Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

WATU 29 WAFARIKI KWA AJALI ZA BARABARANI KWA KIPINDI CHA MIEZI MITATU.MKOANI RUVUMA

$
0
0
Watu zaidi ya 29 wamepoteza maisha huku 42 wakiwa wamepata majeraha mbalimbali kutokana na ajali zilizotokea mkoani wa Ruvuma kwa kipindi cha miezi mitatu kwa mwaka 2018. Huku sababu kubwa za ajali hizo zikitajwa ubovu wa miundombinu pamoja na malipo madogo kwa baadhi ya madereva.

WWF YAZINDUA MRADI WA KUHIFADHI MAZINGIRA-MTWARA

$
0
0
Na Joseph Mpangala-Mtwara

Shirika la Kuhifadhi mazingira duniani WWF imezindua Mradi wa Kuleta mabadiliko katika usimamizi na Uendelezaji wa Maliasiri za misitu,wanyapori na bahari kwa kushirikisha Asasi za Kiraia pamoja na Wananchi katika mikoa ya Kusini.

Mradi huo wa miaka mitano unagharimu zaidi ya shilingi Billion10 fedha ambazo ni msaada kutoka shirika la maendeleo la SIDA kutoka Nchini Sweden kwa lengo la kusaidia Serikali na wananchii katika Kuboresha Usimamizi wa maliasili.

Akiongea katika Uzinduzi wa Mradi huo Mkurugenzi wa shirika la WWF hapa Nchini Dk.Amani Ngusaru amesema katika Mradi Utawezesha akina mama na Vijana ili kuhakikisha wanachochea mabadiliko katika katika usimamizi wa maliasili kwa ajili ya matumizi ya Vizazi vya sasa na Vijavyo.

Dr.Amani ameongeza kuwa Bado Maliasiri zetu zinakabiliwa na Changamoto ya Uharibifu unaochangiwa na Ongezeko la Shughuli za kibinadamu.

“katika hivi karibuni kumekuwepo na uvamizi mkubwa wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya shughuli za Kilimo,Malisho ya Mifugo,Uchimbaji wa madini,ukataji wa miti mjanga ya moto pamoja na uvunaji wa misitu ya asili kwa ajili ya ujenzi”amesema Dk.Amani.

Mradi huu unaafanyakazi katika mikoa ya Lindi,Rumuma pamoja na mtwara.

Mkurugenzi wa WWF hapa nchini Dr.Amani Ngusaru akiongea na wawakilishi wa asasi mbalimbambali za kiraia wakati wa uzinduzi wa Mradi wa uendelezaji Maliasili Mkoani Mtwara. 
.Kaim Mkurugenzi wa Tunduru Jonathan A Haule wakatikati akionesha Kitabu cha WWF mara baada ya kufanya Uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji wa maliasi katika mikoa ya kuzini

MAKALA SHERIA: POLISI HAWARUHUSIWI KUCHUKUA KESI ZA KUDAIANA HELA

$
0
0
Na Bashir Yakub.
Yapo mambo tunatakiwa kuyazungumza mara kwa mara ili watu wayaelewe. Moja ya mambo hayo ni hili la watu kudaiana hela hadi kufikishana polisi. Mtu binafsi, Saccos au taasisi imekukopesha fedha, na hatimaye umeshindwa kulipa, wanachokifanya ni kukupeleka polisi. Huko polisi ati unaandikishwa maelezo na wakati mwingine unatakiwa kusaini mkataba mpya wa lini na namna gani utalipa deni.

Au wakati mwingine unawekwa ndani kabisa, au huwekwi ndani ila siku ambayo umeambiwa kulipa ikifika hujalipa ati askari anakupigia simu kukuuliza kwa nini hujalipa deni , na vitisho vya kukukamata na kukuweka ndani, au wakati mwingine unakamatwa kabisa na kuwekwa ndani.

Kwa ufupi haya yote ni makosa makubwa. Ni makosa kwa askari yeyote ambaye ameamua kuchukua kesi ya aina hii, na ni makosa hata kwa yule anayedai ambaye amekwenda kuripoti .


 

1.KUDAIANA  HELA.
Masuala ya kudaiana hela ni masuala ya madai(civil). Polisi hawahusiki kabisa na masuala ya madai. Polisi wanahusika na masuala ya jinai(criminal). Kudai hela si masuala ya jinai hata kidogo. Masuala ya jinai wanayohusika nayo polisi ni yale yote yaliyoorodheshwa katika Sheria ya Kanuni za adhabu, Sura ya 16 ambayo ni kama kubaka,kuiba, kutukana, kulawiti,kupigana, kuharibu mali , kujeruhi, rushwa, dawa za kulevya, uhaini, mauaji, kughushi, na mengine yaliyo katika sheria nyingine mtambuka yanayofanana na hayo.
2. HATA KUWEKWA CHINI  YA ULINZI TU KWA MADAI YA HELA HAIRUHUSIWI.
Kutoruhusiwa kwa polisi kujihusisha na masuala haya ya madai ya kudaiana hela kumeelezwa kwa mapana. Si tu polisi hawaruhusiwi kukuweka ndani kwa makosa kama haya bali pia hawaruhusiwi hata kukuweka chini ya ulinzi. Kukuweka chini ya ulinzi ni kuzuia uhuru wako wa kutembea kwa namna yoyote ile, hata kwa kukwambia hapo ulipo usitoke.
Katika kesi ya Rudolf v Athumani (1982) TLR 100 mahakama ilisema kuwa ni  kazi ya polisi pale wanapoletewa mashtaka  kuchambua ikiwa mashtaka yaliyoletwa kwao ni madai au ni jinai  ili ikiwa ni jinai wayachukue na ikiwa ni madai waachane nayo na wamshauri mleta mashtaka/malalamiko(informer) hatua sahihi za kuchukua.
Jaji Sammatta aliongeza kuwa polisi hawaruhusiwi kumweka mtu chini ya ulinzi kwa makosa ya madai.


        KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AKEMEA UPOTOSHAJI KUHUSU MUUNGANO

$
0
0
*Awataka waulinde, aonya sukari isiwe sababu
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waulinde Muungano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na akawaonya wasitumie Bunge hilo kuupotosha.

Ametoa kauli hiyo Jumanne, Aprili 10, 2018 Bungeni mjini Dodoma kwenye mkutano wa 11 wa Bunge, wakati akihitimisha mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019.

Waziri Mkuu amesema mjadala ulioibuka jana kuhusu suala la Muungano haukuwa na afya na kwamba hatarajii kuona hali hiyo ikijirudia tena Bungeni kuhusiana na suala la Muungano.

“Mjadala wa jana sijaupenda kabisa na wala haukuwa na afya, ulikuwa ni malumbano baina waheshimiwa wabunge wawili. Hatuzuii Mhe. Mbunge kuuliza jambo ili apate ufafanuzi lakini pia haturuhusu mtu na mtu watumie Bunge kupotosha ukweli wa mambo,” alisisitiza.

Waziri Mkuu amelieleza Bunge kwamba kuna maboresho ambayo yanafanywa hivi sasa na Serikali za pande zote mbili lakini akatumia fursa hiyo kulihakikishia Bunge kwamba majadiliano bado yanaendelea kwenye vikao halali vya SMT na SMZ ambavyo vinaongozwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akitoa ufafanuzi kuhusu chanzo cha malumbano hayo, Waziri Mkuu alisema kiini cha malumbano hayo ni suala la uagizaji sukari kutoka nje ya nchi ili kufidia upungufu wa sukari uliopo nchini (gap sugar). Alisema katika kutimiza azma hiyo, Serikali haiangalii kama muagizaji ametoka Tanzania Bara au Tanzania Zanzibar.

Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema katika mwaka 2016, upungufu uliojitokeza ulikuwa tani 140,000 lakini waagizaji waliopewa vibali walikuwa wawili kutoka Zanzibar, watatu kutoka Bara na kiwanda cha sukari cha Mahonda kilipewa kibali cha kuagiza tani 390.

“Katika mwaka 2017, gap sugar ilikuwa tani 140,000 na waliopewa vibali walikuwa ni wawili kutoka Zanzibar na wawili kutoka Bara, lakini kwa mwaka huu (2018) gap sugar ni tani 135,000. Tofauti na miaka ya nyuma, safari hii tumewapa vibali wenye viwanda ndiyo waagize sukari kutoka nje. Kwa hiyo, jambo hili la sukari lisivuruge Muungano wetu,” alisisitiza.

Waziri Mkuu alisema nia ya Serikali ni kuzalisha sukari ya kutosha hapa nchini ili nchi ijitegemee na kawataka Mawaziri wa Biashara wa Zanzibar na Tanzania wawe makini ili sukari inayoagizwa nje isije kufurika soko la ndani kwa sababu gharama za uzalishaji sukari ya ndani ni kubwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihitimisha Hoja ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma, Aprili 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAHAKAMA KISUTU YATAKA KILA CHOMBO KIHESHIMIWE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kila chombo kinapaswa kufanya kazi zake kwa kuheshimiana na haipendezi kila mara zitolewe amri ambazo hazitekelezwi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ameyasema hayo leo Aprili 11 mwaka wakati kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkaboli mmiliki wa IPTL Harbinder Sethi na mwenzake, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutekeleza amri aliyoitoa ya kumpeleka mshtakiwa Sethi kutibiwa katika Hospital ya Taifa Muhimbili.

"Ninaamini, kila chombo kinapaswa kufanya kazi zake kwa kuheshimiana, haipendezi kila wakati tutoe amri ambazo hazitekelezwi, hivyo naamuru apelekwe hospital kinyume na hapo nitatoa amri nyingine kwa mujibu wa sheria,"amesema Hakimu  Shaidi.

Mapema, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mahakani hapo upelelezi wa kesi hiyo bado hujakamilika, pia wameshindwa kumpeleka Sethi hospital kwa sababu Sethi alihamishwa gereza kutoka Segerea kwenda Ukonga, pia alidai mshtakiwa aliomba daktari wake kutoka Afrika Kusini awepo wakati akipatiwa matibabu.

Wakili wa utetezi, Hajra Mungula alipinga vikali Hoja hizo na kudai kuwa hazina msingi kwa sababu Sethi hakuwahi kuzungumzia suala la daktari na kuongeza, kuwa katika gereza la Ukonga Sethi haruhusiwi kuonana na mtu yoyote hata mke wake wa ndoa.

Kutokana hoja hizo,  Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 25 mwaka 2018.

Mbali ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya dola za Marekani USD 22, 198,544.60 na Sh.bilioni 309.

MATUKIO YA OFISI YA WAZIRI MKUU BAADA YA BUNGE KUPITISHA BAJETI YA OFISI HIYO

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipongezana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Ofisi hiyo Aprili 10, 2018.
 Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja za Wabunge zinazohusu ofisi hao wakati wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Bungeni Dodoma, wa kwanza ni Bw.Erick Shitindi anayeshungulikia Kazi,Ajira, Vijana na wenye ulemavu, kulia kwake ni Prof.Faustin Kamuzora (Sera na Uratibu) kulia kwake ni Bi.Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu).
 Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja za wabunge kuhusu ofisi yao wakati wa kujadili na kupitisha Bajeti hiyo kwa mwaka wa Fedha 2018/2019.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt.Irene Isaka mara baada ya Bunge kupitisha bajeti Ofisi hiyo.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Bunge na Siasa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Yona Mwakilembe Bungeni Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA BALOZI WA UGANDA NCHINI TANZANIA.

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Mabonero (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza mgeni wake Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Mabonero (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

LIGI KUU WANAWAKE BARA HATUA YA NANE BORA KUENDELEA APRILI 21

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya  jamii

LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania Bara hatua ya Nane bora inatarajia kuendelea Jumapili Aprili 21 kwenye viwanja tofauti.

Hatua hiyo ya Nane bora ambayo ilisimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) iliyokuwa kambini kujiandaa na mchezo wake wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake itaendelea katika mzunguko wa Tano.

Pia hatua ya nane bora inachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ikishirikisha timu za Panama FC ya Iringa inayotumia Uwanja wa Samora, Evergreen Queens ya Dar es Salaam inayotumia Uwanja wa Karume, JKT Queens ya Dar es Salaam wanaotumia Uwanja wa Mbweni na Alliance ya Mwanza wanaotumia Uwanja wa Nyamagana.

Timu nyingine ni mabingwa watetezi Mlandizi Queens ya Pwani wanaotumia Uwanja wa Mabatini,Baobab ya Dodoma wanaotumia Uwanja wa Jamhuri Dodoma,Kigoma Sisters ya Kigoma wanaotumia Uwanja wa Lake Tanganyika na Simba Queens wanaotumia Uwanja wa Karume.

Huu ni msimu wa pili wa Ligi ya Wanawake kuchezwa ambapo katika msimu wake wa kwanza timu ya Mlandizi Queens ndio waliibuka na ubingwa.

SIMBA YAIVUTIA KASI MBEYA CITY, WAENDELEA NA MAZOEZI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

KIKOSI cha Simba kimeendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbeya hapo kesho.

Mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Taifa utawakutanisha timu hizo huku Mbeya City akitaka kujinasua kutoka katika hatari ya kunusa kushuka daraja huku Simba wakitaka kuendelea kukalia kiti cha uongozi wa ligi.

Kikosi hicho cha Simba kinajifua kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo jijini Dar es Salaam leo asubuhi na jioni.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba iliwakosa wachezaji Juuko Murushid, James Kotei na Erasto Nyoni ambao walikuwa wanatumikia adhabu ya kadi 3 za njano kwa kila mmoja.

Tayari wachezaji hao wameshamaliza adhabu hiyo na kesho wanatarajia kuwa sehemu ya kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi  Simba.

Kocha Msaidizi wa Simba Masoud Djuma ameonekana hana wasiwasi na kikosi chake kuelekea mchezo huo wa kesho ambapo anaamini ushindi ndiyo jambo la msingi ili kupata ubingwa wa msimu huu.

Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 52 wakifuatiwa na mahasimu wao Yanga wenye alama 46 ambapo wanacheza leo dhidi ya Singida.

MAHAKAMA KISUTU YASOGEZA MBELE TAREHE YA KUSOMWA MAELEZO YA AWALI VIGOGO TFF

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele tarehe ya  kuwasomea maelezo ya awali (PH ) ya vigogo watatu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hadi Aprili 18/2018.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuitaarifu Mahakama kuwa wanaomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwanza ndiyo waendelee na PH.

Wakili Kimaro amedai, "kesi leo imepangwa kwa ajili ya PH, Mimi ndiyo nimepangiwa kuendelea na kesi hii, nimefanya Mawasiliano na (Takukuru) tukapitia ushahidi uliokusanywa hivyo tunaomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka Kwa kuongeza washtakiwa wengine ndiyo tuendelee na PH" ameeleza..

Maelezo hayo ya awali leo yalipaswa kusomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Kimaro aliendelea kudai kuwa mmoja wa washtakiwa wanaopaswa kuunganishwa kwenye kesi hivyo yupo nje ya Dar es Salaam na utaratibu wa kumleta umekamilika.

Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 18 mwaka 2018.

Watuhumiwa katika kesi hiyo ni, aliyekuwa Rais TFF, Jamal  Malinzi(57), Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine(46) na Mhasibu, Nsiande Mwanga(27)

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. 7

Katika kesi hiyo, Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 ya uhujumu uchumi ikiwamo kughushi na utakatishaji wa fedha dola za marekani 375,418.

WAKULIMA WA KOROSHO TANDAHIMBA WAIDAI KAMPUNI YA JOPHULO LIMITED ZAIDI YA BILIONI 3, WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI.

$
0
0
Wakulima wa zao la korosho wilaya ya Tandahimba na Newala mkoani Mtwara wamelalamikia kitendo cha kampuni ya JOPHULO LIMITED kutowalipa fedha zao zenye thamani zaidi ya Shilingi bilioni 3 tangu kufanyika kwa mnada wa 11 Disemba mwaka jana . Wakizungumza na Ruvuma Tv , wakulima hao wanasema hali hiyo inawafanya kushindwa kujipanga na msimu mpya wa kilimo ambapo wanatumia nafasi hii kuomba serikali kuingilia kati sakata hilo.

YANAYOFANYIKA BANDARI DAR YAWAKUNA WANAFUNZI IFM

RC SHINYANGA AWATAKA WAKAZI MKOA WA TABORA KUTUNZA , KULINDA MISITU ASILI

$
0
0
Na Tiganya Vincent
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack amewataka wakazi wa Mkoa wa Tabora kutunza na kulinda mistu ya asili na miti inayopandwa sasa hivi ili ikuyafanya mazingira kuwa endelevu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Alisema kama watafanya mchezo na kuacha baadhi yao watu waingie ndani ya mistu na kukatakata ovyo rasilimali za mistu upo uwezekano wa hali kuwa mbaya  na kukosa hata mvua kidogo zinapatikana hivi sasa kutokana na kutoweka kwa mistu.

Telack alitoa rai hiyo jana mjini Tabora wakati akifunga kongamano la siku la mazingira ambalo liliwahusisha wadau mbalimbali likiwa na lengo la kuweka maazimio ambayo yatasaidia katika kupambana na uharibifu na mistu.

Alisema kama wanataka kuona athari za uharibifu wa mazingira , wanatakiwa kwenda kuangali Shinyanga ilivyoathirika na ukataji ovyo wa miti katika Wilaya mbalimbali kama vile Kishapu.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa ni vema wananchi wakaungana na viongozi na wadau wengine kuwakemea wale wote wanaingia katika mistu na kukata miti hivyo hata bila ya kuwa na vibali vya viongozi.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa siku wa mazingira uliofanyika jana mjini Tabora. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Queen Mlozi.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akifungua jana kongamano la siku moja la wadau mbalimbali la kujadili masuala ya kuboresha hali ya ulinzi na usalama mkoani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack  akisisitiza jambo wakati wa kufunga mkutano wa siku wa mazingira uliofanyika juzi(jana) mjini Tabora.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi na kushoto ni Mkiuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri. Picha na Tiganya Vincent.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

YANGA YATAJA KIKOSI KITAKACHOANZA DHIDI YA SINGIDA UNITED LEO

$
0
0
Zainab Nyamka, Globu ya jamii

KIKOSI cha Young Africans kitakachoanza dhidi ya Singida United katika mechi ya Ligi Kuu Bara inayochezewa leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mlinda mlango ni  Youthe Rostand, namba mbili ni Hassan Kessy, namba tatu Haji Mwinyi, namba 4 Abdallah Shaibu, namba 5 Kelvin Yondani, namba 6 Papy Tshishimbi wakati namba 7 ni  Yusuph Mhilu.

Namba 8 atacheza Raphael Daudi, namba 9 Obrey Chirwa, namba 10 Pius  Buswita na namba 11 ni Ibrahim Ajibu


Wakati kikosi cha akiba
12 Ramadhani Kabwili, namba  
13 Juma Abdul, namba 
14 Nadir Haroub, namba 
15 Said Makapu
16 Geofrey Mwashiuya
17 Emmanuel Martin
18 Juma Mahadhi.

WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Geita wamejitokeza kwa wingi kupata elimu ya mlipakodi inayoambatana na usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) pamoja na kupatiwa makadirio ya kodi kwa wafanyabiashara mbalimbali.

Akizungumza baada ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wa Wilaya ya Bukombe na Mbogwe wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa, Afisa Kodi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Maternus Mallya amesema mwitikio wa wananchi ni mkubwa na unaridhisha.

"Nimefurahishwa sana na mwitikio wa wananchi wa Mkoa wa Geita kwasababu wengi wameonyesha kiu ya kupata elimu na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi na mpaka sasa takribani wafayabiashara 200 wamesajiliwa na kupatiwa namba hiyo pamoja na kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato," alisema Mallya.

Nae mfanyabiashara wa kuchomelea mageti wa Wilaya ya Bukombe, Mandela Alex amesema kuwa, amefurahishwa na ujio wa kampeni hii wilayani kwake  kwani biashara yake imetambulika na kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa kibiashara.
 Afisa wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) George Haule (kushoto) akitoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa na inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.
 Afisa wa Kodi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Maternus Mallya (kulia) akitoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa na inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.
 Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Adela Kayella akimuhudumia mfanyabiashara aliefika kwenye Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani Geita. Kampeni hiyo inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.
 Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakipita katika maduka mbalimbali kutoa elimu ya masuala yanayohusu kodi wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani Geita. Kampeni hiyo inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMPUNI YA TECNO TANZANIA YAMPA UBALOZI GABO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MUGIZAJI wa filamu za kibongo nchini Salim  Ahmed a.k.a Gabo, ametangazwa kuwa balozi wa simu mpya ya mkononi kutoka Kampuni ya Tecno Tanzania iliyopewa jina la Tecno Pop 1 ambayo itauzwa kwenye maduka yote ya Vodashop nchini.

Akizungumza Dar es Salaam wakati wa  kumtangaza Gabo kuwa balozi wa simu hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na ushirikiano wa Tecno,Anuj Khosla amesem wameamua kuileta simu hiyo ili kuwasaidia wananchi wa kipato cha  chini kumiliki simu janja .

"Tuna furaha kubwa kuwatangazia uwepo wa simu hii ambayo mtu akinunua atapata na GB 10 kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ili kuperuzi mtandao na kujielimisha kupitia simu hii janja ambayo ina uwezo mkubwa,"amesema Khosla

Kwa upande wake Gabo amesema anaishukuru Tecno kwa kumpa nafasi hiyo ya kufungua njia kuwa balozi kwani ndio ubalozi wa kwanza kuupata tangu aanze kujulikana katika tasnia ya filamu.

"Naamini huu ndio mwanzo wa mimi kuendelea kufanya kazi na kampuni kubwa baada ya hii kampuni ya simu kuniona Gabo na kunifanya kuwa balozi wa kutangaza bidhaa zao.Ni jambo jema ambalo kila msanii anatamani kulifikia ukiacha mafanikio ya sanaa ya kawaida,"amesema Gabo.


Amesema kwa sasa yeye kama msanii mkubwa anatumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kwa mashabiki na kuwataka watumie simu hizo ambazo zina ubora na bei nafuu mpaka kwa watanzania wa kawaida.
 Mkuu wa kitengo cha Biashara na ushirikiano wa Tecno, Anuj Khosla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Simu mpya ya Tecno POP 1 itakayotolewa na GB 10 za Vodacom   leo Jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa Filamu wa nchini, Salim  Ahmed "Gabo", akionyesha simu aina ya Tecno POP inayotolewa na GB 10 Za Vodacom. kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha manunuzi  ya rejareja ya simu kutoka Vodacom, Brigita Stephene.
Msanii wa Filamu wa nchini Salim  Ahmed "Gabo" akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Vodacom na Tecno Tanzania.

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA

Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu

$
0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Juma Assad amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea vizuri na uwekaji wa mahesabu uliopelekea kupungua kwa hati chafu katika Taasisi na miradi mbalimbali ya Serikali. 

Prof. Assad ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2017.

"Katika ukaguzi wa hesabu nilioufanya katika Serikali Kuu na Taasisi zake, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2016/17 nimetoa jumla ya Hati 561 za ukaguzi. Kati ya hati hizo, Hati zinazoridhisha ni 502 sawa na asilimia 90, Hati zenye shaka ni 45 sawa na asilimia 90, Hati zenye shaka ni 45 sawa na asilimia 8, Hati zisizoridhisha ni Saba sawa na asilimia Moja na Hati Mbaya ni Saba sawa na asilimia Moja," alisema Prof. Assad. 

Amesema, katika ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Taasisi mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ametoa jumla ya Hati za Ukaguzi 742 ambapo Hati zinazoridhisha ni 697 sawa na asilimia 94, Hati zenye shaka ni 44 sawa na asilimia 5.9 na Hati isiyoridhisha ni moja, Hati hii imetolewa kwa mradi wa maji (WSDP) unaotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Wilaya ya Makete. 

Naye, Mjumbe wa Kamati ya LAAC Mhe. Abdallah Mtolea amezipongeza Halmashauri zilizofanya vizuri kwa kuonekana kupunguza idadi ya hati chafu na kushamiri kwa hati safi.

Aidha Mhe. Mtolea amesema kuwa kamati hiyo itaziita Halmaushari na kufanya nazo mahojiano bila kuujali matokeo ya ukaguzi kama zilifanya vizuri au vibaya ili kuhakikisha kuna kuwa matumizi mazuri ya fedha za umma.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Juma Assad akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu  ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2017.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC, Naghenjwa Kaboyoka akizungumza kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali baada ya CAG kuwasilisha ripoti za Hesabu za Serikali  kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2017.
 Sehemu ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Juma Assad  leo mjini Dodoma kuhusu ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2017.
Mbunge wa Temeke, Abdalah Mtolea akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya LAAC mara baada ya  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Juma Assad kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti za Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2017.Katikati ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Juma Assad na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC mhe. Naghenjwa Kaboyoka.(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

RC MAKONDA KUTOA KADI ZA BIMA YA AFYA KWA WATOTO WALIOTELEKEZWA.

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema kinamama wote waliofika ofisini kwake wakiwa na watoto kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa atawapatia kadi za Bima ya Afya (Toto Afya Card) Bure kwa ajili ya matibabu ya watoto wao.

RC Makonda amesema kadi hizo zitatolewa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 17 kwa kila mama aliefika ofisini kwake pasipokujali idadi ya watoto alionao.

Uamuzi huo umekuja baada ya RC Makonda kujionea mateso wanayopata kinamama hao ikiwemo watoto kuugua Magonjwa yanayohitaji gharama kubwa za matibabu na kwakuwa wengi wa kinamama hao wana hali ngumu kimaisha wanashindwa kumudu gharama na kusababisha maumivu na mateso kwa mtoto.

Aidha RC Makonda amesema hadi kufikia mchana wa leo zaidi ya kinamama 1,030 walikuwa tayari wamesikilizwa na Kati ya hao watu mashuhuri 107 wakiwemo wanasiasa na viongozi wa dini wametuhumiwa kutelekeza watoto.

Hata hivyo RC Makonda amesema kuanzia wiki ijayo kinababa waliotelekeza watoto wataitwa ofisini kwake kwaajili ya kutoa ufafanuzi na atakaekaidi kufika atachukuliwa hatua kaliza kisheria.

RC Makonda aliongeza hayo wakati wa zoezi la kubaini Wazazi waliokimbia Watoto wao linaloendelea katika ofisi zake,amesema kuwa idadi hiyo imebainika jana na juzi wakati wa zoezi hilo, pia amesema kuwa si kundi hilo tu la watu mashughuli pia kuna kundi la Watu ambao wanaona aibu kufika katika eneo hilo.

"Hawa Watu wanaona aibu kufika ofisini ofisini hapa, hakuna kukutana na mimi chemba, habari yakupigiana simu kuniambia Mheshimiwa naomba nije peke yangu hakuna", amesisitiza Makonda

"Watu Mashughuli, watu wenye heshima tukikupima DNA nakugundua mtoto ni wako, basi utalipa fidia zote za huyo mtoto".Amesema wale wanaokaidi wito kufika ofisini hapo, kuanzia kesho watapelekewa barua pamoja na kupigiwa simu.

Zoezi hilo lakubaini Wazazi waliokimbia watoto wao lilianza siku ya Jumatatu ya April 9, 2018 na linatarajiwa kumalizika siku ya Ijumaa April 13 mwaka huu.
 Baadhi ya Akina Mama waliojitokeza katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kudai fidia za Watoto wao kwa Wazazi wenzao waliokimbia watoto hao.
 Mmoja wa Maafisa wa Ustawi wa Jamii akiwasikiliza Wazazi wa Kiume walioitikia wito kufika Ofisni kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
 Baadhi ya akina Baba waliotikia wito kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusikiliza malalamiko kwa wake zao. (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA)

MADE IN TANZANIA WEEK IN KENYA

$
0
0



MADE IN TANZANIA WEEK IN KENYA
 The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation through its Embassy in Nairobi, Kenya and in collaboration with the Ministry of Industry, Trade and Investment (Tanzania Mainland); Ministry of Trade, Industry and Marketing (Zanzibar); Tanzania Trade Development Authority (TanTrade); and Tanzania Private Sectors has organized “Made in Tanzania Week” seeking to pursue wider and broader markets opportunities for country’s industrial products and tourism potentials in the East African Community which will take place between 25th to 28th April 2018 in Kenya.

This comes as an effort in the implementation of the country’s Foreign Policy which focuses on Economic Diplomacy with much emphasis on the development of sectors like trade, investment and tourism. The event will fall within the National Day (54th Union Day celebration) on 26th April 2018 and will feature industrial products, services in particular tourism, technology, agribusiness, culture, arts and craft.

It should be recalled that, in 2010 the East African Community Partner States signed an agreement on the Common Market Protocol; hence “Made in Tanzania Week in Kenya” will be amongstGovernment initiatives to promote the forging relationship that has been existing among the Partner States in the Community and spearhead economic development.  
The Tanzania week in Kenya, which will take place at the Kenyatta International Convention Center (KICC) is scheduled as follows; on the 25th– 28th April 2018 "Made in Tanzania” Exhibitions to showcase Tanzanian products will take place followed by Tanzania - Kenya Business to Business (B2B) meeting on 25th April 2018. Again, on 26th April 2018 a reception for the 54th Union Anniversary will be held at the High Commissioner’s residence in Nairobi. The 54th Union celebrations will be concluded by two major events; the Tanzania - Kenya Business Forum that will take place on 27th April 2018 and Made in Tanzania Business Gala Dinner.

On behalf of the Organizing Committee Co-Chaired by Tanzania Trade Development Authority (TanTrade) and Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation would like to invite the key stakeholders particularly the business community to take advantage of this opportunity and participate in the event.

For more information on Made in Tanzania Week in Kenya, kindly call +255767123055 or +255687368443 or register ONLINE via www.tanzaniakenya.com.


Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dar es Salaam.
23rd March 2018
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images