Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

MWENYEKITI JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA AJIUZULU


BENKI YA CRDB YAJITOSA KUKISAIDIA CHAMA CHA MAAFISA HABARI,MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI (TAGCO)

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini .

BENKI ya CRDB imeahidi kuendelea kukisaidia Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikali na kwamba kufanya hivyo kutasaidia upatikanaji wa taarifa zilizo sahihi na kwa wakati sahihi.

Hayo yameelezwa na Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu wakati akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa (AICC) jijini Arusha ,sambamba na mkutano mkuu wa chama hicho (TAGCO) 

"Benki ya CRDB tunaamini "with right information" ambao hawa ni haki yao kuifikisha kwa wananchi ambao watakuwa aware nini kinaendelea,sio tu katika kutangaza nafasi za kazi kama baadhi ya watu wanavyofikiria ,pia wanahusika katika kutangaza Zabuni zilizopo,nafasi za Maendeleo,Nafasi za uwekezaji na sSehemu gani hasa unaweza kuwekeza kwa ajili ya maendeleo."alisema Semunyu.

Amesema Maafisa Habari wa taasisi za Serikali ndio daraja la kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi na kwamba kupitia kwao kila kinachofanyika ndani ya Serikali kitwafikia wananchi kwa njia na wakati sahihi.

"Kama alivyosema Msemaji Mkuu wa Serikali kwamba kuna tofaui kubwa ya kufikisha habari na kufikisha habari sahihi,kwa hiyo daraja hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa halipati heshima stahiki sasa litapa heshima."alisema Semunyu..
Meneja UhusiaNo wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akiwasilisha mada wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB ,Godwin Semunyu wakati wa mkutano huo. kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TAGCO,Pascal Shelutete,Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu na mwisho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Sanaa,Utamadunina Michezo,Susan Mlawa.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo.
Meneja Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akiwasilisha mada juu ya mfumo maalumu wa kadi za kielektroniki maarufu kama Credit Card ,huduma ambayo inatolewaa na Benki ya CRDB.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATUMISHI WA AFYA WAASWA KUJIEPUSHA VITENDO VYA RUSHWA SEHEMU ZAO ZA KAZI

$
0
0
NA WAMJW-DAR ES SALAAM

WATUMISHI wa sekta ya Afya nchini wametakiwa kujiepusha na vitendo vya kutaka rushwa kutoka kwa wananchi wanapokuwa sehemu zao za kazi ili kuendana na maadili ya utumishi wa Umma. 

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es salaam ili kujadili mustakabari wa utoaji huduma za Afya nchini. 

“Marufuku Watumishi wa sekta ya afya nchini kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na kama wapo naomba waache mara moja kwani atakayebainika anajihusisha na rushwa sheria itafuata mkondo wake mara moja” alisema Waziri Ummy. Aidha Waziri Ummy amesema kuwa watumishi wa sekta ya afya hasa katika sehemu ya kutolea huduma za afya wanatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa wananchi pindi wanapotoa huduma sehemu zao za kazi. 
aziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifungua Mkutano Wa Balaza la Wafanyakazi Wa Wizara ya Afya mapema leo Jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu Wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(hayupo kwenye picha)
Mkurugenzi Wa Mafunzo na Rasilimali watu Dkt.Otilie Gowelle wakwanza kulia akifuatilia kwa makini maagizo ya Waziri Wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
eza kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu na mganga Mkuu wa Serikali Prof. Kambi wakati wakiimba wimbo wa kuhamasisha umoja na mshikamano kwa Wafanyakazi, pindi wakifanya mkutano wa Baraza la Wafanyakazi, Wakwanza ni Katibu wa Baraza hilo Mary Ntira na wa mwisho ni Afisa Elimu kazi na mratibu wa Jinsia taifa TUGHE Bw. Nsubisi Mwasandende
Watumishi wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Dorothy Gwajima wapili kutoka kulia.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu katikati waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi kutoka Wizara ya Afya mara baada ya kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Leo jijini Dar es salaam.



JAFO AAGIZA MAAFISA HABARI SERIKALINI KUINGIA KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SERIKALI imeziagiza Halmashauri kuhakikisha Maafisa Habari wanaingia katika vikao vya maamuzi ili waweze kupata na kutoa habari sahihi huku akiwatuhumu baadhi ya maafisa wa Halmashauri kuwa huendi ndio wanazuia maafisa habari kuingia katika vikao kwa lengo la kuficha baadhi ya taarifa.

 Agizo hilo la serikali limetolewa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais ,Serikaliza Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo wakati wa kufunga kikao kazi cha 14 cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichofanyika jijini Arusha kwa muda wa siku tano.

 afo pia ameziagiza Halmashauri kutenga fungu katika Bajeti zao kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya Maafisa Habari ili kusaidia katika kutekeleza majukumu yao kwa urahisi ya kuhabarisha umma shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa Serikali. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza wakati wa kufunga Kikao kazi cha 14 cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichofanika kwa siku tano katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikabodhi cheti kwa Mwenyekiti Mstaafu wa TAGCO ,Innocent Mungi ikiwa ni ishara ya utambuzi wa mchango wake katika chama hicho. 
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikabodhi cheti kwa Mmoja wa viongozi wa zamani wa TAGCO,Silvia Lupembe ambaye pia ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ,Morogoroikiwa ni ishara ya utambuzi wa mchango wake katika chama hicho. 
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikabodhi cheti Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) Leila Muhaji kutambua mchango wa Shirika hilo katika kufanikisha kikao kazi cha maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano  Serikalini kilichofanyika jijini Arusha. 

Mgeni rasmi katika ufugaji wa Kikao kazi cha 14 cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini ,Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais,Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemeni Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa kikao hicho.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA AONGOZA KIKAO MAALUM KUJADILI MIKAKATI YA JESHI LA MAGEREZA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao Maalum cha kujadili mikakati ya utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula.
Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(hayupo pichani).
Washiriki wa Kikao kazi ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifanya maadiliano mbalimbali katika vikundi kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza Mikoa yote Tanzania Bara(waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya ufunguzi rasmi wa kikao maalum cha kujadili mikakati ya utekelezaji wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula. Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja leo 17 Machi, 2018 Mkoani Morogoro.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

WIZARA SABA KUKUTANA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI MPAKANI MWA TANZANIA NA ZAMBIA

$
0
0
Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini, imeamua kuzikutanisha wizara saba zinazohusika moja kwa moja na changamoto zinazopunguza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na Wawekezaji mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Akiongea wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji katika mkoa wa Songwe na maeneo yaliyopo mpakani mwa Tanzania na Zambia, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora amesema mara baada ya kuhitimisha ziara yake tarehe 17 Machi, 2018, atakutana na makatibu wakuu wa wizara zinazopaswa kutoa suluhisho la changamoto hizo.

“Nitakutana na makatibu wakuu wenzangu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) na naamini maazimio tutakayotoa katika kikao hicho yatakuwa suluhisho la kuondoa changamoto zinazojitokeza hapa mpakani mwa Tanzania na Zambia” , amesema Kamuzora.

Akibainisha changamoto za mazingira ya Biashara na uwekezaji mpakani mwa Tanzania na Zambia, Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu, Chiku Galawa amesema, changamoto kubwa mpakani hapo ni usalama kwa wafanyabiashara na biashara zao, ambapo kwa mazingira ya mpaka huo imekuwa vigumu kuuimarisha.
Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu, Chiku Galawa akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji mkoani Songwe, tarehe 17 Machi, 2018.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akiendesha kikao kilicho jumuisha watendaji wa serikali na sekta binafsi wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji mkoani Songwe, tarehe 17 Machi, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akiongozwa na Meneja wa Kituo cha Forodha cha Pamoja Tunduma, Jomimosa Nsindo wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji , mpakani mwa Tanzania na Zambia, tarehe 17 Machi, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akifuatilia maelezo ya wateja wa Kituo cha Forodha cha Pamoja Tunduma (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji , mpakani mwa Tanzania na Zambia, tarehe 17 Machi, 2018. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU.

TAZAMA LIVE MECHI YA SIMBA SC V/S AL MASRY

MRISHO MPOTO AKOSHWA PROGRAMU YA UMILIKISHAJI ARDHI NCHINI,AKUTANA NA WANANCHI WALIOKABIDHIWA HATI ZAO

$
0
0
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ambaye amekuwa kioo cha jamii kwa muda mrefu kutokana na kutoa nyimbo za kijamii zenye kuwataka wananchi kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato cha halali, kukemea rushwa na uonevu, Ijuma hii amefurahishwa na Programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP).
Programu hiyo ambayo inatakelezwa katika Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini ya Waziri wake, Mhe. William Lukuvi ili kukabiliana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiibuka katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Programu hii ni mahsusi kwa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi ambapo takribani vijiji 160 vitanufaika. Hadi sasa, Programu imehakiki na kupima vipande vya ardhi 84,795 katika vijiji 40 vya Wilaya za Kilombero na Ulanga. Kati ya vipande vilivyohakikiwa na kupimwa, jumla ya Hati za Hakimiliki ya Kimila 24,650 zimeandaliwa.

Mpoto ambaye amekuwa akitembea katika maeneo mbalimbali ya nchi kusoma mazingira na kuwasikiliza wananchi wanasema nini juu ya maisha yao ili anapoandika nyimbo zake ziwe na kero za wananchi ambazo amezishuhudia kwa macho yake, wiki hii alipita mkoani Morogoro na kuzungumza na wananchi kuhusu maisha yao ndipo lilipo ibuka suala la programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure Support Programme – LTSP).
Mshairi huyo amesema baada ya kuzungumza na wananchi kadhaa ambao wamepitiwa na Programu hiyo aligundua nyuso zao jinsi zilivyokuwa na furaha baada ya kukabidhiwa hati zao ambazo zimeongeza thamani zaidi ya ardhi yao (viwanja na mashamba) kwa kuwa tayari vinatambulika kisheria.

“Kwa miaka mingi nchi yetu imekua na migogoro ya ardhi kati ya mtu na mtu,kijiji na Kijiji, wakulima na wafugaji, hata wawekezaji na wana nchi, Wizara ya Ardhi kupitia Mpango wa Land Tenure Support Programme (LTSP) inayotekelezwa katika Wilaya Tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi baadae kusambazwa Nchi nzima imefanya kazi kubwa sana,” alisema Mrisho Mpoto.
“Binafsi kama kawaida yangu kuzunguka kila koja na nchi yangu na kuzungumza na wananchi, nimeona ukubwa wa hii Programu, imeona thamani ya hii programu, wananchi wanaongea kwa furaha ya hali ya juu kutokana na hii programu. 

Mimi sio msemaji wa serikali lakini wakati nikiwa katika harakati za kutembea kwa ajili ya shughuli zangu za sanaa huwa napata fursa ya kuongea na wananchi wa eneo husika, wakazi wa Morogoro wanaishukuru sana serikali pamoja na Waziri Lukuvi, naamini hii programu inaweza kuwa mwarobaini wa haya matatizo ya ardhi, maana kila kipande cha ardhi kitapimwa na mwananchi kupewa hati yake ya umiliki, naamini itaweza kuondoa kabisa migogoro ya nrdhi nchini Tanzania, hongera Mhe.Lukuvi,” aliongeza Mpoto.

Alisema bado ataendelea kutembea katika maeno mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kukutana na mashabiki wake wa muziki na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ya nchi na pale ambako ataona kuna haja ya kutoa msaada atawasiliana wahusika kwaajili ya kutatua kero za wananchi.

Kazi nyingine zilizotekelezwa na programu ya LTSP ni pamoja na kusimika alama za msingi 54 za mtandao wa kijiodesia katika Wilaya za Kilombero, Ulanga, Malinyi na Mufindi, Kupima mipaka ya vijiji 121 na kutatua migogoro 71 ya mipaka ya vijiji iliyodumu kwa muda mrefu, Kuandaa vyeti vya Ardhi ya Kijiji kwa vijiji 57, Kuandaa mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji kwa vijiji 53 na Kuchangia katika ujenzi na ukarabati wa masjala za ardhi na ofisi za vijiji katika vijiji 61.

Viongozi wengi wa Wizara wanaitembelea programu hiyo mara kwa mara na uongozi wa Wilaya na wananchi wanatoa ushirikiano mkubwa sana kwa kuwa programu iko katika Wilaya zao.

Hivi karibuni Katibu Mkuu Bibi. Dorothy Mwanyika mara tu baada ya kuteuliwa na Mhe Rais kuwa Katibu Mkuu wa Wizara alitembelea programu hiyo na kujionea namna programu inavyotumia teknolojia ya kisasa kabisa kupima ardhi ya wananchi vijijini. Pia, Mhe Naibu Waziri Mhe. Angelina Mabula nae alifanya ziara katika eneo la programu.

RAIS DKT MAGUFULI AMRUDISHIA PROFESA MAHALU HADHI YA UBALOZI

JAFO AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUBUNI MIKAKATI YA KUONDOA TATIZO LA OMBAOMBA MIJINI.

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka wakuu wa mikoa kubuni mikakati ya kuondoa tatizo la ombaomba mijini.

Waziri Jafo aliyasema hayo alipokuwa akizindua Mpango wa Utalii wa Jiji la Dar es salaam ambao umelenga kuvutia watalii mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo ndani ya jiji hilo.Katika uzinduzi huo, Jafo amesema ombaomba hao wamekuwa wakikaa barabarani hali ambayo haileti sura nzuri kwa nchi na kwa wageni mbalimbali wanaokuja kutalii nchini.

Waziri Jafo amesema changamoto ya watoto wa mitaani na tatizo kubwa la ombaomba ni vyema wakuu hao wakabuni mbinu mbalimbali zikiwemo za kuwawekea maeneo maalum ya kujihusisha na shughuli za ufugaji na kilimo cha bustani ili kuwaondoa mitaani.

“Tukifanya hivi tutakuwa tumefanikiwa kuondokana na kitendo cha wao kukaa barabarani kwa kuwa hakileti sura nzuri kwa nchi yetu kwa wageni mbalimbali wanaokuja kutalii hapa nchini,”amesema Jafo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika uzinduzi wa Utalii wa jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika Uzinduzi wa Mpango wa Utalii wa Jiji la Dar es salaam.
Kikundi cha sanaa kikitumbuiza kwa wananchi walioshiriki uzinduzi wa Mpango wa Utalii wa Jiji la Dar es salaam.
Baadhi ya wananchi walioshiriki uzinduzi wa Mpango wa Utalii katika jiji la Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda pamoja na viongozi mbalimbali na wasanii katika uzinduzi wa Utalii wa jiji la Dar es salaam.
 

Twanga Pepeta waipania Tanga hatari

$
0
0
WAKALI wa muziki wa dansi nchini Tanzania, The African Stars Band, Twanga Pepeta 'Wazee wa Kisigino', wameipania vilivyo ziara yao ya Mkoa wa Tanga, wakisema wanakwenda kuonyesha makali yao halisi kwa mashabiki wao wa muziki, kwa kuanzia na onyesho la Ijumaa Machi 23, katika Ukumbi wa Tanga Hotel, jijini Tanga kwa kiingilio kidogo tu cha Sh 7,000.

Twanga wanapanda jukwaani ikiwa ni miezi kadhaa tangu walivyoenda katika Mkoa wa Tanga, maarufu kwa Wagosi wa Kaya, jambo linaloongeza mguso kwenye shoo zao zote za Mkoa huo kutokana na kiu kubwa ya wadau wao waliokuwa na shauku ya kuiona bendi yao hiyo ikiwa jukwaani.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Twanga Pepeta, Martin Sospeter, alisema wanamuziki wao wamejipanga imara ili kudhihirisha makali yao katika tasnia nzima ya muziki wa dansi kwa kuongozwa na Luiza Mbutu, Kalala Junior, Haji Ramadhan, Msafir Diouf na wengineo wanaotamba kwenye bendi yao.

"Hakuna ubishi kuwa bendi ya Twanga Pepeta ndio alama ya muziki wa dansi nchini, hivyo ili kuonyesha umwamba huo wa kuimba vizuri, kupiga mdundo pamoja na kushambulia jukwaa, niwaombe mashabiki waje kwa wingi Ijumaa katika Ukumbi wa Tanga Hotel, kwakuwa ndio sehemu yetu ya kutangaza makali yetu.

"Mbali na onyesho la Tanga Hotel tutakaloanza mapema kabisa mishale ya saa 1 jioni, tutaendeleza dozi zetu katika Ukumbi wa Rombo Hotel Handeni Mjini siku ya Jumamosi ya Machi 24 na Jumapili ya Machi 25 tutawapa burudani mashabiki wetu wa Korogwe Mjini katika Ukumbi wa Mamba Club, huku kote viingilio vikiwa ni sh 7,000 tu," Alisema Sospeter na kuwataka mashabiki wao waende kwa wingi ukumbini kujionea umahiri wa bendi yao kongwe nchini.

Twanga Pepeta ni miongoni mwa bendi zinazotamba hapa nchini ikiongozwa na mwanamama Asha Baraka, huku ikiweza kujikita kileleni kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwake, huku ikiwa na nyimbo kali kama Mwana Dar es Salaam, Mtu Pesa, Nazi Haivunji Jiwe, Marry na nyinginezo zinazotesa katika ulingo wa muziki wa dansi nchini.

SERIKALI INA MTAZAMO WA KUIFANYA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI KUWA SEKTA YA UZALISHAJI -ULEGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdalah Hamis Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ameiambia kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji kuwa, Serikali ina mpango wa kuifanya sekta ya Mifugo na Uvuvi kuwa na mchango mkubwa katika pato la Taifa. 

Naibu Waziri HamisUlega ameyasema hayo leo Mkoani Kigoma mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji, ilipokuwa katika ziara ya kutembelea chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya kigoma jana.

Mhe. Ulega amesema Wizara yake ina Mkakati wa kulinda rasilimali za Mifugo na Uvuvi, kwa kuimarisha uvuvi wa bahari kuu na kuitoa sekta hiyo kwenye kuchangia kiasi na shilingi Bilioni 19 kwa mwaka katika pato la taifa hadi kufikia kuchangia zaidi ya shilingi Bilioni 50 kwa mwaka.

“Tunaweza kufikia malengo haya kwanza kwa kuimarisha uvuvi wa Bahari kuu kwa kuhakikisha kwanza tasisi yetu ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu inakuwa na nguvu kwa kuweka vizuri sheria na kanuni zetu za uvuvi ikiwa ni pamoja na kufufua shirika letu la TAFICO, Alisema Ulega.”

Sambamba na hilo, Ulega alisema Serikali ina mkakati wa kuwa na Meli ambayo itakuwa na uwezo wa kwenda kuvua na kuchakata mazao ya samaki, jambo ambalo litakwenda sambamba na ufunguaji wa viwanda vya uchakataji wa mazao ya uvuvi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Hamis Ulega (Mb) kulia akiongea na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji ilipotembelea chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Kigoma jana, wabunge wa kamati hiyo wameambata na maafisa mbali mbali kutoka serikalini.
Kushoto Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Hamis Ulega (Mb) akizunguma katika kikao na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji katika chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Kigoma jana, kati kati ni mwenyekiti wa kamati Hiyo Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa (Mb.) Kalenga na kulia ni Makamu Mwenyekiti Mhe. Christine Gabriel Ishengoma (Mb).
Pichani Mbele ni baadhi wa wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji wakifuatilia mazungumzo katika kikao wakati wa ziara yao katika chuo cha wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Kigoma jana,wengine ni watumishi wa serikali.

Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu

$
0
0
NYOTA wa muziki wa singeli nchini, Suleiman Jabir 'Msaga Sumu', amesema anashukuru kwa kupata shoo katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga, akisema kuwa anakwenda kwa watu wake wa nguvu kutokana na kufahamu kuwa wanaupenda muziki wake.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Msaga Sumu anayetamba katika muziki huo alisema kuwa wilaya la Handeni ni kati ya maeneo yaliyoupaisha muziki wake, simu chache baada ya kuibuka kwenye tasnia hiyo kutokana na watu wengi wakiwamo waendesha bodaboda waliokuwa wameziweka nyimbo zake kwenye vyombo vyao vya usafiri na kuzicheza muda wote.

Alisema hivyo shoo mbili alizopata kwa kuanzia Jumamosi ya Machi 24 asubuhi hadi jioni kwenye uwanja wa Mabatini, Mkata, wilayani Handeni pamoja na ile itakayofanyika usiku katika siku hiyo hiyo kwenye Ukumbi wa Rombo Hotel kwa kushirikiana na bendi ya Twanga Pepeta, ni sehemu ya kwenda kutuliza kiu ya mashabiki wake wa muziki wilayani humo, mkoani Tanga.

"Handeni nitaanza Mkata kwenye uzinduzi wa ligi ya Handeni Kwetu Cup Machi 24 na baadae nitakuwapo Rombo Hotel, Handeni Mjini, nikiamini ni sehemu nzuri kwangu kutokana na nguvu ya mashabiki wangu kwa namna moja ama nyingine.

" Ni watu wa nguvu kwasababu wanaupenda sana muziki wangu, ukizingatia kuwa mimi msanii hivyo napaswa kufahamu mahala gani nakubalika ili kuhakikisha kuwa nalinda tbamani yao kwangu kama njia ya kuendelea kuniletea mafanikio katika kona ya muziki wa singeli ambao bila kuficha mimi ndio mfalme wao kutokana na uwezo wangu kimuziki,"Alisema Msaga Sumu.

Msaga Sumu anayetamba pia na nyimbo ya Mwanaume Mashine, Shemeji na nyinginezo, alitumia muda huo kuwataka mashabiki wake kuingia kwa wingi kwenye maonyesho mawili ya uzinduzi wa ligi ya Handeni Kwetu Cup Mkata na lile la Rombo Hotel, ili wajionee mambo mapya kutoka kwake.

Ligi ya Handeni Kwetu Cup inaanzishwa na mdau wa michezo Kambi Mbwana, huku ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi Machi 24 na kufikia ukingoni mwezi Oktoba mwaka huu, huku ikishirikisha timu mbalimbali za wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Mwisho

Viongozi Mkoa wa Iringa hamasisheni wananchi kutunza historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika – Mwakyembe

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa Lugalo alipotembelea mnara wa Lugalo walipozikwa Askari 300 wa kijerumani pamoja na kiongozi wao wakati wa ziara yake katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdala

 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdala (aliyesimama) akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kilolo wakati wa ziara ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. 

 Baadhi wa wananchi wa Kilolo wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. 


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (aliyeshika mkuki) katika picha ya pamoja na wananchi wa Lugalo alipotembelea Mnara wa Lugalo walipozikwa Askari 300 wa kijerumani pamoja na kiongozi wao wakati wa ziara yake katika mkoa wa Iringa kukagua maeneo yaliyotumika kama kambi za wanaharakati wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika jana Mkoani Iringa. Kushoto kwa waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdala.Picha na:Genofeva Matemu - WHUSM

HARAMBEE YA WASANII TANZANIA UINGEREZA - WASATU


HOTUBA YA RAIS DKT.JOHN POME MAGUFULI KATIKA UFUNGUZI WA KIWANDA CHA SIGARA MOROGORO MACHI 15,2018

"MADEREVA" NA MZEE MAKONGORO NA KUNDI LAKE

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

AWAMU YA TANO YA RAIS DKT. MAGUFULI YAWATUA NDOO WANANACHI WA GAIRO

$
0
0



Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (wa kwanza kulia) na wageni wake kutoka Sweden wakishiriki msaragambo na wanawake wa Kata ya Chakwale kuchimba mtaro wa kutandaza mabomba ya Maji.
Mhandisi Magumbo (wa kwanza kushoto) anayekuwa akisimamia mradi huo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Mchembe (katikati) na wafadhili kutoka nchini Sweden mara baada ya kufika kukagua.
Mhandisi wa Wilaya ya Gairo Heke Bulugu akitoa ufafanuzi kwenye baadhi ya mambo.

Wadau mbalimbali wakiwemo Madiwani na Watendaji wa Kata. Neema ya Mradi wa Maji safi na Salama Gairo chini ya uongozi makini wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli unaendelea kwa kasi ya ajabu.

Akitembelea mradi Maji Safi na Salama uliopo Gairo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Mchembe akiwa ameongozana na Mhandisi wa Maji Wilaya Eng. Heke Bulugu, Madiwani wa Chakwale na Madege pamoja na Watendaji wao, na Mhandisi wa Lions Pure Water Eng. Magumbo pamoja na wafadhili wa kutoka nchini Sweden.
 
Mhe. Mchembe ameeleza kuwa Mradi huo unahudumia kata 2 za Madege na Chakwale na vijiji 6 vya Madege, Ng'olong'o , Sanganjelu, Chakwale, Kilimani na Kimashale. Aliongeza kuwa utanufaisha jumla ya wananchi 10,358 kwa gharama ya shs 348,000,000/- kwa mchanganuo ufuatao Lions Pure Water shs 278,000,000/- Halmashauri kupitia Serikali kuu shs 48,000,000/- na Nguvu za wananchi 22,000,000/- Mhe. Mchembe ameisifia serikali ya Rais Dkt. Magufuli ya hapa Kazi tu! kwa kuweza kuwajali wanyonge kwa kuwatua ndoo kichwani akinamama.

MAGARI 50 YA WAGONJWA YAGAIWA KWA HALMASHAURI.

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo, ameendesha zoezi la kugawa magari 50 ya wagonjwa aina ya Suzuki Maruti (Ambulances) kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini Jijini Dar es Salaam.

Magari hayo ambayo awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliagiza yafanyiwe utaratibu wa kisheria wa kiforodha na yagawanywe kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ili yatumike kwa kuwahudumia wananchi katika vituo mbalimbali vya afya nchini.

“Hii ni agenda ya Mhe. Rais ya kutaka kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora, ambulance hizi ulaji wake wa mafuta ni mdogo sana na zitatusaidia katika halmashauri nyingi,”amesema Jafo.Aidha, Mhe. Jafo amemshukuru sana Rais wa John Magufuli kwa kuonyesha mapenzi makubwa lakini pia amependezwa na Watumishi wa Wizara, Mikoa na Halmashauri

zote kuweza kuhudhuria hafla hiyo muhimu iliyofanyika bandarini Jijini Dar es Salaam.Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula amemshukuru Waziri wa Nchi TAMISEMI na Waheshimiwa Wabunge wote kwa utendaji wao na kuwataka wabunge kuwa na lugha ya ufahamu mmoja ili kuboresha utendaji Serikalini.

“Kwa niaba ya watendaji nawashukuru sana waheshimiwa Wabunge, nilitamani tutembee pamoja kwa maana ya kuwa na uelewa wa pamoja na ndio maana Mhe.Waziri amewakabidhi wabunge magari nao watukabidhi sisi,”Amesema

Charles Kichere Kamishna Mkuu wa Mapato Tanzania, amesema awali magari hayo aliyaona Mhe. Rais alipofanya ziara bandarini na kwamba magari hayo yalikuwa yameteleekezwa na mmiliki wake kutofahamika na ndipo rai, aliagiza kufuata utaratibu wa forodha na kuyataifisha magari hayo na kasha yagawiwe kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Kwa upande wake Mhe. Prof Norman Sigalla King, Mbunge wa Makete, amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa ambulance hizo kwa ajili ya kuimarisha huduma za mama wajawazito.“kwanza nitoe shukrani za pekee kabisa kwa kupewa ambulance kwa ajili ya wilaya yangu ya Makete nakumbuka niliomba kwa ajili ya tarafa za Ukutama, Matamba, Magomba, Tulongwa na Niwaho”amsema.

Amebainisha umbali wa kata ya Ukutama hadi Makete mjini ni kilomita 70 na hivyo itawanusuru wakina mama dhidi ya vifo vya uzazi visivyotarajiwa.Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Hakimu Ndatama amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwapatia ambulance ambayo itaokoa vifo vya akina mama na watoto kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya magari aina ya Suzuki Maruti ambayo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliamuru yagawiwe katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuhudumia Sekta ya Afya nchini. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo (Mb) akimkabidhi moja ya gari la wagonjwa aina ya Suzuki Maruti, Ashura Nkya ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati katika bandari ya Dar es Salaam jana.
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images