Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

TanTrade yawapiga msasa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini

$
0
0
Mkufunzi Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kutoka kitengo cha KEIZAN, Janeth Senkondo (akiwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa za ngozi kwenye mafunzo yanayoratibiwa na TanTrade.

Wazalishaji thelathini (30) wa bidhaa za ngozi kutoka Chama cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania (TALEPPA) wamejengewa uwezo kwa kupewa mafunzo ya siku tatu yaliyoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

Mafunzo hayo yaliyoongozwa na Bw Emmanuel Miselya, Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara kutoka TanTrade amesema kuwa lengo la kuwajengea uwezo wazalishaji wa bidhaa za ngozi ni kuwasaidia kuwa na ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

‘’Sekta hii ina rasilimali nyingi na ikitumiwa vizuri kwa kushirikiana na wazalishaji wenyewe Tanzania itakuwa na viwanda vingi vya ngozi na bidhaa zake na wananchi watapata ajira itakayowaongezea kipato kikubwa kwa sababu kuna fursa kubwa ya masoko ndani na nje ya nchi hivyo kuongeza wigo wa kodi”, alisema Bw Miselya.

Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa TanTrade itahakikisha inatoa mafunzo kwa wazalishaji wa bidhaa zenye muelekeo wa viwanda ili rasilimali za nchi zitumike vizuri na kuweza kuvutia ongezeko la uwekezaji nchini.

Nae, Bw Johnson Kiwia, Afisa Viwango kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), amewashauri wazalishaji wa bidhaa za ngozi kuzingatia kutumia malighafi iliyothibitishwa na taasisi hiyo ili kuwapa ujasiri wa kufanya biashara ndani na nje ya nchi na kuweza kumudu ushindani wa soko.

Kwa niaba ya wanufaika wa mafunzo hayo, Bw.Timoth Funto, Katibu wa Chama cha Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania (TALEPPA) ameeleza kuwa kupitia mafunzo hayo wamepata ujuzi wa masoko yatakayowawezesha kutatua changamoto ya namna ya kusimamia biashara zao ili kukidhi hitaji la msingi lililokuwa linawatatiza katika uzalishaji.

Mafunzo ya awamu ya tatu yamejikita kwenye uzalishaji bora wa bidhaa zenye viwango, kuzingatia usalama mahala pa kazi na namna ya kubuni bidhaa zenye mvuto na kuendana na mitindo ya kisasa yenye kupendwa na watumiaji wengi.

Taasisi zilizoshiriki kuwajengea uwezo wazalishaji hao ni Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia kitengo cha KAIZEN, TBS, VETA, OSHA na DIT kampasi ya Mwanza.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Viziwi kutoka Mkoa wa Dodoma pamoja na Shule ya Sekondari Tagamenda kutoka Mkoa wa Iringa wakifuatilia mijadala inayoendelea ndani ya Bunge ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya Mafunzo Bungeni.
 Viongozi  Mbali mbali  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake wakifuatilia jinsi muhimili wa Bunge unavyofanya kazi yake, leo katika ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mheshimiwa Saul Amon (kushoto) leo katika Viwanja vya bunge Mjini Dodoma. Katikati ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mwenye miwani), anaefuata ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya, Ndg. Jacob Mwakasole na wengine ni Viongozi Mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake ambao ni wageni wa Naibu Spika wa Bunge.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akisalimiana na mmoja ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya leo katika Viwanja vya bunge Mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Victor Mwambalaswa.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa saba kulia mbele), Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (wa tisa kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya yake leo katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma. Wa nane kulia mbele ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya, Ndg. Jacob Mwakasole
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

VIJANA WENGI WAMEJAA TAARIFA BADALA YA MAARIFA-JANUARY

$
0
0
*Ahimiza vijana kusaka maarifa kwa nguvu zote ili wawe viongozi bora
*Ataka wazee kurithisha vijana yale yaliyofanywa na Mwalimu Nyerere

Na Said Mwishehe ,Globu ya jamii

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira katika Serikali ya Awamu ya Tano Januari Makamba amesema vijana wengi nchini kwa sasa wamejaa taarifa badala ya
maarifa.

Hivyo amesema ili vijana wawe viongozi bora na wanzuri kwa Taifa letu ni vema wakafanya juhudi na kuhakikisha wanapata maarifa ambayo yatakuwa dira na muelekeo kwa nchi yetu.January amesema hayo leo wakati wa Kongamabo la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere ambayo imefanyika katika Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaa.

Mada kuu kwenye kongamano inasema Kuelekea uchumi wa kati mchango wa Mwalimu Nyerere kuhusu amani,umoja wa kitaifa na uwajibikaji.Amesema yeye kama viongozi kijana ametumia kongamano hilo muhimu kuhusu mchango wa Mwalimu Nyerere katika ujenzi wa taifa hili na kwa sehemu kubwa aliongoza kwa maarifa makubwa na yenye tija kwa nchi yetu.

Hivyo amesema kwa vijana wote wa Tanzania hasa wanaotaka kuwa viongozi ni vema wakajikita kitafuta maarifa zaidi badala ya kujaza taarifa vichwani ambazo nyingine hazina tija.

"Taarifa inakuwezesha tu kuwa mzuri kwenye mazungunzo katika vijiwe vya kahawa na katika kupiga soga.Lakini ukiwa na maarifa yatakufanya kijana kuwa kiongozi bora kwa nchi yetu.Nimebahatika kwenda Butiama na nilipofika nilifanikiwa kuingia maktaba yake Mwalimu, utaona namna ambavyo amesoma vitabu vingi sana ili kuwa na maarifa mapana kwa ajili ya kuliongoza vema taifa letu,"amesema January.

Ametoa mwito kwa vijana nchini kuhakikisha wanatumia muda mwingi kusaka maarifa badala ya taarifa na kuongeza Mwalimu Nyerere alifika Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 32 lakini kutokana na maarifa yake wazee walimuamini na akawa Rais wa Tanu.


Baadhi ya wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere January Makamba(hayupo pichani) leo.
Mgeni rasmi kwenye Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere January Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa na viongozi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere baada ya kufungua rasmi kongamano hilo ambalo lilikuwa na mada mbalimbali. kongamano hilo limefanyika leo chuoni hapo.

VETA DODOMA YAJIPANGA KUCHOCHEA UJENZI WA VIWANDA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHUO cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Dodoma kimesema kuwa kinatekeleza kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuelekea uchumi viwanda katika uzalishaji wa vijana wenye ujuzi wa kutumikia viwanda hivyo.

Hayo yamesemwa leo mkoani Dodoma na Mkuu wa Chuo hicho, Ramadhan Mataka ambaye yupo katika ziara ya kuangalia nafasi ya VETA katika uzalishaji wa vijana katika soko la ajira na fursa ambazo zinazopatikana kuelekea Tanzania ya viwanda.

Amefafanua  kozi zinazozalishwa katika chuo hicho zinamfanya mhutimu kuingia katika soko la ajira bila kuwa na changamoto yeyote kutokana na ujuzi wa walioupata katika chuo hicho.

Ameongeza kozi ambazo zina fursa ya ajira za uhakika  lakini mwitikio wake mdogo ni kozi uchoraji ramani, ujenzi wa barabara na ukarabati ambazo kozi hizo wanafunzi wanaweza kutumika sehemu
kubwa wakala wa barabara wa vijijini na Mjini (Tarula).

Amesema vijana waliotoka kozi hizo wamajiliwa na kampuni za ukandarasi ambapo wamekuwa wakifanya vizuri lakini idadi ya vijana wanaojiunga ikilinganishwa mahitaji yaliyopo katika ujenzi wa barabara na ukarabati pamoja na uchaoraji ramani za majengo.

Mataka amesema katika kuipa uzito kozi ya ujenzi wa barabara na ukarabati wameanzisha lugha ya kichina ambapo wanaasoma kozi hiyo watapohitimu wanaweza kuajiriwa na kampuni za ujenzi za kichina zilizopo nchini kutokana na kujua lugha ya mawasiliano.

Aidha amesema wameanzisha kozi adimu ya watumishi wa kazi za ndani ambapo wakisoma watajua majukumu yao nini wakati wanaingia mkataba kwa kazi wanayoifanya.

Hata hivyo amesema katika kozi mpya ni pamoja utayarishaji na mikato ya Nyama ambapo wanaweza  kutumika katika masoko ya nyama kutokana na mafunzo walioyapata.

Mmoja wa Mwanafunzi wa Kozi ya Ujenzi wa Barababara na Ukarabati, Esther Ipini amesema wasichana wajitoe katika kusoma kozi hiyo kutokana na uhakika wa ajira na kuongeza hakuna kazi ambazo ziko kwa ajili ya wanaume kwani huko ndiko kunafanya wanawake kuwa nyuma kimaendeleo sasa ni wakati wa kujitoa kila sehemu tukapata ujuzi.
 Mkuu wa Chuo cha VETA, Dodoma, Ramadhan Mataka akizungumza na waandishi habari kuhusiana maendeleo ya chuo hicho katika kuzalisha vijana wa kuweza kutumika katika sekta ya viwanda, jijini Dodoma.
 Meneja wa Mawasiliano wa VETA, Sitta Peter akizungumza na waandishi habari kuhusiana na umuhimu wa waandishi kuandika fursa za vyuo vya VETA , jijini Dodoma.
 Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa kozi ya Ujenzi wa Barabara na  Ukarabati wa Barabara, Khadija Mohamed akizungumza na waandishi habari kuhusiana na umahiri anaoupata katika kozi hizo, jijini Dodoma.
 Mwanafunzi wa kozi ya utayarishaji na mikato ya Nyama Victoria Massawe akizungumza na waandishi habari namna  ya kuandaa nyama kuanzia uchinjaji mpaka kumfikia mlaji leo jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wa kozi ya Ujenzi na Ukarabati wa Barabara wakionesha waandishi kuhusiana mafunzo wanayopata katika kozi hiyo.
Wanafunzi wa ukatibu muhtasi wakiwa darasani na mashine za kuchapa

NHIF YAWEKA KAMBI KWA RC MAKONDA KUSAJILI WATOTO NA BIMA YA AFYA

$
0
0
 Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF), wakiendelea na zoezi la usajili wa watoto kwenye bima ya afya ambao wanalipiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda.  Mpango wa TOTO AFYA KADI unamnufaisha mtoto chini ya umri wa miaka 18. 

Wafanyabiashara nchini kutafutiwa Soko Ufaransa

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), inaratibu ziara ya viongozi wa makampuni ya biashara zaidi ya 30 kutoka Ufaransa ambao ni wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Ufaransa (MEDEF) yenye mtandao wa makampuni zaidi ya 7100.

Ziara hiyo itakayofanyika kuanzia tarehe 15 – 18 Aprili 2018, inalenga kukuza ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa; kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania; kushawishi makampuni makubwa ya Ufaransa kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo nishati, miundombinu, viwanda, maji n.k na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania na Ufaransa kubadilishana uzoefu na kuanzisha ushirikiano baina yao.

Ukiwa nchini, ujumbe huo utapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa serikali na kushiriki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Ufaransa litakalofanyika tarehe 18 Aprili 2018, jijini Dar es Salaam. 

Aidha, baada ya kongamano hilo, Wizara kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) itafanya mkutano na wafanyabiashara Wakitanzania wenye nia ya kutafuta masoko nchini Ufaransa, tarehe 20 Aprili 2018. Ubalozi utaelezea fursa zilizopo nchini Ufaransa na mikakati ya kufanya bidhaa za Tanzania hususan za kilimo ziweze kuuzwa nchini humo.

Wizara inatoa wito kwa Wafanyabishara wa Tanzania kushiriki kikamilifu na kuchangamkia fursa hii muhimu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dar es Salaam
13 Aprili, 2018

Tulimuomba CAG afanye Ukaguzi Maalum kwa Kampuni ya Ubia ya StarMedia-Dkt. Harrison Mwakyembe

WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO

$
0
0
Watafiti wa Kodi Barani Afrika wameshauriwa kuimarisha mtandao wao ili kuweza kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika jitihada zao za kufanya utafiti.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John wakati akifunga warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) ambayo imeandaliwa na Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani Afrika (ATAF) kwa kushirikiana na Chuo cha Kodi (ITA).

Bw. Michael amesema kwamba watafiti hao wanategemewa sana na mamlaka za mapato wanazoziwakilisha hivyo kuwataka kutumia ujuzi wa utafiti walioupata wakati wa mafunzo hayo ya siku nne kutatua changamoto mbalimbali na kuziongezea uwezo mamlaka za mapato barani Afrika hivyo kupelekea kuongeza makusanyo.

“Nina imani kwamba baada ya mafunzo haya mtaendelea kushirikiana kupitia mtandao wenu ili kwa pamoja mtimize lengo lenu la kutatua changamoto katika utekelezaji wa taratibu, sheria na sera za kodi barani Afrika kupitia utafiti mtakaoufanya”.

Aidha amewataka watafiti hao kuzitumia vyema nyenzo za ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa ambazo wamepatiwa wakati wa mafunzo hayo ambayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo wa Rasilimali Watu na Utawala ameipongeza Taasisi ya Kodi Barani Afrika pamoja na Chuo cha Kodi kwa kuandaa na kufanikisha mafunzo hayo ambayo ni muhimu katika utendaji wa usimamizi wa Kodi barani Afrika.

Naye Mkuu wa Chuo cha Kodi Pro. Isaya Jairo ameishukuru ATAF na TRA kwa kukiamini Chuo cha Kodi kuendesha mafunzo kwa watafiti ambao wametoka nchi mbalimbali za Afrika. Ambapo pia amewapongeza washiriki hao kwa kupatiwa nafasi kushiriki mafunzo hayo akisema kwamba ushiriki wao unadhihirisha utayari wa mamlaka za mapato barani Afrika kutatua changamoto zilizopo kwa kuwa na watafiti wenye weledi na ujuzi.

Awali akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa Bw. Alfred Mregi alisema kwamba Usimamizi wa Kodi katika Afrika unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo watafiti wanategemewa kuzitatua ili taasisi zinazosimamia mapato Afrika ziwe rafiki kwa walipakodi na hatimaye kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani.

“Tunawategemea nyinyi kufanya utafiti wa mifumo ya kodi na kutoa suluhisho na mapendekezo kwa watunga sera na wasimamizi wa kodi”, alisema Bw. Mregi.

Warsha ya mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti Afrika iliwashirikisha watafiti kutoka baadhi ya nchi za Afrika ambao mapendekezo yao ya utafiti yamekidhi vigezo kwa mujibu wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani Afrika ambayo inaratibu Mtandao wa Wasimamizi wa Kodi Afrika kwa lengo la kuwajengea uwezo waafrika kufanya utafiti katika usimamizi, sheria na sera za kodi na kuwaunganisha watafiti hao na wanataaluma.

Washiriki wa warsha hii ambayo ni ya Tatu kufanyika, wameishukuru ATAF na Chuo cha Kodi kwa kuendesha mafunzo hayo wakisema kwamba imewapa uelewa zaidi wa kuendelea na utafiti wao.

Mafunzo hayo ambayo yaliendeshwa kwa lugha tatu: Kireno, Kifaransa na Kiingereza yaliwashirikisha washiriki 24 kutoka, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Niger, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Togo, Benin, Cape Verde, Tunisia, Ivory Coast, Kenya na Tanzania. 


JUMIA FIX MY HOUSE: It's time to turn your House to a HOME!!

$
0
0
It's time to turn your House to a HOME!!

What's the difference between a house and a home? A house is a structure that provides you basic needs and safety. A home is a place that provides you mental and emotional support, a place you look forward to being in to get away from the outside world.

Feeling like your home is lacking a bit of personality? There’s something powerful about walking into a house that feels like a home and reflects the owner’s personality so perfectly. Do you feel that way about your house? If not, do you wish to achieve a high-end luxurious look without blowing your budget? Believe it or not, your home can look expensive and luxurious without dragging you into debt. The key is to shop SMART...

One of the wonderful experience I had this weekend as I spent some time alone on the internet was to come across one of Jumia’s upcoming campaigns. The name made me look and look again, they call it Big Home Makeover!! Fascinating right?

An online survey released by Jumia Tanzania has revealed that 70% of Tanzanians households keep their home appliances for more than their life span citing sentimental value and uniqueness as opposed to old age.
“Large home appliances like dishwashers, microwaves, washing machines, refrigerators and furniture have an average lifespan of up to 10 years. They are a major investment for customers, and therefore people look for brands that will last. It is quite surprising to discover quite how long they keep them though! The survey showed that people keep them as long as possible - often up to 10 years or more”, said Jumia Head of Home and Living Appliances, Priscilla Eliphas.

I was impressed because at least Jumia Tanzania understands that a house makeover can be an expensive task, That is why they brought us home-lovers  a whole week of shopping for the best prices on home essentials like appliances, kitchen and dining, home decor, dishwashers, washers and dryers, fridges and freezers, ironing and laundry etc, from April 16th-26th.

We, home-lovers have to get ready for a week of the largest discounts as Jumia continues to partner with trusted brands to sell quality and affordable home appliances and offer up to 20,000 products to choose from.  Brands such as Samsung, Bruhm, Sony, Geepas, Nippotec, TCL, Star X, Philips, Aborder, Nikai, Ocean and Tronic.  They will also have some special surprises in the lead up to the event such as give aways, treasure hunts on their website, shopping vouchers etc, I personally can't wait!

Jumia is an online shopping platform that provides sellers and buyers the most convenient shopping and selling experience . A platform for vendors to display and sell their products directly to consumers all over Tanzania and for buyers to have the widest range of products to choose from with the best prices in the market. Jumia Tanzania provides a solution for everything you need, at the best price, with convenient fast home delivery (as quick as 2 days in Dar!) with a very simple process.

Browse the website for the product you need, add it to your online basket, then checkout and leave your details, and Jumia will deliver to your door.  What’s even better? You only pay on delivery!

Top  Reasons You Should shop during Home Makeover

  • Time to replace those old sufurias, mattresses, cookers, sofas, etc! save the date: 16th-26th April
  • Treat your house to a sparkling home makeover by simply - Pendezesha Nyumba na Jumia
  • No hustle and bustle of shopping downtown! - Pay cash on delivery all from the comfort of your home! How cool, right?
  • Enjoy the shortest delivery time on Jumia
  • Unbeatable Prices
  • Flash Sales – Get amazing deals on TV’s, cookers and mattresses duringthe campaign
  • Voucher Discounts-Shopping has never been so much fun! Get voucher discounts to enjoy your shopping  for less!
  • Over 20,000 products to choose from! Spoilt for choice with discounts of up to 60% off!

CHUO CHA UTALII CHAWATUNUKU VYETI MAMA LISHE, MADEREVA TAKSI 50 DAR

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
CHUO cha  Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam leo  kimewakabidhi vyeti Mama Lishe na madereva taksi 50 baada ya kuhitimu mafunzo ya utalii ikiwa ni muendelezo wa kukuza na kuboresha huduma za utalii nchini.

Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo yaliyochukua takribani wiki moja katika ukumbi wa chuo hicho Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Jiji  Sporah Liana amesema, mafunzi hayo yatakuwa ni muendelezo wa kukuza shughuli za utalii nchini na kuongeza uelewa wa Mama lishe na madereva taksi ambao mara nyingi wamekuwa wakitoa huduma kwa watalii bila elimu ya kutosha

"Tumegundua shughuli za utalii zinafanyika katika kila kona ya Jiji hili, tumegundua pia watallii wanapenda kula chakula kwa Mama lishe kwani ambao wengi wao hawana mafunzo ya kutosha.

"Tunajua wanaofanya kwenye mahoteli makubwa wengi wao wanasoma katika Chuo hiki tofauti na mama lishe ambao hawana mafunzo yoyote, tumeonelea no vizuri na mama lishe pia tuwalete katika mafunzo  ili waweza kujua namna  ya kutoa huduma kwa watalii wetu" amesema Liana.

 Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Liana akizungumza alipokuwa anafunga mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni mama lishe na madereva 50 baada ya kuhitimu mafunzo ya utalii ikiwa ni katika uboreshaji na kukuza huduma za utalii nchini.
Baadhi wahitimu wa mafunzo hayo ya utalii kwa wajasiriamali mama lishe na madereva wa taksi wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi 

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr Shogo Mlozi Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafunzo hayo ambayo yatawasaidia wajasiriamali hao katika kutoa huduma zenye viwango na kuongeza thamani ya huduma zao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VOA Swahili: Duniani leo 13th April 2018

WAZIRI MWAKYEMBE NA WAZIRI MWIJAGE WAKIJIBU HOJA ZA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI

$
0
0
 Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitoa ufafanunuzi kuhusu hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu mkataba kati ya kampuni ya ubia ya StarMedia na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Fillip Mpango (katikati) na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kushoto) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akifawafafanulia jambo wakati wa kikao cha Mawaziri hao na waandishi wa habari kufafanua hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu wizara zao, leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitoa ufafanunuzi kuhusu hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu utoaji wa huduma saidizi kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini, leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ufafanunuzi wa hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zilizohusu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa ufafanunuzi kuhusu hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu utoaji wa huduma saidizi kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini, leo mjini Dodoma. 
 Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (katikati) na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati wa ufafanunuzi wa hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zilizohusu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Viwanda na Biashara leo mjini Dodoma.

Dkt. Harrison Mwakyembe Atoa Maagizo Mazito kwa Uongozi wa StarMedia na TBC

Executive Director of Under the Same Sun Tanzania Vicky Ntetema retiring in May.

$
0
0
Dear Friend of Under The Same Sun Tanzania:

I am writing today to inform you about a recent change in the leadership of our Tanzanian office. Our Executive Director, Vicky Ntetema (pictured)  is retiring in May.

Vicky and I began our work together fighting for the rights of persons with albinism almost 10 years ago. She has worked with us as our Executive Director for the past eight years.

Her years of service in the fight for the rights of persons with albinism has been exemplary. Many of you know about the great work she did within the country and beyond in this area. Her dedication to the cause has been truly inspiring.

The Important work of UTSS in Tanzania will continue under the capable leadership of our acting Executive Director, Ester Rwela. Ester has been with us serving in a variety of capacities, and most recently as part of the management team in the role of Program Manager. 

Any inquiries that would normally be directed to Vicky should now be directed to Ester at the following email address: ester@utss.co.tz or mulungiester@gmail.com.

Thank you so much for your alliance with Under The Same Sun.

Peter Ash
Founder/CEO
Under The Same Sun
CANADA 

UDART YAWAPA JUKUMU TTCL KUKUSANYA NAULI MABASI YA MWENDO KASI DAR

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
KAMPUNI ya Huduma ya Mradi wa mabasi ya mwendo kasi (UDART) imefanya marekebisho katika mfumo wa utoaji huduma hasa katika ukusanyaji wa nauli kutoka kampuni ya Max com Afrika na sasa utafanywa na Shirika la simu la Taifa (TTCL)

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Idara ya Mawasiliano (UDART) Deus Bagaywa ameeleza baada ya mkataba na Max Com Afrika kuisha baada ya kudumu takribani kwa miaka miwili kuanzia Mei 2016 hadi leo Aprili 14, hivyo wameamua kuwa na mkataba na TTCL kampuni iliyokuwa inawasaidia hapo awali na hii ni kwa lengo la kuboresha huduma zaidi na ukiangalia shirika la TTCL limeboresha sana mitambo yao.

Kuhusu wafanyakazi waliokuwa wanatoa huduma katika vituo vya mabasi mabadiliko hayo hayatawaathiri, Bugaywa ameeleza wafanyakazi 191waliokuwa wanafanya kazi kupitia Maxcom Afrika na kulipwa na UDART wataendelea na kazi na kubadilishiwa mikataba hivyo hawataathirika.

Aidha ameeleza changamoto zitajitokeza kwa siku mbili hizi ila watajitahidi kutoa huduma kwa ufasaha.

Kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Bugaywa ameeleza kuwa wamejiandaa na mipango ya dharura na wanachukua tahadhari  hivyo wananchi wawe na imani na usafiri huo.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mabadiliko ya utoaji huduma kutoka Maxcom Afrika kwenda kwa Shirika la simu la taifa (TTCL)(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii)

Prof Adolf Mkenda to grace 2nd meeting of the EAC Joint Facilitative Committee in Arusha

$
0
0
President of the African Court Hon Sylvain Oré (r) hands over Court’s information materials to the Permanent Secretary of Tanzania’s Ministry of Foreign Affairs and EA Co-operation Prof Adolf Mkenda before the start of the 2nd meeting of the Joint Facilitative Committee in Arusha  yesterday. Watching on (left) are senior Ministry officials.  

Registrar of the African Court Dr Robert Eno (l) explains on the Court’s Library operations to the Permanent Secretary of Tanzania’s Ministry of Foreign Affairs and EA Co-operation Prof Adolf Mkenda and his delegation before start of the 2nd meeting of the Joint Facilitative Committee in Arusha on yesterday.

SALAMBA MCHEZAJI BORA MWEZI MACHI LIGI KUU YA VODACOM

$
0
0
MSHAMBULIAJI wa Lipuli ya Iringa, Adam Salamba amechaguliwa kuwa  Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)Tanzania Bara. Salamba alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Salum Kimenya wa Prisons na kipa wa Azam, Mwadini Ally katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na Kamati ya Tuzo hizo.

Mshambuliaji huyo kwa Machi alionesha uwezo mkubwa na kuisaidia timu yake kupata mafanikio akifunga mabao matatu kwa dakika 270 alizocheza, ambapo Lipuli ilicheza michezo mitatu ikishinda miwili na kutoka sare mmoja na kupanda kwa nafasi moja kutoka ya nane hadi ya saba kwa mwezi huo.

Kwa upande wa Kimenya alicheza dakika 269 na kufunga mabao mawili, akiiwezesha Prisons kushinda michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza na kutoka sare mmoja, ikipanda kutoka nafasi ya tano hadi ya nne. Mwadini yeye alicheza dakika zote 270 ambazo timu yake ilicheza kwa mwezi Machi, ikishinda michezo yote mitatu iliyocheza, ikibaki katika nafasi yake ya tatu.

Kutokana na ushindi huo, Salamba atazawadiwa tuzo, kisimbusi cha Azam na fedha taslimu sh. Mil. Moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.

Wachezaji wengine ambao tayari wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi wa VPL msimu huu na miezi yao katika mabano ni mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).

Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco (Januari) na kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari).

Tuzo za Mchezo Bora wa jumla wa Ligi Kuu Tanzania Bara zinatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu katika tarehe itakayotangazwa, ambapo licha ya Mchezaji Bora, pia kutakuwa na tuzo nyingine tofauti kwa kategori mbalimbali.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA UNICEF NA BALOZI WA JAPAN LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF nchini Bi. Maniza Zaman aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF nchini Bi. Maniza Zaman leo ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshinda ofisini kwa  Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshinda ofisini kwa  Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) ​

Habari za UN: Machungu ya Grace!

GLOBAL TV HABARI: MSANII NANDY AJISALIMISHA BASATA SAKATA LA VIDEO CHAFU

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images