Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu

$
0
0
KITUO cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kitaendelea kutroa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na ofisi zote zinazofabnya shughuli zake kwenye kiwanja hicho. 

Mkuu wa kituo hicho, Kamishna Msaidizi Juma Yange amesema leo wakati wa kufunga mafunzo ya zimamoto na uokoaji yaliyofanyika kwa washiriki kupata nadharia na baadaye vitendo yaliyofanyika katika maeneo ya kiwanja hicho. 

Afande Yange amesema kwa kuwa wafanyakazi wengi hawajui namna ya kujiokoa wakati wa majanga ya moto, sasa watafanya mafunzo hayo kuwa endelevu kwa kufanya mara kwa mara, endapo moto utatokea basi waweze kujiokoa na kuokoa mali. 

“Mafunzo haya madhumuni yake makubwa ni ili kila mfanyakazi aelewe umuhimu wa kuwa makini dhidi ya adui moto kwenye sehemu yake ya kazi, kufahamu vyanzo na vitu vinavyosababisha moto a vifaa vya huduma ya kwanza vya kuzimia moto vilivyopo eneo lake la kazi, hivyo litakuwa endelevu,” amesema. 
 Kamishna Msaidizi wa Zimamoto, Hamis Telemkeni (mbele) akitoa maelezo kwa  washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuzima moto yaliyofanyika kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) leo.

 Mkaguzi Zimamoto Theresia Tengia  (kushoto) na Sajini Maria Gulam (kulia) wakionesha wafanyakazi wa ofisi mbalimbali zinazoendesha shughuli zake kwenye Kuiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), moja ya kifaa aina ya blanketi linalosaidia kuzima na kufunika  moto endapo utatokea bila kumuathiri kwa kuungua.

 Sajini Maria Gulam (mbele) akionesha namna ya kutumia mtungi wa kuzimia moto kwa washiriki wa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji yaliyofanyika leo kwenye Kituo cha Zimamoto kilichopo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

 Bi. Julieth Fonga (kushoto) wa Kampuni ya General Aviation Services iliyopo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akielekezwa na Afisa Usalama wa Zimamoto na Uokoaji, Leonard Chami namna ya kuzima moto kwa kutumia mtungi, wakati wa mafunzo yaliyofanyika leo kwenye kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha JNIA.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA KUWEZESHA WANAWAKE VIJIJINI-DC MCHEMBE

$
0
0

Wilaya ya Gairo imefanya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Machi 8 kupanda miti ili kuashiria uhai kwa wanawake waliokata tamaa. Zoezi hilo liliongozwa na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe na wanasheria wanawake sita akiwemo Mwanasheria wa Manispaa Mvomerowaliweza kusikiliza kero za muda mrefu za wanawake. 
 
Masuala yaliyoangaliwa katika maadhimisho hayo ni migogoro ya ardhi, mirathi, unyanyasaji kijinsia, ukeketaji na kesi za mimba za utotoni ambapo zaidi Wanawake zaidi ya 65 waliweza kuhudumiwa. Kauli mbiu katika maadhimisho hayo wakati wakiendelea katika Uchumi wa Viwanda, "Tuimarishe usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake vijijini", ambapo ulipokelewa kwa shangwe na wanawake kijiji cha Kisitwi jambo lililomvutia Mkurugenzi Bi. Agnes Mkandya na kugawa miche ya korosho zaidi ya elfu 40, mbegu za pamba na kahawa. 
 
Mhe. Mchembe alisisitiza wanawake kulima Kilimo cha Kibiashara ili kuinua kipato na uchumi wao waondokane na utegemezi. Mkuu wa Wilaya huyo ameziomba Taasisi za kifedha NMB na CRDB kutoa mikopo kwa wanawake yenye riba nafuu, aidha kabla ya mkopo wanawake wapewe Elimu ya fedha, masoko, vifungashio, Sheria mbambali na ujasiriamali katika mapana yake. 

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akimtambulisha kwa wananchi Mkuu wa dawati la Jinsia Polisi Gairo, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Hope Kimaro wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Wilayani humo. 
Mgeni rasmi Mhe. Mchembe akipokea taarifa ya Wanawake Gairo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Gairo, Agnes Mkandya. 
Uongozi wote wa Wilaya ya Gairo, upande wa Chama na Serikali ukielekea kwenye kupanda miti kuashiria alama ya uhai mpya kwa wanawake waliokata tamaa. 
Viongozi Wanawake wa Wilaya ya Gairo wakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (wa pili toka kushoto), Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Nyangasi (watatu kushoto) na Agnes Mkandya wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya siku ya Wanawake Duniani. Wilaya ya Gairo inaendeshwa na wanawake kwa asilimia zaidi ya 95 (tisini na tano).
Wanawake wakipima VVU wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Wilayani humo.

Introducing "Sitokuweza" Official Video by Byson Barlow

INTRODUCING "WAYU WAYU" BY DOGO JANJA

CRDB TAWI LA VIVA WASHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUWAHAMASISHA WANAWAKE KUFUNGUA AKAUNTI YA MALKIA

$
0
0
 Mgeni rasmi GeminaLukuvi akizungumza wakati wa benki ya CRDB tawi la VIVA wakisheherekea siku ya wanawake dunia pamoja na kuwashawishi  jinsi ya kuhifadhi pesa zao za akiba kwa kila mwezi kwa mwaka mmoja.

WAFANYAKAZI benki ya CRDB tawi la VIVA jijini Dar es Salaam washeherekea siku ya mwanamke duniani kwa kuwahamasisha akina mama na wanawake kwa ujumla kufungua akaundi ya Malkia kwaajili ya kujiwekea akiba zao.

Hii ni sawa na kibubu cha wanawake ambapo kila mmoja anaweza kuweka akiba yake ndani ya mwaka mmoja pamoja na kupata faida.
Hii inaleta amani ya moyo kwakuwa akiba inakuwa salama pamoja na kuwa na kinga yake ni imara.

Pia tujifunze kwa baadhi ya wanawake waliofanikiwa ili kila mwanamke afanikiwe kwa kufanyka kazi kwa bidii zaidi na kutumia utashi katika kufanya shughuli zetu mbalumbali.
 Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawila Viva waiwa na mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la VIVA, Naomi Mwamfupe akizungumza na wanawake wa Benki hiyo jijin Dar es Salaam jana wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
Baadhi ya wanawake wakiungana na wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la VIVA jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanawake wakiwa katika benki ya CRDB tawi la Viva jijini Dar es Salaam wakisheherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila Machi 8 kila mwaka kwaajili ya kujua mchango wa mwanamke katika nafasi mbalimbali za ajira pamoja na kujua dhamani ya Mwanamke katika jamii.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB  tawi la VIVA jijii Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakisheherekea siku ya wanawake duniani.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la VIVA, Ester Kitoka akizungumza na wanawake wakati wakisheherekea siku ya mwanamke duniani iliyofanyika katika tawi la VIVA.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la VIVA, Ester Kitoka akizungumza na wanawake waliungana pamoja na kuzungumza namna mwanamke anaweza kuhifadhi pesa zao kwa kufunguua akaunti ya Malkia.
Injinia wamajengo na barabara na Mjasiliamali na Maida waziri akizungumza wakati wa kusheherekea siku ya wanawake duniani ambay hufanyika kila Machi 8 kila mwaka . pia amewahamasisha vijama pamoja na kinamama kujiamini wakati wakifanya shughuli zao za maendeleo.

ASASI YA KIRAIA YA FEDHA KUJA NA MRADI WA “VIJANA NA ELIMU YA PESA” (VIEPE)

$
0
0
 Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo pamoja na kutambulisha mradi wa "Viepe" kwa kutoa elimu kwa vijana wa sekondari kakika mkoa wa Dar es Salaam na baadae Tanzania kwa ujumla.
Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu wa FEDHA, Mohamed Mchoro na kushoto ni  Afisa mradi wa FEDHA, Linus Amedei. 

ASASI ya kiraia ya Financial Education for Development and human Achievement (FEDHA) Machi 28 mwaka huu kuzindua mradi wake juu ya kuelimisha vijana kuhusu udhibiti sahihi wa pesa binafsi katika nyanja za utafutaji na utumiaji pesa, uwekaji akiba, uandaaji wa bajeti na uwekezaji wa pesa ili kuwawezesha kukuza ustawi wao wa kipesa na kufikia uhuru wa kifedha.

Hayo ameyasema Mkurugenzi mtendaji wa asasi ya kiraia ya FEDHA Jafari Selemani wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa 

Akizungumza kuhusu asasi ya FEDHA, Bw. Jafari Selemani – Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo amesema “Asasi ya kiraia ya FEDHA ni asasi pekee ambayo imejikita katika utoaji wa elimu ya udhibiti pesa binafsi ili 
kukuza uelewa wa masuala ya kifedha kwa umma wa watanzania kuanzia ngazi ya chini yaani wakiwemo watoto, vijana hadi watu wazima, dhima yetu ni kuwafanya watanzania wapate ujuzi,weledi na taarifa sahihi 
juu ya masuala ya kifedha ambapo itawasaidi kufanya maamuzi ya kujiamini yenye manuufaa kwao binafsi na kwa nchi katika kuhakikisha tunapata sekta ya fedha na uchumi imara na endelevu”

“Malengo ya FEDHA ni, kukuza ustawi wa 
kipesa kwa kutoa elimu; kuwezesha watanzania kutambua wajibu na haki zao kama watumia wa bidhaa na huduma za kifedha; kushiriki kuleta ujumuishi wa uchumi na kifedha Tanzania; na Kushirikiana na wadau 
mbalimbali katika kupambana na Umasikini pamoja na udhibiti finyu wa rasilimali fedha.” amesema Selemani.

Kwaupande wake Afisa mradi wa FEDHA, Linus Amedei amesema  kuwa,”Mradi wa Vijana na Elimu ya Pesa ni mradi ambao unalenga kuongeza weledi, ujuzi na uwezo wa vijana juu ya udhibiti na matumizi 
mazuri ya pesa, mradi umelenga vijana hasa wa Elimu ya sekondari.

Vijana ndio muhimili,injini na nguvu kazi ya kuleta maegeuzi ya kiuchumi na hususani tukiwa katika kufanikisha sera ya Tanzania ya viwanda, kwahiyo elimu ya pesa binafsi ni msingi madhubuti kwa uchumi wetu.

Ametoa rai kwa wadau mbalimbali wakiwemo, Serikali kupitia wizara na taasisi zake kama wizara ya fedha na uchumi, wizara ya ajira vijana na kazi, wizara ya elimu, DSE, TIRA, TIC, TIB na  SSRA kuwaunga mkono na 
kuwapa ushirikiano ili waweze kuwafikia vijana na watanzania wengi.

AzamFc kuvaana na Mbao FC kesho.

$
0
0
Kikosi cha Azam FC

Na Agness Francis Globu ya jamii. 
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na kati AzamFc  kuvaana na MbaoFC ya Jijini Mwanza   baada ya kumalizana na Mwadui FC  ambapo wanalambalamba hao walitoka kifua mbele kwa kuifunga timu hiyo bao 1-0 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi. 

Timu hizo mbili zitapimana nguvu hapo kesho majira ya saa1 Usiku katika dimba la Uwanja Wa Azam Complex Chamazi. 

Ambapo kila timu zina presha ya kutaka kupata ushindi wa kuibuka na Alama 3 ili kuweza kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi.

Akizungumza na waandishi Wa Habari  
Ofisa Habari AzamFc Jaffary Iddy  leo katika ofisi zao Mzizima Jijini Dar es salaam amesema kuwa kikosi tayari kipo kambini na kinaendelea na mazoezi. 

"Kikosi kipo  kambini kinaendelea na mazoezi yake  katika kuelekea kwenye mchezo huo wa aina yake Ambapo kila timu inaitaji ushidi, tunaieshimu Timu ya Mbao iko vizuri na Ina kikosi kizuri lakini na sisi Tumejipanga vema kubakiza Alama 3 Nyumbani"amesema msemaji huyo  Jaffary. 

Maganga amesema kuwa wataendelea kumkosa mchezaji wao Yakubu Mohammed  ambaye alipata majeraha pamoja na Kipa wao namba 1 Razack Abarola. 

"Wachezaji Wote wako fiti ila tutaendelea kumkosa mchezaji wetu Yakubu Mohammed aliyepata majeraha katika mchezo wa michuano ya kombe la shirikisho FA  Cup ambapo  tulicheza na timu ya  KMC pamoja na kipa wetu Razack Abarola anaemalizia  kutumikia adhabu ya kutoshiriki Mechi tatu" amesema Jaffary Maganga.

TATU MZUKA YAKABIDHTI KALENDA 500 KWA JESHI LA POLISI,IGP SIRRO ATOA NENO

$
0
0
Kampuni ya Bahati Nasibu Tatu Mzuka imekabidhi kalenda 500 kwa Jeshi la Polisi nchini,kama mwanzo wa uhusiano mwema utakaozaa matunda kati ya Tatu Mzuka na Jeshi la Polisi. 

Akizungumza na waandishi habari wakati makabidhiano ya kalenda kwa Jeshi la Polisi mapema jana , Msemaji wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga amesema wameamua kutengeneza kalenda 500 za Jeshi la Polisi kama sehemu ya kujenga uhusiano bora, lakini pia kuendeleza kauli mbiu ya Tatu Mzuka ya ukishinda Tanzania inashinda pia. 

Maganga amesema wao ni raia wema wa Tanzania hivyo ni nafasi ya pekee kuwa mbele kutokana na kazi ambayo inafanya jeshi la Polisi katika kulinda watu na mali zao chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi(IGP), Simon Sirro,na kwamba Kauli mbiu ya Tatu Mzuka “Ukishinda Tanzania inashinda”, 

“Mchezo wa bahati nasibu wameweza kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Temeke katika kusaidia ujenzi wa kituo cha polisi kuwasaidia wananchi wa Mbande baada ya mapolisi kuuliwa kwa kutokuwa na kituo maeneo ya karibu. " Tumefanya kitu hiki kwa niaba ya washindi wa mchezo wetu wa bahati nasibu,ambao mpaka sasa wamefikia idadi ya milioni 6 ambao wote wamehakikishiwa usalama wao na jeshi la polisi.

Mkuu wa jeshi la Polisi ( IGP ) Simon Sirro ameeleza kuukubali mchezo wa kubahatisha nchini wa Tatu Mzuka unaoshika kasi kwa kubadilisha maisha ya Watanzania wengi. 

IGP Sirro amesema hayo wakati akipokea kalenda za jeshi hilo zilizokabidhiwa na viongozi wa Tatu Mzuka kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi, Posta jijini Dar es Salaam juzi."Mmefanya jambo jema lakini pia mmeonyesha mfano kwa wengine, binafsi nimeguswa na mwamko wenu, hongereni sana na endeleeni kuchapa kazi," alisema IGP Sirro. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro akikabidhiwa moja ya Kalenda kati ya 500 zilizotolewa na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Tatu Mzuka,kutoka kwa Mratibu wa Mawasiliano kampuni hiyo Sebastian Maganga (pichani kati).kulia ni Mmoja wa Wakilishi Simon Simalenga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikabidhiwa moja ya faluna ya Tatu Mzuka kutoka kwa  Mratibu wa Mawasiliano  Tatu Mzuka, Sebastian  Maganga (pichani kati).kulia ni Mmoja wa Wakilishi Simon Simalenga.

TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII ITB BERLIN 2018 NCHINI UJERUMANI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu - Berlin, Ujerumani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi ameongoza msafara wa Tanzania unaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya ITB 2018 yanayoendelea Jijini Berlin nchini Ujerumani.

Lengo la Maonesho hayo ni kutangaza fursa za utalii zilizopo nchini Tanzania katika masoko mbalimbali ya utalii barani Ulaya na duniani kote.Sekta ya utalii inachangia wastani wa asilimia 25 ya fedha zote za kigeni zinazoingia nchini Tanzania na asilimia 17.5 ya pato la Taifa .


Maonesho hayo yalianza tarehe 7 mwezi huu na yanatarajiwa kufikia tamati keshokutwa tarehe 11 Machi, 2018. Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo umehusisha Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.

Washiriki kutoka sekta ya umma ni pamoja na Idara ya Utalii – Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania, Shirika la Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania.
Kwa upande wa Sekta Binafsi jumla ya kampuni 60 zimeshiriki maonyesho hayo ikiwemo Kampuni moja inayoshughulika na uratibu wa matukio (Events and Exhibitions management), Kampuni tatu zinazoshughulika na usafiri wa anga, Kampuni ishirini na saba zinazoshughulika na huduma za malazi (hoteli, loji na kambi za utalii), na Kampuni ishirini na tisa za Wakala wa biashara ya kusafirisha watalii.
Pamoja na shughuli za maonyesho hayo, Katibu Mkuu Milanzi amefanya pia mikutano kadhaa na wadau wa utalii na washirika wa maendeleo waliopo nchini Ujerumani.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi (wa tano kushoto) na baadhi ya washiriki wa maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya ITB 2018 yanayoendelea Jijini Berlin nchini Ujerumani.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) akijadili jambo na wadau walioshiriki maonesho hayo kutoka Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii TANAPA, Ibrahim Mussa.

SDA YATOA MAFUNZO KWA SANAA YA MAIGIZO YA JUKWAANI

$
0
0
Ili kupunguza Changamoto zinazomkabili Mwanafunzi hasa wa KikeShirika la Sports Development Aid SDA Limefundisha Sanaa ya Jukwaani walimu wa shule kumi za Mkoa wa Mtwara Manispaa na Mtwara Vijijini kwa lengo la Kuwafundisha wanafunzi Madhara ya Mimba za Utotoni.

Shirika Hilo ambalo Linawatumia wakufunzi waliobobea katika sanaa za Jukwaa kutoka Nchini Finland tayari limenza kuzunguka mashulni na kukagua kwa jinsi Gani Mafunzo waliyoyatoa yameweza kuwafikia wanafunzi kupitia walim wa Michezo waliokwisha kupewa Mafunzo.

Katika mafunzo hayo Walimu walipewa Fursa ya kuandaa mada ya Igizo Kuhusiana na Changamoto za Mimba mashuleni zinazowakabili na baadaye Kuonesha Igizo kwa njia ya Sanaa za majukwaani kwa lengo la Kutatuz Changamoto zinazotokana na Mila na Desturi za Jamii Husika.

Thea Swai ni Meneja Mradi wa SDA anasema Muda wa Kufanya Mafunzo kwa Njia ya Vitendo ni mdogo kwa wanafunzi kutokana na Baadhi ya shule Kushindwa kutenga Ratiba maalum kwa ajiili ya wanafunzi kuweza Kufanyia mazoezi na Kufikisha Ujumbe.
 Msanii wa Maigizo Yvone Sherry maarufu Monalisa Akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Naliendele Mkoani Mtwara Katika Moja ya Onesho la sanaa za Maigizo ya Jukwaani  Kuhusiana na Changamoto zinazowakumba Wanafunzi wa Kike.
 Wakufunzi wa Sanaa ya Maigizo ya Jukwaani  Pinja Hanton na Niina Sillanpaa kutoka nchini Finlanda Finland Wakiongea na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya naliendele Kuhusiana na Sanaa Hiyo
 Ari Koivo Mkurugenzi wa shirika la LiiKery-Sports& Development la Finland akiongea na wanafunzi wa Sekondari ya Naliendele kuhusiana na majukumu yanayofanywa na shirika lake.
 Mwenyekiti wa Waigizaji Tanzania BONGO MOVIE Elia Mjatta  akitoa mafunzo ya Jinsi ya Ushirikishwa katika sanaa ya maigizo ya Jukwaani.

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 
 
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi (aliekaa kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira Na Walemavu Jenista Mhagama , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi wakizungumza kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SERIKALI YAONGEZA HUDUMA ZA MATIBABU YA UGONJWA WA FIGO.

$
0
0
Na WAMJW. Dar Es salaam.

SERIKALI kupitia Wizara wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeongeza wigo wa kutoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa figo nchini kwa kuongeza vituo vya usafishaji damu hadi kufikia vituo zaidi ya 17, na kufanya mafunzo kwa madaktari bingwa ili kuongezea nguvu madaktari bingwa 13 waliopo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika mapema leo katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam.

“Wataalamu tunao 13 kwa upande wa madaktari, tumeiona hiyo changamoto kama Serikali, tumeongeza wigo wakufanya mafunzo kwa madaktari bingwa, na hivi karibuni tutatangaza ufadhili kupitia Serikali, vile vile tumetenga fedha kwaajili ya kuwafundisha madaktari ili kuweza kufanya matibabu ya figo” alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile aliendelea kusema kwamba Serikali imeongeza wigo wa usafishaji damu kwa kuongeza vituo Zaidi ya 17 ambavyo vinatoa huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa Figo katika hospitali binafsi na Hospitali za Serikali.

“Tumeongeza wigo wa usafishaji damu hadi tunavyoongea, tunavituo Zaidi ya 17 ambavyo vinatoa huduma ya kusafisha damu katika hospitali binafsi pamoja na hospitali zetu za Serikali , Muhimbili kuna vitanda 42, Mloganzira kuna vitanda 12, Bugando vitanda 6, KCMC vitanda 6, Mbeya vitanda 6, bila kusahau Regency, TMJ, Agakhan, Hindumandal, na tunaendelea kuimarisha huduma”. Alisema Dkt. Ndugulile.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria ufunguzi wa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo huazimishwa kila machi 8, ambayo yamefanyika katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam
  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile katika matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika leo katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa wa Figo Dkt. Onesmo Kisanga.
Kiongozi wa Lions International Club Sayed Rizwan Qadri akikabidhi hundi ya shilingi Milioni 1.4 kwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile ikiwa moja ya juhudi za kuunga mkono kupambana dhidi ya magonjwa ya Figo. Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa wa Figo Dkt. Onesmo Kisanga.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile akifanya mazoezi ya viungo wakati wa kujiandaa kuanza kwa matembezi ya Siku ya figo duniani ambayo yamefanyika katika viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA UYOVU-BWANGA KM 45 ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika eneo la Uyovu mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika eneo la Uyovu mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi wa Uyovu mkoani Geita kabla ya kufungua rasmi wa Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanakwaya ya Baraka wakati alipowasili Uyovu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Sehemu ya Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Uyovu mara baada ya kufungua Barabara ya Uyovu- Bwanga- Km 45 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. PICHA NA IKULU. 

UWT YAUNGA MKONO KAULI YA RAIS MAGUFULI KUZUIA MAANDAMANO

$
0
0
*Watangaza vipaumbele vinne watakavyoanza navyo
*Waomba viongozi kutoa kauli za kudumisha mshikamano

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

KAMATI ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT)kwa kauli moja wamempongeza Rais John Magufuli kwa kauli yake ya kuzuia maandamano nchini na kusisitiza wanawake wa Tanzania hawapo tayari kuandamana.

Pia wamempongeza Rais Magufuli na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohammed Shein kwa usimamizi mzuri wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)kwani wamefanikisha uchumi wa Tanzania kuimarika.Pamoja na hayo Kamati hiyo imetangaza kuanza kazi rasmi za UWT ambapo kati ya vipaumbele ambavyo wamepanga kuvifanya kwa kipindi cha miaka mitano ni 18 lakini wametangaza na vipaumbele vinne.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka wakati akitangaza maazimio ya kikao cha Kamati ya Baraza Kuu la jumuiya hiyo.

WAKATAA MAANDAMANO

Akizungumzia kauli ya Rais Magufuli ya kuzuia maandamano nchini,Kabaka amesema wanaukanga mkono kauli hiyo na kusisitiza kuwa wanawake wa Tanzania hawapo tayari kushiriki kwenye kufanya maandamano.

Amesema kuwa jukumu la wanawake wa Tanzania ni kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha nchi inapiga hatua kimaendeleo na kwamba wanalaani kauli za baadhi ya viongozi na watu wengine ambao wamekuwa wakitoa lugha zinazoashiria uvunjifu wa amani nchini.

"Tunaomba viongizi wa dini na viongozi wa kimila kuhakikisha wanatoa kauli za kujenga na kuhamasisha umoja,amani ,upendo ,heshima na mshikamano." Tunampongeza Rais Magufuli na Rais Shein kwa kuendelea kukemea watu wasiotakia nchi yetu iwe na amani kwa kutaka kufanya maandamano au matamko ya uchochezi,"amesema Kabaka.

Ameongeza kuwa "Watanzania hatuna muda wa maandamano ,tuna muda wa kufanya kazi ili kujiletea maendeleo ya nchi yetu tajiri,"amesema.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT)Gaudentia Kabaka(katikati)akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati akielezea maazimio ya Kamati ya Utekelezaji wa Baraza Kuu la jumuiya iliyokutana leo.Picha na said Mwishehe.


RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA ISAKA-USHIROMBO KM 132 KATIKA MJI WA KAHAMA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi wa Kahama mara baada ya kufungua barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
 Sehemu ya Wananchi waliofika kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telak wakwanza kushoto, wabunge wa mkoa wa Shinyanga pamoja na Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi CCM waliohamia kutoka vyama vya Upinzani.
 Sehemu ya Barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Kahama mara baada ya kufungua barabara ya Isaka-Ushirombo km 132 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Masumbwe Mbogwe mkoani Geita wakati akielekea Kahama mkoani Shinyanga. PICHA NA IKULU

SORING WOMEN INTERNATIONAL WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2018

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
 
Wanawake wanaweza kuleta mabadiliko ya maendeleo katika jamii ikiwa watasimama imara kwa pamoja na kuwezesha wenzao ambao hawana elimu ya kutosha. Hayo yamesemwa na mapema leo Machi 10, 2018 na Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi wakati akizungumza katika mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 
Amesema kuwa wanawake wanaweza kufanya mabadiliko kwa kila mmoja kuwa imara na kuamsha wanawake wengine ambao hawajafikiwa na fursa zikiwemo cha uchumi au za ubunifu za kuweza Marsha amasema kuwa kuadhimisha siku ya wanawake lazima kulete mabadiliko sio kuadhimisha tu halafu hakuna matokeo chanya yanayoonekana kwa wanawake tutakuwa hatujatenda haki katika kujipambanua ili kuweza kufikia malengo kwa wale wale walioasisi. 
 
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soring Women International, Luphurise Lema amesema kuwa wakati alipokuwa anafanya kazi aliona kuwa watu waliosoma nje ya ndio wana akili lakini alitambua kuwa sio hivyo tofauti yake ni kujiamini tu na kuamini kila kinachofanyika hata mwanamke anaweza. Luphurise amesema kuwa kila mwanamke asimame imara na kuamini kila anachofanya anaweza kuleta mabadiliko hata ya dunia. 
 
Nae mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri Ali Masoud ‘Masoud Kipanya’ ambaye ni mchora katuni na mtangazaji wa Cloud Radio/Tv ja ya Watengeneza mjadala, Ali Masoud ‘Masoud Kipanya’ amesema kuwa wanawake ni watu muhimu na majukumu anayofanya mwanamke akipewa mwanaume hawezi kuyafanya isipokuwa alioanzisha kauli kuwa hawawezi ndio imewafikisha wanawake lakini wakaze buti wanaweza kuleta mabadiliko. Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi akizungumza wakati wa mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soring Women International, Luphurise Lema akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2018 aliyoandaa jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (katikati) akiwa katika moja waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke katika maadhimisho ya siku wanawake Duniani leo jijini Dar es Salaam. Kutoka ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura, na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soring Women International, Luphurise Lema (kushoto).

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura (katikati) akichangia mada ya nafasi ya mwanamke katika jamii katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mchoraji wa Katuni na Mtangazaji wa Clouds Radio/TV, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (kushoto) na Mratibu wa UN Global Compact Network Tanzania, Emmanuel Nnko (kulia) na Dk. Florence Temu kutoka AMREF (wa kwanza kulia). 

WATOTO WASIORIPOTI MASHULENI WAZAZI WAO KUCHUKULIWA HATUA -SANGA

$
0
0
Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga imesema mpaka ifikapo machi 31 mwaka huu, itawachukulia hatua Kali za kisheria wazazi na walezi wote ambao watoto wao wamefaulu na hawajaripoti shuleni mpaka sasa kwa Sababu zisizo na msingi. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu Wa wilaya ya Mkuranga wakati akifungua kikao cha bajeti ya mwaka 2018/2019 cha baraza la madiwani kilicho fanyika wilayani humo,na kusema kuwa wanafunzi walioripoti ni 3,439 sawa na asilimia 46 na wanafunzi 217 hawajaripoti mpaka sasa ambao ni sawa na asilimia 5.46.

Aidha amesema mpaka ifikapo march 31 mwaka huu,wazazi na walezi ambao watakuwa hawajatoa taarifa zozote kuhusu sababu za watoto wao kutoripoti shuleni watachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Aidha Sanga amewataka madiwani wote  wa wilaya hiyo kushirikiana nae kufuatilia kwa undani suala hilo ili kuhakikisha kuwa wanabaini changamoto zilizopelekea wanafunzi hao kutofika shuleni mpaka sasa."tunachotaka watoto wetu wasome,hatutaki kusukia mtu ameacha shule kwasababu ya kuolewa,wazazi watoe taarifa vinginevyo hatua zitachukuliwa dhidi yao".alisema Sanga.
Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Mkuranga,Juma Abeid akizungumza na Madiwani wa Wilaya ya Mkuranga katika mkutano wa bajeti ya mwaka 2018/2019.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Diwani wa kata ya Mwanandege,Adroph Kowero akifafanua jambo katika mkutano huo.
Madiwani wakimsikiliza Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Mkuranga,Juma Abeid.

JAFO AWATAKA WATANZANIA KUJENGA UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO

$
0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo ameongoza zoezi la kufanya mazoezi kwa watumishi wa Wizara hiyo na Taasisi zake za Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mfuko wa Pension wa LAPF, Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa (LGLB), Wakala wa Barabara za Vijijini(TARURA) na Shirika la Elimu Kibaha (KEC) huku akitoa wito kwa Watanzania kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi.

Mazoezi hayo yamelenga kujenga afya kwa Watanzania na kujiondoa katika hatari ya magonjwa nyemelezi ambapo michezo ya Soka, Riadha, kutembea kwa kasi na Kuvuta kamba ilishindaniwa.

Mhe. Jafo ameambatana na Viongozi wengine wakiwemo Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Joseph Kakunda, Naibu Katibu Mkuu (AFYA) Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt.Zainab Chaula, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Deogratius Ndejembi na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Manispaa ya Dodoma, pia baadhi yakazi wa Manispaa ya Dodoma.

Akizungumza wakati wa mazoezi hayo yaliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri Mkoani hapa, Jafo alisema Watanzania wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuiweka miili yao vizuri na ametoa agizo kwa ofisi yake kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara moja ili kufahamiana pamoja na kujenga hamasa ya kufanya kazi.

“Haya mazoezi tunamuunga mkono Makamu wa Rais Mama Samia katika juhudi zake za kufanya mazoezi,mazoezi ni muhimu kwa afya sasa kila mwezi tutakuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara moja kwa mwezi ili kuongeza hamasa ya kufanya kazi,”alisema.Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda alitoa dua maalum ya kuombea wote waliohudhuria, Mhe. Rais John Magufuli na kumshukuru Mhe. Jafo kwa kuandaa bonanza hilo ambalo linaleta hamasa, upendo na mshikamano wa watumishi Umma na watanzania.

Naye Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Afya, Dk.Zainabu Chaula alimshukuru Jafo kwa kuandaa mazoezi hayo kwani yatawasaidia k kujenga afya pamoja na kupongeza hamasa ya kufanya kazi.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dk.Mahenge alisema kutokana na Mkoa huo kuwa Makao Makuu ya Nchi ni lazima kuwe na viwanja bora vya Michezo.

“Mheshimiwa Rais ameanza ujenzi wa Uwanja wa michezo wa Kisasa katika eneo la Nzuguni lazima tumuunge mkono kwani tunataka Mkoa wa Dodoma uwe wa kuvutia hivyo ni lazima kuwe na viwanja vingi vya michezo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiongoza mazoezi kwa watumishi wa wizara yake akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiongoza mazoezi kwa watumishi wa wizara yake akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiongoza mazoezi kwa watumishi wa wizara yake akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa wizara yake.

GREAT HOPE FOUNDATION YAZINDUA TUZO ZA UWEZO KWA SHULE 100 NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Great Hope Foundation, Noelle Mahuvi akizungumza wakati wa Sherehe ya uzinduzi wa tuzo za uwezo kwa shule za Sekondari zilizopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro ,ambapo wanafunzi wanaweza kuwasilisha mawazo yao na kuwezeshwa na taasisi hiyo.
 Sehemu ya Wajumbe wa Meza kuu ambao walifika katika Uzinduzi huo wakishuhudia moja ya mawasilisho ya Wanafunzi kupitia Sanaa.
 Mmoja ya Majaji wa Tuzo za Uwezo , Hyasinta Ntuyeko akieleza vigezo vitakavyowafanya wanafunzi wa shule mbalimbali watakavyoweza kushinda pindi watakapowasilisha kazi zao katika shindano hilo, ambapo mwaka jana shule ya Mugabe iliibuka kidedea .
 Muwezeshaji , Samweli Ndandala akitoa somo namna ya kufikiri sana ili kushinda katika shindano hilo, ambalo linajumuisha shule zaidi ya 100 za Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Sehemu ya Wanafunzi walioshiriki katika uzinduzi wa tuzo za uwezo kwa shule za Sekondari zilizopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.

EFM REDIO YAWAWEZESHA KINAMAMA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

$
0
0
Efm redio katika kuadhimisha siku ya wanawake ambayo huadhimishwa duniani kote tarehe 8 machi kila mwaka, imetimiza jukumu iliyojipatia kuwasaidia wanawake wanaolea watoto wao wenyewe “single mothers” bila msaada wa wazazi wenza kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali kama mtaji katika kuendeleza biashara zao ndogondogo.
Kampeni hii iliobeba kauli mbiu ya “hatupoi” ilianza mwezi wa pili katika siku ya wapendanao, ambapo Jumla ya wanawake 19 wamefanikiwa kuwezeshwa.
Vilevile Efm redio imetoa hamasa kwa jamii hususani wanawake kuto chagua kazi ili kuleta usawa wa kazi katika jamii kwa kuwatambua na kuwakabidhi wanawake baadhi hati maalum ya utambuzi kama “wanawake wa shoka”. kwa uthubutu wao wa kufanya kazi ambazo wanawake wengi wamekua wakiziogopa kutokana na ugumu wake na imani iliyoko ndani ya jamii kuwa kazi hizo hufanywa na wanaume pekee.
 Kulia ni Meneja matukio wa efm redio Jesca Mwanyika akikabidhi vifaa vya biashara ya juisi ikiwa ni friji na Brenda kwa bi. Siwatu Mathew
  Mmoja wa single mother akikabidhiwa pesa taslimu kiasi cha shilingi 250,000/= na Afisa habari wa Efm radio Tuyu Mwaleni
 Fundi selemala Bi. Evodia Eliya akipokea cheti cha utambuzi kama “mwanamke wa shoka” kwa uthubutu wake katika kazi
 Mjasiliamali wa kuuza mbogamboga akikabidhiwa Kiasi cha shilingi  250,000/= katika kukuza mtaji wake wa biashara.
 Mjasiliamali wa biashara ya chakula cha kuku (kulia) akikabidhiwa na Afisa habari Efm redio Eunice Yona Mzani na mifuko miwili ya chakula cha kuku katika kuelendeleza mtaji wake.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images