Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mh. Ummy Mwalimu ametoa miezi mitatu kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga asilimia 4 za fedha za halmashauri kwaajili ya kuwapa wanawake mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuunga mkono juhudi za serikali katika uchumi wa viwanda.

Amesema kuwa serikali haitasita kuwawajibisha wakurugenzi watakaokiuka maelekezo ya serikali yanayolenga kutekeleza ahadi za Mheshimiwa Rais kwa wananchi ili kuwawezesha wanawake wa mijini na vijijini kiuchumi na hatimae kujiongezea kipato na kuwezesha uchumi wa viwanda.

“Linapokuja suala la kuwawezesha wanawake kiuchumi hatutanii, chama cha mapinduzi tumepewa kura na wanawake wa Tanzania hasa wanawake wa vijijini na tumewaahidi wanawake kwamba tutawapa mikopo yenye masharti nafuu, kwahiyo pale ambapo mkurugenzi anashindwa kutenga fedha kwaajili ya kuwapatia wanawake mikopo hatutaelewana, na tunasubiri mpaka tarehe 30 June 2018 wakurugenzi wote ambao hawajatenga fedha na kuzitoa kwaajili ya wanawake  tutapeleka majina yao kwa Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli,” Mh. Ummy alisisitiza.

Halikadhalika Mh. Ummy amepiga marufuku suala la kutoa fedha ndogo kwa kikundi kikubwa cha kinamama huku akitolea mfano kikundi cha watu sita kupewa 300,000 kuwa haitawasaidia kinamama hao katika juhudi za kujikwamua kiuchumi na kuongeza kuwa ni heri fedha hizo zikabaki kwa mkurugenzi ili ifanye shughuli nyingine lakini sio kuwakwamua kinamama.

 Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu akiserebuka na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizwite katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika manispaa ya Sumbawanga, kushoto kwake niMwakilishi wa Balozi wa Canada. Bi. Susan Steffen pamoja na wanafuinzi. 
 Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu (wa pili toka kushoto)  akiwana  Mwakilishi wa Balozi wa Canada Bi. Susan Steffen (anayemfuatia) na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dk. Khalfan Haule muda mfupi kabla ya Mh. Ummy kutoa hotuba yake.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mh. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa wakurugenzi nchini Tanzania bara juu ya kutenga fedha za mikopo kwa wanawake.
Baadhi ya wanawake walihudhuria kilelelcha siku ya wanawake Duniani yaliyoadhimishwa kimkoa Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa huku mgeni rasmi wa sherehe hizo akiwa Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


MKUTANO WA MPANGO KAZI WA WATAALAM WA MALARIA KUTOKA MAREKANI NA ZANZIBAR WAFANA

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Wataalamu wa maswala ya afya wametakiwa kutanua wigo katika Tafiti zao na wajikite zaidi katika tafiti za maradhi yatokanayo na vyanzo vya maji (Water born diseases)

Maradhi hayo ambayo hutokana na maji ikiwemo Kichocho, Matende, Minyoo, Vikope na Malaria huchukua asilimia 60 ya maradhi yanayowasumbua wananchi.

Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohamed ametoa wito huo alipokuwa akizindua Mpango kazi wa Wataalam wa Malaria kutoka Shirika la Misaada la Marekani na Wizara ya Afya Zanzibar uliofanyika Ukumbi wa Hotel ya Ngalawa mjini Unguja.

Amesema tafiti zitakapofanywa juu ya maradhi hayo zitabainisha chanzo na njia nzuri za kujikinga na mwisho kuifanya Zanzibar kuwa sehemu isiyosumbuliwa na magonjwa hayo.

Waziri Hamad amefahamisha kuwa licha ya Zanzibar kupiga hatua kubwa katika kudhibiti ugonjwa wa malaria bado juhudi zinahitajika za kutokomeza moja kwa moja malaria ifikapo mwaka 2023.
 Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akitoa salamu zake kabl ya kumkaribisha Waziri wa Afya kufungua mkutano wa Mpango kazi wa Wataalam wa Malaria kutoka Shirika la Misaada la Marekani na Wizara ya Afya Zanzibar uliofanyika Ukumbi wa Hotel ya NGalawa mjini Unguja. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Mpango kazi wa Wataalam wa Malaria kutoka Shirika la Misaada la Marekani na Wizara ya Afya Zanzibar uliofanyika Ukumbi wa Hotel ya NGalawa mjini Unguja. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Abdulla akitoa neno la shukran kwa Mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria (PMI) kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali kila hatua. 
 Mkuu wa kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar Dkt. Abdalla Ali akiwasilisha taarifa ya tahmini ya hatua walizozichukua za kupambana na Malaria kwa mwaka 2017 na mikakati yao kwa mwaka huu mbele ya Wajumbe walioshiriki Mkutano wa Mpango kazi wa Wataalam wa Malaria Zanzibar.

HALMASHAURI YA WILAYA KONDOA KUJENGA HOSPITALI YAKE

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Kondoa.

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma kutenga fedha kwenye bajeti ya Mwaka ujao wa Fedha 2018/2019 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Kondoa ili kukabiliana na changamoto za afya zinazowakabili wananchi.

Dkt. Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wakati akianza ziara yake ya siku mbili wilayani humo kukagua shughuli za maendeleo zinazotokana na fedha zilizotolewa na Serikali ikiwemo ujenzi wa vituo vipya vya afya pamoja na miundombinu ya elimu wilayani humo.

Alisisitiza kuwa atafuatilia na kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa ili kusogeza huduma ya afya karibu zaidi na wananchi hususan waishio vijijini ambao wanakosa huduma ya uhakika kutokana na kukosekana kwa hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Kondoa.

Aidha, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amewataka watendaji wa halmashauri hiyo ya Wilaya ya Kondoa kuhakikisha kuwa wanawatumikia wananchi kwa moyo, umoja na mshikamano ili malengo ya kitaifa ya kuwaletea maendeleo kupitia dhana ya Tanzania ya viwanda yaweze kufikiwa.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Kondoa Vijijini Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akielezea maendeleo ya viwanda katika Halmashauri hiyo kwa kusisitiza kujikita katika kilimo ili kupata malighafi wakati wa Mkutano na viongozi wa Idara mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Falesy Mohamed Kibassa (wa pili kulia) akipongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Kondoa Vijijini Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) katika kufanikisha maendeleo ya Wilaya hiyo wakati wa Mkutano kati yake na viongozi wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Kondoa Vijijini Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) akizungumza jambo na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bi. Hilda Saganda (kulia) baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Naibu Waziri huyo na viongozi wa idara katika Halmashauri hiyo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Tigo Yawakabidhi simu washindi 84 wa Promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus

$
0
0
 Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, leo imewazawadia washindi 84 wapya wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus simu aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G.

Akikabidhi zawadi hizo kwa baadhi ya washindi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo, Mtaalam wa usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza alisema kuwa kufikia sasa promosheni hiyo imeibua washindi wa simu 240 kutoka sehemu mbalimbali za nchi.

‘Kila anayenunua bando la intaneti kuanzia TZS 1,000 kupita *147*00# anapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pia anaingizwa kwenye droo ya kushinda mojawapo ya simu zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zinazoshindaniwa katika promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus.’

Mtalaam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kulia) akimkabidhi mfanyabiashara wa Mbezi Beach, Michael Peter Ngwashi, zawadi ya simu ya kisasa aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#. Kushoto ni balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali.
Mtalaam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kulia) akimkabidhi mfanyabiashara wa Mbagala, Grace Gastory Mandai, zawadi ya simu ya kisasa aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#. Kushoto ni balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali.
Mtalaam wa Usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza (kulia) akimkabidhi mfanyabiashara wa Mbezi Beach, Mohammed Omar Sabuni, zawadi ya simu ya kisasa aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus. Jumla ya washindi 240 wamejishindia smartphoni hizo baada ya kununua vifurushi vya intaneti kupitia *147*00#. Kushoto ni balozi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Meena Ali. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


MCHENGERWA AZUNGUMZIA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA JIMBONI KWAKE RUFIJI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MBUNGE wa Rufiji mkoani Pwani, Mohamed Mchengerwa amesema tangu amechaguliwa na wananchi kuwa mbunge wa jimbo hilo amefanikiwa kusukuma upatikanaji wa maendeleo na kuboresha upatikanaji wa huduma bora za kijamii.

Mchengerwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia utekelezaji wa ahadi za maendeleo ya wananchi na hasa katika elimu, miundombinu ya barabara, nishati ya umeme pamoja na maji safi na salama.

"Katika kipindi cha  miaka miwili ya ubunge kuna maendeleo mengi yamepatikana na haijawi kutokea.Hiyo yote inatokana na jitihada zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na mimi mwenyewe katika kuelezea matatizo ya wananchi kwa Serikali,"amesema.

Amesema katika mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge utasukuma maendeleo ya wananchi wa Rufiji na kuongeza ajira kwa  wananchi katika kuinua uchumi wa jimbo hilo.Ujenzi wa mradi huo ulikuwa ni kilio cha muda mrefu lakini kutokana na Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza kwa vitendo. 

Mchengerwa amesema ujenzi wa mradi wa Stiegler's Gorge utakwenda pamoja na ujenzi wa daraja la Utete ambalo lilikuwa changamoto ya muda mrefu na kufanya baadhi ya huduma kwa jamii zishindwe kuendelea.

Amesema katika jitihada hizo Serikali imekarabati shule za msingi na sekondari pamoja hospitali, zahanati  na vituo vya afya.

Amesema katika kujenga afya za wananchi wa Jimbo la Rufiji ameandaa mashindano ya Mchengerwa Cup ambalo ltaanza siku za karibuni kwa kushindanisha timu mbalimbali.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Rufiji,  Rajab Mbonde amesema mbunge afanya kazi nzuri na kufanya viongozi wa Chama kutembea kifua mbele katika ukarabati wa ofisi yao ngazi ya Wilaya.
.Mbunge wa Rufiji , Mohamed Mchengerwa  akizungumza na waandishi habari kuhusu utekelezaji wa ahadi mbalimbali katika jimbo la Rufiji.
 Mwenyekiti wa Wilaya ya  Rufiji , Rajab Mbonde akizungumza na waandishi kuhusu utekelezaji wa ahadi za mbunge kama wasimamizi wa ilani ya Uchaguzi .

 Mbunge wa Rufiji , Mohamedi Mchengerwa akimkabidhi Katibu wa Chama cha Mpira wilayani Rufiji Yahya Kisangi kwa ajili ya Ligi ya Wilaya ya Mchengerwa Cup.


MASHINDANO NDONDO CUP YAZINDULIWA RASMI

$
0
0
Na Agness Francis Globu ya jamii
MASHINDANO ya Ligi ya Ndondo CUF kwa mwaka 2018 yanatarajiwa kufanyika kwenye mikoa kadhaa nchini na tayari yamezindulwa rasmi leo huku ikielezwa maandalizi na fedha ambazo zitapatikana kwa kila timu kutokana na hatua ambayo itakuwa inafikia.

Akizungumza leo katika Viwanja vya Escape 1 Mikocheni jijini, Mwenyekiti wa Maandalizi ya mashindano hayo Shafii Dauda amesema mchakato wa usajili katika Mkoa wa Dar es Salaam utaanza leo kupitia usimamizi wa Chama cha Soka Mkoa(DRFA) na ada ya usajili ni Sh.300,000 zitakazolipwa kupitia akaunti ya chama hicho.

Ametaja mikoa mingine ambayo mashindano hayo yatafanyika ni Mwanza na Ruvuma na kufafanua kuwa Mkoa wa Dar es Salaam utafungua mashindano hayo Aprili 4 mpaka Mei 6  mwaka huu.

"Na baada ya kupatikana kwa timu 32 kutoka kwenye hatua za awali yatapangwa rasmi makundi kwa timu zitakazoshiriki na zitaanza kumenyana kwenye Uwanja wa Bandari na Kinesi jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 1 mpaka Julai 22 mwaka huu,"amesema.

Dauda amesema mshindi wa kwanza katika Mkoa wa Dar es Salaam atapata kitita cha Sh.milioni 10, Mshindi wa pili Sh.milioni 5, Mshindi wa 3 atapata  Sh.milioni  3 na Mshindi wa nne atapata Sh.milioni 1.

"Mbali na kitita cha fedha kwa mshindi wa kwanza hadi mshindi wa nne timu zote zitakazoingia kwenye hatua ya 16 bora zitapewa Sh.500,000 kwa kila timu kwa ajili ya maandalizi.Pia zitakuwa zikipewa usafiri kwa kuwachukua kuwapeleka uwanjani na kuwarudisha majumbani.Kila siku ya mechi watapa chakula cha mchana.

"Kwa timu zitakazoingia hatua ya nane bora zitapewa Sh.milioni 1 kwa kila timu kwa ajili ya maandalizi na timu zitakazoingia hatua ya nne bora zitapewa Sh.milioni 1.5 za maandalizi.Kwa timu ambazo zitaingia hatua ya fainali zitapewa Sh.milioni 2 za maandalizi,"amesema Dauda.
Mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Cup, Shafii Dauda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya michuano ya Ndondo Cup itayoanza kutifuana Mwezi ujao mwaka huu leo katika fukwe za  Escape 1 Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

RAIS MAGUFULI AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHATO MKOANI GEITA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali wa Chato waliohudhuria katika ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay mara baada ya Benki hiyo kuchangia mfuko wa Elimu wa mkoa wa Geita kwa kutoa kiasi cha Shilingi milioni 50 kabla ya ufunguzi wa Tawi hilo la Benki.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia kwa kupiga makofi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji wakati msanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Chato alipokuwa akitoa burudani ya ngoma hiyo.
 Mmoja wa wacheza ngoma wa kikundi cha Ngoma za asili cha Chato akimwagiwa Rangi kabla ya kuonesha umahiri wake wa kucheza ngoma hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Denmark hapa nchini Einar Hebogard Jensen wakati akielekea kwenda kufungua Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati msanii wa Msechu Bendi Peter Msechu alipokuwa akiimba mara baada ya kufungua tawi hilo la Benki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Chato mara baada ya kutoka kwenye ufunguzi wa tawi hilo la benki ya CRDB lilopo Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ZIMAMOTO YAWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MOTO WA SOKO MBAGALA

$
0
0
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage, akiwapa pole Waathirika wa moto ulioteketeza vibanda vya Wafanyabiashara wa Soko la Nguo Mbagala Temeke Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
 Kamaishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage akimfariji kwa kumpa pole Mama lishe Bi. Fatma Hassan aliyeunguliwa na vitendea kazi vyake kufuatia tukio la kuungua kwa moto kwa soko la nguo Mbagala.  Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage akikagua eneo la Soko la Nguo Mbagala lililoteketea kwa moto juzi. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
Sehemu ya Wafanyabiashara wa Soko la Nguo Mbagala Temeke Jijini Dar es Salaam walioathirika na moto ulioteketeza vibanda vya wafanyabiashara hao juzi. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)


TAMASHA LA PASAKA WASHIRIKI WAZIDI KUMIMINIKA KANDA YA ZIWA, UPENDO NKONE NA JOSHUA MLELWA NDANI

$
0
0

Mmoja wa Waandaaji wa Tamasha la Pasaka 2018, Ufoo Saro akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Tamsha hili ikiwa ni pamoja na kuwatambulisha waimbaji wengine waliweza kuungana kuleta utamu zaidi ndani ya Kanda ya Ziwa na vitongoji vyake. 

Waimbaji waliotangazwa ni Joshua Mlelwa (Kushoto) na Mwanamama Upendo Nkone (kulia).Ufoo Saro amesema kuwa suala la Usalam limezingatiwa vyema hivyo wajitokeze kwa wingi bila kukosa.

Katika Tamasha hilo, Mwimbaji Rose Muhando anatarajia kuzindua albamu yake ambayo amejiandaa kwa muda mrefu.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Joseph Mlelwa (kushoto) akitoa kiburudisho cha wimbo wake wa Yesu Anaweza aliouimba mwaka 2016. Mlelwa amesema kuwa amejiandaa vyema hivyo wakazi wa Mwanza na Simiyu wajitokeze kwa ngumu ili kuweza kufanikisha zaidi tamasha hilo. Tamasha la Pasaka Mwaka 2018 litafanyika Kanda ya Ziwa ambapo Aprili 1 itakuwa ndani ya Uwanja wa CCM - Kilumba na Aprili 2, 2018 ndani ya Uwanja wa Halmashauri, Simiyu. Mwimbaji Joseph Mlelwa ni mmoja ya waimbaji wa Kwaya ya Kijitonyama Upendo Group ambapo kwa sasa amekuwa akifanya kazi zake peke yake.
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Nkone amethibitisha rasmi kushiriki Tamasha la Pasaka 2018 kwa kuwatoa hofu wakazi wa Kanda ya Ziwa wajitokeze kupata burudani ya kutosha ya kukata na shoka. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wakkitambulisha mbele ya waandishi wa habari (hawapo picha) Mwimbaji huyo amesema kwa sasa amejipanga vyema hivyo wakazi wa Mwanza na Simiyu wakitokeze kwa wingi.

"Sina cha kusema zaidi ya kuwaambia wakazi wa Mwanza na Simiyu wajitokeze kwa wingi maana nimejipanga kuwapa burudani ya kutosha ikiwa ni pamoja na kumshukuru bwana kwa matendo yake makuu aliyonitendea," amesema Nkone.

ACT WAPATA PIGO ,VIONGOZI WA NNE NA WAFUASI 45 WATIMKIA CCM

$
0
0
Chama cha ACT Wazalendo wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma , kimepata pigo baada ya viongozi wake wa nne na wafuasi 14 ambao ni wananchama kuhamia Chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM). Viongozi hao wamesema wamechukua maamuzi ya kuhamia CCM baada ya kuona utendaji kazi wa Mhe , Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Maguful kuwa ni mzuri,pamoja na kusema chama hicho cha ACT hakina uwezo wala mwelekeo wa kuchukua dola, hivyo wamesema wapo sahihi kuhamia CCM ili kuendana na kasi ya Rais kuweza kuleta maendeleo katika wilaya hiyo ya Tunduru na Taifa kwa ujumla.

MBUNGE HAWA MCHAFU AWAASA WANAJAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVUhab

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Pwani  Hawa Mchafu amewataka wanajamii wote kudumisha amani na kujiepusha na vitendo viovu ikiwa ni pamoja na uhalifu, ubakaji, matumizi ya madawa ya  kulevya, pombe haramu maarufu kama virobo na gongo,ukatili na ukandamizaji wa makundi mbalimbali katika jamii kama vile watoto, wanawake, wazee na wenye ulemavu.

Mchafu alisema hayo wakati wa  siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hapo jana yaliyofanyika katika kata ya Nyamato wilayani Mkuranga.
Mchafu aliongeza kwamba pamoja na unyanyasaji juhudi mbalimbali za wadau na serikali katika nchi yetu bado ukatili na unyanyasaji kwa wanawake ni mkubwa mno.”Katika wilaya yetu ya Mkuranga bado vitendo hivi vinaendelea katika baadhi ya maeneo ya kata na vijiji vyetu”. Mchafu alisema

Mchafu aliendelea kusema kwamba tayari serikali imechukua hatua mbalimbali ili kuondoa tofauti za kijinsia kwa kuingiza mitazamo ya kijinsia katika sera zinazowabagua wanawake “Nitumie fursa hii kuwaasa wanawake kujitokeza kushiriki katika fursa na nafasi mbalimbali na kufanya kazi kwa juhudi,maarifa na weledi mkubwa ili kufikia malengo ya Tanzania ya Viwanda.
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akipokea zawadi ya keki kutoka kwa Jukwaa la Wanawake Wila
ya ya Mkuranga.

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akipokea na kusoma mabango ya akina mama wa wilaya hiyo katika maadhimisho ya kilele cha siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Jana.

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akipokea mche wa Mkorosho baada ya kuzindua kitalu hicho katika maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega.Picha na Emanuel Massaka.



VIJANA WA BAGAMAYO TEMBEENI KIFUA MBELE KUMSEMEA RAIS MAGUFULI -MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA PWANI

$
0
0


NA ELISA SHUNDA-BAGAMOYO.

WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Bagamoyo wametakiwa kutembea kifua mbele huku wakijiamini na kuwaelezea vijana wenzao miradi mbalimbali mikubwa inayofanyika hapa nchini chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais,Dk.John Magufuli katika kutimiza malengo ya Tanzania ya Viwanda kwa kujenga barabara za juu (Fly Over),uboreshaji wa miundombinu,mradi wa umeme vijijini (REA),elimu bure shule za msingi na sekondari,ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard Gauge,ununuzi wa ndege za Bombadier pamoja na kutumbua watumishi vyeti feki.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Makwiro wakati akizungumza na vijana wa UVCCM wilayani Bagamoyo jana kwenye muendelezo wa ziara yake ya kutembelea wilaya zote za mkoa wa Pwani ambapo amewashukuru na kuwakumbusha vijana hao kuishi katika ndoto ya Rais Dk.John Magufuli na malengo ya kuifanya nchi kuwa Tanzania ya Viwanda katika hotuba waliyozungumza katika mkutano mkuu wa vijana hao uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni ambapo katika mkutano huo ulimwezesha Kheri James kuwa mwenyekiti wa UVCCM Taifa.

“Nimekuja katika Wilaya hii ya Bagamoyo kwa ajili ya kutoa shukrani zangu kwa ninyi vijana wenzangu kwa kuniamini na kunipigia kura za ndiyo zilizoniwezesha kushinda nafasi hii ya uenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani hivyo basi nitatumia akili zangu,nguvu,uwezo,rasilimali na elimu niliyonayo katika kuhakikisha natatua changamoto za vijana wa mkoa wetu wa Pwani leo kichama naonekana nawawakilisha vijana wa Chama Cha Mapinduzi peke yake lakini ukweli ni kwamba nitakachokipigania mimi kitawaletea faida vijana wote wa mkoa huu hivyo kwa yale nitakayokuwa nayapambania kwa vijana nanyi muwe bega kwa bega mniunge mkono katika kufanikisha changamoto za vijana” Alisema Mwenyekiti Makwiro..
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akizungumza na wajumbe wa baraza la vijana wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo wakati wa ziara yake leo mkoani Pwani. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Mkwayu Makota na Katibu UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto. Picha zote na Elisa Shunda
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akimkabidhi Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Mkwayu Makota (Kulia) kadi za umoja wa vijana 100 kwa ajili ya kusajili wanachama wapya. Anayeshuhudia ni Kulia ni na Katibu UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto.

Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Bagamoyo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Seleman Makwirowakati alipokuwa akizungumza nao katika mkutano huo.
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Bagamoyo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Seleman Makwirowakati alipokuwa akizungumza nao katika mkutano huo.

KLNT holds 3rd Tanzania National Prayer Breakfast meeting in Dodoma

$
0
0
KLNT holds 3rd Tanzania National Prayer Breakfast meeting in Dodoma

Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) in partnership with the Committee of Union of Churches Dar es Salaam, hosted its 3rd annual National Prayer Breakfast at the Morena Hotel -Dodoma. The event was held on Thursday 8th March 2018 with the theme “Integrity in Leadership”

The 3rd National Prayer Breakfast was attended by 200 government, business, religious and community leaders. The event was graced by Hon Mizengo P Pinda the former Prime Minister of The United Republic of Tanzania as the Guest of Honor.

In welcoming participants at the event Mr. Isaac Mpatwa, the Founder and CEO of KLNT introduced Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) as a non-governmental, non-partisan and non-denominational organization that exists to identify, develop, mentor, deploy and support Ethical Value-based leaders for Tanzania and Africa at large. 

He said, “At Kingdom Leadership Network Tanzania we are passionate to see transformation in leadership across all sectors and levels of leadership in our country Tanzania. KLNT is made up of people with a common desire to answer their call into leadership and become custodians of the Nation’s wealth”
Former Prime Minister, Mizengo Peter Pinda addresses participants during the 3rd Tanzania National Prayer Breakfast meeting organized by Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) in Dodoma on Thursday.
Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) CEO and Founder, Isaac Mpatwa giving his welcoming remarks.
Former Vice President World Bank - Africa Region, Dr. Oby Ezekwesili delivers her speech during the 2018 Tanzania National Prayer Breakfast in Dodoma.
A cross section of participants during the 2018 Tanzania National Prayer Breakfast in Dodoma. 
Former Prime Minister, Mizengo Peter Pinda (centre) poses for a souvenir picture with KLNT officials after the 3rd Tanzania National Prayer Breakfast in Dodoma on Thursday. 

MAVUNDE AHAMISHIA OPERESHENI KUWABAINI WAAJIRI WANAOKIUKA SHERIA ZA KAZI MKOANI MOROGORO

$
0
0
OPERESHENI ya nchi nzima kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi sheria ya ajira na mahusiano kazini na wale ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), inayoongozwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, imeingia Mkoani Morogoro leo Machi 9, 2018, ambapo waajiri wamechukuliwa hatua mbalimbali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini. 

Operesheni hiyo iliyoanzia jijini Mwanza Februari 26, 2018 inafuatia agizo alilolitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, jijini Mbeya mwishoni mwa mwaka jana ambapo aliagiza waajiri ambao bado hawajatekeleza Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi, Sura 263 marejeo ya mwaka 2015, ambayo inamtaka kila mwajiri kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania bara awe amejisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko huo, wafikishwe mahakamani. 

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, ambaye anafuatana na Mhe. Mavunde kwenye ziara hiyo ya kushtukiza, kuna jumla ya waajiri 536, na kati ya hao ni waajiri 294 tu ndio waliojisajili na Mfuko huku wengine 242 bado hawajatekeleza takwa la kisheria la kujisajili na Mfuko. 

“Naagiza waajiri hawa ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, wanaofikia 242 wafikishwe mahakamani mara moja ili wakajibu mashtaka kwanini hawajatimiza wajibu wao wa kisheria.” Aliagiza Mhe. Mavunde. 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Tumbaku Alliance One Mkoani Morogopro leo Machi 9, 2018. Mhe. Mavunde ameagiza waajiri 242 Mkoani Morogoro ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF) kufikishwa mahakamani mara moja.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi, kiwanda cha Tumbaku Mkoani Morogoro, Ujaicy Kayera leo Machi 9, 2018 wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya Mkoani humo ili kubaini waajiri ambao bado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na wale ambao hawatekelezi Sheria ya Kazi na Mabhusiano Kazini. Mhe. Mavunde ameagiza waajiri 242 ambao hawajajisajili na Mfuko kufikishwa mahakamani mara moja.
Naibu Waziri Antoni Mavundeakizungumza na Meneja wa Kampuni ya Hood, Faisal Hood. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi.Rehema Kabongo
Naibu Waziri akiwasli kwenye Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance kilichopo Kingolwira, ambapo alizungumza na wafanyakazi na kubaini makosa ya kiutendaji kwa muajili.
Naibu Waziri akiwasli kwenye Kiwanda cha kusindika Tumbaku cha Alliance kilichopo Kingolwira, ambapo alizungumza na wafanyakazi na kubaini makosa ya kiutendaji kwa muajili.

BRIGEDIA JENERELI MSTAAFU AONGOZA MAZISHI YA KABURU KIGOMA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amewaongoza mamia ya wakazi wa viongozi wa Serikali na vyama vya siasa katika mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe nchini na Mwenyekiti msaafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Kigoma, Amani Kaburu.

Akizungumza katika msiba huo Brigedia Jenerali Maganga amesema Kaburu ni mwanasiasa aliyejikita kutetea haki za wananchi wa Kigoma na alikuwa wa kwanza kupigania maendeleo ya mkoa huo.Mwili wa Kaburu umepumzishwa jana kwenye nyumba yake ya milele.

Amesema Serikali na CCM itamkumbuka Kaburu kwa mchango mkubwa ambao ameufanya katika mkoa huo na amekuwa mfano wa kuigwa na wengine na licha kutangulia mbele ya haki ameacha alama.

"Marehemu Kaburu atakumbukwa kwa mchango wake na alipokuwa kiongozi wa vyama mbalimbali na hata katika Bunge la Afrika Mashariki.Hakika ameondoka lakini wana Kigoma tutamkumbuka daima na kwa wanasiasa wengi wanafahamu kuwa vijana wengi mkoani hapa wamejifunza siasa kutoka kwake,"amesema na kuongeza kifo cha Kaburu kimeacha pigo kubwa kwa Serikali, CCM, wananchi wa Kigoma na Watanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Amandusi Nzamba amesema CCM imepata pigo kubwa kwa kumpoteza mwanasiasa huyo aliyekuwa mstari wa mbele kukisaidia chama hicho katika kufikia malengo yao.Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe amesema kama mtoto na mwanafunzi wa Kaburu pamoja na tofauti za kisiasa ndiye aliyekuwa mwalimu wao na aliwazibua masikio wanasiasa wengi wa Mkoa huo.
 Baadhi ya Ndugu,Jamaa na Marafiki wakiwa kwenye mazishi ya Dkt Kaborou hapo jana.


WANAOTAKA KUUZA FIGO ILI WAPATE FEDHA SASA WAPIGWA MARUFUKU

$
0
0
*Rais Chama cha Madaktari bingwa wa figo atoa sababu, atoa ushauri kwa Watanzania

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

CHAMA cha Madaktari Bingwa wa magonjwa ya figo Tanzania kimepiga marufuku biashara  ya uuzaji figo nchini na kueleza kuwa huo si utaratibu mzuri kwa madhara yake ni makubwa.

Pia kimeelezea hali ya ugonjwa wa figo nchini na kwamba kwa mwaka huu wanatarajia kupandikiza figo kwa wagonjwa 50 huku kikielezea jitihada za Serikali katika kuhamasisha wananchi kuzuia ugonjwa figo.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Rais wa Chama cha Madaktari bingwa ya figo Tanzania Dk.Onesmo Kisanga wakati anazungumza na Michuzi Blogu,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Figo Duniani ambayo huadhimishwa kila Alhamis ya pili ya kila Machi.Siku hiyo hutumika kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa figo na hatua ambazo wanataalamu wanachukua ili kukabiliana nao.

Akizungumzia kuhusu tabia ya watu kuuza figo ili kupata fedha,Dk.Kisanga ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema kuwa kwa sasa wamepiga marufuku biashara ya watu kuuza figo kwani ina madhara makubwa.

“Nikiri tunapokea maombi mengi pale Muhimbili kutoka kwa watu ambao wanataka kuuza figo ili wapate fedha.Nieleze tu hii biashara ya kuuza figo haitakiwi kabisa nchini Tanzania.Hata Chama cha madaktari bingwa duniani nacho kimepiga marufuku biashara ya figo,"amesema Dk.Kisanga.

Amesema kikubwa ambacho wanakifanya ni kuendelea kutoa elimu kwa wale ambao wanataka kuuza figo kuwa hairuhusiwi na kubwa zaidi ikifanywa ni biashara maana yake wale wasiokuwa na uwezo watashindwa kununua matokeo yake watokosa matibabu.

WATU 50 KUPANDAKIZWA FIGO MWAKA HUU

Wakati huo huo Dk.Kisanga amesema mwaka huu wanatarajia kupandikiza figo kwa wagonjwa 50 na huo ndio mkakati wao na kufafanua kuwa mwezi huu wanatarajia kupandikiza figo kwa wagonjwa watano na mwezi unaokuna watapandikiza kwa wagonjwa saba.Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kutoa kipaumbele kwenye sekta ya afya na hivyo kufanya idadi ya madaktari bingwa katika kutibu magonjwa ya figo kuongezeka.

"Kwa mara ya kwanza Tanzania tulipandikiza figo mwaka 2017 na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.Aliyepandikizwa figo yupo salama na aliyetoa figo naye yupo salama,"amesema Dk.Kisanga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO MARCH 10,2018

WALENGWA TASAF WILAYANI CHATO MKOANI GEITA WACHANGAMKIA HUDUMA ZA MFUKO WA BIMA YA AFYA YA JAMII.

$
0
0

Takribani kiasi cha Shilingi Milioni 140 zimepatikana katika kipindi cha miaka miwili iliyopita baada ya Wananchi wanaopata huduma za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii-CHF.

Mkuu wa Wilaya ya Chato Bw.Shaaban Ntarambe amewambia Wandishi wa Habari wanaotembelea Mkoani Geita kuona namna Wananchi wanaonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanaovyotumia fursa hiyo kuwa pamoja na kuanzisha shughuli za kiuchumi ,walengwa hao pia wamehamasishwa kujiunga na CHF kwa kuchangia kiasi cha shilingi 10,000 kwa mwaka na kupata huduma za matibabu kwa kipindi chote cha mwaka.

Amesema kumekuwa na mwitikio mzuri kwa Walengwa hao wa TASAF kujiunga na huduma za CHF kwa kutumia sehemu ya ruzuku wanayoipata kupitia utaratibu wa uhawilishaji fedha na hivyo kuboresha afya zao na kupunguzia mzigo wa serikali kuwahudumia hususani pale wanapohitaji huduma ya matibabu.

Kwa Upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chato Dr Athanus Ngambakubi amesema katika vijiji ambavyo TASAF inatoa huduma kwa Kaya Maskini ambazo zimejiunga na CHF,Wataalam wa Afya hawalazimiki kutumia nguvu kubwa kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kupata huduma za matibabu hospitalini kinyume na ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa Mpango huo.

Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF ,Esther Seleman mkazi wa kijiji cha Mabalasana katika halmashauri ya wilaya ya Geita akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) shamba la Mpunga ambalo amelima kwa kutumia sehemu ya ruzuku aliyoipata kupitia utaratibu wa uhawilishaji fedha kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Mmoja wa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Isamilo katika halmashauri ya wilaya ya Geita akiwa katika shughuli ya kushona nguo kwa kutumia cherahani alichokinunua baada ya kudunduliza fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kama njia ya kujiongezea kipato.
Mmoja wa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Mabalasana katika halmashauri ya wilaya ya Geita akiwa mbele ya nyumba na matofari aliyopata kwa kutumia fedha za Mpango wa kunusuru Kaya Maskini katika jitihada za kuboresha makazi yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Geita.Ali Kidwaka akizungumza na Wandishi wa Habari juu ya utekelezaji wa Shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF hususani Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri yake ambapo amesema Mpango huo umekuwa chachu ya kaya za Walengwa kupiga vita umaskini kwa mafanikio makubwa na kutoa wito wa kutekeleza Mpango huo katika vijiji vyote.
Mmoja wa Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ,BI. Sabina Mtangwa (aliyevaa gauni jekundu ) mkazi wa kijiji cha Isamilo katika halmashauri ya wilaya ya Geita ,akimwonyesha Afisa Mawasiliano wa TASAF Estom Sanga mbuzi na ng’ombe waliozaliana baada ya kununua mbuzi na kuwauza aliowapata kwa kutumia fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

WANANCHI TABORA WAJITOKEZA KWA WINGI USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeendelea na zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Tabora, ambapo Wilaya zote zinaendelea na zoezi hilo.

Akizungumzia mwenendo wa zoezi hilo Afisa Usajili Mkoa wa Tabora Bi Grace Msaky, amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa na kwamba wananchi wameelewa umuhimu wa Vitambulisho.

Amesema; kuhakikisha wananchi wanapata huduma na wanafikiwa mahali walipo kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa sasa zoezi wanaendesha kwenye Vijiji na Mitaa wanakokaa wananchi na kwamba wananchi wanajulishwa muda na wakati wa kufika kwenye vituo kupata huduma hiyo.

“ kwa sasa wananchi wanaelewa utaratibu; ila changamoto ni baadhi ya wananchi kufika siku za mwisho wa zoezi na kufanya zoezi kuchukua muda mrefu kwenye baadhi ya Kata kinyume na ratiba iliyopangwa” alisisitiza.Mbali na Tobora mikoa mingine 19 inaendelea na zoezi kwa Tanzania Bara huku Tanzania Zanzibar zoezi hilo likiwa limekamilika kwa asilimia 99%.

Wananchi wa kata ya Ipuli mtaa wa Ipuli Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye mashine maalumu za uchukuaji taarifa muhimu za Usajili zikiwemo upigaji picha, alama za vidole na saini ya kielektroniki.
Mkazi wa Mtaa wa Ipuli Bi Halima Abed akiwa kwenye zoezi la kupigwa pichwa ili
kukamilisha Usajili


Bi Maimuna Shabani Bundala Mkazi wa mtaa wa Ipuli akiweka saini ya kielektroniki kwenye mashiya ya Usajili wakati zoezi hilo likiendelea kwenye mtaa wake.
Bw. Shaban Yasin wa Kata ya Ipuli Mtaa wa Nane Nane akichukuliwa alama za Vidole kwenye zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.

MPISHI WA KIMATAIFA MTANZANIA CHEF ISSA ATIA FORA NCHINI SWEDEN KWA MAPOCHOPOCHO

$
0
0
Bango la  kinamama kutoka kila kona ya dunia waliokusanyika mjini Trollhättan Sweden kusherehekea Siku ya Wanawake Machi 8, 2018 na baadaye kwenda kwenye hoteli ya Mtanzania Chef Issa kwa chakula cha mchana
 Kinamama kutoka kila kona ya dunia waliokusanyika mjini Trollhättan bchini Sweden kusherehekea Siku ya Wanawake Machi 8, 2018 wakiwa  kwenye hoteli ya Mtanzania Chef Issa kwa chakula cha mchana

 Chef Issa akiwahudumia kinamama kutoka kila kona ya dunia waliokusanyika mjini Trollhättan bchini Sweden kusherehekea Siku ya Wanawake Machi 8, 2018 wakiwa  kwenye hoteli ya Mtanzania Chef Issa kwa chakula cha mchana
 Mapochopocho kwa kinamama kutoka kila kona ya dunia waliokusanyika mjini Trollhättan bchini Sweden kusherehekea Siku ya Wanawake Machi 8, 2018 wakiwa  kwenye hoteli ya Mtanzania Chef Issa kwa chakula cha mchana
Kinamama kutoka kila kona ya dunia waliokusanyika mjini Trollhättan bchini Sweden kusherehekea Siku ya Wanawake Machi 8, 2018 wakiwa  kwenye hoteli ya Mtanzania Chef Issa kwa chakula cha mchana
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>