Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

SALAMU ZA WENYEVYITI WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE WAKATI WA UPOKEAJI WA RIPOTI YA CAG IKULU DSM


Rais Magufuli apokea ripoti ya hesabu za Serikali ya 2016/17 kutoka kwa CAG

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mezani kwake mara baada ya kuzipokea kutoka kwa CAG Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizowasilishwa katika taarifa hiyo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya kwenda kuifanyia kazi pamoja na Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali.
Baadhi ya Mawaziri waliohudhuri katika tukio la uwasilishwaji wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG wakifatilia kwa makini taarifa hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.


MBOWE NA VIONGOZI WENGINE WATANO WA CHADEMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

$
0
0
*Mahakama yaamua kuwanyima dhamana kwa usalama wao
*Hatma yao kujulikana Ijumaa iwapo watatoka mahabusu au la

Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho ambao wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wamepelekwa mahabusu baada ya upande wa Jamhuri kuwasilishwa maombi ya kuwanyima dhamana.

Mbali ya Mbowe wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Bara Salum Salum, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent Mashinji.
Hivyo ni baada ya kusikilizwa mabishano marefu ya upande wa Jamhuri na ule wa utetezi juu ya dhamana ya washtakiwa kama wapate au la, mahakama imesema itatoa uamuzi Machi 29 mwak huu, mshtakiwa Mbowe na wenzake wamepelekwa rumande.

Mapema upande wa Jamhuri uliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kunyimwa dhamana kwa washtakiwa kwa njia ya mdomo.
Akiwasilisha sababu za kupinga dhamana mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Mkuu Dk. Zainabu Mango amedai  ni kwa sababu za usalama wa jamii na nchi kiujumla kama ilivyoelezwa kwenye hati ya mashtaka.

Amedai wanatambua dhamana ni haki ya mshtakiwa lakini hakuna haki isiyokuwa na wajibu kwa mujibu wa katiba ya nchi. Kwani Mashtaka yao wanaashiria kutokutii amri yao kikatiba, utekelezaji wa haki binafsi unapaswa kuzingatia haki za watu wengine.

Alidai alidai kwamba makosa yanayowakabili yanahatarisha usalama nchi na kuwapa dhamana ni kuendelea kuwapa nafasi ya kuendelea kufanya makosa hayo.

"Jukumu la dhamana liko chini ya mahakama hii. Hata  hivyo kabla ya mahakama kutumia mamlaka yake kutoa ama kuzuia dhamana inapaswa kuangalia mazingira ya kosa husika", amedai Dk.mango. Ameiomba Mahakama kuzingatia maslahi ya umma kwa ujumla wake kwa hatari ya makosa wanayoshtakiwa nayo na usalama wa taifa.

Wakili Faraja alidai kuwa kama washtakiwa wataruhusiwa kurudi uraiani baada ya matamko hayo ni wazi kwamba haki ya upande wa pili itapotea, matamshi yaliyotolewa na washtakiwa yana madhara endelevu kwa watanzania kwani tuna taarifa za upelelezi kwamba baadhi ya mambo yaliyoongelewa, ushawishi uliotolewa unaonekana kuna utekelezaji wa kihalifu.
Akijibu hoja hizo Wakili wa utetezi Peter Kibatala amedai hakuna chochote cha kisheria kilichozungumzwa kutoka kwenye dawati, kilichoko mbele ya mahakama sio maombi ni pingamizi la dhamana na hakuna ushahidi wowote kwa yaliyosemwa.
Pia Kibatala amedai Wakili anashindwa kutofautisha askari mpelelezi na mawakili wasomi na Mahakama haiwezi kumnyima mtu dhamana kwa taarifa ambazo haziko mahakamani. Aliendelea kudai  hati ya mashtaka haina jina wala sahihi ya aliyeandaa jambo ambalo limekatazwa na Mahakama Kuu.

HOTUBA YA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI BAADA YA KUPOKEA RIPOTI YA CAG,MARCH 27, 2018

DC SOPHIA MJEMA AZINDUA UPANDAJI MITI, APIGA MARUFUKU WANAOPIKA BARABARANI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akipanda mti kuashiria uzinduzi wa wiki ya upandaji Miti katika wiaya hiyo.

Na Heri Shaaban
WILAYA ya Ilala jijini Dar es Salaam wazindua wiki ya upandaji miti katika wilaya hiyo ambapo mwaka huu wamepanga kupanda miti milioni 1.5.

Akizungumza leo Dar as Salaam wakati wa kuzindua kampeni hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema katika kukabiliana na tabia ya nchi na kuboresha mandhari wameendeleza kampeni endelevu ya upandaji miti kama ( Mti Wangu)ambayo ilizinduliwa mwaka Jana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaaam Poul Makonda.

" Katika Wilaya yangu ya Ilala tumezindua wiki ya upandaji miti na utunzaji wa miti ni mpango shirikishi ambapo manispaa yetu inashirikiana na wadau wa mazingira kupanda na kutunza miti katika msimu wa jua na mvua," amesema Mjema.

Ameongeza kampeni hiyo kila mti utakuwa na mmiliki wake hiyo maana halisi ya mti Wangu na kwamba miti ina faida nyingi  kwa jamij  yetu ikiwemo kutupatia matunda,kivuli, dawa za asili, mapambo ,kuzuia mmonyoko wa ardhi , hewa safi, kupunguza hewa ya ukaa na kuleta mvua.

Pia miti husaidia kupatikana mkaa na mbao. Aidha amesema misitu yetu inahifadhi wanyama pori ambao ni kivutio kwa watalii na kuipatia nchi yetu fedha za kigeni.

Amesema kila mwananchi wa wilaya ya Ilala hana budi  kuthamini uwepo wa mti katika mazingira yake na uzinduzi huo unakwenda  sambamba  na upandaji miti katika fukwe, zahanati, hospitali , Shule za msingi na Sekondari  kwenye kata na mitaa.

Ametoa mwito  kila mwananchi aliopo wilayani Ilala kupanda miti katika maeneo yanayowazunguka na viongozi wa halmashauri kuhakikisha miti wanapanda na ina kua ili mchakato huo uwe na tija.

Ameziagiza halmashauri kuwa na vitalu vya miti kwa ajili ya kupunguza gharama kubwa kununua miche kila mwaka pia waeshimu kauli mbiu ya mwaka huu (Tanzania ya kijani inawezekana panda mti kwa Maendeleo ya viwanda.).

Amepiga  marufuku  kupika barabarani ,chakula  wananchi kukatisha sehemu zilizopandwa miti , na kutema mate hovyo.

Kwa upande wake Diwani ya Chanika (CCM) Ojambi Masaburi amesema kata ya Chanika ina wakazi  40,000 na ameagiza wananchi wake kila kaya kupanda miti mitano  mpaka kufikia siku ya kilele miti 100,000 iwe imeshapandwa.

Masaburi amesema wanaunga na Mkuu wa Wilaya katika kutekeleza agizo la Serikali kama sehemu ya utekelezaji wa Ilani .

Mwaka Jana alipanda miti 29,000 na mwaka huu anatarajia kuvuka lengo  kupanda miti  zaidi ya mwaka jana.

RC Wangabo azigeukia NGOs na CSOs kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda kupambana na umasikini

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amezitaka asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali kuchukulia juhudi za uanziswaji wa viwanda nchini unaofanywa na serikali kama suala mtambuka na ukombozi kwa mwananchi katika kupambana vita dhidi ya Umasikini huku wakizingatia utunzaji wa mazingira na kushirikiana na SIDO.

Amesema kuwa takwimu zinaonesha kwamba takribani hekta 300,000 hadi 400,000 za misitu nchini huharibiwa kwa kuchoma Mkaa. Hivyo njia nyingine na muhimu kuokoa mazingira yetu ni kwa kuanzisha viwanda vya kutengeneza Mkaa kwa kutumia marando ya Mbao, Pumba za Mpunga, Mabua ya mahindi n.k. malighafi ambazo hupatikana kwa wingi Mkoani kwetu.

 “Kwa sababu hiyo ninapenda kutoa wito kwa NGOs na CSOs kushiriki kwenye kampeni hii ya uanzishwaji wa viwanda yenye kaulimbiu ya Mkoa wetu, Viwanda vyetu kwa kuanzisha viwanda. Viwanda tunavyovilenga ni vile vidogo vya thamani ya kuanzia milioni 2 hadi Milioni 10,” Alisisitiza.

Kwa upande wake Meneja wa SIDO Emanuel Magere amesema kuwa asasi pamoja na mashirika hayo yamekuwa yakitoa elimu mbalimbali kutegemea matatizo ama changamoto za wananchi lakini imefika wakati kutambua kuwa, wananchi hao wanahitaji pia elimu ya ujasiliamali ili kuanzisha viwanda, na kuziomba taasisi za fedha kuweza kutoa mikopo kwa wanaohitaji kuanzisha viwanda.

“Mwamko katika uazishwaji wa viwanda sio mkubwa sana, wengi wamekuwa wakijiwekeza kwenye sekta ya huduma mfano, mashule, migahawa, maduka na huduma mbalimbali ambayo “return” yake inakuwa ya haraka kuliko viwanda na pia changamoto ya masoko ya bidhaa za ndani ya mkoa kutoka kwa bidhaa za nje ya mkoa ama nje ya nchi imekuwa ni changamoto kwa mkoa,” Alimalizia.

Katika kuhimiza ushirikiano Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda amezitaka NGO na CSO hizo kuweza kufika kwenye ofisi za kiserikali ili kuweza kujitambulisha shughuli wanazofanya na kujitokeza kwenye songambele mbalimbali zinazofanywa na halmashauri katika ujenzi wa madarasa ya shule na vituo vya afya ili michango yao ijulikane na sio kusubiri kutafutwa na serikali.

Katika utekelezaji wa viwanda 100, ndani ya kipindi cha miezi minne kuanzia Disemba mwaka 2017 hadi 26, Machi, 2018 Mkoa wa Rukwa umezalisha viwanda vidogo 51 huku lengo la Mkoa ni kuwa na viwanda vingi zaidi ili kuchangia kwa kiasi kikubwa lengo la Kitaifa la kufikia nchi ya Uchumi wa Kati wa Viwanda ifikapo 2025.

KINARA WA UDHALILISHAJI WANAWAKE MKOANI MOROGORO AKAMATWA.

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro
POLISI mkoani Morogoro imefanikiwa kumnasa mtuhumiwa sugu  ajulikanaye kwa jina la Mabula  Mabula  ( 28), maarufu ‘SIX ‘ mkazi wa Kata ya Mji Mpya , ,Manispaa ya Morogoro , ambaye anajihusisha na matukio ya kubora simu kwa njia ya pikipiki , kubaka wanawake , kuwapora mali zao  kisha kuwabaka na kuwapiga picha za utupu .

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro,  Ulrich Matei alisema hayo  kwa waandishi wa habari kuhusu mkakati wa Jeshi la Polisi mkoani humo kudhibiti matukio ya uharifu na uharifu.

Alisema , kufuatia matukio kadhaa ya ukatili wa aina hiyo yaliyolipotiwa Kituo kikuu cha Polisi ndipo timu ya makachero ikiongozwa na wataalamu wa Cyber – Crime pamoja na kikosi cha kupambana na ujambazi walifuatilia suala hilo kicha kufanikisha ukamataji huo.

“ Matukio matano ya wanawake kufanyiwa vitendo vya ukatili yameripitiwa  kituo kikuu cha Polisi na wahusika wameshindwa kumtambua mihusika  na baada ya kumkamata inaimani watu wanajitokeza “ alisema Matei.

Hata hivyo alisema , baada ya kumhoji mtuhumiwa huyo  alieleza mbinu anazotumia kwamba hijifanya yenye ni akari Polisi ambapo huwakamata wanawake nyakati za usiku na kuwasingizia makosa mbalimbali kasha kuwapeleka mafichoni kwenye kiza kinene maneo ya Tumbaku – Pepsi kuwatishia silaha panga , kupora mali walizonazo na kuwafanyia ukatili wa kuwalawiti na kuwapinga picha za utupu.
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei (kulia) akitoa maalezo ya mtuhumiwa sugu   ajulikanaye kwa jina la Mabula  Mabula  ( 28), maarufu ‘SIX ‘ (  wapili kushoto fulana nyeusi ) mkazi wa Kata ya Mji Mpya , Manispaa ya Morogoro , ambaye anajihusisha na matukio ya kubora simu kwa njia ya pikipiki , kubaka wanawake , kuwapora mali zao  kasha kuwabaka na kuwapiga picha za utupu , mwingine na ( kwanza kushoto) ni mtuhumiwa wa ununuzi wa simu za wizi,  Ramadhan Salumu A.K.A Miondoko.
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei (kulia) akitoa maalezo ya mtuhumiwa sugu   ajulikanaye kwa jina la Mabula  Mabula  ( 28), maarufu ‘SIX ‘ ( kati kati fulana nyeusi ) mkazi wa Kata ya Mji Mpya , ,Manispaa ya Morogoro , ambaye anajihusisha na matukio ya kubora simu kwa njia ya pikipiki , kubaka wanawake , kuwapora mali zao  kasha kuwabaka na kuwapiga picha za utupu .
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei (kulia) akitoa maalezo  kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) juu ya watuhumiwa watatu waliopo kushoto wa wizi wa mitandao  waliokamatwa na  simu tisa aina mbalimbali pamoja na laini 57 za mitandano mbalimbali ikiwa na  kurasa sita za kitabu cha kumbukumbu kwa wakala (Log Book ) za mtandao wa Vodacom ambazo zina namba za siku za wateja. ( Picha zote na John Nditi).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


MAGAZETI YA LEO JUMATANO MARCH 28,2018

MAONESHO YA YST KUFANYIKA MAPEMA AGOSTI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii.

Taasisi ya Young Scientist Tanzania (YST) inapenda kuwaalika wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na walimu kushiriki katika maonesho ya YST 2018 yatakayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kuanzia tarehe 1 hadi 2 Agosti mwaka huu.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwanzilishi mwenza wa taasisi ya YST Gosbert Kamugisha ameeleza kuwa Wanafunzi wanaombwa kutuma kazi mradi zao za kiutafiti wa kisayansi kwa YST hadi  tarehe 21 Aprili, wanafunzi 200 watachaguliwa na kuonesha tafiti zao za ugunduzi wa kisayansi na kupewa mafunzo ya ziada ya kuendeleza tafiti zao toka kwa wataalamu wabobevu kutoka YST.

Nyanja mbalimbali zitaangaliwa na watafiti chipukizi hao katika sayansi kama vile katika Kemia, Fizikia, Hisabati, Bailojia, na Ecolojia na kazi hizo zitalenga katika kuleta masuluhisho katika masuala ya afya, kilimo, chakula, mawasiliano, elimu, usafiri na mabadiliko ya tabia nchi.

Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washiriki watakaofanya vizuri kama fedha, medali pamoja na udhamini wa masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi watakaofanya vizuri.

Taasisi ya YST inaomba ushirikiano kwa wazazi, walimu, Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO'S) kushirikiana nao ili kuweza kupata masuluhisho ya kijamii na uchumi yanayoikumba jamii kwa sasa kupitia wanafunzi wetu(wanasayansi chipukizi.)
 Mwazilishi Mweza wa Taasisi ya YST,Gosbert  Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari hawapo pihani juu ya maonesho ya YST 2018 yatakayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kuanzia tarehe 1 hadi 2 Agosti mwaka huu.
Mwanzilishi wa Tasisi ya Young Scientist Tanzania (YST),Joseph C lowry akizungunmza na waanshi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  washiriki watakaofanya vizuri kama fedha, medali pamoja na udhamini wa masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi watakaofanya vizuri.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mwanzilishi mwenza  wa Taasisi ya YST,Gosbert  Kamugisha

BUBU ANAPOKUWA SHAHIDI MAHAKAMANI.

$
0
0

Na  Bashir  Yakub.


Bubu yaani mtu asiyeweza kuongea  anaweza kuwa shahidi mahakamani iwapo ameshuhudia tukio. Kutokuwa na uwezo wa kuongea hakumwondolei sifa ya kushuhudisha kile ambacho amekishuhudia. 

Ikumbukwe ushuhuda unatokana na  na hatua ya mtu kuona, kusikia, kuhisi, kugusa, au  utambuzi wa tukio kwa namna yoyote  ambao umetokana na kiungo cha mshuhudiaji.


Yumkini, bubu wengi hawasikii. Na tumeona hapo juu kuwa ushuhuda ni pamoja na kusikia. Hata hivyo pamoja na kutosikia kwao bado wanavyo viungo vingine vya mwili ambavyo wanaweza kuvitumia kushuhudia tukio. Viungo hivyo ni pamoja na macho, mikono kugusa, ulimi kuhisi,akili katika utambuzi nk.



1.  SHERIA KUHUSU BUBU SHAHIDI.


Kifungu cha 128( 1 )  cha Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 kinasema kuwa  mtu ambaye  hawezi kuongea(bubu) anaweza kutoa  ushahidi wake  katika namna nyingine ambayo itaweza kuwa fanisi na ya kueleweka.  Njia fanisi na ya kueleweka ni kama kupitia maandishi/kuandika ikiwa anao uwezo wa kuandika, na kwa ishara ikiwa anao uwezo wa kutumia ishara.Wengi tunajua ishara kama njia kuu ya mawasiliano kwa bubu. Basi hiyohiyo inaweza kutumika kwa bubu kutoa ushahidi.

2.  HALI IKOJE KAMA HAKIMU/JAJI HAELEWI  ISHARA YA BUBU.


Bubu anapotoa ushahidi wake kwa ishara panatakiwa pawepo mtu ambaye atatafsiri ishara zile kwa maneno. Hata kamaHakimu/Jaji angekuwa na uwezo wa kujua ishara za bubu bado mtu anayetafsiri anatakiwa kuwepo. Hii ni kwasababu mahakamani hayupo hakimu tu. Bali wapo wapo wengine kama upande wa mashtaka , upande wa utetezi ambao wangependa kujua nini bubu anaongea katika ishara zake ili wapate kumuhoji na kumuuliza maswali kuhusu kile alichoongea.


                    KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com 

TANESCO KUTUMIA MFUMO MPYA WA MALIPO YA SERIKALI KUUZA UMEME,PIA KAMPUNI ZA SIMU,BENKI KUTUMIKA,YAWATOA HOFU WATEJA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema wateja wake wote wanaotumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, mwaka huu shirika hilo itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao Government e-Payment Gateway (GePG).

Imesema mfumo utaanza kutumika kutokana na matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.Taarifa ya Ofisi ya Uhusiano ya Tanesco makao makuu imesema shirika hilo ni miongoni mwa Taasisi za Serikali,hivyo itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi zake.

Pia Kampuni za simu pamoja na benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki. 

"Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa Tanesco itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike Tanesco ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio.

" Baadhi ya taasisi hizo ni Polisi, Brella, Ardhi, TRA pamoja na Mamlaka za maji. Tunapenda kuwahakikishia wateja wote kuwa mbali na Kampuni za simu ofisi zote za Shirika na vituo vya mauzo ya LUKU vitaendelea kutoa huduma katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka,"imesema taarifa hiyo.

Ufafanuzi huo wa Tanesco unakuja baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ambayo inadai mkataba kati ya Tanesco na Maxcom(MaxMalipo)wa kuuza token za umeme utakwisha mwisho mwa nwezi huu na hakuna dalili wataongezewa mkataba.

Taarifa hiyo ikadai kutokana na hali hiyo ni vema wateja wakachukua tahadhari kwani baada ya Machi 31anayetaka kununua umeme itabidi aende ofisi za Tanesco.

Hivyo Tanesco wameamua kufafanua kuhusu mfumo mpya ambao utatumika wateja kununua umeme na kuwahakikishia wataendelea kununu kama zamani na hakutakuwa na tatizo lolote.

Je! Unajua unaweza kupata bei bora za soko kwa shamba lako la kuzalisha kwa kutumia mtandao wa simu?

$
0
0
Je! Unajua unaweza kupata bei bora za soko kwa shamba lako la kuzalisha kwa kutumia mtandao wa simu? Tazama na ujifunze jinsi wengine wanavyofanya.




ALICHOKISEMA WAZIRI JAFO KUHUSU MAAGIZO YA MHE. RAIS JOSEPH POMBE MAGUFULI

TANZIA


MWAKYEMBE AKUTANA NA MSANII DIAMOND,WAMALIZA TOFAUTI ZILIZOJITOKEZA

$
0
0



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zilizochukuliwa na wizara kwa kufungia baadhi ya nyimbo zinazokiuka maadili, kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juliana Shonza na kulia Msanii wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’.
Naibu Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zilizochukuliwa na wizara kwa kufungia baadhi ya nyimbo zinazokiuka maadili, katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe na kulia ni Msanii wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’.
Msanii wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maridhiano yaliyofikiwa kati yake na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jana jijini Dar es Salaam, Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe na kushoto ni Naibu Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza. icha na Idara ya Habari - MAELEZO

KENYA NA TANZANIA WAHAKIKI MPAKA WA KIMATAIFA

$
0
0
Na Rehema Isango, Tarime, Mara

Timu za watalaamu wa upimaji ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Tanzania na taasisi za usimamizi wa Ardhi nchini Kenya zimekutana wilayani Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa kazi ya kuhakiki na kuimarisha mpaka wa Kimataifa baina ya nchi hizi mbili.

Mapema mwezi Machi, Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula alitangaza azma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza kuimarisha mipaka yake kwa nchi jirani za Kenya na Uganda baada ya ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya katika Mbuga ya Wanyama ya Taifa ya Serengeti iliyopo mkoani Mara.

Hatua ya uhakiki na uimarishaji wa alama za mipaka ya mikataifa inatokana na mpaka huu kuwa wa siku nyingi na haukuwa wazi katika maeneo mengi pia baadhi ya alama hizo kuharibiwa, kung’olewa au kuchakaa na hivyo kusababisha Serikali pande zote kushindwa kusimamia kwa ufanisi shughuli za mipakani, rasilimali za nchi pamoja na ulinzi na usalama.

Katika uimarishaji wa alama hizo za mipaka hivi sasa, kutaongezwa alama mpya ndogo zinazoonana kwa umbali wa mita 100 pamoja na kubainisha eneo la ardhi huru kwa kila upande wa nchi (buffer zone).
Wataalam wa masuala ya upimaji ardhi pamoja na maafisa mbalimbali kutoka katika ofisi za Serikali za nchi zote mbili waliojumuika pamoja wilayani Tarime mkoani Mara kupanga namna ya kutekeleza kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kwa pamoja. Wa tatu kutoka kulia (walioketi) ni Mkuu wa Msafara wa wataalam kutoka Tanzania Bw. Huruma Lugala na kulia kwake ni Mkuu wa Msafara kutoka Kenya Bw. Julius Rotich.
Mkuu wa zoezi la Uhamasihaji katika kazi ya kuhakiki na kuimarisha mipaka ya Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya Bw. Raymond Bagenda kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza wakati wa kikao cha pamoja cha wataalam wa masuala ya upimaji ardhi kutoka katika ofisi za Serikali za nchi zote mbili. Kikao hiko kilichofanyika wilayani Tarime mkoani Mara kinapanga namna ya kutekeleza kazi hiyo kwa pamoja. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais nchini Kenya inayohusika na Usimamizi wa Mipaka ya Kimataifa (KIBO) Bw. Joseph Rotich.
Baadhi ya Wataalam wa masuala ya upimaji ardhi pamoja na maafisa mbalimbali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na katika ofisi zingine za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mazungumzo kuhusu namna ya kutekeleza kazi ya uhakiki na uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kati ya Kenya na Tanzania.


RAIS DK. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI LEO

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.

Mwengine aliyeapishwa ni Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Fatma Gharib Bilal  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto katika hafla  iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha  Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais katika  hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
 Baadhi ya Mawaziri waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliwaapisha Viongozi hao Fatma Gharib Bilal  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto na Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Balozi Seif Ali Iddi kabla kuwaapisha  Viongozi aliowateuwa hivi karibuni hafla hiyo ya kiapo ilifanyika leo  ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika kiapo cha Viongozi Fatma Gharib Bilal  kuwa  Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto na Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,walioapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo. (Picha na Ikulu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MILIONI 400/= KUJENGA MAJENGO MANNE YA KISASA

$
0
0
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imepokea fedha kutoka  Ofisi ya Raisi TAMISEMI kwa ajili ya kuongeza majengo katika kituo cha afya Namtumbo.
Ofisa Habari wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo, Yeremias Ngerangera alisema kuwa Halmashauri hiyo ilipokea fedha hizo mwezi Novemba mwaka 2017 na baada ya kupokelewa kwa fedha hizo  Halmashauri ilipitia miongozo ya matumizi ya fedha hizo ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa.
Aidha Ngerangera aliongeza kuwa baada ya kupitia miongozo ya matumizi ya fedha hizo Halmashauri imeanza ujenzi wa majengo hayo  manne katika kituo cha afya Namtumbo kilichopo katika kata ya Rwinga mjini Namtumbo.

Injinia wa majengo Katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo, Hasssani Kinonono aliyabainisha majengo yanayojengwa kuwa  ni pamoja na Jengo la upasuaji, Jengo la wodi ya akina mama wajawazito,Maabara na Nyumba ya waganga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Christopher Kilungu alidai kuwa kutakuwa na ukarabati wa jengo la kuhifadhia maiti  pamoja na kujenga kichomea taka kwa kutumia fedha zitakazo baki katika ujenzi wa majengo hayo manne.
Kilungu pamoja na mambo mengine alidai kuwepo na salio katika ujenzi huo wa majengo manne lililotokana na ujenzi huo kutumia  akaunti ya nguvu ya jamii( Force account) na kusaidia kupunguza matumizi makubwa ya fedha hizo na kuwa na salio linaloweza kufanya kazi ya kukarabati chumba cha maiti na kujenga kichomea taka katika kituo hicho.
Kituo cha afya Namtumbo kina wodi ya watoto,wodi ya wagonjwa ,jengo la upasuaji kwa akinamama wajawazito na jengo la kuhudumia wagonjwa wan je  ambapo kwa sasa ujenzi huo utasaidia kuboresha huduma za jamii katika kituo hicho cha Afya.

MGALU AWATAADHARISHA WAKANDARASI/WATUMISHI WANAOHAMASISHA MAANDAMANO

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

SERIKALI imetoa tahadhari kwa watumishi ,wakandarasi na wadau wa sekta ya Nishati wanao husika na miradi wasitikise kiberiti kwa kuhamasisha maandamano kupitia shida za wananchi.

Aidha wizara ya Nishati imesema itatumia kiasi cha shilingi trilioni sita kwa ajili ya kuyafikia maeneo 7,873 nchi nzima ili yaunganishwe na huduma ya umeme kupitia miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Hayo yalisemwa kwenye mtaa wa Sagale Magengeni kata ya Viziwaziwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa akitembelea maeneo yaliyoko kwenye miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Alisema kuwa ole wake anayetumia tumia shida za wananchi kuhamasisha maandamano kwani akibainika chamoto atakiona.Mgalu alieleza hayo baada ya kauli ya mwananchi mmoja ambaye alikuwa akitaka umeme na kuambiwa kama anataka umeme aandamane maandamano ya Mange Kimambi.

“Serikali imeshtushwa tena inatokea maeneo haya kwa watu waliopewa dhamana mkandarasi ni dhamana huwezi kuleta jeuri kama unazo fedha usingeomba kazi hizi ni fedha za Rais Dk. Magufuli usilete jeuri,” alisema Mgalu.
Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka na Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu wakibonyeza kiwashio ikiwa ni sehemu ya kuuwasha umeme umeme mtaa wa Mbwawa Mkoleni,wilayani Kibaha.Picha na Mwamvua Mwinyi.


Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>