Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

TPDC yawanoa viongozi wa dini kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia

$
0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendeleza utaratibu wake wa kutoa elimu zaidi juu ya sekta ya gesi asilia na mafuta kwa wadau mbalimbali safari hii ikiwa ni kwa viongozi wa dini kutoka Mkoa wa Lindi. Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba, Meneja Mawasiliano wa TPDC, Bi. Marie Msellemu alisema “huu ni muendelezo wa mikakati ya Shirika katika kujenga uelewa na mahusiano bora na wadau ambapo leo hii tupo na viongozi wa dini kutoka katika vijiji na mitaa linapopita bomba la gesi kwa Mkoa wa Lindi”. 

Bi. Msellemu alieleza kwamba, TPDC akiwa kama shirika la mafuta la Taifa linalo jukumu sio tu la kuzalisha na kusambaza gesi asilia bali pia kuhakikisha elimu sahihi juu ya manufaa na faida za miradi ya gesi asilia inapatikana kwa wadau wote. Bi. Msellemu alifafanua kwamba, TPDC iliona ni vema kuwajengea uelewa zaidi viongozi wa dini kwani wao ni nguzo muhimu katika jamii na pia ni watu wenye ushawishi mkubwa hivyo kuelewa kwao juu ya maendeleo ya sekta ya gesi asilia na mafuta kutasaidia kusambaza uelewa zaidi kwa waumini wao. 

Ziara ya viongozi wa dini kutoka Mkoani Lindi haikuishia katika kutembelea kiwanda cha kuchaka gesi asilia pekee bali pia walipata fursa ya kusikiliza mada kuhusiana na maendeleo katika mkondo wa juu na mkondo wa chini katika sekta ya mafuta na gesi asilia. Mada hizi zilitolewa na wataalamu kutoka TPDC ambapo, Ndg. Shaidu Nuru, Mjilojia kutoka TPDC alitoa mada kuhusu maendeleo katika mkondo wa juu na kugusia hali ya utafiti nchini kwa sasa na maendeleo katika mradi mkubwa wa LNG. Akitoa mada hiyo, Ndg. Shaidu alisema “ utafiti wa mafuta na gesi asilia nchini ni zoezi endelevu ambalo limepelekea ugunduzi mkubwa wa shehena ya gesi asilia (futi za ujazo 57.83 trilioni) katika nchi kavu na kina kirefu cha bahari”.
 Viongozi wa dini kutoka mkoani Lindi wakitembelea kiwanda cha kuchakata gesi asilia, Madimba-Mtwara
Maalamu kutoka TPDC, Godbless Swagarya akifafanua jambo kwa viongozi wa dini walipotembelea kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba, Mtwara. 
Sehemu ya viongozi wa dini kutoka Lindi wakiwa katika ziara ya kutembelea kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba, Mtwara. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kutumika kuibua vipaji vya wanamichezo nchini

$
0
0
Na Genofeva Matemu – WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka walimu wa michezo nchini kutumia michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kuibua vipaji kupitia hazina ya vijana wadogo waliopo katika shule za msingi na sekondari wenye uwezo mkubwa katika michezo mbalimbali.
Rai hiyo ameitoa Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao na wadau wa sekta ya michezo kujadili namna ambavyo michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA itakavyoendesha mwaka huu ambapo michezo hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia mwezi Juni mwaka huu Jijini Mwanza.
“Tumedhamira kuibua vipaji kuanzia ngazi ya shule za msingi ili tuweze kuliweka taifa katika taswira ya michezo kwani michezo ni sayansi inayohitaji mazoesi yanayoweza kuisaidia jamii kuwa na afya bora na hata kuweza kuitangaza nchi katika mataifa mengine kupitia michezo mbalimbali” amesema Mhe. Mwakyembe.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amewataka wadau wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi kuchangia ili kufanikisha michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA na kuifanya michezo hiyo kuwa agenda kubwa hapa nchini katika kuendeleza michezo na kuinua vipaji vya michezo mbalimbali.
Aidha Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Dkt. Yahya Msigwa amesema kuwa Michezo ni kila kitu katika jamii kwani michezo ni ajira, michezo ni siasa, michezo ni kinga dhidi ya ukimwi na kinga dhidi ya ujambazi kwa vijana, michezo ni biashara, michezo ni utamaduni na pia michezo haina mipaka kati ya nchi na nchi.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi na wadau kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifafanua jambo wakati wa kikao cha maandalizi na wadau kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Elimu Bw. Tixon Nzunda
 Baadhi ya wadau wa sekta ya michezo wakifuatilia hoja wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Jijini Dar es Salaam
 Mwakilishi kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Maganga Japhet akichangia mada wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA  Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia waliokaa) pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo(wapili kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa michezo walioshiriki katika kikao cha maandalizi kuelekea mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu - WHUSM

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MAHIGA AFUNGUA OFISI YA UBALOZI WA TANZANIA, ISRAEL

$
0
0

Dkt, Mahiga afungua Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, Israel

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amezindua rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania. 

Ufunguzi wa ofisi hiyo ya ubalozi iliyopo katika mji wa Tel Aviv ulifanyika leo na ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Ayelet Shaked, Mabalozi wa nchi za Afrika na Watanzania wanaoishi nchini humo.

Katika hotuba yake, Dkt. Mahiga aliitaja Israel kama nchi ya kupigiwa mfano kwa sababu licha ya changamoto za kimahusiano na baadhi ya jirani zake lakini bado nchi hiyo imepiiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo cha umwagiliaji, viwanda, matibabu, TEHAMA, ulinzi na usalama, uhifadhi wa maji na masuala ya nishati ikiwemo nishati ya kutumia joto ardhi.

Kwa upande wa ulinzi na usalama, Waziri Mahiga alisema Watanzania hawataisahau Israel kwa kuwa ndiyo nchi iliyoisaidia Tanzania kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa ambalo mafanikio na mchango wa jeshi hilo unajulikana na kila Mtanzania. Alisema JKT baada ya lugha ya Kiswahili ndiyo chombo cha pili kilichosaidia kwa kiasi kikubwa kuunganisha makabila zaidi ya 120 ya Watanzania na kuwa wamoja hadi leo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel Ufunguzi huo ulifanyika jijini Tel Aviv tarehe 08 Mei 2018. Wengine katika picha ni Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima.wakigongesheana glasi kwa ajili ya kuwatakia afya njema viongozi wa mataifa yao, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga wakisalimiana na Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked walipowasili kwa ajili ya kushiriki ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiweka saini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili kwenye ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa ajili ya kuzifungua rasmi. Anayemwangalia ni Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked .

Airtel yaja na Fursa ya wekeza na Airtel Money Branch

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Airtel money imedhamiria kuwakomboa Watanzania kwa kutoa ajira kwa kuanzisha ushirikiano wa uwekezaji na uendashaji wa maduka yake ya kisasa maarufu kama Airtel Money Branch.

 Kwa wale ambao watapata fursa hiyo, kampuni ya Airtel itawawezesha kwa kiwapatia vifaa vyotebmuhimu ikiwemo kupiga chapa duka, floti kwenye akaunti ya Airtel Money pamoja na simu za kuendesha duka la Airtel Money kwa mafanikio.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza ushirikiano wa uwekezaji huo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda alisema kuwa Airtel ina nia ya dhati ya kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kujiajiri kupitia Airtel Money.

 Airtel Fursa huwapa vijana fursa ya kuwakilisha ujuzi wao na wangependa kuufanikisha. Mpaka sasa, kuna mamia ya vijana ambao wameweza kufaidikia na kampeini ya Airtel Fursa na mpaka sasa wameweza kujiajiri na hivyo kubadilisha maisha yao. Kupitia Airtel Money branch tuna uhakika maelfu ya vijana wataweza kupata fursa ya kujiajiri na hivyo kubadilisha maisha yao.

 Na ikiwa ni muendelezo wa Airtel Tanzania kuendelea kutoa fursa za kujiajiri kwa Watanzania, Airtel pia imeweza kufungua maduka ya huduma za simu mkononi nchini kote. Lengo ni kuendelea kufanya vijana wajiajiri lakini pia ni mpango kabambe wa kupeleka huduma karibu na wateja wake.

 Maduka haya ya Airtel Money branch yana muonekano unaofanana na yako katika maeneo maalumu ambayo yatawawezesha maelfu ya wakazi kupata huduma kirahisi na kukidhi mahitaji yao kwa ufanisi zaidi

 Maduka hayo yatatoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kifedha, huduma za intaneti, kuongeza salio , kusajili namba na pia kuunganisha wateja wapya kwenye mtandao wa Airtel.

Tunaamini hii ni njia pekee ya kuwafikia wateja wetu na kujua changamoto zao na kuzitatua kwa wakati na vilevile kuwaunganisha na huduma na bidhaa zetu za kipekee na kibunifu zinazosaidia kutatua changamoto zao za kila siku za kijamii na kiuchumi.

 Kuanzishwa kwa maduka haya sehemu mbalimbali nchini kunadhihiriwha kwa vitengo dhamira ya Airtel kuendelea kuwekeza nchini na Afrika kwa ujumla.
 Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akikata utepe wakati wa kuzindua moja kati ya maduka ya Airtel mkoani shinyanga ambapo jumla ya maduka 8 yaLinduliwa kwa lengo lakutoa ajira na kutoa huduma ya mawasiliano katika mkoa wa Shinyanga. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Airtel Tanzania,  Sunil Colaso akifatiwa na Meneja wa Kanda ya kati wa Airtel , Bwn Stephen Akyoo
Mwonekano wa duka jipya la Airtel Money Branch lililopo Wilaya ya Chato mkoani Geita maalum kwa kutoa huduma za mawailiano za Mtandao wa Airtel.

Serikali yafuta tozo saba kwenye mbegu ili kupunguza gharama za uzalishaji

JAFO AAGIZA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI KATIKA VITUO VYOTE VYA AFYA 208 VINAVYOBORESHWA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameagiza kufungwa mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato katika vituo vyote vya Afya 208 vinavyoboreshwa hapa nchini. 

Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo alipotembelea wilayani Chamwino mkoani Dodoma kukagua Ujenzi wa kituo cha Afya Chamwino ambacho kimepokea Sh.Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.

Akizungumza katika ukaguzi huo, Waziri Jafo amewapongeza watendaji wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi vizuri wa miundombinu hiyo ambapo amejulishwa kuwa hadi sasa jengo la upasuaji, maabara, nyumba ya daktari, chumba cha kuhifadhi maiti, na wodi ya wazazi zipo hatua za mwisho. 

Kufuatia maendeleo hayo mazuri ya ujenzi wa vituo hivyo hapa nchini, Jafo ameagiza kufungwa mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato ili vituo hivyo vitakapokamilika viweze kukusanya mapato ipasavyo na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akitoa agizo la ufungwaji wa mifumo ya kielektroniki katika vituo vya afya vinavyojengwa nchin.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wakifanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wakifanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athuman Masasi alipofanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino wakati alipofanya ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika Kituo cha Afya Chamwino.

RC RUVUMA ATOA SIKU SABA VYAMA VYA MSINGI KULIPA MAMILIONI KWA WAKULIMA WA KOROSHO.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME ametoa siku saba kwa vyama vya msingi vya chama kikuu cha ushirika (TAMCU) wilaya ya TUNDURU mkoani humo kuwalipa wakulima wa korosho milioni mia mbili ambazo wanadai.

BENKI YA DUNIA YATOA MAFUNZO YA SIKU MBILI KWA WATUMISHI WA UMMA JUU YA MPANGO KAZI WA MAZINGIRA NA USTAWI WA JAMII

$
0
0


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Somalia, Bela Bird leo amefungua warsha ya siku mbili kwa watalaamu na Watumishi wa Serikali kutoka nchi ya Tanzania na Malawi hili waweze kuendana mpango kazi wa Masuala ya Mazingira na Masuala ya kijamii pindi wanapotekeleza miradi inayotekelezwa na benki hiyo katika nchi hizo mbili.

Bi Bela amesema kuwa Warsha hiyo ambayo itaweza kuwasaidia watumishi wa serikali kujua miradi inayofanywa na benki ya Dunia awezi kuathiri mfumo wa Mazingira wala wanadamu wanaoishi katika eneo husika kwa namna moja ama nyingine hili kuweza kuleta usawa wa ikolojia.

"tumezunguka kama benki kwenye nchi kma 63 na kuwaeleza watu jinsi mpango kazi wa mazingira ulivyobadirika ambao una viwangoi kumi kwa kutizama masuala ya ustawi wa jamii pamoja na kutoathiri Mazingirakwa viumbe vyenye uhai na visivyo na uhai."

alimaliza kwa kusema kuwa mpango kazi huo utaweza kuwasaidia watumishi wa serikali wanaosimamia miradi ya maendeleo inafadhiliwa na benki hiyo inafanikiw abila kuathiri uharibifu wa Mazingira.
 Mkurugenzi wa  Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Malawi, Burundi na Somali,Bela Bird akizungumza wakati w aufunguzi wakati wa kufungua warsha kwa watumishi wa Serikali juu ya Mpango wa Benki hiyo katika masuala ya Mazingira na Kijamii  Jijini Dar es Salaam.
 Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Benki ya Dunia, Nathale Munzberg akizungumza wakati akitoa mada wakati wa warsha kwa watumishi wa Serikali juu ya Mpango wa Benki hiyo katika masuala ya Mazingira na Kijamii  Jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wa warsha kwa watumishi wa Serikali juu ya Mpango wa Benki hiyo katika masuala ya Mazingira na Kijamii  Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha kwa watumishi wa Serikali juu ya Mpango wa Benki hiyo katika masuala ya Mazingira na Kijamii  Jijini Dar es Salaam.

WASHIRIKI WA WAZO LA UBUNIFU WA TEKNOLOJIA YA MAPINDUZI YA KILIMO YA ABINBEV NA TBL GROUP WAPIGWA MSASA DAR

$
0
0
Washiriki wa wazo la ubunifu wa teknolojia ya mapinduzi ya kilimo ya ABINBEV na TBL Group wapigwa msasa Dar es Salaam Washiriki wa wazo la ubunifu la kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo watakaotangazwa katika mkutano mkubwa wa masuala ya ubunifu,matumizi ya teknolojia na ukuzaji wa sekta ya kilimo katika ustawishaji wa jamii unaojulikana kama ,The East Africa (EA) Innovation Event, utakaofanyika jijini Dar es Salaam . 

 Mkutano huu umeandaliwa na kampuni ya ukuzaji ubunifu wa kiteknolojia ya Bits & Bytes kwa kushirikiana na kampuni ya ABIn Bev Africa na Tanzania Breweries Limited,na umelenga kuonyesha ubunifu unavyoweza kuleta mabadiliko endelevu kwenye jamii, mojawapo ikiwa mradi wake kwa kushirikiana na wakulima wadogowadogo unaojulikana kama Smart Barley.

 Utakutanisha washiriki zaidi ya 100 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo wataalamu wa kilimo,wabunifu,wahandisi na jamii mbalimbali za wafugaji na utajikita zaidi kujadili ya kupambana na changamoto zinazowakabili wakulima wadogowadogo nchini na mikakati ya kuwawezesha kuongeza mavuno kutokana na shughuli zao za kilimo. 

 Meneja wa huduma za kilimo wa IBinBev Afrika Mashariki , Coetzee Theunis , alisema katika ukanda wa Afrika Mashariki wapo maelfu ya wakulima wadogowadogo wa zao la Shahiri na mtama wanaoshirikiana na kampuni ya ABInBev katika nchi za Tanzania na Uganda kupitia kampuni zake tanzu za Tanzania Breweries Limited (TBL) na Nile Breweries Limited (NBL),ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa mvua.

Kwa kuwawezesha kupata teknolojia za kisasa wataweza kuongeza mavuno zaidi na maisha yao kuwa bora zaidi. Kwa upande wake mwanzilishi wa kampuni ya Bits&Bytes Convention,Zuweina Farah Zuweina Farah,amesema kuwa mkutano wa mwaka huu unatarajiwa kuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa kwa ushirikiano na kampuni ya ABIn Bev,utajadili changamoto za wakulima wadogo na kuzitafutia ufumbuzi lengo kubwa likiwa ni kuwakwamua.
 Baadhi ya washiriki wa shindano la wazo la ubunifu wakimsikiza Meneja wa sekta ya kilimo wa ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki, Coetzee Theunis
 Makamu wa Rais wa kampuni ya Solutions Africa Zone Lee Dowson wapili (kushoto) akifafanua jambo juu ya mashine ya kupandia nafaka iliyobuniwa na wanachama wa Better Planters Enterprise (BPE) toka Arusha
 Baadhi ya washiriki waliowasilisha mawazo yao ya ubunifu wakiwa kwenye warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na EA Agri Innovation event kwa kushirikiana na TBL Group na ABINBEV
Baadhi ya washiriki waliowasilisha mawazo yao ya ubunifu wakiwa kwenye warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na EA Agri Innovation event kwa kushirikiana na TBL Group na ABINBEV
---

TAPSEA KUFANYA MKUTANO MKUU ZANZIBAR

$
0
0
Na Ali Issa, Maelezo Zanzibar  
Makatibu Mahsusi wa Taasisi za Serikali na Watu Binafsi Wametakiwa Kufanya Kazi zao Kwa Kufuata Sheria na maadili ya kazi hiyo kama zinavyo waelekeza ili kuleta ufanisi katika kazi.

Hayo yamesemwa Katika Hoteli Ya Mansoon Shangani na Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) Zuhura Songambele Maganga wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mkutano Mkuu wa sita wa Chama hicho utakao fanyika chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kampasi ya Tunguu.

Amesema kumekuwa na malalamiko juu ya makatibu mahsusi kufanyakazi kinyume na maadili ya kazi zao hivyo mkutano huo mkuu utaoaza  kesho utaelekeza majukumu ya makatibu mahsusi wanavyotakiwa kutekeleza kazi kwa kufuata maadili ya kazi zao na mamlaka anayoifanyia kazi.

Aidha alisema kuwa makatibu hao wataelekezwa kufanya wajubu wao kwa kuthamini utaifa wao kwa malengo ya kuweka mbele maslahi ya nchi katika utoaji huduma bora kwa jamii.

“lengo la chama chetu mwaka huu ni kukuza taaluma, kudumisha uwajibikaji na kuinuwa hadhi ya taaluma ya katibu muhsusi kitaifa kimataifa,na kusaidia kudumisha utoaji huduma bora katika jamii” alisisitiza mwenyikiti TAPSEA.

Mwenyekiti huyo amesema tangu kuazishwa chama hicho cha makatibu mahsusi kumekuwa na maendeleo yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha makatibu mahsusi wa Tanzania kupitia mikutano yao kwa kuwapa taaluma na kubadilishana uzowefu.

Faida nyengine amesema wamefanikiwa kushawishi na kukubaliwa kuazishwa shahada ya uhazili katika chuo cha utumishi wa umma Tanzania bara baada ya maombi ya muda mrefu.

Aidha amesema wamefanikiwa kununua kiwanja kwa ajili ya kujenga ofisi ya TAPSEA Makao makuu ya serikali Dodoma na kushughulikia malalamiko yanayo pelekwa wanachama na kuyapatia ufumbuzi

Nae mwakilishi wa Chama cha Makatibu mahsusi upande wa Zanzibar Zainabu Ibrahimu aliwataka wafanyakazi wa kada hiyo kujiunga na chama chao kwani kunafaida kubwa wakati wa utumishi wao baada ya kkustaafu kwa kupata ruzuku za utumishi wake iwapo atakuwa mwanachama hai.  
 Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania  (TPSEA) Zuhura Songambele Maganga  akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Mazsons Shangani kuhusu kufanyika mkutano wa sita wa Chama hicho unaoanza tarehe 10.5.2018 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Kempasi ya Tunguu.
Mwakilishi wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania upande wa Zanzibar, Zainab Ibrahim  akieleza kuimarika kwa  chama hicho kwa upande wa Zanzibar katika mkutano  wa waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Mazsons Shangani.

Serikali Kuendelea Kuhakikisha Kuwa Pembejeo Zinawafikia Wakulima kwa Wakati

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO
Serikali imesema itaendelea Kuhakikisha kuwa Pembejeo za Kilimo zinawafikia Wakulima kwa wakati na kwa bei nafuu ili kukuza sekta ya Kilimo.

Akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Mjini Mhe. Sebastian Simon Kapufi, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa amesema kuwa ili kutimiza azma yakuwafikishia wakulima pembejeo kwa wakati Serikali inaratibu mahitaji, upatikanaji na matumizi yake na kuelekeza aina za pembejeo zinazofaa kwa kuzingatia msimu wa kilimo katika eneo husika.

“Serikali imeanzisha na kutumia mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja ili kuhakikisha mbolea inapatikana na kusambazwa kwa wakulima kwa wakati,” alisisistiza Dkt. Mwanjelwa.
Akifafanua Mhe. Dkt. Mwanjwelwa amesema kuwa mfumo huo una faida nyingi ikiwemo kuongezeka kwa upatikanaji wa mbolea kutoka tani zaidi ya laki mbili hadi tani zaidi ya laki tatu kufikia mwezi Aprili 2018 na kupungua kwa bei za mbolea kwa kati ya asilimia 11 hadi 39.5 ikilinganishwa na bei ya mbolea kabla ya kuanza kwa mfumo huo.
"Tayari mbolea tani zaidi ya laki moja ikiwemo mbolea ya kupandia (DAP) tani zaidi ya elfu hamsini na tano na mbolea ya kukuzia (UREA) tani elfu hamsini na nne zimeingizwa na kusambazwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mbolea hizo hutumika kwa zaidi ya asilimia 62 kwa mwaka," alisema Dkt. Mwanjelwa.
Kwa upande wa mbegu bora kuanzia mwaka 2017/2018 Serikali imefuta tozo (7) kwenye mbegu, ambapo mpango huu umelenga kupunguza gharama za uzalishaji, kuongeza upatikanaji na kupunguza bei ya mbegu bora kwa mkulima.
Aidha, Kwa kufutwa kwa tozo hizo Serikali inategemea bei ya mbegu bora itapungua na wakulima wengi wataweza kununua na kutumia ili kukuza kilimo hapa nchini na kuongeza uzalishaji.
Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikisisitiza uzalishaji wenye tija ili kukuza sekta ya viwanda hapa nchini na kuongeza ajira kwa wananchi hali itakayokuza pato la Taifa na uchumi kwa ujumla.

MAKAMANDA WA POLISI WAJINOA KUUKABILI UKATILI WA KIJINSIA

$
0
0

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
 Kamishna wa Polisi (Ushirikishwaji wa Jamii), Mussa Ali Mussa akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
 Baadhi ya Makamanda wa Polisi wakisikiliza kwa makini hotuba ya IGP Simon Sirro (hayupo pichani) wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto (Picha na Jeshi la Polisi).
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Simon Sirro akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utu wa Mtoto, Mtengeti Koshuma (kushoto) na Mwakilishi wa UNFPA nchini Bi Christine Mwanukizi(kulia) baada ya kufungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia. Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto.
Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkamanda wa Polisi wa Mikoa ya Tanzania kuhusu makosa ya ukatili wa kijinsia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameratibiwa na Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi na Shirika la Utu wa mtoto (Picha na Jeshi la Polisi).

Waziri Mwakyembe afungua Mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi

$
0
0
Na Genofeva Matemu- WHUSM
Timu za majeshi kupitia michezo mbalimbali zimetakiwa kuweka mikakati na kuibua wanamichezo wazuri ambao wataiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya kimataifa na kuleta ushindi na medali mbalimbali kama ilivyokuwa hapo zamani.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) katika uwanja wa uhuru jana Jijini Dar es Salaam

“Ni matarajio yangu kuwa uwepo wa michezo hii inaashiria azma na nia thabiti ya kurejesha enzi  za majeshi yetu kutoa uwakilishi ulio mzuri katika michezo ndani na nje ya nchi kama ilivyokuwa hapo zamani” amesema Mhe. Mwakyembe

Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed amesema kuwa kufanyika kwa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi kila mwaka kunathibitisha azma ya JWTZ kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini kwa kuunda timu za JWTZ zitakazotumika kuimarisha timu mbalimbali za Taifa katika mashindano ya Kimataifa. 
Jenerali Yakubu amesema kuwa uwepo wa michezo ya majeshi katika jumuiya ya Afrika Mashariki umekua nyenzo ya kudumisha amani baina ya nchi wanachama hivyo wachezaji watakaopata fursa kushiriki michuano hiyo washiriki vema na kuleta tija kupitia michezo hiyo. 

Mashindano ya Muula wa tano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) yenye kauli mbiu isemayo “Tushiriki Michezo kama sehemu ya kazi, Kulinda   Afya zetu na kudumisha mshikamano” yataendana na uteuzi wa wanamichezo watakaoteuliwa kuunda timu za JWTZ zitakazoshiriki mashindano tarajiwa ya Majeshi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko nchini Kenya mwaka 2019
 Mnadhimu Mkuu; Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed akizungumza wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mnadhimu Mkuu; Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na mchezaji wa Timu ya Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipokua akikagua timu hiyo wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Makao Makuu ya Jeshi wakati wa ufunguzi wa muhula wa tano wa mashindano ya kombe la mkuu wa majeshi ya ulinzi (cdf cup 2018) jana katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu - WHUSM

UZINDUZI WA COPA UMISSETA SINGIDA WAFANA

$
0
0
Mashindano ya Copa Umisseta ngazi ya mikoa yanaendelea ambapo yamezinduliwa mkoani Singida, katika uwanja wa Namfua ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa mkoa huo, Dk. Rehema Nchimbi, aliyemwakilisha Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jafo. Hafla ya uzinduzi huo wa michezo hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya Coca-Cola pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani humo, wadau wa michezo, walimu na wanafunzi wa shule za sekondari ambao walishiriki kucheza michezo mbalimbali. 

 Mkuu wa mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi katika hotuba yake ya ufunguzi,aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kutoa udhamini kwa michezo hiyo na amewaasa washiriki ambao ni wanafunzi kuyatumia kuboresha afya na akili ili kuepuka kushiriki katika matendo ya kihalifu kama matumizi ya madawa ya kulevya na kutojihusisha na mapenzi kabla ya wakati.

 Alisema mashindano hayo ni jukwaa kubwa la kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo na Ushahidi wa suala hili upo kwa kuwa kuna wanamichezo wengi wanaotokea mkoani Singida ambao vipaji vyao viliibuliwa na Umisseta vilevile mkoa huo katika mashindano ya mwaka jana ulifanya vizuri katika ngazi ya kitaifa kwa kushika nafasi ya tatu. 

Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa bidhaa za Coca-Cola mkoani Singida, Joseph Simplis ,amesema Coca-Cola imekuwa ikidhamini mashindano haya kwa kipindi cha miaka 3 na lengo kubwa ni kuhakikisha inawashirikisha wanafunzi wengi zaidi nchini sambamba na kuibua na kukuza vipaji vya michezo.Aliwaasa wanafunzi wa Mtwara kuchangamkia fursa hii. Katika kufanikisha michezo hii, kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikitoa udhamini wa vifaa vya michezo ambapo imelenga kusambaza vifaa kwa shule za sekondari 4,000. 

Katika uzinduzi huo alikabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni kwa wawakilishi wa shule mbalimbali mkoani humo. Uzinduzi wa Copa Umisseta mkoani Singida ni wa tano kufanyika baada ya kufanyika katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Mtwara na Zanzibar. Mashindano hayo ngazi ya kitaifa yatafanyika mwezi Juni mwaka huu mkoani Mwanza.
 Wawakilishi wa shule za sekondari wakipokea vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya Coca-Cola kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi
Mkuu wa mkoa wa singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akifurahia zawadi ya mpira wa kufanyia mazoezi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akijiandaa kupiga penati wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo. Na Mwandishi Wetu- Singida. 

PICHA : NYUMBA ZA KANDO KANDO NA MTO ZINAONDOKA NA MAJI KILA MWAKA

$
0
0
 Kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zimekuwa zikisababisha baadhi ya nyumba zilizojengwa karibu na mito kuondoka na maji ya mvua kila mwaka kama unavyoona nyumba zilizojengwa katika kandokando ya mto kuanzia Ubongo, Mabibo, Kigogo na Magomeni nyumba. Picha na Chalila Kibuda wa Michuzi Media Group (MMG)



WATUMISHI WANAWAKE ILALA WAANZA KAMPENI KUFANIKISHA UJENZI CHOO CHA MTOTO WA KIKE

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WATUMISHI Wanawake katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameamua kuanzisha kampeni maalumu ya ujenzi wa Choo cha mtoto wa kike kwa kuanza na shule zote za msingi katika manispaa hiyo.

Hivyo uzinduzi wa kampeni hiyo unatarajiwa kufanyika Oktoba 11 mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema na imani yao ni kwamba wadau mbalimbali wataungana na watumishi hao katika kufanikisha ujenzi wa choo cha mtoto wa kike.

Mratibu wa kampeni hiyo ambaye pia ni Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa watumishi wanawake wa manispaa hiyo wanatambua na kuthamini jitihada kubwa za Serikali na wadau wa maendeleo za kukabiliana na changamoto za mtoto wa kike.

Akitoa sababu za ujenzi wa choo cha mtoto wa kike, Shaibu amesema kila ifikapo Oktoba 11 ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike duniani na lengo la maashimisho hayo ni kuilimisha na kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutetea haki za mtoto wa kike.

"Tafiti zimefanyika kuhusu sababu zinazochangia mahudhurio hafifu ya mtoto wa kike darasani hasa  wa darasa la saba na takwimu zao zinabainisha wasichana wa darasa la saba hawahudhurii shuleni kati ya siku nne hadi tano kila mwezi.Vyoo visivyofaa kwa matumizi hasa kwa wasichana wanaoingia hedhi huleta changamoto kubwa kwao.

"Kutokana na changamoto hiyo watumishi wanawake wa Manispaa ya Ilala wameona wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za Serikali na kuendelea kuihamasisha jamii na wadau kujenga choo bora cha kisasa kitakachokuwa rafiki kwa mtoto huyu wa kike,"amesema Shaibu.
Mratibu wa Kampeni cha ujenzi cha choo cha Mtoto wa kike ambaye pia ni Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Tabu Shaibu (katikati) akizungumzia maandalizi ya uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo unaotarajia kufanyika Oktoba 11 mwaka huu katika hoteli ya Lamada. Kulia ni Mwenyekiti wa kampeni hiyo na Ofisa Elimu Msingi manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas na kushoto ni moja ya wajumbe wa kampeni hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI UMMY – SERIKALI IMETENGA BILION TATU (3) KWA AJILI YA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI

$
0
0
Dar es salaam: Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) ilizindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kili Challenge 2018), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. Shughuli hii ilifanyika tarehe 4 Mei 2018 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Ummy Mwalimu, aliitikia wito wa kufika Dar es salaam, katika hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge 2018, ambapo alifanya zozezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka mwaka jana 2017 zilizopatikana baada ya wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro. 

Kili Challenge ni mfuko unachangia juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU). Kili Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.

Mfuko huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro. Uzinduzi huo ulishirikisha Tume ya kuthibiti UKIMWI, Tanzania TACAIDS, na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) ambapo zaidi ya shilingi bilioni moja (1) zilikusanywa katika tukio hilo. 

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, ameitaka serikali kutumia mbinu mbalimbali na kuweka mikakati itayohakikisha fedha zinazotwengwa kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI zinatumika kwa kusudi hilo, na hivyo kuondokana na kutegemea misaada kutoka kwa wafadhili.

Mheshimiwa Ummy Mwalimu alisema fedha zilizopatikana kwenye harambee hiyo zinatakiwa zielekezwe moja kwa moja kwa wahusika na sio kutumika kama posho za vikao, huku zikionyesha jitihada zilizofanywa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, pia akiendelea kusema, fedha hizo zinatakiwa kuisaidia nchi katika kuzipa nguvu sekta ndogo ili kuthibiti maambukizi ya UKIMWI nchini. 
Mkurugenzi wa mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) Bw. Richard Jordison, akisoma hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge 2018, iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Mheshimiwa waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abel & Fernandes Communcations, Ms. Fatma Fernandes wa pili kutoka kulia, ambaye alinunua picha ya makamu wa Raisi Mheshimiwa Samia Suluhu katika mnada uliofanyika wakati wa uzinduzi wa Kili Challenge ili kukusanya fedha za kupambana na UKIMWI, jijini Dar es salaam mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni mia moja (100M) kwa watoto wa kituo cha moyo wa huruma kilichopo Geita ili kusaidia mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TACAIDS, Dkt.Leornard Maboko, Mkurugenzi wa GGM, Bw. Richard Jordison na kulia, Mkurugenzi wa kituo cha Moyo wa Huruma Sister Adalbera Mukure.
Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leornard Maboko akisoma hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa Kili Challenge, katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyoko jijini Dar es salaam.
Mheshimiwa waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu akishiriki katika harambe iliyofanyika kwenye uzinduzi wa Kilimanjaro Challenge ili kuchangia mfuko kwa ajili ya kudhibiti UKIMWI nchini.

MASHINDANO YA HISANI YA MBIO ZA MBUZI KUENDELEA MWAKA HUU

$
0
0
Mashindano maarufu ya hisani ya mbio za mbuzi jijini Dar es salaam yanatarajiwa kuendelea mwaka huu. Baada ya tangazo la mwaka jana la kamati iliyokuwa ikiandaa mashindano hayo kuamua kusitisha michuano hiyo maarufu ya hisani, Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam, Oysterbay imeamua kuendelea na uandaaji wa mashindano hayo kuanzia sasa. Waandaji hao wapya wataendelea na utaratibu uleule wa mashindano, huku wakitarajia kuwavutia mashabiki wengi  wapya pamoja na wale mashabiki wa siku zote wa mbio hizo.

Katika kipindi cha miaka 17 iliyopita, ‘Dar es salaam Charity Goat Races’ ilikuwa ni moja ya tukio kuu katika kalenda ya matukio ya kila mwaka na moja ya matukio makuu ya hisani hapa jijini. Uamuzi wa kamati ya watangulizi ya uandaaji wa mashindano hayo ya kutoendelea nayo uliwafanya mashabiki wengi kuvunjika moyo. 

Baada ya majadiliano ya kina na watangulizi hao, Klabu ya Rotary ya Dar es salaam, Oysterbay iliamua kuendelea na mashindano hayo. Kupitia chapa yake mpya ya “The Rotary Goat Races,” mashindano ya mwaka huu yatafanyika Juni 23, eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam, yakitegemea kutumia rasilimali za mwanzo zilizotumiwa katika michuano iliyopita. Tukio hilo litakuwa ni la kiburudani na kifamilia na mapato yake yataelekezwa kwenye miradi ya hisani.

Tofauti na miaka ya nyuma, mapato ya ‘Rotary Goat Races’ hayatapelekwa kwenye mashirika mbalimbali yanayopokea misaada bali yatatumika kwa ajili ya miradi binafsi ya utoaji huduma ya Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay. Miradi hiyo itazingatia hasa masuala mbalimbali ya elimu kwa manufaa ya jamii.
Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’, mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza nia ya klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Pamoja nae  kulia ni Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels na Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela(kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish Shah  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutangaza dhumuni la klabu hiyo kuendeleza mashindano hayo kwa  mwaka 2018. Chini ya chapa mpya ya ‘The Rotary Goat Races’ mashindano hayo kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 23 Juni katika eneo la ‘The Green’ Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela.
Mkuu wa kamati ya maandalizi, Mathew Helela akizungumza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangazwa kurudi kwa mashindano ya mbio za Mbuzi leo jijini Dar es salaam. Pamoja nae, kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.
Mwenyekiti wa Bodi ya mashindano ya mbio za mbuzi za Rotary, Amish akifurahia jambo na Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam, Oysterbay, Anne Saels.


Msajili Baraza la Uuguzi Tanzania Aanza Kazi Rasmi, apokewa kwa shangwe

$
0
0
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa leo ameanza kazi rasmi baada ya kukabidhiwa ofisi tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi uliopita. Bi. Agnes Mtawa anachukua nafasi ya Bi. Lena Mfalila aliyemaliza muda wake.
Awali Bi. Mtawa alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo mwezi uliopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alimteua kuwa Msajili wa Baraza la Uuguzi Tanzania.
Uteuzi huo ulianza rasmi tarehe 16-04-2018 na kwamba utadumu kwa muda wa miaka mitano kuanzia tarehe ya uteuzi.
Nafasi mbalimbali alizowahi kushika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Mtawa ni; Mkuu wa Mafunzo na Uajiri kuanzia mwaka 2004 hadi 2006, Mkuu wa Mafunzo, Utafiti na Elimu kuanzia mwaka 1997 hadi 2004, amewahi kuwa  Katibu Mkuu katika baraza la uuguzi na ukunga Tanzania kuanzia 2002  hadi 2011 na mwaka 2007 aliteuliwa Mkuurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi mwezi uliopita alipoteuliwa.
 Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akikaribishwa leo ofisini na watumishi wa baraza hilo, huku  Bi. Jane Mazigo aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo akimpatia maua. Kulia ni Happy Masenga anayeshughulika na mafunzo katika baraza hilo.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa  akitazama zawadi ya maua aliyokabidhiwa na watumishi wa baraza hilo leo.
 Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akikaribishwa kwa shangwe leo ofisini na watumishi wa baraza hilo. 

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA AVUTIWA NA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

$
0
0


Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili kulia)akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dkt Masudi Senzia juu ya miradi ya upanuzi wa Chuo hicho inayoendelea kazi ziara ya siku moja aliyoifanya Mei 9,2018

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(katikati)akiwa na watumishi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) akikagua moja ya Karakana ya Mitambo inayofanyiwa ukarabati.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(katikati)akiwa pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia(kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Dk Erick Mgaya katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya upanuzi wa Chuo hicho.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kulia)akikagua moja ya makontena yenye vifaa mbalimbali kwaajili ya mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kushoto)akiangalia kiungo cha bomba kwenye Karakana ya wanafunzi wanaosoma kozi fupi kwaajili ya kuwa sehemu ya mafundi watakaojenga Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili kulia)akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia katika ziara aliyoifanya kwenye Chuo hicho kukagua shughuli mbalimbali zinazoendelea.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika moja ya Maabara ya Chuo hicho.

Wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Arusha wakimsikiliza Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako.
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images