Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 219 | 220 | (Page 221) | 222 | 223 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Moto mkubwa unaripotiwa kuzuka asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyetta (JKIA) jijini Nairobi.

  Chanzo cha moto huo bado hakijatambulika na juhudi za kuuzima zinaendelea, ambapo vikosi mbalimbali vya zimamoto vipo uwanjani hapo kuthibiti janga hilo.

  Uwanja huo hivi sasa umefungwa na hakuna ndege kutua ama kuruka isipokuwa kwa dharura tu.

  Moto huo unasemekana ulianza majira ya saa 11 za alfajiri sehemu za idara ya uhamiaji na kusambaa katika eneo la abiria wa kimataifa.

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anaripotiwa kuelekea uwanjani hapo hivi sasa kukagua janga hilo, na habari zinasema hakuna mtu aliyedhurika kwa moto huo ingawa hasara iliyopatikana inasemekana ni kubwa na kwamba abiria wengi wamekwama uwanjani hapo. Barabara kuu ya kuelekea JKIA imefungwa.

  Na habari zinasema kwamba baada ya saa tatu za ku pambana na janga hilo, hatimaye moto huo umeweza kudhibitiwa na hakuna mtu aliyeripotiwa kudhurika. Abiria waliokuwa wanasafiri wamepelekwa mahotelini na ndege zilizokuwa zitue JKIA zimeelekezwa kutua uwanja wa kimataifa wa Moi, Mombasa.

  0 0
 • 08/06/13--23:00: --none--


 • 0 0
 • 08/06/13--23:01: KUMBUKUMBU
 • Hayati Ethro Gadau Wella

  Tarehe 07 Agosti 2008, miaka mitano leo toka ulipoitwa na Muumba wetu.  Ni vigumu kuamini kamahaupo nasi hapa duniani kwani bado tunakukumbuka kwa uongozi wako bora na upendo katika familia.  Mme wako Eleutheirus Wella;  watoto wako Pamela, Andrew, Jane, Clara;  wajukuu zako Labron, Naomi, Janell;  ndugu, jamaa na majirani zako wote wanazidi kukuombea ili upumzike mahali pema huko peponi,  Amina. 


  BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA


  JINA LAKELIHIDIMIWE


  0 0

  Mhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto Shackshazi Rahim dawa ya minyoo katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini.
  Mtoto mkazi wa Kunduchi, Rukia Ramadhani akipimwa uzito katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (Mobile Clinic) la Benki ya NBC mahali hapo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini. Anayempimawa pili kulia ni muuguzi wa gari hilo, Eliza Shayo.
  Mhudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (mobile clinic) la Benki ya NBC, Wilbard Kiria (kushoto) akimpa mtoto Gift Lucas dawa ya minyoo katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari hilo katika eneo la Kunduchi Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini.

  0 0
 • 08/07/13--01:12: HOJA YA MDAU KUHUSU MUUNGANO
 • Bwana michuzi nashukuru sana kwa kazi yako ya kutuelimisha na kutujulisha kwa mambo yanayotekea nyumbani nashukuru pia kwa kuweza kutuwekea hoja kubwa kama hii katika mtandao na kutupa uwanja wa kuweza kuchangia maoni yetu katika kupata katiba ambayo itakuwa ni ngao ya watanzania wa bara na visiwani,

  Ningependa kwanza kwaombea wazee wetu walio tangulia kwenye haki waanzilishiwa taifa letu TANZANIA MZEE J.K.NYERERE NA MZEE ABEID AMANI KARUME, Wazee wetu hawa wakati wanaanzisha huu muungano walikiuwa na nia nzuri ukifatiria na hali ya siasa iliyo kuwepo wakati huo ,ni kweli kabisa upendo wa wazee hawa ulikuwa ni wa haina yake na mpaka walipofikia kuamua kitendo hicho walikuwa ni majasiri na mashujaa.

  Ni kweli muungano umetuletea mambo mazuri mengi na kunamambo ambayo ukiangalia kwa kirefu au kwa upana unaona kuna makosa ambayo yanaweza kutatuliwa na watu wanaoipenda Tanzania (maana yake naposema hivi kuna vibaraka wanaotumiwa na watu kutoka nchi za nje ili kuvunja muungano huu hau kuigawanya nchi kwa makabira na kwa dini).


  0 0

  Pichani juu askari wakikagua mwili wa  Erasto Msuya, mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana ambaye pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kufa papo hapo.

   Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mfanya biashara huyo alifariki dunia mara baada ya majibishano ya risasi baina ya majambazi hayo na mfanya biashara huyo ambapo alizidiwa  nguvu na kupigwa risasi na kufariki dunia

  Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara. 

  Habari zaidi tuvute subra kidoogo,
  tutazidi kufahamishana kadiri ya taarifa zitakapokuwa zikiingia.
  Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2013. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki,  Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla. Picha na IKULU.

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na baadhi ya wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2013. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki,  Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Assah Mwambene (kulia) akizungumza jambo wakati yeye na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko walipotembelea banda la Magazeti ya Serikali  Tanzania Standard Newspapers (TSN) Wachapishaji wa magazeti ya Daily News, HABARILEO, Sunday News, HABARILEO  Jumapili  na Spotileo, jana Nzuguni Dodoma. Kushoto ni Afisa Masoko na Mauzo wa TSN, Chikira Mgheni na Afisa Masoko, Francis Kihinga. Viongozi hao kutoka Wizarani walitembelea Taisisi zote zilizo chini Ya Wizara hiyo ikiwa ni Idara ya MAELEZO, TSN, TBC, BASATA, BODI YA FILAMU, TASUBA, IDARA YA MICHEZO NA ILE YA VIJANA.


   Kihinga akizungumza jambo na Wakurugenzi hao.
   Chikira akimkabidhi zawadi Mwasoko.
   Mwambene akipokea zawadi kutoka kwa Chikira wa TSN
   Wakurugenzi hao walifika banda la MAELEZO na kumkuta Lidya Churi na kuwapa maelezo ya banda.
   Wakiwa Bodi ya Filamu na Kulia ni Afisa Ukaguzi wa Filamu, Tabu Magembe
   Wananchi wakiwa banda la TASUBA

   Wakurugenzi wakiwa Banda la TASUBA
   Wakiwa Idara ya Michezo
   Wakurugenzi wakiwa Banda la Idara ya Vijana


  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Segerea, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akiwaonesha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ilala (Jimbo la Segerea), kituo kipya cha Polisi cha Tabata, Dar es Salaam, walipokuwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu jimboni humo.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Legends dont speak much cause we believe action speaks louder than words. So, come join the legends @isumba lounge (jollies club) this Eid and dance to ur favourite tunes from the 80's to the late 90's, behind the 1 and 2 DJ John Dillinga aka the Legend is Back, DJ Fast Eddy and DJ Young Kelvin. Party starts on eid eve 2 the 2nd eid. Doors open 9pm, entry on the 1st eid 10k b4 mid midnight 15k after mid night dont miss it.


  0 0


  Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwakaribisha wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mufti Mkuu wa Tanzania na Wafanyakazi wa Wizara ya Mamob ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Futari Maalum aliyowaandalia nyumbani kwake jana, jijini Dar es Salaam. 
  Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe. 
  Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Waziri. 

  0 0

  Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifurahia Kombe baada ya kuibuka mshindi wa Kwanza katika Kundi la Wizara za Sekta Huduma ya Jamii kwenye Kilele cha Sherehe za Sikukuu ya Wakulima NaneNane 2013 zilizofanyika Kitaifa kwenye Uwanja vya Nzuguni,Dodoma leo

  Wadau wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI pamoja na Taasisi zake picha ya pamoja ya ushindi huo katika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu 

  0 0

  ???????????????????????????????
  Mwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa kwa vijana Bw. Ahmed Alhendawi alipokutana na Raymond Maro balozi wa Tanzania kwa upande wa vijana kwenye jumuiya ya afrika mashariki. ???????????????????????????????
  Raymond Maro akiwa na Flora Nducha, mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa mataifa 
  . DSC04584
  Raymond Maro ndani ya jiji la Newyork akijionea jiji lisilolala a.k.a Tofaa Kubwa.

  0 0

   Mwezeshaji katika baraza la katiba la wabunge wanawake Tanzania Jaji Mstaafu Mhe. Jaji Mstaafu Eusebio Munuo akiwakilisha mada kuhusu yaliyomo katika rasimu ya katiba.
   Wabunge wanawake wanaunda baraza la katika la Chama cha wabunge wanawake Tanzania (TWPG)  wakifuatilia mada kwa makini
   Wabunge wanawake wanaunda baraza la katika la Chama cha wabunge wanawake Tanzania (TWPG)  wakifuatilia mada kwa makini
   Wabunge wanawake wanaunda baraza la katika la Chama cha wabunge wanawake Tanzania (TWPG)  wakifuatilia mada kwa makini. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova akionesha Bastola aina ya RAM P.9X19 zikiwa na risasi tatu (3) ndani ya Magazine mbele ya waandishi waliokuwepo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Makao makuu ya Polisi Augost 7, 2013.jijini D ar es salaam,baada ya kuendesha msako mkali na kufanikiwa kuzikamata pamoja na kukamatwa kwa watuhumiwa 196 kwa makosa mbalimbali na kukamata magari saba(7)na Bajaji moja ya miguu mitatu.
  Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria kwenye mkutano huo le Augost 7, 2013makao makuu ya polisi jijini Dar es salaam.

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi kitita cha kuhamasisha ulishaji bora wa watoto katika jamii kwa kukata utepe wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 7.8.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia waalikwa na wananchi wa Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani.yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 7.8.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahi alipokutana na mtoto Muktar Abdul mwenye umri wa miezi sita akiwa na mama yake Lucia Lingwanda, mkazi wa Chanika, wilayani Ilala, wakati Mama Salma alipotembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya unyonyeshaji duniani katika sherehe zilizofanyika Mnazi Mmoja tarehe 7.8.2013.
  Baadhi ya wanawake waliohudhuria sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyofanyika Mnazi Mmoja na kufungwa rasmi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 7.8.2013.

  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na madiwani wa CCM wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wiki iliyopita.

  Katika hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chamilion wa Uganda kuwa "fitina yako bahati yangu" wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomo wazi wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM wilayani hapo.
  Diwani wa CCM Ndugu  Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.
  Kuchaguliwa kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.
  Kabla ya uchaguzi huo palikuwa na mgogoro mkubwa kati ya madiwani wa CCM, mgogoro ambao ulitatuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye kufuatia ziara yake ya kimyakimya ya siku moja wilayani Kibondo ambapo alikutana na madiwani hao wa CCM kwa zaidi ya masaa manne.
  Matokeo haya ni kinyume kabisa na kile kilichoandikwa na Gazeti la Tanzania Daima la Agosti 7,2013 kuwa ' WIKI NGUMU KWA CCM" wakieleza kuwa CCM wangepoteza uchaguzi huu. Fitina hiyo ya TanzaniaDaima imegeuka kuwa bahati kwa CCM maana imetembeza kichapo cha haja kwenye uchaguzi huo.
  Nape akiongea juu ya ushindi huo akinukuliwa na redio moja ya Mjini Mwanza alisema "ushindi huo ni mawingu mvua zenyewe zinakuja. Unajua hawa jamaa wanawekeza kwenye migogoro ndani ya CCM ili ikitokea hatukuelewana mahali basi wanazamia, hapa nimewazidi akili" alikaririwa Nape.  0 0

   Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Iddi akimkabidhi Kikombe cha Zawadi ya Mshindi wa kwanza wa jumla wa Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mlasani Kimaro akipokea kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza katika Kilele cha Sherehe za Maonesho ya Nane Nane, yaliyofanyika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma
   
   Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Mlasani Kimaro akinyanyua Kikombe  cha Ushindi wa Jumla katika Kilele cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yaliyofanyika Nzuguni Dodoma na yamefungwa rasmi na Balozi Seif Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(
   Makamanda wa Jeshi la Magereza walioshiriki Maonesho ya Nane Nane Kitaifa wakifurahia ushindi walioupata kuwa Mshindi wa kwanza wa jumla katika Maonesho ya Wakulima  - Nane Nane yaliyofungwa rasmi na Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif
   
  Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza walioshiriki Maonesho ya Nane Nane Kitaifa wakifurahia ushindi wa kwanza wa jumla wa Maonesho hayo huku wakiinua juu Makombe ya ushindi huo baada ya kukabidhiwa rasmi na Mgeni Rasmi
  Picha  zote na  Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

  0 0

   Maandamano ya ushindi baada ya Bunge kuibuka kidedea katika medani ya utoaji wa huduma bora ndani ya viwanja vya Nane Nane mjini Dodoma. Jopo la majaji lililitangaza Bunge kuwa mshindi wa tatu Nane Nane 2013.
  Picha ya pamoja ya kusherehekea ushindi na Prosper Minja- Bunge

  0 0
 • 08/07/13--16:53: HOJA YA HAJA KUHUSU MUUNGANO
 • Bwana michuzi nashukuru sana kwa kazi yako ya kutuelimisha na kutujulisha kwa mambo yanayotekea nyumbani nashukuru pia kwa kuweza kutuwekea hoja kubwa kama hii katika mtandao na kutupa uwanja wa kuweza kuchangia maoni yetu katika kupata katiba ambayo itakuwa ni ngao ya watanzania wa bara na visiwani,

  Ningependa kwanza kwaombea wazee wetu walio tangulia kwenye haki waanzilishiwa taifa letu TANZANIA MZEE J.K.NYERERE NA MZEE ABEID AMANI KARUME, Wazee wetu hawa wakati wanaanzisha huu muungano walikiuwa na nia nzuri ukifatiria na hali ya siasa iliyo kuwepo wakati huo ,ni kweli kabisa upendo wa wazee hawa ulikuwa ni wa haina yake na mpaka walipofikia kuamua kitendo hicho walikuwa ni majasiri na mashujaa,
  Ni kweli muungano umetuletea mambo mazuri mengi na kunamambo ambayo ukiangalia kwa kirefu au kwa upana unaona kuna makosa ambayo yanaweza kutatuliwa na watu wanaoipenda Tanzania (maana yake naposema hivi kuna vibaraka wanaotumiwa na watu kutoka nchi za nje ili kuvunja muungano huu hau kuigawanya nchi kwa makabira na kwa dini)

  Wa Tanzania kubomoa ni rahisi na kujenga siyo mchezo ndugu zangu tukumbuke kitukimoja sisi kama waafrica tumetawailiwa na waarabu wariotoka makwao tumetawaliwa na wazungu walio toka makwao na kutufanya watumwa na  kuuwa  mababu zetu waliokuwa wakitembea maili na maili na kutufanya sisi ni mbwa na leo hii hayo yote tuna aanza kuyasahau na kutaka kurudi katika ukoloni wa mambo leo,

  Ndugu zangu tukumbuke haya yote na damu za mababu zetu kutokea mwanza,kigoma,tabora,songea,tanga manyema congo,na ungunja,pemba, na mikoa yote ya TANZANIA,Damu iliyomwangika isije ikapoteabure tukumbuke tunapotoka ndio tupate katiba yenye utaifa, ni mazuri ghani yaliyopo kwenye katiba ya zamani? na mambo ghani ambayo hayafai kwenye katiba hiyo ya zamani,

  je mfumowa serikali mbili unafaa au vipi? au serikari tatu? au tuwe na serikali moja tuu na nchi iwe na state maana yake itakuwa inaitwa UNITED STATE OF TANZANIA and tuwe na Raisi ,makamu waRaisi na Waziri mkuu ?ndugu zangu kwanza hapa shida siyo serikari tatu au mbili au moja shida ni moja tuu ambayo inarudisha maendeleo nyuma na kufanya asilmia karibu 65 ya waTanzania kubaki masikini na kuendelea kuwa masikini,Tatitizo ni hili hapa ni  Good governance, Responsibility.Acountabilty, Deliverance and good economic policies.nakingine ni hiki agenda ya  Tanzania au Manifesto ya Tanzania iko wapi wakati wa mwalimu ilikuwa ni ujamaa wa kujitegemea je sasa hivi nini?

  kwa upande wangu kutokana na nchi yetu kuwa bado ni maskini hatuwezi kuwa na serikari tatu uendeshaji wake utakuwa ni wagharama na pila atuwezi kuwa na maraisi watatu,maoni yangu yako very simple ningependa tuwe na serikali moja tuu maana yangu mimi sijui kuna nchi inaitwa Tanganyika au Zanzibar kitu nachojuwa ni kwamba nchiziliungana na kutengeneza au kuzaa taifa linaloitwa Tanzania,
  kwa maana yangu au kuelewa kwangu ni kwamba tunapashwa kuwa serikali moja ambayo itakuwa na Raisi na makamu wake na waziri mkuu,
  baadala ya ya kuwa na mikoa tuwe na state na hizi state zitakuwa chini ya serikali ya katikati au central,
  hizi state zitakuwa na Katikiro natumia jina la kiafrika  ambaye hatakuwa anachaguliwa na wananchi na kazi zake ni kuwatumikia wananchi na kuhakikisha hanatimiza mipango yote ya serikali kwa uhakika na bila mchezo na muda wake wa kufanya kazi ni miaka kumi mitano,na mitano kama hatachaguliwa na wananchi tena.
  Raisi hatachaguwa Governor ambaye kazi yake ni kuangalia  mambo ya utendaji wa sela za serikali yani sera za nchi siyo za chama na kazi ya usalama yaani ataitwa Overseer na hii ndiyo itakuwa kazi yake tu na anaweza kuongezewa majukumu mengine,

  Jee hizi state zitaendeshwa vipi zitakuwa zinakusanya mapato na asilimia 37 yawe yanabaki kwenye state na asilimia 63 yanaenda kwenye Central government na tuwe na mawaziri wa kuitumikia nchi moja na na tuwe na bunge moja tu lenye wabunge 250 wabunge 70 kutoka visiwani na wabunge 180 kutoka bara na tuwe na bunge la wezee au nyumba ya juu amabayo itakuwa na wazee 50 tuu ambayo itakuwa na wawakilishi wa dini waislam2,wakristu2,wahindu2,wazee wetu wa au wakuu wa chief2,nafasi zilizi baki watachuguliwa na bunge na kuteuliwa na raisi yaani retired jaji,police,wakuu wa majeshi,doctors,Raisi,mawaziri,na kiwango cha umri ni kuanzia miaka 60.
  Pamaoja na haya yoteniliyosema bado tutakuwa pale pale kama hatutaweza kuwa na agenda au manifesto ya nchi siyo ya CCM,au CHADEMA ,au CAF,DP,auTLP ni mengi ya kusema hapa lakini naona kwanza ni achihe hapo kwenye swala la serikari moja,
  Je kuhusu serikali mbili ni vipi? Kama tutaendela kuwa na serikali mbili je nini kinachotakiwa kufanywa sababu visiwani kunaonekana kwake mpaka sasa inaonekana kama ni nchi ndani ya muungano iko  na bendera,iko na wimbo wa taifa, lakini bara hakuna wimbo wala bendera  kw upande wangu tungeweza kujifunza kwa wenzetu wa hapa uingereza wako na nchi nne ndani ya muungano wa united kingdom, je nini ambacho tunacho weza kujifunza kutoka kwao au tunaweza kijifunza nini  kutoka kwa hawa jamaa wa united emirates
  Ndungu zangu ningependa sana hoja hii tuichambuhe kwa makini na kwa kirefu kutokana na historia yetu na tunapotoka  sababu naamini Tanzania ya leo iko na wasomi wengi na wenye vipaji naomba sana tufunguke tuwe wazi tutoe maoni kwakirefu
  Natanguliza shukrani kwa bwana Mchuzi na kwa waTanzania  wote watako soma maoni yangu au kuchangia maoni yetu
  Asanteni sana 
  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   MUNGU IBARIKI AFRICA 
  MDAU YUSEF

older | 1 | .... | 219 | 220 | (Page 221) | 222 | 223 | .... | 3272 | newer