Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MABONDIA KUONESHANA UMWAMBA MEI 5, 2018 IDD MKWERA NA RAMADHANI SHAURI KUWAONGOZA

$
0
0

Bondia Idd Mkwera baada ya kupoteza mpambano wake wa nje uliofanyika Riga Ratvia kwa point bondia huyo sasa amesaini mkataba wa kuzipiga na bondia machachari Ramadhani Shauri mpambano wa raundi 10 utakaofanyika Mei 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa

Akizungumza wakati wa utaiaji saini uho Mkwera amesema kuwa yeye anachojua ngumi ndio kazi yake hivyo kwake kazi ni kazi tu aijalishi anacheza na nani hivyo kuwataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kushudia mpambano uho wa masumbwi siku hiyo.
Akijibu mapigo Shauri amesema wapenzi wangu na mashabiki zangu mmenikosa tangu mwaka jana nilivyopoteza kwa pointi katika uwanja ule ule sasa nilitoka kidogo nje ya Tanzania hivyo nimerudi na kasi mpya nguvu mpya njoeni mshidie ngumi zinavyopigwa.
Nae Promota wa mchezo huo Evalist Ernest alisisitiza kwa kusema mabondia hawa watacheza mpambano wa raundi 10 katika uzito wa kg 62.5 hivyo muje mushudie masumbwi siku hiyo mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi kwa vijana tulio wasainisha.
Siku hiyo bondia Haidari Mchanjo atazichapa na Amani Bariki 'Manny Chuga' wakati Karimu Ramadhani atakumbana na Jerms Kibazange   na Said Chini ataoneshana umwamba na Hamza Mchanjo.

Mapambano hayo na mengine yote yatakuwa wakisindikiza pambano kuu kati ya Idd Mkwera na Ramadhani Shauri watakaozipiga Raundi kumi

Siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua mpaka kujua kitu kamili katika 
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd 
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Promota wa mpambano wa ngumi Evalist Ernest katikati akiwainua mikono juu mabondia Iddi Mkwera kushoto na Ramadhani Shauri baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Mei 5 katika ukumbi wa Uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS

Article 0

MICHUZI TV GOSSIP: SAKATA LA NANDY

Sekta binafsi Zanzibar yajadili mikakati madhubuti ya kufanikisha wiki ya Tanzania nchi Kenya

$
0
0
Waziri Wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum akizungumza katika ufunguzi wa mkutano na Wafanyabishara wa Zanzibar  uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko  tarehe 13 Aprili 2018. 

Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hassan Khamis Hafidh  na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Katibu wa Kamati ya Taifa ya maandalizi ya maonesho ya bidhaa za Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega.
Katika ufunguzi huo Mhe. Waziri Amina aliwasisitiza wafanyabiashara hao kushiriki katika maonesho pamoja na umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Diplomasia ya uchumi kwa vitendo.
Balozi Anisa Mbega akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya maonyesho pamoja na kutoa ufafanuzi wa matukio mengine yatakayoambatana na maonyesho hayo kama vile kongamano la biashara, maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanzania.

Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Saleh akiwahamasisha wafanyabishara kushiriki maonesho hayo pamoja na kuhakikisha wanafanya maandalizi ili kuweza kukamilisha vigezo na masharti ya ushiriki.

Juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikiwasilishwa na viongozi.

Mkutano ukiendelea.


WAHAMIAJI HARAMU TISA RAIA WA ETHIOPIA NA MTANZANIA MMOJA WALIVYODAKWA NA POLISI MORO.

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro
POLISI Mkoani Morogoro inawashikilia  wahamiaji haramu tisa ambao ni wa Ethiopia na Mtanzania mmoja ambaye ni dereva aliyekuwa anawasafirisha kwa gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili  T229 DBW ikitoka Dar es Salaam kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
Kamanda wa Polisi wa  mkoa wa Morogoro , Ulrich Matei  alisema  kuwa tukio la kukamatwa kwa raia hao lilitoke Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi , mkoani Morogoro katika barabara ya Morogoro- Iringa.
Kamanda Matei alisema, raia hao  walikuwa wamepakiwa wakiwa wamefichwa katika chasis ya gari hilo  baada ya kutandazwa mbao ambalo lilikuwa  likiendshwa na  Mbaruku Kassim (40) mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam ikitkea  kutokea Jijini humo kuelekea Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
Aliwataja raia hao wa Ethiopia waliokamatwa ni Taka Desta (24), Muluma Achiso (22), Mintensinot Workineh (23),Tesfhun Getachew (19), Muligeta Lalago (19), Zachewo Tikaso (20),Sekadu Abate (14), Asra Said (18) na Esafa Ercafo (22).
“ Raia hawa walihifadhiwa chini ya chisis ya gari baada ya kuwekwa mbao na wao kujificha eneo hili jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao ,  kitendo hiki ni kibaya “ alisema Matei.
Hata hivyo alisema , Polisi itaendelea  kufanya ukaguzi na  msako mkali  katika maeneo ya njia zote kuu za mkoa huo ili kukomesha biashara hiyo haramu na watakaokamatwa wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 Kwa mujibu wa Kamanda wa mkoa  kuwa, watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa ili waweze kukabidhiwa kwa Idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kuwafikisha mahakamani.
 Kamanda wa Polisi Morogoro, Ulrich Matei  akitoka kukagua gari iliyokamatwa na  wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia, Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye  gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili  T229 DBW iliyokuwa ikiendeshwa na Mbaruku Kassim (40) ( mwenye shati ya miraba mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam  wakitokea  Jijini humo  kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
 Kamanda wa Polisi Morogoro, Ulrich Matei  akitoka kukagua gari iliyokamatwa na  wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia, Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye  gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili  T229 DBW iliyokuwa ikiendeshwa na Mbaruku Kassim (40) ( mwenye shati ya miraba mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam  wakitokea  Jijini humo  kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
 Kamanda wa Polisi Morogoro, Ulrich Matei  akisoma majina ya wahamiaji haramu tisa raia wa Ethiopia walikamatwa  Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye  gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili  T229 DBW iliyokuwa ikiendeshwa na Mbaruku Kassim (40) ( mwenye shati ya miraba mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam likitokea Jijini humo  kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.
Wahamiaji haramu  tisa raia wa Ethiopia akiwemo na Mtanzania mmoja  ambaye ni dwereva  aliyetambuliwa kwa jina la  Mbaruku Kassim (40) mkazi wa Tabata  Jijini Dar es Salaam   ( wanne kutoka kushoto) wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kukamatwa  Aprili 10, mwaka huu ( 2018) majira ya saa mbili asubuhi eneo la Msimba , Kata na Tarafa ya Mikumi ,mkoani Morogoro wakisafirishwa kwenye  gari  lenye namba za usajili  T 682 DCB aina ya FAW likiwa na tela lenye namba za usajili T229 DBW  wakitokea  Jijini humo  kuelekea  Afrika Kusini kupitia mpaka wa Tunduma.( Picha na John Nditi).

HALMASHAURI KIGAMBONI KUFUNGUA KIDATO CHA TANO,SITA JULAI MWAKA HUU

$
0
0
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni inatarajia kufungua kidato cha tano na sita Julai mwaka huu katika Shule ya Sekondari Nguva kwa kuwa na wanafunzi 160 wa kiume pekee ikiwa na michepuo ya PCM,PCB,HGE na EGM. 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba amesema kuwa katika kutatua changamoto ya ukosefu wa Shule ya Sekondari yenye kidato cha tano na sita kwenye Halmashauri, na kutimiza maelekezo ya Serikali kwa kila Halmashauri kuwa na shule ya kidato cha tano na sita, Manispaa iliamua kuboresha miundombinu ya Shule ya Nguva ili iweze kukidhi mahitaji hayo. 

Aidha amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa thamani ya shilingi 492,864,576 kwa kushirikiana na Serikali kuu, ambapo Serikali kuu imeweza kuchangia kiasi cha shilingi 259,000,000 na vyanzo vya ndani vya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ilichangia shilingi 233,864.576. 

Mkurugenzi amesema kwamba ili kuhakikisha Shule ina hadhi ya kidato cha tano na sita kwa mujibu wa vigezo vya wizara, ujenzi wa mabweni mawili kwaajili ya wanafunzi, vyoo, ujenzi wa daharia ambao bado unaendelea, ujenzi wa madarasa manne na ununuzi wa madawati, ununuzi wa vitanda kwaajili ya mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa maabara ya sayansi na ujenzi wa jengo la utawala linalojengwa kwa juhudi za Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda vimefanyika . 
 Muonekano wa ubavuni wa jengo la bweni la wanafunzi  
  moja ya chumba cha wanafunzi ndani ya bweni  ​
 korido la moja ya bweni litakalotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano
 ujenzi wa jengo la utawala ukiendelea
moja ya jengo la maabara ya kisayansi

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUJADILI UTEKELEZAJI WA SHERIA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

$
0
0



  
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA

SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia, lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama mjini Dodoma mwishoni Aprili 13, 2018, wakati akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma) na Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mhe. Waziri alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.

“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Waziri.

Aidha Mhe. Waziri alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akihutubia wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Eric Shitindi, akitoa hotuba ya ukaribisho wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhsuu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.



Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.


Mkutano ukiendelea.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO

$
0
0
Watafiti wa Kodi Barani Afrika wameshauriwa kuimarisha mtandao wao ili kuweza kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika jitihada zao za kufanya utafiti.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John wakati akifunga warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) ambayo imeandaliwa na Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani Afrika (ATAF) kwa kushirikiana na Chuo cha Kodi (ITA).

Bw. Michael amesema kwamba watafiti hao wanategemewa sana na mamlaka za mapato wanazoziwakilisha hivyo kuwataka kutumia ujuzi wa utafiti walioupata wakati wa mafunzo hayo ya siku nne kutatua changamoto mbalimbali na kuziongezea uwezo mamlaka za mapato barani Afrika hivyo kupelekea kuongeza makusanyo.

“Nina imani kwamba baada ya mafunzo haya mtaendelea kushirikiana kupitia mtandao wenu ili kwa pamoja mtimize lengo lenu la kutatua changamoto katika utekelezaji wa taratibu, sheria na sera za kodi barani Afrika kupitia utafiti mtakaoufanya”.Aidha amewataka watafiti hao kuzitumia vyema nyenzo za ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa ambazo wamepatiwa wakati wa mafunzo hayo ambayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo wa Rasilimali Watu na Utawala ameipongeza Taasisi ya Kodi Barani Afrika pamoja na Chuo cha Kodi kwa kuandaa na kufanikisha mafunzo hayo ambayo ni muhimu katika utendaji wa usimamizi wa Kodi barani Afrika.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John akimkabidhi mshiriki kutoka Tunisia Bw. Jabali Belhanssen cheti cha ushiriki wa mafunzo ya utafiti ambayo yafanyika jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Afrika (ATAF) na Chuo cha Kodi (IAT). Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi na Mwakilishi ATAF Bw. Eugenio Bras.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John (katikati) akifuatilia matukio wakati wa kufunga na kukabidhi vyeti kwa washiriki wa warsha ya mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) ambayo imefanyika jijini Dar es salaam. Wengina kutoka kushoto ni; Mkufunzi wa mafunzo hayo Prof. Nicaise Mede kutoka Benin, Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi na Mwakilishi wa Taasisi ya Utafiti Barani Afrika (ATAF) Bw. Eugenio Bras.
Baadhi ya washiriki wa Warsha ya Mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) waliosimama wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John (aliyekaa katikati) baada ya kufunga mafunzo hayo. Wengine kutoka kulia ni, Mwakilishi wa Taasisi ya Utafiti Barani Afrika (ATAF) Bw. Eugenio Bras, Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi, Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo na Mkufunzi wa mafunzo hayo Prof. Nicaise Mede kutoka Benin

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KATIBU MKUU TARISHI ATETA NA KIKOSI KAZI CHA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI CHA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

$
0
0
Na. Mwandishi Maalum

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ni Taasisi mojawapo iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi amekutana na Kikosi Kazi cha Tume hiyo kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma, lengo ni kuangalia namna serikali inavyoweza kusaidia kwa maeneo inayoruhusiwa kikatiba katika kuwasaidia kutekeleza majukumu yake.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 5 kifungu kidogo cha 3 (a) ambacho kimeweka uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini na Ibara ya 74 kifungu kidogo cha 6 (a) na (e), kinaipa Tume madaraka ya kuchukua jukumu la kuandikisha wapiga Kura nchini Tanzania.

Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 15 (3) kinaipa madaraka Tume ya Uchaguzi kutengeneza mfumo na utaratibu wa uandikishaji wa wapiga Kura nchini na uboreshaji wa daftari hilo mara mbili kati ya Uchaguzi mkuu mmoja na unaofuata. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni miongoni mwa Taasisi ambazo zipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi hiyo ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akifuatilia kikao na Kikosi kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi, leo mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akiongoza kikao na Kikosi kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura walipokutana leo mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.
Mkurugenzi Idara ya Sera na Bunge Ofisi ya Waziri Mkuu,Yona Mwakilembe akitoa ufafanuzi katika kikao hicho wakati Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kilipokutana na Katibu Mkuu (hayupo pichani) leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachohusika na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura wakifuatilia kikao na Katibu Mkuu (hayupo pichani) leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.

WASHINDI WA NYAKANYAKA BONUS KILIMANJARO WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

$
0
0
 Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania - Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka (kushoto) akimkabidhi Rahma Msangi (kulia) zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka kama mmoja kati ya washindi saba wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus katika mkoa wa Kilimanjaro. Tigo imetoa jumla ya simu 84 kwa wateja wake kutoka sehemu mbali mbali katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus wiki hii.
 Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania, Kanda ya Kaskazini ,Nancy Bagaka (kushoto) akimkabidhi mwalimu wa chekechekea Maulidi Hussein  (kulia) zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka kama mmoja kati ya washindi saba wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus katika mkoa wa Kilimanjaro. Tigo imetoa jumla ya simu 84 kwa wateja wake kutoka sehemu mbali mbali katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus wiki hii.
 Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania, Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka (kushoto) akimkabidhi dereva wa daladala, Ally Omari (kulia) zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka kama mmoja kati ya washindi saba wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus katika mkoa wa Kilimanjaro. Tigo imetoa jumla ya simu 84 kwa wateja wake kutoka sehemu mbali mbali katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus wiki hii.
Washindi wa simu janja aina ya Tecno R6 kwa Mkoa wa Kilimanjaro katika promosheni ya Tigo Nyakanyaka Bonus wakionesha zawadi zao mara baada ya kukabidhiwa zawadi hizo mjini Moshi na Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka (kushoto).  Tigo imetoa jumla ya simu 84 kwa wateja wake kutoka sehemu mbali mbali katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus wiki hii.

KATIBU MKUU TARISHI ATETA NA KIKOSI KAZI CHA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI CHA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ni Taasisi mojawapo iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi amekutana na Kikosi Kazi cha Tume hiyo kinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma,  lengo ni kuangalia namna serikali inavyoweza kusaidia kwa maeneo inayoruhusiwa  kikatiba katika  kuwasaidia kutekeleza majukumu yake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 5 kifungu kidogo cha 3 (a) ambacho kimeweka uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini na Ibara ya 74 kifungu kidogo cha 6 (a) na (e), kinaipa Tume madaraka ya kuchukua jukumu la kuandikisha wapiga Kura nchini Tanzania.
Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 15 (3) kinaipa madaraka Tume ya Uchaguzi  kutengeneza mfumo na utaratibu wa  uandikishaji wa wapiga Kura nchini na uboreshaji wa daftari hilo mara mbili kati ya Uchaguzi mkuu mmoja na unaofuata.     
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni miongoni mwa Taasisi ambazo zipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi hiyo ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akifuatilia  kikao na Kikosi kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi, mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akiongoza kikao na Kikosi kazi  cha Tume ya Taifa ya Uchaguzikinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura walipokutana mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.
 Mkurugenzi Idara ya Sera na Bunge Ofisi ya Waziri Mkuu,Yona Mwakilembe akitoa ufafanuzi katika  kikao hicho wakati Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi  kinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kilipokutana na Katibu Mkuu (hayupo pichani) tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa  Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi  kinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura wakifuatilia kikao na  Katibu Mkuu (hayupo pichani) tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.

JESHI LA POLISI LAKAMATA SILAHA,WATUHUMIWA WA UHALIFU 368

$
0
0
Na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kukamata Silaha mbalimbali na watuhumiwa 368 katika Oparesheni Maalum inayoendelea katika Ukanda wa Kusini unaojumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Akizungumza mkoani Mtwara, Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kati ya watuhumiwa 368, 13 tayari wamefikishwa Mahakamani, 152 wamekabidhiwa Idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi, tisa wapo chini ya Upelelezi na 194 wapo chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee).

Sabas amezitaja Silaha zilizokamatwa kuwa ni pamoja na SMG mbili, Pistol tano, Shotgun moja na risasi 145,  Visu 96, Makoti ya Sare za Jeshi la Msumbiji mawili, Raba za Jeshi la Msumbiji jozi mbili pamoja na vifaa vya kutengenezea milipuko. 

“Baadhi ya watuhumiwa ni wale waliokimbia katika Operesheni yetu ya Mkoa wa Kipolisi Rufiji baada ya kuwazidi nguvu na sasa nawaambia tu wajisalimishe kwani hatuna mchezo hata wakimbilie wapi mana tumepata taarifa kuwa wamejificha nchini Msumbiji lakini kule napo wameanzisha operesheni kama hii“. Alisema Sabas.

Aidha Kamanda Sabas amesema Operesheni hiyo  ni endelevu na inashirikisha vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama hivyo ametoa wito kwa raia wema kuendelea kutoa taarifa za siri ili kuendeleza amani na usalama hapa nchini.

Hivi karibuni Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchini Msumbiji alikutana na IGP Simon Sirro jijini Dar es Salaam kwa lengo kuboresha ushirikiano katika mapambano ya uhalifu unaovuka mipaka ambayo ndio imekuwa changamoto katika nchi mbalimbali.
Mkuu wa Operesheni maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha baadhi ya Silaha zilizokamatwa katika Operesheni  maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu inayoendelea katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma. Wengine ni Maofisa mbalimbali waliopo katika Operesheni hiyo. (Picha na Jeshi la Polisi).

BONDIA MKWERE ASAINI MKATABA WA KUZICHAPA NA SHAURI

$
0
0


BONDIA Idd Mkwera amesaini mkataba wa kuzipiga na bondia machachari Ramadhani Shauri katika mpambano wa raundi 10 utakaofanyika Mei 5 mwaka huu Uwanja wa Ndani wa Taifa.

Mkwera amesaini mkataba huo ikiwa ni siku chache zimepita tangu apoteza mpambano wake wa nje uliofanyika Riga Ratvia kwa point. Akizungumza wakati wa utaiaji saini huo leo, Mkwera amesema yeye anachojua ngumi ndio kazi yake,hivyo kwake kazi ni kazi tu na haijalishi anacheza na nani. Hivyo amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kwenda kushudia mpambano huo.

Akijibu mapigo Shauri amesema wapenzi wangu na mashabiki zangu wamemikosa tangu mwaka jana alivyopoteza pointi katika uwanja ule ule. "Sasa nilitoka kidogo nje ya Tanzania hivyo nimerudi na kasi mpya nguvu mpya njoeni mshuhudie ngumi zinavyopigwa," amesema.

Kwa upande wa Promota wa mchezo huo Evalist Ernest amesisitiza kuwa mabondia hao watacheza mpambano wa raundi 10 katika uzito wa kg 62.5. "Hivyo mje mshuhudie masumbwi siku hiyo mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi kwa vijana tulio wasainisha," ameongeza

Hivyo siku hiyo bondia  Haidari Mchanjo atazichapa na Amani Bariki 'Manny Chuga' wakati Karimu Ramadhani atakumbana na Jerms Kibazange   na Said Chini ataoneshana umwamba na Hamza Mchanjo. Mapambano hayo na mengine yote yatakuwa wakisindikiza pambano kuu kati ya Idd Mkwera na Ramadhani Shauri watakaozipiga Raundi kumi 

Pia watatumia siku hiyo kuuza DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani.
Promota wa mpambano wa ngumi, Evalist Ernest katikati akiwainua mikono juu mabondia Iddi Mkwera (kushoto) na Ramadhani Shauri (kulia) mara baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Mei 5 katika ukumbi wa Uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi kumi. Picha na SUPER D BOXING NEWS

WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU

$
0
0

RS TABORA

SERIKALI imezitaka jamii kujiunga na mifuko ya huduma za bima za jamii ili waweze kupata huduma ya tiba kwa gharama nafuu badala ya kutumia mtindo wa kulipa fedha taslimu wanapokwenda kutibiwa.

Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Nzega na Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na wakazi wa Zogolo mara baada ya kukizindua.

Alisema kazi wananchi ambapo hajajiunga na Mifuko ya Afya ya Jamii(CHF) na mingine wanajikuta wakitumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu wakati wangekata Bima za viwango tofauti wangenufaika.

Waziri huyo alisema mtu akimkatia mtoto wake mdogo Bima ya Afya ya shilingi elfu 50 atapata huduma za matibabu mwaka mzima katika Hospitali yoyote hapa nchini zikiwemo za binafsi ambazo zina makataba na Serikali kupitia Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa. Aliwataka Madereva wa boda boda wilayani Nzega nao kujiunga na Bima kwa kulipia shilingi 76000 ili waweze kupata matatibu mwaka mzima popte pindi wanapopata ajali au wanapougua na kuongeza kuwa kwa kutegemea fedha taslimu ni gharama kubwa.

Waziri huyo aliwambia wakijunga pamoja na kutoa kiasi hicho atawaunganisha ili waweze kupata vitambulisho vya Bima ambavyo vitawaweze kupata matibabu kwa gharama nafuu na fedha nyingine kuzielekeza katika shughuli nyingine za maendeleo. “unapokwenda kufanyiwa upasuaji unaweza kutozwa shilingi 100,000/- lakini ukiwa umetoa shilingi elfu 30 kupitia kujiunga Mfuko wa Afya ya Jamii , utatumia kadi kupata huduma hiyo katika Hospitali yoyote bila kudaiwa chochote” alisisitiza Ummy

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri alisema kuwa mwitikio wa wananchi Mkoani humo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) bado uko chini na kuongeza kuwa wameamua kuendesha elimu kupitia mikutano mbalimbali kwa lengo la kuongeza idadi inaongezeka.

Alisema kuwa sehemu kubwa ya wakazi ni wakulima ambao wanategemea mavuno ya msimu kujipatia kipato kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ikiwemo matibabu na hivyo kupata shida wakati mwingine kwa kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama kwa fedha tasilimu kwa kuwa fedha zinakuwa hazipo tena hadi mavuno mengine.

Mwanri alisema njia ya pekee ya kuwasaidia wakulima ni kuhakikisha wengi wao wamejiunga na Mfuko wa Jamii ambapo wakitoa shilingi 10,000 wanapata matibabu watu sita katika familia moja.

MTOTO WA MKULIMA WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA ATAJA MUAROBAINI WA KUZUIA UCHOMAJI MISITU

$
0
0

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA

WAKATI kuna wimbi la uchomaji misitu ovyo hapa nchini, “Mtoto wa Mkulima, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda ametoa “dawa” ya kuzuia uharibifu huo wa maliasili na si nyingine bali ni kufuga nyuki.

Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye alipenda kujitambulisha kama mtoto wa mkulima kutokana na mapenzi yake katika Kilimo, alitoa “elimu” hiyo leo Aprili 14, 2018 wakati akizindua nembo ya “Malkia wa Asali Tanzania” kwenye Hoteli ya Morena mjini Dodoma. 

“Sisi upande wa Katavi tulichofanya, nilmwambia mkuu wa Mkoa sisi kuchoma choama misitu ni “tradition” (utamaduni) yaani kuchoma ni jambo la kawaida na ukitaka kuzuia hili jaribu kutumia ufugaji wa nyuki kama silaha ya kuzuia uchomaji wa miti.” Alisema na kuendelea. 

Kwa hivyo alichofanya maeneo kama Inyonga, tulitenga maeneo na kuweka mabango yetu tukaweka wafugaji wa nyuki na kuwaambia ninyi ndio walinzi wetu na tangu tufanye hivyo kumekuwepo na hali nzuri sana, na uchomaji moto umepungua sana, alisema. 

Mheshimiwa Pinda alitoa mfano mwingine jijini Mbeya (Mbeya city), ambako mji umezungukwa na milima mizuri yenye misitu ambayo imekuwa ikiharibiwa na uchomaji moto mara kwa mara. 

“Alitokea baba mmoja Askofu Mwalyego siku moja akaja kuniambia baba mimi hii inanikera kama inavyokukera sana wewe, hivi nikijaribu ku-introduce ufugaji wa nyuki hapa itasaidia, nikamwambia try (jaribu), ameweka wafugaji wa nyuki kuzunguka milima pale Mbeya mjini na mimi nikamwambia I will buy all your honey na juzi nikawa namuuliza zoezi langu linakwendaje, akaniambia nina miaka miwili mitatu sijaona moshi kwenye lile eneo. 
Mhe. Pinda akiangalia Mvinyo (wine), uliotengenezwa na kampuni ya Nyuki safari ikiwa na nembo mpya ya Malkia wa Asali. 
Mhe. Pinda akiungana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Kuandikwa, (wapili kulia), Mbunge wa Urambo, Mhe. Margareth Sitta, (wakwanza kushoto), Mwanzilishi mwenza na Afisa Mkuu Mbunifu wa kampuni ya kuzalisha asali ya Nyuki Safari, Mary Winzer Canning, (wanne kushoto), na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Profesa Silayo na mrembo aliyebeba nembo hiyo. 
Mhe. Pinda na wageni wengine wakishiriki kwenye uzinduzi wa nembo hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Balozi Luvanda awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Sri Lanka

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa Maithripala SIRISENA.

Hii ni hatua muhimu katika kuendeleza, kuimarisha na kukuza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano mwema uliopo kati ya Tanzania na Sri Lanka ambao ulianza mnamo miaka ya tisini. Wakati huo, Sri Lanka ilikuwa inawakilishwa nchini Tanzania kupitia Ubalozi wake wa mjini Kampala, Uganda ambao baadaye ulifungwa na Tanzania ikiwakilishwa nchini Sri Lanka kupitia Ubalozi wake wa New Delhi. Kwa sasa Sri Lanka inakusudia kumteua Balozi wake mjini Nairobi ambaye pia ataiwakilisha nchi hiyo nchini Tanzania.

Katika hafla hiyo, Balozi Luvanda aliambatana na Mwambata Jeshi wa Tanzania nchini India, Col.Amri Salim MWAMI. Aidha, Balozi Luvanda alifanya mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Sri Lanka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Afrika, ambapo ameahidi kushirikiana kwa karibu na watendaji hao katika kudumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili na ambao utazinufaisha zaidi, hususan katika kuhakikisha uhaulishaji wa uzoefu, teknolojia na utaalam wa Sri Lanka kwa Tanzania kwenye sekta ya viwanda vya nguo, madini na vito mbali mbali na kilimo.

Sri Lanka ni nchi yenye uchumi unaoendelea ingawa imepitia kipindi kigumu cha vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa takriban miaka 25, vita ambavyo vilimalizika mwaka 2009.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto) ambaye anawakilisha pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Maithripala SIRISENA, Rais wa nchi hiyo
Balozi Luvanda akisalimiana na maafisa waandanizi wa Ikulu ya Sri Lanka
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa Maithripala SIRISENA.

EPZA ,TCCAI KUSHIRIKIANA KATIKA KUHAMASISHA WAZAWA KUWEKEZA

Naibu Waziri akutana na kufanya mazungumzo na Spika EALA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Martin Ngoga wakisalimiana walipokutana kwa mazumgumzo katika Ofisi za Wizara Dodoma.

Mhe. Ngoga alimtembelea Naibu Waziri Mhe. Dkt. Kolimba Ofisini kwake ambapo walifanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Jumuiya. Mhe. Dkt.Kolimba katika mazungumzo hayo amemwahidi Spika wa EALA kuwa Wizara na Serikali kwa ujumla itatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge hilo katika utelezaji wa majukumu yake.

Aidha kwa upande wake Spika wa EALA amesema kuwa,kwa sasa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanadumisha ushirikiano na Mabunge ya Nchi wanachama na kutoa mrejesho kwa Nchi wanachama kuhusu masuala mbalimbali ya yanayojili katika Bunge hilo.

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki linafanya vikao vyake mjini Dodoma kuanzia tarehe 9 hadi 28 Aprili, 2018 
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Martin Ngoga akisaini kitabu cha wageni mara baada kuwasili Wizarani Dodoma. 
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Kolimba na Spika wa EALA Mhe. Dkt.Ngoga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge wa EALA na Maafisa kutoka Wizarani na Bunge la EALA 

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AFUNGUA KIKO CHA WAFANYAKAZI IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII MJINI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na watumishi wa Idara Kuu anayoiongoza katika Kikao cha wafanyakazi kilichofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma kilicholenga kukumbushana masuala mbalimbali ya kiutendaji ili kuboresha utendaji kazi na huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Raphael Nombo akifafanua masuala mbalimbalia ya Kiutawala na Kiutumishi kwa watumishi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii katika Kikao cha wafanyakazi kilichofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma kilicholenga kukumbushana masuala mbalimbali ya kiutendaji ili kuboresha utendaji kazi na huduma kwa wananchi.
Afisa Utumishi Bi. Daina Lumelezi akieleza yatokanayo na Kikao kilichopita kwa Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na na watumishi katika Kikao cha wafanyakazi kilichofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma kilicholenga kukumbushana masuala mbalimbali ya kiutendaji ili kuboresha utendaji kazi na huduma kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bi. Sophina Mjangu akiwasilisha Sura ya Bajeti kwa Mwaka 2018/2019 kwa watumishi wa Idara Kuu anayoiongoza katika Kikao cha wafanyakazi kilichofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma kilicholenga kukumbushana masuala mbalimbali ya kiutendaji ili kuboresha utendaji kazi na huduma kwa wananchi.
Baadhi ya watumishi wakifuatilia kikao kati yao na Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani) kilichofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma kilicholenga kukumbushana masuala mbalimbali ya kiutendaji ili kuboresha utendaji kazi na huduma kwa wananchi.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images