Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya The Brothers Johnson ya Stomp! ilitutesa sana

The Rights of Women in Islam

$
0
0
The Rights of Women in Islam

BISMILLAHI RAHMAAN, RAHIM.

 In the name of Allah, the Most Gracious, and the Most Merciful


Compiled by Leila Sheikh






MANY issues are brought to light of the atrocities committed against Muslim Women on the mistaken belief that it is an Islamic Prescription. This is in contrast to the fact that the Koran strongly condemns all forms of oppression and injustice and that Islam is a Faith based on Peace.


Allah (SW) is protective of the downtrodden and oppressed classes of people and in fact favors women but Muslim societies in general based on cultural patriarchy and NOT on Islamic Thought and Practice, tends to be far more concerned with the control of women’s bodies; thoughts and action rather than with the Human Rights of Women as stipulated in the Holy Koran.

When women’s Rights are discussed by the Muslim Orthodoxy which is highly patriarchal for having integrated more`s and beliefs from their ethnic and cultural practices and which are NOT Islamic in origin and practice, women’s chastity is brought into focus, not their Right to Responsible Freedom.


The Koran is particularly solicitous of domestic well being and development but despite this, Muslim Women have been the target of the most serious violation of Human Rights.


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURISHA CHAKECHAKE PEMBA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika swala ya Magharibi na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, wakati wa hafla ya futari ya pamoja aliyoiandaa katika Makazi yake Ikulu ndogo Mjini Pemba jana Agosti 7, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki futari ya pamoja na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, aliyoiandaa katika Makazi yake Ikulu ndogo Mjini Pemba jana Agosti 7, 2013.
Baadhi ya wananchi wa Pemba walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wageni wake baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa katika makazi yake Ikulu ndogo mjini Pemba, jana Agosti 7, 2013. Picha na OMR.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA ASKARI WOTE WALIOSHIRIKI MAONESHO YA NANE NAN

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja (pichani) ameelezea furaha na shangwe yake kufuatia ushindi wa jana, Jumatano Agosti 07, 2013 kwa Jeshi la Magereza kuibuka Mshindi wa jumla katika Maonesho ya Wakulima - Nane Nane Kitaifa yaliyofanyika katika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma.

Katika salaam zake za pongezi Kamishna Jenerali Minja pia amewapongeza Wakuu wa Magereza Mikoa, Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara, na Askari wote kwa jumla kwa namna walivyoweza kushiriki kikamilifu katika kuleta ushindi wa kwanza katika Taasisi za Uzalishaji za Serikali, Banda Bora, Kilimo na Mifugo hata katika Maonesho ya Kikanda ikiwemo Kanda ya Magharibi iliyojumuisha Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora pamoja na Kanda ya Mashariki iliyojumuisha Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro kwa kuibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za Uzalishaji za Serikali.
"Nimepokea kwa furaha kubwa na shangwe habari za ushindi huo wa kwanza wa jumla katika Maonesho ya Wakulima Kitaifa na hata ushindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za Uzalishaji za Serikali katika Baadhi ya Kanda ambazo Jeshi la Magereza limeshiriki".
Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yangu mwenyewe, napenda kuwatumia salaam hizo za pongezi kwa ushindi huo kwani matokeo haya siyo yamenyesha tu kama mvua ya ghafla, bali ni matokeo makubwa ya mpango mkakati tuliouasisi - ninyi na mimi tangu nilipoteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kuapishwa rasmi tarehe 25 Septemba, 2012 kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini.
Aidha, amesisitiza kuwa ushindi huo bado ni changamoto kwa Jeshi la Magereza kuhakikisha kuwa wanajipanga vyema katika Maonesho mengine yanayofuata ili kuendelea kutetea nafasi hiyo ambayo imeleta sifa kubwa kwa Jeshi la Magereza hivyo kutekeleza mpango kazi wa sasa katika utendaji wa kazi unaotaka Matokeo makubwa sasa(Big Results Now).
Maonesho hayo ya Wakulima hufanyika kila Mwaka Kitaifa na Kikanda ambapo Kitaifa katika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma jumla ya washiriki zaidi ya 400 kutoka Wizara, Idara, Taasisi za Serikali zinazojitegemea na Makampuni Binafsi wameshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo ambayo yamefungwa jana na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Seif Idd.
                            Imetolewa na Mkaguzi wa Magereza, Lucas Mboje,
                            Afisa Habari wa Jeshi la Magereza Nchini.

WAKALA WA MAJENGO (TBA) KATIKA MAONESHO YA NANE NANE NZUGUNI DODOMA

$
0
0


Wakala wa Majengo (TBA), ulianzishwa mwaka 2002 kupitia Sheria ya Wakala Namba 30 ya mwaka 1997. Lengo la kuanzishwa TBA ni kutoa huduma bora na ya gharama nafuu ya makazi kwa watumishi wa umma na ofisi kwa Serikali na Taasisi zake.

Ikiwa ni taasisi muhumu ya Serikali iliyochini ya Wizara ya Ujenzi, TBA imeshiriki maonesho ya Wakulima maarufu Nane Nane ambayo hii leo yanafikia Kilele katika kanda mbalimbali na Kitaifa yanafikia Kilele katika Viwanja vya Nzuguni, mjini Dodoma.

Timu ya TBA iliyo katika banda lao Viwanja vya Nzuguni jana ilitembelewa na Blog hii na kuikuta ikiwa kamili katika utoaji huduma kwa wananchi ya nini ambacho TBA inakifanya kila siku katika utekelezaji wa shughuli zake.

Timu hiyo pichani kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Uhusiano, Mariam Lusewa, Meneja Miradi Maalum, Edwin Nnunduma, Afisa Miliki, Pendaeli Mhufu na Mhandizi Mazingira, Mtapuli Juma.
 Afisa Miliki, Pendaeli Mhufu (kushoto) akihudumia wananchi.
 Wageni wakisaini kitabu cha kutembelea banda hilo na kutoa maoni yao juu ya huduma.
 Kutoka Kulia ni Pendaeli Mhufu, Mariam Lusewa na Mtapuli Juma wakiwa na nyuso za furaha wakati wa kuhudumia wananchi waliotembelea banda lao Nzuguni Dodoma.
 Kaimu Afisa Uhusiano, Mariam Lusewa akiwasikiliza mwananchi  aliyetembelea banda lao jana kupata taarifa mbalimbali.
 Meneja Miradi Maalum, Edwin Nnunduma pamoja na Kaimu Afisa Uhusiano, Mariamu Lusewa wakiwasikiliza wananchi na kuwapa maelezo ama majibu ya maswali yao.
Kaimu Afisa Uhusiano, Mariam Lusewa akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda lao jana kupata taarifa mbalimbali.

Article 4

mkataa kwao mtumwa

Shusho, Kilahiro kuhudumu Washington DC wikiendi hii

$
0
0
Watumishi wa Mungu Christina Shusho na Upendo Kilahiro, mwishoni mwa wiki hii watahudumu katika jiji la Washington DC na Vitongoji vyake (DMV).
Shusho na Kilahiro ambao ni miongoni mwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, wameshawasili Washington DC tayari kwa huduma hiyo.

Naibu waziri wa maji alipotembelea miradi ya maji wilayani Siha

$
0
0
 Moja ya tanki la maji (kileleni) lililopo jirani na mashamba ya ngano west Kilimanjaro wilani Siha.
 Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Siha Dk Charles Mlingwa na baadhi ya maafisa wa mamlaka za maji wa wilaya za Moshi na Siha wakipanda kwenda kutizama moja ya matanki ya maji .
 Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Siha Dk Charles Mlingwa na baadhi ya maafisa wa mamlaka za maji wa wilaya za Moshi na Siha wakipanda kwenda kutizama moja ya matanki ya maji.

NMB YASHIRIKI FUTARI NA WATEJA WAKE

$
0
0
Mwishoni mwa wiki Benki ya NMB ilishiriki futari na wateja wake jijini Zanzibar.Hii ni katika kuendeleza mahusiano mazuri ambayo yamekwisha jengeka baina ya wateja wa NMB na Benki ya NMB.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akishukuru uongozi wa NMB kwa kuandaa wasaa mzuri na kushiriki katika kukamilisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Hii ilikua katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB tawi la Zanzibar kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean view Zanzibar mwishon mwa wiki.

Maofisa wa NMB wakiwa wameambatana kuingia ukumbini na mgeni rasmi(katikati) katika hafla hii ya kushiriki futari na wateja wa NMB mjini zanzibar

Meneja Mawasiliano NMB, Josephine Kulwa nae hakubakia nyuma kushiriki wasa mzuri na wateja wa NMB

Mkuu wa kitengo cha akaunti binafsi wa NMB, Abdulmagid Nsekela akiongoza wageni waalikwa katika kupata futari

Tigo yakabidhi Bajaji kwa washindi saba wa droo ya tatu ya 'Miliki Biashara Yako'

$
0
0
 Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa droo ya tatu wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Khalid Shabani katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.
 Washindi wa droo ya tatu wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ (kutoka kushoto) Bw. Sande Juma, Tito Mkude  na Iddi Zonki wakikagua Bajaji walizokabidhiwa kutoka kwa kampuni hiyo ya simu katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga akihojiwa na Waandishi wa Habari katika hafla ya makabidhiano ya washindi wa promosheni 'Miliki Biashara Yako' iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.

CLIMAX - SHORT FILM FULL LENGTH (OFFICIAL VIDEO)

$
0
0
Climax is a short film that focuses on choices we are making and illustrates a life drama dilemma of a couple that found themselves struggling to survive. After husband lost his job and failed to control his family, Amanda, a middle-aged wife decided it was time for her to move on with another man. Jay or Jacob, the husband, couldn't digest it and decided to revenge by murdering both his wife and her new love. After accomplishing his intent, Jay is found dead at the scene leaving behind questions. 

 SHORTFILM: CLIMAX (INLIFETHEREARETWO) 
SET LOCATION: HOUSTON, USA 
DIRECTOR: HENRY 
SHOT/EDITED: HEFEMISTUDIOS 
SCRIPT: HEFEMI RUNNING-TIME: 8:47MIN 
CAST: LAMBERT, SONIA, ABDUL, & TARELL 
RELEASE: 08/08/2013

NMB YAZINDUA ASASI YA MAENDELEO YA KILIMO (NMB FOUNDATION FOR AGRICULTURAL DEVELOPMENT)

$
0
0
Mwanzoni mwa wiki Benki ya NMB ilizindua taasisi ya maendeleo ya Kilimo nchini Tanzania.Taasisi ambayo inakusudi la kuinua sekta ya kilimo kwa kuanzia ngazi ndogo kabisa inayomgusa mkulima mdogo hadi ngazi ya wakulima wakubwa na kilimo cha biashara.Wakulima wadogo wadogo wamekua hawatambuliki kutokana na kutokua na mtaji wa kutosha na uwezeshwaji kutokuwepo.Hivyo Benki ya NMB kwa kupitia taasisi hii itawasaidia wakulima kwa kupitia vyama au vikundi ili kuwezeshwa katika uzalishaji na kuinua sekta nzima ya kilimo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu akisalimiana na baadhi ya wadau wa kilimo waliohudhuria uzinduzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo ya Benki ya NMB mjini Dodoma. Nyuma ya Waziri Nagu ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Mark Wiessing

Mkuu wa Shughuli za Kilimo wa Benki ya NMB, Robert Pascal akitoa maelezo juu ya Taasisi hiyo namna itakavyofanya kazi na kua msaada mkubwa kwa wakulima kabla ya uzinduzi uliohudhuriwa na baadhi ya wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakulima na wadau wa kilimo.

Baadhi ya wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mbalimbali mbali nchini na wadau wa Kilimo wakifuatilia Hotuba ya Afisa Mtedaji Mkuu wa Benki ya NMB, Mark Wiessing (kulia)

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu (katikati) baada ya kuzindua taasisi ya Maendeleo ya Kilimo ya Benki ya NMB mjini Dodoma . Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi,C.E.O wa NMB, Mark Wiessing na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo ya Benki ya NMB, Vallerian Fernandos.

Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB,Josephine Kulwa akimsikiliza kwa makini Mhe. Dk. Mary Nagu kabla ya hafla ya uzinduzi kuanza kati kati ni Meneja wa NMB kanda ya Kati Ole Loibanguti.

Wadau wajadili sera ya taifa ya sekta binafsi, watarajia makubwa

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu (katikati), akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye baada ya kufungua mkutano wa wadau wa sekta binafsi uliokuwa ukijadili mapendekezo ya rasimu ya sera ya Taifa ya Maendeleo ya Sekta Binafsi jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa TPSF, Bw. Aloyce Mwamanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu (katikati), akisisitiza jambo wakati wa kufungua mkutano wa wadau wa sekta binafsi uliokuwa ukijadili mapendekezo ya rasimu ya sera ya Taifa ya Maendeleo ya Sekta Binafsi jana jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (kulia) na Kaimu Mwenyekiti wa TPSF, Bw. Aloyce Mwamanga (kushoto).

TTCL yasaidia vituo vya watoto sikukuu ya Eid

$
0
0
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw.Peter Ngota akikabidhi msaada wa vyakula kwa Mwenyekiti wa Shirika la Femele Youth Help Age Trust,Bw Simon Mganga lililoko Pangani-Kibaha linalohudumia watoto yatima,na wanaoishi katika mazingira magumu katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam jana kusherehekea sikukuu ya Eid.
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Mawasiliano Tanzania, Bw.Peter Ngota akikabidhi msaada wa vyakula kwa wawakilishi wa shirika la Missionary of Charity la watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam jana kusherehekea sikukuu ya Eid.

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

Wadau wa maendeleo wametakiwa kuendeleza juhudi za kusaidia jamii hasa watu waishio katika mazingira magumu ili kuleta maendeleo na ustawi katika jamii.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Mawasiliano Tanzania, Bw.Peter Ngota jijini Dar es salaam jana wakati akikabidhi msaada wa vyakula kwa vikundi vya watu wenye mahitaji ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kushiriki katika kusaidia jamii na kusherehekea sikukuu ya Eid.

Akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa kuna umuhimu wa wadau mbalimbali kushiriki katika kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji ili nao waweze kupata huduma za msingi ikwemo elimu, afya na chakula.

Amesema kuwa TTCL inatambua uwepo wa makundi hayo ndio maana imeamua kuungana nao hasa wakati huu wa sikukuu ya eid el fitri ili nao watambue kuwa wanathaminiwa kama sehemu ya jamii.

Bw. Ngota amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishiriki katika shughuli za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii katika sekta mbalimbali.

Kwa upande mwingine, aliwaasa watoto wanaosaidiwa na vituo hivyo kujitahidi katika masomo na kufanya vizuri ili waje kufanya kazi katika kampuni hiyo ya wazawa hapa nchini.

“Nawaasa mjitahidi katika masomo ili hapo baadaye mje kufanya kazi katika kampuni hii,” alisema. Akizungumza kwa niaba ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu,mtoto Emiliam Joseph ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kuomba wadau wengine kuendeleza juhudi hizo.

Mwenyekiti wa shirika linalohudumia watoto yatima na wanaoishi katika mazigira magumu,Femele Youth Help Age Trust, Bw. Simon Mganga ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kukiri kuwa kampuni hiyo imekuwa mmoja wa wadau muhimu katika kusaidi shirika lake.

Naye mwakilishi wa shirika la Missionary of Charity, St Mary Domitila amesemakuwa msaada waliopata una thamani kubwa kwao kwani itoaji wa msaada huwa hauangalii kiasi bali ni nia ya dhati ya mtu kuamua kusaidia na hivyo kutoa wito kwa wadau wengine keundelea kusaidia.

Msaada huo wenye jumla ya Tsh milioni tatu unajumuisha mchele,unga wa mahindi,mafuta ya kupikia na majani ya chai. Pia TTCL ilitoa simu kwa mashirika hayo katika juhudi za kuwarahisishia mawasiliano.

Kwa muda mrefu sasa, TTCL imekuwa ikishiriki kutoa msaada kwa vituo vinavyohudumia watu wanaoishi katika mazingira magumu.

NSSFyashinda tuzo ya mfuko bora katika maonyesho ya nanenane mkoani Dodoma

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii  (NSSF) yashinda tuzo ya mfuko bora katika maonyesho ya nanenane yaliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma katika viwanja vya Nzuguni, kushoto (mbele) ni Hafidh Y A, Chuga A, Kirondera N (Meneja wa Mkoa wa Dodoma) na Mpogole M, Kushoto (nyuma) Safina K na Amani M wakiwakilisha Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Mjini Dodoma.
Timu ya NSSF waliowakilisha Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii katika maonyesho ya kitaifa ya Nanenane yaliyofanyika mkoani Dodoma, katikati ni Meneja wa mkoa (Kirondera N) akiwa ameshikilia kikombe baada ya kukabidhiwa na mratibu wa maonyesho hayo.
Picha ya hati na kikombe cha mshindi wa kwanza wa maonyesho ya Nanenane ya Kitaifa mkoani Dodoma
Meneja wa NSSF mkoa wa Dodoma ,Bw. Kirondera akishikilia kikombe na hati aliyokabidhiwa baada ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii kuwa mshindi wa kwanza katika maonyesho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma.

BENKI YA FBME YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA SIKUKUU YA IDD

$
0
0
 
.Meneja wa benki ya FBME LTD mkoa wa Arusha Ramadhani Lesso  akikabidhi misaada mbalimbali kwa mama mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr  jijini Arusha leo kwa ajili ya sikukuu ya Idd El Fitiri,misaada hiyo inadhamani ya shilingi laki saba na nusu kwa vituo viwili pamoja na cha Matonyok kilichopo Olasiti.
 Meneja wa benki ya FBME LTD mkoa wa Arusha Ramadhani Lesso  akikabidhi misaada mbalimbali kwa mama mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Matonyok kilichopo Olasiti Bi.Emmy Sitayo kwa ajili ya sikukuu ya  Idd El Fitiri,misaada hiyo ina thamani ya shilingi laki saba na nusu kwa vituo viwili pamoja na cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr  jijini Arusha.
Afisa wa benki ya FBME LTD, Mnukwa Ally akiongea na watoto waishio katika mazingira magumu katika kituo cha Matonyok kilichopo Olasiti,mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali  iliyotolewa na benki hiyo kwaajili ya sikuu ya Idd El Fitiri.Picha na Pamela Mollel.

========  =======  ======
Na Pamela Mollel,Arusha

JAMII nchini imeaswa kuwajali watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko kwenye vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuwapatia misaada mbalimbali ili waweze kuishi kama watoto wengine waishivyo majumbani 

Rai hiyo ilitolewa jana na Meneja wa  FBME Benki LTD mkoa wa Arusha Ramadhani Lesso wakati akikabidhi misaada mbalimbali ya vyakula kwaajili ya sikukuu ya Idd El Fitiri katika vituo viwili vya kulelea  watoto yatima cha Matonyok kilichopo Olasiti na kituo cha Abu-Abdulrahamani kilichopo Jr jijini Arusha

Alisema ni vyema jamii ikatambua uwepo wa watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko kwenye vituo, kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali kama wanavyopata watoto wa majumbani kwani ni haki yao ya msingi na kuondokana na tabia mbaya ya kuwanyanyapaa na kuwaona ni mzigo kwa jamii

“Tukiwajali hawa watoto hata kwa Mungu tunapata dhawabu kwani wengi wao hawajapenda kuwa katika mazingira haya,wengine wamefiwa na wazazi wao hivyo kujikuta wakiwa watoto wa mitaani”alisema Lesso

Aidha alitaja moja ya sababu iliyowafanya kutoa msaada huo ni pamoja na kuguswa kwa hali ya watoto waishio katika mazingira magumu hivyo kuamua kutoa faida kidogo waliyopata kama benki ili wawezekurudisha katika jamii

Meneja huyo alikabidhi misaada yenye dhamani ya  shilingi laki sabana na nusu katika vituo viwili ambapo kila kituo walitoa sukari,mafuta ya kupikia,mchele,sabuni za kufulia,madaftari na penseli

Mlezi katika kituo cha Matonyok kilichopo Olasiti chenye watoto(40) Bi.Emmy Sitayo  na Mlezi wa kituo cha Abu-Abdulrahamani chenye watoto(21) kilichopo Jr ,  Mama Abdulrahamani kwa nyakati tofauti walishukuru benki hiyo ya FBME kwa kuwakumbuka kipindi hichi cha sikukuu ya Idd na kuwataka makampuni na jamii kuiga mfano huo huku wakitaka  zoezi hilo liwe endelevu kwa watoto yatima na wasiojiweza.

news alert: teknolojia ya mstari wa goli yazinduliwa leo kwa ligi kuu ya Uingereza

$
0
0
Teknoljia ya mstari wa goli  ajili ya Ligi Kuu ya Uingereza imezinduliwa leo na kusifiwa kama moja ya maendeleo muhimu toka sharia za soka ziwekwe na kuanza kutumika miaka 150 iliyopita.


Teknolojia hiyo ijulikanayo kama ‘The Hawk-eye’ (jicho la mwewe) inatumia kamera 14 ambazo zitatuma ujumbe ndani ya sekunde moja katika saa ya mwamuzi pamoja na kifaa cha sikioni cha mawasiliano mara tu mpira utapovuka mstari wa goli.



Watumiaji wa kwanza wa kifaa hicho watakuwa timu za Manchester United na Wigan Jumapili ijayo katika mchezo wao wa ngao ya hisani kuashiria kuanza rasmi kwa ligi hiyo katika uwanja wa Wembley.


Cheki Video hii ya jinsi kifaa hicho kitavyofanya kazi

MBUNGE WA TEMEKE MHE ABBAS MTEMVU AFUTURISHA DAR

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Segerea, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, wakati wa kula  futari iliyoandaliwa na Mtemvu kwa waumini mbalimbali juzi jijini Dar es Salaam.
 Wageni waalikwa wakipata futari kwenye mgahawa wa City Garden, Gerezani, Dar es Salaam

                                                       Akina mama wakipata futari

                                                              Acha tupate futari ya mwisho mwisho

 Sheikh wa Msikiti wa Azimio, Tandika Dar es Salaam, akitoa mawaidha wakati wa futari hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema akitoa salmau za serikali wakati wa futari hiyo.
 Mtemvu akimpongeza DC wa Temeke, Sofia Mjema. Kulia ni mkewe Mtemvu
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida akizungumza na wanahabari wakati wa futari ambapo alisisitiza wanachi kudumisha amani nchini.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Tangazo Maalum Kwa Wapenzi na Mashabiki wa Timu ya Yanga Kutoka Kwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji Juu ya Kuitisha Mkutano wa Dharura Agosti 18 Kujadili na Kuamua Swala la AZAMA TV

$
0
0
 Mwenyekiti wa Yanga-Yusuph Manji
---
  1.   Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu (Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016

2.   Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha kuwa mkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGA zisirushwe hewani na Azam Media.

Kwa kuwa wawazi, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA kupitia vyombo vya habari tarehe 29 Julai, 2013 ambapo iliweka bayana sababu zake na kueleza kuwa YANGA haina tatizo na vilabu vingine vya mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake za Vodacom Premier League katika Azam Television.

Sote tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya ziada” inatumika kupotosha msimamo wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha Klabu ya YANGA hadharani.

Juu ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu ambavyo vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu, havina uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati ya Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu zinazojionyesha wazi.

Inadhihirika wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama kuilazimisha YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.

Kwa kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu.

Kwa kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi waje tujadiliane na kuamua suala la Azam Television kurusha mechi za YANGA.

(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images