Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI,AFUNGUA DARAJA KUBWA MTO KILOMBERO LILOLOPEWA JINA NA DARAJA LA MAGUFULI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro.
DCIM100MEDIADJI_0568.JPG
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi mbalimbali wa Dini, Serikali, Wabunge wa mkoa wa Morogoro na Viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali mara baada ya kufungua Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula kona katika Wilaya ya Kilombero wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli lenye urefu wa M384) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika msiba wa mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerald mara baada ya kutoa rambirambi wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mang’ula Mrindoko Msangi mara baada ya kumkabidhi kiasi cha Shilingi milioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule hiyo. Mwanafunzi huyo alielezea kwa ufasaha kero inayowakabili shuleni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye msiba wa mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerald mara baada ya kutoa rambirambi wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

PICHA NA IKULU

MBEYA PRESS CLUB WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KWA MJADALA MKUBWA KATIKA UKUMBI WA MKAPA JIJINI MBEYA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw. Paul Ntinika akizungumza wakati akifungua mkutano wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club) unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo yanafanyika kila mwaka Mei 3 waadishi wa Habari mkoa wa Mbeya wamadhimisha siku hiyo leo, Kutoka kulia ni Frank Leonard Mwenyekiti wa Press Club Iringa, Modest Nkurlu Mwenyekiti wa Mbeya Press Club na kushoto ni Fredy Jackson Kaimu Katibu Mkuu Mbeya Press Club. KAULI MBIU ya maadhimisho hayo mkoa wa Mbeya ni "Uhuru wa Vyombo vya habari ni Chachu ya Uwajibikaji kwa Maendeleo ya Mkoa wa Mbeya" 
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw. Paul Ntinika wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Frank Leonard Mwenyekiti wa Iringa Press Club wakati akizungumza katika mkutano huo kama mmoja wa wageni waalikwa, katikati ni Modest Nkurlu Mwenyekiti wa Mbeya Press Club na kushoto ni Fredy Jackson Kaimu Katibu Mkuu Mbeya Press Club.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya Bi. Julieth Godrey Manech akichangia na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa upande wa Taaisis ya Kuzuia rushwa nchini TAKUKURU jinsi waandishiwa wanavyoweza kushirikiana na tasisi hiyo.

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO AZINDUA MASHINDANO YA AWESO CUP,MURO NA MANARA WANOGESHA

$
0
0



Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akikagua wachezaji wa timu ya Mashabiki wa Yanga muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya mashabiki wa Yanga na timu ya mashabiki wa Simba leo mjini Pangani.




Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya mashabiki wa Simba muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Kushoto kwake ni Msemaji wa Timu ya Simba Bw. Haji Manara na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akifurahia jambo na Msemaji wa Timu ya Simba Bw. Haji Manara wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na Timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdallah.




Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na aliyewahi kuwa Msemaji wa Timu ya Yanga Bw. Jerry Muro wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na Timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdallah.




Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza na waandishin wa Habari muda mfupi kabala ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Aweso Cup kati ya timu ya Mashabiki wa Yanga na Timu ya Mashabiki wa Simba leo mjini Pangani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso ambaye ni mdhamini wa mashindano hayo.




Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akipokea fedha taslimu shilingi milioni moja kutoka kwa Bw. Romanus Mkonda Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani kama mchango kwa ajili ya mashindano ya Aweso Cup.Kulia kwake Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zainabu Abdallah wakishuhudia tukio hilo leo mjini Pangani.


PICHA ZOTE NA:OCTAVIAN Kimario


WHUSM

TIRA IKISHIRIKIANA NA TAASISI YA BIMA NCHINI IIT YAZINDUA MFUMO WA TIIP

$
0
0

Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo A. Saqware akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo mara baada ya kuzindua mfumo wa kieletroniki ujulikanayo kama Tanzania Imports Insurance Portal(TIIP)utakao wezesha waagizaji bidhaa nje ya nchi kununua Bima toka kampuni za kitanzania,mfumo huo umeandaliwa na TIRA ikishirikiana na Taasisi ya Bima nchini (IIT)warsha iliyofanyika juzi jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa Bima.(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Meneja wa kanda kaskazini wa usimamizi mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elieza Rweikiza akizungumza katika mafunzo hayo jijini Arusha Juzi
Wadau wa Bima wakisikiliza kwa makini
Mkurugenzi wa Leseni na Usimamizi wa Mwenendo wa Soko Samwel Mwiru akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ambapo pamojana mambo mengine alisema kuwa Soko la bima Tanzania linaendeshwa na kampuni za bima zipatazo 31,madalali takribani 150 na wakala wa bima wapatao 413,Sekta ya bima husimamiwa na Mamlaka ya usimamizi wa bima (TIRA)kwa mujibu wa sheria ya bima ya mwaka 2009
Rais wa Taasisi ya Bima Tanzania BoscoJames Bugali akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha.

RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY

$
0
0
Rapper maarufu wa nchini Cameroon, Atanga Schneider Ngomah maarufu kama Ngoma, ameachia video ya wimbo wake mpya, All Les Day. All Les Day ina maana ya ‘Kila Siku.’ Ukitayarishwa na producer wake wa miaka mingi, Dijay Karl, huu ni wimbo wenye mahadhi ya Hip hop na Trap iliyonakishwa na mitindo asili ya uchanaji katika viunga vya mitaa maarufu ya Cameroon.
Pia ina vionjo vya mtindo wa Jwe’te ambao ni mchanganyiko wa muziki wa asili wa kabila la Ngemba ambavyo vinasikika kwa mara ya kwanza kwenye wimbo. Amesema vionjo hivyo vitasikika zaidi kwenye nyimbo zake zijazo.  Pamoja na kutumia Pidgin English (Kiingereza kizungumzwacho Cameroon), Ngoma ametumia Kifaransa pamoja na kabila na Ngemba kwenye wimbo huu. Video yake imeongozwa na Shamak Allharamaji.
Ngoma si mgeni kwenye masikio na macho ya mashabiki wa muziki wa Tanzania. Mwaka jana akiwa na wimbo wake maarufu, Mangosi, alifanya ziara ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika vituo vya redio na TV vikiwemo Clouds TV, East Africa Radio, EFM, Times FM na Magic FM.
Katika ziara yake hiyo, Ngoma alifanikiwa kurekodi collabo na Ray Vanny katika studio za Surprise Music chini ya producer Rash Doni, huku mdundo na ukamilishaji wa wimbo ukifanywa na Dijay Karl. Amepanga kuachia wimbo huo mapema mwakani wakati wa shamrashamra za Kombe la Mataifa ya Afrika.  Pia Ngoma amesema baada ya kuachia video takriban nne, ataachia album yake inayosubiriwa kwa hamu, G.O.AT. (Greatest of All Time).

DICOTA Young Leader Scholarship NOW OPEN!

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAPONGEZA KAZI INAYOFANYWA NA TAGLA

Kampuni ya utafiti wa madini ya CANACO yapewa siku saba kuwasilisha mkataba serikalini Inbox x

$
0
0
Na Greyson Mwase, Tanga
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameipa siku saba kampuni  inayojishughulisha na utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wilayani Handeni ya CANACO Tanzania Limited, kuwasilisha mikataba na nyaraka zote kati yake na kampuni ya Tanzania Gold Field Limited ili kubaini namna makubaliano  ya mkataba yalivyofanyika ikiwa ni pamoja na ulipaji kodi serikalini,
Biteko aliyasema hayo  alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyasa kilichopo  wilayani Handeni mkoani Tanga mara baada ya kufanya ziara katika kampuni ya CANACO Tanzania  Limited na kutoridhishwa na utendaji wa kampuni hiyo.
Waziri  Biteko yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua shughuli za madini pamoja na kuzungumza na wananchi na kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika shughuli za madini.
Alisema mara baada ya kufanya ziara katika kampuni ya CANACO Tanzania Limited, amebaini kuwa kampuni hiyo mara baada ya kukamilisha shughuli zake za utafiti wa madini ya dhahabu, kampuni hiyo iliikaribisha kampuni nyingine ijulikanayo kama Tanzania Gold Field Limited ya Canada kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo la Magambasi wilayani Handeni mkoani Tanga pasipo kufuata taratibu za kisheria.
Aliendelea kusema kuwa, kampuni ya Tanzania Gold Field Limited iliwataka wachimbaji wadogo waliokuwa wanaendelea na shughuli za uchimbaji madini katika eneo hilo kuondoka ili waanze uchimbaji madini jambo ambalo lilitekelezwa.
Alieleza kuwa, kampuni ya Tanzania  Gold Field Limited ilianza shughuli zake bila kuwasilisha makubaliano ya kimaandishi kati yake na kampuni ya CANACO Tanzania Limited  Serikalini pamoja na kodi jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.
Biteko aliendelea kusema kuwa kampuni inayotambulika mpaka sasa kisheria ni ya  CANACO Tanzania Limited ambapo shughuli za madini katika eneo la Magambasi zimekuwa zikifanyika bila kufuata sheria na kanuni za mazingira.
“Haiwezekani wachimbaji wadogo ambao ndio wamiliki wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wakaondolewa halafu akapewa mwekezaji mkubwa ambaye mpaka sasa hakuna kilichofanyika zaidi ya kuchejua mabaki wa udongo wenye dhahabu na kuuza na kuharibu mazingira huku wachimbaji wadogo  wenye uwezo wa kuchimba dhahabu wakihangaika na kuishi katika lindi la umaskini,” alisema Biteko.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) akiendelea na ziara katika  eneo la kampuni inayojishughulisha na utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wilayani Handeni ya CANACO Tanzania Limited.

 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( wa pili kutoka kulia) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kampuni  inayojishughulisha na utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Magambasi wilayani Handeni ya CANACO Tanzania Limited.
 Sehemu wa wananchi wa kijiji cha Nyasa kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akifafanua jambo mbele ya wananchi wa kijiji cha Nyasa kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe (kushoto) akielezea mchango wa sekta ya madini kwenye wilaya yake mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia).

KOMBE LA IGP SIRRO KUWAKUTANISHA VIJANA KIBITI.

$
0
0
Maandalizi kwa ajili ya uzinduzi wa michezo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (Sirro CUP Kibiti 2018) hatua ya 16 bora yamekamilika kwa asilimia tisini na yanatarajiwa kuzinduliwa siku ya Jumatatu na IGP Simon Sirro katika uwanja wa Samora wilayani Kibiti.
Akizungumza wilayani Kibiti baada ya kukagua maandalizi hayo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi Barnabas Mwakalukwa amesema lengo la Michezo hiyo ni kuwaweka pamoja wakazi wa Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji baada ya matatizo yaliyowakumba kumalizika.
« Michezo hii ni fursa nyingine ya kuwakutanisha wakazi wa Wilaya hizi na kuihakikishia dunia kuwa sasa maeneo haya ni salama na Tanzania ni salama baada ya wahalifu waliosumbua hapo awali kudhibitiwa » Alisema Mwakaluka.
Aidha amewaomba wakazi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia burudani mbalimbali pamoja na maneno ya viongozi mbalimbali yatakayotolewa katika ufunguzi wa michezo hiyo.
Kwa upande wake Mratibu wa Kombe hilo, Koplo Ramadhan Tamimu amesema michezo hiyo itakapofikia tamati bingwa atajinyakulia kombe na fedha taslimu Milioni moja huku yakichagizwa na kauli mbiu ya “Kibiti Salama, Jamii Salama”

Naye Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kibiti Rashid Mkingaamesema wamejiandaa vyema na anauhakika wa kombe hilo kubaki wilayani Kibiti kwa kuwa pamoja na kuwa na timu bora lakini pia wanatarajia kupata mashabiki wengi.

Ufunguzi huo utapambwa na burudani mbalimbali zikiongozwa na  Bendi ya dansi ya Jeshi la Polisi, Msanii wa nyimbo za asili Ndolela, Man Prince na vikundi mbalimbali kutoka Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

SERIKALI KUTUMIA BILIONI 131.47 KUTEKELELEZA MIRADI YA KIMKAKATI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM,  Dodoma
 Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, Serikali imezindua Mkakati wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za     Mitaa kutekeleza miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea.
 Mkakati huo umezinduliwa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambapo amesema kiasi cha shilingi bilioni 131.47 kitatumika kutoa ruzuku ya utekelezaji wa miradi 22 kwa halmashari 17 zilizoko katika mikoa 10 nchini, katika mwaka wa fedha 2018/19.
 Ameitaja mikoa hiyo ambayo Halmashauri zake zimekidhi vigezo vya kunufaika na miradi ya kimkakati katika awamu ya kwanza ya mpango huo kuwa ni Dar es Salaam, Geita, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Morogoro, Mtwara, Pwani, Simiyu na Songwe.
 Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa Halmashuri zinajenga uwezo wa kujitegemea kwa takribani asilimia 80 hadi 100 ifikapo mwaka 2025, badala ya hali ya sasa ambapo halmashauri hizo zinategemea ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa zaidi ya asilimia 88.
Amezitaka halmashuri zitakazopata fedha za miradi hiyo kuhakikisha fedha hizo zinawekezwa kwenye miradi yenye tija, inayokuza ajira kwa wananchi na kuongeza mapato ya halmashauri.
Ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri kubuni miradi ya kibiashara kwa ajili ya wananchi wanaowaongoza kwa kutengeneza ajira kwa kutumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Alionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watendaji wanaosimamia miradi hiyo ikiwa watatumia fedha hizo kwa malengo tofauti na yaliyokusudiwa na kurejea kauli ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwamba kufuja fedha za Serikali katika kipindi hiki ni sawa na kunywa sumu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, amesema kuwa Serikali inazo fedha za kutosha kufanikisha mkakati huo na kutoa wito kwa viongozi wa Mikoa husika kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanisha miradi yenye tija ili ipatiwe fedha.

Alifafanua kuwa tayari Serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 15 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati katika mkoa wa Dar es Salaam katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwa kujenga Kituo cha Mabasi cha Mbezi Luis, Ujenzi wa Soko la Mburahati katika Manispaa ya Ubungo, Ujenzi wa Soko la Kisasa la Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni na Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kisutu, Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa ya Vingunguti katika Manispaa ya Ilala.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Selemani Jaffo (Mb) amesema kuwa Ofisi yake itaanza kufuatilia na kupima utendaji kazi wa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini ili kuona kama wanaendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliwapongeza Wakurugenzi walioonesha mfano katika kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kubuni miradi yenye tija na ya kimkakati iliyopewa Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango na kuwataka watendaji wengine waige mfano huo.

Baadhi ya miradi itakaotekelezwa na Halmashauri zilizokidhi vigezo ni pamoja na Ujenzi wa Masoko ya Kisasa, Ujenzi wa Maegesho ya Malori, Ujenzi wa stendi za kisasa, Maghala ya kuhifadhi mazao, Masoko ya Kisasa, Machinjio na Ujenzi wa Viwanda.
 Wadau kutoka Sekta mbalimbali wakiwemo wabunge, wakurugenzi wa TAMISEMI na viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango waliohudhuria Uzinduzi wa Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo (Mb).
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa- TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo (Mb) wakinyanyua vitabu vya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka, akinyanyua Kitabu cha Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa-TAMISEMI, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kusaini mikataba ya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushuhudia kutiwa saini mikataba ya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea, Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Sekretarieti ya maandalizi ya Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutekeleza Miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea baada ya kushuhudia utiwaji saini wa mkakati huo, Jijini Dodoma.

SIR ALEX FERGUSON AFANYIWA UPASUAJI KATIKA UBONGO WAKE, AWEKWA CHINI YA UANGALIZI MAALUM

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson imebainika amefanyiwa Upasuaji katika Ubongo wake baada ya hapo awali kuripotiwa kuumwa ghafla.

Manchester United kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter imetoa taarifa ya kuumwa kwa Sir Ferguson kwa kusema kuwa "Tayari ameingia kufanyiwa upasuaji wa Ubongo wake na zoezi linaendelea vizuri lakini anahitaji kuwa katika Uangalizi maalum kwa msaada ili arudi katika hali yake ya kawaida".

Kabla yakuumwa, Sir Alex Ferguson hapo nyuma alinekana katika mchezo kati ya Man United dhidi ya Arsenal, Old Trafford wakati wakumuaga Kocha wa Washika Mitutu wa London (Gunners), Arsene Wenger anayeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.


Sir Alex Furguson alishinda Mataji 13 ya Ligi Kuu Soka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka 26 alipokuwa akiifundisha Manchester United kabla yakustaafu mwaka 2013.

Chanzo: Goal. com
 

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI YAFANA ZANZIBAR

$
0
0
 Baadhi ya Wauguzi wa Zanzibar walioshirki  maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani wakiwa katika maandamano kuelekea Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni ambako maadhimisho hayo yalifanyika rasmi ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed.
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashind Mohamed akizungumza na wakunga katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawawkilishi la zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Bi. Amina Abdulkadir Ali akzungumza na wakunga katika maadhisho hayo yaliyofanyika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulika Idadi ya watu (UNFPA) Batula Abdi Hassan akizungumza na wauguzi walioshiriki maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani katika Ukumbi wa Baraza la Wawawkilishi la zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akimkabidhi cheti mmoja wa Wauguzi bora Bi. Rose Abdalla ambae ni mkufunzi mwandamizi kutoka Chuo cha Taaluma ya Sayansi za Afya ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar
Wauguzi kutoka vituo mbali mbali vya Afya Zanzibar walioshiriki maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni (PICHA NA ABDALLA OMAR – MAELEZO ZANZIBAR).

WAZIRI KAIRUKI AKABIDHI VIFAA VYA DOLA 350,000 KWA OFISI ZA MADINI ZA KANDA

$
0
0

Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amekabidhi vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya jumla ya Dola za Marekani 350,000 kwa Ofisi za Madini za Kanda mbalimbali nchini.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda hizo, jana Mei 4 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma; Waziri Kairuki aliwataka wahusika kuvitunza kutokana na gharama kubwa iliyotumika kuvinunua.
“Serikali imekopa kwa ajili ya kuhakikisha sekta ya madini inaendelezwa ili iweze kuchangia zaidi katika uchumi wa nchi. Tunaamini vitawasaidia sana katika utendaji wa majukumu yenu. Mvitunze.”
Akifafanua kuhusu vifaa vilivyotolewa, Waziri alisema kuwa ni pamoja na kifaa maalum kinachotumia teknolojia ya kisasa kung’amua uwepo wa aina ya gesi hatarishi kwa afya, chini ya Migodi ya Madini.
Alisema kuwa kifaa hicho kinamsaidia muhusika kutambua sehemu yenye hewa hiyo hatarishi na hivyo kuchukua hatua stahiki za kujiepusha na ajali inayotokana na kuvuta hewa ya aina hiyo.
Aidha, alitaja vifaa vingine kuwa ni kifaa maalum cha kukuza taswira za madini kinachojulikana kitaalam kama ‘Hand Lens’. “Kifaa hiki hutumika katika shughuli za uthaminishaji madini ya vito ambapo husaidia kuyakuza madini husika katika ukubwa unaotakiwa ili kukokotoa thamani yake halisi tofauti na unapotumia macho ya kawaida,” alifafanua.
Vingine ni pamoja na GPS zinazotumika kupima mipaka ya maeneo, ‘Printer’, viatu na sare maalum vinavyotumika migodini, Kompyuta, na vifaa vingine vya kijiolojia.
Kwa upande wake, Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya alisema kuwa vifaa hivyo vimetolewa kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (SMMRP).
Alisema kuwa, zoezi la kugawa vifaa hivyo limefanyika katika awamu kadhaa, ambapo kwa awamu ya kwanza, Kanda za Madini zilizogawiwa ni Kanda ya Kusini (Mtwara na Nachingwea), Kanda ya Ziwa Nyasa (Songea, Njombe na Tunduru), Kanda ya Kusini Magharibi (Chunya) na Makao Makuu ya Wizara (Ofisi ya Ukaguzi wa Migodi, wachimbaji wadogo na utoaji leseni).
Nyingine ni Ofisi za Madini za Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga, Handeni, Musoma, Bariadi, Mpanda, Kigoma, Mwanza, Geita, Bukoba, Arusha, Moshi, Mirerani na Tabora.
“Vifaa vilivyobaki ni kwa ajili ya Ofisi za Shinyanga, Kahama, Kituo cha Uongezaji Thamani Madini (TGC), Ofisi ya Biashara ya Madini na Ofisi ya Kamishna wa Madini, ambao ndiyo wanaopatiwa leo hii,” alifafanua Prof. Manya.
Akizungumza baada ya zoezi hilo la kukabidhi vifaa; Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof Idris Kikula alisema kuwa, ni jambo la kutia faraja kwa kupata vitendea kazi kwa Ofisi hizo za Madini, ambazo kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria ya Madini yaliyofanyika mwaka 2017, sasa ziko chini ya Tume.
Alisema kuwa, upatikanaji wa vifaa hivyo vya kisasa utasaidia Tume kutimiza jukumu lake kubwa la kusimamia mapato stahiki ya Taifa yanayotokana na shughuli za madini.

  Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kushoto) akikabidhi vitendea kazi mbalimbali kwa baadhi ya Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda, Makao Makuu ya Wizara Dodoma, Mei 4 mwaka huu.
 Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (mwenye mtandio-mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda na watendaji wengine wa Wizara, baada ya zoezi la kukabidhi vitendea kazi lililofanyika Mei 4 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma. Kushoto kwa Waziri ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akifuatiwa na Kamishna wa Madini ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya. Kulia kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof Idris Kikula.
 Kutoka kulia ni Waziri wa Madini Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (SMMRP) Andrew Eriyo, wakiangalia baadhi ya vitendea kazi kwa ajili ya Ofisi za Madini nchini, muda mfupi kabla ya Waziri kuvikabidhi kwa wahusika, Mei 4 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara Dodoma.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akizungumza na Waandishi wa Habari, baada ya zoezi la kukabidhi vitendea kazi kwa Ofisi za Madini za Kanda, lililofanyika Mei 4 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA JENGO LA HUDUMA ZA MATUNZO NA TIBA KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI MANYARA

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama  akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI linalojengwa katika Halimashauri ya Wilaya ya Simanjaro ,Mkaoani  Manyara Mei 05, 2018.
 Mganga Mfawidhi Hassan Ishabailu akitoa ufafanuzi wa huduma za afya zinazotolewa na  Kituo cha Afya Mirerani kwa  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama  alipozindua Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mkoani Manyara.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakati wa Uzinduzi wa Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mei 05, 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akifafanua jambo wakati wa mkutano na wananchi wa Simanjiro (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi wa Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mkoani Manyara.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wagonjwa aliyekuwa akisubiri huduma za matibabu katika Kituo cha Afya Mirerani wakati wa Uzinduzi wa Jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mei 05, 2018
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwapongea baadhi ya wazazi waliojifungua katika Kituo cha Mirerani Mkoani Manyara wakati wa Uzinduzi wa Jengo la jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi yake anayeshughulikia Waziri Mkuu na Bunge Bi.Maimuna Tarishi wakati wa uzinduzi wa jengo la kutoa huduma za Matunzo na Tiba (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Mkoani Manyara.
Mbunge wa Viti Maalum Manyara, Mhe.Ester Mahawa akikabidhi msaada wa mashuka kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Mirerani kilichopo Wilaya ya Simanjiro kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

INAKUPONGEZA KWA KULA NONDOZ (MASTERS IN INTERNATIONAL BUSINESS COMMUNICATION NCHINI MALAYSIA

$
0
0
Catherine Cornel Nyoni (Mama Gerson Msigwa) ala Nondoz (Masters in International Business Communication, Asia Pacific University Kuala Lumpur Malaysia. Hongera sana. 

BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA KUANZA MITIHANI KIDATO CHA SITA,UALIMU

$
0
0


*Watakaofanya udanganyifu wa aina yoyote kukiona cha moto

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BARAZA la Mitihani la Tanzania(Necta) limetoa onyo kali kwa wamiliki wa shule,walimu na wananchi kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa mitihani ya Kidato cha Sita na Kozi za ualimu inayoanza kesho Mei 7 hadi Mei 25 mwaka huu.

Kwa mujibu wa baraza hilo  ni kwamba jumla ya watahiniwa 87,643 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 77,222 na watahiniwa wa kujitegemea ni 10,421.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Necta Dk.Charles Msonde ametangaza kuanza kwa mitihani hiyo ambapo ameonya watu kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.Akisisitiza Dk.Msonde amesema baraza la mitihani halitasita kumchukulia hatua yeyote atakayejihusisha kufanya udanganyifu katika mihitani kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma na sheria za nchi.

Amefafanua ikiwa panoja na kuwafutia matokeo yote watahiniwa watakaobainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu."Wadadau wore wanaombwa kutoa taarifa katika vyombo husika kila wanapobaini uwepo wa mtu au kikundi cha watu kujihusisha na udanganyifu wa mitihani wa aina yoyote ile," amesema Dk.Msonde.Pia amesema baraza linatoa mwito kwa jamii kutoa ushirikiano katika kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika kwa amani na utulivu .

"Wananchi wanaombwa kuheshimu eneo la mitihani na kuhakikisha asiyehusika  haingii maeneo ya shule,"amesema Dk.Msonde.Ameongeza wamiliki wa shule na vyuo wanatakiwa kutambua shule na vituo vya maalum vya mitihani  na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingiliwa majukumu ya usimamizi wa mitihani kwa kipindi chote hicho.

" Baraza halitosita kukifuta kituo chochote cha mtihani endapo litajiridhisha kuwa uwepo wake ubahatarisha usalama wa mitihani ya Taifa,"amesema Dk.Msonde.Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha taratibu zote za uendeshaji mitihani ya Taiga zinazingatiwa ipasavyo.

Kwa upande wa wawatahiniwa ,amesema baraza linaamini walimu wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha elimu ya sekondari na kozi za mafunzo ya ualimu.Hivyo matarajio yao watahiniwa watafanya mitihani yao kwa kuzingatia kanuni za mitihani ili matokeo yaoneshwe uwezo wao halisi kulingana na maarifa na ujuzi walioupata kipindi cha mafunzo yao.

 Katibu Mtendaji wa Necta Dk.Charles Msonde akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo alipokuwa akitangaza kuanza kwa mitihani hiyo ambapo ameonya watu kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.

WAZIRI UMMY MWALIMU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KIWANDA CHA DAWA CHA M-PHARMACEUTICALS WILAYANI BAGAMOYO

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wapili kulia), akishirikiana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu kulia) Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wanne kulia) na Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Media, Dk. Reginald Mengi (watano kulia) kuzindua uwekaji wa jiwe la msingi la kiwanda cha dawa za binadamu  unaoatarajiwa kuanza hivi karibuni, ikiwa ni katika juhudi za ukuzaji sekta ya viwanda nchini.Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (watatu kulia), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wapili kulia) ,Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo(wakwanza  kulia), Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Media, Dk. Reginald Mengi(wanne kulia) na viongozi wengine wakimsikiliza Mtaalamu wa michoro,Ruchir Sharma akielezea na kuonyesha ramani ya kiwanda cha dawa kinachotarajiwa kujengwa eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo baada ya Waziri Ummy kuweka jiwe la msingi wa ujenzi huo. Hafla hiyo imefanyika  wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa  za Binadamu kinachomilikiwa na Dk. Reginald Mengi, kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo aliwahakikishia wawekezaji wazawa katika sekta ya afya kupata ushirikiano kutoka serikalini.Hafla hiyo imefanyika  wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage   akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa za Binadamu  kinachomilikiwa na Dk. Reginald Mengi, kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo aliwahakikishia wawekezaji wazawa katika sekta ya viwanda na uwekezaji  kupata ushirikiano kutoka serikalini.Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Media, Dk. Reginald Mengi, akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa za Binadamu kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo alishukuru ushirikiano aliopata kutoka serikalini wakati wa mchakato wa uanzishwaji kiwanda hicho .Hafla hiyo imefanyika  wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
 Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza la Bagamoyo,Muyengi Machumu,Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza,Malisa Emmanuel na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bagamoyo Adam Maro, wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(hayupo pichani) wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha dawa za binadamu Kerege wilayani Bagamoyo.
Wasanii kutoka Chuo cha Sanaa Bagamoyo wakitoa burudani wakati wa Sherehe za Uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha dawa za binadamu unaoatajiwa kuanza hivi karibuni katika eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Picha  na Abubakari Akida

MAKAMU MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AWAONGOZA WANANCHI KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE YA MSINGI NYANDOTE WILAYANI RUFIJI

$
0
0
NA ELISA SHUNDA, MUHORO-RUFIJI

WANANCHI na Wadau mbalimbali waombwa kushikamana kwa pamoja na kuondoa tofauti ya itikadi za kivyama na kushiriki kwa pamoja kuisaidia serikali katika ukuzaji wa maendeleo ya jamii katika Nyanja mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Mazingira na sekta ya Miundombinu.



Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mh. Haji Haidari kwenye harambee ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Nyandote iliyopo Kata ya Muhoro wilayani Rufiji ambapo alisema kuwa hadi jumuiya hiyo ya wazazi kufikia uamuzi wa kufanya harambee ya ujenzi wa shule hiyo ni kutokana na umbali uliopo wa Kilometa 12 kutoka kwenye Kijiji cha Nyandote na Shule ya Msingi Muhoro hali iliyosababisha wanafunzi walio wengi kutomaliza shule kulingana na changamoto mbalimbali ikiwemo kubakwa na kulawitiwa njiani na watu waovu,mimba,njaa na umbali wa shule ilipo.



“Nawapongeza wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama na jumuiya zake kwa kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha tunafanikisha harambee hii ya ujenzi wa shule ya msingi ya Nyandote ambapo si kwa faida ya watoto wa wanachama wa CCM peke yake bali ni watoto wa jamii nzima nawashukuru sana kwa mlivyojito.



“Kwa kujitolea kwenu huku shule ya msingi Nyandote ikikamilika tutakuwa tumewasaidia wanafunzi 430 kuanza masomo yao lakini pia tutakuwa tumewaepusha wanafunzi hao na kutembea umbali mrefu wa Kilometa 12 kuja shuleni Muhoro pia tutawaepusha na vishawishi mbalimbali za njiani,tutawaokoa na kubakwa na kulawitiwa njiani na watu waovu” Alisema Mh.Haidari
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Haidari Haji (katikati) akikabidhi mifuko 230 pamoja na fedha taslimu Sh. 650,000 kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa na Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Nyandote iliyopo Kata ya Muhoro Wilayani humo jana. Picha zote na Elisa Shunda. 
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Muhuro,Mary Msigwa (katikati) akizungumza mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Haidari Haji (kulia) kuhusu kupokea mifuko 230 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Nyandote na amekabidhiwa Sh. 440000 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya choo kwenye shule ya Msingi ya Muhuro iliyopo wilayani Rufiji.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Haidari Haji akizungumza na wananchi kuhusu kupokea Sh.200,000 na Mifuko ya Simenti 100 kutoka kwa Mwenyekiti wa Uchumi Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Rufiji,Juma Salum Mpendu “Chogo” kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la Nyandote
Wazee wakifuatilia kwa umakini mkubwa mkutano huo wa harambee kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya choo kwenye shule ya Msingi ya Muhuro iliyopo wilayani Rufiji .

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Pwani, Jackson Kituka akizungumza kwenye mkutano huo wa harambee.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATU 200 WANAAMBUKIZWA VVU KWA SIKU/50 VIJANA -MABOKO

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani.

ASILIMIA 48 ya wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) hawajapima kujua afya zao ambapo asilimia 52 pekee walio na virusi hivyo ndio wanaodaiwa kupima kubaini hali zao.

Aidha imeelezwa watu 81,000 Tanzania wanaambukizwa maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa mwaka, watu 200 wanaambukizwa maambukizi hayo kwa siku,ambapo kati yake 50 ni vijana.

Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) ,Leonard Maboko aliyasema hayo,wakati akifungua mkutano wa mpango mkakati wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo kwa kushirikiana na waandishi wa habari,Mjini Kibaha,Pwani.

Alisema ukimwi bado ni tishio na ni ajali kama zilivyo ajali nyingine ambayo haionekani lakini ni ajali mbaya kutokana na kusababisha maambukizi mapya kila siku kwa watu 200 idadi ambayo sio ndogo.“Kutokana na hali hii kuna malengo ya kitaifa mawili iikiwemo kuwa na 90 tatu, ambapo asimilia 90 ya kwanza ni ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini ambao bado hawajajitambua afya zao kuhakikisha wawe wamepima ifikapo mwaka 2020”alisema Maboko.

Pia ,wanaoishi na virusi vya ukimwi ifikapo 2020 wawe wameingia katika kutumia dawa za kufubaza VVU na ifikapo mwaka huo asilimia 90 ya ambao wanatumia dawa hizo wawe na virusi vilivyokuwa tayari vimefubaa.Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo,lengo jingine ni kutimiza 000 na ifikapo 2030 kuondoa maambukizi mapya ya UKIMWI,Unyanyapaa na Vifo.“Malengo ya 90 tatu ,kwa Tanzania 90 ya kwanza ina shida , tunafanya vizuri katika 90 ya pili na ya tatu ambapo 90 ya pili tuna asilimia 91 tunafanya vizuri, kuwa watanzania waliopima wamehakikisha wanatumia dawa,na 90 ya tatu ni asilimia 88 ambayo walianza dawa na kufubaza virusi .

Maboko ,alisema 90 ya kwanza ya kuhakikisha walio na virusi wanapima hali zao hatufanyi vizuri kwani wanaojitokeza kujua hali zao hawajitokezi.Alielezea asilimia 52 ya walio na virusi waliopima hali zao waliweza kujibaini wakati asilimia 48 hawajui afya zao.“Kwa kutumia kalamu zenu tusaidieni hili,mtusaidie kutoa elimu,kuhamasisha watu wakapime ,na tunatarajia kuanza kampeni za uhamasishaji ,tukumbushane kwani ugonjwa huu una dawa za kufubaza virusi hivyo endapo utagundulika kuambukizwa”alisisitiza Maboko.

Pamoja na hayo,alisema Tume hiyo, inatarajia kuanza kampeni za kitaifa kuhamasisha wanaume kupima afya zao ,ili kujenga tabia ya kujitokeza kupima kwani ni asilimia 45 pekee ya kundi hilo walioaminika kuwa na VVU ndio waliopima kujua hali zao.Alisema ,kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na itakuwa endelevu hadi hapo watakapohakikisha wanatokomeza ama kupunguza gonjwa hilo .

Maboko alisema ,wale watakaobainika kuwa na maambukizi mapya watatakiwa kuanza tiba ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) mapema ili kuondoa vifo vinavyotokana na virusi hivyo .“Asilimia 45 ya wanaume ndio wanaoaminika kuwa wamepima na kujua hali zao ,hali ambayo inaonyesha ni kiwango cha chini “.Hata hivyo Maboko alisema ,maambukizi mapya ya ukimwi yanaongezeka zaidi kwa kundi la vijana hususan wa kike .“Hii inaonyesha huko kipindi cha nyuma hakukuwa na hali hiyo hivyo haina budi kundi hilo likatiliwa mkazo ,ili kupunguza ongezeko hilo “

Maboko alisema katika kundi la vijana, kati ya watu kumi wenye maambukizi mapya kwa mwaka ,vijana wanne sawa na asilimia 40 ugundulika kupata maambukizi hayo.Alielezea, kati ya vijana kumi waliopata maambukizi mapya kila mwaka nane huwa vijana wa kike na wawili ni vijana wa kiume.Alisema, mwaka 2016/2017 walifanya utafiti ambako walitembelea kaya 15,505,ambapo walihoji na kupima wanawake 19,852 , wanaume 16,235 na watoto wenye umri wa miaka 0-14 waliopo 10,452 .

Maboko alisema kwamba, wanawake asilimia 95 walikubali kuhojiwa na kupimwa ,wanaume asilimia 85 walikubali na watoto asilimia 92 waliohojiwa na kupimwa.“Miaka yote tulikuwa tukifanya utafiti na kupima miaka 15 hadi 49, hii ni mara ya kwanza kuanzia miaka 0-64”alisema Maboko.Hali ya maambukizi ya ukimwi Tanzania kwasasa ni asilimia 4.7 kutoka asilimia 5.1 ,hali inapungua lakini inatakiwa kuendelea kupambana na maambukizi mapya ,na Tanzania bila ukimwi inawezekana”.
Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Leonard Maboko ,akionekana akizungumza jambo.(picha na Mwamvua Mwinyi)

TULIA AWASHUKURU WADHAMINI KUFANIKISHA MBIO ZA 'MBEYA TULIA MARATHON 2018'.

$
0
0
SE3
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mbio za Mbeya Tulia Marathon 2018 zilizofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo, Mbio hizo Zimeshirikisha wanariadha mbalimbali wakiwemo wakenya na watanzania pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi wa mkoa wa Mbeya , kumekuwepo na washiriki wa mbio mbalimbali zikiwemo za Kilomita 41, kilomita 21, Kilomita 5, Kilomita 2, Mita 100, Mita 400 na Mita 800.
Dk. Tulia Akson Naibu Spika wa Bunge amewashukuru wadhamini mbalimbali ambao wamewezesha kufanyika kwa mbio hizo kwa mafanikio makubwa mbali ya changamoto ndogondogo ambazo zitaendelea kuboreshwa katika maandalizi ya mbio zingine zitakazofanyika mwakani jijini Mbeya.
1
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk. Tulia Ackson akianzisha Mbio za mita 100 katika mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018 zilizowahusisha viongozi wa serikali , Wabunge na Madiwani kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo,
2
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg Wilson Nkambaku pamoja na baadhi ya wabunge wakishiriki mbio za mita 100 kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati wa mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018 jijini Mbeya.
3
Watoto wakishiriki mbio za mita 1500.
5
Washiriki wa mbio za Baiskeli Kilomita 150 wakiingia uwanja wa Sokoine mara baada ya kumaliza mbio hizo.

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images