Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere


WANAFUNZI VYUO VIKUU WASHAURIWA KUTUMIA VYEMA MAWAZO YAO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
BENKI ya dunia kupitia mradi wake wa kuinua uchumi wa nchi mbalimbali Afrika April 4 umewatangaza washindi wake katika shindano la Blog4Dev2017 lililofanyika mwaka jana likiwa na malengo ya kutafuta vijana walio na mawazo thabiti ambayo yatasaidia katika kutatua tatizo la ajira nchini.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika utoaji wa tuzo kwa washindi hao mkurugenzi mkazi wa benki ya dunia nchini bi Bella Bird  ameeleza kuwa wamewapata washindi hao kutokana na uandishi mzuri wa insha bora katika kuangalia namna ya kutatua matatizo ya ajira nchini katika maeneo ya kilimo na teknolojia.

Bi Bella ameeleza kuwa washindi watawasilisha mawazo yao katika mjadala ulioandaliwa huko Washngton Dc mapema wiki ijayo.

Aidan Nzumi mmoja wa washindi wa shindano hilo ameeleza kuwa amefurahi kuwa mmoja wa vijana wataobadilisha maisha ya vijana wengi  na ameeleza kuwa kilimo ni kizuri katika kujiajiri  licha ya kuwa na changamoto katika hali ya hewa na taarifa hasa za masoko na mikopo pia amewataka  vijana walio shule na vyuo watumie mawazo yao katika kubadilisha maisha yao na ya vijana wengine.

Naye Michael Mollel mshiriki wa shindano hilo ameishukuru benki ya dunia kwa kupokea mawazo yao na kuyafanyia kazi ambazo na kwa namna moja au nyingine zitatoa ajira.
 Bella Bird Mkurugenzi mkazi wa benki ya dunia akiwa na washindi wa Blog4Dev2017 katika picha ya pamoja.
Baadhi ya washiriki na wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo kwa washindi hao.

AIRTEL MONEY YAGAWA BILIONI 14 KWA WATEJA WAKE HADI SASA, YATANGAZA GAWIO JIPWA

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu gawiwo la bilioni 1.8 la robo ya mwaka kwa wateja wa Airtel Money. katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda na Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Marando.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda, akitangaza gawiwo la bilioni 1.8 la robo ya mwaka kwa wateja wa Airtel Money wakati kizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kulia ni Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Marando.

Airtel Tanzania imetoa gawio linalofikia shilingi bilioni 14.8 hadi sasa kwa wateja wake na mawakala nchi nzima ikiwa ni  sehemu ya faida waliyoipata tangu mwaka 2015.

Hili limebainishwa na Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Airtel wakati akitangaza gawio la robo hii ambalo ni shilingi bilioni 1.8.

“Tangu tuanze kugawa sehemu ya faida yetu kwa wateja mwaka 2015, tumeshatoa jumla ya shilingi bilioni 14.8 na huwa tunagawa kila robo ya mwaka na kuhakikisha wateja na mawakala wanapokea fedha hizi kupitia akaunti zao za Airtel Money na wana uhuru wa kutumia fedha hizi wanavyotaka,” alisema.

Kwa mujibu wa Nchunda, hii ni mara ya sita mfulululizo kwa Airtel Tanzania kugawa sehemu ya faida kwa wateja wake tangu mwaka 2015. “Bwana Pesa hutoa gawio hili kwa wateja wa Airtel Money na mawakala kulingana na salio la mteja kila siku,” aliongeza.

Aliwashukuru wateja wa Airtel kwa kuendelea kutumia Airtel Money na kuifanya iwe huduma yenye tija na maarufu zaidi na kuongeza kuwa hadi sasa wana zaidi ya maduka 100 maalum kwa kutoa huduma ya  Airtel Money ambayo yanafanya huduma hii iwe ya kuaminika zaidi na rahisi kupatikana.

“Maduka haya ya Airtel Money huhakikisha mawakala wana salio la kutosha muda wote ili wateja wasipate usumbufu wanapohitaji huduma hiyo,” alisema. 

Kwa upande wake, Meneja wa Airtel Money, alisema kuanzia leo, wateja wa Airtel Money na mawakala watapata gawio linalofikia shilingi bilioni 1.8 kupitia akaunti zao za Airtel Money na wanaweza kutumia gedha hizo wanavyotaka ikiwemo kulipia huduma mbalimbali kama vifurushi vya mtandao, muda wa maongezi na LUKU.

Alitoa wito kwa mawakala wa Airtel Money kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wateja ili kampuni hiyo iendelee kutoa gawio kwa wateja wake kila robo ya mwaka.

“Airtel Money imejizatiti kuendelea kutoa huduma bora na nafuu ambayo ni suluhisho kwa biashara za aina yoyote,” alisema na kuongeza kuwa Airtel inashirikiana na biashara zaidi ya 400 na ziadi na benki 30 katika kutoa huduma za kifedha.

Airtel ina zaidi ya mawakala 50,000 nchi nzima na inaendelea kutanua wigowake ili kuhakikisha huduma za kifedha zinapatikana katika miji na vijijini. 

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yazindua ugawaji endelevu vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu

$
0
0
Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Hamad Rashid leo amezindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa jamii hapa Zanzibar. 

‘Leo kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tunayo furaha kubwa kutangaza ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa kila mama mjamzito ambaye ataudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na watoto wanaopata chanjo ya surua. Vile vile kila Mzanzibari ataweza kupokea chandarua kutoka kituo cha afya kwa kutumia koponi ambayo ataipata kutoka kwa mjumbe wa sheha,’ alisema Hamad Rashid.

Kampeni Endelevu ya ugawaji vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu una lengo la kufanya upatikanaji kwa rahisi vyandarua kupitia vituo vya afya. Ugawaji endelevu wa vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na shirika la Johns Hopkins Center for Communication kupitia mradi wa VectorWorks kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID .
,
kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria na kuratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria Zanzibar - ZAMEP . ‘Serikali inatoa shukrani kwa washirika wa Maendeleo ya afya, Watu wa Marekani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya WHO, Global Fund na wengine wote, aliongeza Mh Rashid.

‘Zanzibar imedhamiria kumaliza ugonjwa wa malaria kwa kusambaza vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu jambo ambalo litafanya upatikanaji wake kuwa rahisi. Upatikanaji kwa urahisi wa vyandarua ni hatua moja muhimu kwenye kupambana na ugonjwa wa malaria’, alisema Mhe Rashid akiongeza kuwa kupitia mradi huu unaozinduliwa leo, kila mama mjamzito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja watapata vyandarua bila Malipo yoyote. Vile vile alitoa wito kwa kila Mzanzibari kubadailisha chandarua chake cha zamani kwa kupata kopuni kutoka kwa Shehia kisha kutembelea kituo chochote cha Afya kupata chandarua.

Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid akiongea na waandishi wa habari jana Zanzibar baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid akiongea na waandishi wa habari jana Zanzibar baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria.
Naibu Meneja wa Kitengo cha Kupambana na Malaria Zanzibar Faiza Bwanaheri akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria. Kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi kutoka VectorWorks Waziri Nyoni.

ALIYEKUWA RAIS BRAZIL JELA MIAKA 12

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
ALIYEKUWA  Rais   wa Brazil  Luiz Inancio Lula da Silva maarufu kama Lula ametakiwa kuanza kutumikia kifungo chake cha miaka 12 gerezani kwa tuhuma za rushwa ya Euro laki saba na tisini wakati wa utawala wake.

Licha ya Lula kukanusha madai hayo nusu ya majaji waliunga mkono kifungo cha da Silva licha ya wananchi wengi kutegemea mkongwe huyu wa siasa kuekana katika mbio za uchaguzi mkuu utakaofanyika mapema Octoba.

Lula anaungwa mkono na wafuasi  wake katika miji ya Sao na Bernardo ambao waliandamana kupinga adhabu hii na kutaka aachiwe huru.

Luiz Inancio da silva (72) alizaliwa October 27, 1945 akiwa Rais wa 35 kuiongoza Brazil kuanzia Januari 1 2003 hadi Januari 1 2011 na ikumbukwe kuwa Lula alikuwa rafiki wa karibu wa aliyekuwa kiongozi wa Cuba  Fidel Castro.

RC SHINYANGA AWATAHADHALISHA WAHARIBIFU WA MISITU

$
0
0
Na Lusungu Helela-Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak amewatahadhalisha wananchi kuwa yeyote atakayeharibu misitu kwa kukata au kuingiza mifugo kwenye  misitu atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza jana wilayani Kishapu  wakati wa  kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani humo,  Mkuu wa Mkoa  alipiga marufuku kukata miti bila ruhusa yake au ya Mkuu wa wilaya. 
Telak alisema marufu hiyo imekuja kwa kuchelewa kwa vile hatua iliyofikia  katika Wilaya hiyo  inatisha  hakuna mahindi yanayostawi kutokana  na  kutokuwa na  mvua ya kutosha. 
‘’Mtu yeyote atakayekata miti ajiandae kupelekwa jela  kwa vile kukata miti katika wilaya hii ni sawa na uuaji.’’ alisema Telak
Alifafanua kuwa mtu yeyote atakayetaka kukata miti hata ule uliopo uwanjani pake ni lazima aombe kibali kwa wahusika na atakayekiuka kukata bila kibali ajue jela inamwita.
 Wakati huo huo, Telak  alitoa agizo kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha wanawakamata wale wote  watakaoingiza mifugo kwenye maeneo yaliyopandwa miti.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak akizungumza na watalaamu pamoja na wadau wa uhifadhi walioshiriki jana kwenye  kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akijibu hoja zilizotolewa na wadau mbalimbali  wa uhifadhi wa Misitu jana  wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu
 Mdau wa Uhifadhi wa Mazingira, Anna Matinye akichangia hoja  jana kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.
 Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akiwasilisha maada   kwa wadau mbalimbali  wa uhifadhi wa Misitu kwa kuwasomea baadhi ya vipengele kwenye kitabu cha Sera ya Taifa ya Misitu  jana wakati wa kongamano ambalo lilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ambayo Kitaifa inafanyika Mkoani Shinyanga wilayani Kishapu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

URAFIKI WA TANZANIA,CHINA NI WA DAMU,LAZIMA UDUMISHWE NA KULINDWA-BALOZI MAHIGA

$
0
0
*Balozi wa Wang Ke aongoza Jumuiya ya marafiki wa China ,Tanzania kuwakumbuka waliopoteza maisha wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

 SERIKALI ya Tanzania imeungana na Jamhuri ya Watu wa China katika kumbukumbu ya vifo vya Wachina 70 waliofarika wakati wa ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Watanzania waliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Kikanda na Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustino Mahiga huku ikiwakilishwa na Balozi wao nchini, Wang Ke. Kumbukumbu hiyo, imeandaliwa na Jumuia ya Marafiki wa Tanzania na China ambayo Mwenyekiti wake Dk.Salim Salim na Katibu wake ni Joseph Kahama.

Kabla ya kuweka mashada kwenye makaburi kwenye makaburi ya wachina hao ambao wengi wao ni wataalamu na wahandisi katika ujenzi wa reli, ilitolewa historia fupi ya vifo vyao.

Akizungumza baada ya kuweka mashada, Balozi Mahiga alisema ujenzi wa reli hiyo ulithibitisha urafiki wa kutoka moyoni kati ya nchi hizo mbili na kufafanua ujenzi wake ulifungua milango kwa China kujenga viwanda vingine kama UFI na Kiwanda cha Nguo cha Urafiki."Wakati wa ujenzi huu damu zilimwagika, wachina wamepoteza maisha na wengine wamebaki na ulemavu wa kudumu...hivyo urafiki wetu sisi na China ni wa damu," amesema.

Naye, Balozi Wang amesema nusu ya karne iliyopita, kupitia ombi la Rais wa Tanzania, Julius Nyerere na Rais wa Zambia, Kenneth Kaunda, viongozi wa kizazi cha China, Mwenyekiti Mao Zedong na Waziri Mkuu, Zhou Enlai walifanya maamuzi ya kimkakati na kihistoria kusaidia ujenzi wa TAZARA.
 Mnara wa Makaburi ya Wachina waliokuwa wakijenga Reli ya Tazara  ambao walifariki wakati wa ujenzi wa reli hiyo miaka zaidi ya 40 iliyopita.
 Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi  Agustine Mahiga akitoa heshima  na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, kwenye Mnara wa makaburi ya Wachina waliofkuja kutengeneza Reli ya Tazara
 Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi  Agustine Mahiga akiwa na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, wakiongoza kuweka mashada ya maua kwenye moja ya kaburi la wakandarasi waliofika nchini kujenga reli ya Tazara
 Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi  Agustine Mahiga  akihutubia Viongozi na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika katika sherehe ya kitamaduni ya watu wa china ya kuwakumbuka mafundi waliojenga reli ya Tazara.
  Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, akihutubia na kutoa historia fupi ya ushirikiano wa Tanzania na China ulivyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MJASILIAMALI ANAEUZA KAZI YA SANAA ZA MIKONO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimasikiliza  mjasiriamali Robinson Mungule anayeuza kazi za sanaa ya mikono katika ufukwe za Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mjasiriamali Robinson Mungule anayeuza kazi za sanaa ya mikono katika ufukwe za Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Timu 28 kushiriki Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2017/18

$
0
0
Timu 28 zinatarajia kushiriki Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2017/18 inayotarajia kuanza Mei 1,2018 mpaka Mei 16,2018 kwenye vituo vinne. Vituo vitakavyotumika ni Geita, Singida, Rukwa na Kilimanjaro. 

Makundi ya RCL yatakuwa na timu saba kila kundi yakipangwa kwa kufuata Jiografia ya kikanda katika soka. 

Mwisho wa kuwasilisha jina la Bingwa wa Mkoa ilikua Machi 30, 2018 ambapo mikoa yote 26 iliweza kutimiza ndani ya muda huo uliowekwa na TFF.

Mikoa iliyothibitisha mabingwa wao wa RCL watakaocheza ligi hiyo msimu huu :

1. Dar Es salaam (Karume Market, Ungindoni FC, Temeke Squard)

2. Pwani (Stand FC)

3. Morogoro (Moro Kids)

4. Dodoma (Gwassa Sports Club)

5. Singida (Stand Dortmund)

6. Tabora (Tabora Football Club)

7. Kigoma (Red Stars FC)

8. Geita ( Gipco FC)

9. Kagera (Kamunyange FC)

10. Mwanza (Fathom Sports Club)

11. Mara (Nyamongo Sports Club)

12. Shinyanga (Zimamoto FC)

13. Simiyu (Ambassador FC)

14. Arusha (Bishoo Durning Sports)

15. Manyara (Usalama Sports Club)

16. Kilimanjaro (Uzunguni FC)

17. Tanga (Sahare All Stars)

18. Lindi (Majimaji Rangers)

19. Mtwara (Mwena FC)

20. Ruvuma (Black Belt)

21. Njombe (Kipagalo FC)

22. Songwe (Migombani FC)

23. Mbeya (Tukuyu Stars)

24. Iringa (Iringa United)

25. Rukwa (Laela FC

26. Katavi (Watu FC)

27.Manyara ()Usalama FC)

Mikoa ya Rukwa, Ruvuma na Tabora  kuna malalamiko ya vilabu kupinga mabingwa wa mikoa, malalamiko ambayo TFF inaendelea kuyafanyia kazi.

Kundi A (GEITA)

Geita, Kagera, Mara, Mwanza,Shinyanga, Simiyu, Dar 2

Kundi B (RUKWA)

Rukwa,Katavi, Kigoma, Tabora, Ruvuma, Songwe, Mbeya 

Kundi C (SINGIDA)

Singida,Dodoma,Iringa, Njombe, Dar 3, Lindi, Mtwara 

Kundi D (KILIMANJARO)

Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Manyara, Pwani, Morogoro, Dar 1

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

WAANDISHI WA HABARI WAPATIWA ELIMU JUU YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

$
0
0
 Mkuu wa Chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi, Yussuf Haji Makame akitoa elimu kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) namna saratani hiyo inavyoathiri katika ukumbi wa hospitali ya Kidongo Chekundu Zanzibar.
 Waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa hospitali ya Kidongo Chekundu Zanzibar.
 Mwandishi wa TIFU TV akiuliza masuala katika Mafunzo hayo.
Mfanyakazi kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Abdulrahman Muhamed Saleh akijibu maswali ya waandishi wa habari (Picha na Abdalla Omar Habari – Maelezo).

MAHAKAMA YAINGIA MKATABA POSTA MLANGONI NA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

$
0
0
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Posta na Mahakama ya Tanzania wa huduma ya Posta Mlangoni inayotolewa na shirika hilo. Hafla hiyo, imefanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. Waliosimama nyuma yao, ni baadhi ya Maofisa waandamizi wa Posta na Mahakama.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi. 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga (kulia), wakibadilishana mkataba huo, mara baada ya kusainiwa katika hafla hiyo.

WAZAZI CCM PWANI WATOA DAMU,WACHANGIA UJENZI SHULE YA MSINGI AMANI

$
0
0
Na Elisa Shunda, Bagamoyo
JUMUIYA ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani imeadhimisha siku ya wazazi kwa mkoa huo kwa kuchangia kutoa damu chupa 120 na kutoa mifuko 50 ya simenti,mabati 100 na matofali 200 vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu na Laki Saba na Hamsini kwa ajili ya ujenzi wa darasa la Shule ya Msingi Amani Voda iliyopo Mbwewe wilayani Bagamoyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa mkoa na wilaya waliohudhuria katika maadhimisho hayo wamesema kuwa jukumu kubwa walilonalo jumuiya ya wazazi ni kuhakikisha wanajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha wanatumia nguvu na mali kusaidia katika elimu,mazingira na afya ambayo yanagusa jamii ya watu wengi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Ramadhan Maneno alisema kuwa muda haumsubiri mtu na kuwasisitiza wawakilishi wa majimbo na kata wa chama hicho kutekeleza ahadi walizoahidi kuzitoa kwa wananchi wao wahakikishe wanazitekeleza wao kama viongozi hawatakubali chama kije kiadhibiwe katika chaguzi zijazo kwa ajili ya uzembe wa mwakilishi wa wananchi hao.

“ndugu zangu wawakilishi mliochaguliwa na wananchi kuwawakilisha bungeni na kwenye vikao vya halmashauri ni muda muafaka sasa wa kuhakikisha kabla ya uchaguzi mkuu haujafika hakikisheni mnatatua changamoto na kero za wananchi wenu mnaowawakilisha,haiwezekani chama chetu kiadhibiwe na wananchi ambao ndiyo wapiga kura kwa uzembe wa kutowajibika ipasavyo kwa watu hawa waliokuchagua hata nyie wenyeviti wa serikali za mitaa wahudumieni kwa haki wananchi wenu kama inavyotakiwa bila ya upendeleo” Alisema Maneno.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Ramadhan Maneno akimkabidhi Mabati 100,Mfuko wa Simenti 50 na Matofali 200,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Mkoa wa Pwani,Jackson Kituka (kulia) iliyotolewa na wadau mbalimbali wa elimu kwa ajili ya ujenzi wa darasa la Shule ya Msingi ya Amani Voda iliyopo Mbwewe. Picha zote na Elisa Shunda.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Ramadhan Maneno (kulia) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Mkoa wa Pwani,Jackson Kituka (katikati) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo.

 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Pwani, Gama J Gama na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda wakipanda miti katika eneo la Kituo cha Afya cha Lugoba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mashindano ya mchezo wa kujihami kufanyika Tanzania Mei

$
0
0
TANZANIA imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya mchezo wa kujihami Tae kwo-ndo kwa nchi za Afrika Mashariki yanayofanyika Mei mwaka huu.

Rais wa Tae kwo-ndo kwa nchi za Afrika Mashariki, Kennedy Said alisema jana kuwa maandalizi ya mashindano hayo yameanza.

Alisema mashindano hayo yatakutanisha wachezaji zaidi ya 70 kutoka nchi za Uganda, Burundi, Kenya, Rwanda na wenyeji Tanzania.

Kennedy ambaye pia ni Rais wa Tae Kwo-ndo Tanzania alisema zimealikwa nchi za Ethiopia na Sweden kushiriki mashindano hayo na zawadi mbalimbali zimeandaliwa kwa ajili ya washindi.

Kennedy alisema Tanzania ilipata nafasi ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindani hayo kutokana na mkutano wa nchi saba wanachama uliofanyika Kampala,Uganda Desemba mwaka jana.

Alisema washindi wa mashindano hayo watapata nafasi ya kushiriki fainali ya kuwania ubingwa wa mchezo huo Afrika utakaofanyika Addis Ababa, Ethiopia Agosti mwaka huu.
Wachezaji wa Tae kwo-ndo wakijiandaa kwa mazoezi.

Wosia wa Dkt. Salmin Amour

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (katikati) bungeni mjini Dodoma Aprili 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, bungeni mjini Dodoma Aprili 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Det. Harrison Mwakyembe kutoka bungeni mjini Dodoma Aprili 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kwenye viwanja vya bange mjini Dodoma Aprili 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wapili kushoto) , Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bibi Maimuna Tarishi (wapili kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 5, 2018.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

FEDHA ZA UPANUZI WA VITUO VYA AFYA ZIFANYE ZAIDI YA KAZI ILIYOTARAJIWA - RC GALLAWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na mafundi wanaojenga katika kituo cha Afya Isansa Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na baadhi ya watendaji na wananchi wa kijiji cha Iyula waliojitokeza katika eneo la ujenzi katika kituo cha Afya cha Iyula Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 400 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.

Grace Gwamagobe-Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amesema atahakikisha anasimamia kwa ukaribu fedha zilizotolewa na serikali Mkoani hapa kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya ili zifanye kazi zaidi ya ile iliyopangwa awali kutokana na kuongezeka kwa nguvu za wananchi.

Gallawa ameyasema hayo mapema jana wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbozi alipokagua maendeleo ya upanuzi wa vituo vya afya vya Isansa kilichopokea milioni 500 na kituo cha Afya cha Iyula Kilichopokea milioni 400, kwa ajili ya ujenzi wa maabara, nyumba ya daktari, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti.

“Fedha hizi lazima zifanye kazi iliyopangwa vizuri na pia tuongeze kazi nyingine ya ziada kutokana na kuwa tumepata nguvu ya wananchi lakini pia mafundi wetu hawa tunaowatumia ni wazawa na wenyeji wa maeneo ya kwetu kwahiyo gharama zao zitatupa unafuu ambao tunatakiwa kuutumia kuongeza kazi nyingine”, amesema Gallawa.

Ameongeza kuwa licha ya upanuzi wa vituo vya afya kuchelewa kuanza bado ana Imani kuwa wataweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa kutokana na uchapakazi wa mafundi wazawa wa maeneo hayo.

Gallawa amesema kukamilika upanuzi wa vituo hivyo vya afya kutavifanya vituo hivyo vivutie na hata mgonjwa akifika apate matumaini ya kupona na sio kukatishwa tamaa na hali mbovu ya mazingira.

“Tiba ya kwanza ya mgonjwa akifika kituo cha afya akute mazingira yanavutia na sio majengo mabovu na uchafu hivyo vitamfanya akate tamaa ya kupata matibabu sahihi, tukimaliza ujenzi wa hayo majengo tutahakikisha tunapaka rangi paa za majengo yote zifanane ili vituo vyetu vya afya vivutie”, amefafanua Gallawa.

Aidha Gallawa amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Lauteri Kanoni kuhakikisha anaweka mfumo wa maji safi katika vituo hivyo hasa mfumo wa kuvuna maji ya mvua ili vituo vikikamilika maji yawepo kwa ajili ya matumizi.

Naye Mkazi wa kijiji cha Isansa Wilaya ya Mbozi Bi Stela Mkeya ameonyeshwa kufurahishwa na upanuzi wa kituo cha Afya Isansa huku akieleza baadhi ya kero walizokuwa wakizipata awali.

“Tunaishukuru sana serikali ya Magufuli kwakweli wametusaidia, tulikuwa tunapata shida kufuata huduma za upasuaji wa akina mama wajawazito huko hospitali ya Wilaya iliyopo Vwawa lakini pia hapa kwenye kituo cha afya mzazi akijifungua hata mazingira ya kwenda kujisafisha vizuri kama vile mabafu yakiwa hayatoshi kabisa”, ameeleza Bi Mkeya.

Kwa upande wao mafundi waliokabidhiwa kazi ya upanuzi wa vituo hivyo vya Afya wameonyesha ari ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na haraka huku wakimuomba Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa awasaidie upatikanaji wa taa ili waweze kufanya kazi mchana na usiku naye Mkuu wa Mkoa amekubaliana na mapendekezo hayo.

MKUTANO WA WADAU KATI YA SERIKALI, WAAJIRI, PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KUHUSU MASUALA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI UTAKAOFANYIKA DODOMA SIKU YA TAREHE 7 APRILI, 2018

$
0
0
Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wanautaarifu Umma kuwa wameandaa Mkutano wa Wadau utakaojadili na kupokea maoni kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi. 

Mkutano huu utawakutanisha Waajiri  na Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) wa Mikoa ya Dodoma na Singida; na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Eneo:Jengo la LAPF,
Mtaa wa Uhindini, Barabara ya Makole,
DODOMA.
Tarehe:7 Aprili, 2018
Muda:4:00 Asubuhi

Imetolewa na:

Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu,
Jengo la LAPF,
Mtaa wa Uhindini,
Barabara ya Makole,
S.L.P. 2890,
DODOMA, TANZANIA.

TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA

$
0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekutana  na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa kwa ajili ya kupata miongozo ya kufanya kiwanda kiweze kujengwa  na kuanza kuzalisha dawa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Adam Fimbo amesema kuwa kuwakutanisha wadau hao umetokana mkutano wa Mawaziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto ambapo TFDA imeona ni muda mwafaka katika kuweza kuwapa muongozo wadau jinsi ya kuweza kuanzisha viwanda hivyo.

Fimbo amesema kuwa TFDA kazi yake kubwa ni kuangalia usalama wa dawa tangu inapozalishwa mpaka inaingia sokoni ikiwa lengo ni kumlinda mlaji na dawa hizo.

Aidha amesema kuwa ili kiwanda cha dawa kiweze kusajiliwa na kuzalisha dawa hizo lazima vigezo vilivyowekwa vizingatiwe.

Fimbo amesema baada ya kupata michoro wa ramani pamoja na ujezi na kuanza kuzalisha dawa usajili hauzidi siku 15 kutokana na hatua zote zilizofanyika TFDA inakuwa imepitia.

Hata hivyo amesema kuwa hakuna urasimu wowote katika kusajili dawa au kiwanda nia kumlinda mlaji kwa dawa anazotumia.

“Bila kuwa na usalama wa dawa unaweza ukaua watu ndio maana TFDA tuka kwa ajili ya kazi hiyo ya kuangalia usalama wa dawa za ndani na zinazoingia”amesema Fimbo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Adam Fimbo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kukutana  na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa kupata miongozo  ya kufanya kuwekeza katika sekta hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mkaguzi wa Viwanda vya Dawa wa TFDA, Proche Patrick akiwapitisha katika miongozo wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa  leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Msajili wa Dawa wa TFDA, Dk. Shani Maboko akizungumza  na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa jinsi ya usajili wa dawa unavyofanyika katika mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa wakisikiliza mada zinazotolewa na TFDA leo jijini Dar es Salaam.

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA UKUTA MIGODI YA TANZANITE MERERANI YAKAMILIKA

$
0
0
Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo kabla ya kikao cha majumuisho kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akipokelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo kabla ya kikao cha majumuisho kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.
PIX7.Mafundi wakiwa katika hatua za mwisho kukamilisha maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.
Mmoja wa mafundi akiendelea na kazi ya kuandaa eneo litakapowekwa jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.
Sehemu ya geti la kuingia katika eneo la mgodi wa Tanzanite kama inavyoonekana katika picha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS DK. SHEIN AZINDUA KONGAMANO LA KUMBUKUMBU YA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akizungumza jambo wakati akizindua kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo Bububu Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.



Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya akizungumza wakati wa  uzinduzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo Bububu Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Viongozi walioshiriki katika Uzinduzi wa  Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  Bububu.
Baadhi ya Vijana  walioshiriki katika Uzinduzi wa  Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Abeid Karume lililofanyika leo katika Ukumbi wa Kampasi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  Bububu ambalo limezinduliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
Picha na Ikulu

KUSOMA ZAIDI SOMA ZAIDI
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images