Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAIKABIDHI TBA NYUMBA ZILIZOREJESHWA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Mhe. Roeland van de Geer wakisaini Hati ya Makabidhiano ya nyumba nne (4) kutoka Umoja wa Ulaya zilizopo katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo zimekabidhiwa kwa Wizara na EU baada ya kutumiwa na Umoja huo tokea miaka ya 1975. Baada ya makabiadhiano hayo, Wizara ilizikabidhi nyumba hizo kwa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA). Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani tarehe 11 Aprili, 2018. 
Balozi Mushy kwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi. Elius Mwakalinga wakisaini hati ya makabidhiano kama ishara kwa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuzikabidhi kwa TBA nyumba nne (4) zilizopokelewa na Wizara kutoka EU. 
Balozi Mushy na Balozi Roeland van de Geer wakibadilishana hati hiyo baada ya kusaini 
Balozi Mushy na Balozi van de Geer wakionesha hati hiyo .


DK. KIGWANGALLA AITAKA KAMATI INAYOCHUNGUZA TUHUMA ZA MAUAJI YA TEMBO IKOLOJIA YA RUGWA-RUAHA KUTENDA HAKI

$
0
0
Na Hamza Temba-Dodoma

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameitaka kamati inayochunguza tuhuma za mauaji ya tembo katika Ikolojia ya Rugwa-Ruaha ambazo zilitolewa mwishoni mwa mwaka jana na kituo cha habari cha ITV London cha Uingereza kufanya kazi hiyo kwa uaminifu na uadilifu mkubwa bila kumuonea mtu ili ukweli ubainike na Serikali iweze kuchukua hatua stahiki.

Dkt. Kigwangalla ametoa rai hiyo leo mjini Dodoma alipokutana na wajumbe wa kamati hiyo ambayo imewasilisha taarifa za awali za kazi ilizoanza kuzifanya za kupitia taarifa mbalimbali kuhusu tuhuma hizo kabla ya kwenda kuzifanyia uchunguzi maeneo husika.

Amewataka wajumbe hao kuchunguza ukweli wa tuhuma hizo ili kubaini kama kweli kuna watumishi wa Wizara waliohusika katika mauaji hayo pamoja na tuhuma kuwa mauaji ya tembo yalikuwa ni makubwa kama ilivyoripotiwa na chombo hicho cha habari.

Dkt. Kigwangalla pia ameitaka kamati hiyo kuchunguza ukweli wa tuhuma kuwa fedha za ufadhili wa mradi wa SPANEST zilizotolewa na Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) zilitumika vibaya kufadhili mauaji hayo kama ilivyoripotiwa na chombo hicho cha habari.

“Msimtafute mtu, wala msimuonee mtu, fanyeni kazi hii kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ukweli ujulikane ili sisi kama Serikali tuweze kuchukua uamuzi unaostahili” alisema Dkt. Kigwangalla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mstaafu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambaye ni Mwenyekiti wa kamati inayochunguza tuhuma za mauaji ya tembo katika Ikolojia ya Rugwa-Ruaha ambazo zilitolewa hivi karibuni na kituo cha habari cha ITV LONDON cha nchini Uingereza, alipokutana na kamati hiyo leo ofisini kwake mjini Dodoma. Wengine pichani ni wajumbe wa kamati hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Ndugu Robert Mande ambaye ni mjumbe wa Kamati hiyo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Bi. Getrude Lyatuu ambaye ni mjumbe wa Kamati hiyo kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

SERIKALI KUZIFUTIA USAJILI NGOs ZITAKAZOFANYA KAZI KINYUME NA SHERIA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu – Mwanza
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) imesema haitasita kulifutia usajali Shirika lolote lisilo la Kiserikali litakaloenda kinyume na Sheria na Taratibu za nchi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba alipokuwa akifungua kikao kati yake na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali na Wadau wa mashirika hayo kwa Mkoa wa Mwanza.

Bw. Katemba amesisitiza kuwa kwa mujibu wa Sheria namba 4 ya Mwaka 2002 ya Mashirika Yasito ya Kiserikali inayataka Mashirika hayo kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Nchi katika utendaji wa kazi zao kwa mujibu wa Katiba na majukumu yao kiusajili.

Ameongeza kuwa kikao hicho kimefanyika ili kuwakumbusha wadau wa NGOs kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria za nchi zilizopo kwani baadhi ya mashirika hayo yamekuwa yakitumika kufanya mambo ambayo yapo kinyume na Sheria.

“Nawataka wamiliki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia matakwa ya usajili wao katika kutekeleza majukumu katika Mashirika yao” alisema Bw.Katemba
 Mkurugenzi wa  Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa Mashirika hayo Bw. Marcel Katemba akizungumza na Wasajili Wasaidizi wa  Mashirka Yasiyo ya Kiserikali kutoka katika Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa Mwanza katika kikao baina yake na Wasajili Wasaidizi hao na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Mkurugenzi  wa Msaidizi Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Leornald Baraka akiwakumbusha washiriki mambo muhimu yanayohitaji kuzingatiwa kabla na baada ya kusajili Shirika Lisilo la Kiserikali kwa wadau kutoka katika Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Baadhi ya wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Mwanza wakifuatilia mada na mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yakitolea na Msajili wa Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA APRIL 11, 2018

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora mhe. Kapteni Mstaafu George Mkuchika akiwasilisha hotuba ya makadirio ya matumizi ya  Ofisi hiyo na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2018/19  leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI mhe. Selemani Jafo akiwasilisha hotuba ya makadirio ya matumizi ya  Ofisi hiyo na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2018/19  leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Naibu Waziri wake mhe Juliana Shonza wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Nishati Dkt. Merdard Kalemani akiteta jambo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. William Lukuvi Bungeni mjini Dodoma leo.
Mbunge wa Msalala mhe. Ezekiel Maige akisisitiza jambo Bungeni wakati wa Kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMPUNI YATOA MAFUNZO WAFANYABISHARA WA VIFAA VYA UJENZI SOKO LA KARIAKOO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Imports International Tanzania imetoa mafunzo ya siku moja kuhusu jasi (gypsum) kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam, Mtaalamu wa ujenzi wa kampuni hiyo  Stanley Katabarwa amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni wafanyabiashara ili wajue aina za gypsum kutokana na sehemu ambayo inakwenda kutumika.

Amesema wafanyabiashara wengi wanauza gypsum lakini hawajui matumizi sahihi, hivyo uwepo wao katika eneo hilo utasaidia wafanyabiashara hao kuuza gypsum kulingana na mahitaji ya mteja.

"Mara nyingi huwa tunakosea gypsum ya kutumia kulingana na shemu inayokwenda kutumia matokeo yake uimara ya hiyo sehemu inakuwa haipo.Tumeshafanya mafunzo ya aina mbili ambayo yalihusisha wadau wengine wa ujenzi na leo tunalenga mafundi na watu ambao wanauza, si kwamba wanauza bidhaa bila kuzielewa. Tunataka tu watu waelewe njia nzuri ya kutumia gypsum bora,"amesema.

Aidha Katabarwa amesema kampuni yao inazo gypsum za aina zote na hivyo kwa wanaohitaji wanaweza kufika katika ofisi zao ili wanunue na kuzitumia katika ujenzi.
 Mkaguzi wa wa Zimamoto Bandari, Dunstan Biyengo akitoa maelezo kwa wanafunzi wa chuo cha IFM waliofika katika maonesho ya maadhimisho ya miaka 13  ya tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari  ya Bandari  kuhusiana na kujihami na majanga yanayoweza kujitokeza wakati bandari yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
 Nahodha wa Bandari, Kapten Nassor Mvuolana akiwapa maelezo wanafunzi wa chuo cha IFM waliofika katika maonesho ya maadhimisho ya miaka 13 ya tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kuhusiana na kazi wanazozifanya wakati wa meli zinapoingia na zinapotoka  yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Bandari, Ernest Nyambo akizungumza na wanafunzi wa chuo cha IFM walipotembelea maonesho bandari ya Dar es Salaam katika ikiwa ni maadhimisho ya miaka 13 ya tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari  ambapo amewaeleza kuhusina  jinsi wanavypokea meli zinapoingia katika bandari hiyo maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wa IFM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea maonesho ya maadhimisho ya miaka 13 ya tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha IFM. Rayson Mbalamwezi akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kushiriki na kujua vitu mbalimbali vinavyofanywa na banadari katika maadhimisho ya miaka 13 ya tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
 Meli ya Ngumi ikiwa imegeshwa kwa ajili ya maonesho ya bandari katika maadhimisho ya miaka 13 ya tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RC MAKONDA AAHIDI KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WOTE WALIOTELEKEZWA

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema watoto wote ambao wametelekezwa na baba zao ambao wamefika kwenye ofisi yake na mama zao ili kupata msaada wa kisheria atahakikisha anawakatia bima ya afya ili kusaidia wapate matibabu bure.

Makonda ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na wanawake ambao wamezalishwa na kisha kutelekezwa na waume zao ambao wamefika kwake kupata msaada wa kisheria ambapo ameelezea kuwa wale wote waliofika kwake basi watoto wao watakatiwa bima ya afya.

Amesema anatambua changamoto ambazo akina mama hao wanazipitia na kuelezea kuwa kutokana na jitihada zake za kuwasaidia ametoa mdau ambaye ameahidi kumsaidia katika kuhakikisha watoto hao wanapata bima ya afya ambayo itawawezesha kupata huduma za afya pindi wanapougua.

"Mungu anatenda miujiza yake, kuna mtu mmoja ameona kazi nayoifanya ya kusaidia mama hawa,basi akajitolea kuwa atakata bima kwa ajili ya watoto wote ambao wamefika hapa na mama zao kwa ajili ya kupata msaada.Hivyo niwaambie wote mliopo hapa watoto wenu tutaeakatia bima ya afya ili wapate huduma za matibabu bure,"amesema Makonda hali iliyoibua shangwe kutoka kwa akina mama hao ambapo wapo waliozimia kutokana na habari hiy njema kwao.

Wakati huohuo Makonda amesema kuwa mpaka sasa  watu mashughuli walitelekeza watoto wao wamefikia 107.

Makonda amesema idadi hiyo imebainika jana na juzi wakati wa mchakato huo ambapo pia amesema si kundi hilo tu la watu mashughuli kuna kundi la watu ambao wanaona aibu kufika katika eneo hilo.

"Hawa watu wanaona aibu kufika ofisini ofisini hapa, hakuna kukutana na mimi chemba, habari yakupigiana simu kuniambia Mheshimiwa naomba nije peke yangu hakuna", amesisitiza Makonda

"Watu Mashughuli, watu wenye heshima tukikupima DNA nakugundua mtoto ni wako, basi utalipa fidia zote za huyo mtoto".

Amesema wale wanaokaidi wito kufika ofisini hapo, kuanzia kesho watapelekewa barua pamoja na kupigiwa simu.

Zoezi hilo lakubaini Wazazi waliokimbia watoto wao lilianza siku ya Jumatatu ya April 9, 2018 na linatarajiwa kumalizika siku ya Ijumaa April 13 mwaka huu.
 Baadhi ya Akina Mama waliojitokeza katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kudai fidia za Watoto wao kwa Wazazi wenzao waliokimbia watoto hao.
 Mmoja wa Maafisa wa Ustawi wa Jamii akiwasikiliza Wazazi wa Kiume walioitikia wito kufika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya akina Baba waliotikia wito kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusikiliza malalamiko kwa wake zao. (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA)

MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA - RAIS MAGUFULI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi kabla ya kuzindua rasmi Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi mara baada ya kumaliza kusoma hotuba yake na kuizindua rasmi Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kabla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuizindua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuizindua. PICHA NA IKULU

*Azungumzia mambo makubwa ambayo aliyafanya kwenye utawala wake ambayo yatakumbukwa
*Azindua rasmi Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation,aahdi Serikali kutoa ushirikiano mkubwa
*Aelezea Kikwete alivyosababisha awe Rais wa Awamu ya Tano, Kikwete azungumzia malengo ya taasisi

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii.

RAIS Dk. John Magufuli amesema kwa kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye uongozi wake kuna mambo makubwa ya maendeleo katika nchi yetu huku akitanguliza uzalendo mkubwa Watanzania wanamkumbuka na wataendelea kukumbuka watake wasitake.

Pia ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake za dhati kwa Rais mstaafu Kikwete kwani ndio amesababisha awe Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano huku akitumia nafasi hiyo kuahidi kuwa atahakikisha Serikali yake itashirikana na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete inayofahamika kwa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)ambayo ameizindua rasmi leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
"Mzee wangu Kikwete naomba niseme kutoka moyoni wakati wa uongozi wako umefanya mambo makubwa ya kuleta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzanania.Kuna miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ameifanya na imeacha alama ambayo itatufanya watanzania tumkumbuke.Kwa kazi ambayo umeifanya kwa uzalendo mkubwa ndani ya nchi yetu Watanzania tunakukumbuka na tutaendelea kukumbuka watake wasitake,"amesema Rais Dk.Magufuli.
Ametaja ipo mifano mingi hai ya mambo ambayo ameyafanya Rais mstaafu Kikwete kwenye Serikali ya Awamu ya nne na baadhi ya miradi hiyo lipo  la ujenzi wa bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam, ujenzi wa miundombinu ya barabara nchi nzima, ujenzi wa miradi ya maji , umeme na kuimarisha sekta muhimu za afya, kilimo na vijana.
"Rais mstaafu Kikwete alilitumikia Taifa la Tanzania kwa uadilifu mkubwa.Tabia ya binadamu wamekuwa na kawaida ya kumsifu mtu baada ya kufa na kusema pengo halitazibika wakati si kweli kwani kama ni nafasi ya uongozi inaweza kujazwa wakati huohuo.Kwa Rais mstaafu na mzee wangu Kikwete naomba nikusifu ukiwa hai tena upo mbele yangu unatabasamu.Umefanya kazi kubwa ya kizalendo kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzania na unastahili sifa na shukrani kutokana na mchango wao wa kuleta maendeleo kwenye nafasi mbalimbali.
"Ulipokuwa Rais wa Tanzania umefanya mambo makubwa zaidi kwa ajili ya nchi yetu. Katika utawala wako umefanikisha ujenzi wa shule za sekondari za kata , ujenzi wa Hospitali ya Mloganzila na miradi mingine mikubwa ambayo umeifanya na sote ni mashahidi kwa yale ambayo umeyafanya,"amesisitiza Rais Dk.Magufuli na kuongeza mbali ya kuwa Rais mzee Kikwete ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Bara la Afrika na nchi za ulaya na Dunia kwa ujumla na kote huko ametoa mchango mkubwa wa kuleta maendeleo.
Rais Magufuli amesema uzalendo wa mzee Kikwete kwa nchi yake umemfanya hata baada ya kustaafu kuamua kuanzisha taasisi ambayo leo amezindua rasmi na vipaumbele vya taasisi hiyo havina tofauti na vile ambavyo anavitekeleza kwenye Serikali yake , hivyo ameahidi kumpa ushirikiana mkubwa kufanikisha malengo hayo na kuomba wadau wengine wakiwamo mabalozi nao kuunga mkono kazi za taasisi hiyo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Mnyama TID kuunguruma Usiku wa BongoFleva Helsinki, Finland, Jumamosi April 14 2018

Next: 1:39 KUONDOKA KWA LWANDAMINA,Canavaro afunguka ShutikaliTV Recommended for you New 14:57 WARARKA TELEFISHINKA BBC SOMALI 11.04.2018 Salim Kikeke 312 views New 7:38 Kutoka mtaji wa Tsh 7000, MakJuice wanazindua MakChicken weekend hii Millard Ayo Recommended for you New 1:00:41 FULL HIGHLIGHTS: YANGA SC 1-1 SINGIDA UNITED (VPL - 11/04/2018) Azam TV 90 views New Kisa cha Mama aliyemwaga Machozi kwa Makonda, Kinasikisha! Global TV Online 22K views New MUSIBA anasema ATAUA ila hakamatwi, Serikali ndio inamtuma? ABC HABARI 81 views New Al Jazeera English | Live Al Jazeera English 1.9K watching LIVE NOW BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 10.04.2018 Salim Kikeke 6.2K views New Msigwa atangaza Kujivua Ubunge wa Iringa Mjini Topten Tv 63K views New BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 09.04.2018 Salim Kikeke 6.1K views New BUNGENI: Maandamano Yazua Gumzo, Ndiyo ni Haki Kikatiba Lakini... Global TV Online Recommended for you New Mama wa mtoto aliyedai baba yake ni Lowassa afunguka Bongo5 57K views New SPIKA AKIRI: MAKONDA AMENITIKISA, NITACHUKUA HATUA HII ABC HABARI Recommended for you New BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 10.04.2018 BBC News Swahili 11K views New Spika Ndugai baada ya kusikia kuna Wabunge wametelekeza watoto Millard Ayo 7.4K views New MAKONDA APEWA ONYO NA WAZIRI, ANADHALILISHA WANAWAKE NA WATOTO ABC HABARI Recommended for you New BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 11.04.2018
$
0
0
Mnyama siku hiyo atatambulisha kazi zake  Mpya kwa wapenzi wa Muziki wa Bongo Fleva. Hakika siyo ya kukosa!

1:39 KUONDOKA KWA LWANDAMINA,Canavaro afunguka ShutikaliTV Recommended for you New 14:57 WARARKA TELEFISHINKA BBC SOMALI 11.04.2018 Salim Kikeke 312 views New 7:38 Kutoka mtaji wa Tsh 7000, MakJuice wanazindua MakChicken weekend hii Millard Ayo Recommended for you New 1:00:41 FULL HIGHLIGHTS: YANGA SC 1-1 SINGIDA UNITED (VPL - 11/04/2018) Azam TV 90 views New Kisa cha Mama aliyemwaga Machozi kwa Makonda, Kinasikisha! Global TV Online 22K views New MUSIBA anasema ATAUA ila hakamatwi, Serikali ndio inamtuma? ABC HABARI 81 views New Al Jazeera English | Live Al Jazeera English 1.9K watching LIVE NOW BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 10.04.2018 Salim Kikeke 6.2K views New Msigwa atangaza Kujivua Ubunge wa Iringa Mjini Topten Tv 63K views New BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 09.04.2018 Salim Kikeke 6.1K views New BUNGENI: Maandamano Yazua Gumzo, Ndiyo ni Haki Kikatiba Lakini... Global TV Online Recommended for you New Mama wa mtoto aliyedai baba yake ni Lowassa afunguka Bongo5 57K views New SPIKA AKIRI: MAKONDA AMENITIKISA, NITACHUKUA HATUA HII ABC HABARI Recommended for you New BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 10.04.2018 BBC News Swahili 11K views New Spika Ndugai baada ya kusikia kuna Wabunge wametelekeza watoto Millard Ayo 7.4K views New MAKONDA APEWA ONYO NA WAZIRI, ANADHALILISHA WANAWAKE NA WATOTO ABC HABARI Recommended for you New BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 11.04.2018

DC ILALA AWATAKA WAJASIRIAMALI WANAWAKE KUJIUNGA JUKWAA LA WANAWAKE

Previous: 1:39 KUONDOKA KWA LWANDAMINA,Canavaro afunguka ShutikaliTV Recommended for you New 14:57 WARARKA TELEFISHINKA BBC SOMALI 11.04.2018 Salim Kikeke 312 views New 7:38 Kutoka mtaji wa Tsh 7000, MakJuice wanazindua MakChicken weekend hii Millard Ayo Recommended for you New 1:00:41 FULL HIGHLIGHTS: YANGA SC 1-1 SINGIDA UNITED (VPL - 11/04/2018) Azam TV 90 views New Kisa cha Mama aliyemwaga Machozi kwa Makonda, Kinasikisha! Global TV Online 22K views New MUSIBA anasema ATAUA ila hakamatwi, Serikali ndio inamtuma? ABC HABARI 81 views New Al Jazeera English | Live Al Jazeera English 1.9K watching LIVE NOW BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 10.04.2018 Salim Kikeke 6.2K views New Msigwa atangaza Kujivua Ubunge wa Iringa Mjini Topten Tv 63K views New BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 09.04.2018 Salim Kikeke 6.1K views New BUNGENI: Maandamano Yazua Gumzo, Ndiyo ni Haki Kikatiba Lakini... Global TV Online Recommended for you New Mama wa mtoto aliyedai baba yake ni Lowassa afunguka Bongo5 57K views New SPIKA AKIRI: MAKONDA AMENITIKISA, NITACHUKUA HATUA HII ABC HABARI Recommended for you New BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 10.04.2018 BBC News Swahili 11K views New Spika Ndugai baada ya kusikia kuna Wabunge wametelekeza watoto Millard Ayo 7.4K views New MAKONDA APEWA ONYO NA WAZIRI, ANADHALILISHA WANAWAKE NA WATOTO ABC HABARI Recommended for you New BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 11.04.2018
$
0
0


Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE Wajasiriamali wametakiwa kujiunga na Jukwaa la Wanawake ili kujiinua kiuchumi.

Mwito huo umetolewa na Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wakati akizindua kikundi cha wajasiriamali cha Mshikamano Mchikichini Sokoni katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana.

Katika hatua nyingine Kalekezi amewataka wanawake hao kuacha unafiki na kupendana jambo litakalowasaidia kusonga mbele kwenye umoja wao huo.

Alisema Dunia imeanzisha Jukwaa la Wanawake ambapo wanawake watakuwa wakukutana kujadili changamoto walizo nazo na jinsi ya kuzikabili pamoja na kuangalia fursa mbalimbali za maendeleo."Jukwaa ili na sisi linatuhusu hivyo hatuna budi kujiunga nalo kwani huko tutapata wataalamu waliobobea katika masuala mbalimbali pamoja na biashara hivyo ni vizuri tukalichangamkia" alisema Kalekezi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality fo Growth (EfG) Jane Magigita alisema wakati huu si wakulala bali ni wakuangalia fursa nyingine ili kujikomboa kiuchumi.Alisema Serikali imeweka mazingira mazuri hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kupambana vilivyo ili kujikwamua kiuchumi kupitia vikundi.

Ofisa Tarafa wa Kata ya Kariakoo Christina Kalekezi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kikundi cha Wajasiriamali cha Mshikamano Mchikichini Sokoni katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Katibu wa Kikundi hicho, Juliana Richard, Mwenyekiti, Anjela Mwamakula na aliyevaa miwani ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita.
Wanachama wa Kikundi cha Mshikamano Mchikichini Sokoni wakiwa kwenye uzinduzi wa kikundi chao.
Hapa wakiserebuka.
Mwenyekiti wa Soko la Mchikichini-Ilala Jumanne Kongogo akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.

NCAA YADHAMINI NGORONGORO MARATHON

$
0
0
Na Yusuph Mussa, Tanga

MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongo (NCAA) imedhamini mashindano ya Ngorongoro Marathon kama sehemu ya njia ya kukuza utalii kwenye eneo hilo lenye vivutio vya pekee duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Aprili 11) jijini Tanga, Naibu Mhifadhi wa NCAA Asangye Bangu, alisema mashindano hayo yatakuwa na faida kubwa kwenye nyanja za utalii na kuwezesha watu wengi ndani na nje ya nchi kuvutiwa na hifadhi hiyo.

"Tumeamua kudhamini mashindano haya ya Ngorongoro Marathon yanayofanyika Aprili 21, mwaka huu. Nia ya kudhamini mashindano haya, kwanza ni kufanikisha mashindano yenyewe na pili ni kuweza kutangaza utalii wetu.

"Tunaamini sisi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro tuna dhima kubwa kuona watalii wa ndani na nje wanaongezeka. Lakini ili waongezeke ni lazima tutumie njia mbalimbali za kutangaza vivutio vya Hifadhi za Ngorongoro ambavyo ni vya kipekee duniani" alisema Bangu.

Bangu alisema Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, pia imekuwa na changamoto ya ujangili na uvamizi, hivyo kwa kutumia mashindano hayo, watawaeleza wananchi wajue umuhimu wa hifadhi hizo kwa maslahi ya nchi.
Mashindano ya Ngorongoro Marathon 2017, ambayo kwa mara ya kwanza yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mamlaka hiyo inadhamini kwa mara ya pili mwaka huu. (Picha na Yusuph Mussa).
Mashindano ya Ngorongoro Marathon 2017, ambayo kwa mara ya kwanza yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mamlaka hiyo inadhamini kwa mara ya pili mwaka huu. (Picha na Yusuph Mussa)

Mashindano ya Ngorongoro Marathon 2017, ambayo kwa mara ya kwanza yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mamlaka hiyo inadhamini kwa mara ya pili mwaka huu. (Picha na Yusuph Mussa).

Mashindano ya Ngorongoro Marathon 2017, ambayo kwa mara ya kwanza yalidhaminiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Mamlaka hiyo inadhamini kwa mara ya pili mwaka huu. (Picha na Yusuph Mussa).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ALIYOZUNGUMZA MSAJILI WA NGOs NA WADAU WAKE MARA BAADA YA KIKAO CHAO JIJINI MWANZA

Uwekaji wa Mahesabu Serikalini Unaendelea kuwa Mzuri Tofauti na hapo Awali-Prof. Mussa Assa

KAYA 6120 ZA WALENGWA WA TASAF ZALIMA PAMBA EKARI 8712 MSIMU WA MWAKA 2017/2018 MKOANI SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Kaya 6120 sawa na asilimia 52 ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu zimewezeshwa kulima pamba ekari 8712 katika Msimu wa mwaka 2017/2018 kwa kutumia fedha za uhawilishaji.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu Bw. Nyasilu Ndulu wakati wa kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi juu ya mpango huo kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.

Nyasilu amesema pamoja na kulima pamba walengwa wa mpango huo katika Wilaya ya Bariadi na wilaya nyingine Mkoani Simiyu, kupitia fedha za uhawilishaji (wanazopewa) wamefanikiwa kujenga nyumba, kufuga, kuanzisha biashara ndogo ndogo na kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).

Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa zoezi la uhawilishaji chini ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini awamu ya tatu mwaka 2015 hadi sasa, tayari awamu 17 za malipo zimekwisha fanyika kwa walengwa 37, 533 na jumla ya shilingi bilioni 28.9 zimelipwa kwa wahusika.

Amesema fedha hizo zimejumuisha ruzuku za aina mbili ikiwa ni ruzuku ya msingi na ile itokanayo na utimizaji wa mashati ya Afya na Elimu ambapo watoto 39,068 sawa na asilimia 90.3 wameweza kupata mahitaji muhimu ya shule na kukuhudhuria shuleni na watoto 51, 280 sawa na asilimia 93.1 wamepata mahitaji ya kliniki na kupelekwa kliniki.

“Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umeweza kuwasaidia walengwa kujikwamua kutoka kwenye umaskini, wapo walioanzisha biashara, wanaolima, wanaofuga, waliojenga nyumba bora; kwa kutumia fedha hizi wanazopewa wapo ambao watoto walikuwa hawahudhurii shuleni na kliniki lakini sasa hivi mahudhurio mazuri” Alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa mkoa huo wakati alipofungua kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa mkoa huo katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.

EACJ Plenary commences in Nairobi to deliberate on the issues of the Court

$
0
0

 East African Court of Justice Nairobi, 12th April 2018:   The Court Plenary which is a court’s activity that takes place twice a year commenced yesterday in Nairobi, Kenya. 

The President of the Court, Justice Dr Emmanuel Ugirashebuja congratulated the new Judge Justice Charles Nyachae from the Republic of Kenya, upon his appointment as Judge of the First Instance Division who will replace Justice Isaac Lenaola whose term will end in June 2018.


His Lordship, the President also congratulated Justice Dr Faustin Ntezilyayo who was designated by the EAC Heads of State in February this year, as a Deputy Principal Judge the same position that Justice Lenaola is holding. The President paid tribute to Justice Lenaola for his dedicated service for the last seven years and to his contribution to the development of the jurisprudence of the Court.

The Plenary received reports from two Divisions of the Court headed by the President and the Principal Judge and the Registrar on the progress, achievements, challenges and new developments of the Court.

The Plenary considered the court’s contribution in training of the bar associations in the region on the rules and procedure of the Court, such as the Rwanda Bar Association and that the rest will also be trained upon their requests. The Court further recommended to strengthen the collaboration of the Court with the Bar Associations in order to engage them as legal fraternity to support the court in raising the quality of advocacy.

Their Lordships during the Plenary, raised and deliberated on several concerns that affect the Court’s performance, including, the Court not holding sessions as scheduled due to budgetary constraints. The Plenary also recommended to the management to look for alternative funding and proposals to the Development Partners to fund the court’s activities. 


MGAZETI YA LEO ALHAMIS APRILI 12,2018

MKUTANO WA CHAMA CHA WANANCHI CUF NA WAANDISHI WA HABARI WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Mratibu wa Mkutano wa CUF Ali Makame akitoa maelezo kuhusiana na Mkutano na kumkaribisha Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF Mussa Haji Kombo kuzungumza na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa CUF kuhusiana na mwenendo na migogoro ndani ya Chama hicho Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF Mussa Haji Kombo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na mwenendo na migogoro ndani ya Chama hicho Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini CUF Mussa Haji Kombo katikati akifafanua baadhi ya maswala mbalimbali ya Mwenendo na Migogoro ndani ya chama hicho kwa Waandishi wa Habari Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.kulia yake ni Kiongozi wa Ulinzi wa CUF Thney Juma na Kushoto ni Mratibu wa Mkutano wa CUF Ali Makame.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO

Viashiria Vyote vya kimataifa vinavyopima uwezo wa kukopa vinaonesha nchi yetu inakopesheka- Dkt Mpango

MAHAKAMA YAELEZWA HALI TETE RAIS WA KLABU YA SIMBA, EVANS AVEVA

$
0
0
Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii.

Mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, hali ya Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva ni mbaya (very Serious), na amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Kufuatia hali hiyo, mahakama imeshindwa kuwasomea maelezo ya awali (PH)  rais huyo Simba ambaye anashtakiwa pamoja na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu.

Kesi imeahirishwa baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leonard Swai kueleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Aveva ni  mgonjwa (very Serious)  amelazwa katika hospitali ya Taifa  ya Muhimbili.

Swai aliomba mahakama iipangie kesi hiyo tarehe nyingine wakati wakisubiri afya ya Aveva iimarike.

Hakimu Simba ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unaandaa maelezo ya awali, ili tarehe inayokuja waweze kusomewa PH na siku ikianza kusikilizwa, isikilizwe mfululizo.

Kesi imeahirishwa hadi Aprili  25/ 2018.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi na kutakatisha fedha dola za kimarekani 300,000.

KAMISHNA WA NISHATI AFANYA ZIARA KITUO CHA KUPOKEA MAFUTA CHA KURASINI

$
0
0
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alifanya ziara katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kukagua shughuli zinazotekelezwa na kituo hicho pamoja na kutatua changamoto mbalimbali. 

Katika ziara hiyo Mhandisi Luoga aliambatana na Kamishna Msaidizi wa Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya, wataalam kutoka Idara ya Nishati na mwakilishi kutoka Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

Kamishna Luoga alielekeza kituo hicho kuendelea kuimarisha ulinzi ili kudhibiti upotevu wa mafuta. Aidha alielekeza kituo hicho kuendelea kushirikiana na wadau wengine kwa karibu zaidi katika kuboresha shughuli zake.
Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (kushoto) akielezea kazi za mita za kupimia mafuta (flow meters) katika kituo hicho kwa Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kulia)
Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (katikati mbele) Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto mbele) na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya (kulia mbele) wakiendelea na ziara katika kituo hicho.
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (katikati) akielekeza jambo katika sehemu ya kupokea mafuta aina ya petroli na dizeli katika kituo hicho.
Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (mbele) akimwongoza Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya pamoja na wajumbe wengine katika ziara hiyo.
Sehemu ya gati za kupokea mafuta katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) Captain Paul R. Paul (katikati) akionesha sehemu ya mita za kupima mafuta (flow meters) katika kituo hicho kwa Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) pamoja na wajumbe wengine (hawapo pichani) katika ziara hiyo.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images