Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

SIKU YA MALARIA DUNIANI,KITAIFA KUFANYIKA KASULU MKOANI KIGOMA,WAZIRI UMMY MGENI RASMI


WAZIRI MKUU MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA MJINI DODOMA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa mwaka 2016/2017 na 2017/2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6. Pia Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa kuiwezesha Wizara ya Kilimo kuongeza uwezo wa hifadhi ya Taifa ya chakula kutoka tani 251,000 za sasa hadi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Aprili 21, 2018) wakati akiweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula, Kizota mjini Dodoma. Waziri Mkuu amesema mkakati huo utahusisha ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuzwa nje ya nchi na hivyo kutoa fursa za ajira na kuwaongezea kipato wananchi.

Amesema Serikali imefungua mipaka na inaendelea na jitihada za kutafuta masoko ya nje pamoja na kuboresha miundombinu ya kuhifadhi chakula kwa kujenga maghala na vihenge vya kisasa katika maeneo mengine yenye uzalishaji mkubwa wa chakula. Pia Waziri Mkuu amewasihi wananchi watumia fursa za kiuchumi kwenye maeneo ambayo mradi huo utatekelezwa kwa lengo la kuboresha na kuinua hali zao za maisha, hivyo watakuwa na uwezo wa kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye mradi huo mkubwa na baada ya kukamilika utakuwa na faida kubwa kwa Taifa, hivyo amewataka viongozi wa NFRA wahakikishe kwamba hakuna mahindi yatayoharibika katika maghala yao.

”Mikakati ya Serikali ni kuhakikisha NFRA inakuwa na uwezo wa kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya dharula lakini pia kuweka mazingira rafiki ya kuwezesha wakulima na wafanyabiashara kuuza mazao yao nje ya nchi bila vikwazo”.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango na Wakuu wa Mikoa ambayo mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wahakikishe wanatimiza wajibu wao ili mradi ukamilike kwa wakati.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Bibi Vumilia Zikankuba alisema mradi huo unatekelezwa katika maeneo manane ya Kanda za Wakala huo ambayo ni Dodoma (Dodoma), Mpanda (Katavi), Songea (Ruvuma), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga (Shinyanga), Babati (Manyara).

Bibi Vumilia alisema katika Kanda ya Dodoma wanajenga vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 na kufanya kanda hiyo kuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 59,000 kutoka uwezo wa sasa wa tani 39,000. Alisema Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.

“Utekelezaji wa mikataba kati ya NFRA na wakandarasi ulianza Desemba 2017 ambapo muda wa utekelezaji ni miezi 18 tangu tarehe rasmi ya kuanza utekelezaji wa mikataba ya wakandarasi, hivyo kabla ya 2020 utakuwa umekamilika”.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Spika wa Bunge Job Ndugai , Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama. Wengine ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira, Anthon Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya na Balozi wa Poland nchini Tanzania, Balozi Krzysztof Buzalski.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaongoza viongozi kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa, Balozi wa Poland nchini, Mhe. Krzystof Buzalski na kulia Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala na vihenge vya kisasa katika eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018.
Spika wa Bunge, Mhe.Job Ndugai akizungumza Katika sherehe ya uwekaji jiwe la msingi la maghala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma, Aprili 21, 2018. Mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wabunge na Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliopozungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa magahala na vihenge vya kisasa kwenye eneo la Kizota mjini Dodoma Aprili 21, 2018.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

CAG LUDOVICK UTOUH ALIPOJIBU HOJA ZA BIL.252/- ZA WIZARA YA UJENZI AMBAZO DKT. MAGUFULI ALISHUTUMIWA KUZITUMIA VIBAYA

WAZIRI TIZEBA AAGIZA MKURUGENZI WA BODI YA KOROSHO KUSIMAMISHWA KAZI

$
0
0
Waziri wa wizara ya kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma, Jumamosi 21 Aprili 2018. 
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini taarifa ya Waziri wa wizara ya kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba ofisini kwake mjini Dodoma, Jumamosi 21 Aprili 2018.
Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisikiliza maagizo ya kusitisha mkatanba wa kazi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Leo Jumamosi 21 Aprili 2018.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo

Waziri wa wizara ya kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kusitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg Hassan Jarufo.

Waziri Tizeba ametoa agizo hilo kwa katibu mkuu wa wizara hiyo leo Jumamosi 21 Aprili 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma ikiwa ni muda mchache mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.

Akielezea sababu za kuagiza kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo, Mhe. Dkt Tizeba alisema kuwa hayo yamejili baada ya kuangalia mwenendo wa Ndg Jarufo na kutafakari jinsi zao la korosho linavyoendeshwa, ikiwa ni pamoja na kutoridhishwa na upatikanaji wa viuwatilifu kwa wakati.

Aidha, Mkataba huo umesitishwa kuanzia leo tarehe 21 Aprili 2018 hivyo Katibu Mkuu wa wizara hiyo atapaswa kufanya taratibu zote za kiutumishi ikiwa ni pamoja na kumpatia taarifa haraka muhusika na utekelezaji wake kuanza haraka.

Alisema ndani ya muda mfupi Wizara ya kilimo itamtangaza Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo ili kuchukua nafasi hiyo kuendeleza kusimamia sekta hiyo.


“Hizi hatua tunazochukua ni kuhakikisha kuwa wadau wakubwa wa korosho ambao ni wakulima wanaendelea kunufaika na zao lao, hivyo wakulima wasiwe na wasiwasi kwani pamoja na kuondolewa Mkurugenzi huyo lakini shughuli za serikali zitaendelea kama kawaida na maslahi yao yatasimamiwa ipasavyo” Alikaririwa Mhe. Dkt Tizeba.

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA BALOZI WA CHINA NCHINI

$
0
0

 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jukwaa la Ushirikiano wa Afrika na China (FOCAC) utakaofanyika mwezi Septemba, 2018 nchini China. Mkutano huo ambao utajadili masuala mbalimbali kwa maendeleo ya Bara la Afrika utatanguliwa na vikao vya maafisa waandamizi na vile vya mawaziri. Kikao kati ya Prof. Mkenda na Balozi Wang Ke kimefanyika Wizarani tarehe 21 Aprili, 2018.
 
Maafisa kutoka Ubalozi wa China nchini wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Balozi Wang Ke (hawapo pichani).


 
Mkutano ukiendelea 

BENKI YA DUNIA YAONESHA NIA KUSHIRIKI UJENZI RELI YA ISAKA - KIGALI

$
0
0
Ujumbe wa Tanzania (kulia) na ujumbe wa Benki ya Dunia (kushoto) wakiwa katika majadiliano ya miradi ya maendelea inayotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka ujao wa fedha.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop akitoa ufafanuzi wa miradi ambayo itatekelezwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird na Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango Benki ya Dunia ukanda wa Afrika Bi. Mamta Murthi .
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akielezea miradi ambayo itatekelezwa kwa mwaka ujao wa fedha. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, Prof. Florens Luoga.

Na. WFM- Washington DC

Benki ya Dunia imeonesha dhamira ya kuisaidia Tanzania katika ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka kwenda Rusumo na baadae Kigali pamoja na miundombinu mingine ya usafirishaji  kama barabara ili kusaidia kuendeleza biashara na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati wa majadiliano na wataalamu wa Benki ya Dunia yaliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, kwenye mikutano ya mwaka ya kipupwe inayoendelea mjini Washington DC Marekani.

Dkt. Mpango amesema kuwa miradi ya Kikanda ambayo Benki hiyo imeonesha nia ya kuitekeleza ni ile ya uboreshaji wa mazingira na bandari katika ziwa Victoria zikiwemo za mikoa ya Mwanza, Musoma na Kigoma na Bandari zilizoko katika Ziwa Tanganyika ambazo zitarahisisha usafiri wa kwenda Burundi na Congo.

‘Miradi hii ya Kikanda na Kitaifa ambayo Benki ya Dunia imepanga kuitekeleza kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa mwaka ujao wa fedha itahakikisha kunakuwa na mazingira endelevu na tija kwa kuwa inagusa nchi zote zinazozunguka maziwa hayo mawili’, alieleza Dkt. Mpango.

Amesema kuwa ni lazima kuhakikisha kunakuwa na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kadri iwezekanavyo ili kuendelea kufaidi rasilimali za maziwa hayo makubwa  kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na nchi jirani zinazozunguka maziwa hayo.

Aidha amebainisha kuwa mwakani, Benki ya Dunia imeonesha nia ya kutoa fedha kwa ajili ya tekeleza mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji eneo la Ruhuji ambapo utakapokamilika unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 300.

‘Eneo hili la sekta ya umeme ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya viwanda kwa kuwa uchumi wa viwanda hauwezi kukua bila kuwepo umeme wa uhakika’ alifafanua Waziri Mpango.

Vilevile Benki ya Dunia (WB) imekubali kuisaidia Tanzania kutoa mafunzo katika uchambuzi wa miradi mbalimbali ili kusaidia Serikali ya Tanzania kutokuingia kwenye madeni makubwa zaidi ambayo hayawezi kulipika.

Waziri Mpango alieleza kuwa kutokuwa na ufanisi wa kutosha katika kuchambua miradi ambayo inagharamiwa na fedha za mikopo inasababisha nchi kubeba mzigo mkubwa wa madeni hivyo ni vyema Tanzania ikahakikisha kuwa miradi hasa ile inayogharamiwa kwa fedha za mikopo inachambuliwa vizuri ili mradi husika unapokamilika uweze kulipa deni.

Amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali itakua na miradi mingi ya kutekeleza, miongoni mwa miradi hiyo ni kupambana na tatizo la utapiamlo hivyo ni vema kama nchi ikaangalia namna bora ambayo Benki ya Dunia inaweza kusaidia katika utekelezaji wake.

“Kitaalamu mpaka mwanadamu anapofikisha siku 1000 ni kipindi muhimu sana kinachoamua maisha ya mwanadamu atakapokuwa mtu mzima atakuwa na uwezo gani wa kufikiri, kutokana na hali hiyo mtu ambaye atakua na utapiamlo uwezo wake utakua ni mdogo zaidi kulinganisha na mtoto aliyepata lishe bora’” alifafanua Dkt. Mpango.

Katika kutekeleza mradi huo Serikali itafanya kazi na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na Taasisi ya Chakula na Lishe ili kuhakikisha kwamba Taifa linapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la utapiamlo.

Mikutano hiyo ya mwaka ya kipupwe kati ya ujumbe wa Serikali ya Tanzania na Wataalamu wa Benki ya Dunia imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa Tanzania itanufaika kutokana programu mbalimbali ambazo zitagharamiwa na Benki ya Dunia kwa mikopo nafuu.

CHANJO YA KUKINGA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI HAIATHIRI UWEZO WA BINTI-HINCHA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

MRATIBU wa chanjo Mkoa wa Pwani, Abbas Hincha amesema, jumla ya watoto wa kike 18,823 waliopo shule na nje ya shule mkoani hapo wanatarajia kupatiwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi mwaka huu. Aidha ameitoa shaka jamii kuwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ni salama, haina madhara na haiathiri uwezo wa binti kupata watoto hapo baadae .

Akitolea ufafanuzi juu ya suala hilo, wakati wa semina kwa wanahabari kuhusu uanzishwaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi, Kibaha, Hincha alisema tayari wameshapokea chanjo na wataanza kuzitoa katika vituo mbalimbali vya huduma.

Pamoja na hayo ,alivitaka vyombo vya habari kubaini uzushi ama uvumi kuhusu chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi na kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya katika mamlaka husika na kutoa mrejesho kwenye jamii baada ya kupata ufafanuzi wa kitaalamu.

Hincha alieleza chanjo hiyo haina madhara na badala yake ina viudhi vichache kama ilivyo kwenye chanjo nyingine ikiwemo kuweka wekundu ama kuweka uvimbe kiasi eneo alilochomwa mhusika mkono wa kushoto. Aliwataka wazazi na jamii kuacha kudanganyana na kuzusha mambo ambayo yatakwamisha juhudi za kutolewa chanjo hiyo .

Mratibu huyo ,alisisitiza serikali imethibitisha usalama wa umadhubuti wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ndiyo maana imeiongeza kwenye mpango wa Taifa wa chanjo ili iweze kusaidia kudhibiti tatizo hilo kwa akinamama.

Alisema mwaka 2018 chanjo itatolewa kwa wasichana waliofikisha umri wa miaka 14 na ili kupata kinga kamili walengwa watahitaji kupatiwa dozi mbili.

"Dozi ya pili itatolewa miezi 6 baada ya kupata dozi ya kwanza" alisema Hincha .

Hincha alisema chanjo ya HPV kwa wasichana huwakinga wasipate saratani ya mlango wa kizazi pindi wawapo watu wazima wakiwa na familia zao.

Kaimu mganga mkuu wa mkoa huo ,Hussein Athumani  ambae pia anaesimamia masuala ya kinywa na meno Mkoani Pwani,alisema  saratani hiyo ina athari kubwa kwa afya ya wanawake ulimwenguni kote. Alisema inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea.

Athumani alisema saratani hiyo inashika nafasi ya pili kwa kusababisha saratani kwa wanawake, nafasi ya kwanza inashikwa na saratani ya matiti .

"Nchini Tanzania saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza kwa vifo ikifuatiwa na saratani ya matiti " Saratani hizi mbili kwa pamoja husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya wakinamam vitokanavyo na saratani"alibainisha Athumani.

Alifafanua chanjo hiyo inagharama kwani dozi moja ni dollar 15 ambapo dozi mbili ni dollar 30. Athumani alielezea ,wanawake 7,304 nchini wamegundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi kati ya hao 4,216 asilimia 18 walifariki kutokana na tatizo hilo .

Kwa upande wake ,mgeni rasmi katika semina hiyo ,Gerald Manase kutoka TAMISEMI alisema ,wasichana na wanawake wanaohitaji huduma ya chanjo ambao sio walengwa wa uanzishwaji wa chanjo hiyo inayotolewa na mlango wa Taifa wa chanjo wanaweza kupata chanjo katika hospital binafsi zinazotoa chanjo hiyo .

Dalili za saratani hiyo ni maumivu ya mgongo,miguu  ,kiuno,kuchoka,kutokwa damu nyingi bila mpangilio baada ya kujamiiana,uchafu kwenye uke wa majimaji,kuvimba miguu na inasababishwa na virusi vinavyojulikana kitaalamu kama human papilloma virus(HPV).

MAKAMBA: MUUNGANO NI URITHI WETU, TU UTUNZE.

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifungua kongamano la vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo mkoani Dodoma. Jumla ya Vyuo sita vimeshiriki katika Kongamano hilo lililofanyika katika Chuo cha Mipango, Dodoma na mada kuu ikiwa ni fursa zilizopo katika Muungano.
Sehemu ya wanafunzi kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo mkoani Dodoma wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. Kongamano hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango Dodoma na kuhudhuriwa na wanafunzi kutoka Vyuo vya Hombolo, Chuo cha Elimu ya Biashara, St. John, Chuo cha Mipango, Chuo cha Madini na Chuo Kikuu cha Dodoma.
Waratibu wa kongamano hilo, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Muungano Bi. Lupy Mwaikambo, Bw. Sifuni Msangi Kaimu Mkurugenzi Idara ya Muungano na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.

BUNGE LAPITISHA BILLIONI 898 BAJETI YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

$
0
0

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia na kupitisha jumla ya Shillingi Billioni 898 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Wakijibu hoja mbalimbali za wabunge kuhusu Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema Wizara itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu kwa wazazi ili wawafundishe watoto wao.

Pia Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa kwa somo la elimu ya uzazi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuwapa uelewa wanafunzi ili waweze kujikinga na kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali imefanya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) nchini kwa kuyahakiki na kuyafuta Mashirika yote ambayo yamekosa sifa na kutofuata utaratibu na Sheria za nchi.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa huduma kwa wazee nchini kwa kuboresha makazi ya kulea wazee wasiojiweza, kuanzisha na kuratibu madirisha maalum ya kutoa huduma za afya kwa wazee katika hospitali na kutoa kadi za matibabu kwa wazee hao. 

Bunge limepitisha Bajeti hii ikiwa imejumuisha fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida na matumizi kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu

UZALISHAJI WA CHAKULA NCHINI UMEIMARIKA-MAJALIWA

$
0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa mwaka 2016/2017 na 2017/2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6.

Pia Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa kuiwezesha Wizara ya Kilimo kuongeza uwezo wa hifadhi ya Taifa ya chakula kutoka tani 251,000 za sasa hadi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Aprili 21, 2018) wakati akiweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula, Kizota mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema mkakati huo utahusisha ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuzwa nje ya nchi na hivyo kutoa fursa za ajira na kuwaongezea kipato wananchi.

Amesema Serikali imefungua mipaka na inaendelea na jitihada za kutafuta masoko ya nje pamoja na kuboresha miundombinu ya kuhifadhi chakula kwa kujenga maghala na vihenge vya kisasa katika maeneo mengine yenye uzalishaji mkubwa wa chakula.

Pia Waziri Mkuu amewasihi wananchi watumia fursa za kiuchumi kwenye maeneo ambayo mradi huo utatekelezwa kwa lengo la kuboresha na kuinua hali zao za maisha, hivyo watakuwa na uwezo wa kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

WANANCHI WATAHADHARISHWA ONGEZEKO MARADHI YA MATUMBO YA KUHARISHA ZANZIBAR

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 

Jamii imetakiwa kuchukua tahadhari juu ya Ongezeko la Maradhi ya Matumbo ya kuharisha ambayo yameanza toka kuanza kwa msimu wa Mvua za masika katika Visiwa vya Unguja na Pemba.

Tahadhari hiyo imetolewa na kaimu Mkurugenzi Kinga Zanzibar Dkt Mohamed Dahoma alipokuwa akizungumza na Wanahabari kuhusiana na mwenendo wa Maradhi Zanzibar.

Amesema toka kuanza kwa msimu wa Mvua za masika Kituo cha ufuatiliaji wa mwenendo wa maradhi Zanzibar kimebaini zaidi ya Wagonjwa 700 wa Matumbo ya kuharisha.“Mpaka sasa hivi hakuna Mgonjwa wa Kipindupindu Zanzibar iliyokuwepo ni kuongezeka kwa Maradhi ya Matumbo ya kuharisha.

Ni wajibu wetu kuchukua tahadhari” Alisema Dkt Dahoma.Hata hivyo amesema hadi sasa hakuna Mgonjwa wowote aliyebaiwa kuugua Maradhi ya Kipindupindu Zanzibar.Kutokana na hali hiyo Wizara ya Afya inatoa tahadhari ili Jamii iweze kujilinda ipasavyo dhidi ya maradhi hayo.

Amesisitiza kuwa Serikali kupitia Taasisi zake mbali mbali inaendelea na juhudi zake kuhakikisha taaluma ya afya kwa wananchi inawafikia na kutoa huduma stahiki kwa wale wote walioahirika na maradhi ya matumbo katika Vituo vya afya.Dkt Dahoma ametoa Wito kwa jamii kuwapeleka katika Vituo vya matibabu wagonjwa wote watakaobainika kuharisha badala ya kuwatibia majumbani.Amesema Serikali imejipanga kwa Vifaa Dawa na Madaktari wa kutosha kuhakikisha kila anayeathirika na maradhi hayo anatibiwa ipasavyo.

Akielezea kuhusua maradhi ya Matumbo ya kuharisha Dkt Dahoma amefafanua kuwa Maradhi hayo hutokana na mrundikano wa uchafu na husambazwa kupitia kinyesi kuingia katika chakula au maji.Hivyo ni wajibu wa jamii kuhifadhi vyanzo vya maji na chakula dhidi ya maradhi hayo.

Aidha amesisitiza kunawa vyema kwa sabuni kabla na baada ya kula na kutumia maji yaliyochemshwa kwa ajili ya kunywa.Zanzibar hukabiliwa na Mvua za Masika kila ifikapo mwezi machi na hadi May ambazo licha ya kuwa Neema kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, huambata na mitihani ikiwemo maafa, maradhi ya kuharisha na kipindupindu.
KAIMU Mkurugenzi Kinga Dkt Moh’d Dahoma akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ongezeko la maradhi ya kuharisha toka kuanza kwa msimu wa Masika-Picha na Abdalla Omar 

BALOZI WA TANZANIA NCHINI CHINA AZUNGUMZIA FURSA AMBAYO NCHI YETU IMEIPATA KWENYE MAONESHO YA UTALII

$
0
0
Na Ripota Wetu, China
BALOZI wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki amesema zaidi watu 1,000 wamepata fursa ya kutembelea banda la Tanzania ambalo lilikuwepo kwenye maonesho ya utalii nchini humo.

Idadi hiyo ya watu ambao wametembelea banda la Tanzania imesaidia kuwapatia taarifa sahihi na za kutosha kuhusu utalii wetu na ni moja ya eneo ambalo limetumika vema kutangaza vivuto vilivyopo.

Balozi Kairuki ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye maoesho ya utalii yaliyofanyika nchini China ambayo yamemalizika hivi karibuni.

Akifafanua zaidi kuhusu Maonyesho ya biashara ya Utalii (China Outboard Travel & Tourism Market COTTM) yaliyomalizika hivi karibuni jijini Beijing China Balozi Kairuki amesema maonesho hayo yamekuwa na mwitikio mkubwa.

"Zaidi ya watu 1,000 wameweza kutembelea banda la Tanzania hatua ambayo imesadia watu wengi kupata taarifa za kutosha kuhusu fursa za Tanzania.Naipongeza bodi ya utalii na mamlaka zote za utalii Tanzania pamoja na mawakala wa utalii ambao walishiriki kwa lengo la kuchangamkia fursa hiyo,"amesema.

Ameogeza soko la China ni jipya na linalokua kwa kasi,hivyo matarajio yao hizo taasisi za bodi ya utalii, Hifadhi ya Ngorongoro ,TANAPA watapewa nguvu zaidi, watawezeshwa kibajeti ili wakushiriki maonyesho mengi zaidi hapa China.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki (Kushoto) akishiriki mahojiano maalumu yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa  Tanzania  kupitia kituo cha runinga cha   "Chinese Satelite Travel" chenye  watazamaji zaidi ya Milioni 100 ndani na nje ya China. Mahojiano hayo yaliongozwa na Bi. Mei Qing  mtangazaji maarufu wa Television hiyo.
 Afisa Utalii kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, Piter Makutian (Kushoto) akizungumza jambo katika  mahojiano maalumu yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa  Tanzania  kupitia kituo cha runinga  cha   "Chinese Satelite Travel" chenye  watazamaji zaidi ya Milioni 100 ndani na nje ya China. Mahojiano hayo yalifanyika wakati wa Maonyesho ya Utalii yaliyofanyika Beijing China mapema wiki hii. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki.
 Mahojiano yakiendelea  yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa  Tanzania  kupitia kituo cha runinga  cha   "Chinese Satelite Travel"
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mahojiano kwenye kituo cha runinga  cha  "Chinese Satelite Travel" 
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(kushoto) akipata maelezo kuhusu Maonyesho ya Utalii  kutoka kwa Afisa Utalii Mwandamizi - Hifadhi ya Taifa Tarangire Theodora Aloyce (katikati), Wa pili kushoto ni Afisa Utalii habari  - Bodi ya Utalii Tanzania, Irene  Mville, Afisa Utalii- Mamlaka ya Hifadhi  ya Eneo la Ngorongoro, Piter Makutian (wa pili kulia) na Afisa Kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China, Lusekelo Gwassa
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi Watanzania nchini China, Remidius Emmanuel(Kushoto)  akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Compass Safari, Peter Larocque inayofanya kazi zake nchini Tanzania.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MKOA WA DAR ES SALAAM KUTOA CHANJO KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WATOTO WA KIKE MIAKA 14

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MAFUNZO ya utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi (Human vaccine) yametolewa leo jijini Dar es salaam na kuwataka watu wa kada zote kuhimiza watoto kupata kinga hiyo ya saratani.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameeleza kuwa chanjo hii itapunguza vifo vya wanawake wengi na ametoa rai kuwa kila mtoto wa miaka 14 apate chanjo hii na aturudie ili kukamilisha dozi kwa zoezi litakaloanza tarehe 23 mwezi huu.

Aidha amewataka wananchi kutumia fursa hii ya Serikali ya awamu ya tano kwa kujitokeza katika vituo 270 vilivyoorodheshwa na amewataka Wenyeviti wa Mitaa kuhamasisha akina Mama kupeleka watoto wao wakapate chanjo hii ili kuokoa maisha ya wanawake wengi pia ameeleza kuwa wana mpango wa kuendesha zoezi la kupima tezi dume nyumba kwa nyumba katika Mkoa wa Dar es salaam.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala bi. Sophia Mjema ameeleza kuwa kila mtoto wa miaka 14 apate chanjo hii na amewaomba akina baba kuwakumbusha akina Mama kuhusiana na chanjo hii.

Mratibu wa huduma za chanjo na uzazi Mkoa Bi. Ziada Sella ameeleza kuwa saratani ya shingo ya uzazi ni ya pili kwa madhara kwa mwanamke ikifuatiwa na saratani ya matiti ambayo huuwa wanawake wengi. Kuhusu dalili za awali la ugonjwa huo ameeleza kuwa kuvimba miguu, kutoka uchafu wa kahawia uliochanganyika na damu, maumivu ya miguu, mgongo na kiuno ni dalili za awali za saratani.

Kuhusiana na chanjo hii bi. Sella ameeleza kuwa watoto wa miaka 14 watapatiwa chanjo hii mara mbili kwa kurudia mara baada ya miezi 6 aidha watoto wenye maambukizi ya virusi ya Ukimwi (HIV) watapata chanjo tatu watakayorudia baada ya miezi 2 watakayochoma katika vituo vya afya na ya tatu watachoma na wenzao mashuleni baada ya miezi sita.

Aidha katika utoaji wa chanjo kuna vituo 270 ikiwa vituo 71 katika Manispaa ya Ilala, 48 Ubungo, 19 Kigamboni, 65 Kinondoni na 48 katika Manispaa ya Temeke.
Aidha amesisitiza wananchi kutokuwa na imani potofu kuhusu chanjo hizo kwani kinga ni bora kuliko tiba. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akizungumza leo katika uzinduziwa zowezi la utoaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa Kizazi.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda akiteta jambo na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, kabla ya uzinguzi wa zowezi la utoaji Chanjo ya kuzuia Salatani ya mlango wa Kizazi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe akifafanua kuhusu zowezi la utoaji Chanjo ya kuzuia Saratani ya mlango wa Kizazi.

Uwekaji Hesabu Serikalini unaendelea kuwa mzuri tofauti na Awali - Prof Assad

MKURUGRNZI WA FADHAGET AUNGA MKONO KWA VITENDO KAULI MBIU YA TANZANIA YA VIWANDA

$
0
0
*Aishukuru Serikali,SIDO kwa kutambua mchango wa kiwanda
chake cha virutubisho tiba

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI wa Kampuni ya Fadhaget inayomiliki kiwanda cha Virutubisho Tiba Fadhaget Nutrition Science, Dkt Fadhili Emily ameishukuru Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo(SIDO) pamoja na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kwa kuwaona vijana wa Tanzania kuwa wanao uwezo wa kumiliki viwanda.

Amesema kuwa kauli ya Rais Magufuli imewafanya vijana wajikwamue na umasikini uliokithiri na sasa wigo wa ajira unaendelea kuongezeka kutikana na viwanda vinavyoanzishwa kutokana na dhamira njema ya Serikali inavyohimiza ujenzi wa viwanda.

Amesema hayo wakati anazungumzia na Michuz Blog baada ya SIDO kumtunuku cheti cha kutambua kiwanda chake na mchango ambao anautoa katika kuelekea nchi ya viwanda ambapo cheti hicho amekabidhiwa jana."Sisi kama kiwanda cha kwanza Tanzania cha kuandaa virutubisho tiba vyenye uwezo wa kupambana na magonjwa mbalimbali ya mfumo wa mwanadamu tunaahidi kuzalisha mara dufu ili kuhakikisha watu wanapatapa kilicho bora zaidi kutoka Fadhaget Nutrition Science,"amefafanua.

Akifafanua zaidi kuhusu Fadhaget Nutrion Science,Fadhili  amesema wamekuwa wakiandaa virutubisho tiba kwa njia za kisasa kabisa kwa kuzingatia kanuni za usalama wa vyakula na virutubisho duniani yaani HACCP(Hazard Analysis and Critical Control Point).Amesema furaha yao ni kuhakikisha watu wanatapa tiba salama isiyo na madhara ya baadae na wamefanikiwa baada ya kuandaa virutubisho kwa magonjwa karibia yote hasa yale ya virusi vya magonjwa ya muda mrefu.

Ametaja baadhi ya magonjwa hayo ni Ukimwi, vidonda vya tumbo, U.T.I sugu, malaria sugu ,upungufu wa nguvu za kiume, figo , ini, kifua kikuu , pumu (arthima), kisukari, matatizo ya uzazi pande zote yaani kutopatikana mtoto katika ndoa , uvimbe wa kizazi na kuziba kwa mirija ya kizazi ."Pia magonjwa ya zinaa na dalili nyngine nyingi za hatali kiafya kama vile miguu kufa ganzi , miguu kuwaka moto, miguu kuvimba na unapoibonyeza lina baki shimo kama unavyobonyeza ndizi mbivu.

"Kuwashwa ukeni kwa akina mama na kutokwa na uchafu mzito mweupe katika via vya uzazi au wa kahawia wenye harufu na unapopata mkojo unakuwa wa njano sana ikiwa ni pamoja na matatizo ya kukosekana kwa hamu ya tendo la ndoa,"amesema.Kuhusu cheti ambacho amepewa na SIDO cha kutambua kiwanda chake amesema kama kijana wa Kitanzania atahakikisha cheti hichi kinakumbusha kuwa analo jukumu la kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Magufuli ya kuwa na Tanzania ya viwanda na kwake na kuongeza itakuwa chache kwake kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu kwa maslahi ya Watanzania wote.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fadhaget inayomiliki Kiwanda cha
Virutubisho Tiba Fadhaget Nutrition Science (kushoto),Fadhili Emily  akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo(SIDO).Cheti hicho ni kwa ajili ya kutambuliwa kwa kiwanda chake ambacho amekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
 



Cheti ambacho amekabidhiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Fadhaget inayomiliki Kiwanda cha Virutubisho Tiba Fadhaget Nutrition Science kutoka Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo vidogo(SIDO).

SERIKALI INAFANYA TATHIMIN YA FIDIA ARIDHI NA MAENDELEZO YAKE MPAKA WA TANZANIA, KENYA

$
0
0

Na Rehema Isango, Tarime, Mara

SERIKALI inafanya tathmini kuhusu fidia ya ardhi na maendelezo yake katika eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya iwapo kutakuwa na utwaaji ardhi wakati wa zoezi la kuimarisha mpaka linaloendelea mkoani Mara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Doroth Mwanyika alisema hayo wakati alipokagua kazi ya uimarishaji mpaka katika eneo la upande wa pwani ya Ziwa Victoria mkoani Mara katika kijiji cha Kirongwe kata ya Bukura Wilayani Rorya hadi eneo la Sirari mkoani Tarime.

Amefafanua Serikali inafanya tahmini hiyo kwa lengo la kuona wananchi waliopo katika eneo huru (buffer zone) iwapo watatakiwa kupisha eneo hilo, itumike njia bora ya kujadiliana nao au namna mbadala ya kuwasaidia wananchi hao.

“Kwanza wananchi walioendeleza maeneo ya mipakani walipewa elimu wakati wa mchakati wa uhamasishaji lililofanywa na wataalam wetu kabla ya kuanza kwa kazi ya uimarishaji mpaka." Wengine wameelewa na kuchukua hatua ya kupisha wakati kazi ya uimarishaji mpaka inaendelea,” amesema Mwanyika.

Aidha Serikali imebainisha kuwa itahakikisha inatatua changamoto hizo zilizojitokeza katika zoezi hilo kwa njia ya amani na kwa kuzingatia haki. Mapema Machi mwaka huu, Serikali za pande zote mbili Tanzania na Kenya zilikubaliana kuanza kazi ya uimarishaji wa mpaka wa Kimataifa katika urefu wa kilomita 238 za nchi kavu kutoka ziwa Victoria mkoani Mara hadi Ziwa Natroni mkoani Arusha.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Doroth Mwanyika ( wa tatu kutoka kushoto  aliyeinama) akigusa moja ya alama mpya zinazoongezwa kila baada ya urefu wa mita mia moja kwenye mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya. Bibi Mwanyika na Makatibu Wakuu wengine wanne walikagua mpaka huo wakati wa kazi ya uimarishaji iliyoanza Machi mwaka huu. Picha zote na Rehema Isango WANMM

KUTOKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB: MAANDALIZI YA KUANGA MWILI WA AGNES MASOGANGE YAENDELEA

$
0
0
 Jeneza lenye mwili wa video queen nchini na muigizaji wa filamu Agnes Gerald maarufu kama Agnes Masogange, likiwekwa sawa tayari kwa zoezi la kuaga mwili huo, katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam hivi sasa. Mwili wa Masogange unatarajiwa kuzikwa kesho huko kijijini kwao, Utengule, jijini Mbeya.
 Sehemu ya Wasanii wa filamu na Muziki nchini, wakiwa wamejumuika pamoja katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kuomboleza msiba wa video queen nchini na muigizaji wa filamu Agnes Gerald maarufu kama Agnes Masogange.
Sehemu ya waombolezaji wengine.

WORK OUT BONANZA

UJENZI WA DARAJA LA PANGANI HUKO KIBAHA KUGHARIMU MIL.100

$
0
0
Sura ya kivuko cha miti kinachotumika kuvuka wakazi wa kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo ambapo kwasasa ujenzi wa daraja umeanza utakaogharimu mil.100.
Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi kuhusu ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo.
Ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo, umeanza utakaogharimu mil.100.(picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi, Globu ya Jamii - Kibaha

UJENZI wa daraja litakalounganisha kata ya Pangani ,Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo umeanza ambapo hadi kukamilika kwake utatumia zaidi ya sh. milioni 100.

Akizungumza na wananchi kwenye eneo la ujenzi Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi alisema, tayari ujenzi umeanza na wameshaweka mawe ambayo yatatumika kama kitako cha daraja kwa kutumia waya ili kuzuia mmomonyoko.

Alieleza, mawe yanayotakiwa ni malori 100 na nyaya hizo kwa ajili ya kuweka kitako cha daraja upande wa Pangani na Mpiji Magohe.

"Baada ya hapo vitalazwa vyuma kwa ajili ya daraja"

“Tumeanza ujenzi ambapo ujenzi wa daraja utafanywa na jeshi ambao tuliwaomba daraja na sasa wameshakubali ambapo mawe yameshawekwa wao wakija wataanza kuweka vyuma vya daraja,” alisema Mdachi.

Alisema ,gharama za ujenzi zinafanywa na wananchi ,kila kaya inatakiwa kutoa kiasi cha sh. 10,000 na kuwataka wananchi kujitolea ili kukamilisha ujenzi huo.

“Tumekubaliana kwenye vikao vya wananchi kuwa kila kaya itoe kiasi hicho lakini kama mtu anauwezo anaweza kutoa zaidi na tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutusaidia kukamilisha ujenzi huu ambao utasaidia kuondoa adha kwa wakazi wa kata ya Pangani,” alisema Mdachi.

Aidha alisema kuwa, kwa kaya ambayo itashindwa kutoa mchanago huo makubaliano watakapofikishwa kwenye ofisi za mtaa itabidi watoe kiasi cha shilingi 50,000 kama adhabu.

“Tunawaomba wale wenye maeneo yao huku na wanakaa jijini Dar es Salaam wanapaswa nao kuchangia ujenzi huo na endapo watashindwa kufanya hivyo watapaswa kulipia na faini kwani wamekuwa hawaonyeshi ushirikiano kwa kuwa hawakai maeneo hayo,” alisema Mdachi.

Alibainisha wananchi wa kata hiyo wanategemea huduma za kijamii Mpiji Magohe ambako ni jirani kuliko kufuata huduma Kibaha kwenye umbali wa zaidi ya kilometa nane.

MASHINDANO YA OLIMPIKI 2020 NCHINI JAPAN KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA TANZANIA - DK. KIGWANGALLA

$
0
0


Na Hamza Temba-Ngorongoro, Arusha

Mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika nchini Japan mwaka 2020 yatatumika kunadi vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia timu ya Taifa ya riadha na banda la maonesho ya utalii.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kukamilika kwa mashindano ya riadha ya Ngorongoro Marathon 2018 katika mji wa Karatu, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimsalimia Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dkt. Fredy Manongi muda mfupi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Dkt. Kigwangalla alitoa kauli hiyo wakati akijibu ombi la Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mtaka ambaye aliiomba wizara yake kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kusaidia maandalizi ya timu ya Taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo.

Mtaka pia aliomba Mamlaka hiyo itumie timu ya Taifa ya riadha Tanzania kama mabalozi wao wa kutangaza vivutio vya utalii vya hifadhi hiyo ya Ngorongoro ndani na nje ya nchi.

Akijibu maombi hayo, Dk. Kigwangalla alisema kitaundwa kikosi kazi cha pamoja kati ya wizara yake kupitia taasisi zake hususan Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Chama cha Riadha Tanzania ili kuainisha mahitaji ya mashindano hayo na kuweka makubaliano yatakayonufaisha pande zote.
Waziri Kigwangalla akiwa tayari kuzindua mashindano hayo katika umbali wa kilomita 21.

"Kama tunaweza kupata jukwaa la nchi zaidi ya 50 au 100 kwa kufadhili wanariadha 200 kwenda kushiriki, manake hilo jukwaa linatulipa, kwa sababu tunawekeza kidogo tunaonekana kwa kiasi kikubwa.

"Mwaka 2020 kwenye Olimpiki lazima tuwekeze, na sisi Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zetu tutapenda tuunde kikosi kazi cha pamoja ili tuangalie gharama zinazohusika, maandalizi yanayohitajika ili na sisi kama Wizara kupitia taasisi zetu kama Ngorongoro tuweze kuona nini mchango wetu, lakini sisi tutataka tujue faida yetu hasa itakuwa ni nini" alisema Dk. Kigwangalla.

Alisema mashindano hayo yatatoa fursa pana kwa Taifa kutangaza vivutio vyake mbali na juhudi zinazofanywa hivi sasa kupitia maonesho ya kimataifa. "Kupitia mashindano hayo tutapeleka pia maombi kwenye ofisi ya balozi wetu nchini Japan ili tupewe banda la kunadi vivutio vyetu vya utalii" alisema.
Washiriki wa mbio hizo kutoka Tanzania na Kenya wakitimua mbio kuanza mashindano hayo ya Ngorongoro Marathon 2018 umbali wa Kilomita 21 mjini Karatu mkoani Arusha. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.

Dk. Kigwangalla pia aliitaka Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kukubali ombi la Chama cha Riadha Tanzania la kuanzisha kituo cha mafunzo ya riadha mjini Karatu ili kuimarisha mchezo huo na timu ya riadha Tanzania sambamba na kutumia kituo hicho kama fursa ya kutangaza utalii wa hifadhi hiyo.

Alisema kituo hicho pia kijengwe sanamu za wanariadha mashuhuri waliowahi kuiletea sifa Tanzania na kuweka rekodi mbalimbali ili kutoa motisha kwa wanariadha wengine wanaochipukia.

Alisema mbali na kuanzisha kituo hicho, timu hiyo ya Riadha Tanzania inaweza pia kupewa jina la Ngorongoro ili kuitangaza hifadhi hiyo yenye vivutio vya kipekee duniani ambavyo vimeifanya itambulike kama sehemu ya urithi wa dunia.

Mashindano ya Ngorongoro Marathon kwa mwaka huu 2018 yamehusisha washikiri kutoka Tanzania na Kenya ambapo washindi wa kwanza wa mbio hizo za kilomita 21 upande wanaume na wanawake wametoka nchini Kenya. Kaulimbiu ya mashindano hayo imelenga kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishiriki mashindano ya mbio za Ngorongoro Marathon 2018 na wanariadha wengine mjini Karatu mkoani Arusha jana ambapo alimaliza mbio hizo kwa kukimbia kilomita 21. Kaulimbiu ya mashindano hayo na kupiga vita ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
Baadhi ya watalii nao walitumia fursa hiyo kusaka medali.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images