Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

BAADA YA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA KUKAMILIKA (NFRA) ITAKUWA NA UWEZO WA KUHIFADHI TANI 501,000

$
0
0
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akitoa taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi huo Mtaa wa Relini-Kizota Mjini Dodoma, Jana 21 Aprili 2018. Picha Na Mathias Canal-NRFA

Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma

Hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini inazidi kuimarika huku serikali kupitia wizara ya kilimo ikiwa imejipanga kukabiliana na changamoto ya uchache wa maghala ya kuhifadhia mazao mbalimbali hususani mahindi.

Katika taarifa ya Bi Vumilia L. Zikankuba Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula katika hafla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa vihenge na maghala ya kisasa katika Mtaa wa Relini-Kizota Mjini Dodoma aliyoitoa mbele ya mgeni rasmi-Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) jana tarehe 21 aprili, 2018 alieleza kuwa mradi huo pindi utakapokamilika utafungua fursa kubwa kwa wakulima nchini.

Alisema kuwa Baada ya Mradi huu kukamilika uwezo wa kuhifadhi wa Wakala wa Taifa wa Kuhifadhi Chakula utakuwa mara mbili ya uwezo wa sasa yaani kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000 huku ikitarajiwa kufikia Tani 700,000 kufikia mwaka 2025.

Bi Vumilia alieleza kuwa Mikataba ya mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula, ilisainiwa na kuanza kazi tarehe 09 Desemba 2017 kati ya (NFRA) na makampuni mawili toka nchini Poland ambayo ni Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o. Aidha, mradi huo utatekelezwa kwa gharama ya Dola za kimarekani milioni 55 na unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi kumi na nane (18) kuanzia mwezi Mei 2018.

Maandalizi ya awali ya mradi huo yalifanywa na kampuni kutoka nchini Poland iliyofanya upembuzi yakinifu wa awali na kupendekeza gharama za mradi kuwa dola za kimarekani millioni 55 ambazo zingetosheleza kujenga vihenge vyenye uwezo wa Tani 150,000 na maghala yenye uwezo wa Tani 50,000, hivyo kufanya uwezo wa jumla wa mradi kuwa Tani 200,000.

Alisema, ili kujiridhisha zaidi Wakala kupitia Wizara mama, iliunda timu ambayo ilifanya upya tathmini ya mradi na kupata thamani halisi ya mradi (value for money) ili kuleta ushindani katika utekelezaji wa mradi kwa kushirikisha timu ya Wataalamu wa ndani. 

Timu hiyo iliundwa na Wahandisi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandisi na Wataalamu wa mazingira kutoka TBA pamoja na Mhandisi toka Wizara ya Kilimo. Hivyo timu hiyo ilifanya upya kazi ya usanifu wa msingi, kuandaa makadirio ya gharama za mradi, na kuandaa makabrasha ya zabuni ili kutimiza azma mbili nilizotangulia kuzitaja hapo awali. 

Matokeo ya jumla ya kazi hiyo, yalibainisha kuwa kiasi cha fedha Dola milioni 55 kinatosheleza ujenzi wa vihenge vya kisasa vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 190,000, na maghala Tani 60,000 hivyo kufanya ongezeko la hifadhi ya Tani 50,000. 

Aidha, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula unamiliki maghala ya kuhifadhi nafaka 34 yenye uwezo wa jumla ya Tani 251,000. Uwezo huu wa sasa wa maghala hautoshelezi mahitaji ya dharula ya chakula kwa mfululizo wa miezi mitatu kwa akiba isiyo pungua Tani 700,000, hivyo kupelekea uhitaji wa kuongeza uwezo wa uhifadhi.

KAOLE SNAKE PARK YAIPIGA TAFU UMISETA NA UMITASHUMITA BAGAMOYO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kaole Snake Park, Kauthar Kihuhe(kushoto) akikabidhi msaada wa Jezi kwa Kaimu Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo, Danny Mporere zenye thamani ya Shilingi milioni moja na laki mbili(1200,000) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika kituo hicho cha utalii wa ndani kilichopo Bagamoyo mwishoni mwa wiki.Kulia ni Afisa Utamaduni Wilaya ya Bagamoyo, Stellah Moshi na Afisa michezo Wilaya ya Bagamoyo, Vedastus Mziba
KITUO cha Utalii wa ndani cha Kaole Snake Park kilichopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani kimetoa msaada wa jezi kwa kambi za Umoja wa Shule za Sekondari Bagamoyo(UMISETA) na Umoja wa Shule za Msingi Bagamoyo(UMITASHUMITA) ambazo ziko kambini zikijiandaa na masindano ya Wilaya kuelekea Mkoa wa Pwani vyote vyenye thamani ya Shilingi milioni moja na laki mbili (1200,000).

Akizungumza wakati wa makabidhiano Mkurugenzi Mtendaji wa Kaole Snake Park, Kauthar Kiguhe alisema Kaule ni wadau wa michezo na kwakutambua thamani ya michezo wamewiwa kutoa msaada huo ili kuleta hamasa kwa vijana waweze kufanya vizuri zaidi tukitambua michezo ni afya, michezo ni kufahamiana lakini michezo hiyo inaweza kuwa ajira kwa vijana hapo baadae mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Alisema Kiguhe, wao kama Kaole wataendelea kusaidia Sekta ya Elimu pale watakapokuwa wananguvu ambapo pia alitoa wito kwa waalimu walipokea msaada huo wawapeleke katika Kituo hicho cha Kaole Snake Park wajue utalii wa ndani unaofanywa na Kaole Snake Park ili wakiulizwa kilichoandikwa kwenye Jezi hozo waweze kuelezea vizuri.
Nae Kaimu Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo, Danny Mporere ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo alishukuru sana msaada huo na kuahidi kuitangaza Kaole Snake Park jinsi inavyjikita katika kutangaza Utalii wa ndani, lakini pia aliahidi kabla ya walengwa wa msaada huo kuanza kuzitumia jezi hizo alisema atawapeleka Wanafunzi kujionea kuifahamu Kaole Snake Park ni nini na inafanya nini.

Mwisho Afisa Michezo wa Wilaya ya Bagamoyo nae alishukuru sana msaada huo kwani umetolewa wakati muafaka timu ziko Kambini kuelekea mashindano ya Wilaya ya kuunda timu ya Wilaya kuelekea Mkoa.

MASHINDANO YA OLIMPIKI 2020 NCHINI JAPAN KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA - DK. KIGWANGALLA

$
0
0



Na Hamza Temba-Ngorongoro, Arusha

Mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika nchini Japan mwaka 2020 yatatumika kunadi vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia timu ya Taifa ya riadha na banda la maonesho ya utalii.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kukamilika kwa mashindano ya riadha ya Ngorongoro Marathon 2018 katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana.

Dkt. Kigwangalla alitoa kauli hiyo wakati akijibu ombi la Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka ambaye aliiomba wizara yake kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kusaidia maandalizi ya timu ya Taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo.

Mtaka pia aliomba Mamlaka hiyo itumie timu ya Taifa ya riadha Tanzania kama mabalozi wao wa kutangaza vivutio vya utalii vya hifadhi hiyo ya Ngorongoro ndani na nje ya nchi.
Washiriki wa mbio hizo kutoka Tanzania na Kenya wakitimua mbio kuanza mashindano hayo ya Ngorongoro Marathon 2018 umbali wa Kilomita 21 mjini Karatu mkoani Arusha. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya watalii nao walitumia fursa hiyo kusaka medali.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihitimisha mbio za kilomita 21 za mashindano ya Ngorongoro Marathon 2018 yaliyofanyika katika mji wa Karatu mkoani Arusha jana. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akionesha medali aliyopewa pamoja na washiriki wengine wa mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 yaliyofanyika mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKAZI DAR AMLILIA RC MAKONDA AMSAIDIE KUPATA NYUMBA YAKE AMBAYO ANADAI AMEDHULUMIWA

$
0
0

Na Emmanul Masaka ,Globu ya jamii

MKAZI wa Mnazi Mmoja barabara ya Sukuma na Mafya jijini Dar es Salaam Wechu Salumu Abdallah amempigia magoti Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda ili amsaidie nyumba yake kwani amedai amedhulumiwa na kupigwa mnada .

Akizungumza na waandishi wa habari Wechu Abdallah amesema anamwomba Mkuu wa Mkoa asikie kilio chake kwani amedhulumiwa nyumba ambayo ni ya urithi,waliyoaachiwa ambapo wapo ndugu wanne wanaimiliki nyumba hiyo.

Amesema nyumba hiyo ya urithi amedhulumiwa na mtu (amemtaja kwa jina)mbaye amemtaja jina(nayefahamika kwa jina)ambaye anaminayo kampuni na alikubaliana naye kujenga ghoropha 8 ambazo wangegawana.

Amesema lakini baadae amegeuka na kuchukua nyumba hiyo na kuipiga mnada ambapo ametakiwa kuweka zuio kwa siku 14 tu."Mkuu wa mkoa naomba unisaidie mimi mnyonge nimeachiwa watoto nawahudumia hakuna anayenisaidia, hivyo nakuomba mkuu wa mkoa wangu unisaidie nipate haki," amesema

Ameeleza yeye pamoja na ndugu zake hao walioachiwa nyumba hiyo walikubali kuwa mjenzi huyo ajenge ghorofa hizo 8 ambapo wangegawana 4 kwa 4 na kutokana na makubaliano hayo walifuata misingi yote ya sheria na wakaandikishana kwa makubaliano ya kujenga ghorofa.Amendelea kueleza mmoja wa mrithi wa mali hizo aliamua kuondoka kwenye mkataba na kutaka apewe gawio la fedha zake ambazo ni takribani ya Sh.milioni 7.6 ambapo walimweleza mjenzi wao na kukubali kumpatika kasi hicho cha fedha wakaandikishiana na wakampatia kiasi cha fedha hizo lakini dada yao huyo alitaka kuongezewa.

Amesema wamwambia kuwa anataka kuongezewa hivyo wakaenda mahakamani na kuhakikisha wakafanya makubaliano ambapo mjenzi huyo aliwapatia fedha hizo na kumpatia dada yao,na baada ya hapo walitakiwa kumwondoa katika makubaliano.Aidha mama huyu amemwomba Makonda kumsaidia kwani nyumba hiyo tayari imeuzwa na mnada ulifanyika bila ya matangazo yoyote na wakati kesi bado uko mahakamani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Baragashi Azimio amesema ni kweli nyumba hiyo imepigwa mnada na watu waliofika kuleta tangazo ofisini kwake.Hata hivyo imepigwa mnada pasipokuwa na matangazo kwa wananchi wa mtaa huo kuwa nyumba inauzwa .

Nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Sukuma Kariakoo Ilala jijini Dar es Salaam ilipigwa mnada na kuuzwa kwa thamani ya Sh. milioni 350 ambapo walifanya mnada bila ya kumshirikishwa Msimamizi wa mirathi hiyo.
 
Mkazi wa Kariakoo jijini Dar as Salaam,Uwechu  Salumu Abdallah akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amsaidie kutokana na kudhulumiwa nyumba ya urithi.

MBUNGE MAULID MTULIA AKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO KATA ZA MSISIRI A, B, NA KAMBANGWA KINONDONI

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam Maulid Mtulia(CCM), ametembelea maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko ya maji huku akitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi wa jimbo hilo ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine na mvua za masika huku akiishauri Halmashauri Manispaa ya Kinondoni kutafuta suluhu ya kudumu ili wananchi wabaki salama.

Pia amesema mbali ya kutoa pole atatumia fedha za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kukodisha mashine za kunyonya maji pamoja na fedha ya kununua mafuta ili maji ambayo bado yapo kwenye makazi ya wananchi wake yaondolewe huku akitoa katazo la watu wasiendelee kujenga kwenye bwawa la Tengeza wala kutupa taka kwani athari zake ni kubwa kwa wananchi walio wengi.

Mbunge Mtulia amesema hayo jana jimboni kwake Kinondoni baada ya kufanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa ambapo pia ameshuhudia baadhi ya watu kujenga makazi kwenye bwawa la Tengeneza na matokeo yake maji kukosa pakwenda na hivyo kuharibu makazi ya watu.

Pia ametembelea baadhi ya nyumba za wananchi wa maeneo hayo ambapo zaidi ya asilimia 70 ya makazi ya watu yamekumbwa na mafuriko ambapo akatumia nafasi hiyo kuiomba Halmashauri ya Kinondoni kurekebisha mitaro iliyopo ili maji yapite kwa urahisi huku akitoa ombi la kuchimbwa kwa mitaro mikubwa ambayo itakuwa suluhu ya maji kutokwenda kwenye makazi ya watu kama ilivyo sasa.
ms1
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa , mtaa wa Msisiri A Jumanne Mbena akielezea changamoto za mafuriko ambazo zimesababishwa na baadhi ya wananchi kujenga kwenye Bwawa Tengeneza lililopo eneo la Msisiri A kwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akifanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
ms2
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akizungumza wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo am bayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
ms5
Muonekano wa maji yaliyozingira nyumba za wakazi wa Kata za Msisiri A na B na Kambangwa katika jimbo la Kinondoni jijini Dar es salaam.
ms6
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akipita kwa tabu wakati  alipofanya ziara ya kukagua mae neo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika en eo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa
ms8
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CCM),akiangalia moja ya madimbwi yaliyojaa maji mtaani alipo fanya ziara ya kukagua maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika katika eneo la Kata ya Msisiri A,Msisiri B na Kambangwa.

MWILI WA AGNES MASOGANGE ULIVYOAGWA LEO JIJINI DAR

KAIMU MURUGENZI MKUU NIDA AFANYA ZIARA SHINYANGA KUKAGUA MAENDELEO YA ZOEZI LA USAJILI NA UTAMBUZI WA WATU

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Ndg. Andrew W. Msssawe amekutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga na kusisitiza umuhimu wa kukamilisha Usajili wananchi mkoani humo mwezi Mei mwaka huu ili NIDA kupata muda wa kutosha kufanya uhakiki na mapingamizi kwa wale wote waliosajiliwa; na kuwezesha Mamlaka kuzalisha vitambulisho kwa wakati.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga kukagua maendeleo ya zoezi la Usajii na Utambuzi wa Watu linaloendelea; akiwa ameambatana na Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Ndg. Alphonce Malibiche, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi.Rose Mdami na Ndg. Steven Kapesa Mkuu wa Kitengo cha Vihatarishi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo; Katibu Tawala wa Mkoa huo Ndg. Albert Msovela amesema mkoa wa Shinyanga una changamoto kubwa ya wahamiaji haramu hususani Wilaya ya Kahama na kwamba wamejipanga Usajili katika eneo hilo kufanyika kwa uangalifu mkubwa kwa kuhusisha vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.
Viongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kikao na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwasajili wananchi na kumaliza zoezi kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. ,Andrew W. Massawe akiweka saini kwenye kitabu cha wageni, mara alipowasili kwenye ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga. Pembeni ni Katibu Tawala huo Ndg Albert Msovela
Wananchi wa Kijiji cha Usanda Kata ya Tinde mkoani Shinyanga walivyokutwa kwenye foleni ya Usajili Vitambulisho vya Taifa kwenye zoezi linaloendelea mkoani humo wakati wa ziara ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu aliyoifanya hivi karibuni.
Bi. Magdalena E. Ngosha mkazi wa kijiji cha Usanda Kata ya Tinde akichukuliwa alama za vidole na Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea kijijini hapo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Vijana Waaswa Kulinda na Kudumisha Muungano

$
0
0

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Vijana Nchini wametakiwa kulinda na kudumisha Muungano kwa Vitendo kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho ikiwa ni sehemu ya kuonesha uzalendo.

Akizungumza wakati wa Kongamano lililofanyika mkoani Dodoma kuhusu Muungano lililowashirikisha wanafunzi zaidi ya 300 wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba amesema kuwa vijana wanalo jukumu kubwa katika kulinda Muungano na kuudumisha.

“Vijana tunawategemea muwe watetezi na walinzi wa Muungano wetu kwa kuwa huu ni urithi wa Taifa tunawajibika kuulinda na kuudumisha kwa faida ya kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Makamba. Akifafanua Makamba amesema kuwa vijna wanaowajibu wakuonesha uzalendo wao kwa kudumisha Muungano ambao unalitambulisha taifa nje ya mipaka yetu.

Mambo mengine yanayolitambulisha Taifa letu ni Lugha, Mipaka yetu, Historia, Utamaduni wa kisiasa na kijamii.“ Waasisi wa Taifa letu walikuwa na dhamira njema ndio maana waliasisi Muungano wetu na kuweka mipaka mipya ya Taifa letu tofauti na ile ya wakoloni hivyo hili ni jambo la kujivunia” Alisisitiza Mhe. Makamba.

Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuwapuuza wale wote wanaobeza Muungano kwa kuwa hawalitakii mema taifa letu.Kwa upande wake mwanasiasa mkongwe na Waziri (mstaafu) wa baraza la kwanza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Kwanza mara baada ya Uhuru Balozi Job Lusinde akizungumza katika mahojiano maalum mjini Dodoma amewaasa vijana kudumisha Muungano kwa kujifunza historia ya Muungano ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuuenzi.

“Vijana wajitahidi wawe waadilifu kwa kulinda uhuru wetu, umoja wetu na muungano wetu kwa faida ya kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Balozi Lusinde.

Akifafanua Balozi Lusinde amesema vijana wanapaswa kuepuka vitendo vya wizi na ufisadi ili kuchochea maendeleo.Mada zilizotolewa katika Kongamano hilo ni pamoja na Historia na faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mtazamo wa Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

Kongamano kuhusu Muungano limefanyika Mkoani Dodoma ikiwa ni siku chache kabla ya maadhimisho ya siku ya Muungano yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26, 2018 mjini Dodoma, Kongamano hilo limewahusisha wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma, Mipango, CBE, St. John, Chuo cha Madini na Chuo cha Maendeleo Vijijini Hombolo.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba

INTRODUCING "DHAHABU" By KARDINAL J.OTENGA

MKUBWA NA WANAWE PRESENTS "SOKOMOKO" BY MNW CREW

MICHUZI TV ONE2ONE: ALIKIBA AMVUTA ABDUKIBA NDOANI, JEBI WA "SWAHIBA" AFARIKI DUNIA..

INTRODUCING "TUONANE" BY JEX

MSANIFU MKONGWE AACHA URITHI WA MAARIFA CHUO KIKUU ARDHI DAR ES SALAAM

$
0
0
 
Mkuu wa Skuli ya Ubunifu Majengo, Usimamizi na Uchumi Ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Livin Mosha akipokea sehemu ya vitabu vya usanifu majengo na ujenzi kutoka kwa Msanifu Majengo Mkongwe Anthony Almeida (wa pili kushoto) alivyokuwa akitumia enzi za kufanya kazi. Hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Aprili mwishoni mwa wiki 2018. Pamoja nao (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Usanifu Majengo wa ARU, Dkt. Ombeni Swai na Mkuu wa Idara ya Mazingira ya Ndani ya Nyumba wa ARU, Dkt. Shubira Kalugila. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

Msanifu Majengo Mkongwe Anthony Almeida akimshirikisha jambo Mkuu wa Skuli ya Ubunifu Majengo, Usimamizi na Uchumi Ujenzi wa ARU)Profesa Livin Mosha wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vitabu hivyo.
Mkuu wa Skuli ya Ubunifu Majengo, Usimamizi na Uchumi Ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU)Profesa Livin Mosha na Dkt. Kalugila wakiondoka na vitabu hivyo kwa ajili ya matumizi ya Chuo Kikuu Ardhi.
Mkuu wa Skuli ya Ubunifu Majengo, Usimamizi na Uchumi Ujenzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Livin Mosha akimshukuru Msanifu Majengo Mkongwe Anthony Almeida baada wakati wa hafla ya kupokea sehemu ya vitabu vya usanifu majengo na ujenzi alivyokuwa akitumia enzi za kufanya kazi. Hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Aprili 20 2018.  

MICHUZI TV: AGNES MASOGANGE AWAONGANISHA WASANII NA WATANZANIA

TAKUKURU yatoa Mafunzo kuhusu kupambana na Rushwa kwa uongozi wa IFM

$
0
0
Mwezeshaji kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Angela Shangali (aliyesimama ) ikiwasilisha mada kwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Tadeo A.Satta pamoja na viongozi waandamizi wa Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM) Prof.Tadeo Satta (wa katikati mstari wa mbele )  akiwa  kwenye picha ya pamoja na uongozi mzima wa Chuo hicho, mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuzuia rushwa  yaliyofanyika chuoni hapo, mafunzo yaliendeshwa na wawezeshaji kutoa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU).

Vijana Waaswa Kulinda na Kudumisha Muungano

$
0
0

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma



Vijana Nchini wametakiwa kulinda na kudumisha Muungano kwa Vitendo kwa manufaa ya kizazi hiki na kijacho ikiwa ni sehemu ya kuonesha uzalendo.

Akizungumza wakati wa Kongamano lililofanyika mkoani Dodoma kuhusu Muungano lililowashirikisha wanafunzi zaidi ya 300 wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba amesema kuwa vijana wanalo jukumu kubwa katika kulinda Muungano na kuudumisha.

“Vijana tunawategemea muwe watetezi na walinzi wa Muungano wetu kwa kuwa huu ni urithi wa Taifa tunawajibika kuulinda na kuudumisha kwa faida ya kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Makamba

Akifafanua Makamba amesema kuwa vijna wanaowajibu wakuonesha uzalendo wao kwa kudumisha Muungano ambao unalitambulisha taifa nje ya mipaka yetu.

Mambo mengine yanayolitambulisha Taifa letu ni Lugha, Mipaka yetu, Historia, Utamaduni wa kisiasa na kijamii.

“ Waasisi wa Taifa letu walikuwa na dhamira njema ndio maana waliasisi Muungano wetu na kuweka mipaka mipya ya Taifa letu tofauti na ile ya wakoloni hivyo hili ni jambo la kujivunia” Alisisitiza Mhe. Makamba.

Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuwapuuza wale wote wanaobeza Muungano kwa kuwa hawalitakii mema taifa letu.

Kwa upande wake mwanasiasa mkongwe na Waziri (mstaafu) wa baraza la kwanza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Kwanza mara baada ya Uhuru Balozi Job Lusinde akizungumza katika mahojiano maalum mjini Dodoma amewaasa vijana kudumisha Muungano kwa kujifunza historia ya Muungano ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuuenzi.

“Vijana wajitahidi wawe waadilifu kwa kulinda uhuru wetu, umoja wetu na muungano wetu kwa faida ya kizazi hiki na kijacho” Alisisitiza Balozi Lusinde.

Akifafanua Balozi Lusinde amesema vijana wanapaswa kuepuka vitendo vya wizi na ufisadi ili kuchochea maendeleo.

Mada zilizotolewa katika Kongamano hilo ni pamoja na Historia na faida za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mtazamo wa Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

Kongamano kuhusu Muungano limefanyika Mkoani Dodoma ikiwa ni siku chache kabla ya maadhimisho ya siku ya Muungano yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26, 2018 mjini Dodoma, Kongamano hilo limewahusisha wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma, Mipango, CBE, St. John, Chuo cha Madini na Chuo cha Maendeleo Vijijini Hombolo.

UJENZI WA JENGO LA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI DODOMA, TBA YATAKIWA KUONGEZA KASI

$
0
0
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage wamefanya ziara ya kutembelea eneo la mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume eneo la Njedengwa mkoani Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hizo.

Ujenzi huo unafanywa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) na Kusimamiwa na Chuo Kikuu Ardhi.

Kufuatia ziara hiyo Wajumbe wa NEC wameonesha kutoridhishwa na Kasi ya ujenzi ya Mkandarasi anayejenga ofisi hizo (TBA) na kutoa wito kwa mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R), Mhe. Semistocles Kaijage (Kulia) na Wajumbe wa Tume wakiangalia eneo la linapojengwa jengwa la Utawala la Tume ya Taifa ya Uchaguzi enero la Njedengwa mkoani Dodoma. Wajumbe wa NEC wametembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Ofisi za NEC mkoani Dodoma
 Hili ni Eneo la Maghala ya kuhifadhia vifaa vya Uchaguzi likiwa katika hatua za Ujenzi.
 Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakipokea taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mradi kutoka TBA, Arch. Steven Simba.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R), Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) na Wajumbe wa Tume wakielekea katika eneo la ujenzi wa Ofisi za Tume mkoani Dodoma. Wengine alioambatana nao ni Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume kutoka Chuo Kikuu Ardhi QS Godwin Maro (kushoto) na Mhandisi Yohana Mashauri - Mhandisi wa Mradi huo kutoka TBA

UJENZI WA DARAJA LA PANGANI HUKO KIBAHA KUTUMIA MIL.100

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

UJENZI wa daraja litakalounganisha kata ya Pangani ,Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo umeanza ambapo hadi kukamilika kwake utatumia zaidi ya sh. milioni 100.

Akizungumza na wananchi kwenye eneo la ujenzi Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi alisema, tayari ujenzi umeanza na wameshaweka mawe ambayo yatatumika kama kitako cha daraja kwa kutumia waya ili kuzuia mmomonyoko.Alieleza, mawe yanayotakiwa ni malori 100 na nyaya hizo kwa ajili ya kuweka kitako cha daraja upande wa Pangani na Mpiji Magohe .
“Baada ya hapo vitalazwa vyuma kwa ajili ya daraja”

“Tumeanza ujenzi ambapo ujenzi wa daraja utafanywa na jeshi ambao tuliwaomba daraja na sasa wameshakubali ambapo mawe yameshawekwa wao wakija wataanza kuweka vyuma vya daraja,” alisema Mdachi.Alisema ,gharama za ujenzi zinafanywa na wananchi ,kila kaya inatakiwa kutoa kiasi cha sh. 10,000 na kuwataka wananchi kujitolea ili kukamilisha ujenzi huo.

“Tumekubaliana kwenye vikao vya wananchi kuwa kila kaya itoe kiasi hicho lakini kama mtu anauwezo anaweza kutoa zaidi na tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutusaidia kukamilisha ujenzi huu ambao utasaidia kuondoa adha kwa wakazi wa kata ya Pangani,” alisema Mdachi.

Aidha alisema kuwa, kwa kaya ambayo itashindwa kutoa mchanago huo makubaliano watakapofikishwa kwenye ofisi za mtaa itabidi watoe kiasi cha shilingi 50,000 kama adhabu.“Tunawaomba wale wenye maeneo yao huku na wanakaa jijini Dar es Salaam wanapaswa nao kuchangia ujenzi huo na endapo watashindwa kufanya hivyo watapaswa kulipia na faini kwani wamekuwa hawaonyeshi ushirikiano kwa kuwa hawakai maeneo hayo,” alisema Mdachi.

Alibainisha wananchi wa kata hiyo wanategemea huduma za kijamii Mpiji Magohe ambako ni jirani kuliko kufuata huduma Kibaha kwenye umbali wa zaidi ya kilometa nane.
Ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo, umeanza utakaogharimu mil.100.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi kuhusu ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo.( picha na Mwamvua Mwinyi)
Sura ya kivuko cha miti kinachotumika kuvuka wakazi wa kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo ambapo kwasasa ujenzi wa daraja umeanza utakaogharimu mil.100.(picha na Mwamvua Mwinyi)

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki ya Posta Tanzania

TANZANIA KUUNGANA NCHI WANACHAMA UMOJA WA MATAIFA KUADHIMISHA SIKU YA MARALIA DUNIANI 2018

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images