Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 13,2018


WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUMIA BANDARI YA TANGA

$
0
0

MENEJA wa Bandari ya Tanga Privical Salama amewataka wafanyabiashara nchini kuendelea kutumia bandari ya Tanga kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuhudumia shehena kwa haraka kutokana na maboresha makubwa yaliyofanyika.

Salama aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema bandari hatua yao ya kuhudumia mzigo nangani hakusababishi ikiwa na uwezo mdogo wa kiutendaji .Alisema hata nchini Singapore bado wanahudumia mzigo nangani na baadae kuleta nchi kavu hivyo wafanyabiashara wanapaswa kutumia bandari hiyo kusafirisha bidhaa zao.

“Bandari ya Tanga kuhudumia mzigo nangani hakusababishi kuwa na uwezo mdogo wa kiutendaji kwani hata nchi ya Singapore bado inatumia kuhudumia mzigo nangani kuleta nchi kavu hivyo niwatake wafanyabiashara kutumia bandari hii kusafirisha mizigo yao“Alisema Meneja Salama.Alisema Bandari hiyo hivi sasa ina uwezo mkubwa wa kuhudumia wateja ambao watakuwa wakipitisha mizigo kutokana na kuwepo kwa matishari ya kutosha kuhamisha mizigo kati ya gatini na melini nangani inapofika.

“Kwani tunaweza kufanya mzunguko wa nyuzi 360 melini hakuna mashine itakayosimama gatini hivyo kuongeza ufanisi mkubwa wakati wa kuhudumia shehena inayowasili “Alisema.Hata hivyo alisema bandari ya Tanga ni bora na ina uwezo wa kutoa huduma kwa kasi kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa ambacho vinatumika kufanya kazi hizo kwa wakati (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga leo kuhusu mikakati wa bandari hiyo kulia ni Afisa Mipango wa Bandari Moshi Mtambalike Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akizungumza kushoto ni Afisa Utekelezaji Mkuu wa Bandari hiyo Donald Ngaire na kulia ni Afisa Mipango wa Bandari Moshi MtambalikePRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu akizungumza katika mkutano huoMwandishi wa Habari wa Daily News na Habari Leo mkoani Tanga Cheji Bakari akiuliza swali kwenye mkutano huoSehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania mkoani Tanga 

MWENYEKITI BAVICHA MANISPAA YA IRINGA AIPONGEZA FAMILIA YA ASAS KUBORESHA SEKTA YA AFYA

$
0
0

Wahenga wanasema hujafa hujaumbika. Na ule msemo usemao kwamba maendeleo hayana vyama ni hakika na bayana. 

Mwezi January mwaka huu nilikamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa mahabusu kwa siku 8 kesi ya kisiasa , Hali hiyo ilimpelekea mke wangu Stellah ambaye alikuwa mjamzito kupata mshutuko na kuharibu mwenendo wa mimba yake. 

Jana usiku mke wangu ninayempenda sana hakuweza kuendelea kumlea mtoto akiwa tumboni badala yake madakatari walihangaika kuokoa uhai wa mwanangu na mama yake na kazi hiyo walifanikisha kwa 100%.

Lengo la ujumbe huu ni shukrani za dhati kwa ASAS FAMILY waliojenga jengo la kuokoa maisha ya watoto wachanga ASAS NEONATAL UNIT watoto ambao walikuwa wanapoteza maisha yao kila siku kutokana na vifaa tiba duni pamoja na ukosefu wa wodi yenyewe ya kutunza ninaoweza kuwaita "Malaika wa Mungu".

Amenidokeza Nesi mmoja katika hosipitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa kuwa kwa juma moja kabla ya ASAS FAMILY kujenga jengo hilo kupitia Mkurugenzi wao SALIM ABRI ASAS wameweza kupunguza kiwango cha vifo kutoka 20 mpaka vifo vya wachanga 2.

Nesi huyo ameendelea mbele na kunieleza kuwa ASAS haohao wamejenga Intesive Care Unit (ICU) ya kisasa ambayo imegharimu zaidi ya 300,000,000/= yenye uwezo wa kuhudumia mahutihuti 10 kwa mara moja ambayo bado haijazindiliwa. 

Ninajua wana Iringa wengi watapata huduma hapo kama mwanangu mwenye 850gm anavyopata huduma leo. 

I humbly acknowledge and pray for the blessings to the efforts made by this family to save hundreds of patients. 

Leonce Marto , 

Mkt BAVICHA IringaMjini.

12.04,2018 .

Waziri Mahiga ahimiza wadhamini kujitokeza Wiki ya Tanzania nchini Kenya

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega walipokutana na Wadhamini na Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya maonesho hayo (hawapo pichani) yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 25 - 28 Aprili 2018 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya. 

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 12 Aprili 2018 katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam na kuambatana na hafla ya kukabidhi udhamini kwa ajili ya kufanikisha maonesho hayo maarufu kama ''Wiki ya Tanzania nchini Kenya'' ambayo yataenda sambamba na sherehe za miaka 54 za Muungano wa Tanzania. 
Sehemu ya wadhamini na wajumbe wa kamati ya maandalizi wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiongozwa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani) 
Viongozi wa Kampuni ya NIDA TEXTILE MILLS (T) wakimkabidhi Mhe. Waziri Mahiga mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 22,700,000/- kwa ajili ya kudhamini maonesho ya didhaa za viwanda vya Tanzania nchini Kenya. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Muhammad Waseem. 
Mhe. Waziri Mahiga akimshukuru Mwakilishi wa Kampuni ya Mohamed Enterprises, Bi. Barbara Gonzale baada ya kutoa ahadi ya udhamini wa kiasi cha shillingi millioni ishirini na tano (25,000,000) kwa ajili ya kudhamini maonesho hayo. 
Mhe. Waziri Mahiga akimshukuru mwakilishi kutoka kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd, Bw. Maleke Hans baada ya kutoa ahadi ya udhamini wa kiasi cha Dola za Marekani 5,000 (sawa na shilingi milioni kumi na moja za Tanzania). 
Mhe. Waziri Mahiga akisikiliza taarifa fupi ya udhamini na hatua ya maandalizi iliyofikiwa kutoka kwa Katibu wa Kamati, Balozi Mbega, pembeni ni baadhi ya Wadhamini na Wajumbe wa Kamati. 
Sehemu nyingine ya wajumbe wa kamati wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Balozi Mbega kwa Mhe. Waziri Mahiga. 
Picha ya pamoja. 

SERIKALI YA POLAND YAFUNGUA RASMI OFISI ZA UBALOZI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Augustine Mahiga kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe. Jacek Czaputowicz wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi za Ubalozi wa Poland hapa nchini. Ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi huo zilizopo Masaki, Jijini Dar es Salaam ulifanyika tarehe 12 Aprili, 2018. Ili kuimarisha na kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Poland, nchi hiyo ilifungua tena Ubalozi wake hapa nchini mwaka 2017 baada ya kuufunga mwaka 2008 na kabla ya uzinduzi wa ofisi hizi hapo nchi hiyo ilikuwa inawakilishwa kutokea Nairobi, Kenya. 
Waziri Mahiga akimpongeza Waziri Czaputowicz kwa uamuzi wa nchi hiyo wa kufungua Ofisi za Ubalozi hapa nchini. 
Mhe. Waziri Mahiga kwa pamoja na Mhe. Waziri Czaputowicz wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa ufunguzi wa ofisi za Ubalozi wa Poland nchini.
Mkutano kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Waziri Czaputowicza na waandishi wa habari ukiendelea. 

MWANDISHI, WAHARIRI WAITWA BUNGENI KWA MADAI YA KUDHALILISHA BUNGE

MWAKYEMBE ATEUA MWENYEKITI WA BODI CHUO CHA MICHEZO MALYA NA WAJUMBE WAPYA

TEWW KUENDELEA KUWA KITOVU CHA KUTOA ELIMU BORA

$
0
0
Taasisi ya Elimu ya Watu wazima yaendelea Kujizatiti katika kutoa elimu bora kwa wale waliokosa elimu katika mfumo rasmi ili waweze kuchangia katika kujenga uchumi wa Viwanda.

Kaimu Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Kassimu Nihuka amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati wa kufunga warsha ya uandaaji wa mihtasari ya Fizikia na kemia iliyowashirikisha walimu wa masomo hayo kutoka baadhi ya shule za sekondari za jijini Dar es Salaam

“Katika kuboresha utoaji wa Elimu ya Sekondari nje ya mfumo rasmi ilishakamilisha uandishi wa mihtasari ya masomo ya Hisabati, Biolojia, Uraia, Historia, Jiografia, Kiswahili na Kiingereza na ambayo inatumika katika vituo vinavyotoa elimu ya Sekondari nje ya mfumo rasmi mikoa yote nchini. “ Alisisitiza Dkt. Nihuka

Kupitia jukumu la kutoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi TEWW imesajili jumla ya vituo 547, kati ya hivyo 93 vinaendeshwa na TEWW na vingine 454 vinaendeshwa na wadau. Jumla ya wanafunzi 10,420 wakiwemo wanawake 6,074 (58.3%) na wengine 4,346 (41.7%) wanaume wanasoma elmu ya sekondari nje ya mfumo rasmi nchi nzima kwa kutumia mitaala iliyoandaliwa na TEWW.

Ili kuwajengea wanafunzi msingi wa masomo ya sayansi hususani Fizikia na Kemia, TEWW imeandaa mitaala ya masomo haya itakayotumika katika kutoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi. Kwa sasa wanafunzi wetu wa sekondari wanasoma masomo saba likiwemo somo la bailojia pamoja na Hesabu. Uandaaji wa mitaala ni moja ya majukumu ya TEWW kisheria.

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Namba 12 ya mwaka 1975 na kupewa majukumu mbalimbali.Pamoja na majukumu mengine, Taasisi inajukumu la kutoa elimu ya sekondari kwa njia ya ujifunzaji huria na masafa pamja na mafunzo ya jioni pamoja na kuandaa mitaala kwa ajili ya kutoa elimu nje ya mfumo rasmi.
Mkuu wa Idara ya Elimu Masasa (teww) Bw. Baraka Kionywaki akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa kuwekeza katika masomo ya fikizia na kemia katika elimu nje ya mfumo rasmi nchini tanzania. kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Kassimu Nihuka .
Wataalamu wa Uandaaji wa Mitaala ya masomo ya Fikizia na Kemia wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Kassimu Nihuka (hayupo pichani) leo Jijini Dar es eslaam.
(Picha zote na TEWW)

WAZIRI MHAGAMA AUPONGEZA UONGOZI WA KANISA LA BAPTIST KWA KUENDELEA KUIOMBEA NCHI YETU.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza uongozi wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendela kuliombea Taifa ili kudumisha Amani na Utulivu uliopo.

Ametoa pongezi hizo hii leo alipokutana na Uongozi wa Kanisa hilo Bungeni Dodoma ili kujadili na kuipongeza Serikali kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.

“Niwapongeza sana uongozi wote wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kutuombea na kuikumbuka nchi yetu kwani bila uwepo wa amani na utulivu maendeleo hayawezi kuwepo.”Alisema Waziri Mhagama

Aliongezea kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha inaboresha na kuleta maendeleo ya nchi yake bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na ushirika mzuri na viongozi wetu wa dini na kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika kufikia azma yake ya “Tanzania ya Viwanda”.

“Kipekee niwashukuru kwa kuona umuhimu wa kutuweka mikononi mwa Mungu Uongozi wote wa nchi, kuanzia kwa Mhe. Rais wetu, Baraza la Mawaziri na Viongozi wote kwa ujumla wao ili kuhakikisha tunakuwa na hekima na weredi wa utekelezaji wa majukumu yetu kuhakikisha Watanzania wanapata maendeleo.”Alisisitiza Waziri Mhagama

Pamoja na hilo aliuomba uongozi huo kuendelea kuchangia katika Huduma za kijamii hususan kupitia mchango wanautoa kwa jamii wa kuwa na Shule, Vyuo na Zahanati zinazohudumia Wananchi wanaochangia katika uzalishaji na maendeleo ya nchi yao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo kwa baadhi ya viongozi wa Kanisa la Baptist nchini walipomtembelea katika Ofisi yake Bungeni Dodoma Aprili 12, 2018.
Askofu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase akifanya maombi kwa kifupi walipomtembelea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama kuzungumza masuala yao na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada za kukuza uchumi na maendeleo kwa ujumla.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipata maelekezo ya hati ya pongezi (ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli) kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiwashukuru viongozi wa Kanisa la Baptist nchini walipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA).

Tigo Pesa Yapata Uthibitisho wa Huduma za Kifedha Kutoka Shirika la Kimataifa la GSMA

$
0
0

Tigo Pesa, huduma ya kifedha kwa simu za mkononi inayoongoza nchini, imepokea uthibitisho wa kimataifa ujulikanao kama ‘GSMA Mobile Money Certification’.

Uthibitisho huu unatambua uwezo mkubwa wa Tigo Pesa katika kutoa huduma salama, kwa uwazi, za kuaminika na thabiti zinazokuza haki za wateja na kuzuia miamala ya kihalifu.

Tigo Pesa ni moja kati ya watoa huduma za kifedha kwa simu za mkononi wa kwanza kabisa duniani kupokea uthibitisho huu kutoka GSMA.

GSMA Mobile Money Certification’ ni mkakati wa kimataifa unaolenga kuleta huduma za kifedha salama, wazi na thabiti zaidi kwa mamilioni ya watumiaji wa huduma za kifedha kwa simu za mkononi duniani kote. Huku kukiwa na zaidi ya akaunti 690 milioni za fedha kwa simu za mkononi duniani, sekta ya simu za mkononi inaboresha maisha duniani na imewezesha mamilioni ya watu wasiokuwa na akaunti za benki kufikiwa na huduma rasmi za kifedha.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu za Mkononi wa Tigo, Hussein Sayed alisema, “Tigo Pesa inajivunia mchango wake mkubwa katika kufanikisha upatikanaji wa huduma rasmi za kifedha nchini kwa kutoa fursa kwa mamilioni ya Watanzania wasio na huduma za kibenki kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa kifedha.’
Uthibitisho huu kutoka GSMA ni ishara tosha kuwa Tigo Pesa imepiga hatua kubwa kuhakikisha kuwa fedha za wateja wetu zipo salama, na kuwa haki zao zinalindwa. Kupitia taratibu zetu za kibiashara tunalenga kutoa huduma zenye viwango vya juu zaidi.  

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Sekta binafsi Zanzibar yajadili mikakati madhubuti ya kufanikisha wiki ya Tanzania nchi Kenya

$
0
0
Waziri Wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum akizungumza katika ufunguzi wa mkutano na Wafanyabishara wa Zanzibar uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko tarehe 13 Aprili 2018. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hassan Khamis Hafidh na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Katibu wa Kamati ya Taifa ya maandalizi ya maonesho ya bidhaa za Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega.

Katika ufunguzi huo Mhe. Waziri Amina aliwasisitiza wafanyabiashara hao kushiriki katika maonesho pamoja na umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Diplomasia ya uchumi kwa vitendo. 
Balozi Anisa Mbega akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya maonyesho pamoja na kutoa ufafanuzi wa matukio mengine yatakayoambatana na maonyesho hayo kama vile kongamano la biashara, maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanzania. 
Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Saleh akiwahamasisha wafanyabishara kushiriki maonesho hayo pamoja na kuhakikisha wanafanya maandalizi ili kuweza kukamilisha vigezo na masharti ya ushiriki. 
Juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikiwasilishwa na viongozi. 
Sehemu ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano. 
Mkutano ukiendelea. 

MKURUGENZI HUDUMA ZA UFUNDI SEKTA YA UJENZI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI TEMESA

$
0
0
 Mtendaji mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA, Dkt. Mussa Mgwatu akisoma taarifa kwa mgeni rasmi, wajumbe na watendaji hawapo pichani wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa wakala huo kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa wakala huo Hans Lyimo, Mkurugenzi wa Huduma za  ufundi sekta ya ujenzi Mhandisi William Nshama na Afisa Rasilimali watu kutoka wakala huo Evarista Asenga.
 Mkurugenzi wa Huduma za ufundi sekta ya ujenzi, Mhandisi William Nshama akizungumza wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi TEMESA na wajumbe na baadhi ya watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA hawapo pichani katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa wakala huo kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtendaji mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa wakala huo Hans Lyimo.
 Naibu katibu mkuu wa TUGHE Taifa Mhandisi Amani Msuya kulia akiimba wimbo wa wafanyakazi mshikamano daima pamoja na Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Ferdinand Mishamo wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa wakala huo kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot jijini Dar es Salaam. 
 Naibu katibu mkuu wa TUGHE Taifa Mhandisi Amani Msuya akifafanua jambo kwa wajumbe na baadhi ya wafanyakazi wa wakala hawapo pichani wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot Keko jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya wajumbe, mameneja na watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA waliohudhuria kikao cha Baraza la wafanyakazi TEMESA wakisikiliza kwa umakini mada zilizokuwa zikitolewa katika kikao hicho cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Mt Depot Keko jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za ufundi sekta ya ujenzi Mhandisi William Nshama katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA mara baada ya kuzindua na kufungua mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Mt Depot Keko jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO TEMESA

HAWA NDIO MAAFISA WAKUU WA JWTZ WALIOPANDISHWA VYEO NA RAIS DKT MAGUFULI

UZINDUZI WA PROGRAM YA MAFUNZO YA KUJIAJIRI NA KUONDOA UMASKINI WAFANYIKA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Ajira Ali Suleiman Ameir akitoa maelezo kuhusiana na Ajira katika Uzinduzi wa  Programu ya Mafunzo ya Kujiajiri na kuondoa Umaskini(Skill development and trade market)  katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.Zaidi ya Madereva 70 wamekabidhiwa Tiket za  kwenda nchini Qatar kufanya kazi ya Udereva.
 Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Fatma Gharib Bilal akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi  katika Uzinduzi wa  Programu ya Mafunzo ya Kujiajiri na kuondoa Umaskini(Skill development and trade market)  katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.Zaidi ya Madereva 70 wamekabiodhiwa Tiket za  kwenda nchini Qatar kufanya kazi ya Udereva.
 Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Custico akitoa hotuba ya Uzinduzi wa   Programu ya Mafunzo ya Kujiajiri na kuondoa Umaskini(Skill development and trade market)  katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.Zaidi ya Madereva 70 wamekabidhiwa Tiket za  kwenda nchini Qatar kufanya kazi ya Udereva.kulia ni Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Shadia Mohammed na kushoto ni Mkurugenzi Ajira Ali Suleiman Ameir. 
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Custico akimkabidhi Tiket ya Kwenda Nchini Qatar Dereva Seif Kurwa Sanga katika Uzinduzi wa   Programu ya Mafunzo ya   Kujiajiri na kuondoa Umaskini(Skill development and trade market)  katika Ukumbi wa Baraza la  Wawakilishi la  Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar. Zaidi ya Madereva 70 wamekabidhiwa Tiket za  kwenda nchini Qatar kufanya kazi ya Udereva.
 Muakilishi kutoka Taasisi ya Usafirishaji ya Hamoup Company Ltd Haji Amour Haji akitoa neno la shukrani katika  Uzinduzi wa   Programu ya Mafunzo ya   Kujiajiri na kuondoa Umaskini(Skill development and trade market)  katika Ukumbi wa Baraza la  Wawakilishi la  Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar. Zaidi ya Madereva 70 wamekabidhiwa Tiket za  kwenda nchini Qatar kufanya kazi ya Udereva.
 Baadhi ya Madereva wanaokwenda Nchini Qatar kufanya kazi ya Udereva kupitia Programu ya Mafunzo ya Kujiajiri na kuondoa Umaskini(Skill development and trade market) iliozinduliwa na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Custico katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Custico katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Madereva waliopatiwa Tiket za kwenda Nchini Qatar katika Uzinduzi  wa   Programu ya Mafunzo ya   Kujiajiri na kuondoa Umaskini(Skill development and trade market)  katika Ukumbi wa Baraza la Wwakilishi la Zamani Kikwajuni mjini Zanzibar.

PICHA  NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) lamlilia Joyce Hagu

$
0
0

Na Sixmund J. Begashe

Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) Bw Adrian Nyangamale ameungana na wasanii wote, wapenda sanaa, Serikali ya Tanzani, na watanzania wote katika kuomboleza kifo cha aliewahi kuwa Kahimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni nchini Bi Joyce Hagu. 
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa msiba wa Dada Joyce Hagu, ni juzi tu tulikuwanae Magomeni kwenye msafara wa Mh Waziri Dr Harison Mwakyembe alipotembelea wanamuziki wa zamani, tukitaniana na kucheka kama ilivyokuwa desturi yake, kumbe ndio alikuja kutuaga.’’ Aliandika Bw Nyangamale kwenye kundi la whatsap la shirikisho hilo lijulikanalo kama JAMVI. 

Kupitia ukurasa huo maarufu nchini wa JAMVI Bw Nyangamale aliongeza kuwa   Marehemu Joyce Hagu alikuwa msaada mkubwa kwenye tasnia ya sanaa za Ufundi nchini kwa kutumia taaluma yake ya sanaa kuuwashauri wasani mambo muhimu katika Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania, kukosa na kutoa njia bora ya kujisahihisha pale wasanii wanapo kwende kinyume na maadili ya Utamaduni wa Mtanzania.


“Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA) tunatoa pole kwa Mhe Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, watumishi na wafanyakazi wa Wizara, na Taasisi zake, Mashirikisho ya Sanaa, Vyama, Vikundi na Jamii yote ya wasanii nchini. Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote bila kusahau Wanajamvi kwa msiba huu mzito.” Alimalizia Bw Nyangamale


Wakiungana na Rais wa TAFCA, wanajamvi Lilian Nabora, Mussa Sango, Wilhadi Tairo na Namsikiliza Mungu wameeleza kwa masikitiko makubwa namna walivyo pokea taarifa za msiba huo na kuwa Marehemu amefariki wataki ikiwa bado machango wake ulikuwa ukihitajika sana katika tasnia ya Sanaa na Utamaduni nchini, na kuahidi kuwa wataendelea kumkumbuka daima.


Taarifa za kuaga dunia kwa Msanii Msomi na Mwalimu gwiji wa sanaa nchini Bi Joyce Hugu zimedhibitishwa na kaka yake aitwae Gabriel pale alipo ongea kwa simu na mwandishi wa habari hizi akisema kuwa dada yao amekutwa na umauti akiwa amelala usiku wakumakia jana.



ADC AMA "MPAMBE" WA RAIS NI NANI?

$
0
0

Kufuatia kupandishwa cheo kwa aliyekuwa Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania (JWTZ) Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Kanali M.N Mkeremy kuwa Brigedia Jenerali na nafasi yake kuchukuliwa na Kanali B.M Mlunga aliyepandishwa kutoka Luteni Kanali kuwa Kanali hapo jana, Uwanja wa Diplomasia tumeona turejee maelezo yetu juu ya maana ya ADC ili jamii ipate kunufaika.

TUELIMIKE
Kwa kawaida kila tumuonapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli nyuma yake huwa amesimama Afisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Uwanja wa Diplomasia tumekuwa tukiulizwa maswali sana juu ya mtaalamu huyo wa Jeshi lakini tumekuwa tukisita kwa kuhofia kuingilia majukumu ya watu.
Tulipoona maswali yanazidi ilibidi tuwasiliane na wahusika ili tuweze kufahamu kama tukitoa elimu juu ya hili tutakuwa tumechupa mipaka ama la. Leo Uwanja wa Diplomasia tunakuletea maelezo kidogo juu ya afisa huyu wa jeshi (JWTZ).

AFISA HUYU KIITIFAKI ANAITWAJE?

Afisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambaye huwa amesimama nyuma ya Rais akiwa na suti ya kijeshi ama kombati kiitifaki hutambulika kama ADC.

ADC ama A de C ni cheo cha heshima ambacho hutunukiwa Msaidizi Mkuu wa kiongozi wa Juu wa Nchi kama Rais, Mfalme ama Malkia. Kirefu cha ADC ni Aide de Camp neno ambalo kwa Kiswahili hujulikana kama Msaidizi (wa Kambi). Neno hili limetoka katika mazingira ya kijeshi kwa kuwa nchi karibu zote duniani zimetokana na vita.

ADC wa Rais huweza kuwa afisa wa ngazi ya juu kuanzia cheo cha Meja, Luteni Kanali au Kanali kulingana na hadhi ya nchi kimataifa na anapofika cheo cha Brigedia Jenerali hupangiwa majukumu mengine.

Mara nyingi ADC wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huwa ni Afisa wa ngazi ya juu wa Jeshi mwenye cheo cha Kanali wakati kwa upande wa Tanzania Visiwani huwa ni Luteni Kanali. Hii ni kutokana na hadhi ya Tanzania kimataifa.
Si Rais tu pekee huwa na ADC bali Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama CDF ana ADC wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP ana ADC wake na hata Mkuu wa Jeshi la Magereza CGP na Uhamiaji CGI huwa na maADC zao.

KAZI ZA ADC WA RAIS NI HIZI ZIFUATAZO:
ADC wa Rais ana kazi nyingi sana kutokana na kuwa kwake Msaidizi Mkuu wa Rais, kazi hizo ni kama zifuatavyo; 

(1) Msaidizi Mkuu wa kazi za kila siku ofisi ya Rais.

(2) Huandaa kalenda, ratiba na safari za Rais.

(3) Huandaa masuala yote ya kiitifaki ya Rais.

(4) Hupokea wageni wa Rais.

(5) Hupokea zawadi mbalimbali kama ngao,mikuki n.k ambayo Rais hupewa kama zawadi akiwa ziarani.

(6) Humbebea Rais Begi/Mkoba wake sambamba na diary na peni.

(7) Huwaongoza na kuwaelekeza staff wengine.

(8) Hufanya kazi mbalimbali kwa mujibu wa muongozo dawati la ofisi ya Rais.

(9) Husimamia e-mails sambamba na kuandaa na kupitia mawasiliano yote ya kiofisi ya Rais.

(10) Husaidia kuandaa safari, kusalimia wageni, mabalozi na kusoma ramani.

Uwanja wa Diplomasia tumewaletea maelezo ya mambo ama shughuli za kila siku za ADC ambazo tunaamini zitakuwa zimefungua uelewa wenu wote mliouliza.  
Karibuni tuendelee kuelimishana.

Abbas Mwalimu.
+255 719 258 484.
Uwanja wa Diplomasia (Facebook)

JUMIA FIX MY HOUSE

$
0
0
It's time to turn your House to a HOME!!
A house can be any basic unit of dwelling, whether its an apartment, a super modern glass box or anything else in between. The form of the house never matters as much as what goes inside  because those are the special things that transform any space into a home.

What's the difference between a house and a home? A house is a structure that provides you basic needs and safety. A home is a place that provides you mental and emotional support, a place you look forward to being in to get away from the outside world.

Feeling like your home is lacking a bit of personality? There’s something powerful about walking into a house that feels like a home and reflects the owner’s personality so perfectly. Do you feel that way about your house? If not? Do you wish to achieve a high-end luxurious look without blowing your budget? Believe it or not, your home can look expensive and luxurious without dragging you into debt.The key is to shop SMART..

One of the wonderful experience i had this weekend as i spend some time alone on my internet was to  bump into one of the Upcoming Jumia’s Campaign. The name made me look and look again,They call it Big Home Makeover!! Fascinating right? 

An online survey released by Jumia Tanzania has revealed that 70% of Tanzanians households keep their home appliances for more than their life span citing sentimental value and uniqueness as opposed to old age.


CLICK HERE TO READ MORE

NUSU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA HAPATOSHI

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
HATIMAYE yametimia, Droo ya Nusu Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imemalizika kupangwa mchana huu, kwa miamba ya soka barani humo kukutana uso kwa uso.
Real Madrid kutoka nchini Hispania itakuwa na kibarua cha kumenyana na Bayern Munich wakati Liverpool wao wakivaana na AS Roma.
Mkondo wa kwanza wa michezo hiyo inatarajiwa kupigwa kati ya April 24/25 wakati mkondo wa pili unatazamiwa kupigwa kati ya May 1/2mwaka huu.

Wakati huo huo Michuano ya UEFA Europa League, droo yake ya Nusu Fainali imemalizika mchana huu, kwa Arsenal ya Uingereza kuikabili Atletico Madrid ya Hispania na Olimpique de Marseille ya Ufaransa kuchuana na FC Salzburg.

HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bi. Kate Kamba ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa utekelezaji wa Ilani wa chama cha Mapinduzi na kusema kuwa ameiona thamani ya fedha katika miradi yote aliyoitembelea hivyo mshikamano uliopo uendelezwe. 

Amayezungumza hayo jana mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi aliyoifanya Manispaaa ya Kigamboni yenye lengo la kuona ni naman gani Ilani ya Chama inatekelezwa. 

Akizungumza na watumishi na wananchi wanao shiriki kusimamia miradi Bi.Kamba amesema kuwa, Miradi yote inatekelezwa katika ubora na ndani ya wakati na thamani ya fedha ( Value for money) inaonekana. 

"Miradi yenu mizuri na inatekelezwa kwa ubora na wakati, mnaspidi nzuri sana hii inaonesha ni naman gani mnaushirikiano, Kigamboni ni Wilaya changa lakini mambo mnayofanya mnawazidi hata Wilaya kongwe, tumependa" Alisema Kamba 

Aliongeza kuwa ameona ushirikishwaji katika utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba jamii imeshiriki kikamilifu hali inayopelekea kuona wanao wajibu wa kutunza na kusimamia miradi yao ndio maana wameweza hata kufikia makubaliano ya kuomba punguzo la bei ya ununuzi wa vifaa vinayohitajika kwenye ujenzi miradi. 

Aidha Bi. Kamba alisema kuwa sheria ya manunuzi inagharimu sana utekelezaji wa miradi , urasimu mwingi tofauti na utaratibu wa local fundi unaosaidia kutumia fedha kidogo na miradi kujengwa kwa wakati huku thamani ya fedha ikionekana. Kamba aliwataka watumishi kuona anao wajibu na sehemu yake ya kufanya kazi na kuhudumia wnanchi ikiwa ni utekelezaji wa ilanai na kuhakikisha lengo lililowekwa linafikiwa kwa kiwango cha juu. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Bi. Kate Kamba akizungumza na kutoa pongezi zake kwa Manispaa ya Kigamboni.

Baadhi ya Wakuu wa idara na vitengo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa alipokuwa akizungumza nao

jengo la wamama wajawazito likiwa kwenye hatua ya renta ​
Jengo la maabara na upasuaji likiwa katika hatua ya upauaji kama inayoonekana katika picha ​
muonekano wa jengo la kuhifadhia maiti.

TPA YAWAKUTANISHA WA WADAU KWA LENGO LA KUFANYA TATHIMINI JUU YA KAZI ZAO

$
0
0
Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye akizungumza kuhusu Serikali  ilivyojipanga kuhakikisha inachukua masoko ya kibandari katika nchi nane zinazoizunguka Tazania pamoja na kutenga dola milioni 400 za upanuzi wa kina cha bandari kuhakikisha meli kubwa zaidi zinaingia nchini na shehena za mizigo zinaongezeka wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kufanya tathimini juu ya shughuli zinazofanywa na TPA.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko akizungumza na wadau kuhusu bandari nyingi ambazo si rasmi kwa jina lingine zinaitwa bandari bubu kuwa kuna mpango kuzirasimisha bandari hizo ili zitambuliwe rasmi na kuchangia pato la taifa lakini pia tupunguze uingizwaji wa dawa za kulevya na bidhaa kinyemela nchini wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kufanya tathimini juu ya shughuli zinazofanywa na TPA.
 Mkurugenzi wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA), Azizi Kilonge  akizungumza kuhusu ongezeko la tani Milioni sita za shehena kwa mwaka 2016 na kufikia tani Milioni 15 ni ishara tosha kuwa bandari inafanya vyema katika soko wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kufanya tathimini juu ya shughuli zinazofanywa na TPA.
 Baadhi ya wadau pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA) wakimsikiliza Naibu waziri wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kufanya tathimini juu ya shughuli zinazofanywa na TPA
Mgeni rasmi Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa TPA.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images