Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

TADB, PASS, FSDT SEEK TZS 100 BILION TO SUPPORT IRRIGATION INFRASTRUCTURE

0
0
By Our Reporter – Morogoro

Tanzania Agricultural Development Bank (TADB), The Private Agricultural Sector Support Trust (PASS) and Financial Sector Deepening Trust (FSDT) are in the process to find initial fund amounting TZS 100 billion to supporting irrigation infrastructure development in the country.

Speaking during the meeting to discuss collaboration on irrigation financing, Acting Managing Director for TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha said lending for agriculture infrastructure is a challenge in Tanzania as a result has been retrograding sector growth in the country.

He added that this is caused due to high cost of borrowing and limited payback period for the loans associated with the limited use of irrigation.

“A consequence of this challenging lending environment to agricultural infrastructure, which requires long-term payback period, is limited investment in agriculture productivity, particularly in irrigation infrastructure,” he said.

On his part, PASS Managing Director, Mr. Nicomed Bohay said that the intervention in irrigation development has verified worldwide that it boosts crop production 3-4 times than that of rain fed agriculture.
PASS Managing Director, Mr. Nicomed Bohay makes a presentation on Irrigation Financing during SUA Agriculture & Agribusiness Conference 2018.
Acting Managing Director for TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (centre) laments on modus operandi of the proposed Irrigation Financing during SUA Agriculture & Agribusiness Conference 2018. Others in picture are FSDT’s Head of Agriculture and Rural Finance, Mr. Mwombeki Baregu (left) and PASS Managing Director, Mr. Nicomed Bohay (right).
FSDT’s Head of Agriculture and Rural Finance, Mr. Mwombeki Baregu (left) contributing during the meeting. Others in picture are PASS Managing Director, Mr. Nicomed Bohay (right) and TADB Acting Managing Director, Mr. Augustino Matutu Chacha (centre)..
The trio Irrigation Financing collaborators attentively taking contributions from the floor.




WAZIRI MKUU AIASA JAMII KUMUENZI MZEE MTOPA KWA KUDUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiasa jamii nchini kujiepusha  na migogoro kwa vile haina tija  na badala yake idumishe amani, upendo na uadilifu ili kumuezi mwanasiasa mkongwe nchini, marehemu  Alhaj Ali Mtopa.

Aliyasema hayo jana (Jumatano, Aprili 11, 2018) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mwanasiasa huyo yaliyofanyika katika kijijini Nanjilinji wilayani Kilwa. Alhaji Mtopa alifariki Jumatatu Aprili 9 jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu alisema haitapendeza kusikia jamii, wanafamilia, watendaji au wanasiasa waliokuzwa au kufunzwa na marehemu Alhaj Mtopa wakifarakana  kwa sababu yoyote ile kwani  siku zote marehemu alikuwa kiongozi aliyejitahidi sana kuwawaunganisha watu na mpenda amani.

“Tumepoteza kiongozi maarufu mwenye historia pana, amekuwa mtumishi ndani chama (CCM) na Serikali kwa muda mrefu. Alikuwa kiongozi mwema muadilifu, mtiifu na mchapakazi kwa miaka mingi”.“Marehemu Alhaj Mtopa hakua mbaguzi kwenye kuielimisha jamii namna ya kuendesha siasaza kistaarabu. Kifo chake kinatuacha na huzuni, kazi yetu kubwa ni kumuombea ili Mwenyezi Mungu aweze kuilaza roho yake mahali pema”. Alisistiza Mheshimiwa Majaliwa.

Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafamilia kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na baba ambaye alikuwa nguzo ya familia na jamii. Hivyo aliwaomba kutoruhusu mgawanyiko wa aina yoyote baina yao.“Katika kipindi hiki kigumu ambacho tumeondokewa na mzee wetu na mwalimu wetu wa siasa na uongozi wetu nawasihi sana wanafamilia kuwa watulivu kwani haitapendeza kusikia kuwa kuna mgogoro au mgawanyiko kati yenu”.

Alisema yeye binafsi amepata msaada mkubwa kutoka kwa maremu Alhaj Mtopa katika masuala ya siasa na kijamii  kwa vile  mara nyingi akiwa katika ziara zake mkoani Lindi na katika jimbo lake la Ruangwa aliambatana na marehemu na kwa pamoja walishirikiana kutatua kero na kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo.
  
Mbali na Waziri Mkuu viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo, ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Mbunge wa Mtama, Napa Nnauye na  Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.

Wengine ni Mke wa Rais wa Awamu ya Nne na Mbunge wa Kuteuliwa Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia na Pamoja na Waziri wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mbunge wa Kilwa Kusini,Selemani Ally Bungara na Mbunge mstaafu wa Mtama, Benard Membe.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, APRILI 12, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati alipowasili  kushiriki mazishi ya Mwanasiasa na Mkongwe na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu wa Mkoa wa Lindi, Alhaj Ali Mtopa katika kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa, Aprili 11, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waombolezaji wakishiriki katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM wa mkoa wa Lindi, Alhaj Ali Mtopa kwenye kijiji cha Nanjilinji wialyani Kilwa Aprili 11, 20918. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu wa Mkoa wa Lindi, Alhaj, Ali Mtopa katika kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa, Apili 11, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akishiriki katika sala ya kumwombea Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM mkoa wa Lindi,   Alhaj Ali Mtopa wakati aposhiriki katika mazishi  ya Mwansiasa huyo yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nanjilinji  wilayani Kilwa, Aprili 11, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) akishiriki katika mazishi ya Mwanasiasa na Mkongwe na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu wa Mkoa wa Lindi, Alhaj Ali Mtopa katika kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa, Aprili 11, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU

0
0

Na Ramadhani Juma ,Ofisi ya Mkurugenzi

HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma kupitia Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu imeendelea kuimarisha miundombinu ya usafi kwa kuongeza vifaa vya kutunza uchafu katika mitaa kadhaa ya Mji ili kuhakikisha Wananchi hawatupi taka ovyo.

Akizungumza wakati wa uwekji wa vifaa hivyo, Mkuu wa Idara hiyo Dickson Kimaro alisema Manispaa inatarajia kuongeza ‘vitunza uchafu’ 11 katika mitaa mbalimbali ili kuweka mazingira rafiki ya kutunza uchafu kwa Wakazi wa Mji wanaokuwa katika shughuli zao za kila siku.

“Hizi ni juhudi za makusudi ili kuhakikisha Mji wetu unakuwa safi muda wote…natoa wito kwa Wakazi wa Manispaa yetu watumie vifaa hivi kuhifadhia uchafu mdogo wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku” alisema Kimaro.

Alisema mbali na vifaa hivyo, tayari Manispaa ilishasambaza vifaa vikubwa vya kukusanyia taka za aina zote (Skip Bucket) 61 katika Kata mbalimbali zinazotumika kama vituo vya kukusanyia taka kabla ya kubebwa na Mitambo ya Manispaa na kupelekwa katika Dampo la Kisasa lililopo eneo la Chidaya Kata ya Matumbulu nje kidogo ya Mji.



Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu wa Manispaa ya Dodoma Dickson Kimaro akikagua moja ya vifaa vipya vilivyowekwa katika Mtaa wa Kuu kwa ajili kutunza uchafu ikiwa ni juhudi za Manispaa hiyo kuhakikisha Mji unakuwa safi wakati wote.

Moja ya vifaa vya kutunzia taka (kulia) kilichopo mkabala na Viwanja vya Nyerere katikati ya Mji wa Dodoma

MEGHJEE ATUNUKIWA CHETI NA KANISA LA AICT BWIRU

0
0
Na Baltazar Mashaka, Mwanza

Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Bwiru la jijini Mwanza limemtunuku cheti Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Alhaji Sibtain Meghjee kwa kutambua huduma za jamii zinazotolewa na taasisi hiyo katika sekta za afya,elimu na maji bila kujali itikadi za dini wala kubagua.

Akizungumza kabla ya hafla hiyo Mchungaji Ephafra Zabron alisema taasisi ya TD & CF imefanya mambo mengi muhimu ya kusaidia jamii kwa kuhudumia watu wa dini na madhehebu mbalimbali bila ubaguzi katika masuala ya afya, elimu na maji lakini pia imejenga shule, nyumba za ibada (misikiti na makanisa) na kuchimba visima.

“Tusipotoshwe na watu kuwa watu wa dini ya Kiislamu wana mitizamo tofauti na wapo watu wanapotosha na kuleta lugha za kufarakanisha watu kuwa ukimwona Muislamu ni adui yako si kweli.Waislamu wanatuzidi mambo mengi na wanatimiza maandiko kwa vitendo ambapo kila Ijumaa wanatoa misaada kwa jamii ya wahitaji,” alisema Mchungaji Ephafra. 

Mchungaji huyo alieleza kuwa Kanisa la AICT Bwiru linatambua mchango mkubwa wa Sibtain Meghjee na taasisi yake kwa jamii kwani anafanya huduma aliyoifanya Yesu na kuwataka waumini wa kanisa hilo na wakazi wa eneo la Bwiru wajifunze kutokana na kazi zinazofanywa na The Desk & Chair.
Mwenyekiti wa The Desk &Chair Foundation (TD &CF) Sibtain Meghjee (kulia) akipokea cheti kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Mchungaji Philipo Majuja kutokana na kutambua mvhango wa taasisi hiyo wa kusaidia jamii.Hafla iliyofanyika kanisani hapo Jumalipili iliyopita.
Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Mchungaji Philipo Majuja (kushoto),akipokea kitabu cha Kuran tukufu kutoka kwa Mwenyekiti wa The Desk &Chair Foundation (TD &CF) Sibtain Meghjee. Anayeshuhudia kushoto wa kwanza ni Mchungaji wa Kanisa la Bwiru, Ephafra zabron na kulia ni Sheikh wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya ziwa Hashimu Ramadhan.Picha na Baltazar Mashaka

HALMASHAURI 182 ZAKAIDI ZADAIWA KUKAIDI AGIZO LA JPM

0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

HALMASHAURI 182 nchini ikiwemo saba za mkoani Pwani ,zinadaiwa kutumia vibaya mabilioni ya fedha yaliyotumika kuondoa zaidi ya lita 100,000 za dawa ya viuadudu vya mazalia ya mbu ,zilizokosa soko katika kiwanda cha Biotech Products Limited,kilichopo Mji Wa Kibaha ,ikiwa ni agizo alilolitoa Rais Dkt.John Magufuli June 22 mwaka jana.

Aidha halmashauri ambazo zinadaiwa kiasi cha sh.bil.1.8 walizochukulia dawa hiyo zimetakiwa kulipa fedha hiyo haraka ili kiwanda kiweze kujiendesha na kulipa watumishi wake mishahara.

Akizungumza katika ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa ya viuadudu inayozalishwa katika kiwanda hicho ,meneja wa udhibiti wa ubora na viwango kiwandani hapo , Samwel Mziray , alisema ni halmashauri mbili pekee zilizochukua dawa hiyo kwa awamu ya pili.

Alieleza halmashauri 184 zilichukua dawa kwa awamu ya kwanza na ya pili zaidi ya lita 200,000 ambazo wameziweka stoo bila kuzitumia wakidai hawana fedha ya kununulia pampu."Wanashindwa kuzitumia kutokana na kukosa pampu ya kupulizia ,hii ni aibu ,nimesikitishwa sana na hali hii, "

"Ni ngumu na jambo la ajabu leo hii Rais atoke kuja kufuatilia agizo lake ama kuzifuatilia halmashauri hizo, serikali ina nia njema lakini watendaji tunashusha juhudi za Rais na serikali ""Ninawaomba wakuu wa mikoa mingine nchini kuiga mfano wa mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ya kuhamasisha kununua dawa hizo, ili kupambana na vita dhidi ya ugonjwa hatari wa malaria." alieleza Mziray .

Mziray alieleza baada ya agizo la Rais walianza na mikoa 14 katika halmashauri 96 na awamu ya pili waligawa kwenye halmashauri za mikoa 12 na kutimiza mikoa 26 na halmashauri 184 nchini .Hata hivyo baada ya mgao wa kwanza halmashauri ya Rufiji iliongeza Lita 540 na Kibaha Vijijini waliongeza lita 520 .
 Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo (wa kulia) ,akimkabidhi dawa ya viuadudu vya mazalia ya mbu ,mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze ,Edes Lukoa wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa hiyo ,Mkoani Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi)
 Meneja wa udhibiti wa ubora na viwango katika kiwanda kinachozalisha dawa ya viuadudu cha Tanzania Biotech Products Ltd kilichopo Mjini Kibaha akionyesha wananchi kuwa dawa hiyo haina madhara, wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa ununuzi wa dawa hiyo,Mkoani Pwani .(picha na Mwamvua Mwinyi).

Newzz alert:Rais Magufuli awapandisha vyeo maafisa wa JWTZ

0
0


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo akitangaza majina ya Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Sekta Binafsi Yachangia Maandalizi Wiki ya Tanzania Nchini Kenya

0
0
Serikali itadumisha ushirikiano na sekta binafsi katika kutafuta fursa za kibiashara katika soko la pamoja la Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani ili kujenga uchumi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga wakati akipokea michango ya wadau toka sekta binafsi kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya wiki ya Tanzania nchini Kenya.
"Ninawashukuru sana kwa ushirikiano wenu na kuonyesha uthubutu wa kuingia katika soko la Kenya, ninyi ni mabalozi wa wafanyabiashara wengine katika kutafuta fursa za kibiashara nje ya Tanzania"alisema Balozi Mahiga.Balozi Mahiga alisema Tanzania inazobidhaa nyingi za viwanda ambazo nchi nyingine hawazijui bidhaa hizo, hivyo kinachofanywa na sekta binafsi kushirikiana na Serikali jambo la kijivunia.
Aidha, Balozi Mahiga alisema kuwa kufanya biashara nje ya nchi kunaimarisha uhusiano wa kisiasa baina ya Serikali ya Tanzania na nchi nyingine na kukuza diplomasia ya uchumi.Aliongeza kuwa hii ni fursa kwa ajili ya ujenzi wa uchumi wa viwanda ambao ni msisitizo na mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Waliotoa michango yao ni Kampuni ya Konyagi ambao wamechangia shilingi milioni 11, Mohamed Enterprises, Shilingi milioni 25 na NIDA TEXTILE MILLS (T) LTD imetoa hundi ya shilingi milioni 22.Balozi Mahiga amewaomba wafanyabiashara wengine wajitokeze kuchangia na kushiriki katika fursa hiyo ya kutafuta masoko nje ya nchi hususan Kenya ambapo bidhaa za Tanzania zitaoneshwa huko kuanzia tarehe 25 hadi 28, Aprili, 2018.
Kwa upande wake, mwakilishi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Rehema Mtingwa, amesema sekta binafsi iko tayari kushirikiana na Serikali katika kufanikisha upatikanaji wa fursa za kibiashara nchini Kenya na sehemu nyingine.Hii ni mara ya pili kwa wadau toka sekta binafsi kuchangia maandalizi hayo, kundi la kwanza ambalo lilijumuisha KNAUF Company LTD, IPP Media, Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), Bravo Logistics na Lake Oil Company Limited, liliwasilisha michango yake juma lililopita.

RC MAKONDA KUKUTANA NA KAMPUNI 30 KUTOKA UFARANSA , AWASHAURI WAFANYABISHARA DAR KUCHANGAMKIA FURSA

0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya jamii

MKUU wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini Federic Clavier ambapo kwa sehemu kubwa mazungumzo yao yamejikita kujadili kuhusu kongamano la uchumi litakalofanyika mapema jumatatu wiki ijayo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Makonda amemshukuru balozi na kueleza kuwa wamekuwa marafiki wazuri na Serikali ya Tanzania.Kuhusu kongamano hilo Makonda amesema siku ya Jumatatu Kampuni 30 kutoka Ufaransa yatawasili nchini na kufanya mkutano wenye malengo ya kuufanya mji wa Dar es salaam kuwa kama miji mingine duniani katika masuala ya maji, afya, usafiri na masuala mengine ya kiteknolojia.

Aidha ameeleza kampuni hizo zitaangalia fursa na vipaumbele vya Serikali watakavyovitumia katika kuleta maendeleo na ametoa rai kwa wafanyabiashara wa Jiji la Dar es salaam kuja katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kujifunza na kuunganishwa na wafanyabiashara hao kutoka ufarasa ili waweze kujifunza na kujenga urafiki katika masoko ya bidhaa zao.

Kwa upande wa Balozi wa Ufaransa nchini Federic Clavier amefurahi na kumshukuru Mkuu ya Mkoa Dar na kueleza kuwa Dar es Salaam  ni mji unaoendelea kukua kiuchumi sambamba na dhamira ya Rais Dk.John Magufuli ya kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.Aidha amesema mkutano huo utakuwa na faida baina ya nchi hizi mbili hasa katika kubadilishana teknolojia katika sekta mbalimbali hasa kwa kuangalia afya, maji pamoja na miundombinu na amehaidi matokeo mazuri yenye faida kwa nchi hizo.

Kuhusu mchakato wa kusaidia watoto waliotelekezwa Makonda amewashukuru wanahabari kwa kuwa sehemu ya wapatanishi wa familia hizo aidha amewataka wananchi kuja kupata huduma katika viwanja vya ofisi yake na si katika simu na mitandao na amefafanua hadi sasa familia 178 wameelewana na kukubaliana kupeana fedha za matunzo na zaidi ya watu 1498 wameshapatiwa huduma.

"Na Jumatatu wataitwa baba wa familia hizo licha ya baadhi yao kuanza kuripoti na ameeleza kuwa walio tayari kupima DNA wajitokeze watakaokaidi watachukuliwa hatua za kisheria.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya mdau moja kutoka Afrika Kusini ambaye ameahidi kuwasaidia watoto waliotelekezwa Toto Afya Card. (Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  akiwa katika banda la Mfuko wa Taifa  wa Bima ya Afya (NHIF) akiangalia namna uandikishaji wa Toto Afya Card ukiendelea leo jijini Dar es Salaam.

MILIONI 250/- KUTUMIKA KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WALIOTELEKEZWA DAR

0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na jukumu la kuwasaidia wanawake ambao wamezalishwa watoto na kisha kutelekezwa na waume zao huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Sh.milioni 250 ndizo zitakazotumika katika kuwakatia bima ya afya watoto zaidi ya 1500 waliotelekezwa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mbele ya umati mkubwa wa akina mama ambao wamefika ofisini kwake kupata msaada huo baada ya kuutangaza kuwasaidia wanawake wa mkoa wake ambao wametelekezwa, amesema anashukuru wadau mbalimbali wameendelea kujitokza na kusaidia watoto hao.

Amefafanua kuwa katika suala la bima ya afya kwa watoto hao ni kwamba jumla ya Sh.milioni 250 zinatarajia kutumika kwa ajili ya kuwakatia bima hiyo ya afya ambayo itawezesha kupata tiba.

"Kuna mdau mmoja kutoka Afrika Kusini ameahidi kuwasaidia watoto hao katika suala la afya hasa katika kupata bima ya afya na tayari mchakato huo umeanza leo hii na mdau huyo ameahidi kusaidia watoto zaidi ya 1500 ambao watagharimu kiasi hicho cha fedha,"amesema Makonda.

Kuhusu sifa za watoto watakaopatiwa bima za afya bure ambayo ni ya mwaka mmoja,Makonda amesema lazima mtoto awe ametelekezwa, awe raia wa Tanzania na awe na umri usiozidi miaka 18.

Kwa upande wa Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Wilaya ya Kinondoni Magreth Malangila ameeleza ili kukamilisha mchakato huo wazazi waje na picha (pasport) ya rangi ya bluu na cheti cha kuzaliwa.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA HAPA NCHINI

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Sarah Cooke, Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.

Lengo la mazungumzo hayo ilikuwa nikuagana na Mheshimiwa Makamu wa Rais ambaye atamuakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola (CHOGM) utakao fanyika mjini London kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 20 Aprili mwaka huu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke mara baada ya kumaliza mazungumzo  ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana  na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke (kulia) pamoja na Mkuu wa Masuala ya Kijamii na Siasa  Bw. Marc Thayre ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) .

WAZIRI KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA SITA BARAZA LA WAFANYAKAZI WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA MJINI DODOMA LEO

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano wa wafanyakazi wakati wa mkutano wa sita wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu TFS uliofanyika leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki na Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Prof. Dos Santos Silayo (wa tatu kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mjini Dodoma leo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo akihutubia baraza hilo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki akihutubia baraza hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania waliohitimu mafunzo ya Jeshi Usu hivi karibuni wakati wa mkutano wa sita wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala huyo uliofanyika leo mjini Dodoma. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Aloyce Nzuki muda mfupi baada ya kufungua baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mjini Dodoma leo. 

SHULE YA FOURTAIN GATE KINARA MATOKEO DARASA LA SABA 2017 MANISPAA YA ILALA

0
0

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

SHULE ya Fourtain Gate iliyopo Tabata Segerea jijini  Dar es Salaam imeshika nafasi ya kwanza katika shule 10 bora zilizofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2017.

Wakati Shule ya Msingi Mtendeni imeshika nafasi ya kwanza kwa shule bora za Serikali ambapo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo imetoa tuzo kwa shule hizo pamoja na nyingine ambazo nazo zimefanya vizuri.

Akizungumza Dar es Salaam leo baada ya kukabidhiwa tuzo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema , Mwalimu Mkuu wa Shule ya Fourtain Gate Julius Luge amesema shule yao imefanya vizuri kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya menejimenti, walimu, wanafunzi na wazazi.

Amesema tuzo hiyo imewapa ari zaidi ya kuendelea kujikita kutoa elimu bura na sahihi kwa wanafunzi wa shuleni kwao na kufafanua mbali ya kufanya vizuri kitaaluma pia wanafunzi wao wamefanya vizuri katika eneo la vipaji,"Moja ya mikakati ya shule yetu ni kufanya vizuri katika eneo la taaluma ya elimu lakini pia tumejikita katika kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wetu .Hivyo tupo vizuri katika taaluma na kukuza vipaji na imani yetu tutaendelea kufanya vizuri zaidi ya hapa,"amesema Mwalimu Luge.

Shule ya Fourtain Gate imeendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana namna ambavyo imejikita katika kutoa elimu bora na kuhakikisha wanashika nafasi za kwanza kwenye matokeo ya kitaifa na hiyo inatokana na kazi kubwa inayofanywa na walimu katika kuandaa wanafunzi wao kitaaluma.Awali Ofisa Elimu Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas akitaja shule zilizofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mbali na Fourtain Gate kwa shule za binafsi nafasi ya pili ni Tusiime, ya tatu St.Joseph Millleniam, nafasi ya nne Genius King, nafasi ya tano Masedonian na sita Lusasaro.

Nafasi ya saba imeshikiliwa na Shule ya Batvalley , nafasi ya nane Nyiwa, nafasi ya tisa Herritage na nafasi ya 10 ni Green Hill.Kwa upande wa shule bora za Serikali Thomas amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Shule ya Msingi Mtendeni,Shule ya Msingi Zanaki imeshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ni Shule ya Msingi Kiwalani.

Ametaja nafasi ya nne ni shule ya msingi Olimpio, nafasi ya tano Shule ya Msimbazi Mseto, nafasi ya sita Shule ya Msingi Diamond, nafasi ya nane Shule ya Msingi Lumumba, nafasi ya tisa Shule ya Msingi Mkoani na nafasi ya 10 Shule ya Msingi Maktaba.Manispaa ya Ilala katika matokeo ya mtihani wa darasa
la saba mwaka jana kimkoa imeshika nafasi ya pili na kitaifa imeshika nafasi ya nne.Hata hivyo shule hizo zimetakiwa kuongeza juhudi ili washike nafasi ya kwanza kwa matokeo ya mwaka huu kwa ngazi ya kitaifa na kimkoa.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam Sophia Mjema(mwenye kiremba) akiwa na Mwalim Mkuu wa Shule ya Fourtain Gate iliyopo Tabata Segerea Julius Luge leo baada ya kumkabidhi tuzo maalumu kutokana na shule hiyo kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 10 bora za binafsi katika matokeo ya mtihani wa darasa saba mwaka 2017 kwa shule zilizopo kwenye manispaa hiyo.
 Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko akizungumza katika hafla za utoaji wa tuzo hizo leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na walimu,wanafunzi katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa shule za msingi zilizofanya vizuri katika Manispaa ya Ilala leo jiji Dar as Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii)

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MZEE SYLVESTER LUBALA SHIMBA, BABA MZAZI WA NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini katika kitabu cha maombolezo alipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa mjane wa marehemu Mama Cesilia Kabula Fidelis alipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho walipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa watoto wa marehemu Bw. Richard Lubala (kushoto kwake) na Charles Lubala (kulia kwake) alipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018
Mama Janeth Magufuli akimpa maneno ya faraja Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, kwa kufiwa na baba yake mzazi Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, kwa kufiwa na baba yake mzazi Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakifariji wafiwa walipojiunga na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu Mzee Sylivester Lubala Shimba, baba mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, Mikocheni jijini Dar es salaam leo Aprili 12, 2018.

OPCW yathibitisha matumizi ya sumu ya kemikali Uingereza

Dkt. Philip Mpango atolea Ufafanuzi Kuhusu Deni la Taifa


Tumewachukulia hatua kali Watumishi 434 Kwa Kushindwa Kusimamia Rasilimali Fedha za Umma-Mhe. Jafo

VOA Swahili: Duniani Leo 12th April 2018

ZOEZI LA UTOAJI BIMA YA AFYA KWA WATOTO WALIOTELEKEZWA...

SERIKALI ITAENDELEA KUMUENZI SOKOINE - WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano itaendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma ili kuenzi fikra za hayati Edward Moringe Sokoine.  
“Tutaendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma kwa kuzingatia yale yote ambayo Mheshimiwa Sokoine aliyaanzisha,” amesema. 
 Ametoa kauli hiyo jana Alhamisi, Aprili 12, 2018 wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi waliohudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo cha Sokoine, iliyofanyika kijijini kwake Engwiki, kata ya Monduli Juu, wilayani Monduli, mkoani Arusha. 
Ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu Mkuu  Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha,  Mhashamu Josephat Lebulu, ilihudhuriwa na viongozi wa dini wa wilaya, viongozi wa Serikali na wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Tate ole Nasha na baadhi ya wabunge.
 Waziri Mkuu amesema Mhe. Sokoine alikuwa adui wa wahujumu uchumi na alihakikisha uchumi wa nchi unakua kwa maslahi ya Watanzania wote. “Mungu alitupa hazina iliyong'ara na kuangaza. Sote tuendelee kuangaza kwa kutenda mema na kuendeleza yale yote aliyoyaanzisha mpendwa wetu,” alisema.  
“Katika maisha yake,  hakuwa na ubinafsi, uroho, wala tamaa ya kujilimbikizia mali. Hili ni jambo la kuigwa na sisi viongozi wa umma. Nasi tulioko kwenye nafasi hizi za uongozi,  tumuombe Mungu atuwezeshe tutende yale aliyoyaanzisha,” alisisitiza.  
Alitumia fursa hiyo kuwafikishia wanafamilia na wananchi waliohudhuria ibada hiyo, salaam za pole kutoka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.  
Mapema, akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria ibada hiyo, Askofu Mst. Lebulu alimuelezea hayati Sokoine kuwa ni kiongozi aliyechapa kazi kwa bidii, mwenye uzalendo, aliyeongozwa na upendo na uwajibikaji kwa wananchi anaowaongoza.  
“Ili tuweze kuwajibika na kuwa wazalendo kwelikweli, tunapaswa kuwa waaminifu na watu tunaomcha Mungu. Mtu awaye wa dini yoyote ile, kama hamchi Mungu, hawezi kuwa muwajibikaji.” 
Alisema kila mtu anapaswa kumheshimu mwenzake kwa dini na imani yake. “Tuheshimiane kila mmoja kwa dini na imani yake, kwa sababu sote tumeumbwa kwa sura na mfano wake. Siyo kwamba tuvumiliane, tunatakiwa tusidharauliane bali tuheshimiane,” alisisitiza.

“Ni lazima tuwe waaminifu, tuache unafiki, tuache kuwa na maisha yenye hila na hiyana na badala yake, tuongozwe na dhamiri safi. Tuwe waaminifu kwa wenzetu, kwa dini na imani zetu na zaidi ya yote tuwe waaminifu kwa nchi yetu,” alisema.  
“Ni aibu kukuta Mtanzania anaitukana nchi yake. Tupende vijiji vyetu, tarafa zetu, mikoa yetu na nchi yetu. Tuipende, tuitunze na tuilinde ili iwe nchi bora. Tuwe mfano kwa watoto wetu na wazazi wetu katika kuijali nchi yetu,” alisisitiza. 
Naye, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Kabudi alipopewa nafasi awasalimie wananchi, alisema kuna watu wanakufa lakini bado wanaendelea kuwa hai na kwa hilo, wanafamilia wanapaswa kuendelea kumshukuru Mungu. 
"Tangu alipofariki mwaka 1984, hakuna mtu aliyejua kwamba hadi sasa, ambapo ni miaka 34 imepita, Edward Moringe Sokoine ataendelea kuwa hai. Ninasema yu hai kwa sababu maneno na matendo yake, bado yanaishi,” alisema. 
“Edward Moringe Sokoine amegoma kufa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere amekataa kufa. Na sisi wasaidizi wa Rais Magufuli, tunapaswa kujitoa kwa wananchi na Taifa; kujiongeza zaidi katika utumishi wetu na hasa kuwajibika kwa kulitumikia zaidi Taifa kuliko kudai mapato ili tutakapoitwa kwenye promosheni iliyo kuu, wanaosalia waone faida ya kuwepo kwetu hapa duniani,” alisema huku akishangiliwa.

Akitoa shukrani kwa niaba ya familia, msemaji wa familia ya marehemu Sokoine, Bw, Lembris Kivuyo alisema wanaishukuru Serikali kwa jinsi ambavyo imekuwa karibu sana na familia hiyo tangu Mhe. Sokoine alipofariki. 
“Tunaishukuru sana Serikali na tunazidi kuwasihi Watanzania waendelee kumuombea Mheshimiwa Rais Magufuli ili aendelee kuongoza Taifa hili bila ajizi na sisi kama familia tutaendelea kumuunga mkono Mhe. Rais katika jitihada zake za kutetea rasilmali za Taifa,” alisema.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mjane (mke mkubwa) wa marehemu Edward M. Sokoine Bibi Napono Sokoine, mara baada ya kuwasili nyumbani kwao kushiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi  Aprili 12, 2018. Kulia ni mke mdogo, Bibi      Nekiteto Sokoine.
 Mjane (mke mkubwa) wa marehemu Edward M. Sokoine Bibi Napono Sokoine, akimvisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mgolole wa Kimasai ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyumbani kwao, kijiji cha Engwiki, kata ya Monduli Juu, wilayani Monduli, mkoani Arusha Alhamisi Aprili 12, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo ya marehemu Edward M. Sokoine kabla ya kuanza kwa ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi  Aprili 12, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwaongoza viongozi wa mkoa wa Arusha na wa Serikali kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi Aprili 12, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafamilia baada ya kutoa salaam zake kwa wananchi waliohudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi Aprili 12, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiomba dua baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Sokoine mara baada ya kuhudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo chake iliyofanyika Alhamisi Aprili 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WADAU WA UKANDA WA KATI WATEMBELEA BANDARI DAR ES SALAAM

0
0
Wadau wa Ukanda wa Kati (Central Corridor) wametembelea bandari ya Dar es Salaam ili kuona namna inavyoendesha shughuli zake pamoja na kupatiwa taarifa ya mipango iliyopo ya kuboresha zaidi huduma zinazotolewa bandarini hapo.
Akizungumzia ziara hiyo, Katibu Mtendaji wa Ukanda wa Kati, Kepteni Dukundane Dieudonne alisema wametembelea bandari baada ya kufanya kikao cha siku mbili na kupokea ripoti ambayo inaelezea utendaji kazi wa bandari hyo ambayo iliwarishidha hivyo wakaona ni vyema kufika bandarini ili kuona utendaji wake.
“Tuna furaha kukaribishwa katika bandari ya Dar es Salaam, tuna furaha ya kuona mambo mengi ambayo bandari inafanya ili kutoa huduma kamilifu kwa wadau wote wa Ukanda wa Kati,” alisema Dukundane na kuongeza.
“Tunaipongeza TPA kwa mafanikio mazuri na tumeona mzigo umeongezeka katika bandari hii, wale waliokuwa wanasema wateja wamehama hiyo sio kweli tumeona wadau wengi wamerudi bandari ya Dar es Salaam.”
Naye Mkurugenzi wa Wadau wa Ukanda wa Kati, Desire Hishamunda aliipongeza hatua zinazochukuliwa na TPA ili kuboresha huduma bandarini hapo na kutaka hatua zaidi ziendelee kuchukuliwa ikiwa na pamoja na kuongeza kasi ya utoaji huduma ili meli ziwe zinashusha mzigo kwa haraka na usafirishwe kwenda kwenye nchi zinazopitisha mizigo hapa nchini.
Wadau wa Ukanda wa Kati waliotembelea bandari ya Dar ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Rwanda na Uganda.Kaimu Mkurugenzi Masomo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Lydia Mallya akizungumza jambo na ujumbe wa wadau wa Ukanda wa Kati uliotembelea bandari ya Dar es Salaam walipotembelea mabanda ya maonesho yao.Afisa wa TPA akitoa maelezo kuhusu wiki ya TPA kwa ujumbe wa wadau wa Ukanda wa Kati uliotembelea bandari ya Dar es SalaamKaimu Mkurugenzi Masomo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Lydia Mallya akitolea ufafanuzi kuhusu TPA upanuzi bandali ili kuboresha huduma ambazo zinatolewa bandarini hapo kwa wadau wa Ukanda wa Kati waliotembea bandari hiyo. Kaimu Mkurugenzi Masomo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Lydia Mallya  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Wadau wa Ukanda wa Kati (Central Corridor) kutembelea banadari ya Dar es Salaam ili kuona namna inaendesha shughuli zake pamoja na kupatiwa taarifa mipango iliyopo ya kuboresha zaidi huduma zinazotolea banadarini hapo.Katibu Mtendaji wa Ukanda wa Kati, Kepteni Dukundane Dieudonne akizungumza na waandishi wa habari mara baada Wadau wa Ukanda wa Kati (Central Corridor) kutembelea banadari ya Dar es Salaam na kujionea ufanisi wa bandari hiyo.Mkurugenzi wa Wadau wa Ukanda wa Kati, Desire Hishamunda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kujionea hatua zilizochukuliwa na TPA ili kuongeza kasi ya utoaji huduma ili meli ziwe zinashusha mzigo kwa haraka na usafirishwe kwenda kwenye nchi zinazopitisha mizigo hapa nchini.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images