Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA ZANZIBAR,UBALOZI WA SWEDEN WASAINI MAKUBALIANO YA BILIONI 13/- KUSAIDA SEKTA YA ELIMU ZANZIBAR

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar (kushoto) akitiliana saini na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden Ulf Kallstig (kulia) kuhusiana na Mradi wa awamu ya pili wa Dola za Kimarekani milioni 5.76 ambazo sawa na shillingi Bilioni 13 za kitanzania kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar (kushoto) akibadilishana hati ya saini na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden, Ulf Kallstig(kulia) kuhusiana na Mradi wa awamu ya pili wa Dola za Kimarekani milioni 5.76 ambazo sawa na shilling Bilioni 13 za kitanzania kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu Zanzibar.
 Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden, Ulf Kallstig akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutiliana saini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar kuhusiana na Mradi wa awamu ya pili wa Dola za Kimarekani milioni 5.76 ambazo sawa na shilling Bilioni 13 za kitanzania kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Khamis Mussa Omar akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutiliana saini na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden  kuhusiana na Mradi wa awamu ya pili wa Dola za Kimarekani milioni 5.76 ambazo sawa na shilling Bilioni 13 za kitanzania kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

WAPENZI WA SIKINDE MSIKOSE DAR CCM FAMILY DAY

NAHODHA WA TIMU YA DR CONGO ATOA SIRI YA KUFUNGWA KWAO

MAHAKAMA YAAMURU MMILIKI IPTL AKATIBIWE HOSPITALI YA MUHIMBILI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Sethi, kupelekwa  kutibiwa  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).

Uamuzi huo umetolewa  Hakimu Mkazi Mkuu wa,  Huruma Shaidi, baada ya mshtakiwa kudai kuwa anaumwa na anatakiwa kwenda kutibiwa ili aweze kuendelea na kesi.

Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi ameyasema hayo leo Machi  29/2018 baada ya mshtakiwa kudai kuwa anaumwa sana.
"Mheshimiwa hali yangu imaribika sana naitaji kupatiwa matibabu", amedai Sethi.

Hata hivyo, baada ya Seth kutoa ombi hilo la matibabu, Wakili wa Serikali, Leornad Swai alidai ni kweli mshtakiwa huyo anaonekana ni dhaifu lakini aliiomba mahakama taratibu za Magereza zifuatwe. 

" Tutawasiliana na magereza waweze kumtibu kwa utaratibu wa serikali", amedai Swai.

Baada ya kudai hayo Hakimu Shaidi amesema, 

"Mshtakiwa ni kweli anaunwa, huhitaji kuwa na daktari kujua mtu anaumwa kwa kumuangalia tu anaonekana, hatuwezi kutenda haki kama mtu ni mgongwa, naamuru apelekewe Muhimbili akatibiwe aweze kuendelea na kesi", amesema Shaidi.

Mapema Wakili wa Takukuru,  Pendo Temu akisaidiana na Swai,  alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri bado haujakamilika.

Alidai, wanafanya mawasiliano na nje ya nchi kupata nyaraka muhimu katika kikamilisha upelelezi. 

Pia ameomba kwenda kuchukua maelezo ya mshtakiwa namba mbili, Seth, afya yake itakapoimarika.

kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 11, mwaka huu itakapotajwa.

Seth na James Rugemarila wanakabiliwa  wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.bilioni 309.

CARRER TIMES LTD KUSAKA VIJANA WABUNIFU

WATAALAM UPIMAJI ARDHI WAANZA UHAKIKI MIPAKA TANZANIA,NCHI JIRANI

$
0
0
Na Rehema Isango, Mara
TIMU ya watalaamu wa upimaji ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini na Taasisi za Usimamizi wa ardhi Kenya zimekutana wilayani Tarime mkoani Mara kwa lengo la kuanza utekelezaji wa uhakiki na kuimarisha mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizi mbili.

Mwanzoni mwa Machi mwaka hu, Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula alitangaza azma  ya Serikali ya Tanzania kuanza  kuimarisha mipaka yake kwa nchi jirani za Kenya na Uganda.

Hiyo ilitokana na ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya katika Mbuga ya Wanyama ya Taifa ya Serengeti iliyopo mkoani Mara.

Kwa mijibu wa Wazara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imefafanua hatua ya uhakiki na uimarishaji wa alama za mipaka ya mikataifa inatokana na mpaka huo kuwa wa siku nyingi na haukuwa wazi katika maeneo mengi.

Pia baadhi ya alama hizo kuharibiwa, kung’olewa au kuchakaa na hivyo kusababisha Serikali pande zote kushindwa kusimamia kwa ufanisi shughuli za mipakani, rasilimali za nchi pamoja na ulinzi na usalama.
Mkuu wa mchakato wa Uhamasihaji katika kazi ya kuhakiki na kuimarisha mipaka ya Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya Raymond Bagenda kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza wakati wa kikao cha pamoja cha wataalam wa masuala ya upimaji ardhi kutoka katika ofisi za Serikali za nchi zote mbili. Kikao hiko kilichofanyika wilayani Tarime mkoani Mara kinapanga namna ya  kutekeleza kazi hiyo kwa pamoja. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais nchini Kenya inayohusika na Usimamizi wa Mipaka ya Kimataifa (KIBO) Joseph Rotich.

Baadhi ya Wataalam wa masuala ya upimaji ardhi pamoja na maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na katika ofisi zingine za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mazungumzo kuhusu  namna ya  kutekeleza kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kati ya Kenya na Tanzania.

Wataalam wa masuala ya upimaji ardhi pamoja na maafisa mbalimbali kutoka katika ofisi za Serikali za nchi zote mbili waliojumuika pamoja wilayani Tarime mkoani Mara kupanga namna ya  kutekeleza kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka ya kimataifa  kwa pamoja. Wa tatu kutoka kulia (walioketi) ni Mkuu wa Msafara wa wataalam kutoka Tanzania Huruma Lugala na kulia kwake ni Mkuu wa Msafara kutoka Kenya Julius Rotich.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RC TABORA: WAKANDARASI WA KITANZANIA HAKIKISHENI MIRADI YENU INAKUWA YA KIWANGO CHA JUU

$
0
0
Na Tiganya Vincent
WAKANDARASI Kitanzania wametakiwa kuzingatia ubora, viwango  vya kazi zao ili waweze kuaminika kwa Serikali na hivyo kupata fursa kubwa ya kupewa miradi mipya inayotarajiwa kujengwa hapa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati alipokutana na ujumbe wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi(CRB)

Alisema ujenzi wa miradi chini ya kiwango na ambayo haidumu kwa muda mrefu kutawasababisha kutopewa kipaumbele pindi miradi inapokuwa ikitangazwa na badala yake miradi hiyo kutekelezw na wakandarasi wa kigeni.

Mwanri alisema ni vema wajenga tabia ya kushirikiana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ili waweze kuwa na nguvu kubwa na vifaa vingi ambavyo ndivyo vitawasaidia kuikamisha kwa wakati na kwa kiwango bora kinachotakiwa.

Alisema matokeo mazuri ya utekelezaji wa miradi yataifanya Serikali kutoa kipaumbele kwa Kampuni za Watanzania katika miradi ya ujenzi , jambo ambalo litawasaidia kujiimarisha zaidi.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri(kulia) akiagana jana na Meneja wa Wakala wa Barabarani Tanzania(TANROADS) Mkoani humo, Damian Ndabalinze (kushoto) mara baada ya mazungumzo yaliyolenga kujua hali ya ukarabati wa barabara zilizoharibiwa na mvua iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha kukatika kwa mawasilano katika njia mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri(kulia) akitoa maagizo jana kwa Mfanyakazi katika Kitalu cha Miche ya Miti mbalimbali cha Manispaa ya Tabora, Mariam Christopher(kushoto) na Meneja wa Wakala wa Mistu Tanzania (TFS) Manispaa ya Tabora Bakilana Mashauri (katikati) kuhusu kuotesha miti maji mingi kwa ajili ya kupanda katika maeneo mbalimbali katika Manispaa hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri(kulia) akitoa maagizo jana kwa Meneja wa Wakala wa Mistu Tanzania (TFS) Manispaa ya Tabora, Bakilana Mashauri (kulia) kuhusu kuotesha miti maji mingi kwa ajili ya kupanda katika maeneo mbalimbali katika Manispaa hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Milioni 260 za Tatumzuka kunyakuliwa katika ‘Jackpot’ ya Pasaka

$
0
0
Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaongoza hapa nchini unawapa fursa Watanzania kushinda kitita cha Shilingi milioni 260 katika droo itakayofanyika jumapili ya pasaka na kuonyeshwa moja kwa moja saa 3:30 usiku

 Taifa linapojiandaa na sherehe za Pasaka, Tatumzuka imeungana na wateja wake kwa kutangaza fursa ya kushinda kitita cha shilingi 260 ambacho lazima kitolewe jumapili ya Pasaka. Kitita hicho kinono cha milioni 260 ambacho hakijawahi kutolewa kwa mtu katika historia ya nchi hii sasa kitatolewa kwa mshindi mmoja atakayebahatika kwenye ‘PasakaMzukaJackpot’ siku ya tarehe 31/3/2018.

Bwana Sebastian Maganga, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Tatumzuka, ameuelezea umma namna ilivyo rahisi kuingia katika droo. “Wiki hii ukiwa na shilingi 500 tu, kwa kutumia; Mpesa, Tigo pesa au Airtel Money, ingiza namba ya kampuni ambayo ni 555111, kisha weka namba zako tatu za bahati na hapo utakuwa umeingia rasmi kwenye droo ya milioni 260 za PasakaMzukaJackpot” alielezea Maganga

Hicho sio kitu pekee ambacho Tatumzuka inatoa msimu huu wa sikukuu, pia una nafasi ya kushinda milioni 10 kila siku na milioni 6 kila saa.“Ukinunua tiketi moja ya shilingi 500, Tatumzuka inakupa nafasi ya kuingia katika droo 3 tofauti na hivyo kukuongezea nafasi za kushinda tofauti na michezo mingine ya namba” Maganga alisisitiza

Tatu Mzuka pia imetumia fursa hiyo kuwatambulisha washindi wa wiki iliyopita ambao walitokana na droo ya 34 ya Tatumzuka jackpot.Bi Hanifa kutoka Magomeni, Dar es Salaam alijishindia milioni 5. Bwana Juma Mkombozi kutoka Magomeni, Kagera alijishindia milioni 7. Bwana Prosper Munuo kutoka Bunju A alijinyakulia milioni 5 na Magreth Nkwabi wa Kahama, Shinyanga alipata milioni 3.

Washindi wote wakiwa wenye furaha baada ya ushindi walisisitiza kwamba wataendelea kucheza kujaribu bahati zao kwenye dau la kihistoria la milioni 260 jumapili hii.‘Droo hii ya kihistoria itaonyeshwa moja kwa moja kupitia ITV, Clouds TV na TV1 jumapili hii saa 3:30 usiku’ Bwana Maganga aliufafanulia umma. 
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano  Sebastian Maganga akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar akielezea kuhusu Tatumzuka kuungana na wateja wake kwa kutangaza fursa ya kushinda kitita cha shilingi 260 ambacho lazima kitolewe jumapili ya Pasaka.
 Mmoja ya washindi akikabidhiwa mfano wa Hundi yake yenye thamani ya shilingi milioni tano na la  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sebastian Maganga.



 Washindi wa Tatu Mzuka Jackpot wa wiki iliyopita kwa pamoja wakifurahi

WAZIRI MKUU AREJEA DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Kasulu Mjini , Daniel Nsanzugwako kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma wakati aliporejea akitoka Dar es salaam Machi 28, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, kushoto ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na watatu kushoto ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI WAMUAGA MAKAMU WA RAIS TAYARI KWA KUELEKEA VITUO VYA KAZI

$
0
0
Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda  Mhe.Ernest Mangu na Meja Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi  wa  Urusi leo wamekutana na kuzungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma.

Mabalozi hao walifika kwenye makazi ya Makamu wa Rais, Kilimani Dodoma  kwa lengo la kumuaga ,walimuahidi Makamu wa Rais kufanya kazi kwa ajili ya Tanzania.

Wamemuambia Makamu wa Rais wanajua dhamana kubwa waliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na dhamira yake ya Tanzania ya Viwanda .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Mhe. Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe. Ernest Mangu ambao walifika nyumbani kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na  Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi(kushoto) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Ernest Mangu(kulia) ambao walifika nyumbani kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KAMATI YA BUNGE YA UONGOZI YAKUTANA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa, Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto kwake) alieambatana na baadhi ya Mawaziri.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa kassim Majaliwa (kushoto) akimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt.Tulia Ackson (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kikao hicho pia kilihudhuriwa na Baadhi ya Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Suleiman Kakoso (watatu kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao cha uongozi kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kikao hicho kiliongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson pia kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alieambatana na baadhi ya Mawaziri kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Adelardus kilangi (katikati) na Mjumbe wa Kamati, Mhe. David Silinde (kushoto) kikao hicho kiliongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson pia kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alieambatana na baadhi ya Mawaziri.
 Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao kilicholenga Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye kamati za kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara Mbali mbali kilichofanyika leo tarehe 28 Machi, 2018 katika ofisi za Bunge Mjini Dodoma. kikao hicho kiliongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson pia kilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alieambatana na baadhi ya Mawaziri kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BancABC YATEKELEZA SERA YA FEDHA YA BoT

$
0
0
BENKI ya BancABC  imesema imetekeleza Sera ya fedha  ya Benki  Kuu ya Tanzania(BoT) kwa kutangaza kutoa punguzo kwa wateja  wake wapya kuwezesha  kukopa kuanzia Aprili 1 mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji was BancABC Dana Botha amesema benki hiyo ni  sehemu ya Atlasi Mara iliyosajiliwa  katika soko la hisa la Londan ikiwa na lengo la kujitanua ili kuwa kinara katika masuala ya kifedha katika ukanda wa Sahara kwa kutumia uzoefu wake na uwezo wa kukuza mitaji.

Hivyo Botha amesema watapungunza riba kwa wateja wao katika mikopo ya masharti ambayo itakuwa ni huduma ya Over draft pamoja na  ya nyumba na kufafanua mwaka jana benki nyingi zilipita katika wakati mgumu wa ukwasi.

"Hivyo kufanya uwezo wa kukopesha kuwa mdogo.Kwa miezi kadhaa sasa,Serikali kupitia BoT imekuwa ikisisitiza kuhusu punguzo la riba hiyo kwa kupunguza masharti kama vile kiwango cha  chini cha fedha kwa mabenki,"amesema Botha.
 Mkurugenzi mtendaji wa BancABC Dana Botha akizungumza na waandishi wa habali katika ofisi zao Leo Jijini Dar es Salaam,kuhusu punguzo la tozo  ya mikopo mbali mbali kwa wateja wao.


Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Dana Botha kulia,kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Hazina BancABC Barton Mwasamengo pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wa BancABC Joyce  Malai katikati wakishika bango linaloonyesha punguzo la tozo za Mikopo.


TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA KANDA YA ZIWA,KUANZIA CCM KIRUMBA APRILI MOSI JIJINI MWANZA

$
0
0

Ni siku nne zimebaki kengele ya Tamasha la Pasaka zinahesabika. Ni Aprili Mosi, kwenye Uwanja  wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Mara nyingi Tamasha la Pasaka limekuwa likifanyika jijini Dar es Salaam safari hii Msama Promotion imeamua kulifanya tamasha hilo Kanda ya Ziwa. Hivyo Pasaka hii, wapenda muziki wa injili wa Kanda ya Ziwa na viunga vyake watapata burudani ya nyimbo za kumsifu na kumtukuza Mungu huku wakipata mahubiri kwa njia ya uinjilisti wa nyimbo.

Aprili Mosi ni CCM Kirumba, Aprili Pili Tamasha la Pasaka litachukua nafasi Uwanja wa Halmashauri, mkoani Simiyu ambako nako watasheherekea kwa nyimbo za injili.

Wakati siku zikikaribia kuelekea Tamasha la Pasaka kwa mkazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa jumla ni kuendelea kumuomba Mungu ili aendelee kukupa uzima na afya njema.Waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotion, mwaka huu wameamua kuweka vionjo tofauti ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika na kuacha historia kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Kila mwanamuziki aliye kwenye chati, nyimbo zake za kumsifu na kumtukuza Mungu zikiwa zinatamba na kusikika, atakuwemo kuburudisha mashabiki wake na kubwa zaidi ni kwamba kuna baadhi ya waimbaji wataimba wakipiga vyombo vya muziki Live ili kuleta ladha na burudani zaidi katika tamasha hilo..

Kwa mujibu wa waandaji wa Tamasha la Pasaka, mwimbaji Rose Muhando atazindua albam yake mpya “Usivunjike Moyo” kati ya waimbaji wengi kutoka hapa nchini Tanzania na nje watakaofanya mambo makubwa katika tamasha hilo. 

Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka akizungumza katika moja ya mikutano yake na waandishi wa habari kuelezea maandalizi ya Tamasha hilo litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Aprili 1 na Kwenye uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mwimbaji Jesca Honore akithibitisha kushiriki katika tamasha hilo kushoto ni Chrstopher Mwahangila mwimbaji mwingine ambaye atashiriki katika tamasha hilo mkoani Mwanza na Simiyu na katikati ni Jimmy Charles mmoja wa waratibu wa tamasha hilo. 
Mwimbaji Upendo Nkone akithibitisha kushiriki katika tamasha hilo kushoto ni Mwimbaji Joshua Mlelwa ambaye pia atakuwepo katika tamasha hilo katikati ni Ufo Saro mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo.
Mwimbaji Martha Baraka akitibitisha kushiriki katika tamasha hilo kutoka kushoto ni Jimmy Charles mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo na katikati ni Mzee Rainfred Masako mmoja wa Viongozi wa Dira TV. 
Mwimbaji Christopher Mwahangila akifanya vitu vyake katika moja ya video zake alizowahi kurekodi.

POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi nchini limesema hali ya usalama nchini ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua kwa kiasia kikubwa huku likieleza kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu

Taarifa iliyotolewa leo jijii Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ,IGP Simon Sirro ameshukuru ushirikiano ambao wananchi wanautoa kwa jeshi hilo ambao umesaidia kupunguza matukio ya uhalifu na nchi kiusalama iko shwari.

"Kiujumla hali ya usalama hapa nchini ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa na jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili  kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia,"amesema.

Kuhusu maandalizi ya jeshi hilo kuelekea Pasaka,Sirro amesea wamejipanga katika mikoa yote na kuwahakikishia wananchi kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha Sikukuu hiyo inasherekewa kwa amani na utulivu.

"Na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo katika hali ya  utulivu,"amesema.

Amewaomba wazazi na walezi kuwa waangalifu kwa watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu."Kwa wanaomilii kumbi za starehe wanatakiwa  kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi".

Wakati huohuo Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.

KIGWANGALLA APOKEA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA

$
0
0
Kufuatia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kutafuta wawekezaji wa Kimataifa kwa ajili ya kuwekeza katika sekta utalii hapa nchini, Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China imejitokeza kwa lengo la kuwekeza katika utoaji wa huduma za kitalii zenye ladha na mandhari ya Kichina.

Mwenyekiti wa Kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Tony, amesema kampuni hiyo imepanga kujenga hoteli za kitalii za kichina katika mji wa Karatu jijini Arusha na Serengeti mkoani Mara.

Akizungumza na Waziri wa Maliasil na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ofisini kwake mjini hapa jana kwa ajili ya kutambulisha mradi huo, Tony alisema mradi huo ni mahsusi kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii wa China wanaotembelea Tanzania.

Alisema kupitia mradi huo jumla ya magari 500 ya safari  za utalii yatanunuliwa (Safari Cars) kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii hao wakati wa kutembelea maeneo ya vivutio hapa nchini.Pamoja na magari hayo alisema kampuni hiyo pia imepanga kuanzisha safari za moja kwa moja za ndege kutoka China hadi Tanzania ili kupunguza muda wa usafiri na gharama.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya pamoja na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
 Wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Kigwangalla ofisini kwake mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi flash yenye picha za wanyamapori wa Tanzania Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing, aliyefahamika kwa jina moja la Tony kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza hapa nchini katika ujenzi wa  mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
 Waziri Kigwangalla akiendelea na mazungumzo na wakezaji hao.Na Hamza Temba - WMU-Dodoma.

HABARI ZAIDI  BOFYA HAPA

KAMPUNI YAJITOSA KUSAKA WABUNIFU WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO

$
0
0
Na Said Mwishehe,  Globu ya Jamii.

KAMPUNI ya Carrer Times Ltd inayoshighulisha na teknolojia imeandaa Africa Technology Awards yenye lengo la kusaka na kuibua wabunifu katika mambo yanayohusu teknolojia na hasa ya habari na mawasiliano nchini.

Imesema kuna vijana wengi ambao wanao uwezo wa kubuni mambo yanayoweza kusaidia maendeleo ya nchi, hivyo wameamua kuchukua jukumu hilo kwa kutoa tuzo hiyo baada ya kushindanisha kazi za ubunifu ambazo washiriki watazionesha kwao.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Carrer Time Ltd Hawa Hongo amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa watatoa tuzo hiyo baada ya kupata washindi kwenye mambo ya ubunifu na kuanzia kesho wataanza kutoa fomu kwa wanaotaka kushiriki.

"Tunafahamu kuna vijana wengi ambao wapo mtaani na wanao uwezo mkubwa katika kubuni mambo yanayohusu teknolojia na hao ndio ambao tunawataka kuwaibua kwa maslahi ya nchi yetu.Tunaka vijana ambao wataoesha uwezo wao halisi katika mambo ya ubunifu,"amesema.

Amesema kumekuwepo na mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yakiibua vipaji lakini kwenye mambo ya ubunifu katika mambo yanayohusu teknolojia haifanyiki sana na hivyo wao kupitia kampuni yao wameamua kusaka vijapaji vilivyojificha mtaani.

Kuhusu taratibu za kupata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano hayo, amesema wataanza kutoa fumu ambazo zitakazokuwa zinatolewa kwenye ofisi zao zilizopo Mikocheni B mtaa wa Huruma jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Carrier Time Ltd, Hawa Hongo akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari alipokuwa anazungumzia Africa Teknology Awards 2018 itakayotolewa na kampuni yao Mei mwaka huu kwa washindi wa shindano la ubunifu katika mambo ya teknolojia

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC HAPI AAGIZA WATENDAJI KUTOA FEDHA BIL 2.3/- KWA WAJASIRIAMALI KINONDONI

$
0
0
Na Agness Francis Blogu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni  Dar es Salaam Ally Hapi amewaagiza watendaji wake kuhakikisha hadi ifikapo Juni mwaka huu wawe tayari wametoa fedha za mkopo Sh.bilioni 2.3 kwa wajasiriamali ambao ndio walengwa wa fedha hizo na kama itakuwa bado ataifumua idara ya maendeleo ya jamii.

Hapi ametoa maagizo hayo leo wilayani Kinondoni jijini wakati anazugumza kikao kati yake, wajasiriamali wa wilaya hiyo pamoja na watendaji ambapo la kikao hicho ilikuwa ni kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili 

Baada ya kusikiliza changamoto za wajasiriamali hao ,Hapi amesema moja ya changamoto ambayo imejitokeza kutofika kwa fedha Sh.bilioni 2.3 kwa wajasiriamali hao.

Amesema kama watendaji hao kazi imewashinda waondoke mara moja kuliko kutowatendea haki wajasiriamali kwa kuchelewesha fedha hizo hadi sasa bila sababu yoyote ya msingi. 

DC Hapi amesema Februari mwaka huu  ilitolewa Sh.bilioni 2.3 kwa ajili ya kukopeshwa vijana wajasiriamali ili kupanua biashara na kuendeleza pato la nchi.

"Nawahakikishia wakazi wa Kinondoni ikifikapo Juni mwaka huu fedha hiyo ikiwa haijafika kwa walengwa nitafumua idara yote ya maendeleo ya jamii.Hatutaki watu wasiofanya kazi kwa bidii,"amesema.

Aidha Hapi amesema ili kuondokana na Taifa la kuwa omba omba ni lazima kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kuongeza bila nguvu za wananchi Rais peke yake hataweza.
 Mkuu wa wilaya wa Halmashauri ya Kinondoni Ally Hapi akizungumza na wajasiriamali  wa wilaya hiyo wakati wa mkutano ambapo amewataka watoe kero na changamoto zinazowakabili ili kuzifanyia ufumbuzi leo katika ukumbi wa King Solomon Jijini Dar es Salaam.
 Afisa maendeleo ya Jamii  kata ya Ndugumi Halmashauri ya Kinondoni, Zuwena Mtani akifafanua jinsi ya kufanya kwa wajasiriamali hao ili kuweza kupata mikopo hiyo leo katika ukumbi wa King Solomon Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajasiriamali waliojitokeza kwa wingi katika mkutano leo ukumbi wa King Solomon  Jijini Dar es Salaam kutoa kero na changamoto zinazowakabili kwa DC Hapi.

UMOJA WA RUDISHA UZALENDO WAANDAA MAANDAMANO KUPONGEZA JUHUDI ZA RAIS

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam  kupitia Umoja wa Rudisha uzalendo Tanzania (RUTA) umepongeza juhudi za Rais Dk.John Magufuli na watendaji kazi wake katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini huku wakitangaza kufanya maandamano ya amani Aprili 12 mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo na Mratibu wa umoja huo Charles Masele amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wananchi wengi wamevutiwa na wanaunga mkono juhudi za Rais Magufuli, hivyo katika kumpongeza wameandaa maandamano ya amani yatayohusisha watu wa itikadi zote yatakayofanyika Aprili 12 mwaka huu kuanzia Karume hadi viwanja vya Mnazi mmoja kuanzia saa moja hadi saa tano asubuhi .

Wakizungumza zaidi  wadau hao wamesema hawana budi kuunga mkono juhudi za Rais kwani huduma nyingi zimeboreshwa zikiwemo miundombinu, afya hasa kwa akina mama na elimu ambayo hutolewa bure, pia mikopo ya elimu ya juu ambayo hutolewa kwa wanafunzi wa hali ya chini.

Aidha wameeleza utiifu wa Rais na watendaji wake wa serikali na taasisi binafsi kwa namna wanavyothamini na kuhudumu kwa haki na usawa hivyo wameona na vyema kumuunga mkono na kumuombea.

Pia umoja huo umewataka vijana na watu wa kada mbalimbali kuunga mkono juhudi hizo kwani zinafanywa kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na baadaye.
 Mratibu wa Umoja wa Rudisha Uzalendo Tanzania (RUTA), Charles Masele  akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu maandamano ya amani yatayohusisha watu wa itikadi zote yanayotarajia kufanyika Aprili 12 April mwaka huu, Picha na Emmanuel Massaa, Globu ya jamii,
Mratibu wa umoja huo,Charles Masele akifafanua jambo

TAVITA YALAANI UCHOCHEZI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WANASIASA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
TAASISI ya Taasisi ya Taswira ya Vijana Tanzania (TAVITA) imelaani vikali uchochezi unaofanywa na baadhi ya wanasiasa kupitia mitandao ya kijamii dhidi ya Serikali ya Awamu ya tano.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa TAVITA Otieno Peter amesema Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi kama vile kuanzisha miradi mikubwa kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania na kurejesha nidhamu kwa watumishi wa umma.

Pia imejikita katika kusimamia rasilimali za nchi, kuhimiza uwajibika na kukomesha vitendo vya rushwa.Hivyo inasikitisha kuona baadhi ya watu wakitumia muda wao mwingi kuchochea uvunjifu wa amani badala ya kuelimisha jamii na endapo amani itapotea itakua imeharibu dira ya nchi yetu.

Ameviomba vyombo vya habari kutumia kalamu zao katika kuelimisha kuhusu masuala ya maendeleo kwa maslahi ya Taifa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa taasisi hiyo Shabani  Mwanga amewataka wananchi kutokubali taarifa zinazotolewa kwa ajili ya kuharibu taswira njema ya nchi kwani hao wanaofanya hivyo wanataka kuvuruga amani ya nchi iliyopo.

"Kamwe tusikubali kuyumbishwa na mawakala ambao wanatumia saa 24 kutoa taarifa za kupaka matope ili kuharibu taswira njema ya taifa letu,"amesema .

Ameongeza taasisi ya Taswira ya Vijana Tanzania ipo tayari kupambana kwa hali yoyote na watu hawa wanaotaka kuchafua amani ya nchi na kwamba wapo tayari kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli kwa maendeleo ya taifa.
 Katibu wa (TAVITA),Otieno Peter (kushoto) akizungumza kuhusu mambo ya maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano ikiwemo miradi ya kufufua umeme na ujenzi wa reli ya kisasa  leo jijini Dar es  Salaam. Kulia ni  Mwenyekiti wa TAVITA, Shabani Mwanga(kulia)
Waandishi wa habari wakimsikiliza  Katibu wa (TAVITA), Otieno Peter

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>