Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

EFM YAWEKA MILIONI 300 SHINDANO LA SHIKA NDINGA

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKURUGEZI Mkuu wa kituo cha Efm Radio, Dennis Busulwa(SEBO) amesema kampuni yake imewekeza kiasi cha zaidi Milioni 300 kwa ajili ya shindano lake la Shika Ndinga  litakalofanyika katika mikoa 6 ya Tanzania bara  na kuanza kutimua vumbi Dar es Salaam katika uwanja wa Mwembe Yanga.

Sebo amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa anazungumza na Waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa shindano hilo na maadhimisho ya miaka minne ya Efm Radio na kuongezeka kwa masafa kwa kutoka mikoa sita hadi kufika kumi.

"Efm Radio imekuwa na bidhaa mbalimbali za uwezeshaji  kwa wasikilizaji wake ambapo shika ndinga kwa mwaka huu 2018 linaweza kuwafikia watanzania katika mikoa sita zaidi ikiwa ni lengo la uwezeshaji katika jamii "amesema Sebo.

Amesema Shindano la shika ndinga mwaka huu linatarajia kufanyika kwa wiki 7 katika mikoa sita amabayo ni Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mtwara , Mbeya na Pwani  ambapo litaanza tarehe 7 April hadi mei 15 ikihusisha jumala ya Pikipiki 14 na gari aina ya kirikuu mbili.

katika hatua nyingine Sebo alitumia mkutano kuwaeleza waandishi wa habari juu ya mafanikio ya Radio yao katika miaka minne tangu kuanzishwa kwake  kwa kuwa radio namba moja kwa kusikilizwa kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani huku ikiwa namba mbili katika mikoa ya bara.
 Meneja Mkuu wa EFM Radio,Dennis Busulwa(SEBO), Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo juu ya shamrashamra za Efm Kutimiza miaka minne sanjari na uzinduzi wa Shindano la Shika ndinga linaloendeshwa na kituo hicho cha Radio kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
 Afisa Habari wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Tatu Mzuka ,Petronila Mtatiro akieleza namana watu watakavyoweza kujishindia zawadi mbalimbali wakati wa shindano la shika ndinga.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Chotec Limited inayosambaza vilainishi vya Shell, Tanzania, Choba Mumba akieleza namna wao watakavyoweza kusambaza vilainishi maalum vya pikipiki nchini.
 Meneja Matukio wa Kampuni ya Efm Radio, Jesca Mwanyika akizungumza juu ya matokeo ya washindi wa shindano la Shika ndinga katika msimu uliopita .

WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA PINGO/MKOANI PWANI-RPC SHANNA

0
0
 Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna akizungumza kuhusiana na misako na doria zinazoendelea Mkoani humo.
 Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna akiakionesha baadhi ya siraha alizokamata.

Wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia ambao wamekamatwa na jeshi la polisi Mkoani Pwani ,huko porini Pingo shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze.

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la polisi mkoani Pwani, limewakamata wahamiaji haramu kumi raia wa nchi ya  Ethiopia ,kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Jeshi hilo pia, limemtia nguvuni mwanamke -Siwema Mgombale akiwa na risasi 23 zinazotumika kwenye silaha aina ya shortgun, huko kijiji cha Manda Mazingara kata ya Miono,tarafa ya Mkange wilaya ya Bagamoyo.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP), Jonathan Shanna alisema, wahamiaji haramu hao wamekamatwa machi 26, wakiwa porini ,Pingo Shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze na askari waliokuwa doria kufuatia kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Akielezea matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo, aliwataja waliokamatwa kuwa ni Tagen Alam (19), Abraham Wolde (19) na Musama Kamal (16).

Wengine ni Abush Tamaskel (16), Ayela Erapo (18) na Ngusie Kechine (18), Zarabel Faisa (16), Tsedhj Yshgee (19), Teyey Ally (18) na Tuktigo Clemag (17).

Watuhumiwa wote hao watafikishwa idara ya uhamiaji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Shanna alielezea ,jeshi hilo linaendelea na juhudi za kuwatafuta watu waliowasaidia kuingia nchini bila kufuata utaratibu wa sheria.

Katika tukio jingine , mwanamke aliyejulikana kwa jina la Felister Mtinga (30-36) amekutwa kitandani akiwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Moreto,iliyopo Chalinze.

Kamanda Shanna alisema kuwa, mwili wa mwanamke huyo ulibainika machi 26 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi baada ya wahudumu kutomuona akitoka tangu alipoingia ndani machi 25 katika nyumba hiyo.

Alifafanua , mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi wa awali na kubaini kutokuwa na majeraha ya aina yoyote hali inayosababisha kuondoa mashaka kuhusu kifo chake na umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi.

Katika tukio la kukutwa na silaha, kamanda Shanna alibainisha wamekamata silaha mbalimbali katika misako inayoendelea kufanyika mkoani hapo, ikiwemo SMG .R.6134, mapanga manne, sime moja na risasi 23.

Alieleza, saa sita usiku machi 27,walimkamata mwamke aliyetambulika kwa jina la Siwema Mgombale akiwa na risasi 23 zinazotumika kwenye short gun na Ramadhani Mdoe akiwa na silaha aina ya SMG.R.6134 .

“Tunaendelea na misako kabambe inayoongozwa na kikosi chao cha siri, tunafanya misako uvungu kwa uvungu,giza kwa giza,pori kwa pori,tunashukuru inazidi kufanikiwa na ni endelevu “alisisitiza kamanda huyo.

Kamanda Shanna aliwaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za wale wachache ambao wanawadhania ni wahalifu kwenye maeneo yao.

MAONESHO YA WAVUMBUZI, WABUNIFU KUANZA APRILI 27 DAR

0
0
Ofisa Habari wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Edward Nkomola akizungumza na waandishi habari kuhusiana na maonesho ya wabunifu na wavumbuzi  yatayofanyika Aprili 27 hadi 29, leo  jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Wabunifu na Wavumbuzi, Edward Magoti(Wapili kulia) akizungumza na waandishi habari kuhusiana na maonesho hayo, leo jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAMATI ya Maonesho ya Wavumbuzi na Wabunifu Tanzania(TICE) kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  wameandaa maonesho ya yayanayotarajia kufanyika kuanzia Aprili 27 hadi 29 mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Magoti amesema maonesho hayo yatahusisha Wavumbuzi na wabunifu na yatakuwa ya aina yake katika ujenzi wa sekta ya viwanda nchini.

Magoti amesema maonesho hayo ni fursa ya wabunifu na wavumbuzi katika nyanja ya kutengeneza mtandao , kujitangaza katika mtandao wa kufanya ubunifu na uvumbuzi pamoja kuendeleza kazi na uzoefu na watu wengine katika sekta hiyo.

Amesema wakati wa maonesho hayo wavumbuzi na wabunifu wa nchini Tanzania watapa fursa ya kukutana na mabalozi wa nchi mbalimbali ,wafanyabiashara wakubwa na kati taasisi za Serikali , Taasisi za fedha na viongozi.

Aidha amesema washiriki watatu kwenye maonesho hayo watapata zawadi ya milioni  Sh.35 kwa mshindi wa kwanza na mshindi mshidni wa tatu Sh.milioni 5.

Kwa upande wa Ofisa wa Habari wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Edward Nkomola amesema maonesho hayo yatakutanisha watoa huduma wote ambapo ni fursa kwa wabunifu na wavumbuzi kukutana na watoa huduma hao.

BancABC YAANZA KUTEKELEZA SERA YA FEDHA YA BoT

0
0
 Mkurugenzi mtendaji wa BancABC Dana Botha akizungumza na waandishi wa habali katika ofisi zao Leo Jijini Dar es Salaam,kuhusu punguzo la tozo  ya mikopo mbali mbali kwa wateja wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Dana Botha kulia,kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Hazina BancABC Barton Mwasamengo pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wa BancABC Joyce  Malai katikati wakishika bango linaloonyesha punguzo la tozo za Mikopo.

Na  Agness Francis, Blogu ya Jamii
BENKI ya BancABC  imesema imetekeleza Sera ya fedha  ya Benki  Kuu ya Tanzania(BoT) kwa kutangaza kutoa punguzo kwa wateja  wake wapya kuwezesha  kukopa kuanzia Aprili 1 mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji was BancABC Dana Botha amesema benki hiyo ni  sehemu ya Atlasi Mara iliyosajiliwa  katika soko la hisa la Londan ikiwa na lengo la kujitanua ili kuwa kinara katika masuala ya kifedha katika ukanda wa Sahara kwa kutumia uzoefu wake na uwezo wa kukuza mitaji.

Hivyo Botha amesema watapungunza riba kwa wateja wao katika mikopo ya masharti ambayo itakuwa ni huduma ya Over draft pamoja na  ya nyumba na kufafanua mwaka jana benki nyingi zilipita katika wakati mgumu wa ukwasi.

"Hivyo kufanya uwezo wa kukopesha kuwa mdogo.Kwa miezi kadhaa sasa,Serikali kupitia BoT imekuwa ikisisitiza kuhusu punguzo la riba hiyo kwa kupunguza masharti kama vile kiwango cha  chini cha fedha kwa mabenki,"amesema Botha.

Ameongezea viwango vya punguzo,hati fungani za hazina na kukopesha 
mabenki kwa viwango vya chini na hiyo imewezesha ukopeshaji kwa watu binafsi na kampuni mbalimbali ili kuimarisha biashara zao na hatimaye kuboresha uchumi. "Na tunajivunia kuwa kati ya benki za kwanza kutangaza wazi kuhusu punguzo hili."

Aidha Mkuu wa kitengo cha Hazina BancABC Barton Mwasamengo amesema kuwa benki hiyo inahudumia wateja zaidi ya 60,000 ambao wanamiliki bidhaa tofauti za kibenki

Mwasomengo amesema fursa hiyo itawawezesha kuwashawishi wateja kupata mikopo ya Nyumba ambayo ilikuwa changamoto kubwa hasa kwa wananchi wa Daraja la kati na chini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wa BancABC Joyce Mlai amemalizia kwa kusema katika kujenga nyumba wanaungana na Serikali kuwapa fursa ya kuwapatia mikopo ya Nyumba  wafanyakazi wa aina zote sekta binafsi,serikalini pmoja na wafanya biashara.

RIPOTI YA CAG YASABABISHA MAGUFULI KUSIMAMISHA WAKURUGENZI WAWILI

0
0
*Aagiza wachunguzwe dhidi ya tuhuma zilizobainika kwenye ripoti
*Ataka iwe fundisho kwa wakurugenzi wengine nchini, atoa angalizo
*Azungumzia ucheleweshaji kesi unaosababsha Serikali kukosa Trilion 4.4/-

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amewasimamisha kazi kuazia leo wakurugenzi wa 
Halmashauri ya Kigoma Ujiji na Pangani baada ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kubaini madudu yakiwemo ya kupata hati chafu.

Ametoa maagizo hayo leo asubuhi hii baada ya kupokea ripoti ya CAG Profesa Juma Asaad ambapo mbali ya kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya akatangaza kuanza kuchukua hatua kwa kuwasimamisha wakurugenzi hao ili iwe fundisho kwa wakurugenzi wengine.

"Ripoti ya CAG imezitaja halmashauri mbili iko ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji na Pangani ,Nitoe maagizo wakurugenzi hao wawili wasimamishwe kazi mara moja na hata kama si vizuri kuchukua hatua basi ni vema nikachukua hatua haraka ili uchunguzi ufanyike kuhusu tuhuma ambazo CAG amezisema kwenye ripoti yake.

"Wakati natangaza kuchukua hatua za kuwasimamisha wakurugenzi hawa naona mmenyamaza najua kwasababu wengine hawependi hatua zichukuliwe lakini nimeanza kuchukua hatua iwe fundisho kwa wengine kwani tusipochukua hatua wengine wataendelea,"amesema Rais Magufuli.

Amesisitiza ni bora kuanza kuchukua hatua na kwamba hata CAG kwenye 
maelekezo yake kwa Serikali amezungumzia umuhimu wa kuchukua hatua na hivyo amenza kutekeleza hapo hapo baada ya kukabidhiwa ripoti na mengine wataendelea kuyatekeleza kwa kuchukua hatua mbalimbali ili mambo yaende.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam. 


WATUMISHI WATANO NCAA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA DOLA ZA KIMAREKANI 35,500

0
0
Na.Vero Ignatus Arusha.

Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA])wamefikishwa mahakamani leo kwa kosa la kuisababishia hasara serikali na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 35,500.

Watuhumiwa waliofikishwa kizimbani na kukabilia na shitaka moja ni pamoja na Joseph Mtwala{36},John Mlambo{42},Mwahu Yunus {38},Mery Njau{38} na Catherini Edward {33}.
Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walisomewa shitaka moja na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa{TAKUKURU} ,Adamu Kilongozi akiwa na Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo kuwa walitenda kosa hilo kati ya desemba 25 mwaka 2013 na juni 6 mwaka 2014.

Kilongozi alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi Mkoani Mara na lango kuu la Loduare Mkoani Arusha watuhumiwa hao walisababishia serikali hasara ya fedha za Kimarekani kiasi hicho wakiwa watumishi wa NCAA.

Mwendesha mashitaka huyo alisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Bernad Nganga na kueleza kuwa walifanya kosa hilo huku wakijua ni kinyume na sheria.Watuhumiwa wote walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya fedha taslimu shilingi milioni 7.9 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo na taratibu za dhamana zilikuwa zikiendelea .

Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU alisema kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na aliiomba mahakama hiyo kupanga Tarehe ya kuanza usikilzwaji wa awali.Watuhumiwa wote watano wamepelekwa rumande kwakushindwa kukidhi masharti ya dhamani ,ambapo watasomewa hoja za awali April 10 mwaka huu.

MKUTANO WA WAJASILIAMALI WILAYA YA KINONDONI

0
0
Mkuu Wa Wilaya Kinondoni Mheshimiwa Ally Salum Hapi Anawaalika Wajasiliamali Wote Wilaya Ya Kinondoni Kesho Siku Ya Jumatano

 MAHALI: Ukumbi Wa King Solomoni- Namanga

MDA: Saa 3 Asubuhi
LENGO: Kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili

WOTE MNAKARIBISHWA

Wakazi wa Dodoma washuhudia uzinduzi wa umisseta ngazi ya mkoa

0
0
MASHINDANO ya shule za sekondari ya UMISSETA ngazi ya mkoa yamezinduliwa mkoani Dodoma, na mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Waziri wa TAMISEMI,Selemani Jafo.Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari,walimu, viongozi mbalimbali wa mkoa na michezo.

Mbali na uzinduzi,Waziri alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za sekondari zilizokuwepo kwenye uzinduzi huo.Vifaa hivyo vya michezo vimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano haya,ambapo mwaka huu imepanga kutoa vifaa vya michezo kwa shule 4,000 za sekondari zilizopo sehemu mbalimbali nchini.

Waziri Jafo, alisema kampuni ya Coca-Cola kwa kudhamini mashindano hayo kutafanikisha jitihada za kuendelea kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi wa michezo ya soka ,mpira wa kikapu na pia kupitia mashindano haya kutaibuliwa vipaji vya wanariadha watakaotamba katika kipindi cha miaka ijayo.
Waziri Jafo akigawa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za sekondari zitakazoshiriki. Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo, akiongea wakati wa uzinduzi huo.

Waziri Jafo katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa UMISSETA baada ya uzinduzi.


Taifa Stars na DR Congo ngoma bado mbichi, mtanange unaendelea Taifa

0
0
Mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kalenda ya FIFA baina ya Taifa Stars na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeanza katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha pili kimeanza matokeo bado 0-0.

Mashabiki wa Taifa Stars wakionesha Uzalendo ndani ya Uwanja wa Taifa.
 Simon Msuva akipambana na Glody Ngoda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
 Kikosi cha Taifa Stars
Kikosi cha DR Congo.

JESHI LA POLISI MBEYA LAKANA KUHUSIKA KIFO CHA KIJANA MUUUZA MACHUNGWA,LATOA UFAFANUZI WA KINA

WAKILI WA NONDO WASUBIRI BARUA INAYOSAMBAA MTANDAONI INAYOSEMA AMESIMAMISHWA CHUO

0
0
Karama Kenyunko,Globu ya jamii.

WAKILI wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Abdul Nondo, Jebrah Kambole amesema barua inayozunguka katika mitandao ya kijamii kuhusu kusimamishwa chuo kwa mwanafunzi bado hawajaipata rasmi.

Pia amesema hata Nondo naye hajaipata barua hiyo zaidi ambapo akizungumza leo jijii Dar es Salaam Kambole amekiri kuiona barua hiyo kwenye mtandao na kama  barua hiyo itakuwa ni ya kweli watakaa wao kama wanasheria, Nondo, ndugu na marafiki kujadiliana na kuangalia kusimamishwa kwake na utaratibu wa kisheria ukoje.Pia haki zake zitakuwaje.

"Kama barua hiyo hata kama itakuwa ni ya kweli tutajadiliana ni njia gani tuichukue na kama ni ya kweli itakuwa ni ukiukwaji wa haki ya mtu kwa kuwa atakuwa amesimamishwa bila ya kusikilizwa.

"Na hata mfanyakazi wa kawaida akisimamishwa anaendelea kupata mshahara wake.Kusimamishwa tu kwake ni adhabu ambapo hata kama baadaye atakuja kusafishika na kuwa itakuwa amekosa masomo kwa muda wote huo,"amesema.Amefafanua kitendo cha kusimamishwa atakuwa amepata hasara ambayo haiwezi kurudishika kwani  itakuwa amepoteza masomo na hata akirudi darasani wenzake watakuwa wameishamaliza na hawezi kupata masomo ambayo angepata akiwa na wenzake.

"Hivyo haki zake nyingi zitakuwa zimepotea.Sheria za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni za muda mrefu na zimepitwa na wakati kimsingi walitakiwa kutumia busara kwa kesi yake unaendelea Iringa aachwe asome masomo yake,"amesema.

Amesema anapozuiliwa asipate masomo haki zake nyingine zinakuwa zimezuiliwa ikiwamo haki ya kupata elimu na kusikilizwa na kwamba Nondo bado anadhaniwa kuwa ametenda kosa hadi hapo kosa lake litakapothibitika, hivyo UDSM itakuwa imemuhukumu bila ya kuisikiliza na bila ya  kudhani kuwa anaweza kuwa hajatenda kosa hilo.Ameongeza kumekuwa na mtindo wa wanafunzi wengine wanaoshtakiwa mahakamani wanaendelea na masomo yao na ni wanafunzi wa Chuo hicho hicho.

Kambole amesema kusimamia sheria kwa njia,za kibaguzi si nzuri kwa Taifa , kusimamia sheria kwa namna ya kukandamiza watu huyu anaadhibiwa hivi na yule anaadhibiwa hivi si vizuri kwa afya ya Taifa letu.Kambole amesema sheria ikisimamiwa kwa mtindo wa kibaguzi ni itatengeneza Taifa lenye mgawanyiko na tutakuwa na sheria ambayo inatungwa kwa mtindo wa kukomoa.
Wakili, Jebrah Kambole.

BALOZI SEIF AWASILI ZANZIBAR AKITOKEA CUBA

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume akitokea Nchini Jamuhuri ya Cuba kwa ziara Maalum. Wa kwanza kutoka Kulia ni Waziri wa Habari, Utalii na Mambio ya Kale Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo.
Balozi Seif alisalimiana na baadhi ya Viongozi na Waasisi wa Vyama vya Siasa Nchini alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume Zanzibar.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Viongozi wa Serikali na vyama vya Kisiasa Ukumbi wa Watu Mashuhuri (VIP) mara baada ya Kuwasili Uwanja wa Abeid Aman Karume.
Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Bwana Ali Davutoglu kati kati akimtambulisha kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mkurugenzi Mkuu wa Maarifa Foundation School iliyopo Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na – OMPR – ZNZ.

MAKONDA:UKIMPA UJAUZITO MWANAMKE DAR ES SALAAM UJIPANGE KWA MATUNZO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. 

Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
JOPO la wataalam kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, maofisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria pamoja na askari Polisi wa dawati la Jinsia  wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wamejidhatiti vyema kuwasikiliza akinamama ambao wametelekezwa na hawapati fedha za matunzo ya watoto kutoka waume zao.

Ofisi ya Mkuu wa Dar es Salaam ilitangaza kutoa msaada wa kisheria kwa kuwasikiliza wanawake hao na kwamba watatoa msaada huo kwa siku tano kuanzia Aprili  kuanza April 9 mwaka huu.

Akizungumza na wataalamu hao leo, Makonda amesema tatizo la wamama waliotelekezwa ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto wenye chuki na baba zao.

Makonda amesema lengo la mchakato huo si  ugomvi bali ni kumwezesha mtoto kupata mahitaji ili aweze kuitumia vyema fursa ya elimu bure chini ya Serikali ya awamu ya tano. 

Pia amesema amewahimiza wataalamu hao kuhakikisha wanawasikiliza kinamama kwa umakini na kusimamia haki pasipo upendeleo.

Pamoja na hayo Makonda amesema wapo kinababa ambao wameanza kutoa fedha ya matunzo ya mtoto baana ya kusikia tangazo ambapo amewaomba kinamama kufika Aprili 9 mwaka huu kwa ajili ya na watalaamu ili waingie kwenye mfumo rasmi wa kimaandishi.

"Ifike hatua mwanaume ukimpa mwanamke ujauzito bila mpangilio aogope kama ilivyo kwenye ubakaji,"amesema Makonda.

DKT KALEMANI AWAPA MAAGIZO WAKANDARASI WA REA NCHINI

0
0
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza wa wakala wa nishati vijijini (REA) nchini kuhakikisha wanaunganisha umeme kwenye vijiji vitatu kila wiki ili kuweza kutoa fursa ya wananchi kufikiwa na huduma hiyo muhimu.

Dkt Kalemani aliyasema hayo leo wakati akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu (REA III) katika kijiji cha Magumbani kitongoji cha Mbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga mkoani Tanga.

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na uwashwaji wa huduma ya umeme katika Kijiji hicho ili kuwawezesha kupata huduma hiyo ilikuwa haipo awali katika eneo hilo

Alisema kwani hayo ndio malengo waliowapa ikiwa ni mpango mkakati wa kuha kikisha wanafikia malengo ya kuwapelekea umeme watanzania wote ifikapo mwaka 2021/2022 ili waweze kunufaika kupitia huduma hiyo

“Leo tutaangalia mlipowasha lakini niwaagize wakandarasi tunataka kuona kila wiki vijiji vitatu vinawashwa umeme kwani wananchi wanauhitaji mkubwa wa kufikiwa na huduma hiyo hivyo hakikisheni hilo mnalitilia mkazo mkubwa “Alisema.

Hata hivyo alisema bado kuna changamoto ya wananchi kutapeliwa na mafundi ambao wamekuwa wakiwabambikia bei kuwaambia walipe kidogo kabla ya kulipia 27000 ambazo wanapaswa kulipa jambo ambalo ametaka likomeshwe haraka.

“Mameneja, Wakandarasi tuna changamoto wananchi kutapeliwa kuna tabia imezuka mafundi wanawabambikia bei wanaawaambia walipe kidogo kabla ya kulipa elfu 27000 labda niwaambie tu kwamba mtu wa namna hiyo atakayepatikana watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria”Alisema Waziri huyo.

Alisema mradi huo utakwenda kila kijiji, kitongoji na nyumba kwa nyumba huku akieleza hata kama nyumba unayokaa utaona hakuna sehemu ya kutundukia waya weka hata kwenye mti ili mradi uweze kufikiwa na huduma hiyo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii ch a Magumbani Kitongoji cha Mbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga,Y ona Mark na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuluni Selemani Omari
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumbani Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katikati akiteta jambo mara baada ya kuzindua upatikanajiwa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijiji niawamu ya tatu (REA III) katika Kijii cha Magumban i Kitongoji chaMbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MBOWE, WENZAKE WATANO WAPANDISHWA KORTINI WAKIKABILIWA NA MAKOSA NANE

0
0
Gari la Jeshi la Polisi lilipowasili katika Maahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam likiwa na Dk.Mashinji, Mnyika, Msigwa na Ester Matiko.

*Yumo pia Dk.Mashinji, Mnyika, Msigwa na Ester Matiko

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe na vingozi wenzake watano wa chama hicho wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka nane yakiwemo ya uchochezi na uasi.

Mbali na Mbowe wahtakiwa wengine ni wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Bara Salum Salum, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent Mashinji.

Katika mashtaka hayo nane, shtaka la kwanza na la pili linawakabili watuhumiwa wote sita, huku Mbowe peke yake anakabiliwa na mashtaka matano, yaani shtaka la tatu hadi la saba na Msigwa akikabiliwa na shtaka moja la peke yake la nane.

Akisoma  hati ya mashitaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Faraja Nchimbi amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa Februari 16, mwaka huu washtakiwa kwa pamoja, wakiwa katika barabara ya Kawawa wilayani Kinondoni, walifanya mkusanyiko na maandamano isivyo halali kinyume na sheria. 

Imedaiwa walikusanyika kutekeleza lengo la pamoja kufanya mkusanyiko usio wa halali wenye vurugu na kufanya watu waogope kwamba watakwenda kusababisha uvunjifu wa amani.

Aidha Nchimbi ameongeza kudai Februari 16, mwaka huu katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa wamekusanyika wao na wenzao 12 ambao bado hawajafikishwa mahakamani, wakiwa kwenye maandamano hayo,licha ya kutolewa  tamko la kuwataka kutawanyika...

Waligoma kutii amri hiyo na kuendelea na maandamano na kusababisha kifo cha Aquilina Akwkilina kusababisha askari wawili kujeruhiwa kutokana na mkusanyiko  huo.

Katika shtaka la tatu imedaiwa Februari 16, mwaka huu katika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, jijini mshtakiwa Mbowe peke yake wakati akihutubia wananchi wa jimbo hilo alihamasisha chuki isivyohalali kwa kutoa matamshi ya kuhamasisha chuki maneno ambayo yalipelekea chuki mioyoni mwa wana jamii wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Mbowe anadaiwa kufanya uchochezi na kusababisha chuki miongoni mwa wanajamii ya watanzania kinyume na sheria.
Aidha Nchimbi amedai
Katika mashitaka ya uchochezi wa uasi yanayomkabili Mbowe, inadaiwa katika maeneo hayo akiwa katika mkutano wa hadhara, 

Akiwa na nia ya kupandikiza chuki na dharau kwa watanzania dhidi ya uongozi wa kiserikali  uliopo madarakani kisheria, alitamka maneno yenye kupandikiza chuki na kuleta ushawishi wa uasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani kisheria.

Nchimbi aliendelea kudai, katika tarehe hiyo hiyo na maeneo hayo mkoani Dar es Salaam, Mbowe alitoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau dhidi ya mamlaka halali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Katika shitaka la saba, Mbowe anakabiliwa na tuhuma za kutenda kosa la kushawishi kutendeka kwa kosa la jinai, ambapo amedaiwa siku hiyo, akiwa pia amejumuika na wengine ambao hawako mahakamani, aliwashawishi wakazi hao wa Kinondoni, kutenda kosa la kufanya maandamano na mkusanyiko usio wa halali.

Mshtakia Msigwa anadaiwa kushawishi raia  kutenda kosa la jinai shtaka analodaiwa kutenda February 16, mwaka huu katika maeneo hayo hayo ya Viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni Dar es Salaam,

Imedaiwa siku hiyo Msigwa aliwashawishi wananchi wa Kinondoni kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha.

Washitakiwa wamekana mashitaka hayo na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo wanaomba ipangwe kesho au keshokutwa kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

RAIS DK.SHEIN AKUTANA UJUMBE WA HUAWEI LEO

0
0
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kulia)  akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Bw.Gao Mengdong, alipofika Ikulu Zanzibar leo kwa mazungumzo pamoja na Ujumbe aliofuatana nao. (Picha na Ikulu) 
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Huawei unaoongozwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Bw.Gao Mengdong (wa pili kulia)  ujumbe huo ulipofika Ikulu Zanzibar  leo kwa mazungumzo. 
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Bw.Gao Mengdong, alipofika Ikulu Zanzibar leo kwa mazungumzo pamoja na Ujumbe aliofuatnana nao (hawapo pichani). 

WAZIRI JAFO AWASIMAMISHA KAZI WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA UJIJI NA PANGANI

0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amewasimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Kigoma Ujiji na Pangani Tanga kutokana na Ofisi zao kupata hati chafu katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne (Machi 27, 2018), Waziri Jafo alisema Ofisi yake imetekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe kuhusiana na ripoti ya CAG kuwataja Watendaji hao kuzembea na kusababisha taasisi zao kupata hati chafu.

Aliwataja Wakurugenzi waliosimamishwa kazi na kupisha uchunguzi kuwa ni Bi. Hanji Godigodi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Bw. Sabas Damian Chambasi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
“Namwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI aunde timu ya Wataalamu kuchunguza utendaji kazi wa Wakurugenzi hao na kunipatia taarifa ndani ya wiki tatu kuanzia leo” alisema Waziri Jafo.

Kuhusu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma, Bw. Judethadeus Mboya ambaye kustaafu utumishi, Waziri Jafo alisema uchunguzi dhidi yake utaendelea kufanyika ili kubainisha kuhusika kwake katika kuisababishia halmashauri hiyo kupata hati chafu.

Akifafanua zaidi Waziri Jafo alisema katika taarifa hiyo ya CAG ya mwaka 2016/17, ripoti hiyo ilibainisha kuwa katika ngazi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuliwepo na jumla ya vitabu 379 vya makusanyo ya mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa CAG kwa ajili ya kufanyika ukaguzi wa mahesabu yake.

Aliongeza kuwa kutokana na taarifa hiyo, Ofisi yake itawasiliana na Wakurugenzi wote kuhakikisha kuwa inawasilisha vitabu hivyo vyenye taarifa na nyaraka za ukaguzi katika ofisi ya CAG haraka iwezekanavyo.

Kwa mujibu wa Jafo alisema kwa sasa Serikali imepata mafanikio makubwa sana katika suala zima la udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali katika mamlaka za Serikali za Mitaa ikilinganisha na miaka ya nyuma ambao hali ya matumizi haikuwa nzuri.

Waziri Jafo alizipongeza Halmashauri 166 zilizopata hati safi na kuendelea kufanya vizuri katika kusimamia taratibu za matumizi ya fedha za umma pamoja na kuzitaka halmashauri 16 zilizopata hati isiyoridhisha kufanya maboresho katika utendaji kazi ili kupata hati safi.

“Kwa upande wa Halmashauri zilizopata hati chafu naziagiza zibadilishe mienendo ya utendaji kazi katika halmashauri zao sambamba na kuyaagiza Mabaraza ya Madiwani kusimamia vyema Halmashauri hizi katika mipango ya matumizi ya fedha za Serikali” alisema Jafo.

Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
DAR ES SALAAM
27.3.2018
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne (Machi 27, 2018),

TAIFA STARS YAIRARUA DR CONGO BILA HURUMA, YAIFUNGA 2-0

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kalenda ya FIFA baina ya Taifa Stars na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umemalizika kwa Tanzania kuondoka na ushindi wa goli 2-0 mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo iliyoanza kwa kasi kila upande wakitaka kupata goli la kuongoza ambapo mpaka kufika dakika ya 45 na kwenda mapumziko hakuna timu iliyoona mlango wa mwenzake.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Tanzania wakifanya mabadiliko kwa kumtoa Mohamed Issa 'Banka' na kuingia Ibrahim Ajib kwa ajili ya kwenda kuongeza nguvu katika safu ya kiungo.

Mabadiliko yaliweza kuleta tija ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Himid Mao na kuingia Mudathir Yahya kuliweza kuwadhoofisha DR Congo na kupitia dakika ya 75 Mshambuliaji wa kimataifa anayekipiga kwenye kikosi cha Genk nchini Ubelgiji Mbwana Samata anaipatia Tanzania goli la kwanza akimalizia Krosi iliyopigwa na Shiza Kichuya.


DR Congo wakiendeleza kutafuta goli la kusawazisha ila katika dakika ya 88 Shiza Ramadhan Kichuya anaipatia Tanzania goli la pili na la ushindi na kuzidi kupeleka kilio katika timu ya DR Congo.



Mashabiki wa Taifa Stars wakionesha Uzalendo ndani ya Uwanja wa Taifa.
 Simon Msuva akipambana na Glody Ngoda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
 Kikosi cha Taifa Stars
Kikosi cha DR Congo.

WAFANYABIASHARA WADOGO WAANZA KUPEWA VITAMBULISHO VYA TRA

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Pamoja naye ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (mwenye miwani) na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Kodi, Dina Kaka jinsi ya kuandaa risiti ya kitambulisho cha Mfanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi Mfanyabiashara Mshamu Nakukwa kitambulisho wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. 

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA SHIMMUTA

0
0
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi kuwaruhusu wafanyakazi kushiriki michezo katika maeneo yao ya kazi lakini pia wawaruhusu wafanyakazi hao kushiriki Michezo ya SHIMMUTA.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amesema michezo ni muhimu sana kwenye Tanzania ya Viwanda kwani michezo husaidia mwili kuwa wenye afya bora na utendaji wao wa kazi unakuwa mzuri zaidi.Makamu wa Rais amesema yeye alikuwa mwanamichezo mzuri wa mpira wa pete (netball) lakini kwa sasa anafanya mazoezi kidogo kidogo asubuhi na jioni.

“Najua Umuhimu wa kufanya mazoezi kwa sababu nikiacha kufanya mazoezi nadorora na katika nafasi hii ukidorora unadorora mpaka akili na kazi zitakushinda”

Makamu wa Rais aliwasihi Viongozi wa Michezo kusimamia masuala ya michezo katika maeneo ya kazi na kuwataka Viongozi wa Taasisi kuweka bajeti ya michezo kwa ajili ya kushiriki michezo ya SHIMMUTA.Makamu wa Rais amesema ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015- 2020 imeleekeza kuendeleza michezo sehemu za kazi.

Aidha Mwenyekiti wa SHIMMUTA Ndugu Hamis Mkanachi alimpongeza Makamu wa Rais kwa juhudi anazozifanya katika kukuza michezo nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) uliofanyika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Machi 27, 2018 mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Wajumbe wakifuatilia kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) uliofanyika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Machi 27, 2018 mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  


Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images