Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) WASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

$
0
0
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya sherehe ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa jana katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijiandaa kushiriki katika maandamano ya maadhimisho ya sherehe ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa jana katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walioshiriki Maadhimisho ya sherehe ya siku ya Wafanyakazi Duniani kitaifa yaliyofanyika jana katika uwanja wa Samora mkoani Iringa. 
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya sherehe ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa jana katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijiandaa kushiriki katika maandamano ya maadhimisho ya Sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kitaifa yaliyofanyika jana katika uwanja wa Samora mkoani Iringa.Picha na JKCI


UBUNGO YAPONGEZWA KWA UTOAJI MIKOPO KWA ASILIMIA 100, YAJIANDAA KUANZISHA VIWANDA

$
0
0
Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

SERIKALI kupitia  Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Joseph Kakunda ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam kwa kuwa Halmshauri ya kwanza na ya mfano kwa kutoa fedha za mikopo ya wanawake na vijana kwa asilimia 100, kutoka katika
mapato ya ndani.

Hivyo Naibu Waziri ameitaka Wizara ya TAMISEMI kuandikia Manispaa ya Ubungo barua ya pongezi,kwani maeneo mengine ni jambo ambalo linaonekana kugumu kutekelezeka lakini Ubungo
wameweza.

Manispaa ya Ubungo juzi wamezindua mchakato wa ugawaji wa mikopo ya Sh.bilioni 1.94 ,wakati ina mwaka Mmoja tu tangu kuanzishwa kwake.Akizungumza  fedha hizo Meya Ubungo Boniface Jacob 
,amesisitiza mikopo itatolewa kwa vigezo bila kuangalia dini,kabila wala chama cha mtu.

"Waosema mikopo ni Ilani ya CCM,wajiulize mbona kwingine kuna Halmashauri za CCM lakini hakuna mambo haya mazuri? Hivyo watu wajue kuna viongozi  makini na imara wanatoka chama cha Chama cha Upinzani upinzani na ndio msingi na chachu ya mafanikio,"amesema Jacob.

Jacob ametoa rai kwa vijana kuomba mikopo hiyo,kwani idadi ya akina mama ni kubwa kuliko idadi ya vijana,huku akiahidi Mei mwaka huu halmashauri kuanzisha viwanda vidogo kwa ajili ya kuwasaidia vijana suala la ajira.Risala iliyosomwa kwa mgeni rasmi imeeleza Halmashauri ya Ubungo imeidhinisha kutoa fedha kwa vikundi 364 ambapo vikundi 119 ni vya vijana na vikundi 245 ni vya wanawake.Jumla watakaonufaika na mikopo hiyo ni wananchi 11,312.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Joseph Kakinda akiwa ameambatana na viongozi wa Ubungo wakitembelea mabanda ya wajasiria mali mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa mikopo kwa vikundi vya wakina Mama na Vijana,walemavu leo jijini Dar as Salaam.Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI,Joseph Kakinda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ubungo wakitembelea katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa mikopo kwa vikundi vya wakina Mama na Vijana,walemavu leo jijini Dar as Salaam.

HAFTRADE YAUNGA MKONO ELIMU BURE KWA KUJENGA MADARASA MAWILI HANDENI MJINI

$
0
0

TAASISI isiyo ya kiserikali ya Haftrade Iliyopo Handeni Mjini mkoani Tanga imeamua kujenga madarasa mawili katika wilaya hiyo ili kuungana na Serikali katika mpango wa elimu bure.

Akizungumza katika ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa mwishoni mwa wiki iliyopita Handeni Mjini mkoani Tanga Mkurugenzi wa Taasisi ya Haftrade Thecla Mingwa amesema ujenzi wa madarasa hayo upo hatua za mwisho na lengo lao ni kuona wanafanzi wanakaa kwenye mazingira mazuri ya kusomea.

Mingwa amesema Hafrade ina wanachama hai 20 mpaka sasa na kufafanua taasisi yao imesajaliwa kwa ajili ya shughuli za kijamii ikiwemo, elimu,mazingira,afya na maji vijijini. " Taasisi yangu ya Hafrade wakati ikiendelea kusimamia ujenzi huo mkakati wake kutafuta wadau kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari ya Kwenjugo, pia kutoa elimu pamoja na kupanda miti ya matunda na mikorosho" amesema Mingwa.

Amesisitiza mikakati yao mingine ni kutoa huduma zao katika maeneo mengi zaidi huku wakidhamiria kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya tano.Aidha amesema mikakati yao mingine ni kuwa na mashamba makubwa kwa ajili ya shughuli za kilimo.uyaendesha kwa kilimo .Alisema Hafrade inashirikiana na Shirika la Save Children katika shughuli zake mbalimbali katika kuleta maendeleo.

"Hafrade inatoa huduma zake Handeni Mjini yenye Kata, 12 ambazo ni Chanika, Kidereko, Konje, Kwamagome,Kwediyamba,Kwenjugo Mangaribi ,Kwenjugo Mashariki,Mabanda,malezi ,mlimani, msasa na vibaoni,"amesema.Mingwa amesema katika utendaji wa shughuli zake Haftrade imegawanyika katika idara nne ambazo ni idara ya elimu, idara ya Afya, idara ya mazingira, na idara ya maji na inaendesha shughuli zake kwa kushirikiana na Serikali kuakikiasha malengo na mikakati iliyopangwa inatumia.

Ametaja baadhi ya kazi ya idara hizo kuwa ni Idara maji kulinda vyanzo vya maji, idara ya mazingira kuandaa maeneo ya shamba kwa ajili ya kilimo cha shamba darasa.cha mihogo na korosho.
 Wanachama wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Haftrade Ikikagua ujenzi wa Vyoo na madarasa ambayo wanajenga Katika kata ambazo wanaosimamia mradi Wilaya ya Handeni mjini mkoani Tanga  jana Picha na Heri Shaaban
 

WAKULIMA ZAO LA KARAFUU WILAYA YA MKINGA WAISHAURI SERIKALI KUWATAFUTIA KUPATA SOKO

$
0
0
Na David John, Tanga

WAKULIMA wa zao la Karafuu wilayani Mkinga mkoani Tanga wameishauri Serikali kusimamia zao hilo kama wanavyofanya katika mazao ikiwa pamoja na kupata soko la uhakika huku pia itambulike hata wakazi wa  wilayani hapa wanalima kwa wingi zao hilo.

Wakulima hao wamefafanua Serikali yenyewe inatambua karafuu inapatikana tu visiwani Zanzibar lakini ukweli ni kwmba nao wanalima kwa wingi zao hilo pamoja na mazao mengine.Akizungumza leo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mhesambia kilichopo Kata ya Kigongoi Mashariki Stephano Banda amesema kijiji chao  kinachounda na vitongoji zaidi ya vitatu wanalima kwa wingi zao la karafuu lakini changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni soko la zao hilo.

Amesema kuna wakulima wanamiliki mashamba makubwa ya karafuu na ndio zao kuu kwao lakini mara zote wamekosekana wawekezaji au wafanyabiashara wakubwa wa kununua zao hilo na kusababisha wakulima wake kukata tamaa ya kilimo hicho."Nataka nikuwahakikishie wananchi wa huku wanalima sana zao la Karafuu lakini changamoto kubwa ni soko , hivyo ni vema Serikali 
wakaweka nguvu kama ambavyo inafanya kwenye mazao mengine,"amesema.

Ameongeza Kijiji cha Mhesambia ni kikubwa mno katika wilaya ya Mkinga na kimsingi wananchi wake ni wakulima na zao kubwa ukiondoa mazao mengine kama mpunga, pilipili na mengineyo lakini Karafuu lakini akasisitiza changamoto ni soko.Mkazi wa Kijiji hicho Agustino Hassan amesema changamoto hizo katika eneo hilo ni  barabara, kukosa soko la uhakika , maji na umeme na hivyo iwapo zitaondolewa wananchi watapiga hatua kibwa kimaendeleo.

Amesema wananchi wanajitahidi kulima  na kuzalisha mazao lakini mvua ikinyesha tu kwa wingi ni shida kwani miundombinu ya barabara inakuwa haipitiki hasa kutoka Maramba hadi Daruni na kupanda Hemsambia.Akizungumzia changamoto za wakulima Diwani wa Kata hiyo ya Kigongoi Mashariki  A Mary Semhunge amesema miudombinu ya barabara inakwamisha wananchi kufanya kazi zao za kilimo kwa uhakika.

"Kuhusu zao la karafuu ni kweli wakulima wanalima kwa wingi na tayari tumekaa na Mbunge kuona namna gani panakuwepo na mkakati wa kuwa na kiwanda kidogo cha kuchenjua na kufungasha 
zao hili ambapo kipekee kuna pia pilipili manga, mdalasini, "amesema Semhunge Kuhusu mkakati wa maji amesema wananchi wapo tayari kwenye mpango wa kuchimba bwawa kubwa na hivi sasa wanamsubiri mhandisi ili kuona mahala sahihi pakuchimba.

Akizungumzia umeme amesema katika umeme wa awamu ya tatu kata hiyo hasa kijiji  cha Kigongoi Mashariki A huku akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana nao.

SERIKALI YAANDAA KITINI CHA MASUALA YA JINSIA KUENDELEZA KASI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI WA KITAIFA WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA KATIKA WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Luhota pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi  Kalambo zilizopo Iringa vijijini wakati alipokuwa njiani kuelekea Wilayani Kilolo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kilolo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Iringa vijijini katika eneo la Ndiwili (hawaonekani pichani) wakati alipokuwa njiani kuelekea Wilayani Kilolo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kilolo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ipogolo mkoni Iringa wakati akitokea Kilolo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi kwa kuimba nyimbo na vijana chipukizi wa Kilolo mara baada ya kuhutubia wananchi waliofika kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa. PICHA NA IKULU

Timu ya Ngobanya yaibuka mshindi wa May Day Tornament

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu Jamii


TIMU ya Ngobanya imeibuka mshindi kati fainali ya May Day Tornament baada ya kuibamiza timu ya Lake Cement kwa bao 2 kwa moja katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Kimbiji kigamboni jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika fainali hiyo ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni…. Alisema kuwa mpira wa miguu unaibua fursa kwa vijana katika kuonyesha kipaji na baadaye kujipatia kipato.

Amesema utaratibu unaofanywa na kiwanda cha Saruji cha Lake Cement ni mzuri katika kuwakutanisha katika mahusiano kati ya kiwanda na wananchi wanaozunguka kiwanda hicho.Nae Meneja wa Rasilimali Watu, Julieth Domel amesema wamekuwa na utaratibu wa kufanya mashindano kila mwaka katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi na maendeleo mazuri ikiwemo uboreshaji wa ligi hiyo.

Amesema kuwa katika mwaka ujao kutakuwa na maboresho ya ligi hiyo ikiwa na lengo la kuibua vipaji kwa wakazi wa Kimbiji .Afisa Uendeshaji na Mkuu wa Kiwanda hicho, Girdhari Jadhao amesema kuwa kama kiwanda ni wajibu kuwa karibu na wananchi wanaozunguka kiwanda hicho .

Kocha wa Timu ya Lake Cement, Azizi Senzey amesema kuwa wamekubali matokeo na watajipanga katika kipindi kingine katika kuchukua ubingwa.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Wangeslaus Lindi akizungumza katika fainali ya kati ya timu ya Ngobanya na Nyati iliyofanyika katika kiwanja cha Kimbiji, jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Wangeslaus Lindi akikagua timu ambazo zilikuwa katika dimba ya fainali zilizofanyika katika kiwanja cha Kimbiji.
Meneja wa Rasilimali Watu, Julieth Domel akizungumza kuhusiana na ufadhili wa Lake Cement katika mashindano mbalimbali ya kujenga ujirani mwema yaliyofanyika katika Uwanja wa mpira cha Kimbiji ,Jijini Dar es Salaam.
Kocha wa timu ya Nyati, Aziz Senzey akizungumza kuhusiana na kushindwa kuibuka kidedea katika fainali kati ya Ngobanya na Nyati katika mchezo uliochezwa katika uwanja cha Kimbiji jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watazamaji wa mashindano ya fainali kati ya Ngobanya dhidi ya Nyati, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kimbiji , jijini Dar es Salaam. 
Mashindano ya kamba katika fainali za mpira wa miguu yaliyofanyika uwanja wa Kimbiji

MAJI YANAYOTIRIRIKA MITAANI KUTOKA VIWANDANI YAPIMWE KEMIKALI.

$
0
0

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka  Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua hatua ya kupima maji yanayotiririka mitaani kutoka viwandani kubaini kama yana kemikali ambazo zinaathiri wananchi au hazina madhara yoyote.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afy, Maendeleo ys Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam.

"Bodi hii ninayoizindua leo inatakiwa kuhakikisha  majibu ya watu wanaokuja kuleta vipimo vyao yatoke mapema na haraka iwezekanavyo ili kupunguza msongamano wa wateja wenu" alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa Mamlaka hiyo inatakiwa kushirikiana na kufanya  mazungumzo na Taasisi ya Chakula na Dawa TFDA na TBS ili kutoingiliana katika majukumu kwani kuna kuna kipengele cha majukumu yao kinafanana katika kusimamia ubora wa chakula.

Aidha Dkt. Ndugulile ameitaka Mamlaka hiyo kuisimamia kikamilifu sheria ya uchafuzi wa Mazingira ili kuepusha wananchi na magonjwa ya kuambukiza na yasioambukiza. Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo Dkt. Fidelis Mafumiko amesema kuwa wanaiomba Serikali kutatua changamoto ya upungufu wa mitambo ya kufanyia kazi katika mamlaka hiyo.

Aidha Dkt. Mafumiko amesema kuwa Bodi hiyo iliyozinduliwa leo ipo tayari kufanya kazi kwa manufaa ya  Watanzania japo mamlka hiyo ina upungufu wa Watumishi kutoka watumishi 400 mpaka kufikia watumishi 220.

Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imezinduliwa leo ikiwa na Wajumbe saba ambao ni Mwenyrkiti wa bodi hiyo Prof. Esther Jason, Katibu Dkt. Fidelis Mafumiko,  Dkt. Eliud Eliakimu,  Dkt. Samwel Gwamaka, Dcp. Hussein Laiser, Bi. Irene Leisure na Bw. Pius Mponzi. 
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu ambae alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Otilie Gowelle.kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt Esther Jason.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Esther Jason mwongozo wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu ambae alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Otilie Gowelle.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mku na viongozi wengine wa Srikali wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Esther akiongea akitoa neno mbele ya viongozi wa Serikali na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.
 Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam

WAJASIRIAMALI WANAWAKE 200 MKOANI KIGOMA WAPATIWA MAFUNZO KUWAIMARISHA KIUCHUMI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

WANAWAKE 200 ambao ni wajasiriamali mkoani Kigoma wanataraja kupata mafunzo yatakayosaidia kuwaimarisha kiuchumi na lengo ni kuhakikisha wanapata maendeleo katika mkoa huo na Taifa kwa ujumla hasa kipindi hiki cha kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda.

Awali akifungua rasmi mafunzo hayo jana mkoani humo na yanatarajiwa kudumu kwa siku 10 katika halmashauri zote mkoani hapa Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Gaden Machunda ametoa msisitizo kwa akina mama kujikita katika ujenzi wa viwanda.

Aidha Machunda amewataka akina mama kuzingatia misingi ya ujasiriamali pamoja na kuwa na nidhamu na biashara wanazozifanya huku akiwataka wauzaji wa hoteli na migawa kuwa nadhifu ili kuwavutia wateja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AJ General Company amesema lengo la mradi huo ni kuwawezesha wanawake na kusaidia kutekeleza Ilani ya Serikali ya awamu ya 5  kuelekea ujenzi wa Tanzania ya viwanda.Ambapo amesema wanawake watainuka kiuchumi kupitia mpango huu na wanawake watapata mikopo isiyokuwa na masharti kama ilivyokuwa hapo awali lakini pia kuwezesha bidhaa zinazozalishwa mkoani hapa kupata soko nje ya nchi.

Katibu wa Umoja wa Wanawake mkoani Kigoma (UWT) Edina Kuguru amesema wao kama viongozi wa wanawake wamejipanga kuhakikisha wanawake wote mkoani hapa wanaondokana na mfumo wa kuwategemea wanaume.Amesema mikakati waliyonayo ni kutoa elimu ya ujasiriama na jinsi ya kutumia fedha wanazopewe zinatumika ipasavyo na kuwatafutia masoko kwani wana mipango ya kuanzisha viwanda vya mihogo kwa kuwa zao hilo linalimwa sana mkoani Kigoma.

Mmoja wa wajasiriamali wa Mkoa wa Kigoa Maisala Barakabise amesema wanawake wa mkoa huo wanajitahidi kufanya biashara kwa kutumia mitaji yao na wao ndio walezi wa familia na ni wathubutu.Hivyo wakiwezeshwa wanaweza zaidi na kuongeza wamekuwa wakiibua fursa nyingi.

Amesema changamoto wanazokumbana nazo katika kutafuta kipato na kujiondoa katika dimbwi la umasikini ni mitaji modogo.Mjasiriamali mwingine Sakina Kabeza amesema wanawake wa Kigoma ni wachapakazi na wanajituma na kufafanua kipindi cha nyuma fursa zilikuwa ni chache lakini kwa sasa Awamu ya tano imejipanga kikamilifu kutoa fursa kwa wanawake wote.

"Na endapo wanawake wa Kigoma wakipatiwa elimu na mitaji wanaouwezo wa kufanya vitu vya tofauti na wanao uwezo wa kuchangamkia fursa kujikwamua kimaisha,"amesema.Aidha ameipongeza taasisi hiyo iliyojitokeza na kutoa elimu na mikopo kwa wanawake mkoani Kigoma.

Wito kwa jamii kuondokana na mila potofu,Jamii yaaswa kupeana elimu

$
0
0
Kuwepo kwa mila potofu katika jamii ya watanzania ni moja na ya jambo ambalo limekuwa ni kikwazo katika juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi mbalimbali za kijamii katika kupunguza au kutokomeza kabisa matatizo ya kiafya ambayo huwapata watoto wachanga wanaozaliwa na walio na umri chini ya miaka mitano.

Watoto wengi katika rika hilo huwa katika athari ya kuzaliwa au kupata magonjwa ambayo ni kuwa na vichwa maji, pamoja na mgongo wazi, ikiwa ni magonjwa ambayo huweza kuepukwa endapo tu jamii nzima ya watanzania wataweza kupatiwa elimu sahihi ya namna ya kuepuka au kuzuia magonjwa hayo na endapo kutabainika watoto wenye matatizo hayo jamii isiweze kuwaficha kutokana na imani potofu.

Hayo yamebainishwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Bwana Laurent Lemeri Mchome, wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel walipowatembelea watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi pamoja na wazazi/walezi wao waliolazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya kuwapa mahitaji mbalimbali ya kijamii kama sehemu ya msaada wao kama wafanyakazi. 

“Akiongea baada ya kukabidhiwa msaada huo, kwa niaba ya madaktari na wauguzi wodini hapo Dr Laurent Mchome amesema kila mwaka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) tumekuwa tukitoa matibabu kwa wagonjwa zaidi ya 350 nchi nzima kupitia kampeni ya watoto wenye vichwa maji na mgongo wazi. Pia tumekuwa tukiweka kambi ya kutibu watoto kila mkoa kwa kila kanda nchini na changamoto kubwa ni kwamba jamii kubwa ya watanzania hawana elimu ya kutosha kuhusu magoinjwa haya kuwa yanatiwa na watoto hupona kabisa”.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Halotel Bwana Trieu Thanh Binh na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya Kijamii kwa baadhi wa wauguzi leo wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kuwapelekea mahitaji hayo.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Halotel Bwana Trieu Thanh Binh akikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kijamii yenye kwa baadhi wa wauguzi leo wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kuwapelekea mahitaji 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Halotel Stella Pius akikabidhi moja ya msaada wa mahitaji mbalimbali ya kijamii kwa mmoja wa wazazi wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea watoto walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)na kuwapelekea mahitaji hayo.

Serikali Kupeleka Umeme Vijiji Vyote Ifikapo Juni 2021

STANBIC FC YAISULUBU TRAVEL PARTNER FC WAKISHEREKEA SHEREHE ZA MEI MOSI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KATIKA Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) benki ya Stanbic sambamba na wadau wao wakubwa Travel Partner wamesherekea kwa kucheza kandanda katika viwanja vya 
Don Bosco Oysterbay jijini Dar es salaam.

Katika mtanange huu Stanbic Fc walimaliza kwa kutoka kifua mbele kwa mabao 9 na Travel Partner wakiambulia bao 1 pekee lililofungwa kipindi cha pili na James Malola.Akizungumza na Michuzi blog, Mkurugenzi Mkuu wa Travel Partner Erick Mashauri amesema wameamua kusheherekea Mei Mosi kwa namna hiyo ili kujenga mahusiano ya kikazi, kufurahi na kujenga mwili.

Licha ya kupoteza mchezo huo Mashauri ameeleza sababu za kushindwa kwao ni kutokana na uchanga wa timu na amehaidi watafanya mazoezi ili kuwapiku vinara hao.

Pia Mashauri amewaomba wafanyakazi wengine kutumia siku hiyo kusherekea kwa namna mbalimbali zinazolenga kujenga, 
kushirikiana na kubadilishana mawazo katika kazi zao.Kiongozi wa Timu ya Stanbic William Kimaro ameeleza siri ya ushindi huo ni mazoezi ya kutosha na kufafanua mchezo huo umewafanya waendelee kudumisha uhusiano na kampuni hiyo.

Aidha James Malola aliyeipatia bao pekee Travel Partner amesema licha ya kupoteza mchezo bado wana nguvu katika mechi zinazofuata na kukiri  mazoezi makali ya Stanbic Fc ndio yaliruhusu magoli 9 wavuni.
Mkurugenzi mkuu wa Travel partner, Erick Mashauri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.
 Kikosi cha timu ya Stanbic Fc kilichocheza na na Travel partner katika kusherekea siku ya Mei mosi. 
 Mechi baina ya Stanbic Fc Dhidi ya Travel partner ikiendelea katika viwanja vya Oysterbay jijini Dar es salaam.(picha zote  na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
 Kocha wa Travel partner  Aziz Chonya akizungumza na wachezaji wake mara baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

NGORONGORO HEROES KUVAANA NA MALI MEI 12 MWAKA HUU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

TIMU ya Taifa ya chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes inashuka dimbani  Mei 12 mwaka huu kuvaana na kikosi cha Timu ya Mali utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ngorongoro Heroes walifanikiwa kuwaondoa timu ya vijana ya Congo DR kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoka sare ya 1-1 hapa jijini Dar  es salaam na 0-0 nchini Congo  kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba

Akizungumza kuelekea mtanange huo Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini.(TFF) Clifford Ndimbo amesema mchezo huo utakaoanza majira ya saa 10 alasir utakuwa ni kwa ajili ya kufuzu kwenda katika fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba. 

Ndimbo amesema timu hiyo ambayo tayari ipo kambini kujiandaa na mchezo huo muhimu na tayari benchi la ufundi limeanza mikakati ya kuhakikisha wanatoka na ushindi ili kuweza kuvuka hatua inayofuata.

Viingilio vya michezo hiyo ni Sh.3000 kwa VIP na mzunguko ikiwa ni Sh.1000 Ngorongoro Heroes inatakiwa kuhakikisha wanatoka na ushindi nyumbani ili mchezo wa marudiano usiwe mgumu kwa upande wao.
TIMU ya Taifa ya chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes

RAIS DKT.MAGUFULI KUWA MGENI RASMI TUZO ZA CTI MEI 4

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Mafoto Blog, Dar

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tuzo za Rais za Mzalishaji bora wa Viwandani (PMAYA) za mwaka 2017 zinazotarajiwa kufanyika Mei 4 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo la PMAYA zinazoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) hutoa tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri katika mwaka uliopita likiwahusisha wanachama wa CTI na wasio wanachama.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam,mchana huu, Mkurugenzi mtendaji wa CIT Leodger Tenga amesema kuwa tarehe 7 Desemba mwaka jana walizindua shindano la mzalishaji bora wa kampuni na tayari kampuni 36 ziliweza kujitokeza kwenye mchakato huo ukiwa umeenda vizuri na washindi wamepatikana ambao watakabidhiwa zawadi zao siku hiyo ya ijumaa, Mei 4.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Leodgar Tenga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,leo mchana wakati akitangaza rasmi \tarehe ya kutoa Tuzo za Rais za Viwanda zinazotarajia kufanyika Mei 4 mwaka katika Hoteli ya Serena, ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Katikati ni Mwenyekiti wa CTI, Dkt. Samuel Nyantahe na Makamu wa pili wa Mwenyekiti CTI, Shabbir Zavery. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Machapisho wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Thomas Kimbunga, akitangaza utaratibu wa upatikanaji wa washiriki wa tuzo hizo,wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, ambao ni sehemu ya waratibu mkutano huo, Teddy Mapunda, akiongoza mkutano huo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Machapisho wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Thomas Kimbunga, akitangaza utaratibu wa upatikanaji wa washiriki wa tuzo hizo,wakati wa mkutano huo. kutoka (kushoto) ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Alaf Tanzania, Theresia Mmary, Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa CTI, Shabbir Zavery, Mwenyekiti wa CTI, Dkt. Samuel Nyantahe na Mkurugenzi Mtendaji, Leodgar Tenga.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania CTI, Dkt. Samuel Nyantahe, akizungumza na waandhishi wa habari kuhusu tuzo hizo.


Kwa upande wa mwenyekiti wa shirikisho hilo Dkt. Samwel Nyantahe ameeleza kuwa shirikisho hilo ni la wamiliki wa viwanda nchini ni kwa lengo la kuweka mazingira ya uzalishaji nchini na shindano hilo linatoa nafasi ya kutangaza bidhaa kwa wafanyabiashara na kupata nafasi ya kukutana na Rais na kuzungumza naye ikiwa ni muhimu kwa kuwa tunaelekea katika uchumi wa viwanda.

Mashindano hayo yanahusisha zaidi ya sekta 18 na makampuni 36 na kuna zawadi maalumu kwa washindi wa matumizi bora ya nishati katika viwanda vyao.

Mkurugenzi wa machapisho wa (CTI) Thomas Kimbunga ameeleza kuwa namna ya kushiriki ilikuwa katika makundi matatu ya viwanda yaani vile vikubwa, vidogo na vya kati na washiriki wameshindanishwa kulingana na makundi waliyoshindania na vigezo katika kila kundi ni pamoja na mazingira, mahusiano kazini na kuendeleza wafanyakazi sambamba na suala la ubora wa bidhaa kwa kuthibitishwa na TBS.

Aidha ameeleza kuwa shindano hilo litatasaidia kuongeza ufanisi hasa katika utendaji kazi katika sekta mbalimbali za viwanda pia washiriki watapata nafasi ya kujua maeneo waliyofanya vizuri na kupata nafasi ya kuboresha vyema bidhaa zao.Baadhi ya vigezo ambavyo vimezingatiwa ni pamoja na faida kwa jamii, afya na usalama, uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, utendaji kiuchumi, utendaji kiteknolojia na matumizi bora ya nishati.

STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI

$
0
0
*Kutumia lugha ya Kiswahili katika kuutangaza

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd yenye chapa ya StarTimes imetangaza rasmi kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 Mubashara kupitia king’amuzi chake. StarTimes imethibitisha kuonesha michuano hiyo leo katika hafla fupi iliyofanyika Terrace, Slipway Masaki jijini Dar es Salaam na kushirikisha waandishi wa Habari pamoja na wadau mbalimbali wa soka nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo David Malisa amesema “Mwaka huu katika Kombe la Dunia la 21, StarTimes ni mrushaji rasmi wa michuano hiyo itakayoanza Juni 14 hadi Julai 15 nchini Urusi. Mechi zote 64 zitakazochezwa Urusi katika Kombe la Dunia zitarushwa moja kwa moja.

" Amefafanua mbali na kurusha tu michuano hiyo maarufu zaidi Duniani, StarTimes watarusha matangazo ya michezo yote katika lugha ya Kiswahili na hiyo ni katika jitihada za kuienzi na kuikuza   lugha ya Kiswahili lugha ambayo ni maarufu zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Meneja masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes.
Mkuu wa Kitengo cha Maudhui ya Startimes, Zamarad Nzowa akizungumzia namna walivyojipanga wakishirikiana na wasanii mbalimbali wa hapa nchini kwenye msimu wa kombe la Dunia litakalochezwa nchini Urusi hasa kwenye vipindi mbalimbali  vitakavyokuwa vinarushwa kupitia kwenye king'amuzi cha Startimes.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la utangazaji nchini Tanzania (TBC), Edna Rajab akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes.
Balozi wa Startimes Tanzania kwenye msimu wa Kombe la Dunia na Msanii wa Bongo Movies, Wema Sepetu akizungumzia namna walivyojipanga na wasanii wenzake wakati wa kipindi chote cha Kombe la dunia wakishirikiana na Startimes Tanzania.
Mchambuzi wa Michezo, Jeff Leya akizungumzia fulsa aliyoipata mara baada kuingia mkataba na Startimes kuchambua mpira kwenye kombe la dunia kupitia king'amuzi cha Startimes.
Mkurugenziwa Startimes Tanzania, Wang Xiaobo akipiga mpira golini
Viongozi wa Startimes wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wakati wa wa uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes kwenye ukumbi wa Hotel ya Slip Way jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT. MWIGULU, WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YAKE, WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI YA KUWASILISHA BAJETI BUNGENI, JIJINI DODOMA KESHO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba akitoa Maelekezo kwa Watendaji Wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Wizara hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kusomwa bajeti ya Wizara hiyo, Bungeni jijini Dodoma, kesho. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini humo leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba (katikati meza kuu), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira alipokua anatoa maelezo katika kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Wizara hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kusomwa Bungeni jijini Dodoma, kesho. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini humo leo. 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Issa Ng'imba, kabla ya kuanza kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Wizara hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kusomwa Bungeni jijini Dodoma, kesho. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini humo leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba (katikati meza kuu), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira alipokua anatoa maelezo katika kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Wizara hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kusomwa Bungeni jijini Dodoma, kesho. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini humo leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

AUNT EZEKIEL KUZINDUA FILAMU YA MAMA MEI 13 MLIMANI CITY

RAIS DR SHEIN AONGOZA MKUTANO WA MABALOZI WILAYA MKOANI PEMBA

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akitia sani kitabu cha wageni alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo kwa kuzungumza na Mabalozi   akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi (kushoto) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali Juma.
 Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi katika Shehia Mbali mbali za Wilaya ya Mkoani Pemba wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akizungumzanao leo  katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari  Mohamed Juma Pindua Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba  akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi
 Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliohudhuria katika Mkutano wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Ngazi ya Mashina (Mabalozi) katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Mohamed Juma Pindua Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadala (Mabodi) alipokuwa akimkaribisha   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Ngazi ya Mashina (Mabalozi) katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Mohamed Juma Pindua Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Ngazi ya Mashina (Mabalozi) katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari  wa Mohamed Juma Pindua  Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akionesha Ilani ya Chama kwa  Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Ngazi ya Mashina (Mabalozi) alipokuwa akizungumza nao leo katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Mohamed Juma Pindua Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Ngazi ya Mashina (Mabalozi) katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Jumapindua Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi. (Picha na Ikulu)

DAWASCO KUANZA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI WA MALIPO SERIKALINI

$
0
0
Na Emanuel Masaka, Glogu ya Jamii
SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limesema linatarajia kuokoa takriban Sh.milioni 200 kila mwezi, kutokana na kuanza kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo serikalini (GePG).

Mfumo huo umetajwa kulinufaisha shirika hilo kwa sababu utaondoa ulipaji wa tozo za kamisheni ya asilimia 4 kwa kila mihamala ya Shirika hilo, ambayo awali ilikuwa ikilipwa kwa wakala wakiwemo Maxcom na Selcom.

DAWASCO imesema mfumo huo unaanza kutumika kwenye malipo yote ya ankara za maji kuanzia leo, ambapo wateja watalipia kwa kutumia huduma za kifedha kwa simu za mkononi za M-PESA, tiGo PESA na Airtel Money.

Hayo yamesemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja,wakati anazungumzia mfumo huo wa ulipaji kwa njia ya kieletroniki.

Luhemeja amesema GePG ni mfumo wa Serikali ambao unaunganisha taasisi zote za umma zinazotoa huduma na mteja wa huduma husika moja kwa moja bila kuwepo mtu wa kati.

"Katika mfumo huu mpya, malipo yatafanyika kwa kutumia kumbukumbu namba yaani Control Number ambayo ina tarakimu 12 na tutakuwa tunaitoa kwa mteja ili itumike kwenye malipo hayo kwa mihamala ya kifedha kwa njia ya simu.

" Shirika litapata fedha zake kwa wakati, kwa sababu zitakuwa zikiingia moja kwa moja kwenye akaunti yetu ya makusanyo na zitakazokuwa zimeokolewa kutokana na kupungua kwa gharama ya uendeshaji tutazirudisha kwenye utoaji huduma," amesema.

Mhandisi Luhemeja ameongeza:  "Kwa utaratibu huu DAWASCO haitohusika kwenye kulipia kamisheni ya mihamala itakayokuwa ikifanyika na badala yake, mteja atakuwa anakatwa kiasi kisichopungua asilimia moja ya kila mihamala ya malipo atakayofanya."

Pamoja na ankara za maji, malipo mengine yatakayofanyika kwa mfumo wa GePG DAWASCO ni maunganisho mapya ya majisafi na majitaka, urejeshaji wa maji yaliyositishwa katika deni na manunuzi ya vitabu vya zabuni.
Afisa Mtendaji wa DAWASCO  Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza leo jijini Dar as Salaam juu ya matumizi ya mfumo mpya  wa kieletroniki wa malipo serikalini(GePG).

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO , DK PHILIP MPANGO AFUNGUA MKUTANO WA KIUCHUMI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa Uchumi ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Sera za Kiuchumi na Kijamii(ESRF) wakishirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini lengo ikiwa kujadili masuala mbalimbali ya ukuzaji uchumi.Mkutano huo unafanyika leo,jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Sera za Kiuchumi na Kijamii(ESRF),Dk. Tausi Kida, akizungumza wakati wa ufunguzi wa  Mkutano wa Uchumi ulioandaliwa na Taasisi hiyo wakishirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini lengo ikiwa kujadili masuala mbalimbali ya ukuzaji uchumi.Mkutano huo unafanyika leo,jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt,  akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa Uchumi ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Sera za Kiuchumi na Kijamii(ESRF) wakishirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini lengo ikiwa kujadili masuala mbalimbali ya ukuzaji uchumi.Mkutano huo unafanyika leo,jijini Dar es Salaam.
 Profesa Joseph Stiglitz  akitoa mada katika  Mkutano wa Uchumi ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Sera za Kiuchumi na Kijamii(ESRF) wakishirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini lengo ikiwa kujadili masuala mbalimbali ya ukuzaji uchumi.Mkutano huo unafanyika leo,jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Mkutano wa Uchumi ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Sera za Kiuchumi na Kijamii(ESRF) wakishirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini, wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano huo unaofanyika leo jijini Dar es Salaam. .Picha na Abubakari Akida
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images