Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAFAFANUA JUU TAARIFA POTOFU KUHUSU WAMASAI LOLIONDO


BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 10.05.2018

AZAM TV: Kilichowatoa Sugu na Masonga chatajwa na kufafanuliwa

DKT. MAHIGA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ISRAEL MHE. BENJAMIN NETANYAHU JIJINI JERUSALEM

$
0
0
Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga kwa ajili ya kufanya mazungumzo jijini Jerusalem, Israel leo.  Wawili hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, elimu, afya, utalii na uwekezaji.

Waziri Mkuu wa Israel, Mhe. Benjamin Netanyahu akiwa tayari kuanza mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga 

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ukiwa katika mazungumzo rasmi na Mhe. Netanyahu.
Pande mbili zikiwa katika mazungumzo.



LIVE: Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania - TAPSEA

NINI UFANYE IKIWA MNUNUZI WA ARDHI YAKO AMESHINDWA KUMALIZIA MALIPO.

$
0
0

Na  Bashir  Yakub.


Ume;muuzia mtu kiwanja au nyumba. Mmeandika mkataba na kuusaini tena mbele ya mwanasheria. Kwenye mkataba mmeweka vipengele vingi  lakini kimojawapo kinahusu umaliziaji wa pesa ya manunuzi.  Hii ni kwasababu mnunuzi amelipa kiasi kidogo na kiasi kingine ameahidi kwenye mkataba kukimalizia baada ya muda fulani.


Mkataba umesainiwa na umekamilika. 

Mda umeenda na kufika ule ambao mnunuzi alitakiwa kumalizia kiasi kilichobaki  lakini bado haoneshi dalili za kumalizia kiasi hicho.  Umejaribu kumkumbusha mara kadhaa lakini maneno yake ni yaleyale  na pesa halipi.  Muda mlioahidiana sasa umepita lakini bado  mnunuzi hajamalizia hela .  Na pengine sasa hapokei hata simu  au hujui aliko au anatoa majibu ya dharau au yasiyoridhisha au vinginevyo.

Nini ufanye katika mazingira kama haya, zipi haki zako, ipi hadhi ya mkataba wenu wa mauziano ambao uliusaini nk, nk. Tutaona hapa chini.


1.KUHUSU KUUZIANA NA KUBAKI NA DENI.

Sheria haikatazi kuuziana ardhi na likabaki deni. Suala hilo limeachwa katika hiari ya muuzaji na mnunuzi.Ni wao watakoamua kuhusu kulipa hela yote au kulipa kiasi na kubaki na deni.  Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mikataba kimesema  mkataba ni halali ikiwa umefanywa na wahusika timamu/kamili,huku wakiuziana kitu halali, na kwa masharti  halali ya kisheria. Basi madhali haya yametimia  jambo la kubaki na deni halikatazwi kisheria.



TAARIFA YA MAONESHO YA NISHATI MBADALA YA MKAA KATIKA WIKI YA MAADHIMISHO SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Watumishi MAELEZO Wakunwa na Huduma TTCL

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Rodney Thadeus akifafanua jambo mbele ya watumishi wa Idara hiyo walipokutana na ujumbe kutoka Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kwa ajili ya kujengewa uelewa kuhusu huduma za Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Afisa Mauzo wa TTCL, Bi. Rahel Mremi na Esther Killango. TTCL ni shirika la Serikali linalotoa huduma za mawasiliano likiwa na kauli mbiu "Rudi Nyumbani Kumenoga."
 Afisa Mauzo wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Bi. Rahel Mremi akionyesha Line za TTCL mbele ya Watumishi wa Idara ya Habari -MAELEZO walipotembelea ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Rodney Thadeus na Afisa Mauzo wa TTCL, Esther Killango(kushoto).


 Afisa Mauzo wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Bi. Esther Killango akifafanua jambo mbele ya Watumishi wa Idara ya Habari -MAELEZO walipotembelea ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Msaidizi wa Mauzo wa TTCL, Bi. Damiana Shemweta, Afisa Mauzo wa TTCL, Bi. Rahel Mremi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Rodney Thadeus(wapili kutoka kushoto). 

 Baadhi ya watumishi wa Idara ya Habari - MAELEZO, kituo cha Dar es Salaam wakifuatilia maelezo kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na Shirika la Simu Tanzania (TTCL) walipotembelewa na maafisa mauzo kutoka shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.

 Afisa Mauzo wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Bi. Rahel Mremi akionyesha moja ya aina ya simu zinazotumika kwa ajili ya huduma ya sauti mbele ya watumishi wa Idara ya Habari -MAELEZO walipotembelea ofisi za Idara hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Rodney Thadeus(katikati) na Afisa Mauzo wa TTCL, Esther Killango.


Msaidizi wa mauzo toka Shirika la Simu Tanzania (TTCL), Bi. Damiana Shemweta akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya huduma na bidhaa za shirika hilo kwa watumishi wa Idara ya Habari -MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO)



TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA UJUMBE WA EU

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (katikati) akieleza jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Ubalozi wa Jumuiya ya Ulaya kujadiliana Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 iliyotolewa na jumuiya hiyo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mkuu Mst. (Znz) Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Giveness Aswile.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage (wa nne kushoto) akifafanua jambo kwa Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) Roeland Van de Geer (wa pili kushoto) na Mtaalau wa Masuala ya Siasa wa EU, Anna Costantin.Ujumbe huo ulifika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam kujadili Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ilyotolewa na jumuiya hiyo.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Asina Omari (wa pili kulia) akiwasilisha taarifa fup kuhusu Tume na majukumu yake kwa ujumbe kutoka Ubalozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) (kushoto) uliofika ofisi za NEC kujadili Taarifa ya Utazamaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 iliyotolewa na jumuiya hiyo.Katikati ni Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage.

Picha na Hussein Makame-NEC

BAGAMOYO YAFANYA TATHMINI YA MAFURIKO -LATU

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani inafanya tathmini ya mafuriko ya mvua yaliyotokea ili waweze kununua dawa kwa ajili ya kuua wadudu wanaoweza kuleta magonjwa mbalimbali yatokanayo na kutuama kwa maji ya mvua.

Hayo yalisemwa Bagamoyo na mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Fatuma Latu wakati wa kikao cha baraza la madiwani.Latu alisema kutokana na tatizo la maji kutuama katika maeneo mengi yakiwemo kwenye makazi ya watu,inabidi kuwekwa dawa ya kuua wadudu hao .

Aidha alieleza athari za mvua ni kubwa , kila kata kupitia madiwani wamekubaliana na madiwani ,kamati husika zitakaa ili kufuatilia suala hilo.Latu alisema kuwa suala hilo lililetwa kwenye baraza kama dharura kutokana na hali ya mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.

Awali Diwani wa kata ya Makurunge Paul Kabile alisema kuwa mvua hizo zimeleta athari kubwa sana kwa wananchi ambapo wamezungukwa na maji ambayo yanaweza kuleta athari ya magonjwa ya mlipuko.Kabile alisema ,athari ni kubwa ambapo baadhi ni uharibifu wa makazi,barabara,miundombinu mbalimbali hali inayofanya wananchi wawe na wakati mgumu kuingia au kutokana kwenye majumba yao.

Naye Diwani wa viti maalum Shumina Abdala alisema kuwa licha ya makazi kuathiriwa na mvua hizo hata taasisi za umma kama shule,zahanati na vituo vya afya.Abdala alisema kuwa kuna haja ya kuwa na dharura juu ya suala la kupatikana dawa za kuwa wadudu wanaoweza kuleta magonjwa kwani uchafu umetapakaa kila mahali.
Mkurugenzi halmashauri ya Bagamoyo,Mkoani Pwani Fatuma Latu akizungumza katika baraza la madiwani.
Baadhi ya madiwani wa wilaya ya Bagamoyo, wakifuatilia kwa makini yaliyojiri katika baraza la madiwani wilayani hapo
Diwani wa viti maalum ,Shumina Abdala (mwenye aliyeaimama mwenye blauzi yekundu)akizungumza jambo wakati wa baraza la madiwani wilayani Bagamoyo.Picha na Mwamvua Mwinyi

Mkuu wa Mkoa Simiyu alishukuru shirika la Amref kwa kubabidhi "Ambulance".

$
0
0
Na BMG
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe.Antony Mtaka amelishukuru na kulipongeza shirika la Amref Health Africa kwa mchango wake mkubwa wa kuboresha huduma za afya katika mkoa huo.

Mhe.Mtaka ametoa pongezi hizo leo Mei 11, 2018 wakati akipokea gari la wagonjwa (Ambulance) lililotolewa na shirika la Amref kwa ajili ya hospitali teule ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa inakabiliwa na ukosefu wa gari hilo.

Mhe.Mtaka amesema shirika hilo kupitia mradi wake wa Uzazi Uzima limesaidia kuboresha huduma mbalimbali za afya mkoani Simiyu ikiwemo ujenzi na ukarabati Zahanati, Vituo vya Afya, wodi (Mama Ngojea) pamoja na kuwajengea uwezo wahudumu wa afya.

Meneja Programu ya Afya ya Mama na Mtoto, shirika la Amref nchini Tanzania Dr.Serafina Mkuwa amesema gari hilo lina thamani ya shilingi milioni 150 pamoja na kodi na kwamba limekabidhiwa kupitia mradi wa Uzazi Uzima unaolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla na baada ya kujifungua.Shirika la Amref Health Africa linatekeleza miradi mbalimbai ya afya hapa nchini kupitia ufadhili ya serikali ya Canada.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Antony Mtaka akipokea Ambulance iliyotolewa na shirika la Amref.
Mkurugenzi wa Shirika la Amref Canada, Onome Ako akitoa salami sake wakati wa makabidhiano ya Ambulance hiyo.
Meneja wa Programu ya Afya ya Mama na Mtoto, shirika la Amref nchini Tanzania Dr. Serafina Mkuwa akizungumza wakati wa shughuli hiyo.

MADAKTARI WAZALENDO WAPATIWA MAFUNZO YA SIKU TATU UBONGO NA UTI WA MGONGO

$
0
0

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 

Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohamed amesema kuwepo kwa Taasisi ya kutibu maradhi ya mishapa ya fahamu na uti wa mgongo (Neuro) hapa Zanzibar ni heshma kubwa na amewashauri wananchi wanaokabiliwa na matitizo hayo kutumia fursa ya kuwepo taasisi hiyo kwenda kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu kwani kinauwezo mzuri wa kutibu maradhi hayo.

Amesema Taasisi hiyo itasaidia kuwajengea uwezo wataalamu wachache waliopo Zanzibar wanaoshughulika na magonjwa hayo na imeipunguzia Serikali gharama ya kuwasafirisha wagonjwa nje ya Zanzibar.Waziri wa Afya ameeleza hayo katika Taasisi ya Neuro iliyopo Hospitali kuu ya Mnazimmoja, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu ya madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka nchi za Afrika zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Amesema kuwepo Taasisi hiyo Zanzibar imeipunguzia Serikali kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mgonjwa mmoja kumsafirisha kwenda kufanyiwa matibabu nje ya Zanzibar na wagonjwa wengi wenyematatizo ya mishipa ya fahamu na uti wa mgongo wanatibiwa bila kutoa malipo.

Waziri Hamad Rashid ameongeza kuwa taasisi hiyo inahitaji madaktari bingwa wazalendo sita na hivi sasa wapo watatu tu na utaratibu wa kuitumia taasisi hiyo kufanya warsha za Kimataifa itawasaidia madaktari wa Zanzibar kuwajengea uwezo zaidi.Amewashauri wananchi wa Zanzibar kujenga utaratibu wa kuvitumia vituo vya afya vya Wilaya na Mikoa kwa matatizo madogo ya kiafya ili Hospitali Kuu ya Mnazimmoja itumike kwa matatizo makubwa yaliyoshindikana kwani Serikali imevijengea uwezo vituo vya vijijini kwa vifaa tiba na dawa muhimu.

Daktari bingwa wa maradhi ya ubongo na uti wa mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Aga Khan Nairobi Kenya Dkt. Mahmood Qureish ambae anaratibu mafunzo hayo amesema Taasisi ya Neuro ya Zanzibar imekuwa maarufu kwa nchi za Afrika Mashariki na wagonjwa kutoka mataifa hayo wanafika kwa ajili ya matibabu.

Amesema mafunzo ya Taasisi ya Neuro ya Zanzibar ambayo ni ya kwanza kufanyika yataendeshwa darasani na vitendo katika vyumba vya upasuaji ili kuwajengea uwezo washiriki kufanya matibabu ya ubongo na uti wa mgongo watakaporejea nchini mwao.Mafunzo hayo yanawashirikisha madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka Kenya, Sudan, Afrika Kusini, Zimbabwe Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed akifungua warsha ya siku tatu ya Madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka mataifa ya Afrika chini ya Jagwa la Sahara inayofanyika Taasisi ya Neuro iliyopo Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka mataifa ya Afrika chini ya Jagwa la Sahara waliohudhuria katika mkutano unaofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed katikat alievalia suti rangi ya krimu akipiga picha ya pamoja na Madaktari wa mishipa ya fahamu na uti wa mgongo kutoka mataifa ya Afrika chini ya Jagwa la Sahara (Picha na Abdalla Omar 
Daktari bingwa wa maradhi ya ubongo na uti wa mgongo kutoka Chuo Kikuu cha Aga Khan Nairobi Kenya Dkt. Mahmood Qureish ambae anaratibu mafunzo hayo akizungumza na waandishi wa habari (Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar).

MAKAMISHNA WASTAAFU POLISI WAAGWA RASMI KWA GWARIDE MAALUM

$
0
0
 Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda wakiwaaga Maofisa na Askari Polisi huku wakisukumwa katika gari maalumu wakati wa Gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi.Gwaride hilo lilifanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam . 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na IGP Mstaafu Omar Mahita wakati hafla maalum ya kuwaaga  Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi).

 Kamishna Mstaafu wa Polisi Clodwing Mtweve akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake wakati wa hafla maalum ya kumuaga baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam  (Picha na Jeshi la Polisi).


Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla maalum ya kuwaaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).

 Askari wa Kikosi cha Kutuliza ghasia FFU wakitoa heshima wakati  wa gwaride maalam la kuwaaga Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifurahia jambo na Makamishna wastaafu Clodwing Mtweve (katikati) na Elice Mapunda (kushoto) wakati wa hafla maalum ya kuwaaga baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).

SUMAJKT KUINUA UCHUMI WA HANANG,MANYARA

$
0
0
Na Mahmoud Ahmad,Hanang.

Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la KujengaTaifa(SUMAJKT) linakusudia kujenga hoteli kubwa ya kisasa yenye hadhi ya nyota tano na miradi mingine mikubwa ya kiuchumi wilayani Hanan’g mkoani Manyara kwa lengo la kuinua kiuchumi wilaya hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT Brigedia Jenerali Charo Yateri aliyasema hayo jana katika hafla fupi ya kutia saini makubaliano ya kufanya uwekezaji wilayani Hanang kati ya SUMA JKT na Halmashauri ya wilaya ya Hanang yaliyofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Halmashauri hiyo.

Alisema kuwa wameamua kuwekeza wilayani Hanang kwa kuwa kuna fursa kubwa za uwekezaji ikiwemo upatikanaji wa ardhi isiyo na migogoro,mandhari nzuri ya kuvutia na hali ya hewa inayofaa kwa kilimo na ufugaji ambapo kupitia miradi yake inayotekelezwa eneo hilo litawafaa .

Kwa mujibu wa Brigedia Yateri Makubaliano hayo ya uwekezaji yatahusika katika ujenzi wa miradi mingine ya kiuchumi ya Karakana ya zana za kilimo, Duka la vipuri vya matrekta, uuzaji wa matrekta,Kituo cha mafuta,Kilimo, Kiwanda cha usindikaji wa nafaka.

Alisema kupitia uwekezaji huo viongozi kutoka makao makuu ya nchi Dodoma watapata nafasi ya kulala katika hoteli hiyo ya kisasa wakiwa na familia zao pasipo kuwa na mwingiliano wa watu wengi jambo ambalo litaongeza mzunguko wa fedha kwa wakazi wa Hanang.

Alisema watu wengi wamekuwa hawajui shirika hilo kuwa ni la umma na la serikali, lina Nyanja nyingi za kufanya kazi pamoja na jamii kuanzia kwenye kilimo ambapo awali liliendesha mashamba yaliyokuwa ya JKT kwa sasa yametengenishwa kwa ajili ya kuzalisha chakula na kuelimisha wananchi kuzalisha chakula kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kulisha vijana wanaojiunga na JKT.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI,RAIS DKT. MAGUFULI AKIWA KATIKA OFISI NDOGO ZA CCM LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 . Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Philip Mangula katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati akiondoka akiwa katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.


YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Mwenyekiti wa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge  akiongoza kikao cha ishirini na saba cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Mtera Mhe.Livingstone  Lusinde akiuliza swali wakati wa kikao cha ishirini na saba cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Asunga akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge wakati wa  kikao cha ishirini na saba cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Stanslaus Nyongo ,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk Ashatu Kijaji na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt Mary Mwanjelwa wakati wa  kikao cha ishirini na saba cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Vunjo Mhe.James Mbatia akifurahia jambo na wabunge wenzie  wakati wa kikao cha ishirini na saba cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
Mbunge wa Kwimba Mhe.Mansoor Hirani akizungumza jambo na Manaibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.Josephat Kandege na Joseph Kakunda wakati wa  kikao cha ishirini na saba cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO

MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI

$
0
0
Na Mahmoud Ahmad Dodoma

Imeelezwa kuwa Ukuaji wa sekta ya utalii hapa nchini, umedhihirika mapato yatokanayo na utalii kuongezaka kutoka Dola bilioni 1.7 mwaka 2012 hadi kufikia Dola bilioni 2.2 mwaka 2017. 

Ongezeko la mapato hayo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka 1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,327,143 mwaka 2017. Ambapo Sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni (foreign exchange earnings).

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkta Hamis Kigwangala wakati akifungua kongamano la kupitia rasimu ya sera ya Taifa ya utalii ya mwaka1999 linalofanyika jijini hapa na kuwashirikisha wadau wa sekta ya utalii nchini kutoka sekta binafsi na za umma.

Kigwangala amesema kuwa maboresho hayo yaende sambamba na mwendelezo wa mchakato wa kazi nzima ya kupitia Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 ambayo ni muhimu kwa mstakabali wa sekta ya utalii hapa nchini ambayo Kama ilivyoelezwa hapo awali, mojawapo ya dhumuni la msingi la hatua hiyo linalenga kuwa na Sera inayoendana na mabadiliko ya kiuchumi, mazingira, tecknolojia, kijamii na kisiasa yanayotokea ndani na nje ya nchi yetu ambayo yanagusa maendeleo ya sekta ya utalii nchini.

Amesema kuwa warsha imejumuisha Wadau mbalimbali wa Sekta ya Umma na Binafsi ambao kwa namna moja au nyingine huguswa au hushiriki katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Aidha, kama mnavyofahamu, utalii ni sekta mtambuka na ili kufanikisha ukuaji wake unahitajika ushirikiano thabiti baina ya wadau wote. Ushirikiano huu utaweza kuleta matokeo chanya iwapo kuna Sera madhubuti ambayo mchakato wake wa maandalizi umeshirikisha wadau kikamilifu.

ABINBEV NA WASHIRIKA KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KWA WAKULIMA WADOGO

$
0
0
Ni kutokana na matumizi ya teknolojia za kisasa Wataalamu mbalimbali walioudhuria kongamano la The East Africa (EA) Innovation Event la kampuni mama ya TBL Group ya ABInBev lenye lengo la kuleta mapinduzi ya kilimo kupitia sayansi na teknolojia lililoandaliwa na taasisi ya Bits&Bites Technology Convention na kufanyika jijini Dar es Salaam, wamedhihirisha kuwa mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo nchini na barani Afrika kwa ujumla yanawezekana kupitia matumizi ya teknolojia za kisayansi. 

 Kongamano hilo ambalo lilijumuisha wataalamu wa fani ya kilimo,watafiti,wahandisi na wabunifu kutoka kanda ya Afrika Mashariki walijadili jinsi ya kupata ufumbuzi wa kuinua kilimo cha wakulima wadogo kupitia teknolojia za kisasa na za gharama nafuu ambapo pia walishiriki shindano la ubunifu wa nyenzo za kiteknolojia ambapo walipata fursa ya kuwasilisha kazi zao walizogundua.

 Makampuni ya Imara Tech,Mobisol na Back Save Equipment yaliibuka na ushindi baada ya jopo la majaji waliokuwa wanasimamia shindano hilo kubainisha kuwa ugunduzi wao wa nyenzo za kiteknolojia unaweza kusaidia kuinua maisha ya wakulima wadogo.Kazi zilizowapatia ushindi washiriki zitaanza kufanyiwa majaribio kabla ya mchakato wa kuzifikisha kwa walengwa ambao ni wakulima hususani wadogowadogo.

 Akiongea wakati wa kufunga kongamano hilo, Mkurugenzi wa taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Godfrey Sembeye, alisema kuwa kongamano hili limefanyika kwa wakati mwafaka ambapo Tanzania inajipanga kuingia katika uchumi wa viwanda ambao unaenda sambamba na kufanya mapinduzi ya kilimo kwa ajili ya kupata malighafi ya viwanda vitakavyoanzishwa,pia kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha.

 Sembeye, alisema njia pekee ya kuleta mapinduzi ya kilimo ni kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa na za gharama nafuu ambazo wakulima wengi wa hali ya chini wanaweza kumudu kuzinunua na kuzitumia kwa ajili ya kuwawezesha kupata tija na ufanisi katika kazi zao. 
Washindi wa shindano la ubunifu wa kiteknolojia katika picha ya pamoja na mgeni rasmi baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

BAADHI YA WABUNGE WAWAKILISHI JUKWAA LA KIBUNGE NCHI ZA MAZIWA MAKUU KUTOKA TANZANIA WAKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KATIKU MKUU WA NCHI ZA UKANDA HUO

$
0
0

 Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Najma Giga (kushoto) akimsikiliza na mgeni wake Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu Mhe. Onyango kakoba (kulia) alipomtembelea leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma. 
 Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Najma Giga (kulia) akisalimiana na mgeni wake Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu Mhe. Onyango kakoba (kushoto) alipomtembelea leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu Mhe. Onyango kakoba, akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuzungumza na Wabunge wawakilishi kwenye Jukwaa la Kibunge kwenye nchi za Maziwa Makuu ambao pia ni Wabunge wa Bunge la Tanzania katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.

Baadhi ya Wabunge wawakilishi kwenye Jukwaa la Kibunge kwenye nchi za Maziwa Makuu ambao pia ni Wabunge wa Bunge la Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mhe. Najma Giga (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni wao Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu Mhe. Onyango kakoba (wa pili kushoto) na msaidizi wake Ndg. Jenny Mbodi (kulia)

(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

BALOZI SEIF ALI IDD AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TAPSEA, ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akitoa hotuba yake katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja,  Zanzibar leo. 
 Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd wakati akitoa hotuba yake katika Ufunguzi wa Mkutano wao Mkuu, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.
 Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee na Wanawake - Zanzibar, Modlen Kastiko akizungumza na kuwahusia Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), katika Mkutano wao Mkuu, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Doroth Mwaluko akisisitiza jambo katika Mkutano Mkuu Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akihamasisha jambo kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu Chama hicho, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.
Wajumbe wa Chama Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakifurahia jambo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wa pili kushoto) akimpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga, kwa hotuba yake aliyoisomba mbele ya Mkutano Mkuu Chama hicho, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Doroth Mwaluko na Kulia ni Katibu Mkuu wa TAPSEA, Festo Melikiory.
  Sehemu ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakifatilia hotuba ya Mgeni Rasmi.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images