Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

CCK WAJADILI HALI YA SIASA NCHINI,WAZUNGUMZIA RUZUKU INAYOTOLEWA KWA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

CHAMA Cha Kijamii (CCK) kimekutana na wawakilishi kutoka mikoa 20 nchini kwa mara ya kwanza tangu kilipopata usajili wa kudumu mnamo mwaka 2012.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam  katika mkutano huo aliyekuwa mwenyekiti ambaye amejiuzulu nafasi yake Costastine Akitanda ameeleza kutokana na majukumu mengine aliyopewa ya kusimamia kilimo barani Afrika ameona aachie nafasi hiyo na anaamini Chama hicho kitafika mbali zaidi.

Akitanda ameeleza lengo la chama hicho ni kuwasaidia wananchi katika masuala mbalimbali ya kijamii hasa uchumi na kufafanua wanachama ndio wenye maamuzi katika chama katika kuhakikisha chama kinaenda mbele zaidi.

Kuhusu suala la ruzuku kwa vyama vya siasa Akitanda ameshauri kuwa ruzuku zitolewe kugharamia chaguzi ili kuwe na usawa katika uwakilishi na si kutolewa katika vyama.

Katibu wa chama hicho Renatus Muhabi ameeleza kuwa licha ya changamoto zilizopo kama vyama vingine kama vile kukosa ruzuku  jambo linalosababisha  ugumu katika kuendesha chama na amewaomba wanachama kuendeleza malengo ya chama hicho sambamba na kushika dola mwaka 2020.

Hivyo amewataka wasikatishwe tamaa na upotoshaji kuhusu hali ya kisiasa ya sasa kuhusu utendaji kazi wa awamu ya tano inayofanya mapinduzi katika jamii ya kitanzania.

Aidha amesema kuwa chama hiki kimepokelewa vizuri na wananchi hivyo wanataraji watafanya mapinduzi katika siasa na kuifikisha nchi katika mahali sahihi.

Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo ameshiriki mkutano huo na ameeleza kuwa amefurahi kualikwa na chama hicho ili aweze kutoa nasaha na ameeleza kuwa vyama vya siasa lazima viwe na urafiki kwa kuzungumza pamoja.

Amefafanua hiyo italeta siasa za amani na kusikilizana na hakuna chama pinzani bali vyote vina mlengo wa kuleta maendeleo nchini. Kuhusu ruzuku kwa vyama ameeleza ni muhimu zitolewe katika chaguzi ili kuweza kupata uwakilishi bungeni.

Mkutano huu ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama ya siasa kama vile UPDP, SAUTI YA UMMA, TLP na Demokrasia Makini.

BALOZI MASILINGI AMVALISHA CHEO BRIGEDIA JENERALI AP MUTTA MWAMBATA WA JESHI UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI NA CANADA

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta (hayupo pichani) kwenye hafla fupi ya kuvikwa cheo cha Brigedia Jenerali iliyofanyika siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22, Washington, DC.Balozi Wilson Masilingi alimwagia sifa kwa kazi nzuri anayofanya kwa nidhamu ya hali ya juu, kujituma kwake na kushirikiana ndio chachu ya mafanikio yake. 

Wambata wengine waliovikwa vyeo vya Brigedia Jenerali ni Brig Gen AS Nwamy- Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini India, Brig Gen AM Alphonce Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Brig Gen JJ Mwaseba- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na Brig Gen RC Ng'umbi- Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini China. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production kwa hisani ya Kilimanjaro Studio.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akitoa hotuba fupi ya kumpongeza Brigedia Jenerali Adolph Mutta kwa Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akiondoa cheo cha Colonel na kumvisha cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Brigedia Jenerali AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbu wa mkutano a Nyerere hall uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimvua kofia ya cheo cha Colonel na kumvisha kofia ya cheo cha Brigedia Jenerali Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani AP Mutta siku ya Jumatatu April 30, 2018 katika ukumbi wa mkutano wa Nyerere Hall.uliopo ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi akimpongeza Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta 
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta akipongzwa na mkewe Agnes Mutta.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta akitoa shukurani kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkuu wa majeshi Tanzania Luteni Jenerali Venance Mabeyo. Katika hotuba yake ya shukurani alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumfikisha pale alipo na kushukuru familia yake hasa mke wake. Brigedia Jenerali AP Mutta aliwashukuri Balozi mstaafu Mhe. Liberata Mulamula na Mhe. Balozi Wilson Masilingi wakiwemo Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ushirikiano wanaompa na akaahidi ataendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha wanaiwakilisha vyema nchi yetu nchini Marekani.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi (watatu toka kushoto) na wengine toka kushoto ni EdgarMutta (mtoto wa Brigedia Jenerali Mutta), Bi. Agnes Mutta (Mke wa Birigedia Jenerali Mutta),Bi Marystela Masilingi (mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi) na kulia ni Judy Mutta (mtoto wa Brigedia Jenerali Mutta)
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto waliokaa) wengine waliokaa toka kushoto ni aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula, Bi. Agnes Mutta, mke wa Brigedia Jenerali AP Mutta na Kulia na Bi. Marystela Masilibgi mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi. Wengine waliosimama ni Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi(watatu toka kushoto waliokaa) wengine waliokaa toka kushoto ni aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula, Bi. Agnes Mutta, mke wa Brigedia Jenerali AP Mutta na Kulia na Bi. Marystela Masilingi mke wa Mhe. Balozi Wilson Masilingi. Wengine waliosimama ni Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na familia yake kutoka kushoto ni Edgar Mutta, mkewe Bi. Agnes Mutta na kulia ni Judy Mutta.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Adolph Mutta katika picha ya pamoja na mkewe Bi. Agnes Mutta.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI SAUDI ARABIA WAADHIMISHA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akikata keki ya sherehe ya Muungano na Mgeni Rasmi katika sherehe hiyo Naibu Gavana wa Jiji la Riyadh Dkt. Adel Al Jubail.

Ubalozi wa Tanzania nchini uliadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanzania mjini Riyadh kwa sherehe iliyojumuisha jumuiya wa wanadiplomasia, Watanzania na Wanadiaspora waishio nchini Saudi Arabia.
 Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza(kulia) akizungumza jambo na Naibu Gavana wa Jiji la Riyadh Dkt. Adel Al Jubail wakati wa sherehe ya miaka 54 ya muungano wa Tanzania.
 Baadhi ya Watanzania waishio Saudi Arabia wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanzania.
 Picha ya pamoja na madaktari wa hisani wanaotoa huduma za afya Tanzania Bara na Zanzibar wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 Baadhi ya wake wa Mabalozi wa Afrika waliohudhuria sherehe hizo kutoka kushoto Gabon, Gambia, Eritrea, Burkina Fasso, Tanzania, Cameroon, Ghana na Nigeria.  
Baadhi ya wageni na waalikwa mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo.

PROFESA KAMUZORA ATEMBELEA OFISI ZA TNCM DAR ES SALAAM

$
0
0
 Katibu Mtendaji Dr. Rachel Makunde wa Kamati ya Uratibu wa Fedha za Mfuko wa Dunia kwa ajili ya Kudhibiti UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu (TNCM) akimweleza katibu Mkuu Ofisiya waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora jinsi kamati yake inavyoshiriki kuratibu masuala ya afya nchini kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia (Global Fund) ofisini kwake tarehe 30 Aprili, 2018 Jijini Dar es Salaam zilizopo katika Ofisi ya Tume ya Kuthibiti UKIMWI.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora akisisitiza jambo wakati akizungumza na Katibu Mtendaji Dr. Rachel Makunde wa Kamati ya Uratibu wa Fedha za Mfuko wa Dunia kwa ajili ya Kudhibiti UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu (TNCM) wakati alipofanya ziara fupi  Ofisi kwao Dar es Salaam Tarehe 30 Aprili, 2018.

WAFANYAKAZI OFISI YA WAZIRI MKUU KUENDELEA KUTOA HUDUMA KWA UFANISI KWA WATANZANIA

$
0
0
Katika kusherehekea siku ya Wafanyakazi Duniani, wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameungana na wafanyakazi wote Duniani kwa kujumuika na wafanyakazi wengine wa hapa nchini jijini  Dodoma na kuahidi  kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi kwa Watanzania.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa sherehe hizo wafanyakazi hao, wamesema kuwa ofisi ya Waziri Mkuu kama mratibu wa shughuli zote za serikali nchini na kama mratibu wa shughuli za Kazi na ajira nchini wataendelea kutekeleza majikumu hayo kwa uadilifu na ufanisi ili huduma zinazotolewa na serkali ziwe zenye tija kwa Watanzania.

Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na kuratibu Shughuli zote za serikali ndani na nje ya Bunge pia inaratibu masuala mtambuka, kama  shughuliza maafa, Udhibiti wa matumizi ya madawa ya Kulevya, Vita dhidi ya UKIMWI, Huduma kwa watu wenye Ulemavu. Aidha inahusika na  kuchapa nyaraka za uendesheshaji shughuli za serikali, masuala ya Vyama vya siasa, Masuala ya Uchaguzi, Masuala ya kazi, Ajira na maendeleo ya vijana, pamoja na masuala ya uwekezaji na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Maadhimisho ya sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka huu zimebebwana kauli mbiu ya “Uunganishaji wa Mifuko ya Jamii ulenge kuboresha mafao ya mfanyakazi”
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakipita katika viunga vya jiji la Dodoma kuelekea katika uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri kushiriki seherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani, leo tarehe 1 Mei, 2018.
 Baadhi ya Wafanyakazi  wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakishiriki maandamano ya kuelekea katika uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri kushiriki seherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani, leo tarehe 1 Mei, 2018, Jijini Dodoma.
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakipita mbele ya mgeni rasm wakati wa sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani  zilizofanyika katika uwanja wa mpira wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 1 Mei, 2018.
Baadhi ya Wafanyakazi  wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia sherehe za siku ya wafanyakazi Duniani katika uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri leo tarehe 1 Mei, 2018, Jijini Dodoma.

RAIS MHE. DKT MAGUFULI AHUTUBIA KATIKA SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI ZILIZOFANYIKA KITAIFA MKOANI IRINGA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
 Wafanyakazi mbalimbali wakipita kwa maandamano katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
 Sehemu ya Wafanyakazi waliohudhuria katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi mara baada ya kuhutubia mamia ya wafanyakazi katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na wasanii wa kizazi kipya kutoka mkoani Iringa waliotumbuiza katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa.
 Sehemu ya Walimu waliohudhuria katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa wakipiga makofi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiwa na Chifu wa Wahehe, Mtwa Adam Mkwawa II ambaye alihudhuria katika katika Maadhimisho ya Sherehe ya Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika katika uwanja wa Samora mkoni Iringa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiondoka katika uwanja wa CCM wa Samora mkoani Iringa mara baada ya kuhutubia katika shere za Mei Mosi. 
PICHA NA IKULU

WAFANYAKAZI WA TIB CORPORATE BANK WAUNGANA NA WAFANYAKAZI WENGINE KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA MEI MOSI LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Wafanyakazi wa TIB Corporate Bank katika maadhimisho ya Mei Mosi leo jijini Dar es Salaam wakionesha bango lao lenye ujumbe wa kuhamsisha wananchi juu ya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwaajili ya kulenga kuboresha mafao ya wafanyakazi ikiwa hiyo ndio kaauli mbiu yao katika kuadhimisha sikukuu ya Mei mosi kwa mwaka huu 2018.

Leo wafanyakazi kazi wa TIB Corporate Bank wamejiunga na wafanyakazi wote Tanzania katika kuadhimisha sikukuu ya Mei Mosi ambayo hufanyika kila mwaka kila ifikapo mwezi May 1.
 TIB Corporate Bank wakinadi moja ya bidhaa mpya kabisa ya jipange inayowezesha kuwa na akaunti inayozaa riba kubwa na kukuwezesha kupata mkopo nafuu kwa haraka zaidi.
Wafanyakazi wa TIB Corporate Bank wakiwa jukwaani tayari kumsikiliza mgeni rasmi ktk maadhimisho ya siku ya wafanyakazi maarufu kama Mei mosi wakiwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam leo.

SERENGETI BOYS WAREJEA NCHINI KISHUJAA NA KOMBE LA UBINGWA WA CECAFA U 17

$
0
0
 Nahodha wa Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys Morice Michael akiwa amenyanyua juu kombe la ubingwa wa CECAFA 2018 walilonyakua nchini Burundi baada ya kuwasili Dar es salaam alfajiri ya leo. Serengeti Boys wametwaa ubingwa huo wa Cecafa baada ya kuifunga Somalia katika mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Ngozi kwa mabao ya EdsonJeremiah na Jaffar Juma Mtoo.Katika mashindano hayo Serengeti Boys ilitoka sare 1-1 na Uganda kabla ya kuifunga Sudan 6-0 na baadaye kuichapa Kenya kwa mabao 2-1 kwenye nusu fainali na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa fainali.

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akikabidhiwa na RAis wa TFF kombe la ubingwa wa CECAFA la vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya Serengeti boys kuwasili nalo  Dar es salaam
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe  akiwa na Serengeti Boys na viongozi wao baada ya mabingwa hao wa U-17 CECAFA 2018 kuwasili nalo  Dar es salaam

MICHUZI TV: Rais Dkt Magufuli akihutubia Taifa kwenye sherehe za Mei Mosi mjini Iringa

WAAJIRI ACHENI KUWEKA ZAWADI HEWA KWA WAFANYAKAZI WENU RC DODOMA

$
0
0
MKUU wa mkoa Dodoma,Dk.Binilithi Mahenge amepiga marufuku waajiri wote kutoa ahadi hewa kwa wafanyakazi wanaotangazwa kuwa wafanyakazi bora na badala yake wafanyakazi hao wanatakiwa kupewa zawadi zao na vyeti kadri ilivyopangwa na halmashauri husika au mwajiri.

Mkuu huyo wa mkoa alisema imekuwa desturi waajiri wamekuwa wakitafuta sifa ya kutangaza dau kubwa au zawadi kubwa kwa wafanyakazi waliotangazwa kuwa bora lakini kinyume chake wafanyakazi hao wamekuwa wakiambulia vyeti huku pesa hawapewi na linakuwa deni sugu.

Dk.Mahenge alitoa kalipio hilo baada ya wafanyakazi bora wa jiji la Dodoma pamoja na wafanyakazi bora wa Wilaya ya Chemba kupewa vyeti tu huku wakiahidiwa kupewa fedha baadaye badala ya kupewa fedha muda huo huo.

Akizungumza na wafanyakazi wakati wa utoaji wa vyeti, zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu kiongozi huyo wa mkoa aliagiza mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,Godwin Kunambi pamoja na uongozi wa halmashauri ya Chemba kuhakikisha wanawapatia fedha zao wale wote waliochaguliwa kuwa wafanyakazi bora na si vinginevyo.

Alisema imekuwa tabia ya halmashauri nyngi kutangaza wafanyakazi bora na kutangaza kuwapatia vyeti na fedha taslimu lakini hawafanyi hivyo matokeo yake wafanyakazi wamekuwa wakizurumiwa au kupewa hundi feki jambo ambalo alisema ni kuwakatisha tamaa wafanyakazi wanaojibidisha kufanya kazi kwa bidii.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkta Bilinith Mahenge akizungumza na wafanyakazi katika maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi zinazofanyika duniani kote kila Tarehe 1 ya mwezi wa 5 zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ambapo kitaifa mwaka huu zinafanyika mkoani Iringa
Sehemu ya wafanyakazi wa mkoani hapa wakifuatilia Hotuba ya mkuu wa mkoa hayupo piachani) kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi zenye kauli mbiu ya kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Leo picha na Mahmoud ahmad Dodoma.

TASAF YAJIVUNIA MAFANIKIO KATIKA UTEKELEZAJI MIRADI YA KUPAMBANA NA UMASKINI NCHINI.

$
0
0
NA Estom Sanga - DAR ES SALAAM 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umefanikiwa kutekeleza miradi 14,051 yenye thamani ya shilingi bilioni 502 Tanzania Bara na Zanzibar tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999/2000. 

Akitoa taarifa kwa ujumbe wa Maafisa wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Sweden-SIDA waliotemebelea ofisi za TASAF jijini Dar es salaam na kisha kutembelea eneo la Makangarawe,katika Wilaya ya Temeke,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga ametaja miradi iliyotekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya Elimu, Afya,Maji, Barabara, Hifadhi ya Mazingira, Kilimo ,ufugaji n.k ambayo ilitekelezwa kwa mafanikio makubwa kwa kuwashirikisha wananchi kwenye maeneo yao. 

Bwana Mwamanga amesema kutokana na Mafanikio ya awamu ya I na II ya TASAF, Serikali iliamua kuanzisha awamu ya III ambayo kwa kiwango kikubwa inajielekeza katika kuzikwamua Kaya zinazokabiliwa na umaskini uliokithiri baada ya kugundua kuwa hazikuwa zinanufaika na huduma zilizokuwa zinapatikana kwenye maeneo yao kutokana na umaskini. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF ameuambia ujumbe huo kutoka SIDA kuwa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umeanza kuonyesha mafanikio na Walengwa wameanza kuwekeza katika miradi ya kiuchumi na hivyo kujiongeza kipato chao hususani katika nyanja za kilimo,mifugo na ujenzi wa nyumba huku suala la elimu na afyakwa watoto wao likipewa kipaumbele. 

Amesema hadi sasa TASAF inahudumia takribani kaya MILIONI MOJA NA LAKI MOJA ambazo zimeendelea kupata ruzuku na huduma nyingine kama elimu ya ujasiliamali, hifadhi ya mazingira,lishe, huku mkazo pia ukielekezwa katika kuhamasisha walengwa kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana ili kukuza shughuli za kiuchumi kwenye maeneo yao. 

Ujumbe huo kutoka SIDA baada ya kupata taarifa pia ulipata fursa ya kuuliza maswali juu ya Utekelezaji wa shughuli za Mpango na kujibiwa na Viongozi wa TASAF na kisha kuelekea katika eneo la Makangarawe,katika wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam ambako ulikutana na baadhi ya vikundi vya Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini na kujionea biadhaa mbalimbali zinazotengezwa na walengwa hao kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 

Hata hivyo katika maelezo yao,Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini huko Makangarawe wameonyesha kukabiliwa na tatizo la upatikanaji wa soko la bidhaa wanazozitengeneza huku pia wakiomba kupatiwa eneo mahususi kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao kwa ufanikisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga akiwa ameshika kikapu alichokinunua kutoka kwa Kikundi cha Walengwa wa TASAF,katika eneo la Makangarawe ,wilaya ya Temeke,Jijini Dar es salaam bidhaa wanazotengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (aliyeshika kitabu) akiangalia bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika eneo la Makangarawe,wilayani Temeke,Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga akiwa ameshika kikapu alichokinunua kutoka kwa Kikundi cha Walengwa wa TASAF,katika eneo la Makangarawe ,wilaya ya Temeke,Jijini Dar es salaam bidhaa wanazotengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (wapili kutoka kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka SIDA waliotembelea Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika eneo la Makangarawe,wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam kuona namna walengwa hao wanavyonufaika na huduma za Mpango huo.

DKT SHEIN AONGOZA KILELE CHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI WETE PEMBA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi wa Serikali na Sekta Binafsi katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakinyanyua mikono juu wakati wakiimba wimbo maaluma wa mshikamano katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba

Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wakinyanyua mikono juu wakati wakiimba wimbo maaluma wa mshikamano katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wakiwa katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
Wananchi wakiwa wamejifunika Mvua wakati walipokuwa wakiingika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)

Wafanyakazi mbali mbali wa Serikali na Sekta Binafsi wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba

TPA YAPATA TUZO YA OSHA

$
0
0
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepata tuzo ya mshindi wa tatu wa masuala ya usalama na afya sehemu ya kazi (OSHA) kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahali pa kazi yanayofanyika Mkoani Iringa.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa TPA wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya kichangani mjini Iringa. 
 Waziri wa Kazi, Vijana,  Ajira, Jinsia, Wazee, Watoto na Walemavu, Mhe Jenista Mhagama  akitoa tuzo ya mshindi wa tatu wa tuzo za OSHA za masuala ya usalama na afya sehemu ya kazi kwa Mwakilishi wa TPA, Abiduna Athumani katika maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya kichangani mjini  Iringa.

Mwakilishi wa TPA, Abiduna Athumani akionesha cheti walichotunukiwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya kichangani mjini  Iringa.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage akizungumza na Mkaguzi wa Zimamoto, Usalama, Afya  na Mazingira wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Bw.  Dunstan Biyengo mara baada ya kutembelea banda la TPA kwenye maonyesho  OSHA wakati wa maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi duniani

TFDA,TAASISI BARANI AFRIKA WAANZISHA MIRADI YA KUFUATILIA UBORA WA DAWA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania(T FDA ) kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali Afrika wamebuni miradi mikubwa miwiliyenye lengo la boresha,kuhakiki na kufuatilia ubora na viwango vya dawa zinazosambazwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati ufunguzi wa miradi hiyo ya PAVIA na PROFORMA, Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Profesa Muhammad Kambi amefafanua lengo ni kuweka mifumo ya kuthibiti ubora wa dawa barani Afrika.

Amesema miradi hiyo inafadhiliwa na programu ya maendeleo ya majaribio ya dawa kwa nchi za Ulaya na Afrika(EDCTP) na kusisitiza itasaidia pia kufuatilia kwa urahisi madhara ya dawa zinasambazwa na kutumiwa kwenye soko.

" Miradi hii itasaidia katika ufuatiliaji wa matukio baada ya mgonjwa kutumia dawa  husika , kubwa ni kuangalia imemsaidia kwa kiwango gani au imeleta madhara ili kuchukua hatua stahiki 
haraka,"amesema Profesa Kambi.

Ameongeza miradi hiyo kwa pamoja itashughulikia usalama wa  dawa kwa watumiaji na kubwa zaidi kudhibiti ubora wa dawa katika sehemu zote nchini na maeneo ya mipakani.Profesa Kambi ameongeza miradi hiyo inatarajiwa pia kuanza kwa kubuni mitaala maalum itakayotumiwa Vyuo Vikuu nchini ikiwa ni mkakati wa kuwandaa waafunzi mapema jinsi ya kukabiliana na matokeo ya dawa kwa mgonjwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Dawa  kutoka TFDA Adam Fimbo amesema usalama wa dawa nchini upo na mamlaka kupitia miradi hiyo miwili wataendelea kuboresha  huduma za upatikanaji na udhibiti wa dawa h afifu na bandia katika soko la dawa nchini . 

"Tumeungana na nchini kadhaa katika uanzishwaji na utekelezaji wa miradi hii katika harakati za kupambana matokeo baada ya mg onjwa kutumia dawa na kutengeneza mifumo inayoweza kuleta taarifa mapema na kuwasiliana kwa haraka na kubadilishana uzoefu,"amesema Fimbo.

Wakati huohuo Ofisa Mradi wa EDCTP Michelle Nderu amesema wameamua kufadhili miradi hiyo ili kuleta uzoefu kutoka nchi zilizoendelea na lengo ni kuboresha matumizi ya dawa sahihi kwa binadamu.
Mganga Mkuu wa Serikali- Wazara ya A f ya, P r of . M o ham mad B akar i Kambi, akiongea katika uzinduzi wa mi r adi mi ku bw a m iw il i ( P A V IA na PROFORMA) , inayolenga kuweka mi fu mo ya kut hi bi ti ub or a n a viwango vya madawa yanasambazwa n a ku tum iw a k atik a ma so ko ya Tanzania na nchi zingine za Afrika. ( P i ch a n a Mp i ga P ic ha W etu ) .

USHAHIDI KESI OFISA TRA ANAYEDAIWA KUMILIKI MAGARI 19 YA THAMANI YA MILIONI 197.6 KUSIKILIZWA KWA SIKU MBILI

$
0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

USHAHIDI dhidi ya kesi inayomkabili Ofisa Msaidizi wa Forodha wa (TRA), Jennifer Mushi anayedaiwa kumiliki magari 19 yenye thamani ya Sh.milioni 197.6 yasiyolingana na kipato chake unatarajia kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo.

Hayo yameelezwa leo Mei 2 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Inspekta Hamis 
kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Hata hivyo, Inspekta Hamis amedai kuwa hana taarifa za kutosha kuhusu usikilizwaji wa shauri hilo kwani lipo chini ya Mawakili wa Takukuru na hawapo mahakamani.Kutokana na taarifa hiyo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 28 na 29, 2018, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa mfululizo.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa anadaiwa kati ya Machi 21, 2016 na Juni 30, mwaka 2016 maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa mfanyakazi wa TRA  alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.Inadaiwa pia, alikutwa akimiliki magari 19, yakiwemo Toyota Ra4,Toyota dyna truck, Toyota viz, Suzuki carry, Toyota Ipsum na 
mengineyo ambayo yote yote yana thamani ya milioni.197,601,207
.
Pia anadaiwa, kati ya Machi 21, 2012 na Machi 30, 2016 maeneo ya Dar es salaam akiwa mwajiriwa wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu (kifahari) yenye thamani ya Sh.milioni 333.2 tofauti na kipato chake.

MBWANA SAMATTA AWAPONGEZA SERENGETI BOYS KWA KUTWAA UBINGWA WA CECAFA, ATOA NENO KWA TFF

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa kulipwa wa Tanzania anayekipiga GRC Genk ya nchini Ubelgiji Mbwana Ally Samatta amewapongeza wachezaji wa kikosi cha chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' kwa kunyakua ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Challenge Cup.

Michuano hiyo imefanyika nchini Burundi kwa kuzikutanisha timu za Afrika Mashariki na Kati ambapo kikosi hicho kimerudi na taji nchini.Samatta kupitia ukurasa wake wa Twitter Samatta amewapongeza wachezaji hao kwa kushinda michezo yote mpaka kufikia  hatua ya fainali na kuwafunga timu ya Somalia kwenye mchezo wa fainali.

Pia Samatta amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa na mipango endelevu kwa ajili ya vijana hao  wanaojiandaa na fainali za Mataifa Afrika (AFCON) chini ya miaka 17 yanayotarajiwa kufanyika hapa nchini mwakani.

Serengeti Boys waliowasili jana jijini Dar es Salaam wakitokea Burundi kulipokua kunafanyika michuano hiyo ya CECAFA ambapo wamepokelewa na  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe sambamba na Rais wa TFF Wallace Karia.

Kwa sasa vijana hao wamepewa mapumziko kwa muda kabla ya kurejea tena kambini kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na michuano ya AFCON wakiwa chini ya Kocha Ammy Ninje. 

INTRODUCING Ommy Dimpoz featuring Seyi Shay - Yanje (Official Music Video)

UBONGO LEARNING YAKABILIANA NA UWEZO WA VIJANA WA KITANZANIA KUPATA AJIRA

$
0
0
Ubongo Learning ambalo ni shirika linaloongoza barani Afrika kwa maudhui ya elimu ya kuburudisha kwa watoto, leo imeandaa mkutano wake wa mwaka ambao ulikuwa na lengo ya kuzungumzia uwezeshwaji kiuchumi, haswa kwa wasichana ambao wanaweza kuathirika zaidi ya wavulana kutokana na mabadiliko katika soko la ajira.

Kwa kipindi cha miezi 6 sasa, Ubongo Learning, shirika lisilo la kibiashara ambalo ndiyo lilibuni katuni za kuelimisha za Ubongo Kids, limekuwa likifanya utafiti juu ya uwezo wa kupata ajira na usimamizi wa fedha miongoni mwa vijana nchini Tanzania. 
 
Lengo la mradi huu, uliofadhiliwa na Data for Local Impact (DLI), ni kuelimisha vijana, haswa wasichana jinsi ya kutumia maelezo, taarifa na takwimu zinazopatikana ili kufanya maamuzi bora juu ya maisha yao ya mbeleni, na zaidi ya hilo kupitia ujuzi wa masala ya kifedha. Vipindi vya televisheni vya Ubongo vinatazamwa na zaidi ya watu milioni 6.4 kila mwezi, hivyo kuvifanya kuwa vipindi vya watoto vyenye watazamaji wengi kuliko vyote Afrika Mashariki na kuwa sehemu nzuri sana kuwasilisha maswala muhimu kwa vijana.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano huo, Meneja Masoko Ubongo Learning Iman Lipumba alisema licha ya kuwa na Maendeleo makubwa ya kuhakikisha wasichana wanaandikishwa shule za msingi, lakini bado jamii nyingi nchini Tanzania bado zinawapendelea wavulana kielimu (hususan kwenye elimu ya shule za sekondari na vyuo vikuu) zaidi ya wasichana.
 
 Zaidi ya hilo, utafiti wetu unaonyesha kuwa wavulana wanashawishiwa zaidi kusoma masomo ya sayansi, hesabu na ukandarasi, taaluma ambazo zinahitajika sana katika soko la ajira, na wasichana wanashauriwa kuingia kwenye masomo ya sanaa na hatimaye kufanya kazi za utoa huduma ambazo huenda zikapotea katika miaka michache ijayo.
 Mwakilishi wa Catholic Relief Service,Priyanka Jagtap, akiwasilisha mada katika mkutano wa mwaka wa Shirika lilisilo la Kiserikali la Ubongo Learning linalojishughulisha na elimu ya kuburudisha watoto. Mkutano huo ulikuwa na lengo ya kuzungumzia uwezeshwaji kiuchumi, haswa kwa wasichana ambao wanaweza kuathirika zaidi ya wavulana  kutokana na mabadiliko katika soko la ajira leo jijini Dar es Salaam
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lilisilo la Kiserikali la Ubongo Learning linalojishughulisha na elimu ya kuburudisha watoto, Nisha Lagon, akiwasilisha mada katika  mkutano wake wa mwaka ambao ulikuwa na lengo ya kuzungumzia uwezeshwaji kiuchumi, haswa kwa wasichana ambao wanaweza kuathirika zaidi ya wavulana  kutokana na mabadiliko katika soko la ajira leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwakilishi wa Catholic Relief Service,Priyanka Jagtap.
Mwakilishi wa BBC Media Action ,Doreen Bangapi,akichangia mada katika katika mkutano wa mwaka wa wadau wa mwaka wa Shirika lilisilo la Kiserikali la Ubongo Learning linalojishughulisha na elimu ya kuburudisha watoto. Mkutano huo ulikuwa na lengo ya kuzungumzia uwezeshwaji kiuchumi, haswa kwa wasichana ambao wanaweza kuathirika zaidi ya wavulana  kutokana na mabadiliko katika soko la ajira leo jijini Dar es Salaam.



 

NI LIVERPOOL AU AS ROMA KUFUZU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA (UEFA CHAMPIONS LEAGUE)

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Mchezo wa Mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kati ya Liverpool ya Uingereza dhidi ya AS Roma ya Italia unatarajiwa kupigwa leo katika dimba la Uwanja wa Stadio Olimpico mjini Rome nchini Italia.

Liverpool ilishinda bao 5 - 2 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Anfield, Roma wataitaji ushindi ule ule walioupata kwenye mchezo wao dhidi FC Barcelona wa bao 3 - 0 katika Robo Fainali ya Michuano hiyo ya Ulaya, ili kufika Fainali pale mjini Kiev, nchini Ukraine.

Ushindi walioupata dhidi ya Chievo Verona, Jumamosi bado unawapa moyo wa kuindosha Liverpool na kufuzu Fainali ya UEFA msimu wa 2017 – 2018.

Liverpool Mabingwa mara ya Tano Michuano ya Ulaya – ni Mafundi wa Mashambulizi ya Kushtukiza (Counterattack) hivyo Roma wanahitaji kucheza mchezo wakushambulia na kuzuia kwa umakini kutafuta magoli.
AS ROMA, wana Wachezaji wao tegemezi, Kiungo Diego Perotti ambaye anasumbuliwa na Kifundo cha Mguu (ankle), Kevin Strootman (rib) wote huenda wakakosekana katika mchezo huo baada ya kuumia katika mchezo wa mkondo wa kwanza. Beki Rick Karsdorp na Mshambuliaji , Gregoire Defrel huenda wakapewa Fatiki.

Kwa upande wa Liverpool, Kiungo Mshambuliaji wa timu hiyo, Adam Lallana amejumuishwa katika Kikosi cha Wachezaji 23 futuatia kusumbuliwa na maumivu ya Nyama za Paja (Hamstring Injury).

Nyota huyo wa Kimataifa wa Uingereza amesafiri na timu hadi Italia ijapokuwa anaonekana hayupo vizuri tangu kutolewa nje katika mchezo dhidi ya Crystal Palace mwezi March.

Lallana alisafirishwa Afrika ya Kusini kwa matibabu mwezi uliopita na Kocha Mkuu wa Liverpool amesema Wiki iliypita kwamba “Mchezo mmoja au miwili huenda akawa vizuri”, lakini hakuna nafasi ya yeye kucheza mchezo dhiidi ya Roma, siku ya leo.

chanzo: Yahoo Sports

Msekwa Apongeza Utendaji wa Rais Magufuli

$
0
0
Jonas Kamaleki-MAELEZO 

Spika wa Bunge mstaafu, Mhe. Pius Msekwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anafanya kazi vizuri katika kuiletea nchi maendeleo hasa kwa kulinda na kusimamia rasilimali . 

Msekwa alisema hayo jana katika mahojiano na shirika moja la utangazaji la kimataifa yaliyofanyika Ukerewe, mkoani Mwanza. 

"Mwenye macho haambiwi tazama, yanayofanywa na Rais Magufuli yanaonekana wazi hata yanatoka kwenye vyombo vya habari badala ya kubaki kwenye kumbukumbu za serikali", alisema Msekwa. 

Kuhusu demokrasia nchini, Msekwa amesema kuwa hali ya demokrasia nchini inaridhisha kwani viongozi muda wao wa kukaa madarakani ukiisha wanaondoka. Wanaominya demokrasia ni wale wanaong'ang'ania madarakani baada ya kipindi chao kuisha, jambo ambalo kwa Serikali ya Tanzania halipo. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani mambo mengi yamebadilika na kuwa bora zaidi. Mfano, nidhamu ya watumishi na uwajibikaji serikalini imeongezeka na hivyo ukiritimba na urasimu umepungua. 

Huduma za Afya zimeboreshwa kwa kujenga na kukarabati hospitali, zahanati na vituo vya afya. Hii pia ni pamoja na upatikanaji wa dawa hospitalini kupitia bohari ya dawa ya serikali (MSD). Kwa kujali afya za Watanzania, Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 39 hadi bilioni 268, jambo ambalo limefafanya upatikanaji wa dawa kuongezeka. 

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images