Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

BAADA YA KUONDOLEWA WETCU URAMBO, KALIUA KUANZISHA CHAMA CHAO KIKUU CHA USHIRIKA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
HATIMAYE wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) mkoani Tabora kwa kauli moja wameridhia kuganishwa kwa Chama Kikuu cha Ushirika kwa ajili ya kuchukua Wilaya za Urambo na Kaliua ili kuanzisha chama kingine kipya cha maeneo hayo.

Hatua hiyo imefikiwa na viongozi kutoka Vyama vya Msingi (AMCOS)mbalimbali kwenye Mkutano Mkuu wa 25 ulifanyika jana mjini Tabora.

Kaimu Mrajis Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule alisema uamuzi wa kuchukua baadhi ya wanachama wa WETCU na kuanzisha Chama kipya ni kurahisisha usimamizi wa vyama vya msingi na kutekeleza agizo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuvunja Bodi ya WETCU kwa sababu ya kushindwa  kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Alisema kuwa WETCU itaendelea kubaki na usajili wake wa awali na itakuwa na Vyama vya Msingi(AMCOS) kutoka Uyui, Tabora Manispaa, Nzega na Sikonge.

Haule aliongeza kuwa kisheria kama Chama cha WETCU kingevunja ingechukua hata miaka miwili kuanzisha kingine na baada ya kufanyika ufilisi na ndipo chama kipya kianzishe , ndio maana wameona ni vema kiendelee na usajili ule ule na kianzishwe kipya kitakacho hudumia Urambo na Kaliua.

Alisema kuhusu madeni yatabaki  Chama cha  WETCU na kile kipya cha kitakachoanzishwa kitaanza bila deni kama takwa la kisheria linavyohitaji ili kiwe na sifa ya kusajiliwa.

Haule alisema viongozi wanaweza kukutana na kupendekeza jina la Chama kipya au kinaweza kuitwa UKACU ili kuendelea na taratibu za usajili na kuahidi kutangaza Bodi ya Mpito wa Chama kipya tarajiwa hivi karibuni ili hatimaye ifikapo tarehe 16 Mwezi ujao(Juni) kiwe kimesajiliwa.
 Kaimu Mrajis Kaimu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Tito Haule aakitoa ufafanuzi ya taratibu za ugawaji wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) na kuanzisha Chama kipya kwa ajili Wilaya za Urambo na Kaliua jana mjini Tabora wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa chama hicho.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Nathalis Linuma alitoa maoni yake jana wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) ulifanyika mjini Tabora.
 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Tumbuku Hassan Wakasubi alitoa maoni yake jana wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) ulifanyika mjini Tabora.
 Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Msingi (AMCOS) wakifuatilia mada mbalimbali jana wakati wa Mkutano Mkuu wa 25 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) ulifanyika mjini Tabora.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mobisol na StarTimes kuleta shangwe za Kombe la Dunia vijijini

$
0
0
Wapenzi wa Soka vijiji kufurahia michuano ya Kombe la dunia mwaka huu. Hii ni kutokana na Kampuni ya Star Times ambayo ina mkataba hapa nchini wa kutangaza mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 2018, yatakayofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi ujao, Kampuni hiyo imeingia ushirikiano na kampuni ya kusambaza nishati ya  jua na vifaa vinavyotumia nishati hiyo ya Mobisol, kutumia mtandao wake kuwezesha wananchi wanaoishi maeneo yasio na  umeme wanaotumia nishati ya umeme wa jua nchini na nchi jirani za Kenya na Uganda kutokupitwa na mashindano hayo ya kihistoria duniani kote.

Ushirikiano huo ambao umetangazwa jijini Dar es Salaam leo unawezesha wateja wanaotumia umeme na vifaa vya  Mobisol  kununua vifaa  maalumu  vya kuboresha mawasiliano vitakavyowezesha kushuhudia mechi za kombe la dunia, sambamba na kupata chaneli mbalimbali za burudani kupitia vingamuzi vya Star Times.

Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mobisol Tanzania,Patric Juma,ameeleza kuwa wateja wa Mobisol nchini, wanaweza kununua vifaa vya mawasiliano kutoka star Times vitakavyowawezesha kufurahia burudani hiyo ya soka  bure na kwa wakati wote kuanzia sasa hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu.Vifaa hivyo baada ya kununuliwa wanafungiwa bure  popote walipo.

“Tunafurahia kuingia ushirikiano huu na Star Time,hasa kwa kuwaletea ofa maalumu wananchi wanaotumia umeme wa nishati ya jua maeneo mengi yasiyo na umeme ili kuwawezesha kupata burudani za mashindano ya Kombe la Dunia ,Mobisol tutahakikisha tunaendelea kusambaza umeme kwenye maeneo yasio na nishati hiyo sambamba na kubuni vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati ya jua”Alisema Patric Juma.
 Makamo wa Rais wa Startimes,Zuhura Hanif(kulia)akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu (wapili kushoto)baada ya Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo wa soka wa msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Wengine kushoto ni Meneja wa Mobisol Lynda Okoko pamoja na Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa.Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa kampuni ya Umeme wa Jua-Mobisol,Lynda Okoko(kushoto)akipeana mkono na Makamo wa Rais wa Startimes kuashiria Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo wa soka wa msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Ambapo wapenzi wa soka waliopo vijijini watanufaika Zaidi,Wengine katika picha wapili kushoto ni Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa na Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu. Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa kampuni ya Umeme wa Jua-Mobisol,Lynda Okoko, Meneja Masoko wa Startimes, David Malisa,Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu pamoja na Makamo wa Rais wa Startimes Zuhura Hanif,wakionyesha vipeperushi vyenye chaneli mbalimbali zitakazorusha kombe la Dunia  wakati wa Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo wa soka wa msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Ambapo wapenzi wa soka waliopo vijijini watanufaika Zaidi. Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa kampuni ya Umeme wa Jua,Seth Matemu(kushoto)akiwaonesha vifaa vya umeme wa Jua,Makamu wa Rais wa Startimes Zuhura Hanif na Meneja Masoko wa Startimes David Malisa,vitakavyotumika kurusha soka msimu wa Kombe la Dunia 2018  wakati wa Uzinduzi wa ubia wakurusha michezo hiyo msimu wa kombe la dunia 2018 kati ya Startimes na Mobisol,Ambapo wapenzi wa soka waliopo vijijini watanufaika Zaidi. Haflahiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DK. SHEIN AFANYA MKUTANO WA MABALOZI WILAYA YA DIMANI

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto)  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Kichama Mohamed Rajab (kushoto)Waziri Kiongozi Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Kijitoupelei Mhe.Shamsi Vuai Nahodha,(kulia) akifuata Mwenyekiti wa Wilaya ya Dimani CCM Hussein Mjema (kimti) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Sadala,wakiimba wa Mashujaa Wimbo wa "Sisi Sote Tumegomboka"wakati wa Mkutano wa mabaalozi Wilaya ya Dimani uliofanyika leo katika Ukumbi wa CCM Amani Mkoa.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza  na Mabalozi wa Wilaya ya Dimani CCM Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika leo katika Ukumbi wa CCM Amani -Mkoa (kushoto) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Mhe,Mohamed Rajab na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Sadala.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dimani Mhe.Hussein Mjema(kimti) alipokuwa akizungumza machache na kumkaribisha Mwenyekiti wa Mkoa wa Mahgaribi Kichama katika mkutano wa Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu wa Maskani wa Wilaya hiyo katika Ukumbi wa CCM Amani Mkoa leo,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Sadala, alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati wa mkutano wa Mabalozi,Wenyeviti wa Matawi,Makatibu wa Maskani wa Wilaya ya Dimani uliofanyika leo  katika Ukumbi wa CCM Amani- Mkoa.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipokea taarifa ya Mabalozi wa Wilaya ya Dimani  baada ya kusomwa na Balozi Mwanakheri Iddi Ramadhan(kulia)katika  mkutano wa Viongozi Mashina(Mabalozi) ,Wenyeviti wa Matawi na Makatibu wa Maskani za CCM  katika Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika leo katika  Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Amani Mkoa.
 Viongozi na Baadhi ya Mabalozi wakiimba   Wimbo wa Mashujaa “Sisi Sote Tumegomboka” katika Mkutano wa  Mabalozi wa Wilaya ya Dimani  CCM Mkoa wa Magharibi (Kichama) uliofanyika leo katika Ukumbi wa CCM- Amani Mkoa  mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Sadala katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Amani Mkoa  wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Mashina,Wenyeviti wa Matawi na Mkatibu wa Maskani wa Wilaya ya Dinami Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATUMISHI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WATAKIWA KUUNGA MKONO MAENDELEO YA VIWANDA KWA VITENDO

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, amewataka  Watumishi wa Wizara hiyo kuongeza ukusanyaji wa mapato na kusimamia nidhamu ya matumizi ya Fedha za Umma ili  kuijengea Serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi na kuifanya nchi iwe na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Dkt. Mpango ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliowakutanisha wajumbe zaidi ya 190 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Amesema kuwa  Wizara  ya Fedha na Mipango inajukumu la kuhakikisha inatekeleza usemi wa “Wizara ya  Fedha na Mipango ndiyo Moyo wa Serikali” kwa kutumia  Baraza la Wafanyakazi katika kushauriana na kuchangia  mawazo yatakayosaidia katika kutekeleza majukumu ya Wizara kama yalivyopangwa na kusukuma kasi ya maendeleo ya uchumi wa Taifa.

“Watumishi wote wa Wizara mnaowajibu wa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia utaalamu mlionao na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na  taratibu za utumishi wa Umma ili kuongeza tija” alieleza Dkt. Mpango.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) akiimba wimbo wa Mshikamano Daima  pamoja na meza kuu kabla ya kufungua rasmi  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wajumbe zaidi ya 190 wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima wakati wa Mkutano wa Baraza hilo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) katikati walio kaa, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara hiyo walioshiriki Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma, kushoto ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Cyprian Kuyava.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja (kushoto) na Mhasibu Mkuu wa Fungu 21 wa Wizara hiyo Bw. Sayi Nsungi, wakifuatilia majadiliano wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Wajumbe Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiendelea na Mkutano Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MPANGO WA MATIBABU KUPITIA CHF ILIYOBORESHWA KUANZA KARIBUNI

$
0
0
*Katibu wa afya Dar, Wizara wazungumzia mafunzo waliyotoa kwa watumishi ili kuufanikisha mpango huo

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MPANGO wa matibabu ya afya kupitia utaratibu wa  Mfuko wa afya wa Jamii(CHF) iliyoboreshwa utakaoendana na utoaji wa kadi za bima kuanzia ngazi za vitongoji, unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa Juni mwaka huu nchini kote.

Hatua hiyo inatokana na kuendelea kukamilika kwa mchakato wa kutoa mafunzo kwa watumishi wa kada mbalimbali katika sekta ya afya ambao watahusika kwa namna moja au nyingine kusimamia mpango huo ambapo inaelezwa mpango huo utatoa fursa kwa wakazi wa majiji na halmashauri kunuifaka na CHF iliyoboreshwa ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanananchi wanakuwa kwenye mfumo wa kulipia matibabu kabla ya kuugua kwa kutumia kadi ya kadi za afya.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa Afya mkoa wa Dar es Salaam Sister Mathew wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa watumishi mbalimbali wa idara ya afya wakiwemo waganga  wakuu wa hospitali za wilaya pamoja na wataalamu katika mifumo ya utoaji wa  huduma hizo.Lengo la mafunzo hayo ilikuwa ni kuwajengea uwezo watumishi hao ili kuhakikisha unafanikiwa.

Mathew amefafanua kwa kuzingatia umuhimu wa utoaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini  kote, Serikali ilifanya majaribio ya mpango huo katika hospitali zote zilizopo mikoa ya Dodoma, Shinyanga na Morogoro na kutoa mafanikio, hatua iliyoilazimu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto kuja na mkakati huo kwa nchi nzima kupitia CHF iliyoboreshwa.

Amesisitiza wanaamini kuanza kwa utaratibu huo utawawezesha wananchi kupata kadi za afya kuanzia ngazi za zahanati zilizopo katika  vitongoji vyao na kwa asilimia kubwa utasaidia kuondoa changamoto kwa wananchi na watakuwa na uhakika wa kupata matibabu ya afya ya uhakika tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Mathew pamoja na mpango huo, kuanzia sasa huduma za utoaji wa kadi za matibabu kupitia utaratibu wa bima za CHF, utamwezesha mwananchi kupata matibabu kupitia vituo vyote vya afya tofauti na hapo awali ambapo utaratibu ulimtaka mwananchi kupata huduma kupitia kituo alichojiandikisha.
Mkufunzi Ally kebby akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo ya mpango wa utoaji huduma wa CHF iliyoboreshwa ambayo wameyatoa kwa watumishi mbalimbali wa sekta ya afya mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wakipatiwa mafunzo kuhusu namna ya kutoa huduma za Afya kupitia Mpango wa Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF)iliyoboreshwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo leo Bungeni Jijini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu .
 Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe. Japhet Hasunga  Akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa migogogoro ya mipaka kati ya hifadhi za Taifa na wananchi inapatiwa ufumbuzi leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Mbunge wa kuteuliwa ( CCM) Mhe. Anne   Kilango Malecela  akisisitiza kuhusu  Serikali kuweka mikakati ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara katika jimbo la Same ili kusaidia kukza uzalishaji wa mazao ya biashasra leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu  Bungeni  Jijini Dodoma leo.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akitoa maelezo Bungeni kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwalipa fidia askari na wapiganaji wanaoathirika wakati wanatekeleza majukumu ya kulinda usalama ndani na nje ya nchi kwenye vyombo vya Umoja wa Mataifa (UN) au SADC  leo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
 Mbunge wa  Geita Mhe.  Msukuma Joseph Kasheku akiuliza swali Bungeni leo Jijini Dodoma kuhusu ni lini Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) utawasilisha bajeti yake ya kuhudumia jamii katika Baraza la Madiwani wa Geita ili waweze kuangalia vipaumbele vyao na kuwapa vipaumbele vya Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus  Nyongo akieleza mikakati ya Serikali kuwawezesha wachimbaji wadogo katika maeneo yote nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma leo.
 Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.

 (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

NGORONGORO YAONGEZA WAWILI KUIVAA MALI, WAAMUZI YANGA vs RAYON SPORTS HADHARANI

JIJI LA DAR ES SALAAM SASA LADAIWA BILIONI 47 NA NSSF KWA MACHINGA COMPLEX


HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA LEO MEI 8, 2018

diamond platunumz show in chicago - save the date!

$
0
0
Hello CHICAGO AND ITS VICINITY
You heard if from the man himself "SAVE THE DATE"

Diamond Platnumz aka "SIMBA" A Boy From Tandale USA Tour will be live in CHICAGO On Friday JULY 6TH 2018.

This is gonna be a show for ages...

VENUE: Alhambra Palace,1240 W. Randolph Street, Chicago, IL 

For Advanced online tickets visit


For more info contact:Twitwi @ 224-623-1244

VOA SWAHILI:Duniani Leo Mei 8, 2018

MUHAS MLOGANZILA WAZINDUA HUDUMA ZA KUSAFISHA DAMU KWA WAGONJWA WA FIGO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya ambaye alikuwa mgeni rasmi (wa tatu toka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili toka kushoto) wakikata utepe wa kuzindua huduma za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) iliyofanyika katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wagongwa wakipata huduma ya  kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo ilipofanyika uzinduzi katika Kampasi ya Mloganzila leo Mei 8, 2018 jijini Dar es Salaam. Mmoja ya madaktari alionyesha mashine ya kusafisha damu.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 08.05.2018

WASATU ILIVYOVIMBA BIRMINGHAM , UINGEREZA, KUSAIDIA VIGOLI BONGO, APRIL 28

$
0
0
PICHA NA HABARI Za Freddy Macha
 Jumuiya ya Wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmingham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, vijijini, Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiriamali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. 
Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula , sanaa usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu, Tengeru. WASATU iliyoundwa mwaka 2016 chini ya udhamini wa Balozi, Uingereza, Mhe Asha Rose Migiro, inakutanisha wasanii wa ala mbalimbali chini ya viongozi- mwanamuziki na mcheza sarakasi mwenye nidhamu ya hali yajuu, Fab Moses na mtangaza mapishi ya Kitanzania, Uingereza, Bi Neema Kitilya, aliyetulizana kama shingo ya twiga....Mwaka jana, 2017, shughuli hii ilifanywa Northampton na asilimia 20 ya kipato iliwafikia Watanzania waliofikwa na maafa ya mafuriko ya maji.

3-bango la WASATU 
7- Ramasax akipuliza vituz- pic by F Macha 2018 
 Rama Sax akipuliza vitu. Zamani alipiga na Simba Wanyika akashiriki kurekodi wimbo wa “Sina Makosa”. Rama Sax pia ni mwimbaji mahiri
2- Warembo walioonesha mavazi ya Kitanzania- pic by F Macha 2018Warembo wa kujitolea, walioonesha mavazi yaliyoandaliwa na kampuni ya “All Things African” (inayoendeshwa na Mtanzania, mchapa kazi, asiyejua uvivu kabila gani, Hamida Mbaga). Toka kushoto, Yvonne Waweru, Georgeous Katega, Victoire Koleilas, Maureen Tibenda
13- Mwanamuziki Saidi Kanda akiwa na WatanzaniaMwanamuziki Saidi Kanda,(aliyesimama) mtukuzaji vyombo asilia vya muziki wa Kitanzania, akijumuika na Wabongo nadhif, waliokuwemo14- F Macha, ikiwa Ismail na Rama SaxMwandishi na mtunzi, Freddy  Macha pamoja na Likiwa Ismail (ngoma) na Rama Sax. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


TAHADHARI NA WEZI WA MITANDAO, UKILETEWA KANYABOYA HII IFUTE HARAKA

$
0
0
Ndugu wadau,
Endapo utaletewa ujume wa aina hii kwa account yako ya Instagram jua kuwa ni wezi wa mtandao na usifuate agizo lolote watalokuelekeza, nia yao kuu ni kukuibia account yako. Toka lini Insragram wakatumia email ya gmail? Anzia hapo..... JIHADHARI NA MATAPELI WA MTANDAO!!

instagramteamverifiedig@gmail.com

22:04 (10 hours ago)
to me
Hi,

Thanks for verifying your identity. You’re almost done recovering your account.

To finish the recovery process:

1. Log out of any Instagram account you may be logged into on your computer, phone or tablet.

2. When you’re completely logged out, please click here:https://goo.gl/DcSFw2

3. After you've regained access to your account, update any inaccurate contact information. Visit the help center to learn how to update your contact information:https://goo.gl/DcSFw2

4. The blue tick✅will appear to your account.

5. Finally after verifying click "yes it was me"

For more information about how to keep your account secure, visit the Instagram help center:https://goo.gl/DcSFw2

CHUO KIKUU MZUMBE CHAJADILI SEKTA ISIYO RASMI

$
0
0
LICHA ya kuchangia asilimia 35 katika pato la taifa, bado sekta isiyo rasmi haijapewa uzito unaostahili kwa kutoshiriki ipasavyo kwenye hifadhi za jamii.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Godbertha Kinyondo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa miaka minne utakaotafiti na kuonesha njia sahihi ya Sekta isiyo rasmi kupata huduma za hifadhi za jamii.
“Tumeona tufanye utafiti ili kuona namna sahihi ya kusaidia waliojiajiri kwenye sekta isiyorasmi kwa kuwa ni kundi kubwa linalofanya biashara ndogondogo zinazochangia karibu asilimia 35 kwenye pato la taifa.
“Katika mradi huu tunaziangalia sekta za aina tatu zisizo rasmi kwanza ujenzi, usafirishaji na wajasiriamali ambao ndio kundi kubwa… kama bodaboda vijana wetu wengi wamejiajiri humu lakini hawana taarifa za kutosha kuhusu haki yao ya kuingia kwenye hifadhi za jamii.
“Hawa mama lishe wengi lakini jiulize wangapi wamejisajili na NSSF? Wangapi wanazo kadi za bima ya afya? Hawa madereva wa bodaboda kila leo wanapata ajali wangapi wanazo bima za matibabu?.
“Hao ndio tunaowazungumzia na tumewaalika kwenye warsha hii waje waseme changamoto zao na tutawaambia namna ya kutoka huko ili wafanye kazi zao kwa furaha na amani wajue kwamba mchango wao kwa taifa ni mkubwa,” alisema Dk. Kinyondo.
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Utawala na Fedha), Prof. Ernest Kihanga, akisoma hotuba yake kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Miaka Minne utakaotafiti na kuonyesha njia sahihi ya sekta isiyo rasmi kupata Huduma za Hifadhi za Jamii.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Lone Riisgaard kutoka Chuo Kikuu cha Roskilde, akitoa mada.
Lone Riisgaard kutoka Chuo Kikuu cha Roskilde, akitoa mada.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NCHINI UJERUMANI ATEMBELEA TAASISI ZA UN TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas  akiwasili katika katika Taasisi ya  Umoja wa Mataifa  (UN) ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa  zilizoko eneo la Laki laki jijini Arusha Tanzania,wapili  kulia ni  Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo Ousman Njikam ,kushoto ni  Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama Sera Attika .Picha na Mahmoud Ahmad
 Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas  akisaini kitabu cha wageni ali[powasili katika katika Taasisi ya  Umoja wa Mataifa  (UN) ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa  zilizoko eneo la Laki laki jijini Arusha nchini  Tanzania .Kulia kwake ni  Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama Sera Attika.
 Msajili wa Mahakama ya jinai ya Umoja wa Mataifa UN nchini Tanzania  Sera Attika akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas  ,katikati ni Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo  Ousman Njikam ,kufuatia ziara ya kwanza ya Wwaziri huyo kutembelea Taasisi ya  Umoja wa Mataifa  (UN) ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa  zilizoko eneo la Laki laki.
 Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas  (katikati) akiwa katika Mahakama za jinai za umoja wa mataifa  zilizoko eneo la Laki laki jijini Arusha Tanzania ,kushoto ni Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama  hiyo Sera Attika .Kulia ni Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo  Ousman Njikam.

WAKULIMA NJOMBE WAFURAHIA MBEGU BORA YA MUHOGO WAWASHUKURU WATAFITI SERIKALI

$
0
0

Na: Calvin Edward Gwabara-Njombe.

Wakulima Mkoani Njombe wamewashukuru watafiti na Serikali kwa kuwezesha kupatikana kwa mbegu bora za muhogo ambazo zinauwezo wa kustawi kwenye maeneo ya baridi hasa nyanda za juu kusini baada ya utafiti wa mwaka mmoja ulifanywa na watafiti kutoka kituo cha utafiti wa kilimo cha Mikocheni MARI na chuo kikuu cha Dar es salaam.

Wakiongea kwa furaha wakati wa zoezi la kuvuna mihogo hiyo ambayo ilipandwa mwaka mmoja uliopita wakulima hao wamesema sasa wamepata zao la biashara la uhakika baada ya zao la la chai kusumbua biashara yake .

Akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake bwana Mapambano Luhongori Mkazi wa kijiji cha Lupembe wilaya ya njombe mkoani humo amesema kuwa Zao la Muhogo sasa litakuwa mkombozi kwa wakulima wengi ambao wamekuwa na shauku ya kulima zao hilo ili kuweza kunufaika na fursa kubwa ambazo wanazipata wakulima wa mikoa mingine kama vile Mara, Geita na Pwani.

‘’ Kutokana na uhitaji na soko kubwa la muhogo mkoani njombe nimejaribu mara kadhaa kulima zao la muhogo bila mafanikio lakini siamini macho yangu leo kuona katika eneo hilihili ambalo tulipanda mbegu hizi bora za watafiti kwenye shamba darasa imetoka mihogo mingi na mizuri kiasi hiki, ila nimegundua kuwa mbegu tulizokuwa tunatumia za kienyeji hazifai ukanda wetu’’ Alisema Luhongoli mkulima kutoka mkoa huo.
Wakulima na wakazi wa kata ya Lupembe Mkoani Njombe wakifurahia mavuno makubwa ya mbegu za Muhogo zinazostawi kwenye maeneo ya baridi kali.
Mtafiti kiongozi wa Utafiti huo Dkt. Joseph Ndunguru akifafanua jambo kwa wakulima mara baada ya kuvuna baadhi ya mashina hayo kwenye kila aina 75 walizopanda eneo hilo. 

Kwa upande wake Bi Rehema Malekela ambaye pia alishiriki kuanzia mwazo wa utafiti mpaka wakati huu wa kuvuna amesema kilimo cha zao hilo kilikuwa kidogo sana ambapo familia zimekuwa zikilima mashina machache kuzunguka nyumba kwaajili ya vitafunywa vya chai tu baada ya kuona zao hilo haliwezi kuwapatia tija kama wakulima wa maene mengine nchini.

Bi Malekela ameongeza kuwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani waislamu hupata shida sana kupata muhogo na hivyo kuwalazimu baadahi ya wafanyabiashara wengi kwenda kufuata mihogo kwenye mikoa mingine inayozalisha zao hilo kwa wingi na kuja kuiuza mkoani humo kwa bei kubwa.

“ Kwakweli ukifunua moyo wangu na moyo wa kila mtu unayemuona hapa aliyekuja kushiriki zoezi hili utaona furaha isiyo na kifani ndio maana unaona tumejitokeza kwa wingi watu kutoka Tarafa nzima kuja kushuhudia kupatikana kwa zao linguine la biashara kwenye eneo letu” Alisema Bi. Malekela kwa niaba ya wakina mama wengine.
Mamia ya wakulima na wakazi wa Kata ya Lupembe na maeneo mengine waliojitokeza kuangalia matokeo hayo ya utafiti kuona kama wanaweza kulima Muhogo kwenye ukanda huo wa baridi kali.

BENKI YA DUNIA YATOA MAFUNZO YA SIKU MBILI KWA WATUMISHI WA SERIKALI

Balozi Seif awataka wananchi kuchangia damu

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa kila Mwananchi mwenye sifa za uchangiaji damu kuanzia umri wa Miaka 18 hadi 65 uzito wa Kilogram 50 ajitokeze kujitolea kuchangia damu ili kuiepusha Jamii kukumbwa na upungufu wa damu salama Nchini ambao wakati mwengine huleta athari.

Alisema upungufu mkubwa wa Damu uliojitokeza Mwaka uliopita hasa katika Kipindi Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa mujibu wa Taarifa za uchangiaji Damu Salama katika Maabara za Mahospitali Zanzibar ulipelekea kwenda kuomba Damu Tanzania Bara.

Akizungumza katika Bonaza la Uchangiaji Damu Salama lililoandaliwa na Mkoa wa Kusini Unguja na kufanyika Dunga Wilaya ya Kati Balozi Seif Ali Iddi alisema kwa mujibu wa Takwimu zilizopo inaonyesha kwamba mahitaji halisi ni chupa 1,250 kwa Mwezi kwa matumizi ya kawaida Unguja na Pemba.

Balozi Seif alisema shughuli za uchangiaji wa damu salama  humgusa kila mwana jamii  hivyo ipo faida kubwa inayopatikana licha ya kuokoa maisha ya walio wengi ambao hupatwa na matatizo ya kiafya lakini pia humrahisishia Mtu kuweza kupima maradhi mbali mbali bure bila ya gharama sambamba na kuelewa afya yake.

Aliwaasa Wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa maisha yao wenyewe wakiwa kama wana Jamii hasa wanapoelekea katika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani  ambao wengi hushindwa kuchangia Damu kwa wakati  pale wanapokuwa na mgonjwa anayehitaji huduma hiyo kwa haraka.
 Wataalamu wa Kitengo cha Huduma  za Damu Salama wakianza zoezi la kuwapima Wananchi waliojitokeza kuchangia Damu kwenye Bonaza la Uchangiaji Damu la Mkoa Kusini Unguja lililofanyika Wilaya ya Kati Dunga.
Wananchi mbali mbali wakipata ushauri nasaha kutoka kwa Wataalamu wa Kitengo cha Huduma  za Damu Salama kabla ya kuchangia Damu kwenye Bonaza la Uchangiaji Damu la Mkoa Kusini Unguja.
Afisa uhamasishaji wa kuchangia Damu kutoka Jumuiya ya Wachangiaji Damu Zanzibar Bwana Bakari Mabarawa aliyenyanyua  mikono akimpatia maelezo Balozi Seif jinsi ya Kampeni ya Uchangiaji Damu Salama unavyofanywa katika maeneo mbali mbali Nchini.
Mmoja wa Mchangiaji Damu aliyejitokeza kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bwana Sabri Yussuf Ali akichangia Damu kwenye Bonaza la Uchangiaji Damu la Mkoa Kusini Unguja lililofanyika Wilaya ya Kati Dunga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wananchi wakati wa kichangia Damu kwenye Bonaza la Uchangiaji Damu la Mkoa Kusini Unguja lililofanyika Wilaya ya Kati Dunga.
Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images