Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

TPDC YAWEZESHA KUWASHWA MITAMBO YA KINYEREZI II JIJINI DAR

$
0
0
Na Mwandishi Wetu.

Mwaka 2004 utaendelea kubaki katika kumbukumbu za nchi yetu kama mwaka wa mageuzi katika sekta ya nishati ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania ilianza kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia. Miaka kumi na nne baadae, Tanzania imeendelea kuwa kinara katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zinatumia gesi asilia kuzalisha umeme ambapo hadi sasa zaidi ya asilimia 50% ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na nishati ya gesi asilia. 
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi II, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Joseph Magufuli alisema “nishati ya umeme ni injini na muhimili muhimu katika ukuzaji uchumi na ustawi wa maisha ya binadamu, umeme unachochea shughuli za uzalishaji na hivyo kutoa fursa za ajira na kuboresha maisha ya watu”. Mh. Rais pia aliongeza “Azma na dhamira yetu ya kujenga uchumi wa viwanda haiwezi kutimia bila ya kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika”. Mitambo ya kufua umeme ya Kiyerezi II ina uwezo wa kuzalisha megawati 240 za umeme na inategemea gesi asilia inayozalishwa na kusambazwa na TPDC kupitia kampuni tanzu ya Gasco inayosimamia shughuli za ukusanyaji na usambazaji wa gesi asilia nchini. 
Kwa upande wake Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alieleza mipango ya Wizara ya Nishati katika kufikia Tanzania ya viwanda kwa kutumia gesi asilia kuzalisha umeme wa uhakika. Dk. Kalemani alisema “ufunguzi wa Kinyerezi II ni muendelezo wa miradi ya umeme wa gesi asilia, baada ya mradi wa leo tunategemea kutekeleza miradi mingine miwili hapa Kinyerezi ambayo yote itatumia gesi asilia na kuzalisha megawati 600, isitoshe tunatarajia kuzalisha umeme wa gesi asilia pale Somangafungu megawati 320 na kule Mtwara megawati 300”. Ni wazi kabisa kwamba mchango wa gesi asilia hususan kwenye upatikanaji wa umeme wa uhakika hapa nchini ni jambo lililo wazi na la kujivunia.
Sehemu ya mitambo ya kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi, kituo hiki ndicho kinachopokea gesi na kuipeleka katika mitambo ya kufua umeme na nyingine kupelekwa katika viwanda. 
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba alisema “TPDC imejipanga vema kuhakikisha gesi asilia inaendelea kupatikana kwa wingi ili kuwezesha Tanzania ya viwanda sio tu kwenye umeme bali hata kwenye viwanda moja kwa moja ambapo hutumika kama chanzo cha nishati au malighafi”. Mhandisi Musomba alieleza namna ambavyo TPDC kupitia kampuni tanzu ya Gasco walivyohakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuwezesha kuwashwa kwa mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi II. 
TPDC ambalo ni Shirika la Mafuta la Taifa ndio mmiliki wa leseni zote za utafiti na uendelezaji wa gesi asilia na mafuta nchini. Katika kutekekeleza majukumu yake, TPDC huingia mikataba ya kugawana mapato ijulikanayo kama “Production Sharing Agreement (PSA)” na kampuni za kimataifa za mafuta na gesi (IOC) ambazo hujulikana kama mkandarasi. Kazi ya mkandarasi huyu ni kufanya kazi za utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi kwa kushirikiana na TPDC ambapo TPDC husimamia maslahi ya nchi na kuhakikisha tozo zote pamoja na hisa za Serikali katika mikataba hiyo zinalindwa na kulipwa kwa wakati.

KAMATI ZA WATU WENYE ULEMAVU ZA MKOA KUTAMBULIKA KISHERIA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu kwa kuzingatia sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na kusimamia uundwaji wa kamati zinazoshughulikia masuala yao hapa nchini.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 4, 2018) wakati akiwasilisha hotuba ya mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Bungeni dodoma.

Amesema Serikali itaboresha mazingira ya watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha uundwaji wa kamati zao zinazotambulika kisheria ili kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili na kuhakikisha kila mkoa unaunda kamati hizo ambapo hadi sasa mikoa 12 imekamilisha zoezi la uundwaji wa kamati hizo.

“Tayari Serikali imeunda kamati za watu wenye ulemavu katika mikoa 12 ya Geita, Kagera, Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza, Njombe, Pwani, Singida, Rukwa, Shinyanga, Simiyu na Tabora. Ufuatiliaji unaendelea kufanyika ili kuhakikisha kuwa mikoa mingine nayo inaunda kamati hizo,” alisema Waziri Mkuu.Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha uboreshaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu, Serikali imeendelea kutoa vifaa zaidi ili waweze kushiriki katika shughuli za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutoa vifaa saidizi kwa jamii ya watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kufanya shughuli zao bila utegemezi kwa kuwapatia baadhi ya vifaa ikiwemo viti mwendo 240, bajaji 6, magongo ya kutembelea 350, kofia pana 128, fimbo nyeupe 175, miwani maalum kwa wenye uoni hafifu 70, shime sikio 20, vyerehani 8, vifaa vya kukuzia maandishi 65, mafuta maalum ya kukinga ngozi dhidi ya mionzi ya jua 35, viti maalum vya kuogea 50 na nyenzo nyingine za kujimudu,” alisema.

Alisema Serikali imeendelea kuviboresha vyuo vya watu wenye ulemavu vya Yombo, Dar es Salaam na Sabasaba, Singida ili kuhakikisha wanashiriki katika fursa zote ikiwemo za elimu ili wawe na ujuzi utakaowawezesha kushiriki katika fursa za ajira nchini ikiwa ni utekelezaji wa Sheria Na. 9 ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2010.

Alisema Serikali itaendelea kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kukamilisha uanzishwaji wa Mfuko wa Taifa wa Maendeleo wa Watu wenye Ulemavu, kuanzisha madawati ya watu wenye ulemavu, kuhamasisha sekta binafsi na umma kuweka miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu na kuwataka waajiri wote wawaajiri watu wenye ulemavu wenye sifa kwenye nafasi mbalimbali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Afisa Mtetezi CCBRT Bw. Fredrick Msigala kwenye viwanja vya Bunge baada ya kuwasilisha hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA MKOA WA MJINI MAGHARIBI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namba umeme wa majumbani na viwandani unavyofanya kazi kutoka kwa mkufunzi wa umeme wa Chuo cha Mwenge Community College Mwalimu Mohamed Mbarawa wakati wa ziara ya Makamu wa Rais chuoni hapo wilaya ya mjini mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanafunzi wa kozi ya uuguzi wanaosoma kwenye chuo cha Mwenge Community College kilichopo wilaya ya mjini mkoa wa Mjini Magharibi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kozi ya uuguzi wanaosoma kwenye chuo cha Mwenge Community College kilichopo wilaya ya mjini mkoa wa Mjini Magharibi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya ujenzi wa miundo mbinu katika mradi wa maji utakao nufaisha wakazi wa elfu saba mia tano (7500) katika Shehia 4 mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa tanki la maji safi Kikawajuni kwa Mselem katika jimbo la Kikwajuni, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi Ndugu Ayoub Mohammed Mahmoud .Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

ALICHOKISEMA DKT. ABBASI KWA WAANDISHI WA HABARI CHIPUKIZI WALIONELEWA NA TMF

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kufanya utafiti wa taarifa wanazozitengeneza kabla hawajazitoa kwa jamii kupitia vyombo vya habari.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ametoa rai hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga mafunzo ya Waandishi wa Habari za maendeleo yaliyotolewa na Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF) juu ya usalama barabarani pamoja na masuala ya maendeleo.

Dkt. Abbasi amesema kuwa Waandishi wa Habari wanatakiwa kufahamu haki na wajibu wa taaluma hiyo ambapo moja wapo ya wajibu wa mwanahabari ni kufanya utafiti wa chanzo na habari husika kabla ya kuifikisha kwa jamii ikiwa ni njia itakayosaidia kuzuia utoaji wa habari zisizo na uhakika kwa jamii.

“Kutoa taarifa za uhakika kwa jamii kunahitaji taaluma na weledi wa hali ya juu, hivyo Wanahabari wanatakiwa wajikite zaidi katika kutafuta taarifa sahihi na kusisambaza kwa wananchi. Nawapongeza sana TMF pamoja na wadau wote walioshiriki katika uandaaji wa mafunzo haya.” amesema Dkt. Abbasi.Dkt. Abbasi amefafanua kuwa Waandishi wa Habari wana haki ya kuikosoa Serikali ambapo Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kifungu cha 52 (2) imebainisha suaka hilo lakini taaluma, weledi haki na wajibu katika uandishi wa habari lazima vifuatwe.

Amewaomba wafadhili wa mafunzo hayo pamoja na wadau wengine kutochoka kuwasaidia wanahabari ili waweze kutimiza majukumu yao ya kutoa taarifa kikamilifu na kuendelea kuwa washirika wa maendeleo nchini.Kwa upande wake Mkurugenzi wa TMF, Fausta Msokwa amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari kuwa wabobezi katika kutoa taarifa za uhakika za masuala mbalimbali ya maendeleo.

“Mafunzo hayo yameleta uhai endelevu katika tasnia ya habari na kuwafanya Waandishi wa Habari kutoa habari zenye tija hasa katika kuelezea changamoto zilizopo maeneo ya vijijini,” amesema Mkurugenzi Fausta.Mafunzo hayo yaliyoanza mwezi Mei mwaka jana na kuhusisha waandishi wa habari 15, yamefanyika kwa ushirikiano wa Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na baraza la usalama barabarani na kufadhiliwa na Shirika la Afya Duniani pamoja na Taasisi ya Bloomberg.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa Waandishi wa Habari aliyepata tuzo zijulikanazo kama ‘simema zetu’ kwa kuandaa makala bora za Televisheni,Anwaly Msechu wakati wa kufunga mafunzo ya Waandishi wa Habari yaliyotolewa na Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF) juu ya usalama barabarani pamoja na masuala ya maendeleo.Ufungaji huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa Waandishi wa Habari aliyefanya vizuri katika mafunzo hayo, Adelina Bosco wakati wa kufunga mafunzo ya Waandishi wa Habari yaliyotolewa na Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF) juu ya usalama barabarani pamoja na masuala ya maendeleo.Ufungaji huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau, washiriki na wakufunzi baada ya kufunga mafunzo ya Waandishi wa Habari yaliyotolewa na Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF) juu ya usalama barabarani pamoja na masuala ya maendeleo.Ufungaji huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

SERIKALI KUIMARISHA MASOKO YA MAZAO MAKUU MATANO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuimarisha vyama vya msingi vya ushirika vya mazao ya kilimo na masoko vinavyozalisha mazao ya kimkakati ya biashara ya pamba, kahawa, korosho, chai na tumbaku. 
Amesema katika mwaka 2018/2019, Serikali inalenga kuimarisha masoko ya mazao hayo kwa kuhamasisha mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo mazao hayo yatazalishwa na kuuzwa kupitia vyama vya ushirika kwa njia ya minada. 

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 4, 2018) Bungeni mjini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019 kwenye mkutano wa 11 wa Bunge.

Waziri Mkuu amesema pamoja na hatua hizo, Soko la Bidhaa ambalo limeshaanzishwa, litasaidia sana kuimarisha masoko ya mazao kwani yatakuwa yanauzwa kwa njia ya ushindani mkubwa huku wakulima wanaozalisha kwa ubora wakinufaika na bei ya juu zaidi.

“Serikali imeamua kuweka mkazo maalum wa kuyaendeleza kwa kasi mazao matano ya biashara ambayo ni chai, kahawa, korosho, pamba na tumbaku. Lengo ni kuongeza mapato ya wakulima, kuwa chanzo cha kuaminika cha malighafi katika uchumi wa viwanda, na kuendelea kuwa chanzo kikuu cha ajira na fedha za kigeni. 

Amesema uamuzi wa kuongeza usimamizi katika uzalishaji wa mazao hayo makuu ya biashara unatokana na ukweli kwamba, kwa kipindi kirefu uzalishaji ulishuka kutokana na changamoto kadhaa. 

“Miongoni mwa changamoto hizo ni kupungua tija katika uzalishaji, baadhi ya wakulima kuacha kulima mazao hayo kutokana na kukata tamaa kwa sababu mbalimbali zikiwemo vyama vya ushirika kutotekeleza vema wajibu wao, wizi, dhuluma na pia ushiriki mdogo wa maafisa kilimo katika kusimamia kilimo cha kitaalamu,” alisema. 

PROF KABUDI ATAJA HATUA INAZOCHUKUA SERIKALI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza  Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na hatua  za kuhakikisha kunakuwepo mazingira wezeshaji yatayofanikisha ujenzi wa viwanda nchini. 

Prof.Kabudi amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya utafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya REPOA ambapo mada kuu ilikuwa kujadili kuelekea jamii inayoendeleza viwanda 2025 : kwanini ushindani ni muhimu.

Pia kwenye warsha hiyo wadau wamejadili masuala ya kisera katika safari ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi mseto na shindani ,ukiongozwa na viwanda , pamoja na kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama inavyotarajiwa kwenye dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

akizungumza  baada ya ufunguzi wa washa hiyo Profesa Kabudi ametaja hatua mbalimbali ambazo Serikali inachukua katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini na kufafanua kinachoendelea ni kuangalia jinsi gani kufanya bidhaa za Tanzania kuwa na ushindani kwenye soko la Dunia.

"Kuna mambo mengi ya kufanya katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini .Nikumbushe tu wakati tunapata uhuru tulikuwa na viwanda viwili , hivyo jukumu la wakati ule ikawa ni kuanza kujenga viwanda na vilijengwa na kutoa ajira kwa wananchi.

"Hata hivyo ilipofika mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki tukarudi nyuma kidogo na baadae tukaingia kwenye vita dhidi ya Uganda ambapo tulitumia dola za Marekani milioni 5 kwenye vita.Hivyo tukawa hatuna fedha za kuendeleza viwanda.

"Pamoja na magumu ambayo tumeyapitia bado leo hii tunavyo viwanda vingi ingawa jukumu la Serikali ni kujenga viwanda zaidi ili kuboresha maisha ya wananchi wake katika kuleta maendeleo,"amesema Profesa Kabudi.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi akizungumza na wadau wa utafiti wakati akifungua Warsha ya siku mbili kwa watafiti wa Tanzania na kutoka nje iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya REPOA jana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi  Amina Salim Alli akizungumza wakati anaongoza mjadala juu ya Uchumi wa Viwanda kufikia 2025
 Mtoa mada Mkuu wa Warsha hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za kusini mwa Afrika katika mausuala ya forodha(SACU), Paulina Mbala Elago akitoa mada yake juu kwanini Ushindani na jinsi ya kuufikia katika maendeleo ya viwanda katika nchi hizo.
 Mkurugenzi Mkuuu wa Tasisi  ya utafiti nchini Repoa Dk Donald Mmari akizungumza kabla ya kumkaribisha msemaji mkuu katika warsha hiyo ya kwanini ushindani juu ya viwanda kufikia 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Infotech Investment Group LTD , Ali Mufuruki akiongoza majadiliano ya hali ya biashara kwa sasa katika Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Repoa nchini.
 Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali
  Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KIWANDA CHA KUSINDIKA TUMBAKU SONAMCU KUFUFULIWA MKOANI RUVUMA

$
0
0
Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Songea Namtumbo ( SONAMCU) kilichopo Songea Mjini mkoani Ruvuma kinatarajia kuanza kufanyakazi ya ya kusindika tumbaku katika msimu wa 2018- 2019 mara tu baada kukamilika kwa matengenezo.

NEWZ ALERT.....: Watu zaidi ya 20 wadaiwa kupoteza maisha ajali ya basi Igunga

$
0
0
Zaidi ya watu 20 wanadaiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajari ya basi la kampuni ya City bus lililogana uso kwa uso na fuso katika kijiji cha makomelo wilayani Nzega mkoani TABORA.

Ajari hiyo imetokea usiku wa kuamkia Leo katika kijiji hicho baada ya kudaiwa dereva wa fuso kutaka kukwepa shimo na kujikuta fuso hilo likimshinda,hivyo  kupelekea kugongana USO kwa USO.

MPAKA sasa kamanda wa jeshi la polisi mkoani TABORA na viongozi wengine wa serikali wamefika katika eneo la tukio huku basi hilo likitarajiwa kunyanyuriwa ili kuona kama kuna watu wengine waliosalia.

Hata hivyo miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospital ya wilaya ya Igunga kwa ajili taratibu zingine.

Globu ya Jamii inafuatilia kwa ukaribu tukio hili,itaendelea kuwaletea taarifa kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana kutoka Mamlaka husika.

Mungu azilaze roho za Marehemu mahali pema peponi-Amen


TAZAMA UJENZI ULIPOFIKIA WA JENGO LA ABIRIA TERMINAL 3 - JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT

Gawio la Airtel Money kwa wateja lafikia bilioni 14.8,

$
0
0

Airtel Tanzania imetoa gawio linalofikia shilingi bilioni 14.8 hadi sasa kwa wateja wake na mawakala nchi nzima ikiwa ni sehemu ya faida waliyoipata tangu mwaka 2015. 

Hili limebainishwa na Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Airtel wakati akitangaza gawio la robo hii ambalo ni shilingi bilioni 1.8. 

“Tangu tuanze kugawa sehemu ya faida yetu kwa wateja mwaka 2015, tumeshatoa jumla ya shilingi bilioni 14.8 na huwa tunagawa kila robo ya mwaka na kuhakikisha wateja na mawakala wanapokea fedha hizi kupitia akaunti zao za Airtel Money na wana uhuru wa kutumia fedha hizi wanavyotaka,” alisema. 

Kwa mujibu wa Nchunda, hii ni mara ya sita mfulululizo kwa Airtel Tanzania kugawa sehemu ya faida kwa wateja wake tangu mwaka 2015. “Bwana Pesa hutoa gawio hili kwa wateja wa Airtel Money na mawakala kulingana na salio la mteja kila siku,” aliongeza. Aliwashukuru wateja wa Airtel kwa kuendelea kutumia Airtel Money na kuifanya iwe huduma yenye tija na maarufu zaidi na kuongeza kuwa hadi sasa wana zaidi ya maduka 100 maalum kwa kutoa huduma ya Airtel Money ambayo yanafanya huduma hii iwe ya kuaminika zaidi na rahisi kupatikana. 

“Maduka haya ya Airtel Money huhakikisha mawakala wana salio la kutosha muda wote ili wateja wasipate usumbufu wanapohitaji huduma hiyo,” alisema. Kwa upande wake, Meneja wa Airtel Money, alisema kuanzia leo, wateja wa Airtel Money na mawakala watapata gawio linalofikia shilingi bilioni 1.8 kupitia akaunti zao za Airtel Money na wanaweza kutumia gedha hizo wanavyotaka ikiwemo kulipia huduma mbalimbali kama vifurushi vya mtandao, muda wa maongezi na LUKU. 

Alitoa wito kwa mawakala wa Airtel Money kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wateja ili kampuni hiyo iendelee kutoa gawio kwa wateja wake kila robo ya mwaka. “Airtel Money imejizatiti kuendelea kutoa huduma bora na nafuu ambayo ni suluhisho kwa biashara za aina yoyote,” alisema na kuongeza kuwa Airtel inashirikiana na biashara zaidi ya 400 na ziadi na benki 30 katika kutoa huduma za kifedha. 

Airtel ina zaidi ya mawakala 50,000 nchi nzima na inaendelea kutanua wigowake ili kuhakikisha huduma za kifedha zinapatikana katika miji na vijijini. 

Mwalimu Rufiji ashinda pasaka mzuka jackpot ya milioni 260.

$
0
0
Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini leo umetangaza na kumtambulisha kwa wana habari mtanzania aliyebahatika kushinda milioni 260 kwenye Pasaka Mzuka Jackpot ambayo ilionyeshwa mubashara kupitia ITV, Clouds TV na TV 1 jumapili ya Pasaka.

Edward Msengi (56), ambaye anatokea Rufiji, Pwani ndiye aliyebahatika kuondoka na kitita cha shilingi milioni 260 ambayo ni jackpot kubwa kuwahi kutolewa kwa mshindi mmoja katika nchi hii.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga alimtambulisha mshindi na kumpongeza kwa ushindi huo mkubwa. “ Sisi Tatu Mzuka tunayo furaha kiasi kwamba tumeamua kumleta mshindi Dar es salaam ili kushiriki pamoja nanyi katika tukio hili kubwa” . Msengi ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Singida na baba wa watoto wanne alikuwepo kudhihirisha furaha yake na kuhadithia safari yake aliyopitia mpaka kushinda kitita kikubwa cha milioni 260.

“ Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kwa muda sasa. Nina furaha kubwa sana. Sikuwahi hata kuota kama ningeweza kupata fursa kubwa kama hii. Ninategemea kujenga nyumba nzuri kwa ajili ya familia yangu na kuwekeza katika biashara pamoja na kuhakikisha kwamba watoto wangu wote wapo katika shule nzuri” alisema Bwana Msengi
 
Mbali ya tukio hilo adhim,Maganga aliufahamisha umma juu ya ujio wa  kampeni ya mwezi April ijulikanayo kama Mzuka FULL CHARGE.

“Maisha ni kusaidiana ndio maana unaposhinda Tatu Mzuka na kuwa ‘FULLCHARGE’; tunakupa fursa ya kumbusti mtu mwingine ambaye utamchagua. Shinda milioni 6 kila saa na upate nafasi ya kuingia kwenye jackpot ya milioni 10 kila siku na milioni 60 jumapili hii ili umbusti yoyote unayemtaka”.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza na wanahabari  mapema leo jijini Dar wakati wa kumtambulisha mshindi 
Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msenga (Kulia) na kumpongeza kwa ushindi mkubwa wa kujishindia kiasi cha Shiling Milion 260. Kushoto ni Mkaguzi kutoka michezo ya Bahati Nasibu  Bakari Maggid.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 260 kwa 
mshindi wa Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msenga .

Mshindi wa 
Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msengi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutambulishwa na kushukuru kwa kupata fedha hizo na kuwataka watanzania waamini kuwa mchezo huo unatenda haki.

MSHTAKIWA MWINGINE KUONGEZWA KESI YA AVEVA NA KABURU, KUSOMEWA MAELEZO YA AWALI BAADA YA UPEPELEZI KUKAMILIKA

$
0
0
Baada ya kulazwa kwa muda mrefu hatimae leo Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amefika mahakamani kuhudhuria kesi yake ya utakatishaji wa fedha inayomkabili yeye pamoja na makamu wake Godfrey Nyange ' Kaburu'. Pia Upande wa mashtaka umedai kuwa unatarajia kumuongeza mshtakiwa mmoja katika kesi hiyo.

Aveva ambaye alikuwa akiugua na kulazwa kwa muda mrefu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, leo amefika mahakamani akiwa anatembea kwa shida huku akiwa ameshikiliwa mkono na mshtakiwa mwenzake Kaburu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, wakili wa Serikali kutoka Takukuru Leornad Swai amedai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali baada ya upelelezi kukamilika.

Hata hivyo, wakili Swai ameiomba mahakama  ahirisho fupi kwa kuwa wanatarajia kufanyia mabadiliko hati ya mashtaka kwa kuongeza mshtakiwa mmoja.Kufuatia ombi hilo, kesi imeahirishwa hadi Aprili 12 mwaka huu kwa ajili ya upande wa mashtaka kufanya mabadiliko hayo na washtakiwa kusomewa Maelezo ya awali.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na Mashtaka matano ya uhujumu uchumi ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na utakatishaji ea fedha ambazo ni Dola za Marekani (USD) 300,000.
Baada ya kuugua kwa muda mrefu hatimae leo Rais  wa klabu ya Simba, Evans Aveva amefika katika mahakamani, pichani akitoka mahakamani baada ya kesi yake inayomkabili yeye na makamu wake Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu kuahirishwa hadi Aprili 12, mwaka Huu.

HUDUMA YA UOKOAJI KUTUMIA HELIKOPTA YAANZISHWA MLIMA KILIMANJARO.

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

KAMPUNI ya Kilimanjaro SAR ya mkoani Kilimanjaro imeanza rasmi shughuli za utafutaji na uokoaji kwa wapandaji wa Milima miwili ya Kilimanjaro na Meru kwa kutumia ndege aina ya Helkopta. 

Kilimanjaro SAR inakua kampuni ya kwanza kuweka historia katika bara la Afrika ya utoaji wa huduma hiyo muhimu na maada kwa maisha ya wapandaji wa Milima ikizingatiwa asilimia 75 ya magonjwa uwapo mlimani yanatokana na mbadiliko ya Hali ya Hewa kulingana na urefu wa Mlima.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR,Ivan Braun raia wa Denmark ameeleza kuwa kuanza kwa shughuli hiyo kutasaidia aliyepata matatizo akiwa mlimani kuhudumiwa ndani ya dakika 5 baada ya kupokea simu ya hitaji la msaada.

“Kampuni hii itatoa huduma kamili ya uokoaji wa dharura kwa wapanda Mlima,Takwimu zinaonyesha zaidi ya watalii 45,000 hutamani kupanda kilele cha mlima mrefu Africa, kwa bahati mbaya hofu juu ya usalama wa maisha yao imekua kizuizi kwao kutimiza ndoto hii.”imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

“Mabadiliko chanya sasa yamepatikana kutoka katika huduma za uokoaji zisizo na ufanisi mpaka zenye ubora wa hali ya juu.”alieleza Braun ambaye ni mtaalamu wa kupanda Milima.Alisema mbali na kuwa na Helikopta bora na zenye uwezo wa juu maalumu kwa huduma hiyo ya utafutaji na uokoaji pia ina timu maalumu ya madaktari wa kimataifa na wasaidizi wa kliniki.

“Kampuni hii inaleta usalama katika maana pana zaidi kwa kuanzisha kliniki ya kwanza Afrika maalumu kwa matibabu ya magonjwa yatokanayo na mlima.Kampuni ya Kilimanjaro SAR itahakikisha inaifanya Kilimanjaro kuwa sehemu salama zaidi ya utalii Africa.”alisema Braun.

Kuanza kwa utolewaji wa huduma hiyo kutasaidia sekta ya Utalii nchini kupata suluhu ya Changamoto ya muda mrefu ya utoaji wa msaada wa kitabibu, utafutaji na uokoaji wa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru .

Hivi karibuni kampuni ya Kilimanjaro SAR iliingia makubaliano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi kuanza kutoa huduma za kitabibu kwa wagonjwa watakao pata matatizo wakati wa kupanda Milima hiyo zoezi lililoenda sambamba na uzinduzi wa Kliniki ya kwanza Afrika ya magonjwa yatokanayo na muinuko wa juu.Katika uzinduzi huo mgeni rasmi ,Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba alisema hii ni fursa mpya kwa sekta ya Utalii kuutangaza vyema Mlima Kilimanjaro kwamba kwa kiasi kikubwa itasaidia katika kuongeza idadi ya Watalii. 

Hata hivyo kuanza kwa huduma hiyo muhimu kwa sekta ya Utalii nchini ,bado ipo changamoto ya matumizi ya uwanja mdogo wa ndege wa Moshi hali inayowalazimu kutumia uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).
Moja ya ndege aina ya Helkopta ilipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya utoaji wa Huduma ya Utafutaji na uokoaji kwa wapanda Milima
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR ya mkoani Kilimanjaro Ivan Broun akionekana mwenye tabasamu mara baada ya moja ya ndege aina ya Helkopta kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya utoaji wa Huduma ya Utafutaji na uokoaji kwa wapanda Milima.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 12 katika ajali huko Igunga Tabora


DC RUANGWA AWATAKA WAKURUGENZI KUSIMAMIA MATUMIZI YA FEDHA ZA MISITU

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Joseph Mkirikiti, amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Lindi kusimamia na kuhakikisha Maafisa Misitu wanaandaa mpango kazi na kuwasilisha taarifa ya matumizi ya fedha ambazo wamepokea na kuzifanyia kazi kutoka kwa Mfuko wa Misitu Tanzania( TaFF). 

Mkirikiti amesema hatua hiyo itaziwezesha Halmashauri kurejeshewa fedha kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za upandaji miti kwa mwaka wa fedha 2017/2018. 

” Fedha hizo zinazopaswa kurejeshwa katika Halmashauri ni zinazotoka na wafanyabiashara wa mazao ya misitu ambapo wanapaswa kulipa tozo ya asilimia 5 ya makusanyo kutoka misitu ya asili kwa ajili ya kugharamia shughuli ya upandaji miti Wilayani” amesema Mkirikiti. 

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa muongozo huo wa uvunaji na biashara ya mazao ya misitu, tozo ya asilimia tano ya fedha za upandaji miti inatozwa kwenye mazao ya misitu kama vile kuni, mkaa, magogo, na nguzo.

“Kuna fedha ambazo zinapaswa kurudishwa katika halmashauri zetu kwa ajili ya kuratibu shughuli hizi ila watu mnaohusika mnafanya uzembe wa kutokutekeleza majukumu yenu ,Wakurugenzi msiwafumbie macho hawa watu wanaotaka kuturudisha nyuma, Kila mtumishi wa serikali azingatie majukumu yake na hakikisheni hizo fedha kwa Halmashauri ambazo hamjazipata watu wenu wawasilishe vitu vinavyotakiwa ili zipatikane” amesema Mkirikiti.

Naye Mtendaji wa mradi Usimamizi Shirika rasimali za uvuvi Thomas Chale amesema shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), watashirikiana na viongozi kuhakikisha mazingira ya Mkoa wa Lindi na Wilaya zake yanatunzwa kama inavyopaswa. 
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Joseph Mkirikiti akishiriki katika zoezi la kupanda Miti

TUTASALIA LIGI KUU MSIMU UJAO - KOCHA NJOMBE MJI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kocha Msaidizi wa kikosi cha Njombe Mji Mrange Kabange amesema kuwa bado wana nafasi ya kuendelea kusalia ligi kuu hata baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba hapo jana.

Njombe Mji walishindwa kutamba kwenye uwanja wa Sabasaba baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa wekundu wa Msimbazi Simba magoli yote yakifungwa na John Bocco.

Baada ya kipigo hicho, Njombe Mji wamesalia katika nafasi ya 15 wakiwa na alama 18 nyuma ya Majimaji inayoshika mkia.

Kocha huyo amesema kuwa, bado wana michezo nane ambapo kama watafaniliwa kuondoka na ushindi wanauwezo wa kuendelea kusalia katika ligi kuu msimu ujao.

"Bado tuna nafasi kuendelea kusalia ligi kuu msimu ujao, tuna michezo nane ambapo mipango yetu ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwenye mechi hizo na tunaamini tunabaki kwani kikosi changu kina uwezo,"amesema Kabange.

"Kikosi changu kina wachezaji wazuri na wanauwezo wa kukupa matokeo, katika mchezo wa jana hatukuwa vizuri ila mechi zilizobaki tutapambana kufa na kupona kupata matokeo mazuri,"

Njombe Mji ilifanikiwa kupanda ligi kuu msimu wa mwaka 2017/2018 na wameonekana kusuasua hususani raundi ya pili lakini walifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup na kuondolewa na Stand United.

MBUNGE CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO

$
0
0
Mbunge wa Tarime Vijijini, kupitia tiketi ya Chama cha Maendeleo Chadema, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu kujibu mashtaka ya kufanyaka mkusanyiko/maandamano yasiyo halali yenye vurugu na uchochezi wa chuki kinyume na sheria.

Heche anafanya jumla ya viongozi wa Chadema wanaoshtakiwa mahakamani hapo kwa makosa kama hayo ni kufikia nane ambao ni Washtakiwa hao ni Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika,Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko na Katibu wa chama hicho Dk Vicenti Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Akisomewa hati ya mashtaka na wakili wa Serikali Mwandamizi Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri imedaiwa, Februari 16,2018, katika barabara ya Kawawa Mkwajuni wilayani Kinondoni Dar es Salaam.

Mshtakiwa akiwa na vingozi wenzake hao walikusanyika kutekeleza lengo la pamoja waliendelea katika mkusanyiko huo na kufanya watu waogope kwamba watakwenda kusababisha uvunjifu wa amani.

Pia wanadaiwa February 16, 2018 katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni Dar es Salaam, wakiwa wamekusanyika wao na wenzao 12 ambao hawajafikishwa mahakamani, wakiwa kwenye maandamano na pasipo kuzingatia agizo lililotolewa na afisa polisi Gerald Ngiichi waligoma na kuendelea na maandamano na kusababisha kifo cha Aquilina Akwiline na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi waliumia kutokana na mkusanyiko huo.

Aidha Heche anadaiwa kuwa, siku hiyo katika viwanja vya Buibui vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam akiwa anahutubia wananchi na wakazi wa eneo hilo katika mkutano wa Hadhara alitoa matamshi ambayo yalielekea kuleta chuki na manung'uniko miongoni mwa wananchi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Hata hivyo mshtakiwa amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana. Na kesi imeahirishwa hadi Aprili 16 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya washtakiwa wote kusomewa Maelezo ya awali.
 
 Mbunge wa Tarime Vijijini, kupitia tiketi ya Chama cha Maendeleo Chadema, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu kujibu mashtaka ya kufanyaka mkusanyiko/maandamano yasiyo halali yenye vurugu na uchochezi wa chuki kinyume na sheria.

Rais Magufuli kuzindua Nyumba za Polisi Arusha ,April 7

$
0
0
Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pohn Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa nyumba za polisi na vituo vya polisi Jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi jijini hapa DCP Charles Mkumbo amesema kuwa kutakuwa na uzinduzi wa vituo viwili cha Utalii na Diplomasia na kingine ni Kituo cha daraja la kati kilichopo Murieti Jijini Arusha.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa kutakuwepo pia na maonyesho mbalimbali ya  Jeshi la Polisi linavyofanya kazi za kuwahudumia wananchi ambapo maonesho hayo yatafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid .

Amewataka wananchi kutokuwa na hofu kwani hali ya usalama Jijini hapa umeimarishwa na amewaomba wajitokeze kwa wingi katika sherehe hizo.
Kituo chaPolisi cha Utalii na Diplomasia kinachotarajiwa kuzinduliwa April 7 Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.

Baadhi ya Nyumba za Polisi zinazotarajiwa kuzinduliwa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli

DICKSON JOB ASAINI MKATABA MPYA MTIBWA SUGER

$
0
0
Na Zaynab Nyamka, Globu ya Jamii.

Beki wa timu ya taifa ya vijana  chini ya miaka 20 na timu ya Mtibwa Sugar, Dickson Job amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom.

Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur amesema kuwa  katika kusaini mkataba huo mpya Job alikuwa  Sambamba  na kaka yake anayetambulika kwa jina George Job kwa sababu yeye mwenyewe hajafikisha umri wa miaka 18.

Swabur amesema kuwa hii ni kawaida kwa timu yao kuwa na vijana wengi sana na hasa ukizingatia waliweza kuwa na Job kwaa muda kidogo kwahiyo wameonelea bora wampe mkataba kamili kwa ajili ya kuwa nae katika kupindi hiki ili awezw kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

 Ameendelea kusema kuwa Mtibwa Sugar inaendeleza sera zake za kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka chipukizi nchini kwa kumpa mkataba mzuri Job.

“Huu ndiyo umekuwa utamaduni wa Mtibwa kwa miaka mingi, kuchukua wachezaji wakiwa vijana wadogo na kuja kuuwalea huku. Nasi tunaahidi kuuendeleza, hatutaishia hapa Kwa Job tu, hivi karibuni mtasikia zaidi,”alisema Swabur. 

Kwaa upande wa mchezaji mwenyewe, Job amesema kuwa amefurahi kuongeza mkataba na wakata miwa hao wa manungu cha zaidi anaahidi kufanya kazi ili aweza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwani anaamini ana uwezo huo.

Job alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za Afrika (AFCON U17) nchini Gabon Mei mwaka jana na kwa sasa amepandishwa kwenye kikosi cha U20, Ngorongoro kinachoshiriki mechi za kufuzu AFCON U20 mwakani nchini Niger.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images