Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Tatu Mzuka yatangaza ushirikiano wa kibiashara na Wema Sepetu

$
0
0
Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, leo imetangaza kuanza ushirikiano wa kibiashara na mrembo maarufu nchini Bi. Wema Sepetu.

Ushirikiano huu ni mwendelezo wa mpango mkakakati wa Tatu Mzuka wa kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania katika kuboresha maisha yao. Kusudi hasa la Tatu Mzuka kama ilivyoelezwa ni kusambaza fursa kwa watu wengi kadri inavyowezekana ili kubadilisha maisha yao.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga alisema kuwa ushirikiano huu ni mmojawapo kati ya nyingi ambazo Tatu Mzuka wanajihusisha nazo.‘Muda wote tunaangalia kipaji ambacho tunahisi kinaendana na bidhaa yetu na hivyo kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Katika biashara yetu tayari tuna ushirikiano na Millard Ayo, Brother K, Shilawadu na wengine wengi na leo tunatangaza kumwongeza Wema Sepetu kwenye orodha hiyo’ alisema Maganga.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar kuhusu Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, kutangaza kuanza ushirikiano wa kibiashara na mrembo maarufu nchini Bi. Wema Sepetu pichani kushoto.

‘Muda wote tunaangalia kipaji ambacho tunahisi kinaendana na bidhaa yetu na hivyo kuanzisha ushirikiano wa kibiashara. Katika biashara yetu tayari tuna ushirikiano na Millard Ayo, Brother K, Shilawadu na wengine wengi na leo tunatangaza kumwongeza Wema Sepetu kwenye orodha hiyo’ alisema Maganga.

Wema ambaye alikuwepo pia kuelezea furaha yake baada ya kutangaza ushirikiano na Tatu Mzuka, alisisitiza kwamba ana hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha mashabiki wake mambo mazuri ambayo amewaandalia.

Bi Wema Sepetu akizungumza mbele ya waanidishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Kampuni ya ‘The Network’ ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania, kutangaza kuanza ushirikiano nae wa kibiashara .




Wema Sepetu akifurahia jambo mara baada ya kutangazwa ushirikiano wake na kampuni ya The Netwek-ambayo ni kampuni mama inayoendesha mchezo wa namba wa Tatu Mzuka nchini Tanzania.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI KUTAFTIA MBIA MPYA ILI KUONGEZA USHINDANI KATIKA KUIMARISHA USAFIRI WA DSM

TAARIFA YA KUACHILIWA KWA ALIYEKUWA MFUNGWA JOSEPH MBILINYI 'SUGU'.

BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI WAPYA 40,000

$
0
0
*Maombi yote kupokelewa kwa njia ya mtandao, kurugenzi ataja vipaumbele 
*Wenye ulemavu, yatima kupewa kipaumbele, RITA nao kuhakiki cheti cha kuzaliwa

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) imesema mwaka wa masomo wa 2018/2019 wamejipanga kutoa mikopo kwa jumla ya wanafunzi wapya 40,000 na wanaoendelea zaidi ya 80,000 huku ikitangaza rasmi kuanza kupokea maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa muda wa miezi miwili na maombi yote yatapokelewa kwa njia ya mtandao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Abdul -Razaq Badru wakati anatangaza kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa miezi miwili na kufafanua jumla ya Sh.bilioni 427 zimetengwa.

Kuhusu maombi ya mkopo, Badru amesema leo wametangaza kupokea maombi ya mikopo ya elimu ya juu na maombi yote yawe kwa njia ya mtandao.

Amesema maombi hayo yatatumwa kupitia www.olas.heslb.go.tz na ni kuanzia leo hadi Julai 15 mwaka huu ili kuwapa fursa wanafunzi wahitaji kuwasilisha maombi hayo.

"Mwaka jana tulitoa mwezi mmoja,mwaka huu tumetoa muda wa zaidi ili kuwawezesha kusoma mwongozo kwa makini na kuzingatia maelekezo tunayopewa,"amesema Badru.

Amefafanua kuwa mwongozo huo kuna mambo muhimu yakiwamo ya sifa na taratibu za utoaji mikopo kwa mwaka 2018/2019.Mwongozo huo unapatikana katika lugha ya Kiswahili na Kingereza kwenye tovuti ya www.heslb.go.tz.

Amesema mambo muhimu yaliyomo kwenye mwongozo  ni kwamba kipaumbele kitatolewa kwa Watanzania wahitaji wanaosoma kozi zenye uhitaji mkubwa zaidi  kitaifa kama walimu wa masomo ya sayansi na hisabati, na sayansi ya afya ya binadamu.

Amesisitiza watatoa kipaumbele pia kwa wahitaji ambao ni yatima na wana nakala za vyeti vya vifo vilivyothibitishwa na Wakala wa Usajili na Udhamini (RITA) nao watapewa kipaumbele bila kujali kozi wanazosoma. Pia wengine watakaopewa kipaumbele ni waombaji wenye ulemavu uliothibitishwa na Mganga wa Mkoa au wilaya.
Mkurugenzi Mtendahi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul -Razaq Badru (kulia) akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuhusu kutangaza rasmi kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 leo Alhamisi, Mei 10, 2018 jijini Dar es salaam. Katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe na kushoto Meneja Usajili wa RITA, Patricia Mpuya. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya  Mkazi Kisutu imeelezwa mkataba uliongiwa na Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando na  Channel 2 Group Corporation (BV1) haukujulikana na bodi ya Wakurugenzi wala bodi ya zabuni za TBC.

Mwanasheria wa  shirika hilo, Gwakisa  Mlawa ameeleza hayo leo Mei mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi alipokuka akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya  Sh.milioni 887. inayomkabili Tido.

Akiongozwa  na Wakili wa Takukuru, Leonard Swai, Gwakisa ambaye ni shahidi wa pili wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo amedai alifahamu kuwepo kwa mkataba huo baada ya kupelekewa taarifa ya kesi Juni mwaka 2012 na Channel 2 Group Corporation (BV1) ambapo walikuwa wakidai TBC wamekiuka mkataba walioingia kwa ajili ya kuwekeza kwenye mitambo ya digital.

Shahidi huyo alidai, mkataba huo ulisainiwa na Tido na watu wawili wa Channel 2 Group Corporation (BV1)  na kwamba kulikuwepo na nyongeza ya mkataba ama marekebisho ya mkataba yaliyosainiwa Juni, Agosti na Novemba mwaka 2008.

Alidai baada ya kupokea taarifa hiyo, TBC ilimwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuomba ushauri na baada ya AG kuliangalia suala hilo Kwa ujumla wake aliagiza ateuliwe mwanasheria wa kimataifa ambaye ni mjuzi katika masuala hayo.

Amedai iliteuliwa kampuni ya uwakili ya Freshfield Bruckhaus Derringer us  LLP ambaye  baada ya kuteuliwa alifika, TBC na kufanya uchunguzi wa nyaraka na kwamba ililipwa maalipo ya awali zaidi ya milioni 800.

Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa kuwa Tido alisababisha hasara kutokana na kiasi hicho cha fedha hicho ambacho kililipwa kwa kampuni hiyo ya uwakili.

Akijibu swali la Wakili wa Tido, Ramadhan Maleta, kama aliwahi kuiona hiyo mikataba iliyoingiwa na Tido na kwamba ilikuwa ikimpa kazi, channel 2 Group Corporation (BV1) alidai kuwa ilikuwa ni kama wameingia katika makubaliano ya awali ya maandalizi ya mchakato wa kuelekea kwenye digital.

"Wewe kama mwanasheria wa TBC kwa jinsi ulivyoipitia hiyo mikataba ulichukua hatua gani." Aliuliza Maleta, 

Akijibu swali hilo shahidi huyo alidai, taarifa ya kesi ilifika wakati akiwa nje ya TBC lakini baadae alirudi. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, mwaka 2008,   akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

SPIKA DUGAI ALIPOKUTANA NA WALIOKUWA WANAFUNZI WENZAKE WAKATI ANASOMA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana  na waliokuwa Wanafunzi wenzake wakati anasoma Shule ya Sekondari Kibaha, Mkoani Pwani walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Anayesalimiana na Mhe. Spika ni Ndg. Sadiki Alli na wengine kutoka kushoto ni Ndg. Jackson Kalikumtima, Eng. Hussein Mzara na Ndg. David Mchaina.
 Spika wa Bunge  akizungumza na waliokuwa Wanafunzi wenzake wakati anasoma Shule ya Sekondari Kibaha, Mkoani Pwani walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wakwanza kushoto kwa Mhe. Spika ni Ndg. Jackson Kalikumtima, Eng. Hussein Mzara, Ndg. Sadiki Alli na Ndg. David Mchaina.
 Spika wa Bunge  akizungumza na waliokuwa Wanafunzi wenzake wakati anasoma Shule ya Sekondari Kibaha, Mkoani Pwani walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wakwanza kushoto kwa Mhe. Spika ni Ndg. Jackson Kalikumtima, Eng. Hussein Mzara, Ndg. Sadiki Alli na Ndg. David Mchaina.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na waliokuwa Wanafunzi wenzake wakati anasoma Shule ya Sekondari Kibaha, Mkoani Pwani walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wakwanza kulia ni Ndg. Jackson Kalikumtima, Ndg. David Mchaina na kutoka kushoto ni Eng.Hussein Mzara na Ndg. Sadiki Alli.

TAPSEA YAANZA MKUTANO WAKE ZANZIBAR

$
0
0
 Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakifatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mhadhiri wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Charles George Magaya katika siku ya kwanza ya Mkutano wao, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar. ambapo alisema kuwa Kada ya Makatibu Mahsusi ni kati ya kada kongwe kabisa katika historia ya Utumishi Serikalini, Taasisi za umma hata kwenye Sekta binafsi. Ni dhahiri Watendaji Wakuu na Viongozi wengi sehemu ya kazi wamekuwa wanauhitaji utendaji mzuri wa Katibu Mahsusi ili wafanye kazi zao kwa haraka na ufanisi zaidi.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akizungumza jambo katika siku ya kwanza ya Mkutano wao, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.
Sehemu ya Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika siku ya kwanza ya Mkutano wao, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.

NAIBU WAZIRI JULIANA SHONZA MGENI RASMI FAINALI YA KUSAKA VIPAJI VYA WATANGAZAJI

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali ya kutafuta watangazaji watatu wenye vipaji  kati ya 30  itakayofanyika Mei 12 mwaka huu katika ukumbi Dar Live jijini Dar es Salaam.
Akizuungumza leo Dar es Salaam, Ofisa Uhusiano wa Times FM Radio, Flora Matthew  amesema walioshiriki katika shindano la kusaka vipaji walikuwa watu 1000 na baadae wamechujwa na kufikia 30 ambao wanaingia katika fainali ya kutafuta washindi watatu.

Amesema kuwa washindi hao watasomeshwa na radio hiyo kwa lengo la pata taaluma ya habari kutokana na sheria ya utangazaji inavyotakiwa. Frola amesema washiriki 27 wataobakia ni wazuri lakini mahitaji ya shindano ya watangazaji wa wenye vipaji ilikuwa inahitaji watangazaji watatu.

Fainali zitaambatana na burdani mbalimbali kwa wasanii ambao ni Barnaba Classic , Khadija Kopa, Country Boy, QBoy, Chemical  Whitnes na Ochu, Cheen Bees , Nchama , Enock Bella, Whozu , Kisamaki na Getu  wengine Young Tuso, Jovi , Mabantu , Orbit  na wengi ambao watakuwepo katika fainali hizo.

Amesema kiingilio cha fainali ya hizo ni sh. 5000 katika kuwashudia washindi watatu wataoibuka.
Ofisa Uhusiano wa Times FM Radio, Flora Matthew akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na fainali ya kusaka vipaji iliyokuwa inaendeshwa na radio hiyo leo jijini Dar es Salaam

BARAZA LA WAFANYAKAZI TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZMA LAKUTANA, MWENYEKITI WAO DK. NIHUKA AZUNGUMZIA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MWENYEKITI wa Baraza la Wafanyakazi wa Tasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dk.Kassim Nihuka amesema pamoja na mafanikio ambayo imeyapata taasisi hiyo bado wangepata mafaniko makubwa zaidi iwapo changamoto zinazowakabili ikiwamo ya uhaba wa watumishi pamoja na miundombinu ingekuwa imepata ufumbuzi wake huku akifafanua tayari wameweka mikakati ya kuhakikisha wanaondoa changamoto hizo.

Dk. Nihuka ametoa kauli wakati anazungumza kwenye Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima uliofanyika leo ambapo mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mbando.

Akizungumza kwenye hotuba yake kwa mgeni rasmi ,Dk.Nihuka amesema mafanikio hayo huenda yangekuwa makubwa na mengi zaidi kama siyo changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwamo za ukosefu wa ofisi za kudumu  katika baadhi ya mikoa, upungufu wa wafanyakazi kutokana na kustaafu na vifo pamoja na
upungufu wa fedha za ndani.

Pia amesema ili kuendana na na msimamo wa Serikali wa Awamu ya Tano ,Menejimenti ya taasisi hiyo imedhamiria kuimarisha ukusanyaji wa mapato pamoja na kuhakikisha yanaenaelekezwa  katika kutekeleza malengo ya kipaumbele  kadiri ya mpango kazi wa taasisi na ule wa vituo,kampasi,idara na vitengo kwa ujumla.

"Katika kutekeleza hili wakufunzi wakazi, wakuu wa kampasi na mkuu wa idara ya mafunzo yanaagizwa kusimamia ukusanyaji wa ada kwa umakini mkubwa pamoja na kuhakikisha wanafunzi wale tu waliolipa ada ndio wanasajiliwa na kupata huduma katika vituo vyote,"amesema Dk.Nihuka.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dk.Kassimu Nihuka akizungumza kuhusu mafanikio na changamoto mbele ya wajumbe wa baraza hilo waliokutana leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando akizungumza leo wakati akifungua rasmi Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima wakishiriki mkutano huo leo jijini Dar es Salaam

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii

KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC imepoteza matumaini yake ya kunyakuwa kombe la Ligi Kuu vodacom Tanzania bara msimu huu.

Kwa sasa Azam FC ana michezo 3 iliyobakia mpaka hivi sasa ambayo akishinda yote atanyakuwa pointi 9,miwili ikiwa ni ya Nyumbani na mmoja wa ugenini.

Wanalambalamba hao watawakaribisha wanalizombe Maji maji kutoka mkoani Ruvuma katika dimba la Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam utakaochezwa kesho saa 10 jioni.

Msemaji wa Azam FC Jafarry Maganga amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wanahitaji kulinda heshima yao hasa kwa kuzingatia mechi hiyo inachezwa kwenye uwanja wao wa  nyumbani huku akifafanua mchezo huo ni wa umuhimu kwao ili kuongeza alama za kuendelea  kubakia  katika nafasi waliyonayo sasa.

"Tutafanya vizuri kwa kushinda michezo yote iliyobaki ili kuendelea kushikilia nafasi ya pili ambayo ina heshima katika ligi hii japo huwezi kuwakilisha nchi kimataifa,"amesema Jaffary.

Ameongeza kulingana na alama walizonazo huku wakiwa wamebakiza  michezo 3 ni ndoto kushika nafasi ya kwanza ambayo anaishikilia mnyama Simba kwa alama 65 huku Azam wakiwa nafasi ya Pili kwa alama 49 wakifatiwa na Mabingwa watetezi Yanga ambao wana alama 48.

Pia Jaffary amesema hatawaonea huruma Majimaji ambao wana wakati mgumu na wapo hatarini kushuka daraja msimu huu wa ligi.

"Hatuta angalia kuwa timu hiyo ina hati hati ya kushuka daraja, muda wa huruma haupo tena ikiwa kila mmoja alipewa mechi ya kwanza hadi ya mwisho na alitakiwa kujipanga mapema ili asifikie hatua hii mbaya,"amesema.

Baada ya kumalizana hiyo kesho na Majimaji, Azam FC watabakiza michezo yao miwili ambapo watawakaribisha Tanzania Prison baada ya hapo watakutana na watoto wa Jangwani akiwa wageni dhidi ha Yanga

SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZAIDI YA 6, 000 KATIKA SEKTA YA AFYA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
SERIKALI imetangaza nafasi za ajira katika sekta ya afya 6,180 katika kuhakikisha kuwa upungufu wa watumishi wa kada ya afya inatatuliwa na kuimarika katika upatikanaji wa huduma bora ya afya nchini.
Akitangaza ajira hizo leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema watakapoajiriwa watumishi hao watapangiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuzingatia uhitaji.
"Watumishi watakaoajiriwa katika sekta ya afya ni madaktari, wafamasia wauguzi , Tabibu pamoja na wahudumu wa afya.Wenye sifa za taaluma za afya wajitokeze kuomba nafasi hizo ili waweze kuajiriwa na kutoa huduma kwa wananchi,"amesema Jafo na kuongeza vigezo  vyote vya waombaji vitazingatiwa ili kutoa huduma bora za afya kutokana na taaluma walizosomea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Tawala za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati anatangaza ajira hizo.

SH. BILIONI 50/- ZATOLEWA KUANZA UJENZI WA STENDI MPYA YA MABASI INAYOJENGWA MBEZI LUIS JIJINI DAR

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezungumza na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya watendaji hadi wakurugenzi wa Manispaa kuhusu miradi mbalimbali ya kichumi katika kujenga nchi.

Makonda ameeleza hayo leo wakati anzungumzia ujenzi wa Stendi ya mabasi ya abiria yaendayo mikoani Ubungo ambao tayari  Sh.bilioni 50 imetolewa kwa ajili ya kuanza kujengwa kituo hicho kitakachokuwa cha kisasa kikiwa na huduma mbalimbali za jamii ikiwemo hoteli, supermarketi na huduma za kibenki.

Makonda  ameeleza kituo hicho kinatarajiwa kujengwa eneo la Mbezi Luis  ambapo amebainisha Manispaa za Jiji hilo imetengewa bajeti ya Sh. bilioni 250 kutoka Mfuko wa Rais kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali.

Pia amesema miradi inayosimamiwa na Manispaa ambayo Serikali inaifanyia kazi kama fukwe ya Coco beach ambayo ni mali ya wananchi na itatengenezwa ili wananchi wafurahi kutembelea na kushiriki kula keki ya taifa.

Aidha ameongeza kuwa mapato yameongezeka kutoka Sh.milioni 87 hadi Sh.bilioni moja na kuwasisitiza watendaji kuwa wakali kuhusu matumizi ya fedha.

Makonda amesema lazima manispaa zote ziwe na uchumi madhubuti na kuwahudumia wananchi na kuiacha Serikali kuu kujenga miradi mikubwa kama Standard gauge, miradi ya umeme sambamba  na kuangalia usalama nchini.

Pia amewataka wananchi wa Mkoa huo kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa kazi kubwa ya kuleta mabadiliko nchini na ameahidi kama watendaji watashirikiana katika kuifikisha Tanzania katika maendeleo na kueleza kuwa haina haja ya kumbeza Rais Magufuli kwani kazi anayoifanya ni kwa faida ya wananchi kama vile miradi ya maji, barabara na  umeme hivyo lazima tutambue mchango huu na tuunge mkono juhudi zake.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (katikati)  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu ujenzi wa Stendi ya mabasi ya kwenda mkoani kinatachotarajiwa kujengwa eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa standi hiyo ya kisasa inayotarajiwa kujengwa ambayo itakuwa na sehemu za kupumzikia abiria,itakuwa na sehemu za kupaki magari madogo takribani 300,pamoja na Mabasi makubwa 200,na sehemu za biashara. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).
Baadhi ya watendaji wa  Manispaa wakisikiliza mjadala uliokuwa ukiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

SERIKALI YAKUSUDIA KUTAFUTA MBIA MWINGINE MRADI WA UDART

$
0
0
*Yasema maitosita kumuondoa mwendeshaji wa sasa 

SERIKALI imesema inakusudia kuongeza mtoa huduma mwingine katika uendeshaji wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) ambayeataingiza mabasi yake na kutathmini ufanisi wa mbia wa sasa ili kuimarisha huduma ya usafiri Jijini Dar es salaam . 
Amesema iwapo itabainika kwamba mwendeshaji wa sasa ana matatizo yaliyokithiri, Serikali haitasita kumuondoa na kumpa mwendeshaji mwingine kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa uhakika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 10, 2018) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Bw.Maulid Mtulya katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

Katika swali lake Bw. Mtulia alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya uboreshaji wa wa mradi wa UDART unaotoa huduma ya usafirishaji wa abiria Jijini Dar Es Salaam ili kuweza kuwaondolea wananchi changamoto ya usafiri.

“Tunatafuta mbia mwingine aweze kuingiza mabasi yake kwenye mradi huu ili aweze kuongeza ushindani na nasi tupate kupata huduma bora kwa maana ya ushindani utaongeza huduma bora zaidi,” amesisitiza.Waziri Mkuu ameongeza kuwawako wawekezaji wa ndani na nje ukiwemo Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar Es Salaam (UWADAR) ambao wameonyesha nia na uwezo wa kutoa huduma hiyo na kuufanya mradi huo kutoa huduma kwa ubora unaotakiwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao la sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.“Mheshimiwa Spika Kupitia Bunge lako tukufu, nawaagiza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Maafisa Afya wasimamie zoezi la usafi na kuboresha miundombinu yote na utawapima kupitia zoezi hili,” amesema.

Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kutatua tatizo la usafi wa mazingira pamoja na miundombinu hususani katika masoko hali ya kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakusanya fedha nyingi bila kuboresha maeneo na kukithiri kwa uchafu.

Waziri Mkuu amesema suala la usafi limekuwa likifanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi baada ya kuasisiwa na Rais Dkt. John Magufuli, hivyo ametumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji hao wahakikishe maeneo yao yanakuwa safi na miundombinu inayoweza kutumika wakati wote.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, Mei 10, 2018.

Waziri Mwijage Aainisha Vipaumbele vya Wizara ya Viwanda mwaka 2018/19

WAFANYABIASHARA SOKO LA MAGOMENI WASINYANYASWE-JAFO

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kukamilisha ndani ya muda ujenzi wa soko Jipya la Kinondoni na kuwapa kipaumbele wafanyabiashara 693 waliopo hivi sasa.

Jafo ametaka wafanyabiashara hao wawe wa kwanza kumpatia maeneo ya Biashara bila kunyanyaswa baada ya ujenzi wa soko hilo jipya la kisasa kukamilika.Akizungumza alipotembelea soko hilo leo, Waziri Jafo amesema kuna kasumba imejengeka ambapo masoko yanapojengwa wale waliokutwa sokoni kabla ya ujenzi huwa watatupwa nje na badala yake watu wengine wapya wenye fedha ndio hupatiwa.

"Nataka hawa wananchi waliopo sasa hapa sokoni ndio wawe watu wa kwanza kukabidhiwa maeneo ya biashara baada ya ujenzi kukamilika," amesisitiza Jafo.Waziri Jafo amemwagia sifa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia kwa kuwa ndiye aliyewasilisha kilio cha wanafanyabishara wa Magomeni na serikali imekisikia na kuamua kupeleka fedha.

Pia amewapongeza viongozi wa wilaya ya Kinondoni kwa mshikamano mkubwa chini ya Mkuu wa wilaya yao Ally Hapi na kwamba chini ya Mkuu huyo wilaya hiyo imetulia sana na inasonga mbele na hakuna migogoro ya viongozi inayoweza kurudisha nyuma maendeleo.

Aidha, Waziri Jafo amempongeza pia kwa kuanza utekelezaji wa utoaji wa mikopo kwa Vijana na wanawake bila Riba.Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni imepata Kiasi cha Sh.Bilioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo kutoka serikali kuu katika mpango wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa ameshika orodha ya wafanyabiashara wa soko la Magomeni akisisitiza wapewe kipaumbele baada ya soko kukamilika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kinondoni.
Wananchi wa Magomeni wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo(hayupo pichani).

Muonekano wa soko la Kisasa linalojengwa Magomeni

USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANANCHI NI BURE-NIDA

BENKI YA EXIM YA INDIA YAIPATIA SERIKALI YA TANZANIA MKOPO WA MASHARTI NAFUU

$
0
0
Serikali ya India kupitia Benki ya Exim imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 500, sawa na shilingi Trilioni 1.14 za Tanzania, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 23 ya Tanzania.

Hafla ya uwekaji saini wa mkataba huo imefanyika leo tarehe 10 Mei, 2018 mjini New Delhi, India ambapo Bi. Amina Kh. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango na Bw. David Resquinha, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim walisaini kwa niaba ya Serikali zao..

Miji itakayonufaika na Fedha za mkopo huu ni Muheza, Makambako, Kayanga, Njombe, Manyoni, Songea, Sikonge, Chunya, Kasulu, Kilwa Masoko, Rujewa, Mugumu, Geita, Makonde, Wangingómbe, Handeni , Singida mjini, Kiomboi, Mpanda, Chemba, Mafinga, Urambo-Kaliua pamoja na miji ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba, Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Kh. Shaaban, amesema kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa sababu itawezesha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika miji husika hivyo kusaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko yanayotokana na maji yasiyo salama. 

Aidha, miradi itasaidia kufikiwa kwa malengo na mipango ya Taifa na Kimataifa ya Maendeleo ikiwemo: Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano awamu ya pili (FYDPII) , Mkakati wa Kukuza na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA III) na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDG’s).

Vilevile, amesema uamuzi wa Serikali wa kuboresha huduma za maji umelenga kuwapunguzia Wananchi husususan Wanawake adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji, na hivyo kupata muda wa kutosha kufanya shughuli mbali mbali za maendeleo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Kh. Shaaban kwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim ya India, Bw. David Resquinha wakisaini kwa niaba ya Serikali zao Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 23 ya Tanzania. 
Bi. Shaaban na Bw. Resquinha wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kusaini 
Picha ya pamoja 

TASAF stakeholders meet with Deputy Permanent Secretary Ministry of Finance in Dar es Salaam.

$
0
0

 TASAF stakeholders from World Bank, WFP, DFID, UNICEF, USAID and Government of Tanzania met with the Deputy Permanent Secretary of Ministry of Finance Mr. Khatibu Kazungu yesterday. The main agenda was to share a progress report of the project TASAF is implementing i.e. Production Social Safety Net (PSSN) I and Preparation of PSSN II.  This meeting follows a combined joint mission conducted recently with stakeholders from the Government, Donors and TASAF.

In his remarks the Deputy Permanent Secretary commended TASAF for the achievements obtained so far.  He further highlighted the Government of Tanzania fully supports the initiative done by TASAF as it compliments efforts done by the President Dr. Magufuli to enhance economic activities that will eventually eradicate poverty in the Country and improve living condition of many Tanzanians.


Mr. Muderis Abdallah (first right) from World Bank clarifying a point to the Deputy Permanent Secretary Mr. Kazungu, Listening carefully is Mr. Matteo Caravani from World Food Program
Mr. Ladislaus Mwamanga, Executive director for TASAF (with spectacles), responding to the stakeholders during the meeting.
 Stakeholders listening to a presentation made by Mr. Muderis of the WB, indicating the progress report of what TASAF has done to date and the way forward.

Tanzania Establishes 3,306 Industries by March 2018

$
0
0
Minister of Industries, Trade and Investment, Mr. Charles Mwijage

By Fatma Salum - MAELEZO
A total of 3,306 industries have been constructed by March 2018 following President Dr. John Pombe Magufuli’s vision of realizing middle income by 2025 basing on industrial economy.
This has been revealed by the Minister of Industries, Trade and Investment, Mr. Charles Mwijage while tabling his ministry budget of the Year 2018/ 2019 at the National Assembly in Dodoma City today.
Mr. Mwijage said that the country was fully determined to embark on Industrial Economy which is a shift from Agrarian Economy that had been in place before and after independence.
“Honorable Speaker, when we talk of Industrial Economy, we mean people’s economy and that of things but prioritizing people’s development and having that economy at the centre for enhancing other sectors of development such as agriculture, fishing, mining, forestry and animal husbandry”, said Mwijage.
Minister Mwijage noted further that industrial growth and establishment depends on other facilitating factors that include infrastructure development such roads, railways, aviation, human resources who are heath sounding.
Stressing on agriculture as one of components for industrial development, Mwijage said that Warehouse Management Board and Councils Board have reached the agreement for buying agricultural products such as crops through special centres and assist peasants to ensure quality of their crops and securing information on markets and competitive prices.  He further said that the ministry has made to the point that the price of cashew nut hikes to Tshs 3,880 per kilogram in 2017/2018 compared to Tshs. 3,346 in 2016/2017.
Speaking on attracting investment, Mwijage said that his ministry through the Tanzania Investment Centre has created conducive environment especially by reducing red tapes on investment.
Mwijage said that by July, 2017 to February 2018, TIC has registered 169 new projects worth  capital of USD 107,855,688 expecting to employ 19,799 people.

The ministry has requested the House to approve 143,334,153,648 for Fiscal Year 2018/2019 of which Tshs. 43,309,628,648 is recurrent expenditure while  100,024,525,000 is set for development.

SPIKA DUGAI ALIPOKUTANA NA WALIOKUWA WANAFUNZI WENZAKE WAKATI ANASOMA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana  na waliokuwa Wanafunzi wenzake wakati anasoma Shule ya Sekondari Kibaha, Mkoani Pwani walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Anayesalimiana na Mhe. Spika ni Ndg. Sadiki Alli na wengine kutoka kushoto ni Ndg. Jackson Kalikumtima, Eng. Hussein Mzara na Ndg. David Mchaina.
 Spika wa Bunge  akizungumza na waliokuwa Wanafunzi wenzake wakati anasoma Shule ya Sekondari Kibaha, Mkoani Pwani walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wakwanza kushoto kwa Mhe. Spika ni Ndg. Jackson Kalikumtima, Eng. Hussein Mzara, Ndg. Sadiki Alli na Ndg. David Mchaina.
 Spika wa Bunge  akizungumza na waliokuwa Wanafunzi wenzake wakati anasoma Shule ya Sekondari Kibaha, Mkoani Pwani walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto kwa Mhe. Spika ni Ndg. Jackson Kalikumtima, Eng. Hussein Mzara, Ndg. Sadiki Alli na Ndg. David Mchaina.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na waliokuwa Wanafunzi wenzake wakati anasoma Shule ya Sekondari Kibaha, Mkoani Pwani walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. Wakwanza kulia ni Ndg. Jackson Kalikumtima, Ndg. David Mchaina na kutoka kushoto ni Eng.Hussein Mzara na Ndg. Sadiki Alli.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images