Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

balozi dkt dau ashiriki kongamano la Kitaifa kujadili zao la nazi nchini indonesia.

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Thailand, Philippines, Cambodia, Brunei, Laos pamoja na Indonesia Mhe Dkt Ramadhani Kitwana Dau, leo ameshiriki  katika Kongamano la Kitaifa kujadili zao la nazi kwenye mji wa Gorontalo Indonesia .

Balozi Dau alishiriki kwenye mjadala huo (panellist) kwa kutoa historia ya zao la nazi Tanzania ikiwemo uzalishaji na changamoto zake. Mkutano huo wa siku 2 umeanza leo na unashirikisha Wadau wote wa zao la nazi nchini Indonesia. 

Indonesia inaongoza katika uzalishaji wa nazi Duniani kwa kulima hekta 3.6 milioni na kuzalisha nazi zaidi ya tani 17 milioni. Kwa upande wake, Tanzania inaongoza kwa zao hilo Barani Afrika lakini inalima hekta 350,000. 

Zao la nazi kwa sasa linaongoza kwa bei kwenye soko la Dunia na kulipita zao la chikichi na hata mafuta ya Petroli . Nchini Indonesia mnazi mmoja unatoa kati ya nazi 100 hadi 150 ingawa wastani wa kitaifa Ni nazi 70 kwa mnazi mmoja. 

Katika mkutano huo Balozi Dau alipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Kilimo wa Indonesia Mhe Dr Amran Sulaiman ambapo walikubaliana kukuza zaidi ushirikiano kwenye kilimo baina ya nchi hizi mbili. 

Pamoja na zao la nazi, Indonesia inaongoza Duniani kwenye mazao  kadhaa yakiwemo muhogo, Mahindi ya njano nk. 

Jumatatu Balozi Dau atakutana na wawekezaji wa sukari michikichi na mihogo kwa madhumuni ya kuwashawishi kuja kuwekeza Tanzania .
Pichani Balozi Dau akisisitiza jambo katika kongamano hilo 
 




TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMW

$
0
0

Na.WAMJW

Serikali inatarajia kupata dola ya kimarekani milioni 512 kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI kutoka Serikali ya Marekani kupitia fungu la mradi wa dharura wa Rais wa kupambana na UKIMWI Duniani.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa akipokea rasmi taarifa ya kutolewa fedha za UKIMWI kwenye hafla iliyofanyika kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja jijini hapa.

Dkt.Ndugulile alisema fedha hizo ambazo serikali itapatiwa zitatumika kwa ajili ya kununulia dawa za kufubaza makali ya Virus vya UKIMWI pia zitagawiwa kwa afua mbalimbali za kupambana na kuzuia maambukizi ya UKIMWI pamoja na uhamasishaji wa upimaji wa Virus vya UKIMWI nchini. 

Aidha ,alisema kiasi hicho cha fedha zinatakiwa kutumika ndani ya mwaka mmoja kwa kwa kujikita kwenye malengo ya Dunia ya tisini tatu(90,90,90) kwa kuhakikisha kwamba asilimia 90 ya watanzania wote wanaohisiwa kuwa na Virusi vya UKIMWi wanafikiwa,asilimia 90 ya wenye Virusi baada ya kupima wana pata tiba na asilimia 90 wanaopata tiba kuweza kufumbaza Virusi vya UKIMWI.

Alisema kama nchi imekuwa na changamoto kubwa sana na asilimia 90 ya kwanza ya upimaji kutokana na Takwimu za mwaka jana za hali ya maambukizi nchini zinaonyesha bado kuna changamoto kubwa hususan kwenye makundi ya vijana bado maambukizi yanaongezeka hasa kwa wasichana”vilevile kwa upande wa wanaume ambao ni wagumu kwenda kupima na wengine wanapima ila wanachelewa kuanza dawa na kutofuata misingi ya umezaji dawa na hivyo kufa zaidi”.

“Mkakati ambao tunautafakari na kuja nao ni ule wa mwananchi kuweza kujipima wenyewe kwa kutumia mate(Self-Test) hivyo kila mtu aweze kujijpima mwenyewe kwa kwenda kununua kipimo duka la dawa kama ilivyo kwa wanawake kujipima ujauzito”alisema Dkt.Ndugulile

Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwatoa hofu wananchi kwamba Serikali haitawapima wanaume kwa nguvu kwenye ma bar bali itatumika utaratibu ule ule katika makundi yao kwa kuwapatia ushauri nasaha na kupima kwa hiari “hatusemi wanaume watapimwa kwa nguvu hapana utaratibu utakua ule ule hivyo wananchi msipate hofu” alisema dkt.Ndugulile

Alitaja mikakati mingine ni kwenda kuwafikia makundi mahususi ambayo inaonekana yana maambukizi makubwa ikiwemo ya wavuvi pamoja na migodini hivyo alitoa rai kwa watanzania kujitokeza ili kuweza kufikia asilimia 90 kutoka 52 ya upimaji wa Virus vya UKIMWI.Naye Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inm alisema nchi yake ipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Tanzania kujenga Tanzania yenye afya nzuri.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 04.05.2018

Kitabu kinachofichua siri za mauaji ya ALBINO

$
0
0
Kitabu kinachofichua siri za mauaji ya ALBINO ambacho ni kazi ya uchunguzi wa takriban miezi minane iliyofanywa na mwanahabari Daniel Mbega baada ya kuzunguka katika mikoa yote ya Kanda ya Maziwa Makuu.

Wafanyakazi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wauaga Mwili Wa Mfanyakazi Mwenzao

$
0
0
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mfanyakazi mwenzao ambaye ni Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa aliyefariki tarehe 02/05/2018 jijini Dar es Salaam. Dkt. Onesmo anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 5/5/2018 katika kijiji cha Nzihi kilichopo Iringa vijijini.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakielekea katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya kuchukuwa jeneza lenye mwili wa mfanyakazi mwenzao ambaye ni Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa aliyefariki tarehe 02/05/2018.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiimba wimbo wa maombolezo kabla ya kwenda katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya kuchukuwa jeneza lenye mwili wa mfanyakazi mwenzao ambaye ni Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa aliyefariki tarehe 02/05/2018 .
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani na Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambao ni marafiki wa karibu wa Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Marehemu Onesmo Mhewa wakieleza jinsi walivyofanya kazi kwa ukaribu na marehemu wakati wa halfa fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) lililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa na sura za majonzi wakati wa hafla fupi ya kuuaga mwili wa Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa iliyofanyika leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) lililopo Hospitali ya Taifa Muhimbili . Dkt. Onesmo anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 5/5/2018 katika kijiji cha Nzihi kilichopo Iringa vijijini. Picha na JKCI

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MWALIMU NOVATI SIMEON RUTAGERUKA

$
0
0
TAREHE 5 - MEI - 2018, UMETIMIZA MIAKA NANE TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI.  PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA.
UNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WAKO FLORIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU MWALIMU NOVATI RUTAGERUKA ITAADHIMISHWA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE  5 - MEI - 2018, KATIKA KANISA LA MTAKATIFU GASPER, MBEZI BEACH, DAR-ES-SALAAM SAA 12.30 ASUBUHI BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMINA

VOA Swahili: Maonesho ya utamaduni wa Kenya jijini Atlanta, Marekani

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA KIDATU –IFAKARA YENYE KM 66.9 PAMOJA NA DARAJA LA MTO RUAHA KATIKA ENEO LA NYANDEO KIDATU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy kushoto  na Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer kulia kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kushoto pamoja viongozi mbalimbali na wabunge wa mkoa wa Morogoro.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi pamoja na viongozi wengine wakiwemo Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy anayevuta utepe, Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer pamoja na wabunge mbalimbali wa mkoa wa Morogoro
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru Mkuu wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya Balozi Roeland van de Geer na Mwakilishi wa DFID nchini Beth Arthy mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 katika sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Nyandeo Kidatu mkoani Morogoro.
Mbunge wa Mikumi Joseph Haule akitumbuiza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kutoka Kidatu hadi Ifakara yenye jumla ya kilometa 66.9 pamoja na daraja la mto Ruaha lenye urefu wa mita 130.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwa njia ya simu ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kuhusu matatizo ya mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya  Kidodi mkoani Morogoro.


MENEJIMENTI YA MAHAKAMA YA TANZANIA YAWAAGA MAJAJI WAPYA WALIOTEULIWA KUTOKA MAHAKAMA

$
0
0
Waheshimiwa Majaji wapya wa Mahakama Kuu walioteuliwa kutoka Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja, katikati ni Mhe. Ilvin Mugeta, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kushoto ni Mhe. Elinaza Luvanda, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na aliyesimama kulia ni Mhe. Mustapher Siyani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Majaji hawa wameagwa rasmi mapema Mei 04, 2018 na Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania.
Sehemu ya Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wakiwa katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Maktaba-Mahakama ya Rufani, katika kikao hicho Wajumbe hao walipata fursa ya kuwaaga waliokuwa Wajumbe wa Menejimenti ambao waliteuliwa hivi karibuni kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, walioketi mbele (katikati) ni Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa kikao hicho ambaye pia ni Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na kushoto ni Msajili-Mahakama ya Rufani, Mhe. John Kahyoza.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta (aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe wa Menejimenti, katika salaam zake za shukrani, Mhe. Jaji Mugeta ameishukuru Menejimenti kwa ushirikiano katika kipindi chote alichofanya kazi katika nafasi ya Msajili-Mahakama Kuu, aidha; Mhe. Mugeta ameomba ushirikiano zaidi katika nafasi hii mpya.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Elinaza Luvanda akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe wa Menejimenti, amemshukuru Mhe. Rais na Viongozi wengine wa Mahakama kwa uteuzi wa nafasi hiyo, na ameahidi kutoa ushirikiano katika kazi yake.
Mwenyekiti wa kikao cha Menejimenti ya Mahakama ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (kushoto) akikabidhi zawadi ya nakala za Vitabu vya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, kwa Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Ilvin Mugeta (kulia), anayeshuhudia zoezi hilo (katikati) ni Msajili Mkuu- Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati.
Mwenyekiti wa kikao cha Menejimenti ya Mahakama ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (kushoto) akikabidhi zawadi ya nakala za Vitabu vya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2020) kwa Mhe. Jaji Elinaza Luvanda (kulia) anayeshuhudia ni Msajili Mkuu- Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati.
Mhe. Jaji Elinaza Luvanda (kulia) akipeana mkono na Msajili wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. John Kahyoza (kushoto) mara baada ya kupokea nakala zake za Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (kulia) akipokea nakala ya Kitabu cha Mpango Mkakati kutoka kwa Mtandaji Mkuu Mahakama (kushoto).
Picha ya pamoja Wahe. Majaji na Wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania, aliyeketi katikati ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta, wa pili kushoto ni Mhe. Elinaza Luvanda, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa pili kulia ni Mhe. Mustapher Siyani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania na wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania.(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

PROF NDALICHAKO AVIAGIZA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWACHUKULIA HATUA WANAOICHAFUA SERIKALI

SERIKALI KUREJESHA MIKOPO KWENYE MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

DK RICHARD MASIKA ATEULIWA MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA(AUWSA)

$
0
0
Filbert Rweyemamu,Arusha.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Isack Kamwele amemteua Mhandisi Dk. Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jiji la Arusha(AUWSA) kuanzia April 23 hadi April 22, 2021.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini,Athumani Shariff ilisema Dk Masika alikua Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha hadi alipostaafu Septemba 30,2017.

Pia Mhandisi Kamwele amewateua wajumbe tisa wa bodi ya AUWSA ambao ni Richard Kwitega(Katibu Tawala mkoa),Athumani Kihamia(Mkurugenzi wa Jiji),Francis Mbise(Diwani wa Kata ya Muriet,Vincent Lasway(Mfanyabiashara) na Elishilia Kaaya(Mkurugenzi Mtendaji-AICC).

Wajumbe wengine ni Jackiline Mkindi(Mkurugenzi wa (TAHA),Mhandisi Ruth Koya(Mkurugenzi Mtendaji wa AUWSA),Edward Mrosso(Wakili) na Agnela Nyoni(Mwakilishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji).

Katika uteuzi mpya Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha kwa nafasi yake huingia moja kwa moja lakini wakati huu hakuteuliwa baada ya Bodi iliyopita kuvunjwa Januari 19,2018 na Waziri wa Maji kwasababu ya kutoridhishwa kiutendaji.Bodi iliyopita Mwenyekiti alikua Dk Job Laizer,Richard Kwitega,Athumani Kihamia,Kalist Lazaro,Agnela Nyoni,Charles Marunda,Thomas Mosso,Halima Mamuya,Mhandisi Felix Godfrey na Mhandisi Ruth Koya.

Pia Dk Masika ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Michezo Malya katika uteuzi uliofanywa na Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Dk Harrison Mwakyembe April 4 mwaka huu.Akizungumza na Mwananchi jana,Dk Masika alisema bado ni mapema kuzungumzia mikakati ya Bodi mpya kwakua haijazinduliwa ila atajitahidi kuongeza tija,ufanisi na kutoa huduma bora zaidi.

"Bodi ikishazinduliwa na kuanza kazi tutajitahidi kutekeleza wajibu wetu kwa weledi,ubunifu,bidii na uaminifu kwaajili ya kuwahudumia wananchi wetu,"alisema Dk Masika.Serikali imetoa kiasi cha Sh 514 bilioni kwaajili ya kuhakikisha kero ya maji katika jiji la Arusha na viunga vyake linakua historia na utekelezaji wa mradi umeshaanza.
Mhandisi Dk Richard Masika 

INTRODUCING Rayvanny Ft S2kizzy - Pochi Nene (Official Music Video)

NAIBU SPIKA TULIA ACKSON AJIFUA KUJIANDAA NA MBIO ZA MTM KESHO

$
0
0

 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson (katikati mbele) akiwaongoza baadhi ya wanamichezo Jijini Mbeya katika mazoezi ya kukimbia zaidi ya Kilomita 8 kutokea Uzunguni hadi kiwanja cha michezo Ruanda Nzovwe kujiandaa na Mbio za Mbeya Tulia Marathon (MTM) zinazofanyika kesho jijini Mbeya kuanzia saa 12 asubuhi katika Uwanja wa Sokoine. 

Halmashauri ya Manispaa Kigamboni yapongezwa kwa kupata Hati safi

$
0
0
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni limeipongeza Manispaa kwa kupata Hati safi baada ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba kutoa taarifa ya kupokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG )inayoonesha Manispaa kuwa na hati safi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Pongezi hizo zimetolewa leo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la kawaida la robo ya tatu ya mwaka (Jan-Mach 2018) lililofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Kisota .Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Hoja Maabad amesema kuwa Hati safi imepatikana kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Wataalamu wa Manispaa na Madiwani na kwamba ni faraja kwa Manispaa nzima.

"Tumefarijika sana kupata matokeo haya, hati hii safi isingepatikana kama kungekuwepo na kutokuelewana baina ya wataalamu na madiwani, tunajivunia umoja wetu"Alisema Mh.Hoja .Diwani wa Kata ya Kimbiji Mh.Sanya Bunaya amesema kuwa kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani Baraza lina kila sababu ya kuipongeza Manispaa kwa kazi kubwa waliyoifanya kuhakikisha pamoja na upya wake hati safi inapatikana.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba amesema kuwa tafsiri ya matokea haya ni ushirikiano uliopo kati ya watendaji , wasimamizi pamoja na Waheshimiwa Madiwani ndio uliopelekea kupatikana kwa Hati safi.

Ameongeza kuwa kuangalia nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali, kusimamia vizuri miradi ya maendeleo na kuhakikisha kwamba rasilimali watu ambao anawaongoza wapo katika kuhakikisha lengo lililokusudiwa linafikiwa la wananchi kupata huduma zile zilizokusudiwa. Tunashukuru tumeweza kufikia malengo yaliyotarajiwa na tunaamini hata katika mwaka wa fedha unaokuja tutaendelea kufanya vizuri" Alisema Mkurugenzi.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepata hati safi ( Unqualified Report) kwenye sekta zote na miradi ya maendeleo ikiwemo ya Barabara na Maji inayotekelezwa na Manipsaa

Imeandaliwa na:
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni
04/05/2018.
 Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakifatilia taarifa za Kata kwa makini
 Baadhi ya Wataalamu walioshiriki kwenye kikao cha Baraza
 Diwani wa Kata ya Kimbiji Mh.Sanya Bunaya akitoa pongezi kwa watendaji wa Manispaa kwaniaba ya Madiwani wote.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba akitoa taarifa ya kupokea  Hati safi kutoka CAG
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Hoja Maabad akiwapongeza Wataalamna Madiwani  kwa ushirikiano uliopelekeakupatikana kwa Hati safi.
 

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA UTAWALA NA SERIKALI YAFANYA ZIARA TAGLA JIJINI DAR

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakiwa katika mkutano ulioendeshwa kwa kwa njia ya video kwa kuunaga na wadau waliokuwepo Dodoma, Arusha na Nairobi nchini Kenya, wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA), uliopo kwenye Jengo la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), jijini Dar es salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA), Charles Senkondo akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, waliofanya ziara kwenye ofisi zao, zilizopo kwenye Jengo la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), jijini Dar es salaam leo.
 Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye Mkutano huo.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Venance Mwamoto (picha ya kushoto) akiuliza swali katika Mkutano huo kupitia teknolojia video.  

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA MIPIRA 25 KUTOKA KWA MKURUGENZI MKUU WA COCACOLA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mipira 25 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Cocacola Tanzania Basil Gadcios, kwa ajili ya timu ya Namungo FC ya Wilayani Ruangwa, kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Mei 5, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA KIMATAIFA MASUALA YA MANUNUZI

$
0
0
 Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma Wizara ya Fedha na Mipango, Dk.Frewdrick Mwakibinga akizungumza kuhusu Kongamano la Kimataifa la Ununuzi wa Umma linalo tarajia kufanyika Agosti 8 mpaka 10 Jijini Arusha ,ambapo litaweza kuzikutanisha nchi zaidi ya 50 kutoka kila pembe ya Dunia.
 Afisa Uhusiano kutoka Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi PSPTB, Shamimu Mwasha akizungumza jambo wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari juu ya kongamno hilo kubwa litakalo fanyika nchini.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi kutoka tasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara ya fedha wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Maandalizi
 Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma Wizara ya Fedha na Mipango, Dk.Frewdrick Mwakibinga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa kimataifa wa Masuala ya Manunuzi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe 

SERIKALI YAELEZA FURSA YA UFUGAJI WA NYUKI HAPA NCHINI - NAIBU WAZIRI JAPHET HASUNGA

$
0
0
Na Hamza Temba - Dodoma

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa kubwa iliyopo hapa nchini ya ufugaji nyuki na uwepo wa masoko ya ndani na nje ya nchi kwa kuongeza uzalishaji wa mazao yake na kuyaongezea thamani ili kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Ametoa wito huo leo mbele ya wadau wa sekta ya ufugaji nyuki kutoka mikoa yote nchini katika mkutano aliouitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Amesema kwa sasa mchango wa sekta ya nyuki katika pato la taifa bado ni mdogo ukilinganisha na fursa zilizopo za ufugaji nyuki hapa nchini ambazo zikitumiwa ipasavyo zitasaidia kuinua pato la wananchi na taifa kwa ujumla.

Amesema mbali na kuongeza uzalishaji, mazao hayo pia yanatakiwa kuongezewa thamani na kuwekewa ngazi za ubora ili yaweze kuhimili masoko ya ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa, ili kuimarisha sekta hiyo Serikali itashirikiana na wadau kutatua changamoto zilizopo ikiwemo kutafuta masoko, kuimarisha uwekezaji na kuanzisha viwanda vidogo vya kuchakata mazao ya nyuki ikiwemo asali na nta ambayo ina soko kubwa nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini katika kikao alichokiitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo. Kushoto ni MKuu wa Kitengo cha Masoko, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mwanahamisi Mapolu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Deosdedit Bwoyo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya ufugaji nyuki nchini katika kikao alichokiitisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo ikiwemo marekebisho ya kanuni za ufugaji nyuki za mwaka 2017 katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo.Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Deosdedit Bwoyo akiwasilisha hotuba yake kwa wadau hao.Mkurugenzi Msaidi wa Uendelezaji Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Allen Richard akitambulisha meza kuu katika mkutano huo.

Wizara ya Mambo ya Nje yajipanga kutekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda

$
0
0

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kutimiza malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Kauli hiyo ilitolewa leo jijini Dar Es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Waziri Mahiga alieleza kuwa Wizara inatakiwa kuweka Sera na mikakati ya utekelezaji kwa kuzingatia miongozo na maelekezo ya Viongozi wa juu akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. “Sera ya Serikali ya awamu ya tano ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, hivyo Sera yetu ya Mambo ya Nje lazima ijikite katika diplomasia ya uchumi wa viwanda”. Dkt. Mahiga alieleza.

Dkt. Mahiga alihitimisha hotuba yake kwa kuwataka watumishi kuhakikisha kuwa Wizara inatekeleza majukumu yake kwa kujiwekea ratiba ya kuyakamilisha kwa kuzingatia hotuba za Mhe. Rais Magufuli alizozitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao cha Mabalozi na Mhe. Rais Magufuli na kikao cha watumishi wa Wizara na Mhe. Rais Magufuli. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Wizara yake imejipanga ipasavyo kuhakikisha kwamba jukumu la kuchochea uchumi wa nchi kupitia Sera ya Mambo ya Nje inayojikita katika diplomasia ya uchumi inatekelezwa kikamilifu.

Prof. Mkenda alisema Wizara kwa kushirikiana na ofisi zake za Ubalozi, licha ya changamoto mbalimbali inazokutana nazo, lakini imekuwa ikitafuta fursa za uwekezaji, mitaji, masoko, utalii na elimu na kuzileta nchini ili kufikia azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020.

Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images