Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live

SHULE YA KIMATAIFA TANGANYIKA ILIYOPO UPANGA DAR YAWAKUMBUKA WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

0
0

 Na Heri Shaaban
SHULE ya Kimataifa  Tanganyika iliyopo Upanga wilayani Ilala jijini Dar es Salaam imetoa msaada wa nguo kusaidia wananchi waliokumbwa  na mafuriko.
Msaada  huo ulitolewa na Mwasisi wa Shule hiyo Ally Dewji ulipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ofisini kwake leo. 

Akizungumza mara baada kukabidhi msaada huo Dewji amesema shule yao ya Tanganyika inafundisha watoto wa miaka minne hadi 12,mara baada kutokea mafuriko hayo wanafunzi wa shule hiyo waliguswa. 

"Wanafunzi wa shule yetu wameguswa wameungana na Serikali leo tumekabidhi msaada wetu kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, "amesema Dewji. 

Dewji ametaja  vitu walivyotoa ni vyandarua, viatu na nguo .

Kwa upande wake  Mjema ameshukuru msaada huo uliotolewa na Shule hiyo  .

Sophia Mjema alisema katika wilaya yaIlala nyumba 70 na shule moja zote ziliathirika na mvua za masika. 

"Misaada hii itapelekwa kwa familia zilizopata mafuriko zote  kila mtu itamfikia,"amesema Mjema  

na kutoa mwito wa kuwataka wananchi wa mabondeni kuondoka mvua kubwa zinakuja hivyo wasikae katika maeneo hatarishi kwa usalama wao.

Wakati huohuo Taasisi ya Khoja Shia Ishanashari Kamat imekabidhidhi msaada wa sinki kwa ajili ya vyoo mia,Taulo za kike na Biskuti. 

ESRF yaratibu ziara ya wataalamu wa uchumi kutembelea shughuli za wajasiriamali wa SIDO

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji   wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii. (ESRF), Dkt. Tausi  Kida (kushoto) na Profesa Kaushik Basu (katikati), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni inayojishughulisha na uuzaji wa asali , Fredy Swai , wakati wa ziara ya kutembelea Shirika la Uendelezaji Viwanda Vidogo (SIDO),  ili kuona jinsi wajasiriamali wanavyoendesha shughuli zao. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Abubakari Akida)
 Mkurugenzi Mtendaji   wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi  Kida, akimuelekeza jambo Profesa Joseph Stiglitz  wakati wa ziara ya kutembelea Shirika la Uendelezaji Viwanda Vidogo (SIDO),  ili kuona jinsi wajasiriamali wanavyoendesha shughuli zao. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kampuni inayotengeneza bidhaa ya mafuta ya kupaka kwa kutumia malighafi ya mimea, Obed Musiba (kulia), akitoa maelezo juu ya bidhaa zake kwa Mkurugenzi Mtendaji   wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi   Kida (aliyeshika losheni) na Profesa Joseph Stiglitz, wakati wa ziara ya kutembelea Shirika la Uendelezaji Viwanda Vidogo (SIDO), ili kuona jinsi wajasiriamali wanavyoendesha shughuli zao. Ziara hiyo imefanyika  jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji   wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi  Kida (katikati), akiwaongoza wageni kutembelea eneo la Shirika la Uendelezaji Viwanda Vidogo(SIDO), ili kuweza kukagua shughuli za wajasiriamali wanaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.Kulia ni Profesa Kaushik Basu na Kushoto ni Profesa Sabina Alkire, ziara hiyo imefanyika  jijini Dar es Salaam. (Picha na Abubakari Akida)

Habari za UN leo Mei 2, 2018

VOA Swahili: Duniani Leo Mei 2, 2018

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 02.05.2018

Accreditation of H.E. George Kahema Madafa as High Commissioner of the United Republic of Tanzania to the Republic of Malta

0
0
The High Commissioner of the United Republic of Tanzania H.E. George Kahema Madafa presented the Letters of Credence to Her Excellency, Marie-Louise Coleiro Preca, President of Malta, on 10/04/2018. H.E. High Commissioner Madafa was accompanied by two officers from the Tanzanian Embassy in Rome together with his wife Mrs Esther Bhoke Madafa.
 The High Commissioner of Tanzania H.E. George Kahema Madafa presenting his credentials to the President of Malta, H.E. Marie-Louise Coleiro Preca at the Presidential Palace.
 H.E. President of Malta Marie-Louise Coleiro Preca and H.E. High Commissioner Madafa in a brief discussion after presentation of credentials.
 The diplomats from both sides in a short discussion following the event at the Presidential Palace.
 H.E. High Commissioner George Kahema Madafa signing visitor’s book.
 A group picture at the end of the ceremony at the Palace in Valleta.




RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA KILOLO, ATEMBELEA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA UALIMU CHA MKWAWA MJINI IRINGA

0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akipatiwa maelezo kutoka kwa msimamizi wa ukandarasi wa TBA  juu ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo leo Mei 2, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akipiga makofi baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la  ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa leo Mei 2, 2018*

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana  na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah  kwenye sherehe ya kuweka jiwe la  la msingi la  ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa leo Mei 2, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa  mkoani Iringa alipotembelea leo Mei 2, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zwadi kutoa kwa Rasi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa  mkoani Iringa alipotembelea leo Mei 2, 2018. Kulia ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Profesa Bonaventure Rutinwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya  wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa  mkoani Iringa alipotembelea leo Mei 2, 2018.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI AWAANDALIA CHAKULA CHA JIONI WAZEE WA IRINGA, VIONGOZI WA DINI NA SIASA, TUCTA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakaribisha wazee wa Kihehe kwenye hafla ya chakula cha jioni aliyowaandalia wao pamoja na viongozi wa dini, siasa na wa TUCTA katika Ikulu ndogo ya mjini Iringa usiku wa Mei Mosi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza Naibu Chifu wa Wahehe Gerald Malangalila akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakielezea historia ya Iringa katika hafla hiyo
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahigaakisimulia  historia ya machifuIringa katika hafla hiyo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakaribisha wazee wa Kihehe kujipatia  chakula cha jioni aliyowaandalia wao pamoja na viongozi wa dini, siasa na wa TUCTA katika Ikulu ndogo ya mjini Iringa usiku wa Mei Mosi
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wageni wengine wakimsikikiza Mbunge wa Iringa mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mch. Peter Msigwa akiongea machache wakati wa hafla hiyo ya  chakula cha jioni  Ikulu ndogo ya mjini Iringa usiku wa Mei Mosi

Madiwani wa kata mbalimbali za mji wa Iringa waliohamia CCM kutoka CHADEMA wakijitambulisha kwenye hafla hiyo. Picha na IKULU

Mkongwe Ndimara ataka serikali kutopewa sababu ya ‘kubana’ waandishi wa habari

0
0
Na Mwandishi wetu, Dodoma
WAANDISHI wa habari wanapaswa kuandika na kutangaza habari zao kwa weledi na kuzingatia maadili ili kuepuka kuandika habari zinazoipa serikali sababu ya kufungia vyombo vyao.
Kauli hiyo imetolewa mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania Bw. Ndimara Tegambwage wakati akitoa mada ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania kwenye kongamano la maadhimisho ya siku ya Uhuru Wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo nchini Tanzania yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Kila Mei 2-3 kila mwaka ni siku za kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani.
Aidha katika mada yake hiyo Ndimara alisema Serikali barani Afrika zimekuwa zikikosa uvumilivu na kunyima uhuru vyombo vya habari licha ya kuwa uhuru huo unatambuliwa na katiba za mataifa ya Afrika.
Bw. Ndimara amebainisha kuwa, wakati serikali za Africa zikitoa haki ya kusajili vyombo vya habari hususani Radio, Runinga na Magazeti, serikali zinapokosolewa huvifungia vyombo hivyo kwa tuhuma za kukiuka maadili jambo ambalo alidai kuwa si la ukweli.
Mkongwe huyo wa tasnia ya habari nchini Tanzania amebainisha kuwa serikali nyingi barani Afrika zimekosa uvumilivu na kutumia nguvu nyingi kunyamanzisha wanahabari.
Huku akinukuu hotuba ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai ambaye ameonya kuwepo kwa wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya aliwataka waandishi wa habari kuwa makini kutokana na sheria mbalimbali zinazowazunguka zinaohitaji weledi wa hali ya juu katika kuhabarisha.
Awali akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania, Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema Tanzania inautambua mchango wa vyombo vya habari katika kurahisisha mawasiliano ya jamii na kuharakisha maendeleo lakini inakwazwa na kuwepo kwa baadhi ya vyombo vya habari na wanahabari ambao huandika habari nyingi za kutungwa na za uongozi.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akifungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit akitoa salamu za Unesco wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai kufungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumzia malengo ya maendeleo endelevu na jukumu la waandishi wa habari kutumia nafasi zao kutoa taarifa kuhusu malengo hayo kwa jamii ili yatekelezeke kwa urahisi, katika kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari na Mkufunzi wa kujitegemea, Rose Haji Mwalimu akiongoza mjadala kuhusu mada: Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana inatendeka wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mwandishi wa Habari Nguli, Ndimara Tegambwage na mwezeshaji wa mada inayohusu; Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana inatendeka: wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Wakili na Mwandishi wa Habari ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, James Marenga akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Nashera jijini Dodoma.
 Mdau wa Habari Ernest Sungura akishiriki kuchangia maoni katika mjadala uliowasilishwa na mwandishi nguli Ndimara Tegambwage (hayupo pichani) wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege (kulia) na Mshauri wa Utawala Bora na Haki za Binadamu wa Ubalozi wa Sweden nchini, Anette Widholm Bolme wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Pichani juu na chini Sehemu ya washiriki ambao ni wahariri, waandishi wa habari, wadau wa tasnia ya habari na wageni waalikwa waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wakiwemo wahariri, wadau wa habari na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa habari na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, Ubalozi wa Umoja wa Ulaya pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari vya kijamii waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS MAGUFULI,MBUNGE MAVUNDE NA DC NDEJEMBI WATIMIZA AHADI YAO YA KUCHANGIA SHULE YA MSINGI VEYULA-JIJINI DODOMA

0
0
Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli jana amewasilisha mchango wake wa  10,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Veyula iliyopo Jijini Dodoma ikiwa ni ahadi aliyoitoa kwa wananchi  wakati aliposimama kuwasilimia akitokea katika hafla ya Ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati.

Mchango huo umewasilishwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Deogratious Ndejembi ambaye pia amechangia Tsh 1,000,000 kutimiza ahadi yake na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kuanza kuchimba Msingi wa ujenzi wa madarasa na kutumia fursa hiyo kuwataka watendaji wote kusimamia zoezi la ujenzi kwa ufanisi na kumwagiza Lt Col Matina Mkuu wa Kikosi cha JKT Makutupora kusimamia ukamilishwaji wa ujenzi wa madarasa hayo ndani ya wiki tatu.

Aidha,Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Mavunde na DC Ndejembi waliungana na wananchi katika zoezi la uchimbaji msingi na baadaye Mh Mavunde alikabidhi kiasi cha Tsh 5,000,000  mifuko ya Saruji 100 na kuahidi kuongeza Tsh 5,000,000 ya ziada mapema wiki ijayo ikiwa ni mchango kutoka kwa marafiki wa Mbunge huyo,na pia alitumia fursa hiyo kumshukuru Mh Rais kwa kusaidia ujenzi wa madarasa hayo.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amewahakikishia wananchi kwamba Halmashauri ya Jiji la Dodoma italipia vifaa na gharama zote za kupaua madarasa hayo ikiwa ni sehemu ya mchango wa Jiji.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki kuchimba msingi wa ujenzi wa madarasa shule ya msingi Veyula.
 Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki kuchimba msingi wa ujenzi wa madarasa shule ya msingi Veyula pamoja na wananchi.
 Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akimkabidhi fedha Kaimu Mkuu wa wilaya wa Dodoma Deogratias Ndejembi ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Veyula(katikati) ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akimkabidhi saruji Kaimu Mkuu wa wilaya wa Dodoma Deogratias Ndejembi ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Veyula.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki ushushaji mifuko ya saruji.

MZEE MAJUTO KUELEKEA INDIA KWA MATIBABU SIKU YA IJUMAA

NEW PROPERTY AVAILABLE FOR IMMEDIATE LEASE

0
0
New Property available for immediate lease at UDOE HOUSE is a spacious new building located on plot no 30 block 61 at UDOE Street, Kariakoo, Ilala - Dar es Salaam.

UDOE House is a brand new property with 8 floors whereby each floor comes with 2 units of 3 bedroom apartments, each unit has a master bedroom, balconies, store, kitchen and large living room. The living room of Master bedroom comes with Air condition anemity.
Each apartment has 79 square metres, There is 16 apartment units in the building, Ground floor has area space of 82 square metres.

Looking for potential leaser for different business purposes such as banks, hospital, schools, religious communities, even if it will include alterations on the property.

For serious inquiries please contact +255713 465 336 or +255713 272 203.

DC KIGAMBONI AWAONDOLEA TAHARUKI WANANCHI WA KIBADA KUBOLEWA NYUMBA ZAO

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa ameondoa hali ya taharuki iliyokuwa imetanda miongoni mwa wananchi wa Kata ya Kibada waliowekewa alama ya kubomoa majengo yao na  wakala wa barabara (TANROADS) mbali na kununua viwanja hivyo kihalali kutoka wizara ya ardhi.


Akizungumza na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye ofisi za Kata ya Kibada Mh.Mgandilwa amesema kuwa ofisi yake na wataalamu hawapo tayari kuona wananchi wao wanaonewa.


Aliongeza kuwa mgongano huo umebainika kwenye mradi wa ujenzi wa barabara uliopo kwenye hatua za awali na ubainishaji wa mipaka wa Tanroads unaolenga kujenga barabara kiwango cha lami kuanzia Kibada-Somangila hadi Kimbiji.


Mgandilwa alisema kuwa wizara ya ardhi ilikuwa na mradi wa viwanja ishirini elfu vilivyouzwa kwa wananchi kihalali ambapo baada ya Tanroads kubainisha mipaka yake ndipo ilipobainika kuwa wizara ya ardhi iliuza viwanja vyake hadi kwenye hifadhi ya barabara.


"Viwanja hivi vilinunuliwa wizara ya ardhi ambapo wananchi walikuwa na uhakika wa usalama wa viwanja vyao kutokana na kununua kwene wizara husika, leo hii kuja kuwawekea alama ya kubomoa sio haki, mwananchi anakuwa anawajibishwa kwa kosa ambalo si lake ndiomaana tumekutana hapa ili tuweze kuona namna gani tunaweza kufikia muafaka" Alisema Mkuu wa Wilaya.


Aliongeza kuwa wao kama Serikali wameona ni bora kuzungumza na wananchi  kwasababu Serikali haipaswi kukinzana na sheria badala yake inaangalia mahali ambapo pamekosewa na kurekebisha.


Aidha Mkuu wa Wilaya aliwataka wananchi wote waliowekea alama za kubomoa majengo yao ndani ya siku 90 kufika ofisini kwake siku ya jumamosi tarehe 5/5/2018 ambapo kutakuwa na wataalamu kutoka wizara ya Ardhi na Tanroads ili kuona namna bora ya kufikia muafaka.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa akisistiza kuwa Sheria itafuatwa kuhakikisha wananchi wanapata haki yao.
 Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa na wananchi wa kibada wakisoma ra,mani ili kubaini mipaka .
 Diwani wa Kata ya Kibada Mh.Amin Sambo  akishiriki kuchimba eneo linalodaiwa kuwa na jiwe la mpaka kwenye eneo la mkazi wa Kibada wakati walipokuwa wakitafuta mawe ya Mipaka.
 Kamati ya ulinzi na usalama na waanchi wakizulu kwenye moja ya nyumba iliyowekwa alama ya kubomoa na wakala wa barabara Tanroads ili kubaini mpaka uliopo.
  Mthamini wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Mpoki Daimon  akifafanua taratibu za uthamini na ulipwaji fidia kwa wananchi wa Kata ya Somangila Mtaa wa Dege.
Baadhi ya wananchi na wataalamu mbalimbali  walishirki kwenye mkutano huo wa hadhara Kibada.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

GGM na TACAIDS kuzindua Kilimanjaro Challenge 2018

0
0
Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inatarajia kuzindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2018), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. Shughuli hii inatarajiwa kufanyika tarehe 4 Mei 2018 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambapo atafanya zozezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka mwaka jana 2017 zilizopatikana baada ya wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro .

Kilimanjaro Challenge against HIV & AIDS ni mfuko unachangia juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU).

Kilimanjaro Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.

Mfuko huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro.Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 % mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa zoezi la upandaji wa Mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2018), litakalo kwenda sambamba na kuendesha harambee kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya kusaidia mapambano ya kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI nchini. Kulia ni Makamu wa Rais miradi endelevu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo. 
Makamu wa Rais miradi endelevu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa zoezi la upandaji wa Mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2018), litakalo kwenda sambamba na kuendesha harambee kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya kusaidia mapambano ya kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko.
Watendaji wa MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wakijadili jambo mara baada ya kumaliza mkuatano wa waandishi wa habari mapema jana  
Watendaji wa MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkuatano wa waandishi wa habari mapema  jana.


WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI KUWASILI NCHINI LEO

0
0

Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Mhe. Heiko Maas anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini tarehe 03 na 04 Mei, 2018. 

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Ujerumani na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano. Waziri huyo atakuja nchini kwa ndege binafsi akiambatana na ujumbe wa watu hamsini (50). 

Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri huyo nchini Tanzania na Barani Afrika tangu ateuliwe tarehe 14 Machi, 2018 kwenye wadhifa wa sasa kutoka kwenye wadhifa aliokuwa nao awali wa Waziri wa Sheria. Kwenye ziara yake hii ya awali Barani Afrika, atatembelea nchi mbili tu ambazo ni Tanzania na Ethiopia ambayo ni Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (Afican Union). Hii inadhihirisha dhamira ya Ujerumani na hasa Waziri huyo mpya wa Mambo ya Nje kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Tanzania.

Wakati wa ziara hiyo nchini, Mhe. Maas ataonana kwa mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na baadaye kwa pamoja watakutana na vyombo vya habari kuelezea madhumuni ya ziara ya Waziri huyo nchini.

Aidha, tarehe o4 Mei, 2018, Mhe. Waziri Maas anatarajiwa kuweka shada la maua kwenye Mnara wa Askari (Askari Monument) Jijini Dar es Salaam pamoja na kutembelea Shule ya Sekondari ya Majaribio ya Chang’ombe. 

Siku hiyo hiyo, Mhe. Maas ataondoka Dar es Salaam kuelekea Arusha. Akiwa Arusha Mhe. Waziri Maas atakutana na viongozi wa Mahakama ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (United Nations Mechanism for International Criminal Tribiunals-MICT) na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (African Court on Human and Peoples’ Rights). Pamoja na kutembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Tanzania na Ujerumani zimekuwa na mahusiano mazuri na ya muda mrefu na Tanzania ni kati ya nchi zinazoongoza kwa kunufaika na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwenye nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tangu kuanza kwa mahusiano kati ya nchi hizi mbili, Ujerumani imekuwa ikiisadia Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo afya, elimu, miundombinu, nishati mbadala, mapambano dhidi ya vitendo vya ujangili na uwindaji haramu.

Mhe. Maas ataondoka nchini tarehe 04 Mei, 2018 kurejea Ujerumani.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dar es Salaam, 02 Mei, 2018

TRA ZANZIBAR YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI

0
0
  Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Afisi ya Zanzibar Abdallah Seif akiwasilisha mada ya Sheria za Kodi zinazoisimamiwa na Mamlaka hiyo katika mafunzo ya waandishi wa Habari ya kuwajengea uelewa wa Kodi yaliyofanyika Taasisi ya Utalii ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Maruhubi.
 Waandishi wa Habari walioshiriki mafunzo ya Sheria za Kodi zinazosimamiwa na TRA wakimsikiliza Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi wa Mamlaka hiyo (hayupo pichani) yaliyofanyika  Taasisi ya Utalii ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Maruhubi Mjini Mjini Zanzibar.
 Meneja Msaidizi wa Ukaguzi wa Kodi wa TRA Afisi ya Zanzibar Mbarouk Khalid Ussi akijibu masuala ya waandishi wa Habari katika mafunzo ya kuwajengea uelewa wa Sheria za Kodi zinazosimamiwa na Mamlaka hiyo katika Ukumbi wa Taasisi ya Utalii ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Maruhubi. PICHA NA RAMADHANI ALI - MAELEZO ZANZIBA

KALEMANI, MGALU WAONGOZA KIKAO CHA MAJADILIANO YA MAENDELEO MRADI WA LNG

0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu Waziri Subira Mgalu wameongoza kikao kilichojadili maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG).
Kikao hicho kilifanyika Aprili 30 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kushirikisha Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na wataalamu kutoka wizarani.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiongoza kikao kujadili maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG), kilichofanyika Aprili 30 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri Subira Mgalu.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Naibu Waziri Subira Mgalu (kushoto), wakiongoza kikao kujadili maendeleo ya Mradi wa Gesi ya Kusindikwa (LNG), kilichofanyika Aprili 30 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Wengine pichani ni Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi, wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, wajumbe kutoka TPD, EWURA na PURA.

 
 Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na  wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, wakiwa katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akisalimiana na Mabalozi wa nchi za Norway, Uingereza na Uholanzi pamoja na  wawakilishi wa Kampuni mbalimbali za utafutaji wa mafuta kwa ajili ya Mradi wa LNG, muda mfupi kabla ya kuanza kikao baina yao kujadili maendeleo ya Mradi huo.

WADAU WA MASUALA YA JINSIA WAENDELEZA MAJADILIANO KATIKA UANDAAJI WA KITINI CHA MASUALA YA JINSIA

0
0
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mboni Mgaza akifafanua jambo kuhusu masuala ya kijinsia  kwa wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika  kikao cha  kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa Mwaka 2017/18-2021/22 kinachoendelea mjini Morogoro leo Mei 03, 2018.
 Mwezeshaji wa Kikao Bw.Clarence Kipobota akitoa mwelekeo wa uaandaaji  wa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” katika mchakato wa kuandaa kitini hicho kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa Mwaka 2017/18-2021/22 katika kikao kati ya Serikali na wadau kinachoendelea  mjini Morogoro leo Mei 03,2018 .
 Mwakilishi wa AMREF Health Africa Bi. Sophia Kimaro akitoa maoni kuhusu uboreshaji wa kitini maalaum cha masuala ya Jinsia “Gender Module” katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika kuandaa kitini hicho kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa Mwaka 2017/18-2021/22 kinachoendelea mjini Morogoro leo Mei 03,2018.
 Mwakilishi wa TGNP Mtandao Bi. Agnes Lukanga akitoa maoni kuhusu kuzingatia masuala ya unyanyasaji kwa jinsi zote  katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa Mwaka 2017/18-2021/22 kinachoendelea mjini Morogoro leo Mei 03,2018.
 Mchumi kutoka Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Seto Ojwando akitoa maoni kuhusu uzingatiwa wa masuala ya Kisera katika uaandaji wa kitini maalum cha masuala ya Jinsia “Gender Module” katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika kuandaa kitini hicho kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa Mwaka 2017/18-2021/22 kinachoendelea mjini Morogoro leo Mei 03,2018.

 Baadhi ya wadau na wataalamu wa masuala ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha wataalam na wadau wa maendeleo ya Jinsia katika kuandaa kitini cha kufundishia masuala ya Jinsia “Gender Module” kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa Mwaka 2017/18-2021/22 kinachoendelea mjini Morogoro leo Mei 03, 2018.
 Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

WANAHABARI KIGOMA WAHIMIZWA KUZINGATIA WELEDI, KUONGEZA UBUNIFU ILI KUCHOCHEA MAENDELEO

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WANAHABARI mkoani Kigoma wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuongeza ubunifu katika kazi zao ili kuchochea maendeleo ya mkoa huo.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo amesema uandishi wa habari za matukio umepitwa na wakati kama waandishi wenye taaaluma wanatakiwa kutumia kalamu zao kuandika habari zenye ubunifu na weledi mkubwa kwa kutafuta undani wa habari wanazo ziandika. 
Aidha amewataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuwashawishi vijana wadogo kuipenda fani ya uandishi wa habari, kwa kuwatembelea wanafunzi shuleni na kutoa elimu kuhusu fani hiyo ili kuepukana na fani hiyo kuonekana wanaoingia huko ni wale wanaoshindwa kutimiza ndoto zao kwakuwa fani hiyo ni sawa na Fani zingine.

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoani wa Kigoma (KGPC)Adela Madyane amesema chama cha waandishi wa habari kina mpango wa kuwaunganisha waandishi wa habari wote mkoani Kigoma ili kuhakikisha wanakuwa na maadili na kuzingatia misingi ya uandishi wa habari.

Amesema Chama hicho kinaendelea kusimamia misingi na taratibu za kitaaluma zilizowekwa kisheria ilikuondoa migogoro baina ya Wanahabari na wadau wa maendeleo, na wanachama wenye vigezo ili kuepuka waandishi wasio na taaluma .
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waandishi wa habari mkoani wa Kigoma.

Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma Fadhili Abdallah amesema kama waandishi wa habari watahakikisha wanashirikiana na wananchi na viongozi kuhakikisha wanaripoti habari zenye tija na maendeleo kwa ajili ya kuuinua mkoa wa Kigoma.

Amesema changamoto wanazokutana nazo kama Waandishi wa habari ni pamoja na baadhi ya viongozi na wadau kuzuia baadhi ya taarifa na kuwanyima ushirikiano Waaandishi pindi wanapo hitaji taarifa na kuomba Viongozi wote kutoa ushirikiano kwakuwa Waandishi wa habari wana mchango Mkubwa wa Kuinua maendeleo hasa katika mikoa ambayo bado iko nyuma.
Pica ya pamoja

UPELELEZI KESI KIGOGO WA TPA ANAYEDAIWA KUJILIMBIKIZA MALI ZA BILIONI 1.4/- BADO HAUJAKAMILIKA, APATA DHAMANA

0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ,imeelezwa upelelezi wa kesi ya kujilimbikizia mali zenye thamani ya Sh.bilioni 1.4  zisizolingana na kipato chake halali inayomkabili Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,(TPA), Prosper Kimaro bado haujakamilika.

Taatifa hiyo imeelezwa leo mahakamani hapo na Wakili wa Serikali  Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ambapo  kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Kutokana na taarifa hiyo, ksi hiyo imeahirishwa hadi Juni 5 mwaka huu na kuutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi. Mshtakiwa huyo anashtakiwa  chini ya kifungu cha 27 (1)(4) cha sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kimaro anadaiwa kumiliki nyumba zenye thamani ya Sh.1,178,370,334,  na magari  yenye thamani Sh 307,364,678.20, zisizolingana na kipato chake ambapo anadaiwa ametenda kosa hilo kati ya mwaka 2012 na 2016.

Alidai mshtakiwa  akiwa maeneo ya Temeke  na mtumishi wa umma wa TPA kama Meneja wa Fedha, amekutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake halali cha zamani na  cha sasa.

Mali hizo ni nyumba mbili  zilizopo mtaa wa Uwazi Temeke zenye thamani ya Sh.milioni 124.2,  kiwanja kilichopo Yombo Vituka chenye thamani ya Sh.milioni 12.9 . Nyumba   mbili  zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh.milioni 63.5, nyumba tatu zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh.milioni  159.

 Nyumba nyingine tatu zenye thamani ya Sh.milioni  170.1,  nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.milioni   71.3.kiwanja  kilichopo Temeke chenye thamani ya Sh.milioni  35.Pia kiwanja chenye thamani ya Sh.milioni 25 na amejenga nyumba tatu ambazo zinathamani ya Sh.milioni  159 pamoja na  nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.milioni 106.Nyumba zenye thamani ya Sh.milioni  214,  nyumba  nne eneo la Viziwaziwa Kibaha Mjini zenye thamani ya Sh.milioni 199.7 na nyumba nyingine iliyopo Kilimahewa Tandika yenye thamani ya Sh.milioni 70.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa pia anamiliki magari aina ya Toyota Land cruise lenye thamani ya Sh.milioni 180.1,  Mitsubishi lenye thamani ya Sh.milioni 38.4,  Massey Ferguson lenye thamani ya Sh.milioni  24 na Trailer lenye thamani ya Sh.milioni  4.5.
Mengine ni  Toyota Harrier yenye thamani ya Sh.milioni  35.8,  Trailer lenye thamani ya Sh.milioni 4.8,  na Massey Ferguson lenye lenye thamani ya Sh.milioni 19.1.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa  huyo alikana shtaka  na yupo nje kwa dhamana. Hiyo ni baada ya kukamilisha masharti ya  kuwa na wadhamini wawili ambao kila mdhamini  awasilishe hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh.milioni 200.

Pia alimtaka mshtakiwa huyo  asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama na mshtakiwa awasilishe hati zake za kisafiria mahakamani.
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live




Latest Images