Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

BAADA YA TAMASHA LA PASAKA KURINDIMA JIJINI MWANZA,SIMIYU SASA ZAMU YA WAKAZI WA DODOMA JUMAPILI HII.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akizungumza na Wakazi wa Bariadi waliojitokeza kwenye tamasha la Pasaka lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu.Tamasha hilo lilianzia mkoani Mwanza na baadaye kufanyika simiyu na jumapili hii ndani ya mkoa wa Dodoma katika uwanja wa Jamuhuri.Tamasha hilo linaandaliwa na  kampuni ya Msama Promotions Ltd  likiongozwa na Mkurugenzi wake Alex Msama.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka akitambulishwa jukwaani mbele ya wapenzi wa muziki wa Injili (hawapo pichani) akiwa pamoja na baadhi ya vongozi wa wilaya ya Bariadi,mkoani Simiyu katika tamasha la Pasaka lililofanyika Jumatatu ya Pasaka katika uwanja wa Halmashauri Mjini  humo.
Baadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakifuatilia yaliyokuwa yakifanyika kwenye jukwaa la tamasha hilo.
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba kibao chake kipya cha “Lazima Wakae” huku akicheza na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka ndani ya Jumatatu ya Pasaka,katika uwanja wa Halmashauri Mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Kwaya ya Vijana KKKT-Kimanga wakiimba mbele ya wakazi wa mji wa Bariadi katika uwanja wa Halmashauri,siku ya jumatatu ya pasaka.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Joshua Mlelwa akiimba mbele ya mashabiki wake ndani ya uwanja wa Halmashauri mjini Baridi,ndani ya jumatatu ya Pasaka mkoani Simiyu.
Mwimbaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu Sifaeli Mwabuka akiwaimbisha washabiki wake mapema mwishoni mwa wiki jumatatu ya pasaka ndani ya uwanja wa Halmashauri mjini Bariasi mkoani Simiyu.Tamasha hilo lilianzia mkoani Mwanza na baadaye kufanyika simiyu na jumapili hii ndani ya mkoa wa Dodoma katika uwanaja wa Jamuhuri.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KITUO CHA DALADALA JAMATINI KUENDELEA KUTUMIKA, MABASI YA MIKOANI YAONYWA

$
0
0
Na Ramadhani Juma,Ofisi ya Mkurugenzi

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameelekeza matumizi ya kilichokuwa kituo Kikuu cha Mabasi madogo maarufu kama Daladala cha Jamatini Mjini Dodoma kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria wanaotoka katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo yaendelee kama kawaida wakati Manispaa ikiandaa eneo mbadala.

Mkuu huyo wa Mkoa pia ameagiza ‘ruti’ za Daladala zifupishwe kama ilivyokuwa awali, na kwamba upangaji wa ‘ruti’ ndefu ujadiliwe upya na wadau wote wanaohusika na endapo utakubaliwa na wengi ndipo utekelezaji wake uanze.Dokta Mahenge ametoa maelekezo hayo leo Aprili 3, 2018, alipokuwa akizungumza na wadau wa usafirishaji katika kituo kikuu cha mabasi ya Mikoani cha muda kilichopo Nanenane Manispaa ya Dodoma baada ya kituo hicho kufungwa wiki iliyopita kwa ajili ya kupisha mradi wa Reli ya Kisasa.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya majadiliano na wadau wote ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMTRA), Manispaa, Jeshi la Polisi, na Shirika la Reli ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, na kwamba matumizi ya stendi hiyo yataendelea kwa muda wa miezi miwili kuanzia sasa, kipindi ambacho Manispaa itatakiwa kuwa imeshapata na kuandaa stendi mbadala.

Akizungumza katika eneo la tukio, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alisema Manispaa imepokea maagizo yote na itahakikisha inaandaa eneo kwa ajili ya Stendi ya Mabasi madogo Mjini katika kipindi cha miezi miwili kama ilivyoelekezwa na Mkuu wa Mkoa.Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza mabasi yote yanayosafirisha abiria Mikoa mbalimbali Nchini kupakia na kuanzia safari zao katika kituo Kikuu cha mabasi ya muda kilichopo Nanenane na Kampuni itakayokiuka itachukuliwa hatua kali za Kisheria.

“Namuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani wa Mkoa kuwa, kuanzia kesho mabasi yote yauze tiketi na kuanza safari zao hapa katika kituo hiki Kikuu cha mabasi cha muda cha Nanenane…hakuna Mkubwa wala mdogo katika kutoa huduma kwa Wananchi” alisisitiza Dkt. Mahenge.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na wadau wa usafishaji katika Stendi Kuu ya muda Mabasi ya Mikoani iliyopo eneo la Nanenane jana Aprili 3, 2018 alipofanya ziara fupi katika stendi hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akifafanua jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge alipozungumza na wadau wa usafishaji katika Stendi Kuu ya muda ya Mabasi ya Mikoani iliyopo eneo la Nanenane jana Aprili 3, 2018 alipofanya ziara fupi katika stendi hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (katikati) akifafanua jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) alipofanya ziara fupi kukagua maeneo yanayoweza kuwekewa miundombinu muhimu na kutumika kama kituo cha daladala cha Mjini, jana Aprili 3, 2018. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Mhandisi Ludigija Ndwata. 

Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi Kupunguza Majanga Yatokanayo na Athari za Mabadiliko Hayo

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma

Makubaliano ya Paris chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa mabadiliko ya Tabianchi utainufaisha nchi kwa kuimarika kwa Mipango ya Taifa ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi ili kupunguza majanga yatokanayo na athari hizo.

Hayo yameelezwa Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba wakati akiwasilisha Azimio la Bunge la kuridhia makubaliano ya mkataba huo.

"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka saini makubaliano hayo na hatimaye kuyatekeleza itanufaika na mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha hali ya uchumi wa nchi na kujenga uchumi endelevu wa viwanda wenye kustahimili mabadiliko ya tabianchi," alisema Mhe. Makamba.

Makamba Amesema,  Mkataba huo utaongeza upatikanaji wa fursa zilizopo za miradi na teknolojia safi itakayowezesha matumizi ya gesi asilia majumbani na viwandani ili kuchochea maendeleo ya viwanda kwa kutumia nishati yenye bei nafuu.

Vilevile, utaimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa katika kusimamia na kutekeleza masuala yanayohusu mabadiliko ya tabianchi.

"Makubaliano ya Paris yanalenga kuboresha utekelezaji wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka 1992 kwa  kutunza misitu inayonyonya joto, kuandaa na kutekeleza mipango ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi na kuwa na mifumo ya upatikanaji wa fedha na teknolojia safi kwa nchi zinazoendelea ili kukabiliana na changamoto ya tabianchi," alifafanua Mhe. Makamba.

Aidha amesema, kwa kuzingatia manufaa yatokanayo na Mkataba huo pamoja na itifaki yake kwa Tanzania na pia umuhimu na manufaa ya makubaliano hayo, Bunge katika Mkutano wake wa Kumi na Moja na kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, linaazimia kuridhia makubaliano ya Paris kuhusu kuboresha utekelezaji wa Mkataba wa mabadiliko ya Tabianchi yaani "THE PARIS AGREEMENT UNDER THE UN FRAMEWORK CONVENTIN ON CLIMATE CHANGE".

Ujenzi wa Vivuko Barabara ya Lamelock - Loltepes - Sunya wapigwa "Stop"

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kushoto) akikagua ujenzi wa Vivuko katika barabara ya Namelock-Loltepes- Sunya yenye urefu wa Km 88 iliyopo katika Wilaya ya Kiteto.

Nteghenjwa Hosseah, Kiteto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesimamisha ujenzi wa vivuko vyote katika ujenzi wa barabara ya Namelock-Loltepes Sunya yenye urefu wa Km 88.1 inayojengwa katika Wilaya ya Kiteto na Mkandarasi Deniko Constraction Ltd.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo mapema jana wakati wa ziara yake Wilayani humo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kubaini mapungufu makubwa katika ujenzi wa vivuko zaidi ya kumi alivyovipitia ndipo alipoagiza kusitisha ujenzi huo mara moja hadi hapo Wataalamu wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) watakapofika kukagua barabara ma kuwasilisha ripoti.

Aidha kutokana na hali hiyo ya aligiza Mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa barabara hiyo Deniko Construction sambamba na Mhandisi Mshauri Luptain Consult Ltd, Mhandisi Consulting Engineers pamoja na ACE Consultant kufika Ofisini kwake mara moja kutoa maelezo ya kina ya mapungufu hayo yaliyojitokeza katika ujennzi wa barabara hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kulia) akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Vivuko katika barabara Namelock-Sunya wakati wa ziara yake Wilayani Kiteto.

“Ni mara ya tatu sasa nakuja kukagua Barabara hii na kila mara nabaini changamoto tofauti sjui kuna tatizo gani nahitaji kusikia zaidi kutoka kwa wataalamu wa pande zote ili tutafute suluhisho kwa pamoja”Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa hapo awali Barabara hii iligawanywa kwa wakandarasi wajenzi wawili ambaye ni huyu Deniko alikuwa anajenga upande mmoja wenye Km 44 na Km 44 zilizobakia alipewa Maginga Construction ambaye alishindwa kabisa kazi hii ndipo nilipoagiza taratibu zifuatwe ili kuvunja mkataba wa awali na kazi ile apewe Mkandarasi mwingine.

“Kazi hiyo aliongezewa Deniko Construction ambaye kwa sasa ndiye anayejengwa barabara hii yote yenye Km 88. Hapo awali kazi yake ilionekana nzuri sana na ya kuridhisha lakini baada ya mvua za msimu huu mapungufu makubwa yamebainika hasa katika vivuko vyote vilivyojengwa haviendani na mahitaji ya barabara hii” Alisema Jafo.
Huu ni muonekano wa baadhi ya Kivuko kinachojengwa katika barabara ya Namelock – Loltepes – Sunya ambavyo Waziri Jafo amesimamisha ujenzi wake kutokana na dosari zilizojitokeza.

Naye Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Kiteto Elias Paul alisema kuwa tatizo lililobainika katika ujenzi wa vivuko hivyo ni Vivuko hivyo haviendani na wingi wa maji ya maji yanayopita na vipenyo vya vivuko ni vidogo hivyo havina uwezo wa kuhimili maji na takataka zingine zinazotakiwa kupita hapo na ni rahis sana kuziba na hata kivuko chote kubebwa na maji ndani ya kipindi kifupi.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Nmelock – Loltepes – Sunya unatekelezwa na Serikali kupitia Fedha za wafadhili kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) chini ya mpango wa (FEED FOR FUTURE) unaotekelezwa katika Wilaya Nne Nchini ambazo ni Kilombero, Mvomero, Kongwa na Kiteto.

Wilaya ya Kiteto kupitia kwa Wakala wa Babarabara za Mijini na Vijiji (TARURA) inahudumia mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa Km 1,088.35 kati ya barabara hizo km 2.8 ni za Lami, Changarawe Km 132 na Udongo Km 955.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kulia) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Namelock – Loltepes – Sunya yenye urefu wa Km 88 wakati wa ziara yake Wilayani Kiteto.

WAKUU WA IDARA NA VITENGO WASHIRIKI UJENZI UWANJA WA MPIRA RUANGWA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue, ameitaka Menejimeti ya Halmashauri hiyo kutoa ushirikiano wa kusimamia ujengaji wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira. 

Chezue amesema hayo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri wakati akiongea na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri hiyo.

 “Kuna wakuu wa idara na vitengo wanaingia moja kwa moja kutokana na idara zao msisubiri kuambiwa fanya kitu Fulani jitume na washirikishe waliochini yako ili kufanikisha lengo hili kwani uwanja huo ni wa Halmashauri na si Mkurugenzi pekee yake ”Amesema Chezue. 

Aidha Mkurugenzi amesema uwanja huo utakuwa ni chanzo cha mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kutokana na kukodisha Hostel, kukodisha vibanda vya biashara na viingilio vya milangoni. Pia kuinua kipato cha wajasiriamali ambao watapata fursa ya kufanya biashara wakati wa michezo, na jamii itapata fursa ya kuziona timu mbalimbali. 

Vilevile amesema lengo la kujenga uwanja huu ni kuibua na kukuza vipaji vya vijana wa Ruangwa kwenye michezo mbalimbali ili kuweza kupata ajira kwani michezo kwa sasa ni ajira. “Uwanja huo utatumika kwa michezo ya kitaifa na kimataifa kwasababu vipimo vyake ni vya kimataifa”Amesema Chezue. Naye Afisa Michezo wa Wilaya Simon Mwambe amesema kwasasa kazi zinaendelea wameishapeleka mchanga kwa ajili ya kufyatua tofali za kujengea ukuta katika uwanja huo. 

“Tumeisha chimba msingi wa kujenga ukuta, tuna cement za kutosha na maji yapo tumefunga pampu kwenye kisima kilichochimbwa uwanjani hapo na kesho zoezi la kufyatua tofali litaanza” amesema Mwambe. Hata hivyo Afisa Michezo amesema suala la kuazima vitendea kazi kwa watu binafsi linasababisha kazi zisimame kwa sababu wakati vifaa vinaenda kukodiwa na muhusika anakuwa amekodisha au anatumia kwa shughuli zake.

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI - WASOMI, WAZAWA NA WAPENDA MAENDELEO WAUNGANA KUJENGA ZAHANATI BUTATA

$
0
0
Na Verdiana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge

WASOMI na wananchi wapenda maendeleo waishio nje na ndani ya Kijiji cha Butata wameungana pamoja ili kufanikisha ujenzi wa zahanati katika kijiji chao ili kuondoa adha kubwa ya ukosefu wa huduma za kiafaya kijijini hapo.

Awali akizungumza na Msaidizi wa Mbunge ambae ni mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Butata Ndugu Cleophace M. Kasala ameeleza kuwa Wananchi wa Kijiji cha Butata wamekuwa na muamko katika suala la ujenzi wa zahanati hata kufikia hatua ya kuhamasishana kwa kuchangia nguvu kazi ili kuwaunga mkono ndugu zao waliojitolea kuwachangia mifuko ya saruji na fedha za kujengea zahanati hiyo.

"Wananchi baada ya kupata Wafadhili ambao ni Wazawa wa Kijiji cha Butata wao wamehamasika na kujitolea kuchimba msingi, kusomba mawe, mchanga n.k"

Kwa upande wake Amina Kasaka ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Butata ameeleza kuwa, wao kama akina mama kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu sana katika upatikanaji wa huduma za afya. Ameongezea kuwa hali hiyo imekuwa ikihatarisha maisha ya mama na mtoto na hata wazee.

Naye Diwani wa Kata ya Bukima Mh. January Simula ameeleza mpango kazi wa Kata yake katika ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji. Katika kutekeleza Ilani ya CCM, wamefanikisha kwa vijiji viwili ambapo hadi sasa wana zahanati moja ya Bukima na ya pili wameanza ujenzi wake Kijijini Butata. Pia Serikali ya Kata hiyo imeanza hatua za upanuzi wa Zahanati ya Bukima kuwa Kituo cha Afya cha Kata.

Katika kulifanikisha hilo, Diwani amesema yuko bega kwa bega na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. S. Muhongo kwa hamasa na michango yake kwenye sekta za Afya, Elimu na Kilimo ikiwa ni vipaumbele vya Jimbo la Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge imesema inashirikiana na wananchi wapenda maendeleo wa Kijiji cha Butata kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Picha ya hapo chini inaonyesha ujenzi wa Zahanati ya Butata ikiwa kwenye hatua ya ujenzi wa msingi.

Ofisi ya Mbunge
www.musomavijijini.or.tz

WAJASIRIAMALI VIJANA KUWEZESHWA KUPITIA SHINDANO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
Shirika la Tujenge Tz Innovation limeanzisha mradi kupitia shindano Ubunifu la Tujenge TZ lenye lengo la kuchochea uwezo wa vijana katika kubuni na kuboresha mfumo mzima wa uendeshaji shughuli za ujasiliamali zenye manufaa kwa jamii. Shindano hili litakuwa la wazi na haki kwa wajasiriamali  wote vijana watakaoshiriki kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha cha jamii.

Akizungumza leo Mwanzilishi wa mradi huu ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Unleashed Afrika, Khalila Kellz Mbowe ameeleza kuwa mradi huu umenuia kuongeza uwezekano na ukuaji wa kasi wa biashara zinazoendeshwa na vijana hivyo kuzifanya ziwe na wigo mpana wa kunufaisha jamii.

Aidha ameeleza kuwa washindi watapata fursa ya kipekee ya kuhudhuria mafunzo ya kina ya wiki moja ya kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi yao.

Naye Kadele Mabumba Meneja mradi kwa Tanzania na Uganda wa Hanns Foundation amesema Mradi wa Tujenge Tz Innovation Challenge ni wa kukuza shughuli za ujasiriamali  wenye kuleta manufaa ya kijamii hasa ujasiriamali hapa Tanzania.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa True Maisha, Erick Chrispin  amesema mradi huu unalenga kuongeza ubora wa manufaa ya jamii yanayotokana na shughuli  za kijasiriamali katika maeneo yao.

Mradi huu umeanzishwa ili kuchochea uwezo wa vijana katika kubuni na kuboresha mfumo mzima wa uendeshaji shughuli za ujasiriamali zenye manufaa kwa jamii.
Shindano hilo litaendeshwa sambamba na kampuni ya Unleashed Afrika, True Maisha pamoja na shirika la Kijerumani la Hanns Seidel Foundation.
 Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Unleashed Africa, Khalila Mbowe(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shindano wajasiriamali vijana lililozinduliwa leo kwa ajili ya kuinua vijana kiuchumi hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Julia Berger
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya True Maisha, Erick Chrispin akizungumza na waandishi wa habari kuhusu watakavyosimamia shindano hilo kwa kutoa mafunzo kwa washindi watakaopatikana mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo lililozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mradi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Kadele Mabumba.
 Meneja Mradi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Kadele Mabumba(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyojipanga kutekeleza shindano la wajasiliamali vijana. Kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya True Maisha, Erick Chrispin na kushoto ni  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Julia Berger
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Hunus Seidel - Tanzania na Uganda, Julia Berger akibonyeza kitufe kuashiria ufunguzi wa shindano la wajasilamali vijana kwa mkoa wa Dar es Salaam watakaoshiriki kupitia tovuti ya  www.tujengetzchallenge.co.tz.

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TAWLA CHAKUTANA NA WADAU KUJADILI MABORESHO YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

$
0
0
Kikosi cha Usalama barabarani kimesema sheria zilizopitwa na wakati zimetajwa kuwa chanzo cha ajari za barabarani nchini hivyo zinatakiwa zifanyiwe marekebisho.

Mkuu wa Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Marison Mwakyoma alipokutana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA) ili kujadili mapendekezo ya mabadiliko na maboresho ya sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973. Amesema sheria ya usalama barabarani ilitungwa mwaka 1973na kufanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambayo ni ya muda mrefu ukilinganisha na mabadiliko yaliyopo ikiwemo magari kuongezeka pamoja na watu.

Mwakyoma alisema sheria ya mwaka 1973 ikibadilishwa itaweza kupunguza ajali za barabarani alitolea mfano ukisoma sheria ya kufunga mkanda hakuna sheria haijamzungumzia abiria kama afunge mkanda na haimlazimishi imuadhibu kwa sheria gani.
 
 Pia kwa upande wa magari madogo sheria inasema anayetakiwa kufunga mkanda ni dereva na abiria aliyepanda mbele lakini aliyepanda nyuma haionyeshi kwenye sheria anatakiwa afunge mkanda Mwakyoma alisema abiria wanaopanda basi ambalo limejaa bado wanaengia kusimama hakuna sheria inaonyesha yule aliyesimama adhibiwe.

Hivyo sheria hiyo ikirekebishwa na kuwekwa adhabu inayoendana na kosa husika watu wataogopa kuvunja sheria za usalama barabarani na itasaidia kupunguza ajari zinazoendelea kutokea. Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA),Isabella Nchimbi alisema utafiti waliofanya walibaini kuwa mapungufu katika sheria ya usalama barabarani vinavyosababisha ajali nyingi ikiwemo dereva kutumia simu ya mkononi wakati anaendesha gari akiwa barabarani. Mapungufu mengine uvaaji wa kofia ngumu kwa dereva na abiria wa pikipiki,uvaaji wa mikanda wakati ukiwa kwenye gari,kuendesha mwendo kasi na matumizi ya uvukaji kwenye vivuko . 
Mkuu wa Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Marison Mwakyoma akiongea na washiriki katika semeina ya kujadili sheria za usalama barabarani
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA), Bi Isabella Nchimbi akiwasilisha hutuba ya ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria za usalama barabarani.
Picha ya pamoja
 

UJIO WA NDEGE ZA SERIKALI KUONGEZA MAPATO,HUDUMA ZA USAFIRI WA ANGA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Ujio wa ndege za serikali kutaongeza huduma ya usafiri wa anga,mapato ya serikali pamoja na wananchi kuona huduma ya usafiri wa anga sio anasa kama ilivyokuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu.

Hayo ameyesema leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA),Richard Mayongela wakati akizungumza na Michuzi Media, amesema kuwa katika kwenda na uchumi wa viwanda ni lazima kuwepo kwa viwanja bora vya ndege katika kurahisisha usafiri mali ghafi pamoja na abiria.

Amesema kuwa viwanja vyote vya ndege vinaboreshwa kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri wa anga katika mikoa mbalimbali ambapo ndege zinazonunuliwa zitatumika katika safari za mikoa hiyo.Mayongela amesema kuwa fedha zinazotumika kujenga viwanja hivyo ni za watanzania kutokana na nguvu ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika ukarabati wa viwanja ili kuweza kutoa huduma bora katika usafiri.

“Mapinduzi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli anayoyafanya katika sekta ya usafiri wa anga kwa kununua ndege baadhi ya watu hawawezi kujua faida lakini watajua baada ya muda mfupi kutokana na ajira katika viwanja vya ndege pamoja na usafirishaji wa haraka wa bidhaa ambazo zinaharibika kwa muda mfupi kwenda kuuza nje ya nchi”amesema Mayongela.

Amesema katika viwanja vya ndege watajenga sehemu za kuhifadhi bidhaa ambazo zinaharibika katika kipindi kifupi ikiwa ni kuwafanya wafanyabiashara kuwa na uhakika bidhaa hizo katika kusafirisha kwenda nje ya nchi kwa ajili soko.Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo amesema katika kipindi hiki hakuna kulala ikiwa nia ya kumsaidia Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati wenye maisha bora ya watanzania.

“Kazi yetu mamlaka ni kusimamia huduma ya usafiri kwa kujenga viwanja vya kisasa ili ndege zinazotumia viwanja hivi viweze kusukuma maendeleo ya nchi yetu na kama watanzania tunayofanya kazi hizi kuacha alama kwa vizazi vya sasa na vijavyo” amesema Mayongela.Amesema ujenzi wa Rada ni moja ya kuhakikisha hali ya usalama wa usafiri wa anga ina kuwa kwa viwango vya kimataifa ambavyo vimeanishwa katika utoaji wa huduma za ndege.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Richard Mayongela akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na masuala mbalimbali katika usimamizi wa viwanja vya ndege nchini,(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Richard Mayongela akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana na masuala mbalimbali katika usimamizi wa viwanja vya ndege nchini, leo jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa sehemu ya uwanja wa Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ndege zikiwa katika uwanja huo .

WAZIRI MKUU AWASILISHA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea kwenye eneo la kuwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018. 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeongeza idadi ya Wakaguzi wa Mazingira kutoka 62 hadi kufikia 512 ili kuimarisha ukaguzi wa masuala ya hifadhi ya mazingira nchini. Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 4, 2018) Bungeni mjini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019 kwenye mkutano wa 11 wa Bunge.

Amesema katika mwaka wa fedha uliopita, jumla ya kaguzi 380 zimefanyika kwenye viwanda kwa lengo la kufanya tathmini za mazingira pamoja na kutoa elimu na uelewa kuhusu uendeshaji endelevu wa viwanda unaozingatia utunzaji bora wa mazingira.

“Kama nilivyoeleza katika Mkutano wa Kumi wa Bunge hili, halmashauri zote nchini zinapaswa ziweke mpango mahsusi wa kuhifadhi mazingira unaojumuisha kupanda na kutunza miti. Serikali itaweka utaratibu wa upimaji wa utendaji wa wakuu wote wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri unaozingatia uendelezaji na utunzaji wa mazingira katika maeneo yao,” alisisitiza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua hotuba   kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali inachukua hatua madhubuti za kuendeleza ardhi kutokana na umuhimu wake kama kitovu cha uzalishaji mali. Alizitaja hatua hizo kuwa ni kutekeleza mpango kabambe wa majiji, manispaa na miji; kudhibiti migogoro baina ya watumiaji wa ardhi na kuimarisha mfumo unganishi wa kuhifadhi kumbukumbu za ardhi nchini.

“Napenda kulijulisha Bunge lako tukufu kwamba Mipango Kabambe ya Manispaa za Iringa, Singida na Mji wa Kibaha imekamilika na mipango mingine 20 ipo katika hatua mbalimbali za uandaaji. Hadi sasa, michoro 1,110 ya mipango miji imeshaidhinishwa kati ya 1,148 iliyopokelewa kutoka Halmashauri za miji mbalimbali,” alisema.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wote wanapofanya shughuli za maendeleo, wazingatie mipango kabambe inayoandaliwa na mamlaka za upangaji miji kwenye maeneo yao husika. Alisema Serikali imechukua hatua kadhaa za kukabiliana na changamoto ya migogoro ya ardhi miongoni mwa watumiaji ikiwemo migogoro ya mipaka ya vijiji, wakulima na wafugaji, wanavijiji na hifadhi na mapori ya akiba.
 Baadhi ya wakuu wa Taasisi zilizoko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa wakati alipowasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018.

“Moja ya hatua zilizochukuliwa ni kuunda timu ya kisekta ya kushughulikia migogoro ya ardhi ambayo imetembelea mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Morogoro na Tabora na kufanya majadiliano na wadau 1,106. Hatua mbalimbali za utatuzi wa migogoro ya ardhi zinaendelea kuchukuliwa.”

Kuhusu utendaji wa bandari nchini, Waziri Mkuu alisema Serikali imeendelea kuboresha Bandari ya Dar es Salaam ili kuifanya Tanzania iwe kitovu cha usafiri wa majini. Alisema uboreshaji huo utaanza na gati namba moja hadi saba; kuongeza kina na upana wa lango la kuingilia meli na eneo la kugeuzia meli; kuimarisha mtandao wa reli bandarini pamoja na kujenga gati maalumu la kuhudumia meli za magari.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba  baada ya kuwasilisha hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2018. 

“Vilevile, Mamlaka ya Bandari Tanzania imefungua ofisi katika baadhi ya nchi jirani kwa lengo la kuongeza urahisi wa kutoa huduma. Katika mwaka 2018/2019, Serikali itaendelea na uboreshaji wa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara,” alisema.

“Serikali itatekeleza mradi wa dirisha moja la forodha (Tanzania Electronic Single Window System-eSWS) ili kuwaweka pamoja wadau wote wa kuondosha shehena bandarini na mipakani. Kukamilika kwa mradi huo, kutarahisisha na kupunguza muda na gharama za utoaji na upitishaji wa shehena bandarini,” alisema Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umejumuisha ujenzi wa mtandao wa miundombinu ya itifaki (Internet Protocol – Multiplier Label Switching) pamoja na ujenzi wa kituo cha kuhifadhi data ambacho hadi sasa mifumo ya taasisi 27 imeunganishwa ukiwemo mfumo wa ukusanyaji mapato wa TRA.

“Kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaongeza usalama, usiri wa data, kujikinga na majanga na kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali na muingiliano wa mifumo katika Kituo cha Data cha Taifa na vituo vingine vitakavyojengwa nchini,” alisema.

Kuhusu huduma ya mawasiliano vijijini, Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ambapo vijiji 1,921 vimepatiwa huduma hiyo. “Serikali imeimarisha huduma za simu na intaneti katika taasisi za umma zikiwemo shule, vituo vya afya, vituo vya polisi na ofisi za posta.


“Katika mwaka 2018/2019, Serikali itaendelea kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kupanua matumizi yake hadi katika ngazi ya wilaya na kuzisimamia kampuni za simu nchini ili ziweze kutoa kumbukumbu sahihi kwa lengo la kukokotoa mapato yatokanayo na malipo ya huduma za simu za kitaifa na kimataifa,” alisema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi kwenye viwanja vya Bunge Mini Dodoma baada ya hotuba  kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya  fedha  za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2018/2019, bungeni mini Dodoma Aprili 4, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mkutano wa Wadau wenye nia ya Kuwekeza Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba wafanyika leo jijini Dar

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau leo jijini Dar es Salaam. 
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau hao leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akitoa taarifa ya hali ya soko la dawa nchini kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau hao jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Appolinary Kamuhabwa akisisitiza jambo kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau hao  leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Geofrey Mwambe akielezea vivutio vya uwekezaji katika viwanda vya dawa nchini kwa wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini, leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wa mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini wakimsikiliza Mgeni rasmi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa wadau hao leo jijini Dar es Salaam.

SERIKALI KUTOSITISHA MKATABA WA KAMPUNI YA CHAI MARUKU

$
0
0
Serikali imesema kuwa haitasitisha mkataba na Mwekezaji wa Kampuni ya Chai Maruku, iliyoko mkoani Kagera, kwa sababu mgogoro wa malipo uliopo baina ya  kampuni hiyo na wakulima pamoja na wafanyakazi wake unaelekea kutatuliwa.

Hayo yameelezwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Bukoba Vijijini Mhe. Jason Rweikiza (CCM), aliyetaka kujua sababu za Serikali kutovunja mkataba na mwekezaji huyo na kurejesha umiliki kwa Serikali au kwa mwekezaji mwingine atakayejali maslahi ya wakulima na wafanyakazi.

Katika swali lake la msingi, Mhe.   Rweikiza alisema kuwa tangu Kampuni hiyo ibinafsishwe kwa mwekezaji, kumekuwa na malalamiko ya wakulima kutolipwa  fedha za mauzo ya chai kwa wakati na wafanyakazi kutolipwa  mishahara na stahiki zao ipasavyo.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, katika kutatua mgogoro huo Serikali kupitia ofisi ya Msajili wa Hazina imekuwa ikifuatilia kwa karibu mwenendo wa utendaji na uendeshaji wa Kampuni hiyo kwa kufanya vikao kwa nyakati tofauti kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera, Bodi ya Chai na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima wadogo wa Chai (TASHTIDA).

Alisema kuwa katika vikao hivyo haki ya kila upande ilizingatiwa ikiwemo suala la haki za wafanyakazi pamoja na madai ya wakulima, ambapo mpaka sasa mwekezaji amekubali kulipa madai ya wakulima kiasi cha Sh. milioni 12 huku wakiendelea kujadili namna ya kutatua suala la madai ya wafanyakazi.

Dkt. Kijaji aliahidi kuwa Serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu suala hilo ili kuhakikisha haki za wakulima na wafanyakazi hazipotei.

Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Mkuu wa  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
4/4/2018

VIDEO: UZINDUZI WA SHINDANO LA CLUB RAHA LEO SHOW 2018 ULIVYOFANA JIJINI DAR ES SALAAM

Mwarobaini Utoaji Huduma za Afya Wapatikana

$
0
0
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Constatine Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Mifumo iliyoborehswa ya Bima ya Afya ya Pamoja (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na wa Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD, (Jazia - Prime Vendors System) leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3. Kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Robert Salim, Meneja Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mkoa wa Mbeya Bw. Gasper Materu na Mwakilishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Nkinda Shekalage. 
 Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Janeth Kibambo akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Mifumo iliyoboreshwa ya Bima ya Afya ya Pamoja (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na wa Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD, (Jazia - Prime Vendors System) leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.
 Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Bi. Nkinda Shekalage akifafanua juu ya madhumuni ya mafunzo ya siku tano kuhusu mifumo iliyoboreshwa ya Bima ya Afya ya Pamoja (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD, (Jazia - Prime Vendors System) leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu mifumo iliyoboreshwa ya Bima ya Afya ya Pamoja (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD, (Jazia - Prime Vendors System) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.
Baadhi ya wawezeshaji wa mafunzo ya siku tano kuhusu mifumo iliyoboreshwa ya Bima ya Afya ya Pamoja (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD(Jazia - Prime Vendors System) wakijadiliana jambo mara baada ya uzinduzi rasmi wa mafuynzo hayo leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO, Mbeya.)

WAUGUZI,WAKUNGA WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI SEHEMU ZAO ZA KAZI.

$
0
0

 NA WAMJW-DODOMA.
 
Serikali imewataka Wauguzi na Wakunga nchini kufuata na kusimamia misingi ya maadili ya taaluma zao wakati wa kutoa huduma.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini.

Najua kuwa Idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga inalishughulikia suala la maadili kwa wauguzi na wakunga hivyo nitoe msisitizo tena huduma za Uuguzi na Ukunga zinapimwa zaidi na uadilifu wa mtoa huduma hivyo muendelee kusimamia kwa ukaribu misingi ya maadili ya taaluma zenu amesema Dkt Ndugulile.

Aidha, Dkt Ndugulile amewataka Wauguzi na Wakunga kupitia vyama vyao vya kitaaluma kushirikiana na Baraza la Uuguzi na Ukunga kuendelea kuwakumbusha mara kwa mara wauguzi kuhusu maadili ya taaluma yenu.

Mteja anapokuja kwenye vituo vya kutolea huduma anategemea kupata huduma ya upendo na huruma, anategemea kupewa maneno ya faraja na matumaini hivyo basi, wale wote wanaoichafua taaluma yenu kwa kutotekeleza wajibu wao kwa wakati, kuwadhalilisha, kuwashambulia au kutowasikiliza wateja wenu wabainishwe na wahimizwe kujirekebishaamefafanua Dkt Ndugulile.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau,wakunga na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wauguzi na wakunga hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi vyeti vya kufanya vizuri baadhi ya wawakilishi wa  mashirika yanayoshirikiana na Wizara ya Afya wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 Baadhi ya Wauguzi na Wakunga wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bw. Gustav Moyo akiongea na wauguzi na wakunga hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.

 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha uuguzi na Ukunga Dodoma wakiwakilisha salamu zao kwa kutumia wimbo kwa  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.PICHA NA WIZARA YA AFYA DODOMA.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Ecobank mobile app reaches 4 million users milestone

$
0
0
Ecobank Group CEO, Ade Ayeyemi
The upgraded version of Ecobank’s revolutionary mobile app has attracted 3 million new customers in just 6 months, taking the total number of users to 4 million.

The app builds on the core functionality that saw the original version applauded as a game changer for African banking by using digital technology to combat many of the financial inclusion barriers faced by those on the continent. This includes the dearth of rural branches, affordability of products, high transaction costs and minimum opening balance requirements.

Ade Ayeyemi, Ecobank Group CEO, says Ecobank’s strategic mission is built around using mobile banking to deliver innovative, efficient and cost-effective services to those who have typically sat outside of the formal economy, and therefore goes far beyond the reach of the traditional branch and ATM networks. Subsequently, while the app won one million customers in its first year of launch, upgraded features have seen the rate of sign-ups treble in half of the time.

So far this year, app usage has been growing at an average 700k new customers per month. “Customers can use the app on their mobile to instantly open Ecobank Xpress AccountTM, which doesn’t have any account fees, paperwork or minimum balance requirements, or to send and receive money across 33 African countries,” he explains. 

“Therefore, our app not only removes the barriers that have financially excluded so many Africans but offers next generation functionality to help them send money, make withdrawals or pay for goods and services.”


Patrick Akinwuntan, Ecobank’s Group Executive, Consumer Banking, says that Ecobank is committed to providing all Africans with access to financial services, but doing so in a way that conjoins functionality with convenient, accessible and efficient banking channels, such as the rollout of Ecobank Xpress TM Point Agents.


“We want to be the digital bank of choice for all Africans,” he said. “Functionality is one thing – giving our customers unrivalled convenience is another.

The Ecobank Xpress TM Point Agents that can now be found in your local neighbourhood enable you to deposit money into your app-based Ecobank Xpress AccountTM and begin to make digital payments on the app using Ecobankpay.

You can also withdraw funds in local currency that may have been sent to you from friends or relatives using our innovative instant transfer or Xpress Cash capabilities.”

The Ecobank Mobile App is available for download from the Google Play Store or Apple Store.

RAIS DK.SHEIN ATEMBELEA MPIGADURI NA MARUHUBI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji , Mustafa Aboud Jumbe (Mwenye kipaza sauti) akitoa maelezo kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) wakati wa ziara maalum  Rais alipotembelea Mpigaduri na Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo  kutembelea Eneo  linalotarajiwa  kujengwa  Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China.
 Eneo la ufukwe wa Mpigaduri,Maruhubi  linalotarajiwa  kujengwa  Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, Salama Aboud Twalib wakati alipotembelea Eneo la Mpigaduri na Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea Ufukwe wa Eneo  linalotarajiwa  kujengwa  Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa maelekezo kwa watendaji  wakati alipotembelea Eneo la Mpigaduri na Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea Ufukwe wa Eneo  linalotarajiwa  kujengwa  Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Siara Ubwa Mamboya (wa pili kulia) na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji , Mustafa Aboud Jumbe (Kushoto) alipofika Eneo la fukwe ya Bwawani  wakati wa ziara maalum ya  kutembelea eneo hilo sambamba  na kutembelea Mpigaduri na Maruhubi Eneo  linalotarajiwa  kujengwa  Bandari Mpya ya kisasa itakayojengwa na Kampuni ya Chek kutoka Nchini China.
 ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji,  Mustafa Aboud Jumbe (katikati) alipofika Eneo la fukwe ya Bwawani  wakati wa ziara maalum  alipotembelea  Eneo hilo linalotarajiwa kujengwa  Mji Mpya wa kisasa.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa maelekezo wa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi wakati walipofika eneo hilo.
(Picha na Ikulu)

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWAPA SOMO WATUMISHI WAPYA

$
0
0
Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Doroth Mwanyika amewaasa maafisa wapya  walioajiriwa katika Wizara yake kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wawapo kazini.

Ameyasema hayo wakati alipokutana na watumishi 59 waliopata ajira katika Wizara ya Ardhi wakati wakipewa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na taratibuza utumishi wa umma yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

“Suala la huduma bora katika Taasisi za Serikali limekuwa likisisitizwa sana. Sisi kama watumishi wa Serikali ni lazima tutambue wajibu wetu kwa Umma ambao kimsingi ndio waajiri wetu. Wajibu wetu ni kutoa huduma iliyobora na inayokidhi matarajio ya wateja”. Amesema Mwanyika.

Katibu mkuu huo amewaasa watumishi hao kuzingatia Maadili mema ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma, kutoa Huduma kwa Mteja na Namna ya kushughulikia Malalamiko, Umuhimu wa Utunzaji wa Kumbukumbu.

Aidha, aliwata watumishi hao kuzingatia mafunzo watakayo pata kuhusu namna ya kujikinga na Janga la Ukimwi na Athari zake, Umuhimu wa Kuwajali Wateja na namna ya Kuwahudumia, Maadili ya Utendaji Bora ikiwa ni pamoja na kujiepusha na rushwa kazini.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Doroth Mwanyika akiongea na  watumishi 59 waliopata ajira katika Wizara ya Ardhi wakati wakipewa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na taratibuza utumishi wa umma yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
 Baadhi ya watumishi waliopata ajira katika Wizara ya Ardhi wakati wakipewa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na taratibuza utumishi wa umma yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Katibu Mkuu, Doroth Mwanyika akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wapya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

HOTUBA YA WAZIRI MKUU KUHUSU MAPITIO NA MWELEKEO WA KAZI ZA SERIKALI NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA BUNGE KWA MWAKA2018/19

WAJASIRIAMALI WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA YAWAPATIA ELIMU YA KUTENGENEZA MIKOBA NA MAZULIA

$
0
0
 Mwakilishi wa Jimbo la Gando, Maryam Thani Juma akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wajasiriamali wa Mkoa wa Kaskazini Pemba yaliyoandaliwa na Jumuiya Maendeleo ya Elimu Zanzibae (ZEDO) yaliyofanyika Ofisi ya Umati na Malezi Bora Tanzania iliyopo Wete Pemba.
 Wajasiriamali wa vikundi mbali mbali vya Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa kwenye mafunzo ya utengenezaji wa mikoba na mazulia yaliyoandaliwa na (ZEDO)  yaliyofanyika Wete Pemba.
 Waziri wa Afya Zanzibar, Khamad Rashid Mohammed akiteta jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya Maendeleo ya Elimu Zanzibae (ZEDO) Ussi Said Suleiman katika sherehe ya ufungaji wa mafunzo ya siku tatu ya utengenezaji wa mikoba na mazulia yaliyofanyika Ukumbi wa Jamuhuri Holl Wete Pemba.
 Waziri wa Afya Zanzibar, Khamad Rashid Mohammed akifunga mafunzo ya utengezaji wa Mikoba na Mazulia katika Ukumbi wa Jamuhuri Holl Wete Pemba.
 Mwenyekiti wa Jumuiya Maendeleo ya Elimu Zanzibae (ZEDO) Ussi Said Suleiman (kulia) akiagana na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Khamad Rashid Mohammed mara baada ya kuyafunga mafunzo kwa wajasiriamali wa Mkoa wa Kaskazini Pemba. Picha na Makame Mshenga Pemba.​
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images