Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MPINA ALIA NA WANAODANGANYA CHAPA

$
0
0

Na. John Mapepele, Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa, Luhaga Mpina ametoa onyo kali kwa viongozi wa Serikali katika Halmashauri zote nchini wanayoihujumu operesheni maalum ya kitaifa ya kupiga chapa mifugo inayoendelea nchi nzima kwa kutoa taarifa za uongo zinazoonesha kuwa mifugo mingi imepigwa chapa tofauti na hali halisi ambapo amesema Wizara yake itapita kila Wilaya kufanya tathmini ya kina baada ya tarehe ya mwisho ya upigaji chapa kitaifa iliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Marchi 31 mwaka huu ambapo watendaji watakaobainika kudanganya sheria zitachukua mkondo wake.

Aidha ametoa maelekezo kwa Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha kwamba mifugo yote inatakiwa iwe imepigwa chapa hadi tarehe ya mwisho iliyopangwa na kusiwe na visingizio vyaaina yoyote ikiwa ni utekelezazi wa Sheria ya Utambuzi,Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo Namba 12 ya Mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011. 

Maelekezo hayo aliyatoa jana akiwa Naibu Waziri wake Mhe. Abdalah Ulega na Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipotembelea mnada wa upili wa Kizota pembeni kidogo wa mji wa Dodoma kutoa tathmini ya zoezi la upigaji chapa nchini kabla ya siku ya mwisho ya upigaji chapa mifugo yote nchini ambayo ni tarehe 31/3/2018.

Waziri Mpina alisema, kulingana na takwimu ambazo Wizara imeletewa hadi tarehe 11 Machi, 2018 inaonyesha kwamba, jumla ya ng’ombe 16,744,355 kati ya 17,390,090 sawa na asilimia 96.3 ya ng’ombe wote nchini wamepigwa chapa. Aidha, jumla ya Punda 51,494 wamepigwa chapa nchini. 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) akimshika mkia ng’ombe kuangalia kama amepigwa chapa alipotembelea mnada wa Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma leo ambapo ametoa tathimini ya upigaji chapa unaoendelea nchini. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega(aliyenyosha mkono)akimwonyesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (mwenye kofia) chapa ya mifugo alipotembelea mnada wa Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma leo ambapo wametoa tathimini ya upigaji chapa unaoendelea nchini.Nyuma yake ni Kaimu Katibu Mkuu wa Mifugo Bi. Selina Lyimo, wakwanza kushoto mwenye shati la kitenge ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Wizara Dkt. Angelo Mwilawa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo mkoani Kigoma hivi karibuni. Tarehe ya mwisho kitaifa ya uhitimishaji wa kupiga chapa mifugo yote nchini iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa ni 31/3/2018. 


MKURUGENZI MADABA AMTUMBUA AFISA MANUNUZI

$
0
0
Habari na ruvumatv.co.tz

UKIUKAJI wa taratibu za manunuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma, ambako kumefanywa na Mkuu wa idara ya Manunuzi katika Halmashauri hiyo, Boniface Soko kumemfanya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Shafi Mpenda kumsimamisha kazi mtumishi huyo. 

  Mpenda alisema kuwa, Soko amekuwa akifanya hivyo kwa makusudi na kwamba Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imekuwa ikisisitiza na kutoa miongozo mara kwa mara namna ya kutumia mfumo wa Force Account, lakini yeye hazingatii hilo. 

Alisema kuwa mfumo huo umekuwa mzuri kwani unalenga kutumia mafundi wanaopatikana katika jamii, badala ya kutumia Makandarasi ili kuweza kuepuka gharama kubwa ambazo Serikali imekuwa ikitumia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali. 

  “Kimsingi akiwa ni mtaalamu ambaye nilikuwa nikimuamini na kumteua Katibu wa kamati ya manunuzi ndani ya Wilaya, kama mwongozo unavyoelekeza kwamba maafisa ugavi kuwa sehemu ya muundo wa kamati hiyo”, alisema Mpenda. 

Vilevile alibainisha kuwa cha kushangaza aliamua kutumia mfumo wa kikandarasi kutengeneza nyaraka husika akiaminisha kuwa ndiyo mfumo sahihi wa Force Acount, hali ambayo ilisababisha usumbufu mkubwa kwa uongozi wa Wilaya katika kutekeleza miradi miwili ya Vituo vya afya vilivyopo Wilayani humo. 

  Mpenda alifafanua kuwa, Soko alitengeneza malipo ya shilingi Milioni 8 na kuyapeleka Ofisi ya Mkurugenzi huyo ili aweze kumpitishia (Posho) kwa ajili ya kufanya malipo mbalimbali bila kupitisha kwenye kamati husika ya manunuzi ili iweze kuridhia juu ya malipo hayo. 

  Hivi sasa jambo hilo lipo katika hatua ya uchunguzi wa awali kwa kutumia kanuni ya 36 ya kanuni za kudumu, katika utumishi wa umma za mwaka 2003 ili kuweza kubaini chanzo cha madai hayo.“Sipo tayari kuona utaratibu wa kisheria ikiwemo na maelekezo ya Serikali kutozingatiwa katika Halmashauri hii, mtumishi atakayefanya hivyo sitosita kumshugulikia”, alisisitiza.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashuri ya Madaba Shafii Mpenda.

RC MAKONDA KUVITAJIRISHA VIKUNDI VYA JOGGING DAR.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametangaza mpango kabambe wa kuviwezesha vikundi vya mazoezi ya kukimbia (Jogging club) kwa kuweka utaratibu wa mashindano  ya kila Mwisho wa Mwezi ambapo kikundi kitakachoshinda kitapatiwa kiasi cha shilingi Million 10 Kama mtaji wa kufanya shughuli za kujikwamua kiuchumi.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kubaini idadi kubwa ya vijana hao wakimaliza mazoezi asubuhi hawana shughuli za kufanya hivyo wanakaa vijiweni na kitendo cha kukaa kijiweni wanaweza kushawishika kufanya vitendo vya uhalifu hivyo kwa kuwapatia mtaji itawawezesha kufanya shughuli za uzalishaji Mali utakaowakwamua kiuchumi.
HUU NI MWENDELEZO WA RC MAKONDA KUWEZESHA AJIRA KWA VIJANA.

Makamu wa Rais awasili Pemba kwa ziara ya siku tatu

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mshauri wa Rais wa Zanzibar Pemba Dkt. Maua Daftari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

MATUKIO YA PICHA WAKATI WA UZINDUZI VITUO SITA VYA POLISI VINAVYOHAMISHIKA

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, kukagua mazingira ya ndani ya moja kati ya Vituo vya Polisi Vinavyohamishika baada ya kuzinduliwa mwishoni mwa wiki na naibu waziri huyo lengo ikiwa ni kusogeza huduma za kipolisi karibu na wananchi.Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya Polisi Oysterbay,jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ahmada Khamis(kulia), baada ya kuzindua Vituo vya Polisi Vinavyohamishika katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, lengo ikiwa ni usogezaji karibu wa huduma za kipolisi kwa wananchi.Katikati ni Mkuu wa Shirika linaloshughulika na Usafirishaji wa Wakimbizi nchini (IOM), Dk. Qasim Sufi.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali ya Waandishi wa Habari baada ya Uzinduzi wa Vituo vya Polisi Vinavyohamishika lengo ikiwa ni usogezaji wa huduma za kipolisi kwa wananchi.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ,Mhandisi Hamad Masauni, akiwasili katika Viwanja vya Polisi Oysterbay wakati wa Uzinduzi wa Vituo vya Polisi Vinavyohamishika lengo ikiwa ni kusogeza huduma za kipolisi karibu na wananchi.Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na wengine kutoka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Emmanuel Lukula na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Muliro.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi na wageni waalikwa baada ya kuzindua Vituo vya Polisi Vinavyohamishika, lengo ikiwa ni kusogeza huduma za kipolisi kwa wananchi. Waliosimama ni Kikundi cha Polisi Jamii cha Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MAKAMU WA RAIS AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE LA Dkt. OMAR ALI JUMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya siku tatu Pemba ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli za maendeleo. 

Makamu wa Rais ambaye amewasili Pemba alasiri ya leo na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama ambapo alipokea taarifa za mikoa miwili ya Pemba. Pia Makamu wa Rais alizuru kaburi la Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi, Pemba na kuweka shada la maua. 

Aidha Makamu wa Rais aliwataka Wananchi wa Chumbageni kukumbuka historia na kurudi nyumbani, Makamu wa Rais aliyasema hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Chumbageni Wambaa. 

Kesho Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatazamiwa kuendelea na ziara yake ambapo ataweka jiwe la msingi katika Kituo cha Huduma za Mama na Mtoto Shumba Vyamboni .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Dk Omar Ali Juma (26 Juni 1941 – 4 Julai 2001) alikuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu nchini Tanzania, iliyokuwa inaongozwa na Rais Benjamin William Mkapa


Introduicing new bomb "Fimbo" (Official Music Video) by Jux

$
0
0
Award winning Tanzanian R&B Singer, Songwriter and performer Jux has released his first official track of 2018  ‘Fimbo’ Produced by Bob Manecky from AM Records and Abbah. 
The crooner is back after a 7 month silence since his chart topping last release ‘UTANIUA’. Jux is breaking his silence with this mid tempo feel good ballad and certified radio smash, ‘Fimbo’. This wavy Afro-pop tune has that signature Jux - Bob Manecky touch that has won him a multitude of fans over the years. The word Fimbo is Swahili for ‘Cane or Stick’ in the song he refers to his lover as a Cane/Stick as she’s been somewhat disciplinary and has set him on the right path in life and love.
When speaking about FIMBO Jux said, “I am so happy that my fans will get to hear Fimbo, It’s my first release of 2018 and I have not released anything since August last year so you can tell how excited I am to give them something to jam to”
The visuals to Fimbo were shot in Zanzibar, Tanzania and Directed by Hanscana.
Jux is also set to release his highly anticipated debut album later this year, ‘Fimbo’ is his first release aided by Mdee Music PR
Born as Juma Mussa Mkambala in 1989, Jux  is a Tanzanian recording artist and a songwriter. He entered the music industry in 2005 as a rapper before switching to RnB. His first solo track "Nimedata" which surprisingly did better than expected introduced him to the game where he has managed to dominate the R&B scene in Tanzania by dropping hit after hit.  
Over the years Jux has not only established himself as an RnB crooner but also a style Icon in the music industry with his fine sense of fashion and his undeniable swag. Jux is the CEO and Creative Director of East Africa’s most popular independently owned clothing brand ‘African Boy‘.

Introducing debut bomb "Jibebe" by Frida amani FT GBPY


MJADALA: Ni Yupi Afisa Mawasiliano wa Karne ya 21

ULEGA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA KWA MKAKATI MZURI WA KUINUA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kwa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na uvuvi haramu na kutatua kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwekeza kwenye Ranchi za mifugo.
Ulega ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kugagua Mwalo wa Muyobosi uliyopo Wilayani uvinza ambapo alisema jitihada hizo za wilaya zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na serikali kwa ujumla, kwani ina mkakati wa kutenga maeneo ya Ranchi kwa ajili ya wafugaji.
“Nataka niwahakikishie mimi na wizara yangu tutakuwa tayari kuhamia hapa kulisimamia jambo hili mtakapo tenga hayo maeneo ya kufugia, ili kuwaweka tayari wafugaji katika maeneo hayo na huo ndiyo muharobaini wa kwenda kuondoa  matatizo ya wakulima na wafugaji katika nchi yetu kwa mipango ya namna hii inawezekana kabisa, hicho ni kipaumbele chetu mimi na waziri wangu Mhe. Luhaga Mpina katika uongozi wetu tutahakikisha kama siyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji basi tutaindoa kabisa, kwa kushirikiana vyema na Halmashauri zetu” Alisema Ulega.
Ulega alisisitiza suala la mapambano dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa Rasilimali za uvuvi na suala zima la ufugaji wa samaki, nakuwaasa kuachana kabisa na utamaduni wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.
Naibu Waziri Ulega  alisema kuwa fedha nyingi zimewekwa katika mwalo huo wa Muyobozi na kuwataka wavuvi katika eneo hilo kuutumia vizuri mwalo huo wenye hadhi ya kimataifa ambapo ameleza kwa mwaka wa fedha uliopita mwalo huo peke yake umechangia kiashi cha shilingi milioni 28 “ Ninaamini kama mtapasimamia vyema mahala hapa patachangia pato la taifa mara nne zaidi ya mwaka jana. Ninyi ndo muwe walinzi wa kwanza wa rasilimali hizi ili nchi yetu iweze kuinuka” Alisisitiza
Awali, akiongea katika ziara hiyo mwenyekiti wa kijji cha Mwakizega ambapo mwalo wa Muhyobozi umejengwa Bw. Jaffari Abdalah, alisema mwalo huo unakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na gati la mwalo huo kuwa na urefu wa mia 20 ambazo ni chache kwa boti kuegesha kupakua na kupakia kabla na baadha ya shuguli za uvuvi , hivyo ameiomba serikali kuongeza urefu wa gati hiyo ili mitumbwi mikubwa na midogo iweze kufanya shughuli za uvuvi vizuri.
Bw. Jaffar pia alisema wavuvi wa Muyobozi wanakabiliana na changamoto ya kukosa elimu kupitia mafunzo yanayoendana na wakati huu wa kisasa katika sekta ys uvuvi.
 Chaga za kisasaa za kukaushia dagaa katika mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza, Mwalo ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria LIVEMP , chaga hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega na Ujumbe wake wakitoka kukagua gati katika mwalwo wa Muyobozi uliyopo Wilayani uvinza katika kijiji cha Mwakizega ambapo Naibu Waziri Ulega alifanya ziara leo.
Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Uvinza Bw. Haroon Chande akimueleza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega Anayeangalia Chaga kuhusu chaga hizo za kuanikia dagaa zilizojengwa na mradi wa kuhifadhi mazingira wa ziwa Victoria LIVEMP chaga ambazo ameeleza zimekuwa na msaada mkubwa kwa wavuvi wa dagaa wanaotumia mwalo wa Muyobozi uliyobo Wilayani uvinza katika kijiji cha Mwakizega.
 Katika Picha katikati Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akipata maelezo kuhusu Mwalo wa Muyowozi toka kwa Afisa Uvuvi wa Wilaya ya uvinza Bw. Haroon Chande, wakati wa ziara yake mwaloni hapo leo.
 Wavuvi wakiteketeza wao wenyewe nyavu haramu zilizokamatwa katika oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika Mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alipofanya ziara katika Mwalo wa Muyobozi Wilayani Uvinza leo
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega kushoto akizungumza na mfanyabiashara wa samaki aliyejulikana kwa jina la Bw. Ntakokola Issa katika Mwalo wa Kibirizi Mjini Kigoma kuhusu usafi wa vifaa maalum na gari la kubebea samaki, gari no T389 AZY linalotumiwa na Mfanyabiashara huyo lilipokuwa linaonekana  katika hali ya uchafu, Naibu Waziri Ulega alikagua Mwalo wa Kibirizi uliyopo Mjini Kigoma leo baada ya kumaliza Ziara yake wilayani Uvinza.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAVUTIWA NA MIRADI YA TASAF MKOANI SIMIYU.

$
0
0

NA ESTOM SANGA- BARIADI

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wamefanya ziara mkoani Simiyu na kuvutiwa na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF-mkoani humo.

Wajumbe hao walianza ziara yao kwa kusomewa taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambapo Katibu Tawala wa Mkoa huo , Jumanne Sagini aliwajulisha Wajumbe hao kuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF,umekuwa chachu muhimu katika kuleta maendeleo ya wananchi katika mkoa huo mpya.

Amesema kupitia Mpango huo Walengwa wameboresha maisha kwa kuendelea kujenga mkazi bora, kuchimba visima vya maji, uanzishwaji wa mashamba ya pamba ili kujiongezea kipato huku pia sekta za Afya na Elimu zikiendelea kunufaika na utekelezwaji wa Miradi ya TASAF.

Wakiwa katika Wilaya ya Maswa ,mkoani humo, Wajumbe hao walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Dkt Jasson Samson Rweikiza, walipata fursa ya kutembelea baadhi ya kaya za Walengwa ambako walishuhudia mafanikio ya ujenzi wa Nyumba ya mmoja wa Walengwa wa TASAF ,Monica Kwilasa katika kijiji cha Shanwa ambaye ametumia sehemu ya ruzuku aliyopata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuboresha Makazi yake.

Kama Wahenga wasemavyo “ Kuona ni kuamini” Wajumbe wa kamati hiyo walionyesha kushangazwa na mafanikio ya Mlengwa huyo ambaye aliwajulisha namna alivyotumia fedha alizozipata kutoka TASAF kuanzisha biashara ndogo ndogo iliyomwongezea kipato na kumwezesha kujenga nyumba kwa matofali ya saruji na kuezeka kwa mabati.

Akizungumza na Walengwa na Wananchi katika eneo la shule ya Sekondari ya Nyalikulungu ambako pia TASAF imejenga majengo, Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Rweikiza,amesema mafanikio yaliyoanza kupatikana katika utekelezaji wa Mpango huo ni kielelezo cha namna Serikali inavyopiga vita umaskini kwa kutumia mbinu mbalimbali ambazo amesema zinapaswa kuungwa mkono na wananchi. Zifuatazo ni picha za ziara hiyo ya kamati ya huduma za jamii ya bunge.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ,Mhe. Venance Mwamoto (aliyevaa koti) akitoka ndani ya nyumba iliyojengwa na mmoja wa walengwa kwa ruzuku ya TASAF.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa , Wakikagua moja ya Majengo yaliyojengwa na TASAF katika shule ya Sekondari ya Nyalikulungu katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Shanwa wilaya ya Maswa wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Rweikiza( hayupo pichani) wakati kamati hiyo ilipokagua miradi ya TASAF mkoani Simiyu.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa , wakimsikiliza mmoja wa Walengwa wa TASAF Bi.Monica Mwalu mkazi wa kijiji cha Shanwa wilayani Maswa namna alivyotumia sehemu ya ruzuku kujiongezea kipato na kujenga nyumba (iliyoko nyuma yao) kuboresha makazi yake.
Waziri Mkuchika (aliyevaa kofia ) na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakikagua zoezi la ilipaji wa ruzuku kwa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Shanwa Wilayani Maswa ruzuku ambayo imeanza kuboresha maisha yao kwa kiwango kikubwa.

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA MAPORI YA AKIBA YA BIHARAMULO, BURIGI, KIMISI (BBK) MKOANI KAGERA

$
0
0
Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambayo ipo mkoani Kagera imeridhishwa na utendaji kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) baada ya kutembelea Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi (BBK) kuangalia kazi za uhifadhi zinazofanywa ambapo wameipongeza TAWA kwa kitendo cha kurudisha hali ya mapori hayo ikiwemo kurejea kwa wanyamapori na uoto wa asili ambapo awali mapori hayo yalikuwa yameharibiwa kwa kasi kutokana na makundi ya mifugo kufanya malisho katika maeneo hayo.

Katika ziara hiyo,iliyoanzia katika Wilaya ya Biharamulo, Wajumbe wa Kamati hiyo waliweza kushuhudia eneo la Pori hilo lilipoanzia katika ziwa Victoria na baadaye kushuhudia Pori la Burigi lililopo katika wilaya za Karagwe na Biharamulo na badaye Pori la Kimisi ambalo lipo katika wilaya mbili za Karagwe na Ngara.

Hata hivyo,Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nape Nnauye aliridhishwa na masuala ya uendeshaji wa mapori hayo huku akiahidi kuyasaidia mapori hayo kwa kuishauri serikali iweze kuwekeza miundombinu ili kukuza utalii katika ukanda wa ziwa Victoria
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kushuhudia maporomoko ya maji ya Rusumo yaliyopo wilayani Ngara ambapo moja ya vyanzo vyake vikubwa vya maji vimeanzia katika Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi (BBK) wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara mwishoni mwa wiki mkoani wa Kagera.
Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kuhusu mipaka ya Pori la Akiba ya Biharamulo kutoka ziwa Victoria katika kituo cha Katete kutoka kwa Meneja wa Mapori ya Biharamulo, Burigi, Kimisi (BBK), Bw. Bigilamungu Kagoma (wa kwanza kushoto) wakati Kamati hiyo ilipotembelea mapori yaliyopo mkoani Kagera mwishoni mwa wiki
Meneja wa Mapori ya Biharamulo, Burigi, Kimisi (BBK), Bw. Bigilamungu Kagoma (wa kwanza kushoto) akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika ramani mahali ambako Pori la Akiba la Burigi lilipoanzia wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara katika Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi (BBK), yaliyopo mkoani Kagera hayo mwishoni mwa wiki mkoani Kagera
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye akiwazungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kujionea Pori la Akiba la Burigi katika wilaya ya Karagwe ambayo ni moja ya kati avyanzo vyake vikubwa vya maji ambavyo vimeanzia katika Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi (BBK) wakati kamati hiyo ilipofanya ziara mwishoni mwa wiki mkoani wa Kagera.Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia hema ambalo askari wanyamapori hulitumia kumpumzika wakiwa katika Mapori wakati wanapofanya doria za kuwabaini majangili.Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakipewa maelezo kuhusiana na mali mbalimbali za watuhumiwa wa ujangili zikiwemo baiskeli na pikipiki zilizokamatwa katika kituo cha Katete kwenye Pori la Akiba ya Biharamulo kutoka kwa Meneja wa Mapori ya Biharamulo, Burigi, Kimisi (BBK), Bw. Bigilamungu Kagoma (wa kwanza kushoto) wakati Kamati hiyo ilipotembelea mapori yaliyopo mkoani Kagera hayo mwishoni mwa wiki
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT).


MWANAFUNZI UDOM ANAOMBA MSAADA WA MASOMO

$
0
0
MWANAFUNZI wa Shahada ya Sheria mwaka wa Kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Amaniel Furahini(21) ameiomba serikali na watanzania kumsaidia kulipa ada ili aweze kuendelea na masomo yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Mwanafunzi huyo amesema amekuwa akisoma katika mazingira magumu kutokana na kukosa ada huku akidai kuwa wazazi wake hawana uwezo wa kumsomesha kwa kuwa ni wakulima wanaotegemea mvua za msimu wilayani Same.

Amesema alipochaguliwa kujiunga na masomo kwa mwaka 2017/18, aliomba mkopo kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HELB) ambao alitegemea ungeweza kuwa msaada mkubwa lakini hakuweza kufanikiwa kupata.

Furahini amesema kutokana na hali hiyo aliweza kuhangaika na kufanikiwa kulipa ada kiasi cha Sh.350,000 kati ya Sh. Milioni 1.5 anazotakiwa kulipa kwa mwaka chuoni hapo.“Hizi fedha nilizipata kutokana na kazi ya kubeba mizigo ya Watalii waliokuwa wakipanda Mlima Kilimanjaro na Meru ambapo pia nilifanikiwa kulipa fedha ya ‘Accommodation’ kiasi cha Sh.186,000 kwa muhula wa kwanza ambao umeisha,”amesema Mwanafunzi huyo.

Furahini amesema alishawasilisha suala lake kwenye uongozi wa Chuo na kwamba alishauriwa alipe kidogo kidogo au arudi nyumbani jambo ambalo anadai kuwa kwake ni vigumu kwa kuwa hana kitu chochote kinachomuingizia kipato na wazazi wake hawana uwezo.

“Nadaiwa fedha nyingi na wazazi wangu nimewaambia kwa kuwa hawana uwezo wamesema nirudi tu, na mimi nahitaji kusoma ili nifikie ndoto zangu, naiomba serikali, watanzania na wafadhili mbalimbali wanisaidie nifikie ndoto zangu maana hadi ikifika Julai mwaka huu kama nitakuwa sijalipa nitafukuzwa chuo,”ameomba Mwanafunzi huyo.

Akizungumzia maisha yake chuoni, Mwanafunzi huyo amesema amekuwa akisaidiwa na ndugu, jamaa na marafiki ambao ni wanafunzi wenzake.

“Wamekuwa wakinisaidia kuninunulia chakula naishi kwa misaada ya rafiki zangu chuoni, sasa kwenye suala la ada ndo limekuwa gumu kwangu nimekosa msaada.Naomba msaada wa kusomeshwa kwa watanzania watakaoguswa na ombi langu,”amesema Furahini.Amesema amemaliza kidato cha sita mwaka 2017 katika Shule ya Sekondari Kalangalala ambayo ipo mkoani Geita na alifanikiwa kupata ufaulu daraja la kwanza uliomuwezesha kujiunga na chuo hicho.

Furahini amesema anaona kama ndoto zake za kuisaidia nchi yake zikizimika kama asipoweza kulipa ada ili aendelee na masomo yake.

NAMBA YAKE YA MAWASILIANO - 0678873841

MAGAZETI YA JUMATATU LEO MARCH 19,2018

Mwandishi wa habari Daily News Digital afariki Dunia

$
0
0

  MWANDISHI wa habari chipukizi wa vyombo vya habari vya Digital vinavyomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) maarufu kama Daily News Digital, Katuma Masamba (pichani) amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah ilisema Katuma (24) alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam, alikokimbizwa ili kupatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla juzi akishiriki Jukwaa la Biashara la TSN mjini Zanzibar.

Mjomba wa marehemu, Shamte Ally alisema hospitalini hapo jana kuwa mipango ya mazishi ya Katuma ambaye awali alikuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo, itafanyika baada ya kikao cha familia kukaa leo na hasa baada ya mama.

Dada wa Katuma, ambaye ni mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Nyambona Masamba alisema ndugu wamepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo hicho cha Katuma. Taarifa zaidi kuhusu mazishi ya Katuma, zitaendelea kutolewa kwa kadri mipango itakavyokuwa inakwenda.

Alfajiri ya leo Mjomba wa Marehemu Katuma, Shamte Ally alituma ujumbe mfupi kwa mmoja wa waandishi wa Gazeti tando hili la Daily News Online Blog, Mroki Mroki aliyeko Dodoma na kusema kuwa wanamsubiri mama mzazi wa Katuma anaewasili leo kwa maamuzi juu ya maziko ya mtoto wake.

Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa TSN, wanaungana na familia ya marehemu katika wakati huu mgumu wa maombolezo.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

ULEGA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA KWA MKAKATI MZURI WA KUINUA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega kushoto akizungumza na mfanyabiashara wa samaki aliyejulikana kwa jina la Bw. Ntakokola Issa katika Mwalo wa Kibirizi Mjini Kigoma kuhusu usafi wa vifaa maalum na gari la kubebea samaki, gari no T389 AZY linalotumiwa na Mfanyabiashara huyo lilipokuwa linaonekana katika hali ya uchafu, Naibu Waziri Ulega alikagua Mwalo wa Kibirizi uliyopo Mjini Kigoma leo baada ya kumaliza Ziara yake wilayani Uvinza.
Katika Picha ni chaga za kisasaa za kukaushia dagaa katika mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza, Mwalo ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria LIVEMP , chaga hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.
Pichani wavuvi wakiteketeza wao wenyewe nyavu haramu zilizokamatwa katika oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika Mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alipofanya ziara katika Mwalo wa Muyobozi Wilayani Uvinza leo. 
(Habari na Picha na Mwandishi Maalum).

NA; MWANDISHI MAALUM – UVINZA
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kwa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na uvuvi haramu na kutatua kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwekeza kwenye Ranchi za mifugo.

Ulega ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kugagua Mwalo wa Muyobosi uliyopo Wilayani uvinza ambapo alisema jitihada hizo za wilaya zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na serikali kwa ujumla, kwani ina mkakati wa kutenga maeneo ya Ranchi kwa ajili ya wafugaji.

“Nataka niwahakikishie mimi na wizara yangu tutakuwa tayari kuhamia hapa kulisimamia jambo hili mtakapo tenga hayo maeneo ya kufugia, ili kuwaweka tayari wafugaji katika maeneo hayo na huo ndiyo muharobaini wa kwenda kuondoa matatizo ya wakulima na wafugaji katika nchi yetu kwa mipango ya namna hii inawezekana kabisa, hicho ni kipaumbele chetu mimi na waziri wangu Mhe. Luhaga Mpina katika uongozi wetu tutahakikisha kama siyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji basi tutaindoa kabisa, kwa kushirikiana vyema na Halmashauri zetu” Alisema Ulega.

Ulega alisisitiza suala la mapambano dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa Rasilimali za uvuvi na suala zima la ufugaji wa samaki, nakuwaasa kuachana kabisa na utamaduni wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.

Naibu Waziri Ulega alisema kuwa fedha nyingi zimewekwa katika mwalo huo wa Muyobozi na kuwataka wavuvi katika eneo hilo kuutumia vizuri mwalo huo wenye hadhi ya kimataifa ambapo ameleza kwa mwaka wa fedha uliopita mwalo huo peke yake umechangia kiashi cha shilingi milioni 28 “ Ninaamini kama mtapasimamia vyema mahala hapa patachangia pato la taifa mara nne zaidi ya mwaka jana. Ninyi ndo muwe walinzi wa kwanza wa rasilimali hizi ili nchi yetu iweze kuinuka” Alisisitiza

Awali, akiongea katika ziara hiyo mwenyekiti wa kijji cha Mwakizega ambapo mwalo wa Muhyobozi umejengwa Bw. Jaffari Abdalah, alisema mwalo huo unakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na gati la mwalo huo kuwa na urefu wa mia 20 ambazo ni chache kwa boti kuegesha kupakua na kupakia kabla na baadha ya shuguli za uvuvi , hivyo ameiomba serikali kuongeza urefu wa gati hiyo ili mitumbwi mikubwa na midogo iweze kufanya shughuli za uvuvi vizuri.

Bw. Jaffar pia alisema wavuvi wa Muyobozi wanakabiliana na changamoto ya kukosa elimu kupitia mafunzo yanayoendana na wakati huu wa kisasa katika sekta ys uvuvi.

KUMBILAMOTO ATOA SHUKRANI YA MBUZI KWA FATHER KAMILI WA PAROKIA YA YOMBO DOVYA

$
0
0



Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, akiajadili jambo na Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga ya Yombo Dovya, Father Kamili mara baada ya kumkabidhi zawadi ya Mbuzi.

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akimkabidhi Padre wa Kanisa Katoliki Yombo Father Kamili Zawadi ya Mbuzi kama sehemu yake ya shukrani mara baada ya kufanyiwa maombi wakati wa uchaguzi.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, akizungumza na Viajana wa Kwaya wa Parokia ya Karoli Lwanga iliyopo Yombo Dovya jijini Dare s Salaam.

Mwakyembe atembelea Maeneo ya kihistoria Mkoani Iringa

$
0
0
 : Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Chief wa kihehe Evaristo Sambiligunga Mwambeta alipokutana na machief wa kihehe kuzungumza nao kuhusu namna ya kuhifadhi historia ya ukomboziwa Bara la Afrika kwa vizazi vijavyo jana Mkoani Iringa.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa ameshika silaha za jadi alizokuwa anatumia Mtwa Mkwawa wakati wa harakati za kuwakomboa wahehe kutoka katika utumwa wa wajerumani jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiangalia kaburi la Mtwa Abdul Adam Sapi Mkwawa alipotembelea makaburi ya machief kutoka ukoo wa Mkwawa jana katika makumbusho ya Mkwawa iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Mkoa wa Iringa.
Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Tumaini Dkt. Gibson Sanga (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) baadhi ya vifaa vya kitamaduni vinavyotumiwa na kabila la wahehe alipotembelea makumbusho ya Iringa jana Mkoani Iringa
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

MPOTO AKOSHWA NA PROGRAMU YA UMILIKISHAJI ARDHI WA WIZARA YA ARDHI CHINI.

$
0
0
Waziri Lukuvi akutana na wananchi waliokabidiwa hati zao

Na Mwandishi wetu, Globu ya jamii.
MSANII wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ambaye amekuwa kioo cha jamii kwa muda mrefu kutokana na kutoa nyimbo za kijamii zenye kuwataka wananchi kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato cha halali, kukemea rushwa na uonevu, Ijuma hii amefurahishwa na Programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme - LTSP).

Programu hiyo ambayo inatakelezwa katika Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini ya Waziri wake, Mhe. William Lukuvi  ili kukabiliana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiibuka katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Programu hii ni mahsusi kwa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi ambapo takribani vijiji 160 vitanufaika. Hadi sasa, Programu imehakiki na kupima vipande vya ardhi 84,795 katika vijiji 40 vya Wilaya za Kilombero na Ulanga. 

Kati ya vipande vilivyohakikiwa na kupimwa, jumla ya Hati za Hakimiliki ya Kimila 24,650 zimeandaliwa.

Mpoto ambaye amekuwa akitembea katika maeneo mbalimbali ya nchi kusoma mazingira na kuwasikiliza wananchi wanasema nini juu ya maisha yao ili anapoandika nyimbo zake ziwe na kero za wananchi ambazo amezishuhudia kwa macho yake, wiki hii alipita mkoani Morogoro na kuzungumza na wananchi kuhusu maisha yao ndipo lilipo ibuka suala la programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme - LTSP).

Mshairi huyo amesema baada ya kuzungumza  na wananchi kadhaa ambao wamepitiwa na Programu hiyo aligundua nyuso zao jinsi zilivyokuwa na furaha baada ya kukabidhiwa hati zao ambazo zimeongeza thamani zaidi ya ardhi yao (viwanja na mashamba)  kwa kuwa tayari vinatambulika kisheria.

“Kwa miaka mingi nchi yetu imekua na migogoro ya ardhi kati ya mtu na mtu,kijiji na Kijiji, wakulima na wafugaji, hata wawekezaji na wana nchi, Wizara ya Ardhi kupitia Mpango wa Land Tenure Support Programme (LTSP) inayotekelezwa katika Wilaya Tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi baadae kusambazwa Nchi nzima imefanya kazi kubwa sana,” alisema Mrisho Mpoto.

“Binafsi kama kawaida yangu kuzunguka kila koja na nchi yangu na kuzungumza na wananchi, nimeona ukubwa wa hii Programu, imeona thamani ya hii programu, wananchi wanaongea kwa furaha ya hali ya juu kutokana na hii programu. Mimi sio msemaji wa serikali lakini wakati nikiwa katika harakati za kutembea kwa ajili ya shughuli zangu za sanaa huwa napata fursa ya kuongea na wananchi wa eneo husika, wakazi wa Morogoro wanaishukuru sana serikali pamoja na Waziri Lukuvi,  naamini hii programu inaweza kuwa mwarobaini wa haya matatizo ya ardhi, maana kila kipande cha ardhi kitapimwa na mwananchi kupewa hati yake ya umiliki, naamini itaweza kuondoa kabisa migogoro ya nrdhi nchini Tanzania, hongera Mhe.Lukuvi,” aliongeza Mpoto.

Alisema bado ataendelea kutembea katika maeno mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kukutana na mashabiki wake wa muziki na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ya nchi na pale ambako ataona kuna haja ya kutoa msaada atawasiliana wahusika kwaajili  ya kutatua kero za wananchi.

Kazi nyingine zilizotekelezwa na programu ya LTSP ni pamoja na kusimika alama za msingi 54 za mtandao wa kijiodesia katika Wilaya za Kilombero, Ulanga, Malinyi na Mufindi,  Kupima mipaka ya vijiji 121 na kutatua migogoro 71 ya mipaka ya vijiji iliyodumu kwa muda mrefu, Kuandaa vyeti vya Ardhi ya Kijiji kwa vijiji 57, Kuandaa mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji kwa vijiji 53 na Kuchangia katika ujenzi na ukarabati wa masjala za ardhi na ofisi za vijiji katika vijiji 61.

Viongozi wengi wa Wizara wanaitembelea programu hiyo mara kwa mara na uongozi wa Wilaya na wananchi wanatoa ushirikiano mkubwa sana kwa kuwa programu iko katika Wilaya zao.

Hivi karibuni Katibu Mkuu Bibi. Dorothy Mwanyika mara tu baada ya kuteuliwa na Mhe Rais kuwa Katibu Mkuu wa Wizara alitembelea programu hiyo na kujionea namna programu inavyotumia teknolojia ya kisasa kabisa kupima ardhi ya wananchi vijijini. Pia, Mhe Naibu Waziri Mhe. Angelina Mabula nae alifanya ziara katika eneo la programu.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi akikabidhi hati kwa mmoja wazee waliofanikiwa kumilikishwa ardhi.

Je! Unajua unaweza kuboresha mbinu zako za kilimo kwa kutumia mtandao wa simu?

$
0
0
Je! Unajua unaweza kuboresha mbinu zako za kilimo kwa kutumia mtandao wa simu? Bonyeza video hii kuangalia na kuona jinsi wengine wanavyofanya.




Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images