Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Mawaidha ya Sheikh Hamad Jongo Wakati wa Swala ya Idd El Fitr jijini Dar


Michuzi Blog Exclusive: sheikh ponda issa ponda aibukia Morogoro katika kongamano la kiislamu

$
0
0
KATIBU  wa Jumuiya ya Kiislamu nchini , Shekhe Ponda Issa Ponda akihutubia kwenye Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege , Kata ya Saba Saba , Manispaa ya Morogoro, Jumamosi Agosti 10, 2013.
 
Shekhe Ponda Issa Ponda akihutubia kwenye Kongamano hilo.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
'Love Come Down' ya Evelyn Champagne King ilitamba enzi zake na hadi leo...

Dr Josee Chameleon alivyokamua ndani ya Escape one usiku wa kuamkia leo jijini Dar.

dc makete ataka elimu ya vvu iende pamoja na ujasiriamali

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mhe. Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya akisikiliza maelezo ya mradi huo kutoka SUMASESU
 Mkurugenzi wa shirika la SUMASESU Egnatio Mtawa akitoa maelezo kwa washiriki kuhusu utambulisho wa mradi uitwao "Vijana wa makete na mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi" katika ukumbi wa HIMA Makete wakati wa utambulisho wa mradi huo ngazi ya wilaya Augusti 09, 2013. Shirika la SUMASESU ndilo litakalotekeleza mradi huo kwa ushirikiano na UNICEF
Na Edwin Moshi, Makete
 Washiriki wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mkurugenzi wa SUMASESU (hayupo pichani)
 Mratibu wa ukimwi halmashauri ya wilaya ya Makete CHAC Ester Lamosai(kushoto) akiwa na Anifa Mwakitalima kutoka SUMASESU
Mtaribu wa ukimwi sekta ya afya (DAC) Dk Shadrack Sanga akichangia hoja kwenye kikao hicho
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mhe. Josephine Matiro akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mradi huo ngazi ya wilaya katika ukumbi wa HIMA Makete
Makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Makete Jison Mbalizi akiahirisha kikao hicho
=======
Habari na picha na Edwin Moshi, Makete
Wadau wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kwa vijana wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutoa elimu hiyo sanjari na elimu ya ujasiriamali kwa pamoja kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo kwa kasi zaidi

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro wakati akifungua mradi wa vijana wa Makete na mapambano dhidi ya UKIMWI uliozinduliwa Ijumaa Agosti 9, 2013 ngazi ya wilaya, mradi ambao utatekelezwa na shirika la sumasesu kwa ufadhili wa UNICEF
Matiro amesema vijana wengi wamekuwa wakipatiwa elimu hiyo ya namna ya kujilinda na maambukizi mapya ya vvu na baada ya hapo wanakosa kazi ya kufanya hivyo kuwa rahisi kwao kujiingiza kwenye vitendo vitakavyowasababishia kupata vvu.
"Kijana anapewa elimu sawa lakini hana cha kufanya mwishowe akija mtu wa kuwarubuni hasa kifedha wanaingia kilaini kwa kuwa hana shughuli yeyote inayomuingizia kipato, mwishowe anaweza kupata vvu"alisema Matiro
Amewataka vijana kujiunga na vikundi mbalimbali ili waweze kupatiwa mikopo nafuu kwa ajili ya shughuli hasa kilimo kwa kuwa wakishajiunda na kutoa taarifa yeye kwa kushirikiana na halmashauri watawasaidia kupata mkopo ambapo wakati huo huo wakiwa na shughuli ya kufanya halafu wakapata elimu ya kujikinga na vvu itakuwa bora na yenye manufaa kwao.
Wadau walioshiriki katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa HIMA Makete akiwemo mratibu wa ukimwi sekta ya afya (DAC) Dk Shadrack Sanga amelitaka shirika hilo wakati wa kutekeleza mradi huo watoe elimu ya tohara kwa vijana wa kiume ambapo akiwataarifu wao kama idara ya afya wako tayari kuungana nao jambo lililoungwa mkono na kaimu mganga mkuu Boniphace Sanga ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho.
Kwa upande wao shirika la SUMASESU kupitia kwa mkurugenzi Egnatio Mtawa alipongeza kwa ushirikiano uliooneshwa na wadau wote huku akimuahidi mkuu wa wilaya kuwa wataingiza mada ya ujasiriamali wakati wakitoa elimu ya ukimwi kwa vijana ili iwasaidie huku akiahidi kushirikiana na kila wahusika ili mradi huo ufanikiwe
Mradi huo utakaotekelezwa hadi Julai 2015, utahusisha kata za Ipelele, Iniho, Iwawa, Isapulano na Kitulo

JK amtembelea mzee wa kijijini msoga mzee Khalfan Tengeneza Mchaga

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mzee Khalfan Tengeneza Mchaga, mmoja wa wazee katika kijiji cha Msoga,kata ya Chalinze ,wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani  leo wakati Rais alipomtembelea kumjulia hali.Rais Kikwete alikuwa katika mapumziko ya mwisho wa wiki kijijini Msoga. Picha na Freddy Maro.

LEDGER PLAZA-BAHARI BEACH HOTEL DAR ES SALAAM KUMEKUCHA

$
0
0
 Geti kuu la hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza-Bahari Beach jijini Dar es salaam ambayo imefunguliwa hivi karibuni na kuwa kivutio kwa wadau wa kila aina hasa siku za Jumapili na Sikukuu. Tofauti na hoteli kibao za ufukweni hapa kiingilio ni bure ila unatozwa huduma kama vile kutumia bwawa la kuogelea, chakula na michezo ya watoto
 Ankal akiwa na wadau Bahari Beach katika Iddi tatu leo Jumapili.

MAJENGO YA KISASA NJE YA DAR ES SALAAM YAZIDI KUMEA

$
0
0
 Kibo Commercial Complex lililopo maeneo ya Tegeta pembeni mwa barabara ya Bagamoyo Road ni moja tu ya majengo mengi ya biashara yanayomea kwa kasi pembezoni mwa jiji la Dar es salaam ambalo muda si mrefu ujao utakuwa hauna City Centre tena. Hvyo sio kweli kwamba majengo mapya yote yanajengwa 'Posta'
 Ni mjengo wa nguvu. Hata ukumbi wa muziki na mikutano pia umo humo
Benki ya CRDB imesogeza huduma zake kwa wadau wa maeneo hayo ya Tegeta

Shining the Spotlight on Linda Bezuidenhout

$
0
0


Linda Bezuidenhout (LB) is a fashion designer who is based in Atlanta, USA. Linda has been involved in fashion industry for over 20 years, in Africa, Europe and the USA. The LB line is influenced by a wide range of world fashion, cultures and trends.
Linda comes from a Dutch-Tanzanian background and has been influenced with fashion since the age of 8 when she used to insist on designing her own holiday & special occasion clothes and have local tailors sew the dresses. As a teenager she lived in several different countries in Europe which developed her fashion vision and exposure. In her 20′s she moved back to Africa (Tanzania) and continued contributing to the fashion scene there as a top beautician with involvement in various beauty pageants in conjunction with some of the top African female singers such as M'bilia Bel & Vivic Motuwa. In her late 20′s she moved to USA and got involved in the men's world of fashion as well and owned several menswear stores in different malls in the US.
For more video and exclusive interviews 
go on www.swahilitv.blogspot.com

news alert: FEZA KESSY ATOLEWA BIG BROTHER AFRICA HOUSE MUDA

$
0
0
Mshiriki wa Big Brother House Feza Kessy ametolewa muda huu katika mjengo akiwa Mtanzania wa emwisho aliyesalia kwenye nyumba hiyo.
Hii ni habari ya kusikitisha kwa Bongo ambapo wadau wamekuwa wakijitahidi kumpigia kura mwanadada huyu mcheshi...

DADA DINACARES YALA CHAKULA CHA MCHANA NA WATOTO YATIMA AZULA BEACH KAWE JIONI YA LEO.

$
0
0
  Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares (pichani Mbele),akiwa sambamba na baadhi ya Wadau waliojitokeza kuifanikisha hafla hiyo ya chakula cha mchana na watoto Yatima kutoka vituo vitatu,kushoto ni  Dada  Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet na wadau wengineo.
 Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akiongea na Watoto kutoka vituo Yatima,kabla ya kukata keki na kuwalisha.
Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akimlisha keki mmoja wa watoto waishio katika mazingira Magumu kutoka kituo cha Watoto yatima cha Vetenari Temeke.
 Watoto wakipakuliwa chakula safi kabisa.
Baadhi ya watoto kutoka vituo vya watoto Yatima,kituo cha Sifa Bunju,Zaidia Sinza pamoja na Vetenari Temeke,wamekutana leo mchana kwenye Fukwe ya Azura Beach Kawe kwa ajili ya kupata chakula cha pamoja na watoto wengine,huku michezo mbalimbali kama vile face painting,jumping castle,kuogelea,kuvuta kamba,mpira wa miguu,kucheza mziki n.k.Michezo hiyo iliyoandaliwa na Kids Event na mingineyo ilitawala na kuwaburudisha sana watoto.
Aidha mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares,amesema kuwa mkusanyiko huo unafanyika kufuatia zoezi zima la kukamilisha ule mpango ulioanza wa kuchangia vituo vya watoto yatima.

Pamoja na hafla hiyo pia Keki iliyoandaliwa na flying chefs  ilikatwa huku wasanii mbalimbali wakishiriki kwa pamoja,akiwemo Shilole,Snura,Quenn Darlin,Mwasiti na wengineo.Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet na Wasanii wengine walijitolea kuwahudumia na kuwaangalia watoto.
Dina Marios anawashukuru watu wote walioshiriki kuchangia vituo hivyo.Wadau wa blog yake www.dinamarios.blogspot.com wasikilizaji wa leo tena ya clouds fm na wote walioguswa. Mpango huo utaendelea siku nyingine tena maana ni endelevu.
PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

YANGA YAIBAMIZA SC VILLA YA UGANDA MABAO 4-1 LEO

$
0
0
 Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, akijiandaa kupiga shuti golini baada ya kuwapiga chenga kipa na mlinzi wa SC Villa ya Uganda klatika mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.Yanga imeshinda bao 4-1  Picha na Richard Mwaikenda









ajali ya gari la tanesco usiku huu Kwa sadala, moshi

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi. 
 Gari la shirika la umeme Tanzania (Tanesco) imepinduka usiku huu baada ya kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Corola katika eneo la Kwa Sadala barabara ya Moshi/Arusha. 
 Kwa mujubu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari la Tanesco lilikuwa limepakia wafanyakazi wa shirika hilo wapatao 18 wakitokea eneo la KIA kuelekea mjini Moshi. 
 Amesema dereva wa gari dogo alikuwa akijaribu kuzipita gari kadhaa zilizokuwa zikielekea Arusha ndipo akakutana na Loli hilo kabla ya kurudi  upande wake.
Ndipo gari magari hayo yakagongana na kisha gari la Tanesco kupinduka. Shuhuda  amesema majerhi wa ajali hiyo walikimbizwa hosptali ya KCMC huku dereva wa gari hilo dogo akiingia mitini na kutokomea kusiko julikana.
Toyota Corola lililosababisha ajali hii
Askari wa usalama barabarani na gari la tanesco lililopinduka
wadau eneo la  tukio

mkataa kwao mtumwa

$
0
0
Kikundi cha utamreators kikitumbuiza hoteli ya Ledger Plaza-Bahari Beach hotel jijini Dar es salaam Jumapili Agosti 11, 2013

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya Ray C ya 'Umenikataa bila Sababu' ni mbichi bado

//michuzi2.rssing.com/chan-7007653/article4496-live.html

Sherehe ya Eid Mubarak New York yafana

$
0
0
Mpiganaji na mfanyabishara maarufu wa kimataifa "The CEO" Davis Mosha akiongea machache baada ya kukaribishwa kuongea kama kijana mwenye mafanikio na maendeleo kiuchumi, na kijamii wakati wa sherehe za Eid jijini New York. Alitoa ujumbe kwa vijana hasa changamoto za maendeleo zinazo patikana Tanzania. Zaidi Bwana David Mosha amewaasa vijana wa kitanzania kujipatia fedha kwa njia za halali na kusikitishwa sana na wimbi la vijana kujiingiza katika biashara za madawa ya kulevya na nyingine harafu zinazoharibu maisha ya watu na wenyewe kwa ujumla. Mpiganaji Davis Mosha amekuwa Marekani kwa likizo na kila alikokwenda alikutana na watanzania na kuzungumza nao.
David Mosha akisalimiana na waheshimiwa mabalozi..
Waheshimiwa wakikaribishana kwenye meza kuu kwenye sherehe ya Eid Mubarak iliyofanyika 30 Overhill Rd Mt Vernon NY. Sherehe hizo ziliandaliwa na Waislam wa New York na kukaribisha wana jumuia wote pamoja na familia zao bila kujari dini. Hiyo ndiyo dhana tunayojivunia watanzania ya kushirikia katika shughuri za kijamii bila kubaguana Tanzania Oyeeee Mungu ibariki Tanzania.
Katibu wa jumuia ya wataznania New York bwana Shaban Mseba akimuongaza Mgeni rasmi Mh. Balozi Manongi akiwaslri kwenye sherehe hiyo 
Mh. Balozi Manongi akiongea machache mbele ya watanzania waliojitokeza kwenye sherehe hiyo 
Sherehe hizo ziliudhuriwa na mabalozi wetu wote wawili wa hapa New York, Hapa ni Mh. Balozi Mwinyi akiongea kwenye sherehe hiyo.

Hapa ni Mh. Balozi Mero akiongea machache na pia alitumia nafasi hii kuwaaga wananewyork community, Mh. Mero ameteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Geneva na muda wowote ataodoka. 
Katibu wa new York Community bwana Shaban Mseba akiongea
Bwana Hajji Khamis mwenyekiti wa New York Community akitoa shukrani mbele ya watanzania waliojitokeza katika sherehe hizo za Eid Mubarak. Kwa picha bofya read more
Baada ya hivi karibuni kurudi toka safari uko Dubai na Saudia Shekh Maftaha alipata fursa ya kutoa mawahiza katika sherehe hizo za Eid.

Flaviana Matata aendelea kuitoa kimasomaso Tanzania Afrika na Kimataifa: ashika nafasi ya juu Afrika na Kimataifa kwa kipato

$
0
0
NYOTA ya mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata (pichani) amezidi kung’ara baada ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa upande kipato.
Kwa mujibu wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes kwa bara la Afrika (Forbes Africa) lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee aliyeingia katika orodha hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na kuzidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.
Katika orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiyo aliibuka namba moja na  wengine sita pamoja na Flaviana wakibaki kutoa ushindani mkubwa kwa mlimbwende huyo wa Angola.
Mbali ya Flaviana, wanamitindo wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni Candice Swaenpoel, Katryn Kruger wote wakitokea Afrika Kusini, Ajak Deng, Grace Bol ( Sudan) na Liya Kebede wa Ethiopia.
Flaviana Matata aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania mwaka 2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora na baada ya kumaliza muda wake aliendelea na fani ya  uanamitindo Afrika kusini na baadaye alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika makampuni makubwa ya uanamitindo ya Next Models International na sasa yuko Wilhelmina Models. A
kizungumza kutoka New York, Flaviana ameeleza kufurahia mafanikio haya hata hivyo ameongeza “Mpango wangu ni kuzidi kumweka Mungu mbele na kuhakikisha kuwa najitahidi kadri ya uwezo wangu na kuiletea sifa familia yangu na nchi yangu”.

Push Mobile kumwaga vitz 4, pikipiki 12 kwa Serengeti Fiesta 2013

$
0
0
Meneja Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rugambo Rodney akimkabidhi funguo mbili Diana Elis Mkoba baada ya kushinda shindano la Tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Diana alikabidhiwa magari mawili aina ya Vitz yenye thamani ya shs milioni 18.Katikati ni Baba mdogo wa mshindi, Gratian Mkoba ambaye ni Rais wa chama cha Walimu Tanzania (CWT). Mwaka huu, Kampuni hiyo itatoa magari manne, pikipiki 12 na fedha taslim shs 100,000 ikiwa juma ya zawadi zote ni sh million 80

KAMPUNI ya Push Mobile Media Limited itatoa zawadi za magari aina ya Vitz manne (4) na pikipiki 12 kwa mashabiki mbali mbali watakaoshinda bahati nasibu maalum ya tamasha la Serengeti Fiesta linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi mjini Kigoma.
Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa zawadi mbali ya magari na pikipiki, pia watatoa zawadi za fedha taslim (sh 100,000) kwa mashabiki hao ambao ili kushinda wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili kuweza kushinda gari, pikipiki au fedha taslim na unaweza kushinda tiketi ya VIP kwa kutuma jina la msanii kwa mfano Diamond na kuacha nafasi na baadaye kuwema maoni yako kwenda namba hiyo hiyo.
Rodney alisema kuwa mbali ya kushinda tiketi, mshiriki atalipiwa tiketi ya ndege kuja Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la fiesta la mwisho. Alisema kuwa wameamua kuweza zawadi hizo nono ili kunogesha zaidi tamasha hilo ambalo kwa kuwanufaisha mashabiki  wa muziki hapa nchini.
Aliongeza kuwa wamejipanga ili kuwashirikisha wananchi wote katika tamasha hilo kwani watatoa pia watazindua huduma mpya ijulikanayo kwa jina la Simu TV ambapo itamwezesha mashabiki kuona video mbali mbali za muziki na matukio mengine, kupata nyimbo mbali mbali, kupata taarifa mbali mbali ikiwa pamoja na za michezo kwa kupitia simu ya mkononi.
kuhusiana na zawadi za fedha, Rodney alisema kuwa zawadi hiyo itakuwa inatolewa kila siku kwa mashabiki watakaoshinda bahati nasibu hiyo. Alifafanua kuwa jumla ya sh milioni 80 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili litakalodumu kwa kipindi cha miezi mitatu.

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU OMARY SAIDI ULEMBO
 05-05-1966 – 12-08-2010

Ni miaka 3 sasa tangu ututoke ghafla, wakati ulipotuaga kuwa unaenda Nairobi Kenya kwa shughuli za kikazi ukiwa mzima wa afya lakini ukarejea ukiwa marehemu.

Unakumbukwa zaidi na mpenzi mke wako Sheilla, watoto wako Harith na Shamim, mama yako Bi. Husna, mama zako wadogo na wakubwa, dada zako, kaka zako, wadogo zako, ndugu jamaa na marafiki wote.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho yako mahali pema peponi,

AMEEN.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>