Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Tamasha la Afrika Marekani-FestAfrica 2013 lafana sana

0
0
IMG_3439
Tanzania iliwakilishwa vyema kwenye tamasha la kila mwaka liitwalo FestAfrica lililofanyika mwishoni mwa juma huko Silver Spring Md na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi.Pichani ni Mdau Nene ambaye ni Mtanzania aliyeongoza kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo akijivunia kazi yake. IMG_3269Maonyesho ya Mavazi ya Kiafrika yalitia fora kwenye Tamasha hilo. IMG_3282IMG_3300IMG_3326IMG_3337
Kwa picha zaidi ungana na Sundayshomari.com

WAZIRI MAGHEMBE AZINDUA BODI MPYA YA MAMLAKA YA MAJI MJINI MOSHI

0
0
Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe akizungumza na wajumbe wapya wa bodi ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)wakati wa hfla fui ya kuizindua bodi hiyo iliyofanyika katika ukumbu wa bodi wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA) Cyprian Luhemeja akisoma taarifa mbele ya waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya mamlaka hiyo.
Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi kwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA) Hajira Mbande ambaye pia ni meneja wa Azania Bank tawi la Moshi.
Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi kwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA) cyprian Luhemeja ambaye pia ni mkurugenzi wa MUWSA.

Jaji Mkuu wa Tanzania afungua Kongamano la Majaji Wanawake wa nchi za Afrika jijini Arusha leo

0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akilakiwa na baadhi ya Majaji na Wanasheria kutoka Tanzania na kwingineko Afrika, anayesalimiana naye ni Mhe. Jaji Sanji Mmasenono Monageng, ambaye ni Makamu wa Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kihalifu (ICC), na Kamishna wa International Commission of Jurists, anayefuata mwenye koti refu jekundu ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jaji Eusebia Munuo, Kongamano hilo limefunguliwa mapema Leo na Jaji Mkuu katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) akiwa katika meza Kuu na viongozi wengine wa Mahakama, kulia ni Mhe. Jaji Mstaafu, Eusebia Munuo, anayefuata ni Mhe. Jaji Sanji Monageng, Makamu wa Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kihalifu (ICC), wa pili kutoka kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wa kwanza kushoto, Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania
Baadhi ya Majaji wanawake wakiwa katika Kongamano hilo tayari kwa ufunguzi rasmi.
Jaji Mkuu wa Tanzania katika picha ya pamoja na Majaji Wanawake kutoka nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Naigeria, Zambia, Swaziland, Zimbabwe, Botswana, Msumbiji, Namibia, Sierraleone, Eritrea, Lesotho, Mauritius na Malawi. (Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII IMEKANUSHA UVUMI KUWAWATEULE WA WAZIRI WAMESAINI POSHO MBILI

MISA YA AROBAINI YA MAMA CECILIA SICHALWE

0
0
Marehemu Mama Cecilia Joyce Sichalwe

Ndugu wanafamiia na marafiki,

Tarehe 16/08/2013 (ijumaa) kuamkia 17/08/2013 lushoto, kutakua na mkesha wa 40 na kuafuatiwa na misa ya arobaini ya mama yetu mpendwa Cecilia Joyce Sichalwe.

Kwaniaba ya familia nawakaribisha wote mjumuike nasi nyumbani lushoto(Jaegestal Magharibi farm).

Bwana ametoa,bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe.

Familia ya Mzee Mambo & Sichalwe.

The Weruweru Girls met this Sunday at Cine Club,Mikocheni

0
0
The Weruweru Girls met this Sunday at Cine Club,Mikocheni..being part of the meetings for the Golden Jubilee Celebrations scheduled for September 21st.
 The different committees and members of the Weruweru Family from the era of Asumpta to present (1963-2012) were all invited for the meeting.
 Besides discussing the preparations for the celebrations, the Weruweru girls also had fun talking about their various memories of the Weruweru Days. Do you remember scrabbing the covered-ways? Do you remember burning VIGODORO? hahahah what memories!
 The Golden Jubilee meetings and preparations gave me a chance to meet and know many of Weruweru Alumni that I never knew went to the same school as me! Did you know Dr Asha Rose Migiro went to Weruweru Secondary? What about Ambassador Mwanaidi Maajar? Dr Mary Nagu? Dr. Hellen Kijo Bisimba? Dr. Mary Nagu?....Missie Popular?hahahahha
 Yes...we do run things in all spheres of lives! Now,I know there are so many others out there...Lawyers,Entrepreneurs, Farmers, Teachers, Artists, Engineers, Architects etc...Please register yourself on our DATABASE http://www.weruweru.mediart.co.tz and let's re-connect!
 The Next meeting is on 25,August,2013 at the same place,Cine Club.
Looking foward to seeing many more of my classmates...the Rafikiel, Beatrice Dengenesa, Rachael George, Catherine Matasha, ...RED SKIRTS at its best! What about the Green skirts? The Blue Skirts?All of you...Let's show up at 25,August at Cine Club and remember the good old days :)

Mambo Ya Kuzingatiwa Na Kamati Za Bunge Katika Kusimamia Fedha Na Rasilimali Za Umma - Zitto Kabwe

Big Brother The Chase 2013: FAREWELL, FEZA

0
0
Fabulous Feza followed her recently-departed beau Oneal out of Big Brother: The Chase during Sunday’s live eviction show. Her departure leaves 7 housemates in contention for the USD300 000 prize, with just 14 days of The Chase to go.

After joining IK on stage, she shared her thoughts on life, love and everything else with the continent. She told IK that she’d originally liked Elikem when they walked into the house, but things had changed. “I liked what I saw, but he’s just a bit immature,” said the Tanzanian. “Do you really love Oneal?” asked IK. “Yes,” replied a shy-looking Feza.

Feza told IK that she and Oneal had argued often because he sometimes thought she was using him and he didn’t trust her. “Did that change before he left?” asked IK. “I had my doubts – I tried so hard because I wanted him to trust me. Then I put myself in his shoes and I realized I would react the same way. I thought I owed it to him to earn that trust,” she said. IK asked the Tanzanian whether she thought Oneal had another lady waiting for him outside the house. Her response was that she wasn’t sure. “So you’re still not 100% on the trust thing?” asked IK, to which Feza replied: “No”.

When IK showed her who had nominated her, she was shocked to see Dillish pop up on screen. She said she would have been surprised to be nominated by Melvin, but he had spoken to her about it. Asked who she thought would win, she said she wasn’t sure if he would or not, but that Angelo was her favourite.


KUMBUKUMBU

0
0
MAREHEMU MAMA FATUMA NINDI

Siku kama ya leo tarehe 12 augusti mwaka 2010 mama ulitutoka.Siku hii ilikuwa ngumu sana kwetu kwani si rahisi kuelezeka.

Mama kwetu ulikuwa si mama tu bali mshauri na rafiki yetu mkubwa.Huku mshauri na rafiki bora kwetu tu bali hata kwa marafiki na majirani zako ambao wote wanakukumbuka kila siku.

Kila nafsi itaonja mauti bali kwetu sisi wanao tunaona kama umetutoka mapema sana na katika muda ambao tulikuwa tunakuhitaji zaidi. Mama tulikupenda sana ila Mwenyezi Mungu alikupenda zaidi yetu na ndiyo maana akakutwaa.

Tutaendelea kutenda yale mema yote uliyotufundisha kubwa likiwa ni UPENDO.

Unakumbukwa na sisi wanao Anna,Patrick na James bila kusahau wajukuu zako Browne Kelvin(Costa) na Evelyn.

MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI MAMA,AMEN.

TAMASHA la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha kufanyika Septemba 8, 2013

0
0
Rais Kikwete akiwa na wanahabari wa Arusha katika moja ya ziara zake mkoani hum. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulongo na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Nyirembe Munasa.

TAMASHA la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Septemba 8 katika viwanja vya General tyre Arusha na kushirikisha waandishi kutoka jijini Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro na mkoa wa Manyara. Tamasha hili, ambalo hufanyika kila mwaka, limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA) Mussa Juma, alisema  zaidi ya waandishi wa habari na wadau wa habari 500 wanatarajiwa kushiriki katika Tamasha hilo.
Juma alisema kwa upande wa michezo timu ambazo zitashiriki ni TASWA FC kutoka jijini Dar es Salaam, TASWA Arusha, Radio Sunrise, Radio 5, Radio Triple A, Arusha One Radio na Chuo cha Uandishi wa habari Arusha ambao ndio mabingwa watetezi.

Alisema pia kutakuwa na timu ambazo zimealikwa ambazo ni timu ya TBL Arusha ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, timu ya Wazee Klabu,Kitambi Noma, Timu ya Pepsi na timu ya NSSF Arusha.

Juma alisema katika tamasha hilo, ambalo huandaliwa na TASWA na kampuni ya Ms Unique, kutakuwa na michezo ya soka, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mpira wa mikono na mbio za magunia.

Alisema Septemba 7 bonanza hilo, litatanguliwa na semina ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoa wa Arusha kuhusiana na sheria za michezo, masuala ya afya na jinsi ya kutumia michezo katika kutangaza utalii.  Juma alisema bado wadhamini zaidi wanatakiwa na wanaombwa kujitokeza kudhamini tamasha hilo.

MWANAFUNZI ALAZIMISHWA NGONO BILA KONDOMU NA MAJANGA MENGINE WILAYANI MAKETE

0
0

Kata ya Iwawa ilipo shule hiyo.
 
Na Edwin Moshi wa
Globu ya Jamii, Makete
Wafunzi wa shule ya sekondari Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe wamekiri uwepo wa wanafunzi wenzao ambao wanajihusisha na vitendo vya ngono na wengine wanaishi na virusi vya UKIMWI, licha ya jamii kudhani kuwa wanafunzi hawawezi kuwa na virusi hivyo kwa minajili kwamba bado ni wadogo.
Hayo yamebainika baada ya mtandao huu kufanya mahojiano ya kina na baadhi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hivi karibuni kwa ruhusa ya mkuu wa shule hiyo Bw. Christopher Haule hapo kufuatia wananchi wengi wilayani hapo kudhani kuwa wanafunzi hao hawana maambukizi ya VVU  kwa kuwa ni wadogo na huwenda hawajaanza kujihusisha na vitendo vya ngono.
Mwanafunzi mmoja (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) amesema ana marafiki zake zaidi ya watano ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI na hajui walivipataje, hivyo anaamini wapo wanafunzi wengi ambao wana maambukizi. kusoma taarifa kamili BOFYA HAPA

BALOZI MULAMULA AHUDHURIA MAADHIMISH​O YA MIAKA 5 YA KANISA LA THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES

0
0

CHRISTINA SHUSHO, UPENDO KILAHIRO WAPENDEZESHA JUKWAA
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata  Mulamula ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries yaliyofanyika kwenye kanisa hilo College Park Maryland na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka DMV na majimbo ya jirani. Maadhimisho haya yalianzia Ijumaa na Jana Jumapili Aug 11, 2013 ndiyo ilikua hitimisho lililoambatama sala, nyimbo za injili kutoka vikundi mbalimbali wakiwemo waimbaji wa nyimbo za injili toka Tanzania Upendo Kilahiro na Christina Shusho waliokuja maalum kwenye maadhimisho hayo.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa utawalawa na fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula na Dr Nicku Kyangu Mordi.
Meza kuu katika picha ya pamoja kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The cross Gospel Ministries yaliyofikia mwisho siku ya Jumapili Aug 11, 2013 College Park Maryland.
Juu na chini ni Mhe. Balozi Mulamula akiongea na Watanzania waliohudhuria maadhimisho hayo ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries yaliyofikia mwisho siku ya Jumapili Aug 11, 2013 College Park, Maryland.
Wachungaji kutoka makanisa mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo ya miaka 5 katika picha ya pamoja.
Upendo Kilahiro, mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Tanzania akipamba jukwaa kwa nyimbo mbalimbali siku ya mwisho  maadhimisho hayo siku ya  Jumapili Aug 11, 2013, College Park, Maryland.
Mwimbaji wa nyimbo za injili toka Tanzania, Christina Shusho akiimba moja ya nyimbo zake siku ya mwisho ya maadhimisho ya miaka 5 ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries yaliyofanyika Jumapili Aug 11, 2013, College Park Maryland.

RAIS KIKWETE APOKEA HATI YA UTAMBULISHO TOKA KWA BALOZI WA UHOLANZI NCHINI LEO

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi Mteule wa Uholanzi hapa nchini Mhe Jaap Frederiks Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 12, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Balozi Mteule wa Uholanzi hapa nchini Mhe Jaap Frederiks baada ya kupokea hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 12, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kwa Balozi Mteule wa Uholanzi hapa nchini Mhe Jaap Frederiks Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 12, 2013. PICHA NA IKULU

KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA BALOZI WA CANADA LEO

0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Caanada hapa nchini, Alexandre Leveque, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013. Balozi huyo alipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimwelewesha jambo Balozi wa Caanada hapa nchini, Alexandre Leveque, alipomkarivisha Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013. Balozi huyo alipomtembelea na kuwa na mazungumzo naye. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza Balozi wa Caanada hapa nchini, Alexandre Leveque, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Caanada hapa nchini, Alexandre Leveque, baada ya mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 12, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).

WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA MONTAGE WASHEREHEKEA SIKUKUU YA EID NA WANAFUNZI YATIMA WA SHULE YA SEKONDARI YA WAMA - NAKAYAMA

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Tanzania Teddy Mapunda akiwagawia soda wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe za sikuku ya Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana. Wafanyakazi wa kampuni hiyo walisherehekea sikuu hiyo na wanafunzi hao ili kuonyesha upendo.
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daud Nasibu akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama inayomilikiwa na taasisi hiyo wakati wa sherehe za Eid Mubarak ziliyofanyika shuleni hapo jana.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Montage ya jijini Dar es Salaam wakiwahudumia chakula cha mchana wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliamua kusherehekea sikukuu ya Eid Mubarak na wanafunzi hao jana ili kuonyesha upendo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakila chakula cha mchana kilichoandaliwa na kampuni ya Montage Tanzania wakati wa sherehe za Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo jana.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya watoto wa kike ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA-Nakayama iliyopo kijiji cha Nyamisati wilaya ya Rufiji mkoani Pwani wakicheza mziki aina ya Kwaito jana wakati wa sherehe za Eid Mubarak zilizofanyika shuleni hapo. Picha na Anna Nkinda - Maelezo

RADIO 5 WAIBUKA WASHINDI WA KWANZA MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI.

0
0
 Wafanyakazi  wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 kushoto ni Semio Sonyo ,Sarah Keiya meneja masoko,katikati ni David Rwenyagira na Deo Gee wakifurahia  kikombe cha ushindi ambapo jana waliibuka washindi wa kwanza kwenye maonyesho ya 20 ya Nane nane kwa kanda ya kaskazini,yaliyofanyika katika viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha.
Meneja masoko wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio5 Sarah Keiya pamoja na Dadiv Rwenyagira wakiwa wameshikilia kikombe mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza maonyesho ya 20,ya nane nane kwa kanda ya kaskazini yaliyofanyika katika viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha.

CRDB YAKABIDHI WODI YA WAZAZI NA VIFAA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA META-MBEYA

0
0
 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyiwa ukarabati na benki hiyo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Huduma ya Akinamama na Watoto-Meta. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya, mwishoni mwa wiki. 
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyiwa ukarabati na benki hiyo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Huduma ya Akinamama na Watoto-Meta. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya, mwishoni mwa wiki. 
 Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akipanda mti wa kumbukumbu katika hospitali ya Rufaa ya Meta wakati wa hafla ya kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyiwa ukarabati mkubwa na benki ya CRDB. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigalla na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akimwagilia mti wa kumbukumbu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati benki hiyo ilipokabidhi wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Huduma ya Akinamama na Watoto-Meta.
Zoezi la upandaji miti likiendelea. 

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akikata utepe wakati wa kukabidhi wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa Meta, ambayo imefanyiwa ukarabati na benki ya CRDB. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mbeya. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei, kushoto ni Murugenzi wa tawi la Mbeya, Benson Mwakyusa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigalla.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkabidhi kasha la juisi, Salome Zakaria, ambaye ni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya Kitengo cha Huduma ya Akinamama na Watoto-Metawakati wa hafla ya benki hiyo kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyika mjini Mbeya, mwishoni mwa wiki.

 Pole mama, pokea zawadi.
 Tucheze kwaito.
 Mfanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Viwawa, Mbozi, Beatrice Kyando akimwagilia maji mti wa kumbukumbu alioupanda.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akipaka rangi wodi ya wazazi katika hospitali ya Rufaa ya Meta, wakati wa hafla ya kukabidhi wodi hiyo kwa uongozi wa hospitali hiyo baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa na benki ya CRDB. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mbeya.
 Mke wa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akiwafariji wagojwa waliolazwa katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Rufaa ya Meta.
 Pole sana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wadau na wateja wa benki hiyo iliyofanyika mjini Mbeya.
 Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla hiyo. 
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB pamoja na wadau wa benki hiyo wakicheza muziki.
 Tucheze mduara
 Wadau wakicheza Kwaito.

REDD'S MISS ILALA 2013 KUFANYIKA IJUMAA UKUMBI WA GOLDEN JUBILEE JIJINI DAR

0
0
 Warembo wanaotarajia kushiriki Redd's Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini.
 Warembo wanaotarajia kushiriki Redd's Miss Ilala, wakiwa wamepozi wakati wa mazoezi kwenye Mgahawa wa Billicanas, Dar es Salaam, tayari kwa mashindano yatakayofanyika Ijumaa kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini
 Warembo wakiwa katika moja ya miondoko wakati wamazoezi
 Mwalimu wa warembo hao, AKHSAS PETER akiwapanga vizuri kabla ya kupigwa picha na wandishi wa habari.
 Warembo wakipita Mtaa wa Makunganya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, wakitokea mazoezini katika Mgahawa wa Billicanas.
 Mwandishi Mwandamizi wa Habari za Michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula (kulia), akitoa maelezo kuhusu kazi za kila siku za waandishi wa habari kwa warembo wa wanaotarajia kushiriki mashindano ya Redd,s Miss Ilala walipotembelea chumba cha habari cha Jambo Leo
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), Juma Pinto (aliyekaa kulia), akizungumza na warembo hao waliomtembelea ofisini kwake, Dar es Salaam. Aliyekaa katikati ni Mratibu wa mashindano hayo, Juma Mabakila. JCPL ni wachapishaji wa magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania.

SALAMU MAALUM ZA SHUKURANI KUTOKA MBEYA YETU BLOG BAADA YA KUPATA USHINDI WA KUWA CHOMBO BORA KATIKA MATANGAZO YA DIGITALI WAKATI WA MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI MBEYA.

0
0

Hii ndiyo hati ya Ushindi tuliyopewa na TASO
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawilo aliye simama Mbele akipokea Maelezo ya Kina juu ya Mbeya yetu Blog inavyofanya kazi na mitandao mbalimbali ya Kijamii kutoka kwa Mtaalam wa Mambo ya Mitandao ya Digitali kutoka Tone Multimedia Group Fredy Anthony, alipo tembelea katika Banda la Mbeya Yetu Blog.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Dr. Christine Ishengoma aliyevaa kofia akipokea Ufafanuzi wa Jambo Kuhusu Blog ya Mbeya yetu kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa Mtandao wa Mbeya yetu Ambaye Pia ni mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Tone Multimedia Ndugu Joseph Mwaisango wa Pili kutoka Kushoto
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akitaka kupata ufafanuzi wa jinsi gani Mbeya yetu Blog tunavyopata habari na kuziweka kwa Muda kama alivyo kuta tukio lake likiwa Live mara alipotembelea Banda la Mbeya yetu na kujionea mwenyewe.
Kutoka Kushoto ni Venance Matinya na David Nyembe wote kikosi kazi cha Mbeya yetu Blog, wakiwa wanapita Mbele kuonesha Bango la Mbeya yetu kwa Mgeni Rasmi wakati wa sherehe za Kilele cha siku  ya Wakulima Nane nane Mbeya.
 Msimamizi Mkuu wa Mtandao wa Mbeya yetu Ambaye Pia ni mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Tone Multimedia  Ndugu Joseph Mwaisango akipokea Hati ya Ushindi kutoka kwa Mgeni Rasmi aliyevaa Skafu Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Capt (RTD) Aseri Msangi 
Baadhi ya kikosi kazi cha Mbeya Yetu Blog, Kutoka kushoto ni Venance Matinya, Joseph Mwaisango, Ezekiel Kamanga na Fredy Anthony
 ********************
Chama Cha Wakulima Tanzania (TASO) kanda ya Nyanda za juu Kusini, kimeutunuku cheti mtandao wa kijamii wa www.mbeyayetu.blogspot.com ambao upo chini ya Tone Multimedia Company Limited kutokana na kuibuka mshindi wa kwanza wa kurusha matangazo kwa njia ya Kidigitali katika maonesho ya Wakulima nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakagale Uyole Jijini Mbeya.
 Tuzo hiyo imekuja kutokana na kikosi cha Mtandao huu kuweka kambi katika maonesho hayo na kufanya shughuli za kurusha matangazo moja kwa moja kutoka uwanjani hapo na kuwapagawisha wakulima ambao walipata fursa ya kutembelea banda letu na kujionea habari zilizotokea muda huo huo na kuonekjana hewani.
 Mbali na wakulima na watu mbali mbali waliokuwepo uwanjani hapo pia viongozi wa Taso na wakuu wa Mikoa pia walipata fursa ya kutembelea banda la Mtandao huu katika ziara zao za kukagua mabanda na hivyo kutoa sifa kwa wamiliki wa Mtandao huu namna habari zilivyokuwa zikienda kwa wakati.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawilo ndiye aliyekuwa wa Kwanza kufanya ziara hiyo na kukuta habari zake tokea akipokelea mlangoni hadi kufikia mabanda habari zilikuwa hewani, mwingine alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma ambaye pia alionekana kuufagilia mtandao huu kwa namna walivyoweza kutangaza Nanenane  iliyofanyika kikanda na kuonekana kama ni Kitaifa.
 Aidha kufuatia mchango huo wa Taso na wakulima kwa ujumla Uongozi wa Tone Multimedia Group Kupitia  Mbeya Yetu Blog unatoa shukrani kwa wote waliuofanikisha shughuli za Nanenane hadi zinafikia kilele Agosti 8,  na kupelekea kupata cheti cha ushindi.
 Tunapenda kuwashukuru TASO kwa namna ya pekee, SBC (T) Ltdkupitia kinywaji chao cha Pepsi, Shirika la Bima ya Afya (NHIF) kwa kutupatia gazebo lililotusitili tukiwa kazini na wengine wengi ambao hatutaweza kuwataja majina lakini tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja.
Pia tunapenda kuwashukuru Bloggers wote na waandishi wa habari kwa ujumla hatutaweza kutaja kila chombo lakini tumekuwa pamoja mpaka kufanikisha yote haya.
Mwisho kabisa Tunapenda kukushukuru wewe Mdau wetu Mkubwa wa Mbeya yetu Blog kwa kuonesha Moyo na Kutembelea kila wakati mtandao huu, Tunasema asanteni sana, Bila nyie sisi hatuwezi fanya kazi.
 KWA PAMOJA TUUPENDE MKOA WETU WA MBEYA, KUPITIA MTANDAO WA MBEYA YETU BLOG.

KAMPUNI YA LAJANN E- System Enteprises ya Jijini Dar Es Salaam yasaidia yatima Uyole, Mbeya

0
0
Meneja wa Kampuni  inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao, Nzowa Wawila akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Aman Nsagala Uyole. Kwa picha zaidi na habari BOFYA HAPA
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images