Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

Jose Chameleon kupagawisha Dar Escape One Eid Pili

$
0
0
Mwanamuziki kutoka nchini Uganda
, Dr. Jose Chameleon anatarajiwa kufanya onyesho kali kesho kwenye ukumbi mpya wa burudani wa Escape Complex.

Chameleon, ambaye ndie mwanamuziki mashuhuri kuliko wote kwenye ukanda huu wa Afrrika Mashariki anatarajiwa kukonga nyoyo za wakazi wa Dar es Salaam kwa kuimba nyimbo zake zote kali, ikiwemo Valuvalu.

Usiku huo wa Chameleon utaenda sambamba na burudani kali kutoka kwa MA DJ wakali, DJ Pac na DJ Senorita ambao watafanya show ya utangulizi.

Akizungumzia burudani hizo, Meneja Uendelezi wa Biashara wa Escape Complex, Anthony David, alisema watu watarajie burudani kali siku ya jumamosi hasa kwa kuwa sherehe hizo zitaenda sambamba na sherehe za Eid za pale Escape Complex.

‘Kama lilivyo jina lake, Escape ni mahali ambapo mtu anakuja kupumzika kukwepa mihangaiko ya kila siku, iwe kikazi au kimaisha, lakini Eid hii tumeandaa burudani hii ili kuwapa wakazi wa Dar es Salaam kitu tofauti’ anasema Anthony.

Mbali na Chameleon siku ya jumamosi, Escape Complex imeandaa burudani siku ya Eid Mosi, ambapo DJ maarufu Boni Luv atatoa burudani kali, na siku ya Jumpili, bendi inayokuja kwa kasi Skylight, itawaburudisha wapenzi wake kuanzia asubuhi ili kuimaliza wikiendi ndefu.

Escape Complex, ambayo ipo Mikocheni/Kawe karibu nyuma ya ukumbi wa Safari Carnival, ni Club mpya ambayo inapendezeshwa na ufukwe pamoja na mandhari ya kuvutia, pamoja na chakula kizuri kwa wateja wake.

Mashabiki wa Chameleon watalipia shilingi elfu kumi na tano ili kuburudishwa na mwanamuziki huyo mashuhuri. Na VIP watalipa elfu 40,000/= ikiwemo kinywaji cha bure pamoja na nafasi ya kumuona msanii huyo baada ya maonyesho.

Balozi wa Vijana Raymond Maro katika mahojiano VOA

$
0
0
??????????????????????????????? 
Raymond Maro akiwa katika picha ya furaha pamoja Laurine Ogoma Prisca na mtangazaji Roger Rajar baada ya mahojiano na idhaa ya Kifaransa ya VOA. ??????????????????????????????? 
Mtangazaji maarufu wa VOA Straight Talk Africa Shaka Ssali akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Vijana katika Jumuiya ya Afrika mashariki kwa upande wa Tanzania ndugu Raymond Maro pamoja na mtangazaji mwenza Mariama Diallo na Martin Buhendwa kiongozi wa kundi la Friends of Congo kwa upande wa Vijana ndani ya studio za VOA siku ya Kipindi cha Straight Talk Africa kilichojadili nafasi ya vijana katika jamii na siasa. Best moment at VOA 101 
Raymond Maro akishiriki kipindi cha televisheni cha VOA - French akiwa na Laurene Saucer na mtangazaji wa kipindi Roger Rajah Muntu ndani ya jumba la VOA

Article 5

Kwa mara nyingine tena Sober Night inawakaribisha kuhudhuria Inspirational Night.

BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO AMKALISHA MZAMBIA KWA K,O RAUNDI YA 8

$
0
0
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kulia  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane picha zote na SUPER D
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kushoto  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane 

Bondia Fidelis Lupupa wa Zambia akiwa chini amekaa akijifikilia kuwa aendelee au asienderee baada ya kupigwa na bondia Mtanzania Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,o ya raundi ya nane 

Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kulia  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane 
Bondia Fidelis Lupupa wa Zambia akiwa chini amekaa akijifikilia kuwa aendelee au asienderee baada ya kupigwa na bondia Mtanzania Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,o ya raundi ya nane 

MIYEYUSHO AKISHANGILIA USHINDI



WITO WATOLEWA KWA WAZAZI KUWAPELEKA WATOTO KUJIFUNZA GOFU

$
0
0
Mwalimu wa Gofu kwa watoto wadogo klabu ya Gymkhana, Dar es Salaam Bw. Claude Nkawamba akimfundisha Vanessa Nkurlu (7) mchezo huo,Mwalimu huyo alitoa wito kwa wazazi wakitanzania kuwapeleka watoto wao kujifunza mchezo huo jana.
Mtoto mwanafunzi wa Gofu Vanessa Nkurlu (7) akiangalia mpira aliyeupiga ukielekea katika shimo la pili katika uwanja wa klabu ya Gymkhana, Dar es Salaam,jana.
Amani Nkurlu akijiandaa kupiga mpira wa gofu katika uwanja wa klabu ya Gymkhana jijini Dar es Salaam,Wakishuhudia ni Mwalimu wa Gofu Bw. Claude Nkawamba na mwanafunzi wa gofu Vanessa Nkurlu.

Twanga Pepeta kumtambulisha Ige Moyaba, Miss Ilala leo

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

Bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta' leo itawatambulisha wanamuziki wake wapya akiwemo muimbaji wao wa zamani Ige Moyaba na warembo watakaoshiriki Miss Ilala 2013.

Utambulisho huo ambao ni sehemu ya shamrashamra za sikukuu ya Idd el Fitri utafanyika leo katika ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni.

Mratibu wa onyesho hilo, Joseph Kapinga alisema maandalizi yote ya onyesho hilo yamekamilika. “Ige Moyaba aliyekuwa Ufaransa amewasili nchini tangu juzi usiku na alishajiunga na wanamuziki wenzake,” Kapinga alisema. 

Kapinga alisema warembo watakaoshiriki shindano la kumtafuta Miss Ilala pia watatambulishwa kwenye onyesho hilo linaloandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, Freddito Entertainment, Saluti5 na Twitter Pub.

Pia bendi hiyo itaambulisha wanenguaji wake wapya wa kike kwenye onyesho hilo maalum ya kusherekea Idd Pili. "Tumeamua kuleta wanenguaji wapya kabisa, wenye damu changa ili kuleta mapinduzi kwenye muziki wa dansi. 

Madansa wetu ni mabinti warembo, pia tuna wanenguaji watanashati,” alisema Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka na kuongeza kuwa; "Tumebadilisha na kuongeza safu mpya ya unenguaji ili kwenda na wakati pamoja na soko la muziki linavyotaka."

Kwa upande wa Ige Moyaba aliyetamba kwenye albamu ya ‘Mtu Pesa’ ya mwaka wa 2004, Asha alisema ameandaa vitu vipya kuwapa mashabiki wa bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigino.

“Kwa kweli hi siyo onyesho la kukosa kwani itakuwa ni zawadi yetu ya Idd kwa mashabiki wetu,” mkurugenzi huyo alisema. Mwezi uliyopita Twanga Pepeta walizindua albamu yao ya 10 iitwayo “Nyumbani ni Nyumbani”, ambapo nyimbo zake zitapigwa katika onyesho hilo la leo.

Nyimbo nyingine zitakazopigwa katika onyesho hilo ni zila za albamu za nyuma kama 'Jirani', 'Fainali Uzeeni', 'Chuki Binafsi', 'Ukubwa Jiwe', 'Mtu Pesa', 'Safari', 'Password', 'Mtaa wa Kwanza', 'Mwana Dar es Salaam' na 'Dunia Daraja'.

MAZISHI YA ALIYEKUWA KAIMU KAMANDA WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOA WA KATAVI , KATIKA KATA YA MZUMBE, WILAYA AYA MVOMERO

$
0
0
Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Katavi, Mrakibu msaidizi, Mohamed   Madulika,  mara baada ya kifikishwa nyumbani kwake , Kijiji cha Mikongeni, Kata ya Mzumbe, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro kwa ajili ya utaratibu wa mazishi , Madulika alifariki dunia kwa ajali ya gari Augoti 5, mwaka huu ,Wilayani Sumbawanga wakati akielekea mkoani Katavi akitokea Jijini Dar es Salaam na mazishi yake yamefanyika Augost 8, mwaka huu kijijini hapo.
Baadhi ya Maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Majeshi mengine , wakitoa saluti ya  heshima ya mwisho mara baada ya kukamilika kwa  mazishi ya Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa mkoa wa Katavi, Mrakibu msaidizi, Mohamed   Madulika, katika  makaburi ya  Kijiji cha Mikongeni, Kata ya Mzumbe, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro , Madulika alifariki dunia kwa ajali ya gari Augoti 5, mwaka huu ,Wilayani Sumbawanga wakati akielekea mkoani Katavi akitokea Jijini Dar es Salaam na kuzikwa Augost 8, mwaka huu   Kijiji hapo.


Wajapani wavutiwa na fursa za uwekezaji nchini

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara/Wawekezaji kutoka Japan waliofika Ofisini kwake jijini Dar es Salaam Agosti 9, mwaka huu kumtembelea na kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji hapa nchini hususan katika sekta ya nishati. Wafanyabiashara hao waliambatana na Waziri wao wa Uchumi, Biashara na Viwanda, Mhe.Toshimitsu Motegi.
Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japani, Mhe. Toshimitsu Motegi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (anayeshuhudia), alipomtembelea hivi karibuni akiongozana na wafanyabiashara kutoka nchini kwake, na kujadili fursa za uwekezaji hapa nchini hususan katika sekta ya nishati.
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (kulia), akiagana na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japani, Mhe. Toshimitsu Motegi, ambaye alimtembelea Waziri Muhongo akiongoza Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini kwake walioonesha nia ya kuwekeza hapa nchini, hususan katika sekta ya nishati.
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akiwa na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japani Mhe. Toshimitsu Motegi (kushoto) na Balozi wa Japani nchini, Mhe. Masaki Okada, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakiwa na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini kwao na kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji hapa nchini, hususan katika sekta ya nishati.

Na Veronica Simba

Serikali ya Japani imekiri kuvutiwa na kuhamasishwa na fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini hususan katika sekta ya nishati na imeonesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo.

Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan Mhe.Toshimitsu Motegi aliyasema hayo hivi karibuni alipofanya mazungumzo na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo ofisini kwake jijini Dar es Salaaam.

Waziri Motegi, ambaye aliongoza Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Japani, alitaja maeneo kadhaa ambayo nchi yake ingependa kufanya uwekezaji ikiwa ni pamoja na uzalishaji na usambazaji wa umeme.

Aidha, wafanyabiashara walioambatana na Waziri Motegi, walimweleza Waziri Muhongo kuwa fursa za uwekezaji zilizopo nchini na zinazoendelea kubainika siku hadi siku hususan upatikanaji wa gesi asilia zimekuwa ni kivutio na kichocheo kikubwa kwao kutamani kuwekeza Tanzania.

Mbali na kuonesha nia ya kuwekeza hapa nchini, Wajapani wameonyesha utayari wa kuwasaidia Watanzania katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali zilizopo kwa kutoa mafunzo.

“Serikali yangu iko tayari kupokea wanafunzi kutoka Tanzania kwa ajili ya mafunzo katika fani ya masuala ya jotoardhi,” alisema Waziri Motegi. Hata hivyo alibainisha kuwa kwa sasa serikali yake inafanya maandalizi ya kuanza kupokea watanzania kwa mafunzo husika na kwamba endapo mambo yataenda sawa, huenda mafunzo yakaanza rasmi mapema mwakani.

Kwa upande wake, Waziri Muhongo aliishukuru Serikali ya Japani kwa utayari wa kuwapatia mafunzo Watanzania na kusisitiza kuwa hilo ni jambo la msingi kwa nchi kuweza kusimamia rasilimali zake kikamilifu.

“Serikali imedhamiria kuongeza wataalamu wazawa watakaoweza kusimamia rasilimali zetu vizuri pasipo kutegemea wataalamu kutoka nchi za nje,” alisema.

Aidha, Prof. Muhongo aliwahakikishia Wajapani kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji na hivyo kuwakaribisha Wafanyabiashara hao kuja kuwekeza hususan katika miradi mbalimbali ya uzalishaji na usambazaji umeme kupitia vipaumbele vilivyoanishwa na serikali vya jototardhi, tungamotaka, gesi asilia, upepo na umemejua.

POLISI KUSHIRIKI MICHEZO NCHINI NAMIBIA

$
0
0
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

Timu ya Jeshi la Polisi itakayoshiriki michezo ya Shirikisho la Wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO Games) inatarajiwa kuondoka Jumanne Agosti 13 mwaka huu kuelekea katika jiji la Windhock nchini Namibia kwa ajili ya michezo hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Afisa Michezo wa Jeshi la Polisi Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Jonas Mahanga alisema timu hiyo itaondoka na wanamichezo 67 ambao wanaunda timu za Mpira wa miguu wanaume, Mpira wa pete Wanawake, Riadha wanaumwe na wanawake na mchezo wa Vishale (Dats).

Mahanga alisema timu hiyo inaendelea na mazoezi katika kambi yao ya maandalizi iliyopo katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) ambapo mpaka hivi sasa wameshacheza michezo kadhaa ya kujipima nguvu na kufanikiwa kufanya vizuri.

Alisema michezo hiyo itashirikisha Nchi kumi na nne (14) katika michezo mbalimbali na lengo la michezo hiyo ni kujenga ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama wa SARPCCO katika kukabiliana na uhalifu.

“Michezo hii pamoja na kuweka vyema kiafya miili ya Askari wetu, lakini pia itakuwa ni fursa kwa Askari wetu kufahamiana na wenzao na kubadilishana uzoefu katika kukabiliana na uhalifu hasa unaovuka mipaka”Alisema Mahanga.

Mara ya mwisho Tanzania kushiriki katika michezo hiyo ilikuwa mwaka 2009 nchini Malawi ambapo timu hiyo ilinyakua ushindi wa pili kiujumla .

Wasanii Wapagawisha Dar Live

$
0
0
  Msanii wa muziki wa kizazi kipwa, Ali Kiba, akiwapagawisha maelfu ya mashambiki wa muziki katika ukumbi wa Dar Live, Dar es Salaam, kwenye tamasha iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kusherekea sikukuu ya Idd siku ya Ijumaa. Wasanii wengine waliokuwa kwenye tamasha hilo ni TMK wanaume halisi na H-Baba.
 T.M.K Wanaume Family  wakikamua wakipagawisha maelfu ya mashambiki wa muziki katika ukumbi wa Dar Live, Dar es Salaam, kwenye tamasha iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kusherekea sikukuu ya Idd siku ya Ijumaa. Wasanii wengine waliokuwa kwenye tamasha hilo ni Ali Kiba na H-Baba.
Msanii wa muziki wa kisasa, H-Baba akipagawisha maelfu ya mashambiki wa muziki katika ukumbi wa Dar Live, Dar es Salaam, kwenye tamasha iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kusherekea sikukuu ya Idd siku ya Ijumaa. Wasanii wengine waliokuwa kwenye tamasha hilo ni Ali Kiba na TMK wanaume halisi.

JK akutana na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi leo

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi (wa tatu kushoto, mbele)  na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Uchukuzi  Dkt.  Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia),  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Dr Mary Nagu (wa pili kulia), Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda (wa pili kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe Salome  Sijaona  (wa kwanza kushoto) alipokutana na kufanya mazungumzo naye  Ikulu, Dar Es Salaam, leo Agosti 10, 2013
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe Salome Sijaona. Wengine  Waziri wa Uchukuzi  Dkt.  Harrison Mwakyembe , Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Dr Mary Nagu, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda  alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi Ikulu, Dar Es Salaam, leo Agosti 10, 2013
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

NANE NANE kanda ya kusini yafungwa mjini Lindi

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Mkoa  wa Lindi ambae pia ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM wa Mikoa,Ally Mohamedi Mtopa
 Kikundi cha ngoma cha Kiwalala kikitumbuiza katika maonyesho hayo
 Jengo la Maonesho ya Nane Nane
 Kutoka kushoto....Waziri wa Tamisemi, Mhe HawGhasia Mwenyekiti wa Taso kanda ya kusini,Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Mathias Chikawe (Mgeni Rasmi) Mkuu wa mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi
 Wakuu wa wilaya za mkoa wa Lindi na Mtwara
Washindi wa jumla maonesho ya nane nane wakisherehekea
-------------------
Na Abdulaziz Video
SERIKALI imetakiwa kutekeleza agizo lililotolewa na Chama cha mapinduzi (CCM) la kuwalipa fedha zilizobaki wakulima wa korosho kanda ya kusini,inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara,ili kuondoa malalamiko yasiyo ya msingi zidi ya Serikali yao. 
Akitoa salamu za CCM,Mwenyekiti wa Mkoa ambae pia ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM wa Mikoa,Ally Mohamedi wakati wa ufungaji wa maonesho ya 4 ya wakulima nanenane,kanda ya kusini yaliyofanyika viwanja vya ngongo katika Manispaa ya Lindi,alisema anashangazwa kuona Serikali ikishikwa na kigugumizi katika kutekeleza agizo iliyopewa Na Chama chake kuingilia kati mgogoro wa wakulima wa korosho,ikiwemo kuwalipa fedha zao zilizosalia baada ya zao hilo kukosa soko. 
“Chama kilishatoa agizo kwa kuitaka Serikali kuingilia kati ikiwa ni pamoja na kuwalipa wakulima wa korosho fedha zao zilizobakia Baada ya pilikapilika na kupiga kelele juu ya masuala ya korosho,Chama kilinituma nikaonane na waziri mkuu,kumuulizia lile agizo April 23 mwaka huu,la kuwalipa wakulima wa korosho Sh,600/-limefikia wapi?,,,,,,lakini kwa bahati mbaya sikupata nafasi ya kuonana nae kutokana na kuwa katika ziara za kiserikali sasa serikali ipo hapa nyie mawaziri ndio serikali mnamuogopa nani?”Alisema Mtopa. 
 Akasema kitendo cha Serikali kuendelea kulifumbia macho agizo lililotolewa na Chama chake,juu ya malalamiko ya wananchi, kinawanyong’onyesha na kuwakatisha tama wakulima wakiwemo wa korosho. Pia,mwenyekiti huyo wa Chama mkoani Lindi,alisema inakuwaje Bodi ya korosho au vyama vya msingi vya ushirika wa ununuzi wa mazao vinakuwa na nguvu kuishinda Serikali katika kutatua kero za wananchi wake. 
 Mtopa amesisitiza kwa kutoa angalizo,iwapo Serikali hawatalipa fedha kwa wakulima hao wa korosho,kuna hatari ya wananchi kutoendelea kukiamini tena Chama hicho katika chaguzi zijazo ikiwemo katika utekelezaji wa Stakabadhi ghalani. 
 Naye,waziri wa katiba na Sheria,Mathias Chikawe,ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo ya nanenane,amehaidi kukutana na mawaziri wenzake kwa lengo kuyazungumza,kabla ya kukutana na waziri mkuu. 
"Naahidi kulifanyia kazi pamoja na mawaziri wenzangu hata hivyo tutapiga debe pia ili Nane nane mwakani Kitaifa iwe Viwanja vya Ngongo kwa mara ya kwanza kanda ya kusini Mwanzoni mwa mwaka huu,wakulima wa korosho wilaya tatu kati ya tano za mkoa wa Lindi, ambazo ni Liwale, Ruangwa na Kilwa,walifanya vurugu ikiwemo kuharibu mali za viongozi wakiwemo wanasiasa na vyama vya msingi vya ushirika.

wanyarwanda walia na tanzania wakidai amri ya kuwataka wanaoishi sheria inawalenga wao

$
0
0
photo


Yesterday’s arrivals pushed the number of such returnees to 1,000 after Tanzanian authorities gave those they described as ‘illigal immigrants’ two weeks to leave the country.

The deadline passed yesterday and it remains unclear what the fate of those who were unable to beat it would be.

The evictees told Saturday Times that Tanzanian security personnel, including the army and police, as well as neighbours were combing the communities ordering everyone they perceive to be of Rwandan origin out of the country.

Some of the victims had lived in the east African country for more than 50 years.

Tanzanian authorities claim they are targeting those without ‘valid residential documents’ but some of those affected claim they had all the necessary documents – some alleged security agents had confiscated and destroyed them.

news alert: sheikh ponda ajeruhiwa morogoro

$
0
0
Taarifa ambazo bado kuthibitishwa kutoka Morogoro zinadai  kwamba Sheikh Issa Ponda (pichani) amejeruhiwa na kile kinachosadikwia kuwa ni risasi akitoka  kuhudhuria kongamano la kidini lililofanyika mjini humo na kuhudhuriwa na watu wa kada mbalimbali.

Inaelezwa kuwa Sheikh Ponda, ambaye naye alikuwa mmoja wa watoa mada, aliondoka baada ya kongamano kumalizika akiwa katika gari ndogo kabla ya kupatwa na mkasa huo.
Inaelezwa kuwa baada ya kujeruhiwa Sheikh Ponda alikimbizwa hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu, ambako inasemekana hakukaa sana kwani alitoweka na jina lake halikuwahi kuandikikao wa kwenye daftari la wagonjwa wafikao hospitali.
Hadi sasa habari za uhakika kuwa amejeruhiwa kiasi gani na nani aliyemjeruhi  hazijapatikana. Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa  Morogoro,  Faustine Shilogile, amekanusha  madai  hayo  ya  kupigwa  risasi  kwa Sheikh Ponda  na  kueleza  kuwa  hali  ni  shwari  mkoani  Morogoro    kwa  sasa  baada  ya  machafuko  ya  muda  mfupi  mida  ya  jioni ya leo.
Kamanda Shilogile  amesema  kuwa  yeye  hajui hali yake maana polisi walizuia gari lake  ili wamkamate  kwa  tuhuma  za  uchochezi  zinazomkabili, lakini wananchi wakaanza kuwashambulia polisi   na  wakafanikiwa  kumtorosha kupitia mlango wa uwani wa hospitali ya mkoa.
Amesema baada  ya  shambulio hilo, Polisi  walilazimika  kurusha risasi hewani kuwatawanya wananchi. Kamnada Shilogile anatoa  wito  kwa  mtu  yeyote  anayejua  alipo  Ponda awaarifu  polisi  mapema


yale yaleeee....Rundo la taka lamwagwa katikati ya barabara usiku huu vingunguti, dar es salaam

$
0
0
 Rundo la takataka linalosemekana kumwagwa na gari la taka barabara ya Nyerere katika mataa ya kona ya Vingunguti jioni ya leo. Ripota wa zamu aliye katika doria ya sikukuu ya Iddi ambaye amefika hapo kiasi cha nusu saa iliyopita anasema gari hilo lilipata ajali sehemu hiyo na askari trafiki aliyefika kuhudumu aliamuru liende kituoni bila hizo takataka na ndipo likafanya hayo uyaonayo. Tunafuatilia swala hili la aibu na tutawajulisha matokeo yake
 Magari yakipita kwa shida eneo hilo
Bado haiingii akilini kwa mtu mwenye akili timamu kufanya haya
Nani wa kulaumiwa katika hili?

majumba makuukuu mtaa wa samora jijini dar yapigwa nyundo kupisha ujenzi wa mapya

$
0
0
 Ubomoaji wa moja ya majumba kadhaa makukuu katika mtaa wa Samora jijini Dar es salaam umeanza leo jioni na kuendelea hadi usiku kupisha ujenzi wa majumba mapya ambayo hapana shaka yatabadilisha taswira ya mtaa huo ulioanzaa kwa jina la Acacia na baadaye Independence na sasa Samora. Ripota wa zamu katika doria ya sikuu anasema zoezi hilo linaendelea kwa amani na usalama chini ya ulinzi mkali wa polisi
 Bomoa bomoa ya majumba ya Samora ikiendelea
 Jumba mojawapo likipigwa nyundo
 Ni usiku wa saa nne na zoezi linaendelea
 Mlinzi akiwa kasimama kidete kuhakikisha zoezi linaendeshwa bila rabsha
 Taswira ya eneo la tukio, jirani na iliyokuwa mgahawa wa Salamander ambao nao umeshazungushiwa uzio baada ya kupigwa nyumndo kitambo
Taswira ya mtaa wa Bridge street

wasichana raia wa uingereza waliomwagiwa tindikali wawasili kwao, dunia nzima yalaani kitendo hicho, zawadi yatolewa kwa atakayefanikisha kuwanasa wahusika

$
0
0

Mama mwenye hasira wa mmoja wa wasichana wa Uingereza waliomwagiwa acid mjini Zanzibar ameungana na bintiye nchini humo baada ya jana  kuwasili kwa ndege kwenye hospitali kwa ajili ya matibabu.
£££-The-two-acid-attack-victims-2145123 Katie Gee, aliyefunikwa blanket, na rafiki yake Kirstie Trup wakiwasili kwenye hospitali ya Chelsea and Westminster nchini Uingereza kutibiwa majeraha yao. 

Mama huyo, Nicky Gee alionekana kushindwa kujizuia kulia baada ya kumuona binti yake Katie na rafiki yake Kirstie Trup wakishuka kwenye ambulance akiwa amefunikwa blanket.

£££-The-two-acid-attack-victims-2145124
Wasichana hao ambao wote wana miaka 18 walipelekwa kwenye hospitali ya Chelsea and Westminster kutibiwa haraka majeraha ambayo baba yake Katie ameyaita mabaya yasiyoelezeka.
article-2387651-1B381DE8000005DC-830_634x783
article-2387651-1B381EDA000005DC-119_634x520
Wote wameungua vibaya baada ya kumwagiwa tindikali usoni wakati walipokuwa wakiingia kwenye mgahawa mjini Zanzibar. 

Hilo lilikuwa shambulizi la tatu wakati walipokuwa visiwani humo. Awali mmoja wa wasichana hao alishambuliwa na msichana wa kiislam baada ya kumsika akiimba wimbo wakati wa mwezi wa Ramadhan.
article-2387651-1B383184000005DC-824_634x642


Katie na Kirstie
Polisi wamedai kuwa washukiwa saba akiwemo muongozaji wa watalii wamekamatwa jana asubuhi.Na sasa zawadi ya paundi £4,000 imetangazwa kutolewa na polisi Zanzibar kwa atakayesaidia kupatikana kwa kwa wahalifu hao.
  
Marafiki wanadai kuwa walikuwa wamelengwa kushambuliwa kwasababu walikuwa ni wayahudi na polisi wanadai kuwa walikuwa wanataka kuongea na mhubiri wa kiislam ambaye huenda ndiye alipanga shambulizi hilo.

Polisi wamedai kutoa warrant ya kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda Issa, ambaye inasemekana mafundisho yake yamechochea mashambulizi hayo ya tindikali.

Wasichana hao watapata matibabu ya kina kutokana na mejeraha waliyoyapata kwa kumwagiwa tindikali hiyo iliyomwagika usoni, kifuani, miguuni na mgongoni.
article-2386666-1B3345C0000005DC-753_634x348 Katie
Mikono yao pia imejeruhiwa kwakuwa walikuwa wakijaribu kufuta tindikali hiyo. Baba yake na Miss Trup, Marc, 51, milionea na daktari wa meno alisema mpita njia alienda kuwasaidia wasichana hao baada ya kushambuliwa na alimpigia simu.

Marafiki hao walikuwa wameenda Zanzibar kama walimu wa kujitolea kwenye kituo cha watoto yatima. Tukio hilo linaweza kuathiri vibaya sekta ya utalii visiwani Zanzibar. 

SIMBA YAIBAMIZA VILLA YA UGANDA MABAO 4-1 KATIKA TAMASHA LA SIMBA LEO

$
0
0
 Kikosi cha Simba kilichoibwaga Sports Club Villa ya Uganda mabao 4-1 wamakti wamechi ya kirafiki ya Tamasha la Simba kwenye Uwanja wa Tiafa Dar es Salaam jioni hii.
 Kikosi cha Sports Club Villa ya Uganda iliyopigwa na Simba mabao 4-1
 Mchezaji wa Simba Ramadhan Chombo 'Lidondo' (kushoto) akitafuta mbinu za kuwapita wachezaji wa  Sports Club Villa ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.


 Mchezaji wa Simba, Nassoro Masoud (kushoto) akipigwa chenga na Kalyowa Emma wa Sports Club Villa ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Wapenzi wa Simba wakishangilia bao la pili dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta jijini Dar es salaam leo

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images