Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109936 articles
Browse latest View live

Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa yakagua ujenzi wa shule za sekondari za Ihungo na Nyakato mkoani kagera

$
0
0

Angela Msimbila, Kagera.
Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imeipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri inayoifanya ya kuzijenga upya shule mbili za sekondari za Ihungo na Nyakato ambazo ziliathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwaka 2016.
Kamati hiyo imetoa pongezi hizo leo baada ya kuzitembelea shule hizo na kujionea namna zilivyojengwa upya kisasa. Kamati hiyo ilikuwa katika ziara maalum mkoani Kagera ya kukagua ujenzi wa shule hizo ambazo kukamilika kwake kutawezesha Vijana watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu.
Ujenzi wa shule hizo umegharimu zaidi ya sh.Bilioni 12.6 ambapo kwa shule ya Ihungo ujenzi huo unagharimu Sh.bilioni 10 huku Nyakato ikigharimu Sh.Bilioni 2.6.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo Jasson Rweikiza akiwa na wajumbe wa kamati hiyo, amesema kuwa wameridhishwa na Mradi wa ujenzi wa shule hizo na kuitaka Wakala wa Majengo(TBA) kuhakikisha changamoto ndogondogo zilizopo zinafanyiwa kazi ikiwemo malalamiko ya vibarua kutolipwa fedha zao kwa wakati.

Ameitaka serikali kuhakikisha changamoto hizo zinaisha ili shule hizo ziweze kufunguliwa mapema kabla ya msimu wa masomo ya kidato cha tano kuanza mwaka huu.
Amesema wajibu wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa ni kutatua kero za Wananchi na kuleta maendeleo kwa Taifa.
Naye, Waziri Jafo wameishukuru kamati kwa kutembelea shule hizo sambamba na kuzishukuru Wizara za Elimu, Wizara ya Ujenzi, na Wizara ya Ulinzi kwa kuhakikisha ujenzi wa shule hizo unakamilika. 
Hata hivyo Waziri Jafo ametoa angalizo kwa uongozi wa Mkoa wa Kagera kutoruhusu shule ya Ihungo kwa siku za usoni kugeuzwa kuwa Chuo Kikuu kwa kuwa imejengwa kwa lengo la Vijana wa kidato cha tano na sita.
Aidha, Waziri Jafo wameishukuru serikali ya Uingereza kwa msaada wa sh.Bilioni 10 zilizofanikisha ujenzi wa sekondari ya Ihungo.

 Wajumbe wa Kamati ya Utawala za Serikali za Mitaa wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo walipotembelea kukagua ujenzi wa shule ya sekondari Ihungo.
 Wajumbe wa Kamati ya Utawala za Serikali za Mitaa wakiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo katika shule ya sekondari Nyakato.
 Majengo ya madarasa ya shule ya sekondari Ihungo.
 Majengo ya madarasa ya shule ya sekondari Ihungo.
 Majengo mapya wa shule ya Sekondari ya Nyakato.



WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI

$
0
0
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla amekabidhi magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili.

Magari hayo amewakabidhiwa Wabunge leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma.Wabunge waliokabidhiwa magari hayo ni wa Bunda Vijijini,Boniface Getere ,Itilima,Njalu Silanga ,LongIdo,Dk.Steven Kiruswa,Mbulu Vijijini Flatei Massay,Tanganyika,Moshi Kakoso huku Mbunge wa Ngorongoro,William Ole Nasha yeye hakuweza kufika kutokana na kubanwa na majukumu mengine.

Wabunge hao wamepokea kwa niaba ya Halmashauri hizo.Akizungumza kabla ya kuwakabidhi magari hayo,Dk.Kigwangalla amesema jumla ya Halmashauri 6 zinatarajiwa kunufaika na magari hayo.“Tunakabidhi magari ambapo Halmashauri 6 zitanufaika ambayo yanatokana na jitihada za Waheshimiwa Wabunge kutusumbua sana lakini pia utashi wao katika kuunga mkono katika vita dhidi ya ujangili.

“Lakini pia magari haya yatatusaidia kwenye doria katika maeneo hayo lakini pia ‘kurespond’ haraka kesi za wanyama waharibifu mfano katika maeneo kama kule Bunda Vijijini katika vijiji vya Mugumu na Mgeta kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana wa wanyamapori na makazi ya watu.“Lakini bahati mbaya Halmashauri zinakuwa hazina usafiri wa ‘Kurespond’ haraka kwenda kuwaondoa wale wanyama hivyo tumeona tuwape gari kama kule kwa wahadzabe,Longido tumeona tuwape magari.

“Maeneo kama Itilima hata juzi nilishuhudia kwa masikitiko makubwa watu wawili wakipoteza maisha kwa kuvamiwa na Tembo na Tembo hao walihamia kabisa wakaweka kambi na wamemaliza mazao ya wananchi na wamesababisha vifo.“Tuliona tuzisaidie Halmashauri zetu hivi ili na zenyewe zipate vyombo vya uhakika ili waweze kufika haraka.

Waziri huyo amesema sambamba na makakati huo pia Serikali inakusudia kujenga madungu kwa ajili ya kuangalia wanyama tokea wakiwa mbali ndani ya hifadhi.Pia amesema wanatarajia kuweka uzio wa mizinga ya nyuki ili kuzuia wanyama kama Tembo wasitoke katika maeneo ya hifadhi.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akikabidhi magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla akimkabidhi kadi ya gari Mbunge wa jimbo la Bunda, Boniphace Getere katika hafla ya kutoa magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo na Mbunge wa jimbo la Mbulu vijijini, Flatei Massay mara baada kukabidhiwa gari kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili katika hafla iliyofanyika leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini Dodoma.
Baadhi ya Magari yaliyokikabidhi kwa Wabunge ya Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili katika hafla iliyofanyika leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla akizungumza na Baadhi ya Wabunge wakati akikabidhi magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla akimkabidhi kadi ya gari Mbunge wa jimbo la Longido, Dkt. Steven Kiruswa katika hafla ya kutoa magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma.( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii).



WAZIRI KIGWANGALLA AKABIDHI MAGARI KWA HALMASHAURI 6 KUKABILIANA NA UJANGILI

$
0
0
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla amekabidhi magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili. Magari hayo amewakabidhiwa Wabunge leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma. 
 Wabunge waliokabidhiwa magari hayo ni wa Bunda Vijijini,Boniface Getere ,Itilima,Njalu Silanga ,LongIdo,Dk.Steven Kiruswa,Mbulu Vijijini Flatei Massay,Tanganyika,Moshi Kakoso huku Mbunge wa Ngorongoro,William Ole Nasha yeye hakuweza kufika kutokana na kubanwa na majukumu mengine. 
 Wabunge hao wamepokea kwa niaba ya Halmashauri hizo. Akizungumza kabla ya kuwakabidhi magari hayo,Dk.Kigwangalla amesema jumla ya Halmashauri 6 zinatarajiwa kunufaika na magari hayo. “Tunakabidhi magari ambapo Halmashauri 6 zitanufaika ambayo yanatokana na jitihada za Waheshimiwa Wabunge kutusumbua sana lakini pia utashi wao katika kuunga mkono katika vita dhidi ya ujangili. 
 “Lakini pia magari haya yatatusaidia kwenye doria katika maeneo hayo lakini pia ‘kurespond’ haraka kesi za wanyama waharibifu mfano katika maeneo kama kule Bunda Vijijini katika vijiji vya Mugumu na Mgeta kumekuwa na mwingiliano mkubwa sana wa wanyamapori na makazi ya watu. “Lakini bahati mbaya Halmashauri zinakuwa hazina usafiri wa ‘Kurespond’ haraka kwenda kuwaondoa wale wanyama hivyo tumeona tuwape gari kama kule kwa wahadzabe,Longido tumeona tuwape magari. 
 “Maeneo kama Itilima hata juzi nilishuhudia kwa masikitiko makubwa watu wawili wakipoteza maisha kwa kuvamiwa na Tembo na Tembo hao walihamia kabisa wakaweka kambi na wamemaliza mazao ya wananchi na wamesababisha vifo. 
 “Tuliona tuzisaidie Halmashauri zetu hivi ili na zenyewe zipate vyombo vya uhakika ili waweze kufika haraka. Waziri huyo amesema sambamba na makakati huo pia Serikali inakusudia kujenga madungu kwa ajili ya kuangalia wanyama tokea wakiwa mbali ndani ya hifadhi. 
 Pia amesema wanatarajia kuweka uzio wa mizinga ya nyuki ili kuzuia wanyama kama Tembo wasitoke katika maeneo ya hifadhi. 
 “Wenzetu hawa wa Tanganyika wao wana msitu mzuri wa Tongwe ambao una nyani na tayari tumeishapitisha msitu wa Tongwe uwe hifadhi na utakuwa chini ya Halmashauri hivyo tumeona tuanze kuwajengea uwezo wa usafiri ili waweze kuuendesha. Dk Kigwangalla ametoa angalizo kwa halmashauri zilizopewa magari kuwa yatumike kwa shughuli za maliasili pekee na sio zingine
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla akizungumza na Waandishi wa Habari wakati  akikabidhi magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge  leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini  Dodoma.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla  akimkabidhi kadi ya gari Mbunge wa jimbo la Bunda, Boniphace Getere katika hafla ya kutoa magari kwa  Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge  leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini  Dodoma.
 Baadhi ya Magari  yaliyokikabidhi kwa Wabunge  ya Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili katika hafla iliyofanyika   leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, jijini  Dodoma.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla akizungumza na Baadhi ya Wabunge  wakati akikabidhi magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge  leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini  Dodoma.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamisi Kigwangalla  akimkabidhi kadi ya gari Mbunge wa jimbo la Longido, Dkt. Steven Kiruswa  katika hafla ya kutoa magari kwa Halmashauri 6 kwa ajili ya kupambana na vita dhidi ya ujangili kwa Wabunge  leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini  Dodoma. Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii

Ujenzi wa jengo la maabara kwa Shule ya Sekondari Bulekela wilayani kishapu lakamilika

$
0
0
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi
Wanafunzi wa kike wameaswa kutokuwa bidhaa rahisi kwa kuepuka kurubunika na kujiingiza katika mapenzi hali inayoweza kuwasababisha kupata maradhi na mimba kabla ya wakati. Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ndola Masunga ametoa rai hiyo wakati akikabidhi jengo la maabara kwa Shule ya Sekondari Bulekela lenye thamani ya Sh. milioni 17.13.
Masunga aliwataka wanafunzi kujikita zaidi katika masomo kwa kutumia vizuri maabara hiyo katika masomo ya sayansi kwa vitendo ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.Alisisitiza kuwa ili waweze kufanikiwa wanahitaji kuepuka vishawisishi kutoka kjwa wananume ambao mwisho wa siku wanawakimbia na kuwaachia maradhi na mimba kabla ya wakati.
“Watoto someni kwa bidii haya maisha yapo tu msidanyike na wanaume ambaoi wakiwapa mimba wanawakimbia. Na nyie wavulana msidanyike eti mnaacha shule halafu ili muoe hilo halipo huwezi kuoa wakati huna shughuli ya kufanya, shule inakluongezea maarifa ya maisha,” alisisitiza.
Kwa upande mwingine Masunga ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii aliipongeza Bodi ya Shule na uongozi wake kwa kusimamia vizuri fedha na hatimaye kukamilika kwa mradi huo.Aidha aliwataka walimu na wanafunzi kushikamana ili kuleta ufanisi katikma taaluma na hatimaye kutoa matokeo mazuri huku akiwataka wazazi kuwasimamia vizuri watoto wao na kuhudhuria shuleni bila kukosa.
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Bulekela, Mwalimu C. Chikoti alisema kuwa kazi zote zimefanyika kama ambavyo zilielekezwa kwa kiwango kilichohitajika. Mwalimu Chikoti aliongeza kuwa fedha zilizokuwa zimebaki zilitumika katika shughuli ya upakaji wa rangi majengo mengine ya shule hiyo na kufanya mfanano katika muonekano wake.
Alitaja shughuli zilizofanyika ni pamoja na kuweka masinki ya zege katika vyumba vitatu, kunganisha mfumo wa maji safi, kujenga ngazi kwa kuzingatia mahitaji ya mbalimbali hasa walemavu na kupaki rangi nguzo za maabara. Shughuli nyingine ni kuweka marumaru, kuziba mifereji iliyo inayopitisha maji, kuunganisha mabomba yote kwenye masinki kwa ajili ya kutoa maji taka nje ya maabara pamoja na kuweka dari mpya.    
Ujenzi wa jengo hilo la maabara umefadhiliwa na Serikali kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) huku wananchi wakichangia nguvu kazi katika kuufanikisha.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ndola Masunga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jingo jipya la maabara katika Shule ya Sekondari Bulekela Kata ya Masanga ambalo alililakabidhi tayari kwa matumizi ya kujifunzia masomo ya sayansi.
 Muonekano wa maabara mara baada ya kukamilika tayari kwa matumizi ambapo pichani viongozi mbalimbali wakikagua.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ndola Masunga akitoa nasaha kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bulekela.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Bulekela (kulia) akimkabidhi taarifa ya mradi wa ujenzi wa maabara Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ndola Masunga. Pichani kushoto anayeshuhudia ni Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Paul Kasanda.
Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bulekela Kata ya Masanga wakisikiliza kwa makini nasaha kutoka kwa viongozi wakati wa hafla ya kukabidhiwa jingo la maabara.

BMG MEDIA: Alichobaini RC Mongella baada ya kukagua maghala ya sukari na Mafuta mwanza

RC DKT. KEBWE AZINDUA BODI YA PAROLE YA MKOA WA MOROGORO

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro
MKUU wa Mkoa Morogoro  Dk  Kebwe Stephen  Kebwe amezindua bodi ya parole na kuvitaka vyombo vinavyoshughulikia HAKIJINAI kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa Jeshi la Magereza ili wafungwa wote wanaostahili kunufaika na mpango huo, wanufaike bila kucheleweshwa.
Dk Kebwe alisema hayo katika kwenye kikao cha uzinduzi wa Bodi hiyo kwenye uumbi wa  Magereza Club uliopo kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerera wa Nane Nane , mjini Morogoro. Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wajumbe wote  kutoa ushirikiano wa karibu na Katibu wa Bodi ya Parole Mkoa wa Morogoro ilikufanikisha malengo na makusudi yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria.
Naye Katibu wa Bodi ya Parole Mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Magereza , Mzee Ramadhani Nyamka ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro alieleza kuwa bodi hiyo  ilianzishwa na sheria ya Bodi ya Parole namba 25/1994 na GN. No.563/199. Pia alitaja kuwa , kanuni za Bodi ya Parole zilitangazwa n a kuchapishwa katika gazeti la serikali GN. No. 783/1997  Desemba 26, 1997 .
Hata hivyo alisema  Bodi ya Parole inakabiliwa na changamoto katika utekelezaji wa sheria hiyo na hizo ni pamoja na ugumu wa upatikanaji wa nakala za hukumu kwa wakati kutoka katika mahakama zilizowafunga, taarifa za uhalifu kutoka katika vituo vya Polisi vilivyo wakamata na upatikanaji wa maoni ya waathirika wa matukio.
Nyamka alisema,  mpaka sasa Bodi ya Parole Taifa imeachilia jumla ya wafungwa  177  kutoka katika Magereza Mkoa wa Morogoro, kati ya hao wafungwa 157 wa mekwishamaliza vifungo vyao na wafungwa 20 waliosalia wanaendelea kutumikia adhabu zao katika jamii. 
Katika kikao hicho,  Bodi hiyo  ilifanya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Bodi wa Parole chini ya usimamizi wa Mwenyekiti mteule James   Celestine ambapo wajumbe wa limpendekeza , Wariambora Nkya kuwa makamu mwenyekiti baada ya kukidhi sifa na vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria na kukubaliwa na wajumbe wa Bodi ya Parole. Baada ya uchaguzi huo, wajumbe walijadili na kupendekeza majalada ya wafungwa saba wenye sifa ya kunufaika na mpango huo wa Parole.
 MKUU wa Mkoa Morogoro  Dk  Kebwe Stephen  Kebwe  ( kati kati walioketi) akiwa na wajumbe wa bodi ya parole mkoa wa Morogoro baada ya kuizidua. Kulia ni Katibu wa Bodi ya Parole Mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Magereza , Mzee Ramadhani Nyamka ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro
 Mkuu  wa Mkoa Morogoro  Dk  Kebwe Stephen  Kebwe ( aliyesimama) akizungumza jambo kabla ya kuzindua rasmi  bodi ya parole mkoa wa Morogoro.
Mkuu  wa Mkoa Morogoro  Dk  Kebwe Stephen  Kebwe akiwa katika picha na wajumbe wa  bodi ya parole wa mkoa huo.

AZAM TV: Alichokisema Haji Manara baada ya Ushindi wa Simba Vs Singida.

MICHUZI TV LIVE: Tukio la Mtu aliyenasa kwenye Kontena kwa zaidi ya siku nne eneo la Malindi, Zanzibar


SAFARI YA MWISHO YA ALIYEKUWA MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MAJIRA MAREHEMU KASSIAN NYANDIND

$
0
0
 Baadhi ya vijana wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM)wilaya ya Mbinga wakishusha jeneza lenye mwili wa marehemu Kassian Nyandindi aliyekuwa mwandishi wa Habari  wa Gazeti la Majira na mmiliki wa Blogy ya Nyandind Gwiji la Matukio ambaye alifariki tarehe 10 na kuzikwa tarehe 12 katika  makaburi ya Misheni Mjini Mbinga.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye aliyevaa shati la kitenge na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilayani humo Beda Hyera wakiweka udongo jana, katika kaburi la aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira kituo cha Mbinga Marehemu Kassina Nyandindi ambaye alizikwa katika makaburi ya Misheni Mbinga mjini.
 Baadhi  ya viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari wa mkoa wa Ruvuma,wakiwa katika msiba wa mwandishi wa Habari wa Gazetila Majira kituo cha Mbinga wakati wa Ibada iliyofanyika numbani kwa marehemu Mtaa wa Ruhuwiko Mbinga mjini.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Beda Hyera akitoa salamu za Chama hicho katika msiba wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira wilaya ya Mbinga Marehemu Kassian Nyandindi aliyezikwa jana katika makaburi ya Misheni Mjini Mbinga.
 Mkuu wa wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye, akiongea na ndugu,jamaa,marafiki na waombolezaji waliofika katika msiba wa Marehemu Kassian Nyandindi ambaye alikuwa mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira aliyezikwa jana katika makaburi ya Misheni Mjini Mbinga.
 Mama Mzazi wa maraehemu Kassian Nyandind Mwalimu Nyandindi akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake maraehemu Kassian Nyandindi ambaye alifariki Dunia kufuatia ajali ya pikipiki iliyotokea tarehe 9 katika eneo la Ruhuwiko Mbinga Mjini na kufariki Dunia katika hospitali ya Rufaa Songea tarehe 10 alipo pelekwa kwa ajili ya Matibabu na kufariki  na kuzikwa tarehe 12 katika makaburi ya misheni Mbinga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Shafi Mpenda kushoto na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga Gombo Samandito wakitoa heshima zao katika kaburi la aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira marehemu Kassian Nyandindi aliyefariki tarehe 10 na kuzikwa terehe 12 katika makaburi ya Misheni Mbinga mjini.

PICHA ZOTE NA MUHIDIN AMRI(MBINGA)

DED MBINGA ATUMBUA WATUMISHI 10 WA IDARA YA AFYA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Mbinga
MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Gombo Samandito,amewasimamisha kazi watumishi kumi wa idara ya Afya akiwemo mganga mkuu wa halmashauri hiyo Dkt Hussen Sepoko.

Watumishi hao  kwa pamoja wamesimamishwa kazi kutokana na matumizi mabaya ya fedha   zaidi ya shilingi milioni 11, 270,000/= zilizotolewa na shirika lisilokuwa na kiserikali la Waterled  kwa ajili ya kufanikisha mpango wa kutoa elimu ya Afya kwa wananchi kinyume na utaratibu.

Kwa mujibu wa Gombo, watumishi hao walijilipa  fedha hizo  na kuongopa kwamba wanakwenda kutoa elimu ya Afya ikiwemo masaula ya Ukimwi katika vijiji mbalimbali,hata hivyo katika hali isiokuwa ya kawaida hawakwenda  vijijini licha ya kila mmoja kuchukua fedha  na  kuzitumia kinyume na taratibu.

Mbali na Dkt Sepoko,watumishi wengine ni   Andrew Kapinga, Tulizo Nziku,Sara Komba,Mary Ngonyani, Evarist Towegela tabibu mwandamizi,Agnes Adidas,Bryson Mapunda na katibu wa Afya Georg Mhina ambaye alichukua kiasi cha zaidi  ya shilingi milioni nne na kwenda kuzifanyia  matumizi mengine kinyume na utaratibu na maelekezo ya fedha hizo.

“ ni kweli nimewasimamisha kazi  watumishi kumi wa Idara ya Afya katika halmashauri yangu, hawa watumishi wakiongozwa na Dkt Sepoko walichukua fedha  zilizotolewa na Waterled kwa kisingizio cha kwenda kutoa elimu ya Afya kwa wananchi lakini hawakufanya hivyo”alisisitiza Gombo.

Alisema,alipata  taarifa kuwa watumishi hao kumi  kila mmoja alichukua  kiasi  cha fedha kulingana na cheo chake na kushindwa kwenda vijijini  kutekeleza wajibu wao, na hata alipomtuma mkaguzi wa ndani   aliyefuatilia  ubadhirifu huo katika vijiji vilivyotajwa  kupitia hati za malipo alibaini kuwa ,  watumishi hao hawakwenda  vijijini husika licha ya kuchukua fedha.

Gombo alibainisha kuwa,  taarifa ya ukaguzi  katika kipindi cha Januari hadi March inaonesha kuwa,idara ya Afya imekuwa na matumizi mabaya ya fedha za miradi jambo linalo sababisha  Idara hiyo kushindwa kufanya vizuri  kutokana na kuwepo kwa watumishi wasiokuwa waadilifu na wanao fanya kazi kwa maslahi binafsi.

Alisema, baada ya kuwasimamisha kazi hatua inayofuata ni ya kinidhamu,ambapo ataunda tume maalum  ambayo itawaita na kuwahoji kabla ya kuchukua hatua  nyingine zaidi za kiutumishi kutokana na makosa waliyofanya.

Alisema, ataendelea kuchukua hatua kali kwa watumishi wote wa halmashauri ambao wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya wizi ili kurudisha nidhamu ya matumizi ya fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii na miradi mbalimbali ya maendeleo.

IFM imeaswa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu ya bima- Dk. Kijaji

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imekitaka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu ya bima ili kuweza kuongeza pato la taifa pamoja na ukuaji wa uchumi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Ashantu Kijaji wakati wa uzinduzi program za shahada za uzamili mbili na shahada moja za chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Shahada uzamili zilizinduliwa ni Master of Scence in Social Protection Policy and Development , Master of Science Isuarance and Acturial Science  pamoja na bachelor of Science in Acturial Sciences.

Amesema mchango  wa sekta bima na hifadhi ya jamii ni mdogo kutokana na wananchi kukosa elimu na kufanya sekta ya bima na hifadhi ya jamii kuchangia asilimia moja katika  pato la Taifa.

Dk.Kijaji amesema kuwa chuo cha IFM kimeona mbali katika kuanzisha kozi mbili za uzazmili katika bima ili kuweza kujibu baadhi ya changamoto zilizopo katika  sekta hiyo.

Amesema nchi inakwenda  katika uchumi wa viwanda ambapo uchumi huo sehemu kubwa unashikwa na kilimo kutokana  na kuajiri idadi kubwa ya watanzania lakini idadi hiyo  haina  elimu ya bima.

Nae Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Thaudes Satta  amesema  chuo kimendelea kutoa elimu bora pamoja na kusimamia maadili na kufanya kuendelea kuongeza kozi katika kutatua changamoto katika baadhi ya maeneo ikiwemo sekta ya bima.

Amesema amesema kuwa kutokana na mahitaji ya bima chuo kitaendelea kufanya utafiti ili kuweza kuziba nafasi katika sekta hiyo na nchi kuweza kunufaika na bima.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji akizungumza wakati wa uzinduzi wa program shahada mbili za Uzamili na Shahada moja za Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Profesa Lettice Rutashobya akizungumza kuhusiana na kuanzisha kwa kwa shahada mbili za uzamili pamoja na shahada moja katika mwaka huu , katika halfa ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha IFM, Profesa Thadeus Satta akizungumza kuhusiana na chuo kilivyojipanga katika kutoa elimu bora na kusimamia maadili ya chuo hicho katika hafla uzinduzi wa shahada mbili huo uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii  wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM),Dk. Said Jafari  akitoa maelezo kuanzishwa program ya shahada za uzamili.
 .Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji akikata utepe kuashiria uzinduzi wa program mbili za Uzamili pamoja na shahada moja.
Sehemu ya wanafunzi wahitimu  watendaji na watoa maada na wadau katika uzinduzi wa program shahada za uzamili

KAMPUNI YA HUSEA YAUNGA MKONO KAULI YA RAIS MAGUFULI YA KUHAMISHA SHUGHULI ZA MIPANGO MIJI KUZIPELEKA WIZARANI

$
0
0
KAMPUNI ya Mipango Miji na Vijiji inayotoa ushauri elekezi kuhusu ardhi (HUSEA), imeunga mkono kauli ya Rais Dk. John Magufuli ya kuhamishia shughuli za mipango miji na kuzipeleka wizarani badala ya Tamisemi.

Wiki iliyopita Rais Magufuli aliagiza watalaamu wote wa ardhi na mipango miji katika halmashau zote nchini kusimamiwa moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa kampuni hiyo Renny Chiwa alisema kuwa uamuzi huo utasaidia kuboresha utendaji wa kazi za mipango miji.

"Tunampongeza Rais Magufuli kuhamisha shughuli za mipango mini wizarani Kwa sababu kuna watalamu was fani hiyo wanaweza kusimamia vizuri kuliko ilivyokua awali," alisema Chiwa.

Alisema uamuzi wa rais ni kutaka kuboresha shughuli za mipango miji pamoja na kuwawajibisha watendaji ambao watashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.Alisema kutokana na hali hiyo mabadiliko hayo yanaweza kuleta tija na nchi kuwa na mipango bora ya ardhi itakayotoa sura mpya.

Alisema kimsingi wataalamu wa ardhi na mipango miji katika halmashauri ni sawa na watumishi wengine katika serikali za mitaa, kwani wamekuwa wakiwajibika kiutawala moja kwa moja kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). 

Alisema kumekuwepo na changamoto za kiutendaji ambazo zinahitaji watalaamu was fani hiyo kukaa na kubuni mipango thabiti ya ardhi, hivyo basis ni vema suala hill litasimamiwa na watalaamu wenye fani hiyo.Alisema kutokana na hali hiyo mabadiliko hayo yataimarisha usimamizi wa idara husika ya ardhi na mipango miji katika halmashauri.

Alisema kutokana na hali hiyo watalaamu watakapkuwa katika kitengo hicho wanapasww kufanya kazi zao Kwa weledi ili wasimuangushe Rais.“HUSEA tunaona kuwa uamuzi huu wa Rais utazidi kuongeza ufanisi na kasi ya utekelezaji wa urasimishaji makazi nchini ambayo wizara hiyo yamekuwa yakitekelezwa kwa pamoja chini ya msukumo mkubwa wa Waziri wa wizara hiyo, William Lukuvi.
pichani kushoto ni Mratibu wa miradi wa kampuni ya mipango miji ya Husea,Edward Kinabo,Mwenyekiti wa kampuni Renny Chiwa pamoja na  Mkuu wa idara ya mipango miji na vijiji wa kampuni hiyo Aloyce Nyaisa,wakiunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamisha shughuli za mipango miji kutoka Tamiseni na kuzirudisha wizarani.

LUKUVI ATATUA MGOGORO MKONGWE WA ARDHI SOMJI- BOKO JIJINI DAR

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willium Lukuvi  ametatua mgogoro mkongwe wa ardhi huko Boko kata ya Dovya maarufu kama kwa Somji  jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wananchi Lukuvi  ameeleza Rais John Magufuli amempa maelekezo sambaba na kumaliza mgogoro huo.

Amesema  kuwa ardhi hiyo ni mali ya Serikali na wananchi waliojenga makazi yao ni wavamizi kwani eneo hilo la hekari 366 lilichukuliwa na serikali rasmi mwaka 1975 kutoka kwa Somji ambaye alikuwa mmiliki wa eneo hilo.

Aidha ameeleza  kama Serikali haiwezi kuvunja majengo ya wakazi hao ila lazima wafuate taratibu zilizowekwa ili kupata umiliki halali wa viwanja hivyo.

Lukuvi ameeleza lazima mipaka yote ya shamba la Somoji la mwaka 1952 ipimwe ili iweze kujulikana pia ofisi za mipango miji za wizara na Manispaa iangalie kama kuna mipango yoyote ilitokea kuhisiana na eneo hilo.

Ameeleza kwa wenye hati na michoro lazima ihakikiwe kama ipo sahihi sambamba na maelezo ya ya wamiliki kuhusiana na umiliki wao.

Lukuvi ameeleza kuwa kamati iliyoundwa itashirikiana na wataalamu wa wizara ambao watapima maeneo hayo na kugaiwa kwa wananchi na kuanza kuyalipia kodi rasmi na zoezi limalizike mwezi Septemba mwishoni ili wananchi wakabidhiwe hati zao rasmi.
Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi, akizungumza  katika mkutano  wa hadhara na  wananchi wa Boko ambapo ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa  zaidi ya miaka 40 katika eneo la Somji lenye hekari 366 jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka wa Globu ya jamii)
 Mbunge wa Kawe Halima Mdee akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa kutatua mgogoro wa ardhi ambapo ameishukuru serikali kwa kutatua mgogoro huo.
 Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi  akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Boko ambapo ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa  zaidi ya miaka 40 katika eneo la Somji lenye hekari 366 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi akijibu maswali mabalimbali aliyoulizwa na wananchi wa  Boko ambapo ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa  zaidi ya miaka 40 katika eneo la Somji lenye hekari 366  jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka wa Globu ya jamii)
 Baadhi ya wananchi wa Boko wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi katika mkutano huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Hakutakuwa na Upungufu wa Sukari- Dkt Tizeba

$
0
0
Serikali imeagiza sukari kiasi cha tani 70,354.35 kutoka nchi za nje lengo likiwa ni kujipanga ili kuhakikisha kuwa hapatokei upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini.

Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni waziri  wa kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa tani 60,539.35 ya sukari  itaanza kuingia hapa nchini katikati ya mwezi Mei 2018 ambapo kiasi kilichobaki cha tani 9,815 kitaingia mwezi  June mwaka 2018.


Aidha  Dkt. Tizeba amefafanua kwamba hakutarajiwi kuwa na upungufu wa sukari hapa nchini  kwa sababu hadi kufikia tarehe 10 mei 2018 katika maghala ya wazalishaji na wafanyabiashara  kulikuwa na tani 78,147.67 za sukari na kiasi kingine  tani 25,441.25 kipo Bandarini .Kwa kiasi cha sukari ambacho tayari kipo hapa nchini kikijumlishwa na kiasi ambacho kitaingia hivi karibuni kutoka nje ya nchi ni dhahiri kwamba  nchi haiwezi kupata upungufu wa bidhaa hiyo, alisema Mhe.Waziri.

Awali Dkt.Tizeba  alisema kwamba mahitaji ya sukari nchi nzima ni tani 630,000 ambapo kati ya hizo, tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani na tani 485,000 ni kwajili ya matumizi ya kawaida.Hata hivyo mapitio yanaonesha kwamba  msimu wa mwaka 2017/18  viwanda vya ndani vilizalisha tani 306,226  za sukari kwa matumizi ya kawaida  ambapo mwisho wa msimu huu uzalishaji umefikia tani 307,481.76 aliongezea Dkt. Tizeba.

Akimalizia taarifa yake Mhe. Tizeba amebainisha kuwa kwa kiasi ambacho sukari imeagizwa kutoka nje Pamoja na viwanda vya ndani inadhihirisha kwamba hakutakuwa na upungufu wa aina yeyote ya sukari hapa nchini na ikizingatiwa  kuwa viwanda vitaanza uzalishaji mwingine mwezi mei ambapo ukarabati (services ) itakuwa imekamilika .
Waziri  wa kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba

AGAPE YAENDESHA KONGAMANO KWA WANAFUNZI SHULE 8 ZA KATA YA USANDA SHINYANGA

$
0
0
Shirika la Agape AIDS Control Programme (AACP) limeendesha kongamano kwa wanafunzi 120 kutoka shule nane zilizopo katika kata Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kwa lengo la kuwajengea uelewa wanafunzi kuhusu masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.

Kongamano hilo lililoongozwa na mdahalo wenye mada "Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?" limefanyika leo Jumapili Mei 13,2018 katika ukumbi wa Ibanza Hotel uliopo mjini Shinyanga.

Mbali na kuongozwa na mada hiyo,pia wanafunzi hao wameonesha michezo kadha wa kadha huku mada mbalimbali zikitolewa ikiwemo huduma rafiki kwa vijana,ukatili wa kijinsia na madhara yake,majukumu ya afisa ustawi wa jamii na mazingira rafiki shuleni pamoja na umuhimu wa michezo.

Awali akizungumza, Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana unaotekelezwa na shirika la AGAPE kwa ufadhili wa shirika la Kimataifa la Sida kutoka SWEDEN , Lucy Maganga alizitaja shule hizo kuwa ni shule za msingi Busanda,Nzagaluba,Manyada,Shingida,Shabuluba na shule za sekondari Usanda,Singita na Samuye.“Mdahalo huu umelenga kuwajengea uelewa wanafunzi kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wapate mimba wakiwa shuleni na magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi”,alieleza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akifungua mdahalo akifungua mdahalo huo ambapo aliwataka wanafunzi hao kuepuka tabia hatarishi zinazoweza kusababisha wakatishe masomo yao mfano kupata mimba wakiwa shuleni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola akizungumza ukumbini. Kushoto ni Afisa Elimu kata ya Usanda Essero Ashery, kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Atupokile Maseta aliyehudhuria mdahalo huo kwa niaba ya Afisa Ustawi wa jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE, John Myola ukumbini.
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Ujinsia unaotekelezwa na shirika la AGAPE ,Lucy Maganga akitoa mwongozo wa kuchangia mada ya '"Je Kijana akibalehe/akivunja ungo anakuwa tayari kuoa/kuolewa au kufanya ngono?".


JAFO AFURAHISHWA NA MRADI WA MACHINJIO JIJI LA MWANZA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa mkoa na jiji la Mwanza kwa kuboresha machinjio ya Kisasa ndani ya jiji hilo. 

Jafo ametoa pongezi hizo leo alipotembelea mradi huo mkubwa ambao kukamilika kwake kutawezesha kuchinjwa ng'ombe 700 kwa siku.Aidha mradi huo utaongeza mapato ya jiji hilo ambapo yanatarajiwa kuongezeka kutoka Sh. milioni 30 kwa mwezi hadi Sh.milioni 120 kwa mwezi kwa chanzo hicho pekee. 

Akizungumza katika mradi huo, Waziri Jafo amezitaka Halmashauri zingine nchini kuiga utekelezaji wa mradi huo.Aidha Waziri huyo Jafo amempongeza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Mongela, Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula, Mkuu wa wilaya, pamoja na Mkurugenzi wa jiji na baraza la madiwani kwa usimamizi wa miradi na utendaji kazi wao uliotukuka.

Mbali na kutembelea mradi wa machinjio , katika ziara hiyo pia Jafo amefanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya miradi ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa shule ya wasichana ya Ngaza, eneo linalo tarajiwa kujengwa maegesho ya magari ya mizigo, stendi ya Nyegezi inayotarajiwa kuboresha, miundombinu ya barabara za mawe na Hospitali ya Nyamagana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Viongozi wa mkoa wa Mwanza wakikagua Miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akipongeza ujenzi mzuri wa barabara za changarawe katika mitaa ya jiji la Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Ngaza.
Machinjio inayoboreshwa katika jiji la Mwanza.

MGODI WA MGONGO GOLD MINE WAWAOKOA WANAFUNZI 99 WANAOSOMEA CHINI YA MITI IRAMBA

$
0
0
Na Jumbe Ismailly IRAMBA

WANAFUNZI 99 wa darasa la awali katika shule ya msingi Kibululu,kata ya Mgongo,tarafa ya Shelui,wilayani Iramba,Mkoani Singida wanasoma wakiwa wamekaa chini ya miti huku wakitumia magoti ya miguu yao kama meza wakati wakiandika kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati unaoikabili shule hiyo.

Kaimu Ofisa elimu Kata ya Mgongo,Lazaro Isaya Sakata alithibitisha kuwepo kwa upungufu huo wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati kwenye hafla fupi ya kupokea tani tano za mifuko ya saruji zilizotolewa na Kampuni ya kuchimba madini ya Mgongo Gold Mine kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo.

Alifafanua Ofisa huyo wa elimu kuwa wanafunzi wa awali katika shule ya msingi Kibululu wanasoma wakiwa wamekaa chini ya miti kwa sababu hakuna chumba cha darasa kinachoweza kuwamudu kuingia wote 99 na kuweza kumsikiliza mwalimu wao kikamilifu.

Kwa mujibu wa Sakata wanafunzi hao 99 wanatakiwa kuwa na vyumba vinne vya madarasa kutokana na kwamba uwiano wa mkondo mmoja ni wanafunzi 25,kitu ambacho kimekuwa kigumu na kulazimika kuwakusanya chini ya miti na kuendelea na masomo.

“Sasa namna ya kumudu kwamba niangalie kila mmoja anaumba vipi ile herufi au kile ninachokifundisha,inakuwa ni kazi kidogo mara kuna mvua mnatoka mnakimbia,mara jua kali inabidi msogee mahali Fulani na mara kuna upepo kwa wakati wote wanakuwa ni vurugu halafu mkiwa nje watoto hawajifunzi vizuri”alisisitiza Sakata.

Akikabidhi msaada huo wa tani tano za saruji,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mgongo Gold Mine,Herieth Michael Sagati alitumia fursa hiyo kuyashawishi Makampuni yanayochimba madini katika Kijiji cha Kibululu kujitokeza na kuhakikisha wanawekeza kwenye sekta ya elimu.
Ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kibululu,kata ya Mgongo,wilayani Iramba wakionekana wakipanda juu ya gari dogo lililoleta saruji kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kwa wanafunzi kusomea chini ili waweze kushusha mzigo huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mgongo Gold Mine,Herieth Sagati akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Kibululu,kata ya Mgongo katika picha ya pamoja mara baada ya gari lililobeba saruji kuwasili shuleni hapo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

KUWAIT NA TAASISI YA WAMA ZATIA SAINI MKATABA WA KUWASAIDIA WALEMAVU

$
0
0
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, Jumamosi Mei 12 2018, walitiliana saini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya kuwasaidia walemavu na albino nchini. 

Kwa mujibu wa mkataba huo uliosainiwa katika makao makuu ya Taasisi ya WAMA, Kawe jijini Dar es Salam, Ubalozi wa Kuwait utaipatia Taasisi hiyo dola elfu 50 sawa na takriban shilingi milioni 112  kwa ajili ya kununua vifaa vya kisasa vya walemavu ambavyo vitasambazwa katika vituo husika kama vile Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko na kituo Maalum cha Usonji (Autism) kilichopo Sinza.
Baada ya zoezi la kutia saini, Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete ameushukuru Ubalozi wa Kuwait kwa msaada huo huku akiahidi kuufikisha kwa walengwa, Mama Salma amefafanua kuwa Taasisi yake inajishughulisha zaidi katika mambo matatu makuu ambayo ni Elimu kwa kuwapa kipaombele watoto mayatima na wanaotoka katika mazingira magumu, afya na kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Kwa upande wake Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Al-Najem amesema kuwa Ubalozi umeamua kutia saini mkataba huo ikiwa ni kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete JKMF wiki chache zilizipota uliofanyika Ikulu ambapo Rais Magufuli alitoa wito wa kuzisadida Taasisi zinazoshirikiana na Serikali katika kuwaletea watanzania maendeleo.

Al-Najem amefafanua kuwa Ubalozi utaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na asasi zisizokuwa za kiserikali ili kuwasaidia walemavu huku akisema kuwa siku ya Jumanne ijayo Ubalozi utakabidhi vifaa vya kisasa katika chumba cha upasuaji cha watoto wenye vichwa vikubwa katika Taasisi ya Mifupa MOI Muhimbili ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamo wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Hafla ya Utiaji saini ilishuhudiwa na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya WAMA ambao Bi. Zakia Meghji, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar pamoja na Daud Nasib.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete wakisaini mkataba wa ushirikiano katika program ya kuwasaidia walemavu na albino wenye thamani ya dola za Marekani elfu 50 (sawa na shilingi milioni 112) ambazo zitatumika kununulia vifaa kwa ajili ya vituo mbali mbali chini ya Taasisi hiyo.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (katikati) pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Taasisi hiyo, Zakia Meghji, baada ya kusaini mkataba wa makubalio.
Picha ya pamoja.

DC GAIRO AAGIZA WACHIMBAJI MADINI WASIO NA LESENI KUSIMAMISHA UCHIMBAJI MARA MOJA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kutembelea sehemu ya migodi inayochibwa kinyemela na wachimbaji wasiokuwa na leseni.
Moja ya mashine zilizokutwa eneo la mgodi. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe amesikitishwa na makampuni ya uchimbaji madini ya viwandani wanaochimba madini mbalimbali Wilayani hapo hasa aina ya Felispar bila leseni. Mhe. Mchembe aliyasema hayo alipotembelea migodi ya Kata ya Rubeho ambapo wachimbaji wameweka mashine nzito na wanafanya kazi wakati hawana leseni. 

 Sheria ya Madini ya mwaka 2010, kifungu cha 18 kimeweka bayana adhabu kwa mchimbaji haramu. Ikiwa ni mtu binafsi faini isiyozidi milioni 5 au kifungo miaka mitatu au vyote pamoja. Kama ni kampuni basi ni faini isiyozidi shilingi milioni 50. Mheshimiwa Mchembe aliendelea mbali na kuelezea kifungu cha 6 (4) cha Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji namba 29 ambapo madini yaliyopatikana kupitia uchimbaji haramu yatataifishwa na Serikali chini ya Kamishna wa madini na kuuzwa kwa mnada. Mitambo yote pia inapaswa kutaifishwa. 

 Akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Mchembe ametoa maagizo hayo na kumtaka Afisa Madini Mkoa na Kanda kufatilia jambo hilo kwa karibu. Pia amepiga marufuku raia wa kigeni kutembelea maeneo ya machimbo bila kibali. Aidha uzingatiwaji wa kanuni 3 (1) (2) ambapo mchimbaji anatakiwa kuwasilisha kwa Afisa Madini mkazi kanda taarifa ya tathmini na mpango wake wa utunzaji wa mazingira kabla ya kuanza kuchimba madini. Wilaya ya Gairo ina madini aina mbalimbali na maeneo ya milimani yameachwa na mashimo makubwa.

WAZIRI KIGWANGALLA AMTEUA MISS JOURNALISM TANZANIA 2018 KUWA BALOZI WA UTALII WA PORI LA AKIBA SELOUS

$
0
0
Na Hamza Temba-WMU-Dodoma

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemteua mshindi wa taji la Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous.


Amefanya uteuzi huo mwishoni mwa wiki Jijini Dodoma baada ya mazungumzo na mwanamitindo huyo aliyemtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kuandaa  mradi wa kijamii ambao ni sehemu ya shindano atakaloshiriki la taji la Dunia la Miss Journalism 2018 litakalofanyika Oktoba 27 Jijini Arusha.


Kufuatia uteuzi huo, Dk. Kigwangalla amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi kuandika barua ya uteuzi kwa balozi huyo mpya sambamba na kumkabidhi hati ya uteuzi ili pamoja na mambo mengine aweze kunadi vivutio vya utalii vya pori hilo.


Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara kuandaa safari maalum ya balozi huyo mteule aweze kutembelea Pori la Akiba Selous kwa ajili ya kuona na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu hifadhi hiyo kwa ajili ya utangazaji.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini Afrika ya Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jijini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa taji la urembo la "Miss Garden Route South Africa 2017" ambalo ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha utalii nchini Afrika ya Kusini na Miss Journalism Tanzania 2018, Witness Teddy Kavumo (21) aliyeshinda taji hilo na mataji mengine matatu nchini humo mwaka jana, alipomtembelea ofisini kwake mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki kwenye mashindano ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jijini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa vivutio vya utalii vya Pori la Akiba Selous. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini Afrika ya Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa vivutio vya utalii vya Pori la Akiba Selous.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini Afrika ya Kusini, baada ya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma alipomtembelea mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa wa utalii wa Pori la Akiba Selous. 

Viewing all 109936 articles
Browse latest View live




Latest Images