Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

chamaki nchanga wa ntwala


wasichana raia wa Uingereza waliomwagiwa tindikali zanzibar, mwakilishi Ismail Jussa atoa ujumbe

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taswira ya Zanzibar kama kisiwa cha amani imechafuliwa tena jana usiku pale watu wasiojulikana walipofanya kitendo cha kinyama na kishenzi cha kuwamwagia tindikali (acid) wananchi wawili wa Uingereza katika maeneo ya Shangani, jimbo la Mji Mkongwe.

Taarifa za awali nilizozipata ni kwamba vijana hao wawili wapo Zanzibar wakiwa ni sehemu ya vijana wanaojitolea (volunteers) katika shughuli za sanaa (Arts).

Nikiwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, mwananchi wa Zanzibar ninayeipenda nchi yangu na pia nikiwa kama binadamu ninayethamini utu wa kila mtu nalaani vikali na kwa nguvu zote uovu na uhalifu huo ambao umekiuka misingi ya ubinadamu na utu.

Polisi na mamlaka nyengine za nchi zinapaswa kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka wa kuwajua ni nani waliohusika na tukio hili na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Hili la kuchukua hatua za haraka na za dharura na kuongeza kasi ya uchunguzi ni la muhimu sana maana sasa matukio ya hujuma kwa kutumia tindikali (acid) yamekuwa ni jambo la kawaida na yanaendelea kuongezeka.

Tukio hili la jana linakwenda moja kwa moja na kupiga moyo wa uchumi wa Zanzibar kwa maana ya sekta ya utalii. Tusipochukua hatua za haraka na za dharura na kuonekana tunajali, uchumi wa Zanzibar unaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa na kuyumbisha utoaji wa huduma kwa wananchi, huduma ambazo zinategemea mapato yanayotokana na utalii.

Nilipata nafasi ya kufika haraka pale walipokuwepo waathirika wa tukio hilo mara baada ya kupata taarifa na pia kuwasindikiza hadi Uwanja wa Ndege wa Zanzibar nikiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na
Michezo, viongozi wa Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii (ZATI) na  Balozi wa Heshima wa Uingereza aliyepo Zanzibar. Nawapa pole wasichana hao wawili na nawaombea wapone kwa haraka. Fikra, hisia na dua zetu ziko pamoja nao. Sifa ya Zanzibar kwa karne nyingi imekuwa ni kisiwa cha amani ambacho watu wake ni wastaarabu, wakarimu na wanaopenda wageni. Mjengeko wa jamii ya yetu ya Kizanzibari wenyewe umetokana na mchanganyiko wa watu kutoka sehemu mbali mbali duniani ambao walihamia Zanzibar na kupafanya ndiyo maskani yao. Kitendo kama hichi kilichotokea jana kinakwenda kinyume na misingi ya historia yetu hiyo.

Ni mapema kusema ni nani aliyepo nyuma ya kitendo hichi lakini jambo moja la wazi ni kuwa yeyote anayehusika amekusudia kuiumiza Zanzibar na Wazanzibari. Kuuhujumu utalii ni kuuhujumu uchumi wa Zanzibar na kuyahujumu maisha ya Wazanzibari. Wakati mamlaka zinazohusika zikiendelea na uchunguzi wa tukio hili, kuwasaka waliohusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria, natoa wito kwa Serikali kuchukua hatua zifuatazo:

  1. Kuongeza doria za polisi ndani ya Mji Mkongwe ambao bado unabakia kuwa ndiyo mji mkuu wa Zanzibar na pia kituo kikuu cha harakati zote za kiuchumi ikiwemo biashara na utalii. Kuwepo kwa Polisi Jamii chini ya dhana ya Ulinzi Shirikishi kusiwe ndiyo mbadala wa Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wake hasa kufanya doria za kawaida. 

  2. Kuuwekea Mji Mkongwe kamera za mitaani za kufuatilia nyenendo za watu (surveillance cameras) hasa ikizingatiwa kuwa Mji Mkongwe ndiko kwenye harakati nyingi zinazopelekea mkusanyiko wa watu wengi wakiwemo watalii na wageni wengine wanaotembelea Zanzibar. 

  3. Mji Mkongwe kurejeshewa huduma ya taa za njiani na za mitaa (street lights) ili kuongeza usalama wa watu wakiwemo wageni wanaotembelea eneo hili ambako kuna idadi kubwa ya hoteli za kitalii. 

  4. Jeshi la Polisi Zanzibar limekuwa likilalamika kwa kuwa na bajeti ndogo isiyokidhi mahitaji ya kutekeleza wajibu wao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutokuwa na usafiri wa uhakika, mafuta na vifaa vya kazi. Mamlaka zinazohusika zinapaswa kukaa pamoja na kutatua matatizo haya. 

  5. Serikali, Jeshi la Polisi, na mamlaka nyengine zinazohusika pia wanapaswa kuwa na vikao vya mashauriano vya mara kwa mara na Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii (ZATI) na Jumuiya ya Watoa Huduma za Usafirishaji na Utembezaji Watalii (ZATO) ili kushughulikia matatizo mbali mbali yanayojitokeza hususan yale yanayohusu masuala ya usalama wa wageni wanaotembelea Zanzibar.

Mwisho, natoa wito kwa wananchi na wakaazi wote wa Mji Mkongwe na Zanzibar kwa ujumla kuwa makini na kufuatilia nyenendo zinazotia mashaka au zinazoashiria mwelekeo wa kufanya vitendo vya uhalifu ndani ya Mji wetu na ndani ya Zanzibar au hata nje ya Zanzibar na pale wanapobaini mwelekeo kama huo kutoa taarifa haraka kwa mamlaka zinazohusika. ISMAIL JUSSA MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI JIMBO LA MJI MKONGWE a na Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii (ZATI) na Jumuiya ya Watoa Huduma za Usafirishaji na Utembezaji Watalii (ZATO) ili kushughulikia matatizo mbali mbali yanayojitokeza hususan yale yanayohusu masuala ya usalama wa wageni wanaotembelea Zanzibar.

cristiano ronaldo alivyomliza jose mourinho leo

wasichana raia wa Uingereza waliomwagiwa tindikali wakipelekwa Dar es salaam kwa matibabu

$
0
0
 
 Wasichana rais wa Uingereza Katie Gee and Kirstie Trup wakipelekwa Dar es salaam baada ya kumwagiwa tindikali huko Zanzibar juzi. Hivi sasa wako njiani kuelekea London, Uingereza, kwa matibabu zaidi na kurejea kwao baada ya kufanya kazi za kujitolea kama waalimu huko Kisiwani. Shambulio hili linatangazwa na vyombo vyote vikubwa duniani na tayari vimetia doa pamoja na alama ya kujiuliza kwa visiwa vya Zanzibar 

Katibu Tawala mpya wa wilaya ya Masasi aanza Yohana Miwa alonga

$
0
0

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe George Mkuchika (kulia) akimpongeza Mhe Yohana Miwa kwa kuteuliwa kuwa Katibu Tawala wa wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara 
---------------------------------
Habari na picha na Abdulaziz video
 Serikali ya Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara, imesema kuwa uongozi wa wilaya utahakikisha unaanza kushirikisha makundi ya watu wenye ulemavu katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa asilimia 100 ikiwemo kushiriki kwenye ziara za viongozi wa kitaifa wanaokwenda Wilayani humo jambo ambao litasaidia kuondoa dhana ya kunyanyapaliwa. 
Kauli hiyo imeitolewa Jumamosi na Mhe Yahana Miwa, Katibu Tawala wa wilaya hiyo,  alipokuwa akifungua mafunzo ya mkataba wa umoja wa mataifa (UN) kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanahusu sheria na sera kwa watu wenye ulemavu mkoani Mtwara na kuandaliwa na shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) mkoani humo na kufanyika katika ukumbi wa mami mjini hapa. 
Mhe Miwa alisema serikali itahakikisha kwamba makundi yote ya watu wenye ulemavu yaliyopo Masasi yanashiriki kikamilifu masuala mbalimbali ya maendeleo ili kuyapa fursa kwa makundi hayo kuweza kutoa mchango wao katika mambo ya maendeleo yanayofanyika Wilayani humo kama makundi mengine ya kijamii yanavyoshirikishwa. 
Alisema walemavu ni sawa na watu wasio walemavu hivyo wana haki ya kushiriki katika masuala mbalimbali ya maendeleo yanayofanyika katika maeneo yaliyowazunguka hivyo kuanzia serikali Wilayani Masasi inaahidi kuanza kushirikiana na makundi ya watu wenye ulemavu bega kwa bega ili kwa pamoja kuweza kuleta maendeleo Wilayani humo. 

Ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Joyce Sims na ngoma yake ya 'Come into my life' inanikumbusha mbaaaaaaaalii....

Swala ya Iddi Unguja leo

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid karume kabla ya kuanza kwa Swala ya Idd el Fitri iliyosaliwa Kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman,Mjini Unguja. Kati yao ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi

 Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji ,akiswalisha Swala ya Idd el Fitri,ambayo kitaifa iliwaliwa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja leo katika kufuatia kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Sehemu ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika swala ya Idd el Fitri,iliyoswaliwaa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan
 Akina mama waumini wa Dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Idd el Fitri katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan
  Imamu Mkuu wa Msikiti Masjid  Mushawal Mwembeshauri Sheikh Mziwanda Ng'wali Ahmed,akitoa hutuba ya swala ya idd el fitri,katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Ungujaleo katika kusherehekea sikukuu hiyo kwa wailamu wote Duniani 
 Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi baada ya kumalizika kwa swala ya Iddi el fitrile

Ujumbe wa wawekezaji toka Japan watembelea mamlaka ya bandari (TPA) leo

$
0
0
Ujumbe wa wawekezaji toka Japan unaotembelea mamlaka ya bandari (TPA)  ukiwa katika kikao na maafisa wa bandari jijini Dar es salaam leo. Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imejipanga vizuri kuhudumia wateja wote wa ndani na wa nje, na ili kufikia malengo hayo TPA inakaribisha wawekezaji binafsi ili kushirikiana katika kuendeleza na kujenga miundombinu ya Bandari zetu

EID MUBARAK

$
0
0

Assalaamu'alaykum wa rahmatullah wa barakatuh - 

May God's peace and blessings be upon you
May the Mercy & Blessing's of the Almighty be with you, your family, and friends during this auspicious Eid Blessings Day and continue to be always, and May Allah (swt)  accept all our prayers/duas during this blessed month of Ramadan, insha'Allah (God Willing). 

May your year ahead continue to be filled with a healthy, wealthy, and prosperity life, and May you have a Joyous and Spirited Eid Mubarak (Blessings) day with all your dear ones, including people of all faiths and humanity, filled with Love, Peace, and Happiness .... Ameen

Have A Most Blessed Festival Of Nature.

Respectfully in Prayers & Duas always/ wa Salaam,

Your Friendly... 


SALAMU ZA IDDI TOKA KIBAHA

$
0
0
Alhaji Yusufu Saidi Mfinanga wa Kibaha, Njuweni, mkowa wa Pwani pamoja na Mke wake Mama Mfinanga wamewaomba  Watanzania   kudumisha amani na upendo kwa kuondoa tofauti zetu za kidini kisiasa kwani kufanya hivyo Mwenyezi Mungu ataendelea kuijalia amani na baraka iliyokuwepo hapa nchini  kwani kupendana kutaleta maendeleo katika nchi tuswali na kuheshimu mamlaka za serekali zilizopo kwani mafundisho ya dini zote yafundisha amani upendo na utii

BALOZI MULAMULA, BALOZI NYANG'ANYI WASHEREHEKEA EID EL FITR NA WATANZANIA DMV

$
0
0

Balozi Mulamula akiwasili kwenye park ya Wheaton huku akilakiwa na Afisa Ubalozi Suleiman Saleh.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mustafa Nyang'anyi wakiwemo viongozi wa TAMCO na wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
Mhe.Balozi Liberata Mulamula naye alisisitiza umoja wa Watanzania na kuimwagia sifa Jumuiya ya Waislamu DMV (TAMCO) kwa mshikamano walionao na jitihada zao za kuwaunganisha Watanzania wa DMV bila kujali itikadi za dini zao na kusema kwamba kuanzia jana yeye amejiunga rasmi na atakuwa mwanachama wa kudumu wa TAMCO pia aliwakumbusha enzi ya kidongo chekundu na Zanzibar sikukuu ya Eid ilivyokuwa ikisherehekewa pia alikabidhi Eid yake kwa Afisa Ubalozi Abbas Missana kwa ajili ya  watoto waliokuwepo kwenye sherehe hiyo.
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mustafa Nyang'anyi akiongea machache kwenye sherehe hiyo ya Eid El Fitr iliyofanyika DMV huku akisisitiza umoja wa Watanzania ni kitu muhimu sana bila kujali itikadi zao, alisema amefurahi kukuta TAMCO aliyoianzisha wakati ule yeye akiwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani bado inaendelea kwa nguvu zote pia  Balozi Nyang;anyi alisisitiza Watanzania Waache majungu huku akisema kama mtu una jambo linakukera ni bora uliweke wazi kwani majungu hayajengi, pia aliendelea kwa kusema uwazi wa mapato na matumizi ni jambo kubwa kwenye jumuiya zetu lisipokuwa wazi Wanajumuiya hukosa imani na viongozi wao na hatima yake hufanya Jumuiya kulegalega na baadae kufa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SWALA YA IDD KWENYE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Imam Mkuu wa Msikiti wa Manyema,Sheikh Hamad Jongo akiswalisha Swala ya Idd el Fitri,ambayo kimkoa imeswaliwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.ikiwa ni ibada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Waumin wa Kiislam kutoka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam,wakishiriki kwenye Swala ya Idd el Fitri,ambayo kimkoa imeswaliwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.ikiwa ni ibada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Imam Mkuu wa Msikiti wa Manyema,Sheikh Hamad Jongo akitoa hotuba wakati wa Swala ya Idd el Fitri,ambayo kimkoa imeswaliwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.ikiwa ni ibada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Waumin wa Kiislam kutoka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam,wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Imam Mkuu wa Msikiti wa Manyema,Sheikh Hamad Jongo wakati wa Swala ya Idd el Fitri,ambayo kimkoa imeswaliwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.ikiwa ni ibada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mwenyekiti wa CUF,Prof. Ibrahim Lipumba akiwa akiwa ni miongoni mwa waumini wa kiislam walioswali swala ya Idd el Fitr,kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Waumini.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SWALA YA SIKUKUU YA IDDI KITAIFA MKOANI TABORA

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa salamu maalum za Sikukuu ya Iddi baada ya Swala iliyofanyika Kitaifa Mkoani Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi leo, Agosti 9, 2013. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Shaaban Bin Simba, mara baada ya Swala ya Iddi iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mkoani Tabora leo Agosti 9, 2013

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa sita kutoka kulia), akishiriki na waumini wa dini ya Kiislamu katika Swala ya Sikukuu ya Iddi, iliyoswaliwa Kitaifa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora leo, Agosti 9, 2013.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika Swala ya Sikukuu ya Iddi iliyoswaliwa Kitaifa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora leo, Agosti 9, 2013.
   Sehemu ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliojitokeza kuhudhuria Swala ya Sikukuu ya Iddi, iliyoswaliwa Kitaifa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mkoani Tabora leo, Agosti 9, 2013. Picha n0a OMR
    Sehemu ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliojitokeza kuhudhuria Swala ya Sikukuu ya Iddi, iliyoswaliwa Kitaifa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mkoani Tabora leo, Agosti 9, 2013. Picha n0a OMR.

Kwaya ya Uinjilisti Usharika wa kilutheri kijitonyama kufariji yatima jumapili

$
0
0
Kwaya ya Uinjilisti Usharika wa kilutheri kijitonyama inatarajia kwenda kuwafariji na kuimba na watoto yatima wa kituo cha Kurasini siku ya Jumapili tarehe 1/08/2013

Hivyo tunaomba kwa atakayeguswa kuleta msaada wowote kanisani kijitonyama ofisi ya mwinjilisti, pia tunarajia kufanya uzinduzi wa album yetu mpya iitwayo Namtangaza kristo mapema mwezi wa Tisa tukiwa katika matukio ya kuelekea kuadhimisha Jubilee ya miaka 25 ya kwaya yetu, kwa mawasilino zaidi tumia namba 0655 550 037 au 0712 218 551

Asanteni na karibu

JK ahudhuria swala ya Iddi Kinondoni

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akingia katika msikiti wa Kinondoni Muslim tayari kuhudhuria swala ya Iddi leo asubuhi,jijini Dar es Salaam.

WADAU WAPONGEZA HUDUMA ZA PPF KATIKA MAONESHO YA NANE NANE DODOMA

$
0
0
Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akifurahia taarifa yake ya michango mara baada ya kuhudumiwa, waliopembeni yake ni Maafisa wa Mfuko huo.
Afisa wa Mfuko wa PPF, Bilal Mlendela akisisitiza jambo kwa mwanachama wakati wakipitia kitabu cha Mwongozo wa Mafao.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati, John Mwalisu akitoa elimu juu ya shughuli za Mfuko wa PPF katika Maonesho ya Nane nane.
Afisa Uhusiano wa PPF, Janet Ezekiel akimhudumia mwanafunzi aliyetembelea banda la PPF.
Afisa Uwekezaji wa PPF, Anna Shayo akitoa elimu kuhusu mikopo ya SACCOS. Mfuko huo hutoa mikopo kwa wanachama wake kupitia SACCOS zilizopo katika maeneo ya kazi.

Wakazi wa Jiji la Dar walivyoisherehekea sikukuu ya Idd el Fitr katika Fukwe za Coco Beach na Kawe

$
0
0
 Wakazi wa Maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam,wakiwa katika Fukwe ya Kawe Beach ikiwa ni katika kusherehekea sikukuu ya Idd el Fitr ilioadhimishwa leo Duniani kote,mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
 Watoto wakiogelea kwa raha zao.
 Wengine waliendelea kuwasiliania na wenzao kwa kuwadolishia raha wazipatazo katika fukwe ya Coco Beach jijini Dar. 
 Jamaa wakimuangalia mwenzao akipiga mbizi majini.

mpigie Kura Feza Kessy aweze kubaki ndani ya Jumba la Big Brother

mashindano ya mbio za baiskeli Kanda ya Ziwa (Safari Bike Race 2013) yafana sana

$
0
0
Baadhi ya washiriki wa mbio za Baiskeli Kanda ya Ziwa (Safari Bike Race) 2013, Wanaume wakichuana kuelekea Nzina (Igunga) km 210 kutoka Shinyanga na kurudi wakati wa sherehe za sikuu ya nane nane ambazo hufanyika kila mwaka kwa kanda hiyo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Kaimu katibu tawala Rasilimali na Watu wa Shinyanga, Projestas Lubanzibwa(kushoto) akimkabidhi bingwa wa Mbio za Baskeli Kanda ya Ziwa (Safari Bike Race) 2013, Masunga Duba kutoka Mwanza, kitita cha shilingi milioni moja (1000000/=) zilizofanyika Mkoani Shinyanga wakati wa sherehe za siku kuu ya nanene ambazo hufanyika kila mwaka.
Bingwa wa Mbio za Baskeli Kanda ya Ziwa (Safari Bike Race) 2013, Masunga Duba kutoka Mwanza(kulia) akionyesha kitita cha shilingi milioni moja (1000000/=) mara baada ya kukabidhiwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Kaimu katibu tawala Rasilimali na Watu wa Shinyanga, Projestas Lubanzibwa zilizofanyika Mkoani Shinyanga wakati wa sherehe za siku kuu ya nanene ambazo hufanyika kila mwaka.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa wamefurika katika Uwanja wa mpira wa Miguu wa Kambarage Mkoani Shinyanga kushuhudia mbio za Baiskeli kwa kanda ya Ziwa zinazojulikana kwa “Safari Bike Race” wakati wa kusherehekea sikuu ya nane nane ambazo hufanyika kila mwaka kwa kanda hiyo.
Msanii wa kutoka kampuni ya Integrated Comminications,Jembe Ulaya akitumbuiza mara baada ya mashindano ya Mbio za baiskeli Kanda ya Ziwa(Saafari Bike Race) wakati wa kusherehekea sikuu ya nane nane ambazo hufanyika kila mwaka kwa kanda hiyo.

RAIS WA ZANZIBAR,DKT. SHEIN AHUTUBIA BARAZA LA IDD LEO

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa Serikali itafanya kila iwezalo kuwakamata na kuwapeleka katika Vyombo vya sheria Watu waliohusika kuwamwagia Tindikali Raia wawili wa Uingereza hivi karibuni.

Amesema Vyombo vya Ulinzi na Usalama viko Imara na kwamba vitaendelea kulinda amani ya Nchi ikiwemo kuwabaini Wahalifu wote na kuwapeleka katika Vyombo husika.

Dkt Shein ameyasema hayo leo alipokuwa akiwahutubia Wananchi kupitia Baraza la Idd lililofanyika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.

Amesema kwa mara ya pili kila inapokaribia Sherehe za Sikukuu kumekuwa na mfululizo wa Matukio ya kihalifu na kuongeza kuwa kila aliyehusika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“Vitendo hivi si uungwa ni Ukatili, hatutawatia hatiani Wasiohusika lakini kila aliyehusika hatutamsamehe” Alionya Dkt Shein.

Aidha Dkt. Shein amelaani kushamiri kwa Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji hasa kwa Watoto ambapo jumla ya Watoto wakike 480 Zanzibar wamebakwa katika kipindi cha mwezi Julai 2012 hadi Aprili mwaka huu.

Amesema hilo ni jambo la kushtua sana na kwamba wakati umefika kila mmoja kuchukua hatua zinazofaa kudhibiti hali hiyo.

Dkt Shein ametoa wito kwa Wananchi na Viongozi wote kuendelea kupendana bila kuchukiana na kulinda Amani, Umoja na Kuvumiliana kwa manufaa ya Zanzibar.

Amesema panapotokea tofauti za hoja kuhusu suala la Maendeleo ya Nchi jambo la busara ni kuzungumza na kujadili kwa kuzingatia sheria zilizopo kwa manufaa ya Zanzibar.

Dkt Shein ametoa Shukrani kwa Jeshi la Polisi kwa kudumisha hali ya amani katika kipindi chote cha Mwezi wa Ramadhani na kulitaka Jeshi hilo lizidishe juhudi zake kipindi cha Sherehe za Idd na siku za usoni.

Kabla ya Baraza la Idd Dkt Shein alitoa Mkono wa Idd kwa Wazee na Watu wasiojiweza katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images