Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

VOA Swahili: Duniani leo Mei 9, 2018


THE 8TH INTERNATIONA: TÜBINGEN AFRICA FESTIVAL 2018 IN GERMANY IT IS NOW OFFICIALLY OPEN FOR REGISTRATION & PARTICIPATION.

$
0
0
The 1 year break is over, its time to get back to business as usual and this time on a big note. The festival is now called GAIEXPO as it has included African Small and Medium enterprises worldwide. This sector shall promote the continent Africa not just as tourist but  business destination with endless opportunities in sectors such as Agriculture, Agri-business -food,Tourism, Arts and Culture etc. 

We are calling on all small businesses and enterprises, Africa and Diaspora Entrepreneurs, Traders, workshops givers, trainers, Artist, panelist... in Africa, Germany, Europe & USA to register and participate. GAIEXPO is an African market and meeting place open to countries, companys, Ngo´s with interest in sub-Sahara Africa to share contacts, information, network and do deals.  
We look forward to meeting you in Tübingen, Germany 2018 contact:

Susan Tatah
Managing Director

MAAMBUKIZI YA VVU YAPUNGUA KWA ASILIMIA 3-WAZIRI UMMY

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA LEO MEI 9, 2018

Tanzanian Foreign Minister visits Save a Child's Heart in Israel today

$
0
0
The Minister for Foreign  Affairs and East African Co-operation Dr. Augustine Philip Mahiga today visited Save a Child’s Heart at the Wolfson Medical Center in Jerusalem and nearby Children’s Home. During his visit he met  with Dr. Anat Engel, director of Wolfson Medical Center, and the hospital's dedicated medical team that treats children from Israel and around the world.
Dr. Mahiga also met children from Zanzibar and mainland Tanzania, Ethiopia, Romania and Myanmar receiving treatment there and he spoke with their mothers and wished everyone a quick recovery.

The Minister met doctors and nurses who participate in the Save a Child’s Heart training program, one of which was Dr. David Silvera, a young physician from Tanzania who is training to become a pediatric cardiac surgeon. Dr. Silvera will return to Tanzania in three years and join the local team. Most of the local team, at JKCI hospital in Tanzania, was trained in Israel by Save a Child’s Heart and, today, treat children independently. They are led by Tanzania’s first pediatric cardiac surgeon, Dr. Godwin Godfrey, who completed a 5-year training program with Save a Child's Heart at Wolfson Medical Center in Israel.
The Minister also met other medical team members who are currently training in Israel. Among them were two nurses from Tanzania, a surgeon from Ethiopia and a pediatric cardiologist from Kenya.
Before the visit was finished, the executive director of Save a Child’s Heart, Simon Fisher, thanked the Minister and said: “Save a Child's Heart serves as a bridge between the Wolfson Medical Center in Israel and the Jakaya Kikwete Cardiac Institute in Tanzania. Together, with the team at JKCI under the leadership of Prof. Janabi, Save a Child's Heart is creating a Sub-Saharan Center of Medical Excellence at JKCI hospital for children suffering from cardiac disease in Tanzania and neighboring countries. With the support of the government of Tanzania and the government of Israel, we are turning a dream into reality”.
Since 1999, Save a Child’s Heart has treated more than 700 children from Tanzania & Zanzibar and trained a pediatric cardiac team that includes a surgeon (a second one is currently training in Israel), three pediatric cardiologists, two pediatric anesthesiologists, an intensivist, four perfusionists and dozens of nurses.
During the last four years and as part of this Israeli-Tanzanian cooperative effort, Save a Child’s Heart has held more than ten medical missions in Tanzania for the purposes of both training and working with the local team. During these missions abroad, dozens of Tanzanian children have undergone lifesaving heart surgery and catheterization. 

About Save a Child’s Heart
Save a Child’s Heart is an Israeli-based international non-profit organization, with special consultative status granted by the United Nations Department of Economic and Social Affairs (ECOSOC) and recent recipient of the 2018 prestigious United Nations Population Award. Save a Child’s Heart was founded in 1995 at the Wolfson Medical Center in Holon, Israel, with the mission of improving the quality of pediatric cardiac care for children in developing countries and creating centers of competence in these countries. Save a Child’s Heart’s goal is to improve the health and welfare of all children, regardless of the child's nationality, religion, color, gender or financial situation.
Save a Child's Heart holds preoperative and follow up cardiology clinics in Israel and abroad on a weekly basis, offers a comprehensive training program within Israel for doctors and nurses from developing countries and leads surgical and teaching missions to partner countries.
To date, Save a Child's Heart have saved the lives of more than 4,700 children from 56 countries in Africa, South America, Europe, Asia, and throughout the Middle East and trained more than 150 medical team members from these countries
Save a Child’s Heart is currently building an international pediatric cardiac center at Wolfson Medical Center. The new center will enable Save a Child’s Heart to save more children and will also serve as a children’s hospital to improve the conditions for the Israeli children from the area.

 The Minister for Foreign  Affairs and East African Co-operation Dr. Augustine Philip Mahiga (seated second right) with members of staff of the  Save a Child’s Heart  and doctors and nurses who participate in the Save a Child’s Heart training program at the Wolfson Medical Center in Jerusalem on Wednesday, together with the ambassador of Tanzania to Israel Hon Job Masima ( seated second left) and Mr Suleiman Saleh (seated right)
The Minister for Foreign  Affairs and East African Co-operation Dr. Augustine Philip Mahiga when he visited Save a Child’s Heart at the Wolfson Medical Center in Jerusalem and met children from Zanzibar and mainland Tanzania, Ethiopia, Romania and Myanmar receiving treatment there and he spoke with their mothers.

Kwa kocha Sir Alex Feguson Wiki chache zinazokuja ni muhimu sana: Kutokwa Damu kwenye/ndani ya Ubongo, Maswali na Majibu

$
0
0
Sir Alex Ferguson
 Ni sahihi familia ya Sir Feguson kutopenda kuzungumzia hali ya mgonjwa wao (Sir Alex) baada ya kukimbizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji wa ubongo.

Lakini kwa mtu wa umri wake na historia ya tatizo la moyo alilonalo ikumbukwe mwaka 2003 Sir Alex aliwekewa betri ya moyo (Pacemaker). Sababu kubwa itakuwa kuvuja damu ndani ya ubongo ambayo husababisha adhari zisizoweza tibika( irreparable damage to those cells).
Kwa ugonjwa wa Sir Alex, madaktari walifanya maamuzi ya kufanya upasuaji kwa sababu walihisi uvujaji wa damu ndani ya ubongo ulikuwa unaharibu sehemu zingine za ubongo.  Hii huwa inahatarisha uhai wa mgonjwa. Upasuaji huu husaidia kupunguza adhari za muda mrefu kwa Sir Alex ambazo anaweza kuzipata (kutoweza kuzungumza sawa sawa, kupooza upande mmoja n.k) kifupi alichopata ni kiarusi/stroke).
Sir Alex ugonjwa wake kwa vasilimia 100% ni mishipa kupasuka ndio maana maamuzi yalikuwa kupasua ingekuwa ni mishapa kuziba mara nyingi upasuaji huwa haufanywi.

Nini kilicho sababisha?
sababu ni nyingi kwa mfano:
1. Udhaifu wa mishipa ya damu ndani ya ubongo, 2. Ugonjwa ndani ya ubongo, 3. Hitilafu katika  ugandaji wa damu (clotting disorders au damu kuwa nyepesi ) labda kwa dawa alizo kuwa anatumia k.m Asprin, clopidogrel nk. Kwa hiyo kila mgojwa anakuwa na sababu tofauti na mwingine.



Siku au wiki chache baada ya upasuaji huu ni muhimu sana kwa mgonjwa kuangaliwa kwa ukaribu kwa mfano damu inaweza toka tena (rebleed).
Kama mgonjwa hajapoteza maisha lakini kapooza au hasemi vizuri na hakujarekebishika kwa wiki au miezi kadha uwezekano wa mgonjwa kurudia shughuli zake za kawaida mara nyingi ni vigumu sana.  Kubwa kama madaktari kuna sababu zote za kuendelea kupigania maisha ya mgonjwa husika.
Nini maana ya kutokwa damu kwenye/ndani ya Ubongo?
Maana yake ni kuvuja damu kwenye/ndani ya ubongo(A brain haemorrhage is bleeding in or around the brain).  Inasababisha kuvimba kwa ubongo kwa sababu ya mkusanyiko wa damu (hematoma) hii itapelekea kupanda kwa presha ndani ya ubongo na kupunguza mzunguko wa damu ndani ya ubongo.  Dalili zake zitakuwa sawa na mtu aliyepata kiarusi (Stroke) yaani upungufu wa nguvu/kupooza upande mmoja wa mwili. Mara zingine wagonjwa watasikia kichwa kuuma sana, kutoo weza kusema/kuzungumza vizuri na kutoona vizuri pia.
Nini kinasababisha kutokwa damu kwenye/ndani ya Ubongo?
Kuna sababu nyingi ya kutokwa damu kwenye/ndani ya Ubongo.  Inaweza damu kutoka yenyewe (spontaneous) kwa kupasuka mishapa ya damu  (ruptured aneurysm), inajulikana kama Kiarusi/stroke.  Sababu zingine ni shinikizo la damu, ambalo husababisha mishipa kuwa dhaifu na kupasuka.
Upasuaji wa ubongo nini kinafanywa na je unasaidia?
Baadhi ya wagonjwa wa hili tatizo wanahitaji upasuaji kupunguza pressure ndani ya ubongo. Upasuaji huu unapunguza/unatoa damu iliyovuja ndani ya ubongo wakati huohuo madaktari wanarekebisha mishipa iliopasuka (repair).  Kuna njia kadha za upasuaji ili kupunguza/kutoa damu ndani ya ubongo 1. Kupasua kichwa na kuitoa damu 2. Kutoboa tundu dogo na kuivuta damu iliyovuja ndani ya ubongo.

Nini matokeo ya upasuaji huu wa ubongo?
Matokeo ya upasuaji huu unategemea vitu vingi k.m. sehemu gani ya ubongo umetoka damu, kiasi gani cha damu kimetoka n.k. Wagonjwa wengi hawatakufa kwa tatizo hili lakini kupona kunaweza kuchukua muda mrefu wiki/miezi kadha  mpaka miaka au kutopona kabisa (yaani kuweza kuzungumza sawa sawa, kutembea sawa sawa , au kutumia kikamilifu upande wa mwili uliopooza.
Kila la kheri Sir Alex Ferguson
Mohamed Janabi MD., PhD., FACC
Mpenzi wa mpira wa miguu (Soccer)

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dar es salaam

SERIKALI YATOA SIKU TATU KWA WALIOFICHA MAFUTA NA SUKARI, yasisitiza kamwe haitokubali kuchezewa na wafanyabiashara wasio waaminifu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa wafanyabiashara na wenye viwanda vya mafuta ya kupikia na sukari nchini kuhakikisha bidhaa hizo zinaendelea kupatikana katika maeneo yote na katika bei ya kawaida. 
“Natoa siku tatu kuanzia kesho Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi mafuta yote yaliyoko bohari yaondolewe yaendelee kusambazwa kama kawaida nchini kote ili kuondoa uhaba uliojitokeza na kamwe Serikali haitokubali kuchezewa na wafanyabiashara wasiowaaminifu,” 
Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatano, Mei 9, 2018) Bungeni Jijini Dodoma mara baada ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage kutoa kauli ya Serikali kuhusu uhaba wa mafuta ya kupikia nchini.

Amesema kama uhaba wa bidhaa hiyo utaendelea, ifikapo Jumapili Serikali itaanza kufanya msako kwenye viwanda na maghala na kuchukua hatua kali kwa watakaobainika kuficha mafuta hayo. 
Waziri Mkuu amesema takwimu zinathibitisha kwamba mafuta ya kupikia yaliyoingizwa nchini yanatosha, hivyo nchi haipaswi kuwa na uhaba. Amesema kwa mwezi mafuta yanayotumika nchini tani 28.9 na kila mwezi zinaingizwa tani 30,000.  
“Hatuwezi kukubaliana na jambo hili kwa sababu haliko kwa bahati mbaya ni mpango uliopangwa kwani imekuwa ni kawaida kila tunapoelekea kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kunakuwa na upungufu wa bidhaa hasa sukari, hivyo Serikali haitakubali wananchi wateseke bila sababu za msingi,” amesisitiza.  
Akiwasilisha kauli ya Serikali Bungeni, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Mwijage alisema vyanzo vinavyotumika kuzalishia mafuta nchini vinatosheleza mahitaji kwa asilimia 30, hivyo asilimia 70 ya mafuta huagizwa kutoka nje ya nchi. 
“Miezi mitatu ya mwanzo kwa mwaka huu kuanzia Januari wastani wa mafuta yaliyoingizwa ni tani 30,210.71 kwa mwezi na jumla ya akiba ya mafuta yaliyopo nchini ni wastani wa tani 68, 902, hivyo hakuna upungufu,” alisema.

KUFUNGWA KWA CHOO STENDI YA BAGAMOYO KWASABABISHA KERO KWA WATUMIAJI, HALMASHAURI YAAHIDI KUKIFANYIA KAZI BAADA YA MVUA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
Baadhi ya watumiaji wa choo cha stendi ya Bagamoyo ,mkoani Pwani wameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuharakisha mchakato wa ukarabati wa choo hicho ambacho hakitumiki kwa takriban wiki tatu sasa.
Choo hicho kimefungwa na halmashauri hiyo baada ya kufurika maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo watumiaji wanahofia magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosa huduma hiyo na kusababisha baadhi ya watu kujisaidia kiholela.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye stendi hiyo watumiaji hao wakiwemo wasafiri,madereva na mama lishe  walisema kukosekana kwa huduma hiyo ni hatari kwa afya za wananchi. Agnes Robert ambaye ni mama lishe kwenye stendi hiyo alisema kukosekana kwa huduma hiyo ni changamoto kubwa kwao na kwa wateja wao wanaopata huduma kwenye migahawa yao.
"Tunapata shida kwa wateja wetu ambao wengi ni abiria wakishuka kwenye mabasi huhitaji huduma ya choo kabla ya kupata riziki ya chakula. Tunapowaambia hakuna choo wanalalamika sana hivyo tunaiomba  halmashauri iangalie namna ya kufanya ukarabati kwa haraka" alisema Agnes.
Dereva wa mabasi yanayofanya safari Kiwangwa ,Fikiri Mohammed alieleza kutokana na vyoo kufungwa baadhi ya watu wamekuwa wakijisaidia kiholela kwenye eneo la stendi. Alisema kwamba ,wanahofia hali hiyo  inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko. "Uchafu na maji ya chooni yanazagaa hii ni hatari kwa watu wanaotumia stendi ,choo bora ni kitu muhimu sana hapa kwa afya zetu" alisema Mohammed.
Akijibu malamiko hayo, mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu alisema changamoto hiyo imetokana na eneo hilo kuwa na chemchem inayotoa maji na kufanya eneo hilo kujaa maji.Alielezea ,tayari wameshafanya uchunguzi na kuangalia sehemu nyingine ya eneo pembeni kwa ajili ya kuchimba shimo lingine ambalo halitapitisha maji.
Kwa mujibu wa Latu ,wanaendelea na mchakato na wanatarajia kutumia zaidi ya milioni tatu (3), kwa ajili ya shimo hilo ambapo fedha zitatokana na mapato ya ndani.Latu alisema ,ujenzi huo utaanza kufanyika mara baada ya mvua zinazoendelea kunyesha zitakapo kwisha kwani kwa sasa ujenzi hautaweza kufanyika.
Aliwaasa watu kuacha kujisaidia kiholela na kuwasihi kutumia vyoo vilivyo jirani na stendi hiyo huku wakisubiri mvua hizo ziishe,ili ukarabati ufanyike.
 Mandhari ya  stendi ya Bagamoyo
Choo cha stendi ya Bagamoyo kilivyo baada ya kufungwa

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 09.05.2018

Dkt, Mahiga atembelea taasisi ya Save the Children Haert ya Israel

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameshukuru Ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kuokoa maisha ya watu wengi nchini, hususan watoto.

Waziri Mahiga alitoa shukrani hizo leo alipoitembelea taasisi hiyo jijini Tel Aviv, Israel akiwa anaendelea na ziara yake ya siku tatu aliyoianza jana. "Zamani nilijua kuwa mtu akizaliwa na maradhi ya kurithi, mtu huyo hawezi kuishi lazima atakufa, lakini uwepo wa taasisi yenu kumenifanya niondoe itikadi hiyo" Dkt. Mahiga alisema.

Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart imeisifu Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuwa ni moja ya Taasi bora kusini mwa Jangwa la Sahara na kwamba ina uwezo na wataalam wa kufanya upasuaji bila ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi. "Serikali inachotakiwa kufanya ni kuiboresha taasisi hiyo kwa kujenga majengo mapya na kuipatia vifaa zaidi na itakapofanya hivyo itaokoa maisha ya watu na fedha nyingi ambazo zingelitumika kugharamia matibabu nje ya nchi". Mkurugenzi wa taasisi hiyo alishauri.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo alimweleza Dkt. Mahiga kuwa taasisi ilianzishwa miaka ya 90 kwa madhumuni ya kuokoa maisha ya watoto wenye maradhi ya moyo duniani kote, hususan katika nchi zinazoendelea. Hadi sasa imeshatoa matibabu kwa zaidi ya watoto 460,000 wenye maradhi ya moyo kutoka Afrika, Amerika, Asia na kwingineko.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akiongea na wawakilishi wa Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel mara baada ya kuwasili katika taasisi hiyo kujionea namna inavyoendesha shughuli zao. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimjulia hali mmoja wa watoto kutoka Tanzania anayepata tiba ya maradhi ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Save the Children Heart ya Israel 
Kutoka kulia, mtu wa kwanza na wa pili ni Watanzania wanaosomea fani za tiba za maradhi ya moyo katika taasisi ya Save the Children Haert wakiongea na Mhe. Waziri wakati alipoitembelea taasisi hiyo jijini Tel Aviv, Israel leo. 
Wanne kutoka kushoto ni wanafunzi kutoka Tanzania wanaosomea fani ya tiba ya maradhi ya Moyo wakimsikiliza Mkurugenzi wao hayupo pichani. 
Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe akibadilishana mawasiliano na wanafunzi wanaosomea fani ya tiba ya maradhi ya moyo kutoka Tanzania. 

TAARIFA YA UAPISHO KUTOKA IKULU

CALL TO PARTICIPATE IN THE FIRST NATIONAL SKILLS DEVELOPMENT WORKSHOP AT JNICC DAR ES SALAAM 10th MAY 2018

KUMBILAMOTO ACHOCHEA MAENDELEO KWA KUTOA MITAJI VIKUNDI VYA WANAWAKE NA VIJANA VINGUNGUTI

$
0
0
--
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto akizungumza kabla ya kukabidhi Mitaji na Vifaa vya Michezo kwa Vikundi vya Kinamama na Vijana vya Kata ya Vingunguti hili viweze kuchochea Maendeleo katika Kata hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi Cuf kata ya Buguruni, Mbegu Simba akizungumza namna Diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya chama chake anavyotekeleza ahadi alizoahaidi. 
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto akikabidhi zawadi ya jezi za Mpira wa Miguu kwa Mwanamuziki wa Singeli Nchini Msaga Sumu kwa ajili ya Timu ya Misosi inayoshiriki Ndondo Cup.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto akikabidhi mizani ya kupimia mchele kwa Kikundi cha Vicoba cha wanawake kata ya Vingunguti.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto akikabidhi mabirika na chupa kwa mmoja wa wadu wa kijiwe cha Kahawa katika kata ya Vingunti ambe msingi wake ulichukuliwa na maji.
 sehemu ya Wanawake wa Vikundi Mbalimbali wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto kwa ajili ya kupokea uwezeshwaji wa Maendeleo.

MAFUNZO YA KUKABILI MAKOSA YA KIJINSIA NA WATOTO KWA MAKAMANDA WA POLISI YAENDELEA DAR

$
0
0
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi Hasina Tawfiqi akichangia mada wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
 Mrakibu wa Polisi, Faidha Suleman kutoka Dawati la Jinsia na Watoto akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Naibu Kamishna wa Polisi Charles Mkumbo akichangia mada wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Henry Mwaibambe akichangia mada wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto, Naibu Kamishna wa Polisi, Maria Nzuki akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto (Picha na Jeshi la Polisi).

Waziri Dkt. Mahiga afanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga wa kwanza kulia na akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima na Afisa Dawati wa Israel, Bi Kisa Mwaseba wakiwa katika mazungumzo na ujumbe wa Israel. 
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman wa kwanza kulia akisisitiza jambo kwenye mazungumzo hayo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akikabidhi zawadi kwa Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman walipokutana jijini Tel Aviv leo asubuhi. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga naye akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Israel, Mhe. Avigdor Liberman jijini Tel Aviv leo asubuhi. 
Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe akisalimiana na Waziri wa Ulinzi wa Israaele, Mhe. Avigdor Liberman. 



MGOGORO WA WAKAZI WA PUGU NYAMWEZI WAPATIWA UFUMBUZI

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ametatua mgogoro mkubwa ambao umedumu kwa muda mrefu kati ya wakazi wa eneo la Pugu Nyamwezi na mmiliki wa eneo hilo Bibi Jeshri Rawel.

Waziri Lukuvi ametoa maamuzi ya kuwataka Wakazi wa eneo hilo ambao wamejenga katika shamba la mmiliki huyo lenye ukubwa wa hekari 40 na kuweka makazi yao kulipia gaharama za umilikishwaji ardhi ili waweze kupatiwa haki ya kumiliki eneo hilo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa eneo la Pugu Nyamwezi lenye ukubwa wa hekari 40 ambalo mmiliki wake ni Bibi Jeshri Rawel (kulia kwa waziri) ambaye anadai kuvamiwa na wakazi hao.

YALIYOJIRI BUNGENI LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akimsikiliza Mbunge wa Songea Mjini Mhe Dkt  Damas Ndumbaro wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu Bungeni leo Jijini Dodoma. 
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Nishati wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe wakati wa kikao cha ishirini na sita cha mkutano wa kumi na Moja leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage akionyesha kitabu chenye idadi ya Viwanda vyote nchini wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019.Kitabu hicho kina kurasa mia tisa.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Sumve Mhe.Richard Ndassa  wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)  walipomtembelea leo Bungeni.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe akimskiliza Mbunge wa Sumve Mhe.Richard Ndassa Bungeni leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA

WAZIRI UMMY ATOA TAARIFA KUHUSU UGONJWA WA EBOLA LEO JIJINI DODOMA

$
0
0


 Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akitoa taarifa kuhusu Ugonjwa wa Ebola leo Jijini Dodoma,kulia ni Mkurugenzi wa Tiba dkt. Dorothy Gwajima
Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akitoa taarifa kuhusu Ugonjwa wa Ebola leo Jijini Dodoma,kushoto ni Mkurugenzi huduma za Kinga dkt.Leonard Subi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA NA KATIBU TAWALA WA MKOA WA TABORA LEO

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora  kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mhe. Alphayo Kidata  aliyemuapisha kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora   wakila kiapo cha ahadi na uadilifu kwa viongozi wa umma kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuwaapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza  baada ya kuwaapisha  Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja baada ya kuwaapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018. Kulia ni  Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe.  Selemani Jaffo na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya kuwaapisha Mhe. Alphayo Kidata kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Mhe. Msalika Robert Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018.Wengine mbele Kulia ni  Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe.  Selemani Jaffo na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na  Mhe. Alphayo Kidata aliyemuapisha kuwa balozi wa Tanzania nchini Canada  na Balozi wa Tanzania nchini  Canada aliyemaliza muda wake Mhe. Jack Zoka  kwenye hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 10, 2018. 
Picha na IKULU

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali Bungeni jijini Dodoma, Mei 10, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia, Bungeni jijini Dodoma, Mei 10, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah Salim,  Bungeni mjini Dodoma,  Mei 10, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Bungeni mjini Dodoma, Mei 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akiwasilisha  Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo, Bungeni mjini Dodoma, Mei 10, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulie (kulia), na wabunge wa Viti Maalum, Faida Bakari na Anna Lupembe (wapili kulia) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 10, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 10, 2018.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images