Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

MAANDALIZI YA MFUMO WA PAMOJA WA KIELEKTRONIKI WA UONDOSHAJI SHEHENA YAANZA

0
0

Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam,

Serikali imeanza maadalizi ya kutengeneza Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau mbalimbali wa sekta binafsi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema lengo la kuwashirikisha wakuu hao ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mfumo huo.

“Uwepo wenu katika mkutano huu ni muhimu sana kwasababu mtaweza kupitia mahitaji yote ya mfumo yaliyoandaliwa na watalaamu wetu ikiwa ni pamoja na maeneo ya kisheria, kiufundi na kibiashara ili muweze kuuboresha zaidi”, alisema Kichere.

Kichere alieleza kuwa, uwepo wa wakuu hao na wadau wa sekta binafsi katika mkutano huo ni kiashiria cha kuunga mkono adhma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga mazingira bora ya kufanya biashara ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kamishna huyo Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliongeza kuwa, Serikali imelenga kuwawezesha wadau wote wanaohusika na biashara za kimataifa na usafirishaji wa mizigo kutumia Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena kwa lengo la kuwezesha uwasilishaji wa nyaraka mahali pamoja ili wadau wote waweze kushughulikia nyaraka hizo kwa wakati.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani pamoja na wadau mbalimbali wa sekta binafsi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mussa Shilla.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari akitoa mchango wake wakati wa mkutano huo.

Mwakilishi wa Mkemia Mkuu wa Serikali Daniel Ndiyo akichangia hoja leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani pamoja na wadau mbalimbali wa sekta binafsi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua ugawaji vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu

0
0
Wizara ya afya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria katika juhudi zake za kupambana na ugonjwa wa Malaria kinakusudia kutoa vyandarua laki moja na 95 elfu kwa mama wajawazito na watoto waliochini ya miaka mitano nchi nzima .

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar juu ya uzinduzi wa Kampeni ya kubwa ya matumizi ya vyandarua ambayo inatarajiwa kufanyika April nne mwaka huu visiwani Zanzibar Meneja wa utaribu wa kazi za kumaliza Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ali amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimokatika mchakato wa kumaliza Malaria ambapo kwa sasa ni zaidi ya miaka kumi Zanzibar imekuwa ikipambana na ugonjwa huo .

Amesema Zanzibar kila kipindi kinachomaliza mvua za masika kumekuwa na kiwango kikubwa ugonjwa Malaria lakini jitihada mbali mbali zinachukuliwa ikiwemo kupiga dawa majumbani, kuhakikisha dawa zinapatikana katika vituo vya afya, na kuwepo kwa vipimo cha kuchunguzia ugonjwa huo na matumizi ya vyandarua vilivyopigwa dawa.

Amesema vyandarua ndio kinga tahabiti ya kujikinga na Malaria ambapo kwa Zanzibar Asilimia 77 ya Wananchi wanatumia vyandarua kiwango ambacho bado hakijaridhisha kufikia vigenzo vya wizara ya afya zanizbar ya Asilimia 100 na shirika la afya ulimwenguni WHO Asilimia 85. 


Meneja wa kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ally akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar wakati akitangaza kuanza kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria.
Meneja Miradi kutoka VectorWorks akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar wakati akitangaza kuanza kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti .


NAIBU WAZIRI SHONZA NA DIAMOND WAFIKIA MUAFAKA

MAGAZETI YA LEO AL-HAMISI MARCH 29,2018

MAANDALIZI YA MFUMO WA PAMOJA WA KIELEKTRONIKI WA UONDOSHAJI SHEHENA YAANZA

0
0
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani pamoja na wadau mbalimbali wa sekta binafsi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mussa Shilla.
Mwakilishi wa Mkemia Mkuu wa Serikali Daniel Ndiyo akichangia hoja leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani pamoja na wadau mbalimbali wa sekta binafsi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi.

Na Veronica Kazimoto,
SERIKALI imeanza maadalizi ya kutengeneza Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau mbalimbali wa sekta binafsi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema lengo la kuwashirikisha wakuu hao ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mfumo huo.

“Uwepo wenu katika mkutano huu ni muhimu sana kwasababu mtaweza kupitia mahitaji yote ya mfumo yaliyoandaliwa na watalaamu wetu ikiwa ni pamoja na maeneo ya kisheria, kiufundi na kibiashara ili muweze kuuboresha zaidi”, alisema Kichere.

Kichere alieleza kuwa, uwepo wa wakuu hao na wadau wa sekta binafsi katika mkutano huo ni kiashiria cha kuunga mkono adhma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga mazingira bora ya kufanya biashara ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Kamishna huyo Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliongeza kuwa, Serikali imelenga kuwawezesha wadau wote wanaohusika na biashara za kimataifa na usafirishaji wa mizigo kutumia Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena kwa lengo la kuwezesha uwasilishaji wa nyaraka mahali pamoja ili wadau wote waweze kushughulikia nyaraka hizo kwa wakati.

Naye Mratibu wa Mfumo wa Uondoshaji Shehena kutoka TRA Felix Tinka amezitaja faida za mfumo huo  kuwa ni pamoja na kurahisisha na kuwezesha biashara, kuongeza ufanisi wa matumizi bora ya rasilimali na kuongeza uhiari wa ulipaji ushuru na tozo mbalimbali kwa waingizaji na waondoshaji wa mizigo.

“Mfumo huu una faida nyingi, mbali na hizo nilizozitaja awali, pia kuna kuimarisha usalama, kuimarisha uadilifu na uwazi katika utendaji kazi, kupunguza biashara haramu, kupunguza gharama, kupunguza muda wa uondoshaji mizigo katika vituo vya forodha pamoja na kurahisisha ufuatiliaji wa mizigo kwa wakati”, Alisema Tinka.
Utekelezaji wa Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani umegawanyika katika maeneo makuu matano ambayo ni eneo la usimamizi wa mapato, uwezeshaji wa usafiri na uchukuzi, utekelezaji wa sera na biashara, pamoja na usimamizi wa afya na usalama wa umma, usalama wa uchumi pamoja na ugawaji.

AGPAHI YAKABIDHI MASHINE ZA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI,KOMPYUTA MKOA WA MWANZA

0
0
Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi mashine tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’ mkoa wa Mwanza. 

Msaada huo umetolewa Jumanne Machi 27,2018 katika ukumbi wa mikutano wa Gold Crest Hotel jijini Mwanza wakati wa kikao cha wadau wanaohusika katika mapambano ya VVU na Ukimwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kupanga mipango na mikakati ya kupambana na VVU na Ukimwi. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema mashine hizo ni kwa ajili ya vituo vya afya vya Katunguru na Kabila vilivyopo wilaya ya Sengerema, hospitali ya Ngudu iliyopo wilayani Kwimba na zahanati ya Kirumba na kituo cha afya cha Buzuruga vilivyopo wilayani Ilemela. 

Dk. Sekela alisema mashine hizo tano zenye thamani ya shilingi milioni 6.8 zitatumika kutolea tiba mgando kwa akina mama wanaokutwa na dalili za mwanzo za kansa ya uzazi. “Mbali na shirika letu kuendelea kuboresha huduma za kinga na matunzo pia tunatoa huduma ya uchunguzi wa dalili saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama”,alieleza. 

Alisema huduma hiyo hutolewa katika vituo vya kutolea huduma ya afya 20 katika mkoa wa Mwanza. Dk. Sekela alisema shirika hilo mpaka sasa limetoa msaada wa ‘cryotherapy machines’ 17 katika mikoa sita ambayo ni Mwanza,Shinyanga,Tanga,Geita,Simiyu na Mara zote zikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 115.6. 

Dk. Sekela pia alikabidhi kompyuta 18 zitakazotumika kuhifadhi takwimu za wateja wa CTC katika vituo vya afya husika na kusaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka na kwa usahihi Zaidi mkoani Mwanza. “Tangu tuanze mradi wa Boresha, tutakuwa tumetoa jumla ya kompyuta 82 kwa mkoa wa Mwanza ambazo zinatumika kutunza taarifa za watu wenye VVU na Ukimwi”,alisema. 
Kulia ni Dk. Mwakyusa akiwa ameshikilia moja ya mashine inayotumika kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’. 
Dk. Sekela akizungumza ukumbini. 
Katikati ni Dk. Sekela Mwakyusa akikabidhi mashine kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella (wa pili kushoto) na viongozi wa wilaya ya Sengerema. 
Zoezi la makabidhiano likiendelea. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa CDC nchini, Dk. Eva Matiko. 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MFUMO MPYA WA MALIPO YA LUKU

0
0


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wote wanao tumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, 2018 TANESCO itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG) kama matakwa ya sheria kwa Taasisi za Serikali.

TANESCO ikiwa miongoni mwa Taasisi za Serikali, itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi za TANESCO, Kampuni za simu pamoja na Benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki.
Serikali kwa kushirikiana na Wataalamu wa TANESCO itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike kwamba, TANESCO ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa Taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio, baadhi ya Taasisi hizo ni Polisi, Brella, Ardhi, TRA pamoja na Mamlaka za maji.
TANESCO inapenda kuwahakikishia wateja wote kuwa mbali na Kampuni za simu ofisi zote za Shirika na vituo vya mauzo ya LUKU vitaendelea kutoa huduma katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka.

TANESCO ‘‘Tunayaangaza Maisha yako’’
Kwa mawasiliano
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:
Mitandao ya kijamii
IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
MACHI 27, 2018

RC MASENZA AWAPONGEZA RDO KWA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWENYE BAADHI YA VIJIJI VYA WILAYA YA MUFINDI NA KILOLO

0
0

 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimtusha ndoo ya maji mmoja ya wananchi walihudhulia uzinduzi wa mradi maji ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.

 Na Fredy Mgunda,Iringa. 
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kwa kufanikisha kupatikana kwa maji katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Kilolo na Mufindi ambayo itakuwa njia moja wapo ya kuchochea maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Nandala’ Masenza alisema kuwa amefurahishwa na mfumo ambao unatumiwa na shirika hilo kwa kutoa huduma ya maji kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika.

“Mradi wowote ule ukiwa na ushirikiano mkubwa na wananchi mara nyingi wananchi wanautunza mradi huo kwa kuudhamini na kuulinda,hivyo nawapongeza RDO kwa kufanya maamuzi sahihi ya kubuni mradi huo pamoja na wananchi” alisema  Masenza

Masenza alisema kuwa mradi huo wa maji utatoa huduma kwa wananchi wengi na taasisi binafsi nyingi hivyo wananchi wanatakiwa kuutunza na kuudhamini ili udumu kwa muda mrefu na kuondoa tatizo la maji ambalo limekuwa kero ya muda mrefu.

Nimesikia kwenye risala yenu kuwa mradi huu utahudumia kata zifuatazo Ifwagi,Mdabulo,Ihanu,Luhunga,Mtitu na Kising’a na vijiji vitakavyopata huduma hiyo ni Igonongo,Ludilo,Kidete,Ikanga,Nandala,Ibwanzi,Isipii,Mkonge,Lulanzi,Luhindo,Barabara mbili na Isele hivyo ukiangala utagundua kuwa mradi huu ni mkubwa na upaswi kupuuzwa kwa maendeleo kwa wananchi wa maeneo ambayo mradi huo umepita.

“Jamani wananchi ambao mmepata bahati ya kupitiwa na mradio huu mkubwa wa maji mnapaswa kuulinda na kuudhamini kwa kuwa ni mmoja ya mradi mkubwa ambao unapunguza adha ya upatikanaji wa maji ambayo hapo awali ilikuwa kero kubwa” alisema Masenza

Kwa upande mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali alisema kuwa mradi huo umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100) ambao ndani yake kuna pesa zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya kusaidia kupata huduma ya maji.

“Sisi kama RDO ambao ndio wafadhili namba moja wa mradio huu wa maji tumechangia kiasi cha shilingi milioni themenini na sita,laki nane ishirini na moja elfu (86,821,000) na wananchi walichanga kiasi cha shilingi milioni nane,laki sita themenini na mbili na mia moja (8,682,100)” alisema Filipatali

Filipatali  alisema kuwa mradi huo wa maji  utazaliza ujazo wa lita 776  kwa vijiji vyote ambazo vinatumia huduma hiyo ya maji na pia wananchi watakao pata huduma hiyo ni 10,874 kwa vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi huo na jumla ya taasisi 18 nazo zitanufaika na huduma hiyo.

“Mkuu wa mkoa sasa ukiangalia kwa ujumla ndio utagundua kuwa ni mradi ambao utakuwa unakomba wananchi wengi waliokuwa wanapata tabu juu ya kupata maji hivyo naomba pia nisisitize wananchi kuutunza na kuchangia kwa malipo kidogo kwa ajili ya ukarabati wa mashine na mitambo mingie inayosukuma maji hayo ili isihalibike” alisema Filipatali

Filipatali alisema kuwa mradi huo unakabiliwa na changamoto zifuatazo baadhi ya watumiaji maji kutochangia, viongozi kutotimiza majukumu yao kama kutohudhuria mikutano ya mapato na matumizi,watumiaji maji kutotilia mkazo elimu wanayopewa na wataalamu wa maji,siasa kuingia mfumo mzima wa mradi huu na baadhi ya serikali za vijiji kuchukulia mapato ya miradi ya maji kama sehemu ya mapato ya serikali  kitu ambacho sio kweli mfano kjiji cha Lidilo


“Hizi changamoto zimekuwa kero sana kwenye miradi ambayo imekuwa inatekelezwa kwenye maeneo husika hivyo niwaombe viongozi wa kiasa wawe wa kwanza kutoa elimu juu ya miradi ambayo inafaida na kutatua changamoto za wananchi kwenye maeneo yao” Filipatali

WANANCHI WENGI WANA IMANI KUBWA NA TAARIFA ZINAZOTOLEWA NA RAIS, WAZIRI MKUU-TWAWEZA

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WANANCHI wengi wamesema wana imani kubwa na taarifa zinazotolewa na Rais kwa asilimia 70  na Waziri Mkuu kwa asilimia 64 huku idadi ndogo zaidi wanamwamini mwenyekiti wao wa kijiji kwa asilimia 30, wabunge  wa chama tawala asilimia 26 na  wa upinzani asilimia 12 wakati viongozi wa Serikali kwa ujumla ya asilimia 22.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze wakati anatoa matokeo ya Twaweza yalitokana na utafiti uliofanyika uliojukana kama muhtasari  uitwao Siyo kwa kiasi hicho? 

Pia maoni ya wananchi kuhusu taarifa na mijadala ambapo Eyakuze anafafanua takwimu za muhtasari huo zinatokana na utafiti wa Sauti za Wananchi ambao huratibiwa na taasisi ya yao.Sauti za Wananchi ni utafiti wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.

"Matokeo ya utafiti unaonesha wananchi wengi kuwa na imani kubwa na taarifa zinazotolewa na Rais na Waziri Mkuu,"amesisitiza.

Pia amesema wananchi wanaendelea kuunga mkono kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa taarifa ambapo  wananchi 7 kati ya 10 wanasema taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma ni mali ya umma ni asilimia 70 juu zaidi kutoka asilimia 60 mwaka 2015).

"Na wananchi 9 kati ya 10 wanasema wananchi wa kawaida wapate taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma kwa asilimia 86  juu zaidi kutoka asilimia 77  mwaka 2015) na kwa kuwapa wananchi uwezo wa kupata taarifa kunaweza kupunguza rushwa asilimia 86 , juu zaidi kutoka asilimia 80 mwaka 2015.

"Pamoja na kuunga mkono kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa taarifa, wananchi 9 kati ya 10 hawajawahi kuomba taarifa kutoka katika ofisi za serikali kwa asilimia 95 , mamlaka za maji asilimia 93 , au vituo vya afya  asilimia 93,"amesema. 

Ameongza utafiti unaonesha kuwa wananchi wameendelea kutumia vyanzo vile vile vya habari bila kuwa na mabadiliko makubwa isipokuwa kwa upande wa runinga ambapo mwaka 2013 runinga ilikuwa ni chanzo kikuu cha taarifa kwa asilimia 7 ya wananchi na mwaka 2017 ni asilimia 23 ya wananchi. 

Eyakuze amesema hata hivyo imani kwa aina mbalimbali za vyanzo vya habari inashuka .Radio kutoka asilimia 80 mwaka 2016 hadi asilimia 64 mwaka 2017, runinga kutoka asilimia 73 mwaka 2016 hadi asilimia 69 mwaka 2017 na maneno ya kuambiwa kutoka asilimia 27 mwaka 2016 hadi asilimia 13 mwaka 2017.

 "Pamoja na kushuka kwa imani na vyombo vya habari, wananchi bado wanaunga mkono uhuru wa vyombo vya habari kwani  wananchi wanasema gazeti lililochapisha taarifa za uongo ama zisizo sahihi liombe radhi na kuchapisha marekebisho ni asilimia 62 badala ya gazeti hilo kufungiwa ama kutozwa faini asilimia 38. 

"Idadi kubwa ya wananchi pia wanasema kuwa Serikali ipate ridhaa ya mahakama katika kufanya maamuzi yoyote ya kuliadhibu gazeti kwa kutoa taarifa zenye  maudhui yasiofaa kwa asilimia 54.Japokuwa wananchi wana mtazamo thabiti kuhusu upatikanaji wa taarifa na uhuru wa kuzungumza, ni wananchi wachache sana wanaofahamu sheria zinazohusiana na masuala ya habari,"amesema. 

Kuhusu Sheria inayofahamika zaidi katika suala hilo ni Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015), ambayo inafahamika na asilimia 10 ya wananchi huku asilimia 4 pekee ya wananchi wakifahamu Sheria ya Huduma za Habari (2016). 

Pia wananchi wengi pia hawajaunganishwa kwenye mifumo ya uraia ambapo ni mwananchi 1 kati ya 4 au pungufu mwenye cheti cha kuzaliwa asilimia 25, kitambulisho cha uraia asilimia 21, leseni ya udereva asilimia 9 na hati ya kusafiria asilimia 5. Hata hivyo, karibu wananchi wote asilimia 98 wana vitambulisho vya mpiga kura

Eyakuze, anamesema wananchi wanaunga mkono kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa taarifa na uhuru wa kujieleza lakini ukweli wa mambo ni kwamba hawaombi taarifa hizo, wana imani duni na vyanzo vyote vya taarifa ukiweka kando kauli zinazotolewa na Rais na Waziri Mkuu, na hawajioni kama wanaweza kuwakosoa viongozi wakuu wa serikali.

 “Kutokana na kwamba hivi karibuni serikali imepitisha kanuni za Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa tuna imani kuwa itakidhi kiu ya wananchi ya kupata taarifa kutoka serikalini. 

"Tunaishauri Serikali kuweka wazi taarifa ili kuyafikia matarajio ya wananchi. Cha kusikitisha, wananchi wanakamatwa na serikari kwa kujieleza kupitia mitandao ya kijamii. Ni vyema serikali ikatambua thamani ya mijadala huru ya umma na ukosoaji wenye lengo la kujenga katika mapambano dhidi ya rushwa na katika harakati za kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati,"amesema.

Akifafanua kuhusu utafiti huo amesema uwakilishi wa Tanzania Bara pekee, Zanzibar haihusiki  na kwa  maelezo zaidi kuhusu mbinu za utafiti huu kwa anayetaka kujua zaidi atembelee www.twaweza.org/sauti. Takwimu za muhtasari huo zilikusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,519 kutoka awamu ya 25 ya kundi la pili la Sauti za Wananchi, na zilikusanywa kati ya Novemba 7 na Novemba 27 mwaka 2017.

Wakulima wapata wigo mkubwa wa mazao ya kupanda baada ya kunganishwa vijiji na mtandao wa intaneti wa simu

0
0
Jakulima sasa wapata  wigo mkubwa zaidi wa aina ya mazao ya kupanda baada ya kunganishwa kwa vijiji na mtandao wa intaneti wa simu. Tazama video na ujifundishe pia.




CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KUANZISHA KAMPASI KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA MASOMO YA USIMAMIZI WA BIASHARA.

0
0
Na John Nditi, Morogoro
UONGOZI wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM) kinatarajia kujenga kampasi  tawi la Kigamboni, Jijini Dar es Salaam  itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara na kwa kuanzia na udahili wa wanafunzi 5,000.

Chuo hicho  Kampasi ya  Kigamboni ni kuwezesha  kupata wataalamu wengi wa  usimamizi wa biashara watakaokidhi  mahitaji  ya soko la ajira katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki  pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Makamu mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Hamza Njozi,alisema  wakati wa uwekeji wa jiwe la msingi  kitakapojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya Kigamboni , Jijini Dar es Salaam.

Profesa Njozi alisema, tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho Oktoba 23, 2004 chini ya Mfuko wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF) na kilizinduliwa rasmi Oktoba 22, 2005 na  Rais wa Serikali ya awamu ya tatu , Benjamin William Mkapa .

Makamu Mkuu wa Chuo hicho alisema, hadi  kufikia mahafali ya kumi mwaka jana ,kimeshatoa wahitimu 5,433 wa ngazi ya Shahada, Stashahada na Astashahada  ambapo  kwa sasa kina zaidi ya wanafunzi 3,000 na uwezo wa chuo ni kuchukua wanafunzi 8,000.

Profesa Njozi  alisema , kujengwa kampasi  Tawi la Kigamboni kunatarajiwa kuongeza udahili wa wanafunzi wa ndani na n je ya nchi baada  ya uongozi wa Chuo kupata  eneo la ardhi lenye  ukubwa wa ekari 400 kwa ajili ya ujenzi huo.
 Makamu mkuu wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM) , Profesa Hamza Njozi akipanda mti baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi yake  itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II, Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
 Makamu mkuu wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM) , Profesa Hamza Njozi ( wapili kushoto  fulana pundamilia) akibadirishana mawazo na mmoja wa viongozi wa Chuo hicho baada ya  uwekaji jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi ya Kigamboni  itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi  wakiume  wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakisaidia kubeba tofari  hadi eneo la  uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi  ya Kigamboni  itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wanafunzi wakike wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM)  wakisaidia kusogeza mfuko wa saruji kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi  yake itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SAM KAMANGA WA 'ATI' AWATAKA WADAU WA BIMA WAWEKEZE KWENYE TEKNOLOJIA

0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Bima Tanzania (ATI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Taifa (NIC) Sam Kamanga akiwa na watendaji wake jana katika banda la NIC Mlimani City wakati wa maonyesho ya wadau wa sekta ya bima kandokando ya mkutano wao maarufu kama African Insurance Summit 
Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Bima Tanzania (ATI) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akizungumza wakati wa mkutano huo. 
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Usimamizi wa Bima wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elia Kajiba akizungumza wakati alipotembelea banda Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwenye maonyesho ya makampuni ya Bima nchini yaliyofanyika jana Mlimani City Jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT), kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Bima Tanzania (ATI) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga na kulia ni Afisa Bima Mwandamizi wa NIC Konjeta Mwaipopo.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko waShirika la Bima la Taifa Elisante Maleko, akimkabidhi zawadi ya kikombe Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Usimamizi wa Bima wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elia Kajiba alipotembelea banda la NIC katika maonyesho ya wadau wa bima Jijini Jana 
Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Bima Tanzania (ATI) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga (Kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Usimamizi wa Bima wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Elia Kajiba kando kando ya mkutano huo wa wadau wa bima African Insurance Summit 

Mbulu yapatiwa fedha za kuhamia Haydom

0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, imepokea kutoka serikali kuu kiasi cha sh1 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu mapya yatakayojengwa Mji mdogo wa Haydom. 

Pia, kwenye bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 Halmashauri hiyo imetengewa sh. 2.3 bilioni za ujenzi wa jengo la ofisi na nyumba za kuishi watumishi. 

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Hudson Kamoga aliyasema hayo jana wakati akizungumza juu ya mikakati ya ujenzi wa makao makuu mapya yatakayojengwa Haydom. 

Alisema baada ya kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo kupitisha uamuzi wa ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo kuwa Haydom, hivi sasa wapo kwenye mchakato wa utekelezaji. 

"Hadi mwakani kipindi kama hiki tutakuwa tumeshahamia kwenye makao makuu mapya ya halmashauri yetu kule Haydom na kuondoka hapa Mbulu mjini," alisema Kamoga
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akimkabidhi zawadi ya daftari mwanafunzi wa darasa la tatu wa shule ya msingi Barazani Kata ya Maghang, Julieth John kutokana na utunzaji bora wa vyanzo vya maji na mazingira, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga akizungumza na wananchi wa Kata ya Maghang juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MZUKA WA SOKA NA COKA YAWAFIKIA KANDA YA KASKAZINI

0
0
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers, Chris Loiruk akiongea na wafanyakazi wakati wa uzinduzi wa promosheni.
Wafanyakazi wa Bonite wakisherekea kuzinduliwa kwa promosheni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Bonite wakiandamana katika mitaa ya mji wa Moshi wakati wa uzinduzi

*Kuangalia mashindano ya kombe la Dunia wakiwa majumbani kwao
Wakati mashindano makubwa na maarufu ya soka ya Kombe la Dunia 2018 yanakaribia kuanza, kampuni ya Coca-Cola kupitia kampuni kiwanda cha Bonite Bottlers, imezindua promosheni kubwa itakayowawezesha watumiaji wa vinywaji yake kujishindia luninga bafa za kisasa (flat screen TV sets) zinakazowawezesha kufurahia mashindano ya soka ya Kombe la Dunia wakiwa wakiwa na familia zao majumbani kwao.

Promosheni hii mpya inajulikana kama “Mzuka wa Soka na Coka” na itanufaisha watumiaji wa vinywaji vinavyotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola ambavyo ni Coca-Cola, Sprite, Fanta, Sparletta, Schweppes Stoney Tangawizi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida.

Mbali na kujishindia luninga bapa za kisasa watumiaji wa vinywaji vya Coca-Cola kupitia promosheni hii wanayo fursa ya kujishindia zawadi kubwa ya pikipiki, fedha taslimu kuanzia shilingi 5,000/- hadi shilingi 100,000/- ikiwemo pia kujishindia soda za bure.

Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers, Chris Loiruk, amesema kampuni ya Coca-Cola ikiwa ni mdhamini mkuu wa mashindano yajayo ya Kombe la Dunia ,imewaandalia promosheni hii wakazi wa kanda ya Kaskazini ili kuhakikisha wanafurahia “Mzuka wa Soka na Coka” wakiwa majumbani kwao kupitia luninga za kisasa wakati huohuo wakiburudika na vinywaji vya Coca-Cola.

MADEREVA WAONYWA KUFANYA MBWEMBWE BARABARANI KIPINDI CHA SIKUKUU

0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la Polisi mkoani Pwani limewaasa madereva hususani wa mabasi yanayofanya safari za mikoani ,kuacha kufanya mbwembwe wakati wakiwa barabarani na kutumia vileo katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka ili kuepusha ajali zembe.

Aidha jeshi hilo limetoa onyo kali kwa wale wenye nia ya kutenda uhalifu kwenye kipindi hicho .

Akizungumza na waandishi wa habari na baadhi ya maofisa wa jeshi hilo ,kuhusiana na operesheni za kaguzi hizo ambazo ni endelevu ,na kutoa salamu za Pasaka ,kaimu kamanda wa polisi ,mkoani Pwani ,(SSP) Abdi Issango ,alisema madereva wafuate sheria za usalama barabarani bila kushurutishwa .

Amesema wanafanya operesheni ya kukagua madereva wa mabasi hayo na kufanikiwa kuwakamata madereva 29 kwa makosa ya mwendo kasi na kulipita gari la mbele sehemu isiyoruhusiwa (wrong overtaking).

Pamoja na hayo ,Issango alielezea madereva 22 walikamatwa kwa kosa hilo na madereva saba walikamatwa kwa kosa la mwendo kasi .

Alibainisha dereva mmoja alipewa onyo kutokana na kosa lake ,madereva watano waliadhibiwa kwa kulipishwa faini ,na madereva 23 watafikishwa mahakamani kuweza kujibu mashtaka yanayowakabili .

"Katika operesheni hii ,dereva wa kampuni ya basi la Super Feo lenye namba za usajili T.754 DML linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam -Songea ,Peter Augustino (38) mkazi wa Makambako "

" Yeye tutamfikisha mahakamani kwa makosa mawili ya kulipita gari la mbele sehemu isiyoruhusiwa  na kuendesha gari akiwa ametumia kileo ambapo baada ya kumpima alikutwa akiwa na kilevi 26.8mg/ml.":;alisema Issango.

Kwa mujibu wa Issango machi 28 mwaka huu jeshi hilo limeendesha msako katika maeneo mbalimbali katika mkoa huo na kufanikiwa kukamamata watuhumiwa 21 wakiwa na bangi kete 155 sawa na gramu 77.5.

Alisema huko Mapinga wilayani Bagamoyo ,walimkamata Wilson Jengua akiwa na mtambo mmoja wa kutengeneza pombe ya moshi(gongo) .

"Mbali ya mtambo huo ,tumekamata pombe hiyo lita 62 " alifafanua Issango.

Issango ambae pia ni kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani, alieleza watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao .

Aliwasihi wahalifu wenye mawazo ya kufanya uhalifu kipindi cha Pasaka wabadili mawazo hayo, kabla ya hatari kwani jeshi hilo limejipanga kikamilifu kupambana na uhalifu wa aina yoyote.

KARIBU JUMAPILI YA PASAKA DMV

WARAMI WAISHUKIA KAMATI KUU CHADEMA, KUINGILIA UHURU WA MAHAKAMA

0
0
Na Mwandishi Wetu
WATETEZI wa Rasilimali Wasio na Mipaka(Warami)limesema limesikitishwa na kitendo cha Kamati kuu ya Chadema kuingilia uhuru wa Mahakama baada ya jana kuitisha mkutano kuzungumzia mambo yalipo mahakamani.

Warami wameongeza kuwa si tu kuingilia uhuru wa mahakama pia chama hicho kimekwenda mbali zaidi kwa kutoa masharti yanayoashiria uvunjifu wa amani iwapo Mwenyekiti wa Freeman Mbowe na viongozi wengine watanyimwa dhamana leo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugunzi wa Utafiti wa Warami Philipo Mwakibinga amesema jana baadhi ya viongozi wa Chadema kupitia mkutano wao wameonesha dhahiri kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kuanza kushinikisha maamuzi ya Mahakama.

“Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema, Profesa Abdallah Safari na wenzao wakiwa wanajua kuwa Mahakama ni chombo cha haki walitengeneza mazingira ya kuonesha kuwa viongozi hawatetendewi haki kama hawatapa dhamana leo.

“Wanafanya hivyo wakijua wazi jambo hili limelenga kuishawishi , kushinikiza na kuilazimisha mahakama ifanye watakavyo wao kwa kuacha misingi ya haki wajibu na maadili ya kimahakama,”amesema Mwakibinga.

Amefafanua Watanzania ni mashahidi Mbowe na wenzake ambao wapo Mahakamani wamekamatwa kama matokeo ya matendo yao ya kushawishi na kuchochea chuki miongoni watanzania jambo ambalo si la kiutamaduni kwa Taifa.


“Warami tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa sheria ni kama kaa la moto na unapovunja sharia lazima ujue umeamua kushika kaa la moto kwa hivyo lazima ujiandae kuungua.

“Tunawakumbusha Chadema ,hasa wakina Lema na wenzao watii sheria , waache maneno ya kichochezi yasiyo ya kiuongozi na wasiendelee kuropoka ropoka, zama za kuwachekea waropokaji zimepitwa na wakati,”amesema.

Mwakibinga amesema Lema kukamatwa kwa viongozi wa chama chake ni mkakati uliopangwa na Serikali kwa ajili ya kuwakomoa.

Amesema Warami wanawapa changamoto Chadema , wamuulize Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ajitokeze hadharani wakati Augustino Mrema akiwa NCCR-Mageuzi na baadae TLP alivyokuwa anakamatwa na vyombo vya dola je alikuwa analazimisha vyombo vya dola vimkamate wakati Mrema hakuwa na makosa kwa wakati ule.

“Chadema waache kuharibu sifa ya vyombo vyetu vya kiusalama hasa idara nyeti ya Usalama wa Taifa kwa kuwasingizia mambo ya ajabu ajabu kwa ajili ya kuficha udhaifu wao wa kuimarisha chama,”amesema Mwakibinga.

Ameongeza Warami inawataka Chadema kuacha kukimbia kivuli chao na waswahili wanasema ‘ukilikoroga lazima ulinywe’ .

“Hivyo Chadema walinywe kwa kadiri ya walivyorikoroga.Pia iache Mahakama itafisiri sheria na kwa kuwa wameweka wanasheria wanaowaamini, wawahimize wanasheria wao kuhakikisha wanashinda kesi zinazowakabili,”amesisitiza.


KUHUSU MAASKOFU KUTUMIKA
Mwakibinga amesema mara ya mwisho walihoji iwapo maaskofu wanatumika na vyama vya siasa hasa Chadema.

“Nafikiri wote sasa tumejiridhisha kuwa maaskofu wetu wameamua kutumika kulipa fadhila za waliokuwa wanawapa fedha katika zama za kufanya harambee ya fedha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.

“Matukio ya Chadema kuunga mkono hadharani waraka wa maaskofu ,ACT Wazalendo kunifukuza uanachama kwa mimi kuwakosoa maaskofu na Maalim Seif kutangaza hadharani anaunga mkono madudu yale ya maaskofu,”amesema.

Ameongeza hivyo ni vishiaria na kuthibitisha wazi maaskofu wameamua kutumika na kuyaacha maelekezo na mafunzo ya dini yanayotaka kilicho cha kaisari apewe kaisari na kilicho cha Mungu apewe Mungu.

Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wanasiasa, wanaharakati , wanahabari , viongozi wa dini , taasisi binafsi waanzishe utaratibu wa kuheshimu uhuru wa Mahakama na kutoa kauli za mashinikizo.
Mkurugenzi wa Utafiti kutoka Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI),Philipo Mwakibinga , akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Kamati Kuu ya Chadema uliofanyika jana ukiwa na lengo la kuingia uhuru wa Mahakama.
Mkurugenzi wa Utafiti kutoka Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI),Philipo Mwakibinga, akiwaeleza jambo waandishi wa habari yaliyojiri katika mkutano mkuu wa Chadema.

SERIKALI KUIMARISHA USIMAMIZI WA TAALUMA YA MAENDELEO YA JAMII NCHINI

0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) imeahidi kuimarisha taaluma ya Maendeleo ya Jamii ili iweze kuongeza tija katika jamii. 

Hayo yamesemwa mjini Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka wakati wa kikao cha wadau waliokutana kujadili rasimu ya mitaala na kupata maoni yatakayowezesha kuboresha mitaala ya vyuo hivyo.

Bi. Neema amesema kuwa Wizara itafuatilia kwa karibu utoaji mafunzo ya fani ya Maendeleo ya Jamii kwa vyuo vyake inavyovisimamia na pia kushirikiana na Mamlaka nyingine katika kufuatilia utoaji wa mafunzo hayo kwa Vyuo visivyosimamiwa na Wizara. 

“Kikao cha wadau cha kupitia mitaala ya vyuo vya maendeleo ya jamii kinajenga uwezo wa Wizara katika kuhakikisha usimamizi wa vyuo hivi unazingatia Kanuni na taratibu za Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jukumu ambalo Wizara imekuwa ikilitekeleza kila inapohitajika” alisisitiza Bi Neema. 

Akizungumza katika mkutano huo Kaimu Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George suala la kuwa na mkutano wa wadau kupitia rasimu ya mitaala ya vyuo vya Maendeleo ya Jamii ni hitaji la muhimu ili kupta maoni ya takayosaidia kkuboresha mada, mahudhui, mbinu, stadi za kufundishia na kujifunzia na maarifa.
 Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayesimamia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii,  Neema Ndoboka akieleza mpango wa Wizara katika kusimamia Sekta ya Maendeleo ya Jamii kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati akifungua Kikao cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro Kushoto ni Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George.
 Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Dkt. Bakari George akieleza dhumuni la kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii  kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii  wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro.
 Afisa Maendeleo ya Jamii, Bw. Abel Palala akiwasilisha mada kuhusu Mtaala wa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Stashahada katika  kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii  katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii waliokutana kujadili Mitaala pendekezi ya fani ya Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa TAFOLI Mjini Morogoro.
 Mhadhiri wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Simon Kilasala akitoa taarifa  ya utafiti wa Soko la ajira kwa wataalam wa Maendeleo ya Jamiki wakati wa  kikao cha  kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii  kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wanaokutana kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa TAFOLI Mjini Morogoro.
 Mkufunzi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba, Kidubya Kulamiwa akiwasilisha mada kuhusu Mtaala wa mafunzo ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Astashahada katika  kikao cha kupitia Rasimu ya Mitaala ya Fani ya Maendeleo ya Jamii  katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa Kikao hicho cha siku moja cha wadau wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii waliokutana kujadili Rasimu ya Mitaala ya fani ya Maendeleo ya Jamii kilichofanyika Mjini Morogoro.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VETA yakabidhi vyeti kwa wahitimu 26 wa VSOMO

0
0

Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga, akimkabidhi cheti mhitimu wa Mafunzo ya VSOMO kupiti mtandao wa Simu wa Airtel Tanzania, Elias Joseph. Katikati ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya, akizungumza wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga.
 Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga, akizungumza wakati wa kukabidhi Vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo ya VSOMO kupitia Mtandao wa simu wa Kampuni ya Airtel Tanzania.Kulia ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya
 Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Sospeter Mkasanga,akimkabidhi cheti mhitimu wa Mafunzo ya VSOMO kupiti mtandao wa Simu wa Airtel Tanzania, Mohammed Ali Mohammed.Katikati ni ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya.
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) leo imekabidhi vyeti kwa wanafunzi26 waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao kupitia aplikesheni ya VSOMO ambapo kati yao wanafunzi 18 ni kutoka VETA kipawa na 8 VETA Mwanza
VSOMO ni mfumo unaotoa mafunzo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao unaotolewa chini ya ushirikiano kati ya kampuni ya simu ya Airtel pamoja na Mamlaka ya mafunzo stadi VETA ambao unalenga kuleta tija katika mapinduzi ya elimu nchini.
Akiongea wakati wa kukabidhi vyeti, Mkuu wa VETA Kipawa, Bwn Sospeter Dickson Mkasanga aliwapongeza Airtel kwa kushirikiana nao katika  kuanzisha aplikesheni ya VSOMO inayowawezesha wanafunzi kupata masomo ya ufundi wakati wowote mahali popote nchini kupitia simu zao za mkononi. Pia aliwapongeza wanafunzi waliamua kutumia technologia ya simu katika mambo ya msingi na kupata vyeti”.
Mkasanga aliongeza kwa kusema lengo kubwa la kutumia mfumo huu wa njia ya mtandao ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa mafunzo ya ufundi katika maeneo mbalimbali nchini, jitihada zinazoenda sambamba na adhima ya Serikali ya kutoa elimu kwa wote hususani watanzania waishio katika maeneo ya pembezoni mwa nchi.
 tumeanza kuona jinsi mfumo huu umeanza kuleta tija ambapo mpaka sasa wanafunzi 105 wameshahitimu mafunzo yao na kati ya 36 wanafanya mafunzo ya vitendo katika vituo mbalimbali vya VETA nchini. Hii kwetu ni hatua kubwa kuelekea kuwawezesha watanzania wote kufikiwa na masomo ya ufundi ili kuwa na nguvu kazi yenye ueledi. Napenda kuwapongeza vijana wanahitimu masomo yao leo na kuwahamasisha jamii kuendelea kujiandikisha katika masomo haya”.
 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrce Singano Mallya “ tunajivunia kushuhudia mabadiliko katika matumizi ya technologia ya simu  kwa kuwezesha maelfu ya watanzania kusoma kupitia simu zao za mkononi. Lengo letu ni kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa kuwatengenezea program mbalimbali zitakazowasaidia kukuza ujuzi na kuleta ufanisi katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Tunaamini VSOMO utawavutia vijana wengi kujiunga na masomo ya ufundi kwani inaenda sambamba na ukuaji wa technologia, ni ya gharama nafuu na rahisi kupatikana kupitia simu zao za mkononi lakini pia  masomo yake yamedhibitishwa na mamlaka ya ufundi stadi VETA”.
“tunapenda kuendelea kuwahakikishia kuwa  Airtel itaendelea kushirikiana na VETA pamoja na mashirika mengine katika kuhakikisha inatumia techonologia ya simu kutatua changamoto na kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi kwa ujumla” aliongeza Mallya
Kozi 13 za ufundi zinapatikana katika aplikesheni ya VSOMO ni pamoja na  Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium,  Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

UFAFANUZI KUHUSU RIPOTI ZA MWAKA ZA MDHIBITI NA MKAGUZI MKU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) ZILIZOWASHILISHWA KWA RAIS/ CLARIFICATION ON SUBMISSION OF THE CAG'S ANNUAL GENERAL REPORTS TO THE PRESIDENT

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images