuchapisha taarifa za uchochezi kupitia mtandao wake wa Telegram.
Razack ambaye ni mkazi wa Mbezi Juu jijini Dar es Salaam amesomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi, Martha Mpazi.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Razack anakabiliwa na shtaka moja  la kuchapisha taarifa ya uchochezi kinyume na kifungu cha 53(1)(c) na 52(1)(a) cha sheria ya habari namba 12 ya mwaka 2016.

Akisomewa shtaka lake imedaiwa,  Machi 9 mwaka huu mshtakiwa Razack akiwa jijini Dar es Salaam alitumia mfumo wa kompyuta katika simu yake kupitia mtandao wake wa Telegram kwa kuandika;

"Nimepata wazo kwa group jingine huko tunaweza kukwepa garama pia kuandika hata kwenye kuta za wazi #April 26 Magufuli Out, pinga Dictator" Maneno ambayo yangeibua chuki kwa Watanzania.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda shtaka hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 24 mwaka huu.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na mshtakiwa amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini 2 watakaosani bondi ya Sh.milioni 5.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Aggrey&Clipford, Razack Hamad (aliyevaa sweta) akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa shtaka  la kuchapisha taarifa za uchochezi kupitia mtandao wake wa Telegram nyuma akisindikizwa na askari.

INTRODUCING TUNDA MAN - MAMA (Official Video)

Waziri wa Nishati azindua Baraza la Kwanza la Wizara ya Nishati

$
0
0
Atoa maagizo mbalimbali
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua Baraza la Kwanza la  Wizara ya Nishati na kutoa maagizo mbalimbali kwa Watendaji wa Wizara na Taasisi ili  Sekta ya Nishati iendelee kuwa injini katika ukuaji wa uchumi.
Dkt. Kalemani amezindua Baraza hilo tarehe 11 Mei, 2018 mkoani Dodoma ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria uzinduzi huo akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye alimwakilisha Katibu wa TUGHE Taifa na Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya.
Akizungumza na Wajumbe wa Baraza, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Wajumbe wa TUGHE, Tawi la Wizara ya Nishati, Dkt. Kalemani alisema kuwa, jukumu kuu la Wizara na Taasisi zake ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nishati ya umeme ya kutosha hivyo wana jukumu la kutafakari namna ya kutekeleza suala hilo.
Dkt. Kalemani, aliwaagiza watendaji wa Wizara na Taaisi kuhakikisha kuwa kunakuwepo na miundombinu ya kutosha ya kusafirisha umeme ili umeme unaozalishwa uweze kuwafikia wananchi kwani kuna sehemu ambazo umeme umekuwa ni mwingi kuliko matumizi ya nishati hiyo.
Aidha, Dkt Kalemani aliwataka watendaji hao kuhakikisha kuwa, wananchi waliolipia huduma ya umeme,  wanaunganishwa na huduma hiyo ndani ya wakati ambao ni siku Saba.
Vilevile Dkt. Kalemani, alisema kuwa, kila mtendaji ana jukumu la kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa pili kushoto), Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye ni mwakilishi wa Katibu wa TUGHE Taifa (wa kwanza kulia),  Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya (wa kwanza kushoto) na Katibu Mpya wa Baraza la Wafanyakazi, Wizara ya Nishati, Pascal Mduma (wa pili kulia) wakiimba wimbo wa Mshikamano wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika mjini Dodoma.
 Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Nishati wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.
 Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake wakiimba wimbo wa Mshikamano katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.
 Watendaji kutoka Idara ya Utawala na Rasilimali Watu na Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Nishati wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti (waliosimama) iliyoandaa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati kilichofanyika mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua na kushoto kwake ni Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


POLISI KANDA MAALUM DAR YAWASHIKILIA WATU 10 KWA TUHUMA ZA WIZI WA KUTUMIA SILAHA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka, Globu ya jamii
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa  amesema hali ya usalama ya Jiji hilo ni shwari  huku akielezea matukio kadhaa ambayo yametokea katika kukabiliana na matukio ya uhalifu.

Mambosasa amezungumza leo jijini Dar es Salaam ambapo ameelezea pia kukamatwa kwa watu 10 wanaotuhumiwa kwa ujambazi wa kutumia silaha.

Amewataja watuhumiwa hao ni Bushiri Ally (29) mkazi wa Tandika, Mohamed Ismaili (18) mkazi wa Tandika, Issa Saidi (19) mkazi wa Yombo, Mlekwa Ally (18) mkazi wa Tandika, Shabani Nassoro (17) mkazi wa Tandika, na watano wengine ambao majina yao wameyahifadhi kwa sababu za kiupelelezi.

Mambosasa amesema Aprili 29 mwaka huu, saa sita usiku katika maeneo ya Tandika Foma askari wakiwa doria waliitilia shaka gari namba T 401 CLF aina ya Toyota Alteza rangi ya fedha na kuanza kulifuatilia kisha kulikamata na kukuta watu watano wakiwa ndani ya gari hilo.

Amefafanua askari waliwaweka chini ya ulinzi watu hao na kufanya upekuzi ndani ya gari hilo na kufanikiwa kukamata  Bastola aina ya Browning yenye namba N635BRE ikiwa na risasi mbili ndani ya Magazine ikiwa na Watuhumiwa waliokamatwa kwenye gari hiyo ni Bushiri Ally (29) mkazi wa Tandika, Mohamed Isimaili (18) mkazi wa Tandika, Issa  Saidi (19) mkazi wa Yombo, Mlekwa Ally (18) mkazi wa Tandika na Shabani Nassoro (17) mkazi wa Tandika.

"Watuhumiwa hao walihojiwa na mtumiwa mmoja Bushiri Ally alikiri bastola hiyo ni ya kwake na aliiokota Tandika mtaa wa Mteja mwaka 2014 na huwa anaitumia kufanyia vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji,"amesema.

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kukutwa na Bastola 2 na risasi 16, nyundo moja na bisisi  tatu ambavyo walikuwa wakivitumia katika matukio mbalimbali ya uhalifu wa wizi wa magari hapa Jijini.
Amesema watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na operesheni kali inayoendelea kufanyika dhidi ya wezi wa magari na wahalifu wanaotumia silaha.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akionesha silaha mbalimbali zilizo kamatwa na Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali  jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari leo juu kukamatwa kwa watuhumiwa kumi kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BODI YA MIKOPO YAFAFANUA KUHUSU UMILIKI WA LESENI ZA BIASHARA KWA WAZAZI SIO SIFA YA MWANAFUNZI WA ELIMU YA JUU KUKOSA MKOPO

$
0
0
Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo za kweli zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa waombaji wa mikopo ambao wazazi wao wanamiliki leseni za biashara hawatapata mikopo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2018/2019. Taarifa hizo sio sahihi na zinapotosha waombaji mikopo na umma kwa ujumla.

Ufafanuzi wa kina ni kama ifuatavyo:

a)   Mikopo inayotolewa na Serikali kupitia HESLB inaongozwa na Sheria ya HESLB (SURA 178) pamoja na Mwongozo unaotaja sifa, vigezo na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo. Mwongozo huu unapatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) na hautaji kigezo cha umiliki wa leseni kama sifa ya kukosa mkopo;

b)   Pamoja na mwongozo huu, HESLB pia imeandaa kitabu kwa lugha nyepesi ya kiswahili chenye Maswali na Majibu 21 ili kuwawezesha waombaji mikopo kufahamu sifa na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo kwa ukamilifu na usahihi. Kitabu hiki pia hakijataja umiliki wa leseni kwa mzazi au mlezi kama sifa ya mwanafunzi kukosa mkopo;

c)    HESLB inaamini umiliki wa leseni ya biashara kwa wazazi ni jambo jema na linapaswa kupongezwa kwa kuwa linaimarisha mifumo ya utambuzi kwa wafanyabiashara.

Bodi ya Mikopo inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wazazi, walezi na wanafunzi waombaji wa mikopo kusoma kitabu cha mwongozo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 na kitabu chenye maswali 21 ambavyo vinapatikana katika tovuti (www.heslb.go.tz).

Vitabu hivi ndiyo nyaraka rasmi za HESLB zinazotoa mwongozo kuhusu maombi ya mikopo kwa mwaka 2018/2019. Aidha, HESLB inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wanahabari, kusoma nyaraka hizo na kutumia kalamu na kamera kuwaelimisha waombaji mikopo kwa usahihi.



Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM

DC SOPHIA MJEMA AHIMIZA WATUMISHI ILALA KUCHAPA KAZI, AZINDUA KAMPENI YA UJENZI WA CHOO CHA MTOTO WA KIKE

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema amewahimiza watumishi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii huku akisisitiza kwake ni kazi tu kama kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano inavyohimiza watu kufanya kazi.

Mbali ya kuhimiza watumishi wa Wilaya ya Ilala kufanya kazi Mjema amezindua rasmi kampeni ya ujenzi wa choo cha mtoto wa kike katika wilaya hiyo kwa shule zote za msingi ambapo amesema yeye binafsi anaunga mkono kampeni hiyo kwa kujenga choo cha matundu sita huku akiahidi kuhamasisha wadau wa maendeleo kusaidia ujenzi huo.

Mjema amesema hayo leo mbele ya Watumishi Wanawake wa Manispaa ya Ilala ambao wamekuwa na utamaduni wa kila mwaka siku kama ya leo kukutana na kufanya tathimini ya utendaji kazi wao na kwa mwaka huu wameamua kuhamasishana kujenga choo cha mtoto wa kike ambacho kitakuwa rafiki na kumsaidia mtoto wa kike kupata nafasi ya kujisitiri hasa wakati anapokuwa kwenye hedhi baada ya kubaini kwa sasa wanafunzi hasa wa darasa la saba kuwa na wakati mgumu kutokana na mazingira ya vyoo vilivyopo shuleni kutokuwa rafiki kwao.

"Tumekutana leo moja ya lengo kuu ni kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike wa Wilaya ya Ilala ambaye tunaamini ndio atakuwa mtumishi wa wilaya yetu kwa siku zijazo.Hivyo lazima mtoto huyu tumuangalie na kutatua changamoto zake anapokuwa shuleni.Nimezindua kampeni hii ya ujenzi wa choo cha mtoto wa kike kwa lengo la kumuondolea changamoto wanazokutana nazo sasa.

"Binafsi nitajenga choo cha matundu sita na tayari kuna wadau ambao wamejitolea nao kujenga matundu ya vyoo ambavyo vitakuwa na kila kitu muhimu kwa ajili ya mwanafunzi wa kike aliyeko shuleni.Vyoo vitakavyojengwa vitakuwa na kiti chooni, kutakiwa na kioo cha binti kujiangalia na eneo la kufua nguo yake iwapo itatokea bahati mbaya imechafuka,"amefafanua na kuongeza kazi ya ujenzi wa vyoo hivyo itaanza mara moja kwani awamu hii ni ya Hapa Kazi Tu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza wakati akizindua rasmi kampeni ya ujenzi wa Choo cha mtoto wa kike kwa shule za msingi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi Wanawake wa Manispaa ya Ilala wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema leo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa pamoja na Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu(kulia)wakiwa wameshika tuzo ya heshima ya kutambua mchango wa mkuu huyo wa wilaya hasa katika utumishi wake wa kiongozi katika kuitumikia jamii ya Ilala.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VOA Swahili: Duniani Leo Mei 11, 2018

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA LEO MEI 11, 2018

Wizara ya Mambo ya Nje Kushiriki Maadhimisho ya siku ya Afrika

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Grace Mujuma amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi za Afrika wanao wakilisha nchi zao hapa nchini,Mabalozi hao ni kutoka nchi za Namibia na Malawi, pamoja na mambo mengine katika mazungumzo hayo walijadiliana kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Umoja wa Afrika.
Umoja huo ulioanzishwa Mwaka 1963 kwa lengo la kutetea maslahi mbalimbali ya Bara la Afrika, kuongeza umoja zaidi katika kutetea uhuru na kulinda mipaka yake. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Namibia Mhe. Theresia Samaria, akimwelezea Balozi Mujuma (hayupo pichani), namna wanavyotarajia kuadhimisha hafla hiyo kwa hapa nchini, kulia ni Balozi wa Malawi Mhe. Hawa Olga Ndilowe akimsikiliza kwa makini.

Sehemu ya watumishi waliohudhuria mazungumzo hayo, wa kwanza kulia ni Bw. Salvatory Mbilinyi, Bw. Makamba Dahari na mwisho kushoto ni Bi. Zulekha Tambwe .
Mazungumzo yakiendelea.




RAIS MAGUFULI ANAWEKA HISTORIA KUBWA KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI - Jafo

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewaeleza wananchi wa wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera kwamba Rais Dk.John Pombe Magufuli anaweka historia kubwa hapa nchini katika sekta ya afya kwa kuboresha vituo vya afya 208,  ujenzi wa hospitali mpya 67 kwa shilingi Sh.bilion 105  mwaka 2018/2019.


Sambamba hilo, pia ameimarisha bajeti ya dawa kutoka sh.Bilioni 31 mwaka 2015 hadi sh. bilioni 269 kwa mwaka 2017/2018. Jafo ameyasema hayo leo hii alipokuwa anaweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya Kayanga wilayani Karagwe ambacho ni miongoni mwa vituo 208 vinavyo boreshwa hapa nchini.


Jafo amesema " Historia inajengwa kwani tulikuwa tuna vituo vya afya 115 vilivyokuwa na uwezo wa kufanya upasuaji toka Uhuru lakini kwa miaka miwili na nusu ya Rais Magufuli vituo 208 vitaweza kufanya upasuaji na hivyo kuwa na jumla ya vituo 323 vitakavyoweza kufanya upasuaji.



"Pia tulikuwa na hospitali 77 pekee tokea uhuru lakini mwaka huu TAMISEMI tumetenga shilingi  bilion 105 kwa kujenga hospitali mpya za wilaya 67 na karagwe ikiwemo,"amesema.



Katika uwekaji wa jiwe hilo la msingi ulihudhuriwa na mamia ya  Wananchi wa wilaya ya Karagwe licha ya kuwepo na mvua.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiweka jiwe la msingi kituo cha Afya Kayanga wilaya ya Karagwe.
 Baadhi ya majengo ya kituo cha Afya Kayanga
 Baadhi ya majengo ya kituo cha Afya Kayanga
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi.

Wataalam wa afya kituo cha Afya Kayanga wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo.



MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA KUTOKA DOLA BIL. 1.7 HADI KUFIKIA DOLA BIL. 2.2 - DKT. KIGWANGALLA

UFAFANUZI: UMILIKI WA LESENI ZA BIASHARA WA WAZAZI SIO SIFA KUKOSA MKOPO ELIMU YA JUU

$
0
0
Abdul-Razaq Badru, Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo za kweli zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa waombaji wa mikopo ambao wazazi wao wanamiliki leseni za biashara hawatapata mikopo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2018/2019. Taarifa hizo sio sahihi na zinapotosha waombaji mikopo na umma kwa ujumla.

Ufafanuzi wa kina ni kama ifuatavyo:

a)   Mikopo inayotolewa na Serikali kupitia HESLB inaongozwa na Sheria ya HESLB (SURA 178) pamoja na Mwongozo unaotaja sifa, vigezo na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo. Mwongozo huu unapatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) na hautaji kigezo cha umiliki wa leseni kama sifa ya kukosa mkopo;

b)   Pamoja na mwongozo huu, HESLB pia imeandaa kitabu kwa lugha nyepesi ya kiswahili chenyeMaswali na Majibu 21 ili kuwawezesha waombaji mikopo kufahamu sifa na utaratibu wa kuwasilisha maombi ya mikopo kwa ukamilifu na usahihi. Kitabu hiki pia hakijataja umiliki wa leseni kwa mzazi au mlezi kama sifa ya mwanafunzi kukosa mkopo;

c)    HESLB inaamini umiliki wa leseni ya biashara kwa wazazi ni jambo jema na linapaswa kupongezwa kwa kuwa linaimarisha mifumo ya utambuzi kwa wafanyabiashara.

Bodi ya Mikopo inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wazazi, walezi na wanafunzi waombaji wa mikopo kusoma kitabu cha mwongozo wa utoaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 na kitabu chenye maswali 21 ambavyo vinapatikana katika tovuti (www.heslb.go.tz).

Vitabu hivi ndiyo nyaraka rasmi za HESLB zinazotoa mwongozo kuhusu maombi ya mikopo kwa mwaka 2018/2019. Aidha, HESLB inapenda kuwakumbusha wadau wote, wakiwemo wanahabari, kusoma nyaraka hizo na kutumia kalamu na kamera kuwaelimisha waombaji mikopo kwa usahihi.

Imetolewa na:

Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

DAR ES SALAAM

RC MNDEME AIFUTIA LESENI KAMPUNI YA ZUMA CARGO KWA UPOTEVU WA TANI 15 ZA KOROSHO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme ameifutia leseni kampuni ya Zuma Cargo kwa upotevu wa tani 15  za korosho ambazo hazijulikani ziliko na kuiagizaTaasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa jambo hilo.

PRECISION AIR YAPANDA MITI 1000 HIFADHI YA TAIFA YA MSITU YA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Shirika la Ndege linaloongoza Tanzania, Precision Air, limeshiriki katika jitihada za kuhifadhi mazingira katika maeneo ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro. 
Katika kutimiza zoezi hilo, wafanyakazi wa shirika hilo wakishirikiana na wanakijiji wa kijiji cha Ngarony pamoja na wafanyakazi wa wilaya ya siha wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Siha Valerian Juwal wamefanikisha upandwaji wa miti 1000 (elfu moja) katika eneo linalotenganisha kijiji cha Ngarony na hifadhi ya mlima Kilimanjaro.

Akizungumzia tukio hilo Meneja Masoko na Mawasiliano wa Precision Air Hillary Mremi amesema, Precision Air inatambua inawajibu wa kutunza mlima Kilimanjaro kwani mlima huo una mchango wa moja kwa moja katika shughulli za shirika hilo. 

“Mlima Kilimanjaro unatutunza vyema sisi kama shirika na kama taifa kupitia utalii, hivyo sote tunawajibu wa kuutunza mlima huu na mazingira kwa ujumla wake.” Mremi alisema.

Precision Air imekua ikifanya safari zake ndani ya mkoa wa  Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka ishirini na nne (24) na kama mdau mmojawapo wa utalii, limefanya zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni moja ya jitihada zake za kuhakikisha jamii inayo uzunguka mlima inaendelea kufaidika na uwepo wa mlima, ambao ni moja ya kivutio muhimu cha utalii nchini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Siha Valerian Juwal amesema kuwa Shirika la Ndege  la Precision Air limeonyesha mfano wa kuigwa na wadau wengine wa mazingira na utalii. 
Na ameongeza kuwa ni wakati sasa wa kuchukua hatua madhubuti kulinda mazingira yetu ili vizazi vijavyo viweze kufaidika na uzuri wa nchi yetu wa vivutio kama mlima Kilimanjaro na vingine.
Afisa Maliasili wa Kata ya Siha Lazaro Mwaluko amesema kuwa Precision Air wamefanya jambo zuri katika tasma nzima ua uhifadhi mazingira pamoja na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali na wananchi kwenye uhifadhi wa msitu huo.
.
Wafanyakazi wa Precision Air wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza zoezi la kupanda  miti 1000 kwenye Hifadhi ya Taifa ya Msitu ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Mkoani Kilimanjaro.
.
 Meneja Masoko na Mawasiliano Hillart Mremi pamoja na Afisa Maliasili wa Kata ya Siha Lazaro Mwaluko wakiotesha mti kandokando ya mto uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Mlima Kilimanjaro.
 Wanakijiji wa Kijiji cha Ngarony kata ya Siha wakiotesha miti kwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Precision Air katika Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Mlima Kilimanjaro (KINAPA) katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za misitu.
 Wafanyakazi wa ndege wa Precision Air wakiwa katika picha ya pamoja na wanakijiji mara baada ya kutoka kupanda  miti 1000 kwenye Hifadhi ya Taifa ya Msitu ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Mkoani Kilimanjaro.



UMOJA WA ULAYA (EU) NA SERIKALI WATANGAZA USHIRIKIANO UFADHILI WA MASOMO YA ELIMU YA JUU ULAYA

$
0
0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiongea na wadau wa Elimu na Utafiti jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2018, wakati wa kutangaza ushirikiano kwenye masuala ya utafiti na sayansi pamoja na fursa za ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kutoka nchi za Umoja wa Ulaya. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Roeland van de Geer alisema Umoja huo una lengo la kufanikisha mpango wa pili wa Maendeleo ya miaka mitano. 

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer akiongea na wadau wa elimu na utafiti wakati wa kutangaza ushirikiano katika utafiti na sayansi kwa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kutoka Umoja huo.

Wadau wa elimu na utafiti wakifuatilia matukio wakati wa kutangazwa ushirikiano kati ya Serikali na EU katika utafiti na sayansi kwa kufadhili masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo nchi za Umoja wa Ulaya.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland van de Geer wakiwa katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki hafla hiyo
Picha zote na Robert Okanda.

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images