Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA KITUO CHA MABASI CHA KISASA MSAMVU, MOROGORO

$
0
0




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi na wadau mbalimbali baada ya kufungua  kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiapeana mikono na  wadau mbalimbali baada ya kufungua  rasmi  kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  na viongozi na wadau mbalimbali wakipata maelezo ya mradi kabla ya ya kufungua  kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Abdulazizi Abood wakati wa sherehe za kufungua  kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mbunge wa Morogoro Kusini Mhe. Prosper Mbena wakati wa sherehe za kufungua  kwa kituo cha mabasi cha kisasa kilichojengwa eneo la Msamvu katika manispaa ya Morogoro leo Mei 6, 2018 
 Muonekano wa kituo kipya na cha kisasa cha mabasi kilichopo eneo la Msamvu katika manisapaa ya Morogoro kilichofunguliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo Mei 6, 2018

Picha na IKULU

WAINGEREZA WAVUTIWA KUWEKEZA SELOUS, DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUWEKWA MAKUBALIANO YA AWALI (MOU)

$
0
0

Na Hamza Temba-WMU-Dodoma

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza uandaliwe mkataba wa makubaliano ya awali (MoU) ya utekelezaji wa mradi wa kuendeleza utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.

Mkataba huo wa makubaliano utahusisha wawekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA na  utakapokamilika utasainiwa na pande zote mbili.Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo juzi ofisini kwake Jijini Dodoma kufuatia maombi yaliyowasilishwa kwake na wawekezaji hao, Eva Sanchez na Nicholas Negre.

Akiwasilisha maombi hayo, Sanchez amesema mradi huo utakuwa wa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA ambao ndio wasimamizi wakuu wa Pori la Akiba Selous utakapoanzishwa mradi huo. Amesema pamoja na mambo mengine mradi huo wa utalii wa picha pia utasaidia kupiga vita ujangili na kukuza uchumi wa jamii zinazozunguka pori hilo.

Dk. Kigwangalla amewataka wawekezaji hao kuwasilisha andiko la mradi huo, kufanya utafiti wa kina na tathmini ya athari za kimazingira zitakazoweza kujitokeza kutokana na uanzishwaji wa mradi huo.

Amesema kwa sasa Serikali inafanya marekebisho ya Sheria mbalimbali zitakazoiwezesha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA  kutekelezaji majukumu yake ipasavyo ikiwemo uwekezaji wa aina hiyo kwenye sekta ya Utalii wa Picha na Uwindaji wa Kitalii.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara amesema mamlaka hiyo itatoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji hao ili kutimiza azma ya Serikali ya kushirikisha wadau, watu binafsi na wawekezaji katika kukuza sekta ya utalii nchini.

Pori la akiba Selous ndio hifadhi kubwa kuliko zote nchini ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba takriban 50,000 katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Mwaka 1982, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Uneso) lilitangaza eneo hilo kuwa moja ya eneo la Urithi wa Dunia na kuanza kuhifadhiwa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara (hayuko pichani) kushirikiana na wawekezaji kutoka nchini Uingereza kuandaa mkataba wa makubaliano ya awali (MoU) ya uwekezaji katika sekta ya utalii kwenye Pori la Akiba Selous, ofisini kwake Jijini Dodoma juzi. Wawekezaji hao pichani ni Eva Sanchez na Nicholas Negre.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na muwekezaji kutoka Jiji la London nchini Uingereza, Eva Sanchez ofisini kwake Jijini Dodoma juzi alipowasilisha ombi lake la kuwekeza kwenye sekta ya utalii wa picha katika Pori la Akiba Selous.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara (kulia) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji huo.
 Mkurugenzi wa Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Imani Nkuwi (aliyesimama) akifafanua jambo kuhusiana na uwekezaji huo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

CALL TO PARTICIPATE IN THE FIRST NATIONAL SKILLS DEVELOPMENT WORKSHOP AT JNICC DAR ES SALAAM 10th MAY 2018

WALIDI ASEMA AMERUDI NYUMBANI KUFANYA KAZI NA WANAMUZIKI WA HAPA

Kidato cha 6 Kuanza Mtihani wa Taifa nchi nzima leo

$
0
0

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema watahiniwa 87,643 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita utakaoanza kesho Mei 7, 2018. Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde (pichani) amesema kuwa mtihani utahitimishwa Mei 25, 2018 ambapo amebainisha kwamba kati yao watahiniwa hao, wa shule ni 77,222 na wa kujitegemea ni 10,421.
Dk Msonde amesema mtihani utafanyika sambamba na wa kozi ya ualimu ambao watahiniwa 7,422 wa ngazi ya cheti na stashahada wamesajiliwa kuufanya.
"Maandalizi kwa ajili ya mitihani ya kidato cha sita na ualimu yamekamilika, ikiwamo kusambaza vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mitihani hii," amesema Dk Msonde.

MRS LIGATE FUNERAL ARRANGEMENT FUND

$
0
0


Dearest Family and Friends,

The Family of Brig. Gen (Ret) P.S. LIGATE Announce with Deep Sorrow The Passing of our Beloved Mother Nderikyo Elizabeth Ligate on the 1st of May 2018 at Nakasero Hospital in Kampala, Uganda. 

We have received numerous emails, texts and messages from Family and Friends asking how to help. We have therefore officially launched a campaign to keep everyone up-to-date with our beloved mother's funeral arrangements and also offer a place for Messages and Donations to assist in this difficult time of need for our family.

We truly appreciate all your support during this difficult time. We thank you in advance for your Donations and Kind words, may our lord continue to bless you. Amen

To Donate Please CLICK HERE

CSI waadhimisha siku ya wakunga duniani

Dk Mengi aitikia wito wa rais kujenga kiwanda cha dawa,Ummy azindua ujenzi

$
0
0
Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi ameingia ubia na Mwekezaji kutoka India kujenga kiwanda cha dawa kitakachogharimu dola za kimarekani milioni 55 sawa na shilingi bilioni 55 za Tanzania.

Ujenzi wa kiwanda hicho kipya kiitwacho  M- pharmaceutical Ltd,  katika eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani umewekewa jiwe la msingi na Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mwishoni mwa wiki.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda hicho Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alimpongeza Dr Mengi kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais John Magufuli alilolitoa wakati wa uzinduzi wa hospitali mpya kisasa ya Taaluma na Tiba Muhimbili  Mlonganzila.

Novemba mwaka jana akifungua Hospitali hiyo katika hotuba yake Rais John Magufuli aliwataka wafanyabiashara nchini kuanzisha viwanda vya dawa kwa kuwa fedha nyingi zinatumika kuagiza dawa kutoka nje.

Dk Mengi ambaye pia ni Rais wa sekta binafsi alikuwepo katika uzinduzi huo na kusema kwamba yeye na wenzake watalitafakari rasmi suala hilo.

Waziri Ummy Mwalimu pia amemhimiza Dr Mengi na mbia mwenzake kuharakisha ujenzi wake na kumhakikishia kuwa bidhaa zitakazozalishwa zitapata soko kubwa hapa nchini na nchi za ukanda huu, na kunufaika na upendeleo maalum wa  bidhaa zinazozalishwa nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amesema katika awamu ya kwanza kiwanda hicho kitazalisha chupa milioni 30 kwa mwaka za aina mbalimbali za maji ya dripu zinazotumiwa wakati wa matibabu ya dharura nyakati za ajali, upasuaji, homa kali, na magonjwa ya mlipuko, zinazokidhi vigezo vya kimataifa.

Amesema kipaumbele cha ajira kitatolewa kwa wananchi wa Bagamoyo, na kusisitiza kuwa umuhimu wa Watanzania kujiamini katika kujiletea maendeleo.

Mapema Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Dk Charles Mwijage na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiro  amewataka viongozi wasiwakwamishe wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika maeneo yao.

Aidha walisema kwamba serikali itashughulikia changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa maji, umeme wa uhakika na gesi asilia katika eneo hilo.

Alisema kwamba taifa linajenga uchumi wa viwanda na ni kazi ya serikali kuwezesha mazingira rafiki kwa ajili ya uwekezaji.

Uwekaji jiwe la msingi ulishuhudiwa na wananchi wa Kerege, Balozi wa Ufaransa Frederic Clavier, balozi wa China Wang Ke, Mbunge wa Bagamoyo Dr Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhan Maneno na  viongozi mbalimbali mbalimbali wa serikali na CCM wa mkoa na wilaya ya Bagamoyo.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi, akizungumza wakati wa Sherehe ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Dawa za Binadamu cha M- Pharmaceutical Ltd kilichopo Kerege Wilayani Bagamoyo, ambapo alishukuru ushirikiano aliopata kutoka serikalini wakati wa mchakato wa uanzishwaji kiwanda hicho .Hafla hiyo imefanyika wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani. (Picha na Abubakari Akida)

TTCL YAENDELEA KUTOA LINE BURE MTWARA

$
0
0

JOSEPH MPANGALA , MTWARA

Kampuni ya Mtandao wa sim TTCL Cooperation Imeendelea Kutoa na Kusajili line za sim Bure ili kuwawezesha wateja wake wapya kuweza kuwasilina kwa bei nafuu pamoja na kujiunga na vifurushi vya Internet.

Akiongea katika Kiwanja Cha mashujaa kilichopo mkoa wa mtwara katika Promosheni ya NYAKA NDINGA inayoendeshwa na kituo cha Radio cha EFM/TVE Meneja wa Mkoa Mhandisi Rumishael f. Temba anasema TTCL imeanzisha Bando kwa ajili ya internet ambayo wateja wengi wamekuwa wakiyapenda na Kuyatumia kwa wingi.

“Katika Upande wa mabando kwa TTCL ambayo wateja wake wanayapenda zaidi ni Boom Pack kwa ajili ya wanachuo,Serereka Bando la Kijanja ambalo kila mwananchii anaweza kulipata kwa bei nafuu pamoja na bando la Toboa”

Aidha TTCL imetambulisha Huduma ya T-pesa kwa mtandao ambapo unaweza kutumia kulipia Huduma ya LUKU bila ya kuwa na gharama za ziada.
 Meneja wa Mkoa TTCL Cooperation Mhandisi Rumishael f.Temba akiongea na Wananchii kuhusina na Huduma Zinazotolewa na kampuni Hiyo wananchii waliokuja katika Promosheni ya Nyaka Ndinga Inayoendesha na EFM na TVE.
 Baadhi ya wateja wakiwa wamezunguka Banda la TTCL kwa ajili ya kupata Huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo.

 Meneja wa Mkoa TTCL Cooperation Mhandisi Rumishael f.Temba akitoa zawadi kwa Washiriki Kumi watakaokwenda Dar es Salaam kwa ajili ya shindano kubwa la promosheni ya Nyaka Ndinga.

Radio jamii zaomba ruzuku kwa serikali

$
0
0
Na Mwandishi wetu,
SERIKALI imeombwa ifikirie kutoa ruzuku kwa radio za jamii kupitia Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) ili waweze kuandika habari ya mambo yanayojiri vijijini badala ya kutegemea habari za matukio.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa TADIO, Prosper Kwigizewakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliosajiliwa mwaka jana na msajili wa mashirika ya kiraia na kuhudumu kwa takribani radio zote za jamii nchini.
Alisema kwa sasa wanajivunia kuhudumia watu takaribani milioni 35 lakini wana shida kubwa ya kuweza kuandika habari za maendeleo vijijini kutokana na tatizo la fedha.
Alisema wao kama radio za jamii zinasikilizwa vyema katika maeneo yao kwa kuwa wanaandika habari za wananchi wa huko katika ngazi ya mtaa na kijiji na kama mabadiliko yanatakiwa kufanywa katika nchi wao ndio wanaoweza kuwa chachu.
 Hata hivyo alisema pamoja na kuwa karibu na wananchi wanalazimika kuandika zaidi habari za matukio kutokana na kukosa fedha za kutuma waandishi vijijini kupiga kambi kwa ajili ya habari za uchunguzi ambazo zitaibua masuala mbalimbali.
Alisema pamoja na kupata msaada mkubwa kutoka mataifa ya Sweden na Uswis kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), msaada wao hautoshi na hivyo kuitaka serikali na wadau wa ndani kama Mifuko ya Hifadhi kuwezesha radio hizo kusimama zenyewe kimapato na kitendaji.
Alisema kuna masuala mengi ya vijijini katika mikoa ya pembeni ambayo radio hizo zikiwezesha zinaweza kusaidia kujulisha taasisi nyingine nini kinajiri na nini kinastahili kufanywa.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Prosper Kiwigize akifungua mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Mtandao huo, Marko Mipawa, Afisa Miradi kwenye Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), Rose Mwalongo (wa pili kushoto), pamoja na Mkurugenzi wa MISA-TAN, Gasirigwa Sengiyumva (kushoto).
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Prosper Kiwigize akionyesha cheti cha usajili wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) unaohusisha Tanzania bara na Visiwani wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Afisa Miradi kwenye Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (UNESCO), Rose Mwalongo akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege akitoa salamu kwa wajumbe ambapo ameahidi kuendeleza ushirikiano na TADIO wakati wa mkutano mkuu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Katibu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO), Marco Mipawa akisoma ripoti ya mapato na matumizi kwa kipindi cha Januari 2017 mpaka Mei 2018 pamoja na taarifa ya bodi ya TADIO ya utekelezaji kwa kipindi cha Julai 28, 2017 mpaka Mei 3, 2018 wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa MISA-TAN, Gasirigwa Sengiyumva akizungumza na wajumbe wakati wa mkutano mkuu wa Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Mjumbe wa TADIO kutoka Kahama FM, Maria Lembeli akichangia maoni wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
 Mjumbe wa TADIO kutoka redio Orkonerei FM, Baraka Ole Maika akiuliza swali na kuchangia maoni wakati wa mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.
Wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Asasi ya Habari za Maendeleo (TADIO) katika picha ya pamoja baada kumaliza mkutano mkuu wa mtandao huo uliofanyika katika ukumbi wa Kato jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Biteko apiga marufuku bei holela madini ya ujenzi

$
0
0
Na Greyson Mwase, Tanga
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amepiga marufuku tabia ya wachimbaji wa madini ya ujenzi ya kushusha bei ya madini hayo kwa ajili ya kuuza kwa wingi, badala ya kufuata bei elekezi iliyowekwa na Serikali  huku wakiwalipa  vibarua kiasi kidogo cha fedha kisichoendana na kazi ngumu wanazofanya.
Naibu Waziri Biteko ameyasema hayo  mapema leo alipofanya ziara katika machimbo ya madini ya ujenzi aina ya kokoto katika eneo la Amboni mkoani Tanga lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kuzungumza na wananchi.
Biteko alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki wa leseni kuuza madini aina ya kokoto kwa bei  ya chini na kupata faida huku wakiwalipa kiasi kidogo vibarua wanaofanya kazi ngumu ya kuponda kokoto kwa kutumia vifaa duni.
Akijibu kero mbalimbali zilizowasilishwa na wachimbaji madini ya kokoto Biteko alisema kuwa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na  Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni hukakikisha kuwa rasilimali za madini zinawanufaisha watanzania na kuwataka kuunda vikundi ili kurahisisha upatikanaji wa vifaa na ruzuku kutoka Serikalini.
Alisema Wizara ya Madini kupitia Mradi wa Usimamizi  Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) imepanga mikakati ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kupitia ruzuku na ununuzi wa vifaa vya uchimbaji ili waweze kufanya kazi katika mzaingira rafiki na kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa  Sekta ya Madini.
 Mkuu wa Wilaya ya  Tanga (kulia) Thobias Mwilapwa akielezea Sekta ya Madini katika Wilaya yake kwa watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Vyombo vya Habari (hawapo pichani) kwenye ziara ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) akiendelea na ziara katika eneo linalotumika kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya ujenzi aina ya kokoto  lililopo katika eneo la Amboni Wilayani Tanga mkoani Tanga.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akizungumza na mponda kokoto, Helena  Joackim (aliyekaa chini) kwenye machimbo ya kokoto yanayomilikiwa na Swalehe  Khama yaliyopo katika eneo la Amboni Wilayani  Tanga mkoani Tanga.
 Mchimbaji mdogo wa madini ya kokoto Swalehe Khama akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye ziara hiyo.
 Mponda kokoto, Husna Bakari akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (hayupo pichani) katika ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akifafanua jambo kwa wachimbaji madini ya ujenzi aina ya kokoto kwenye ziara hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wabunge wa Afrika Mashariki wamtembelea Balozi Chikawe - Tokyo

$
0
0
 Wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chapter ya Tanzania hivi kariuni wamezuru Ubalozi wa Tanzania Tokyo,nchini Japan,wakiwa kwenye ziara ya wiki moja nchini humo. Pichani kushoto ni Ndugu Charles Mchome ambaye ni Mtanzania anayeishi Japan na ni Mdau wa globu ya Jamii.
Pichani kushoto ni Dkt Abdullah Hasnuu Makame,Balozi Mathias Chikawe,Mheshimiwa Josephine Lemoyan pamoja na Mhandisi Mohamed Habib Mnyaa wakiwa katika picha ya pamoja.

WADAU WA HABARI DODOMA WAPEWA SOMO

$
0
0
WADAU wa habari mkoa wa Dodoma wameshauriwa kutumia wanahabari katika kuchochea mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye ngazi zote za utawala ili kuhabarisha umma.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athuman Masasi katika mkutano uliowakutanisha wadau wa habari mkoa wa Dodoma ambao ulilenga kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusino baina yao na wanahabari na upatikanaji habari zinahusu maendeleo ya mkoa huo.

Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC) kwa ufadhili wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini(UTPC) ambao hufanyika kila mwaka.Akichangia majadiliano kwenye mkutano huo, Masasi alisema tasnia ya habari ni muhimu kwa ustawi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla na kuwahakikishia wanahabari kuwa halmashauri za mkoa wa Dodoma kwa sasa zina mipango na shughuli nyingi za maendeleo hivyo zinahitaji wanahabari kufikisha taarifa hizo kwa wananchi.

Aidha aliwaomba wanahabari kuwasiliana na mamlaka za serikali hasa pale wanapopata taarifa za tatizo lolote ili kujua juhudi za serikali za kupambana nalo.Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC), Habel Chidawali aliwataka waandishi kuondokana na uandishi wa mazoea ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Aidha aliwaomba wadau katika mkoa wa Dodoma kuvitumia vyombo vya habari katika kutangaza fursa zinazopatikana katika maeneo yao kwa kuwa vina uwezo wa kufikia kundi kubwa la wananchi.Naye, Mwandishi mkongwe nchini, Edna Ndejembi alisema kuwa ili Mkoa wa Dodoma uweze kufikia maendeleo yake hauna budi kuvitumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kwani kwa kufanya hivyo utatoa fursa kubwa kwa wadau kujitokeza na kuwekeza mkoani hapa.

Alisema mkoa wa Dodoma una fursa nyingi kwenye Nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo cha zabibu ambazo zinahitaji kutangazwa ili kupata wawekezaji na kuwezesha mji huo kukua hasa ikizingatiwa tayari umepewa hadhi ya kuwa Jiji.Pamoja na hayo, Mlezi wa CPC Daniel msangya alisisitiza waandishi kujiendeleza kielimu na kujisoma vitabu na sheria mbalimbali ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma Habel Chidawali akifungua Mkutano wa wadau wa habari mkoani Dodoma.
Wajumbe wa mkutano
Mwanahabari Mkongwe Edna Ndejembi akizungumza katika mkutano wa wadau mkoani Dodoma.
Mlezi wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma(CPC) Daniel Msangya akichangia katika mkutano wa wadau wa habari wa mkoa huo.
Mwanahabari Idd Maalim akichangia kwenye mkutano wa wadau wa habari Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari Dodoma.

Kamati za mashindano Handeni Kwetu Cup zaaswa kutimiza wajibu wao

$
0
0
VIONGOZI wa mpira wa miguu katika kata mbalimbali wilayani Handeni, mkoani Tanga, wameaswa kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu wao wa kuratibu na kuyasimamia mashindano ya Ligi ya Handeni Kwetu Cup kwenye Kata zao ili mashindano hayo yawe na tija na kupatikana washindi kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

Ushauri huo umetolewa na muasisi wa mashindano hayo, Kambi Mbwana, alipokuwa akizungumza na gazeti hili wilayani hapa, akisema kuwa kuna baadhi ya Kata zimekuwa zikisua sua kutokana na viongozi waliochaguliwa kutojua umuhimu wa uwajibikaji na kutimiza wajibu kwa maslahi mapana ya mpira wa miguu kwa kupitia mashindano hayo yanayodhaminiwa na bahati nasibu ya Biko 'ijue nguvu ya buku' na Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF).

Akizungumzia suala hilo, Mbwana alisema kabla ya kuanza mashindano hayo, Chama cha Mpira wa miguu wilayani Handeni mkoani Tanga (HDFA), kilichagua viongozi wake kila kata ili pamoja na kuyaratibu mashindano ya Handeni Kwetu kwenye Kata zao kwa ajili ya kutafuta washindi wawili wa kwenda ngazi ya tarafa, pia viongozi hao wangekuwa na majukumu ya kusimamia na kuendeza mpira kwenye kata zao, viongozi ambao upatikanaji wao ulilazimika kutumika kwa gharama ya muda na fedha.

"Kila mdau wa michezo anapaswa kujua kwenye kata yake kuna viongozi wa mpira waliochaguliwa ili kusimamia ligi hii, hivyo wanapaswa kutimiza wajibu wao ili mashindano yetu yaende vizuri kwa ajili ya kutoka kwenye kata na kuingia kwenye tarafa na baadae ngazi ya wilaya kama matarajio yetu.

HUYU NDIYE SAMAKI MWENYE LADHA NZURI KULIKO WENGINE WOTE DUNIANI-PROF MWANDOSYA.

$
0
0
Prof Mark Mwandosya akionesha samaki aina  Mbasa (Opsaridium microlepis),waliovuliwa mapema leo asubuhi Matema,Matema katika Ziwa Nyasa. Prof.Mwandosya amesema kuwa aina Samaki huyo ni mwenye ladha nzuri kuliko wote Duniani."Samaki huyo anapatikana Ziwa Nyasa tu. Mbasa (Opsaridium microlepis), the most tasty and delicious fish in the world, is endemic to Lake Nyasa.

Ufunguzi wa Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP 2018) kufanyika kesho

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kesho tarehe 8 May, 2018 litafungua rasmi mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP) kuanzia saa 6:00 mchana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yakiwa katika mzunguko wa  Tano (5) yatafanyika  kuanzia tarehe 8 Mei , 2018 hadi tarehe 18 Mei, 2018 katika Uwanja wa Uhuru na viwanja vilivyopo katika Kambi ya Jenerali Abdalah Twalipo,  Mgulani.

        Michezo itakayoshindaniwa ni ifuatayo:-
        1.     Mpira wa Miguu -  Wanaume.
        2.     Mpira wa Pete -  Wanawake.
        3.     Mpira wa Kikapu  ­- Wanaume na Wanawake.
4.     Mpira wa Wavu - Wanaume na Wanawake.
5.     Mpira wa Mikono -  Wanaume na Wanawake.
6.     Ngumi za Ridhaa  - Wanaume.
7.     Riadha – Wanaume na Wanawake.
        8.     Ulengaji   Shabaha – Wanaume na Wanawake.
        Washiriki wa Mashindano hayo ni Wanajeshi kutoka Kamandi  za  JWTZ ambazo ni:-
1.     Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi (NGOME).
2.     Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu  (Nyika).
3.     Kamandi ya Jeshi la Anga (AFC).
4.     Kamandi ya Jeshi  la Wanamaji (NC)
5.     Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
        Mgeni rasmi katika siku ya ufunguzi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni  Sanaa na Michezo  Mhe.  Dkt. Harisson  George Mwakyembe (MB).
        Wanahabari na Wananchi Wote wapenda Michezo mnakaribishwa  kwa upendo mkubwa.
        Hakutakuwa na Kiingilio  kwenye Viwanja hivyo katika siku zote za mashindano hayo.

SPIKA NDUGAI AZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA FEDHA KANDA MAALUM YA KIUCHUMI KUTOKA NCHINI GABON LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na mgeni wake Mkurugenzi wa fedha kutoka Kanda Maalum ya kiuchumi nchini Gabon, Ndg. Aashutosh Agarwal (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Kata ya kivukoni, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam Ndg. Sharik Choughule.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na mgeni wake Mkurugenzi wa fedha kutoka Kanda Maalum ya kiuchumi nchini Gabon, Ndg. Aashutosh Agarwal (katikati) alieongozana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Kata ya kivukoni, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam Ndg. Sharik Choughule (kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza mgeni wake Mkurugenzi wa fedha kutoka Kanda Maalum ya kiuchumi nchini Gabon, Ndg. Aashutosh Agarwal (katikati) alieongozana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya kivukoni, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam Ndg. Sharik Choughule (kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

MKURUGENZI MTENDAJI TIC:UKUAJI WA KASI WA UCHUMI WA TANZANIA KIVUTIO KWA WAWEKEZAJI

$
0
0
*Azungumzia miradi mipya 109 waliyoisajili kwa kipindi cha miezi minne,fursa za ajira

Na Said Mwishehe,Globu

MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe ametoa hakikisho kwa wawekezaji na Watanzania kwa ujumla kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kubwa na kwa sasa nchi yetu inashika nafasi ya tano kati ya mataifa 10 duniani ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi.

Amesema kuimarika kwa uchumi huo wa Tanzania na kukuwa kwa kasi, maana yake inatoa usalama kwa anayetaka kuwekeza nchini kuwa na uhakika wa mtaji wake huku akielezea mafanikio ya TIC katika kuhamasisha uwekezaji nchini ambapo kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu wamefanikisha kuandikisha miradi mipya 109 inayotarajia kutoa fursa ya ajira 18,172.

Mwambe amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anatoa mafanikio ya TIC kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu ambapo amefafanua kutokana na matokeo hayo ya haraka ya ukuaji wa uchumi yametokana na jitihada za Serikali  chini ya Rais Dk.John Magufuli katika kupambana na rushwa , kuondoa urasimu kwa kutengeneza mazingira wezeshi ya usajili wa biashara na leseni kwa wawekezaji wa nfani na nje.

Akifafanua zaidi mambo mengine ambayo yamefanyika katika kuwahudumia wawekezaji kwa haraka ni pamoja na kuboresha mfumo wa huduma mahala pamoja ndani ya TIC ambapo kwa sasa kuna maofisa zaidi  10 wanaotoka kwenye wizara,idara na taasisi za Serikali kwa ajili ya kutoa huduma za kusajili kampuni.

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WANANCHI UPATIKANAJI WA MAFUTA YA KULA NCHINI

TAASISI ZA FEDHA ZAKOPESHA BILIONI 59 KWA WANANCHI KUPITIA HATI ZA KIMILA

Viewing all 109941 articles
Browse latest View live




Latest Images