Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

HOTUBA YA WAZIRI UMMY SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI RUKWA


MAYANGA AITA 23 TAIFA STARS KUWAKABILI ALGERIA NA DR CONGO

0
0
Kikosi cha wachezaji 23 wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kitakachocheza michezo miwili ya kirafiki kwenye tarehe za kalenda ya FIFA dhidi ya Algeria na DR Congo kimetajwa leo Alhamis Machi 8, 2018.

Kikosi hicho kitaingia kambini Machi 18, 2018 kwenye hotel ya SeaScape na kuondoka Machi 19, 2018 kuelekea Algeria kwa mchezo utakaochezwa Machi 22, 2018 kitarudi Tanzania Machi 24, 2018 kujiandaa na mchezo wa pili utakaochezwa Uwanja wa Taifa Machi 27, 2018 na DR Congo.

Kikosi kilichoitwa: 
WALINDA MLANGO.
  1.Aishi Manula  (Simba),   2.Ramadhani Kabwili  (Young Africans)
  3.Abdulrahman Mohamed (JKU)
  
WALINZI WA PEMBENI.
  4.Shomari Kapombe (Simba),  5.Hasan Kesy (Young Africans)
  6.Gadiel Michael(Young Africans)
  
WALINZI WA KATI.
  7.Kelvin Yondan(Young Africans),   8.Abdi Banda (Baroka)
  9.Erasto Nyoni(Simba)

VIUNGO WA KATI .
  10.Hamisi Abdallah  (AFC Leopards),   11.Mudathir Yahaya (Singida United),   12.Said Ndemla  (Simba),   13.Faisal Salum (JKU),   14.Abdulazizi Makame (Taifa Jang’ombe)

VIUNGO WA PEMBENI.
  15.Farid Mussa ( Teneriffe),   16.Thomas Ulimwengu  (FK Sloboda Tuzla)
  17.Ibrahim Ajib  (Young Africans),   18.Shiza kichuya  (Simba),  19.Mohamed Issa  (Mtibwa)

WASHAMBULIAJI.
  20.Mbwana Samata (KRC Genk),   21.Saimon Msuva (El Jadida),   22.John Bocco  (Simba),   23.Zayd Yahaya (Azam FC)

BENCHI LA UFUNDI.
  1.Salum Mayanga,   2.Hemed Morocco,   3.Patrick Mwangata,   4.Dani Msangi,   5.Dr.Yomba,   6.Dr.Gilbart Kigadya na   7.Ally Ruvu

NGORONGORO HEROES YAINGIA KAMBINI

0
0
Kikosi cha timu ya Taifa chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wake wa raundi ya kwanza ya kuitafuta tiketi ya kucheza fainali za vijana za Africa dhidi ya Congo mchezo utakaochezwa Machi 31, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa.
Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Morocco ,mchezo utakaochezwa Machi 17, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 
Mchezo huo ni wa kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza fainali za Africa kwa Vijana dhidi ya DR Congo utakaochezswa Machi 31, 2018. 
Morocco wanatarajia kutua Tanzania Machi 14,2018 ikiwa na msafara wa watu 31 wanaojumuisha wachezaji 23 na viongozi 8 wa benchi la ufundi. 

Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni.
Kikosi kilichoingia kambini makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Machi 6, 2018 ni wachezaji 40 ambao watapunguzwa na kubaki wachezaji 30 baada ya kumalizika wiki ya kwanza ya mazoezi.

Kikosi kilichoingia kambini: 
1.Ramadhan Kabwili(Young Africans), 2.Abutwarib Mshedi(Mtibwa), 3.Johny Kwiyenda(Makongo), 4.Ally Salim (Simba)
5.Kibwana Ally Shomari(Mtibwa), 6.Ally Hussein Msengi(Mbao)
7.Enrick Vitalis Nkosi(African Lyon), 8.Dikson Job(Mtibwa)
9.Assad Juma(Singida United), 10.Said Mussa Bakary(Young Africans)
11.Ally Ng’anzi(Singida United), 12.Kelvin Nashin Naftal(JKT Tanzania)
13.Shaban Ada(Lipuli), 14.Issa makamba(Singida United)
15.Mohamed Rashid(Singida United), 16.Marko Gerald(JMK)
17.Syprian Mtesigwa(Dodoma FC), 18.Muhsin Makame(Njombe Mji)
19.Yohana Mkomola(Young Africans), 20.Ibrahim Abdallah (Miembeni City) na 21.Abdul Suleiman(Ndanda).
Wengine ni: 22.Nickson Kibabage(Njombe Mji) ,23.Mussa Najimu(Changanyikeni),24.Maziku Aman(Makongo), 25.Hamis Mustafa(Ndanda), 26.Samson Myati(Toto Africans)
27.Said Mohamed(Azam FC), 28.Ayoub Mohamed(Young Africans)
29.Mohamed Mussa(Azam FC), 30.Emanuel Myati(Tz Prisons)
31.Riffat Hamis(Mtibwa), 32.Oscar Masai(Azam FC)
33.Paul Peter(Azam FC), 34.Vitalis Mayanga(African Lyon) na35.Rajab Mohamed(Azam FC).
Wengine ni: 36.Pontia Ohonya, 37.Maka Anthony(Young Africans)
38.Israel Mwenda(Alliance), 39.Hance Msonga(Alliance) na 40. Moses Kitandu(Simba)

MAMA MWANAMEMA SHEIN AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZANZIBAR

0
0
Akizungumza katika maadhimisho ya ‘Siku ya Wanawake Duniani’ yaliyofanyika leo Machi 8, 2018 katika kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, amesema wanawake ni nguzo muhimu ya kuinua familia  na wana mchango mkubwa katika kutekeleza majukumu ili kuziimarisha familia zao.
Mama Shein amesema akinamama wana mchango mkubwa katika kuimarisha familia ili zipate ustawi na kuzifanya zipige hatua zaidi ya maendeleo nchini, na kwamba wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa kila kunapotokea matatizo nchini yenye mwelekeo wa kupoteza amani.
Kwa hivyo amesisitiza haja ya kuendeleza ushirikiano katika kuendeleza amani na mshikamano ili kuhakikisha wanawake na watoto wanakuwa salama na kuishi bila khofu. Aidha, Mama Shein aliwataka akinamama na akinababa kushirikiana katika malezi bora ya watoto kulingana na maadili, silka na utamaduni wa nchi ili wawe raia wema.
Kuhusu vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia vinavyoendelea kushamiri kwa kasi, Mama Mwanamwema alisema Zanzibar bila ya uovu huo unaoathiri maendeleo ya taifa inawezekana iwapo jamii itakuwa kitu kimoja kwa kushirikiana kuvikomesha
Sambamba na hayo, alisema katika kupinga mapambano dhidi ya maradhi ya ukimwi, wanawake wana mchango mkubwa wa kudhibiti maambukizo ya virusi ifikapo mwaka 2030.
Lakini alieleza kusikitishwa kwake na kiwango kikubwa cha wanawake wanaoambukizwa maradhi hayo ambako kiko juu kuliko kwa wanaume.
“Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini ni mara mbili ya wanaume, hivyo tuchukuwe hatua madhubuti za kujiepusha na vitendo vinavyochangia kupata maradhi hayo,” alisisitiza.
Aidha aliwataka wanawake kuzitumia fursa za kujiunga na vikundi vya ushirika ili kujiimarisha kiuchumi kwa kujiongezea kipato na kupambana na umasikini, hali itakayoipa nguvu Serikali na washirika wengine kutanua wigo wa misaada yao.
 WAZIRI wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe. Maudline Cyrus Castico, akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliofanyika katika viwanja vya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla ya maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani,huadhimishwa kila mwaka ifikapo March 8, maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.( Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar)

TANZASEATTLE COMMUNITY PRESENTS MUUNGANO DAY/DICOTA KICKOFF IN SEATTLE

DC WA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AAHIDI NEEMA KWA KINAMAMA WILAYANI HUMO

0
0
MKUU wa Wilaya ya Kibaha Bi Assumpter Mshama amewaahidi kina mama wajasiriamali wa Wilaya ya Kibaha kuwa atazungumza na uongozi wa Halmashauri ya Mji  ili itengwe  siku na eneo maalum  kwa ajili ya kufanya maonyesho  ya bidhaa wanazozitengeneza ikiwa ni katika kupambana na  changamoto ya ukosefu wa masoko ya kuuzia bidhaa hizo.
Mshama amesema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake  duniani  Kibaha Mkoa wa Pwani, amewataka wanawake kujiamini, kushikamana  na kuachana na dhana potofu ya kupigana vita katika maeneo mbalimbali kwani adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe.
Aidha amesema  kutokana na wanawake wengi  kutofahamu  sheria za ndoa na mirathi , talaka  na sheria ya ardhi  ya mwaka 1999, Halmashauri ya Kibaha  itaendelea kutoka elimu  ya sheria kwa kupitia wadau wa masuala  ya sheria.
Amewataka wanawake wote nchini kuitafakari siku hii maalum  kwa kutafakari mafanikio na changamoto na kuweka  utatuzi wa changamoto wanazokabiliana  nazo wanawake huku  kauli mbiu  ikisema  kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe uswa wa jinsia  na uwezeshaji wanawake vijijini kauli mbiu hii inahamasisha  jamii kuongeza fursa za kiuchumi  kwa wanawake  ili kuwajengea uwezo  katika nyanja zote  za maendeleo, kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kitaaluma.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 08.03.2018

KUWAIT YAZINDUA KISIMA CHA 61 KATIKA WILAYA YA KIGAMBONI

0
0


Na Zaynab Nyamka, Globu ya Jamii
Balozi wa Kuwait nchini  Mhe. Jasem Al-Najema amezindua kisima cha 61 katika Shule ya Msingi ya GEZAULOLE Wilayani Kigamboni, Dar es salaam ikiwa ni mwendelezo wa utekelezezaji wa mradi wa '' KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE'' ulioanzishwa na Ubalozi wa Kuwait mwishoni mwa mwaka 2016.
 Hafla ya uzinduzi wa kisima hicho ilihudhuriwa pia na Diwani wa Sumangila Francis M. Chichi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Maziku Luhemega, Mwenyekiti wa CCM Gezaulole Masiku Lupa, Mwalimu Mkuu Maryam Shaaban pamoja wa walimu na wanafunzi wa Shule hiyo.

Kisima hicho kilichozinduliwa na balozi wa Kuwait Al-Najem kitanufaisha Shule ya Msingi ya GEZAULOLE iliyoanzishwa mwaka 1962 yenye wanafunzi 868 na madarasa kumi na Shule jirani ya Sekondari ya Ibnu Rushdy yenye wanafunzi 250 ilianzishwa mwaka 2007.

Balozi Al-Najem katika hotuba yake baada ya uzinduzi wa kisima amesema kuwa Ubalozi wa nchi yake umeanzisha mradi wa ''KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE'' ili kuitikia wito na kuunga mkono sera ya Rais wa Tanzania Mhe. John Magufuli  ya kutoa elimu bure. 

Al-Najem ameeleza kuwa atashirikiana na viongozi wa eneo hilo katika kutatua changamoto zinazokabili shule hiyo.

Aidha aliahidi kuwapatia wanafunzi wa Shule hiyo madaftari, mikoba na geloni za kuhifadhia maji kwa kila darasa ili wanafunzi wasihangaike kuchukua maji katika kisima mara kwa mara huku akiwataka wanafunzi hao kujihimu katika masomo yao ili wawe madaktari, wahandishi, walimu na watu wa fani mbalimbali baada ya kumaliza masomo yao hapo baadae.

Kwa upande wake Diwani wa Sumangila Francis M. Chichi ameishukuru Kuwait kwa kuchimba kisima cha maji katika Shule hiyo huku akimuomba Balozi Al-Najem kuisaidia Kata yake gari ya kubebea wagonjwa ili kuwaokoa akina mama wajawazito  na watu wazima ambao hulazimika kutembea masafa marefu kufika hospitilini na katika vituo vya afya ambapo baadhi ya wakati hulazimika kukodi pikipiki ili kufika huko jambo ambalo linahatarisha uhai wao.
Wanafunzi wakibeba galoni za maji zilizotolewa msaada na Ubalozi wa Kuwait nchini  wakiwa na Balozi wa Kuwait nchini  Mhe. Jasem Al-Najema ambaye amezindua kisima hicho cha 61 katika Shule ya Msingi ya GEZAULOLE Wilayani Kigamboni, Dar es salaam
Balozi Al-Najem ahutubia hadhira baada ya uzinduzi wa kisima kulia kwake ni Diwani wa Sumangila Fransis Chichi na kushoto kwake ni mwalimu mkuu Maryam Shaban.
Balozi Al-Najem akiwa na mwalimu Mkuu Maryam Shaban (aliyevaa nguo nyekundu) na Sheikh Kaporo msimamizi wa ujenzi wa kisima (alievaa kanzu na kofia) azindua rasmi kisima cha maji katika Shule ya Gezaulole
Balozi akikagua moja ya madarasa ya shule ya Gezaulole akifuatana na viongozi wa serikali ya Mtaa na walimu ambao wamemfafanua hali halisi ya Shule na changamoto zinazoikabili
Balozi Al-Najem akiwa amekaa na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Gezaulole ambapo amewaahidi kuwapatia madaftari na mikoba.

UWT KINONDONI YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTOA MSAADA MWANANYAMALA HOSPITALI

0
0
 Mjumbe wa halmashauri kuu (MNEC UWT), Halima Okashi akitoa zawadi kwa Mmoja ya Wanawake waliolazw aktika wodi ya wamama katika Hospitali ya Mwananyamala ambapo UWT Kinondoni walifika katika Hospitali hiyo kutoa Msaada katika kuadhimisha  siku ya Wanawake Dunia
 Katibu wa UWT CCM Wilaya ya Kinondoni, Nuru Mwaibako, akiwa na Diwani Viti maalum CCM  Kinondoni  Frolenece Masunga wakikabidhi zawadi kwa Wanawake waliofka katika Clinic ya Hospitali ya Mwananyamala na watoto wao, UWT Kinondoni wamefanya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea wamama waliopo katika Hospitali ya Mwananyamala.
Diwani Viti maalum CCM  Kinondoni  Frolenece Masunga akiwa amemshika mmoja ya Watoto waliofika kutibiwa katika Hospitali ya Mwananyamala leo wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.
Ujumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni kwa Pamoja wakimkabidhi zawadi Mganga wa Hospitlai hiyo kwa ajili ya Wanawake wa Hospitali hiyo.
Ujumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, ukiwasili katika Hospitali ya Mwananyamala ukiongozwa na Mjumbe wa halmashauri kuu (MNEC UWT), Halima Okashi

HDIF YAWAWEZESHA WANAWAKE TANZANIA KATIKA NYANJA YA UBUNIFU

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema inaendelea na utaratibu wa ukarabati wa shule kongwe nchini ikiwemo za sekondari na ufundi ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza masuala mbalimbali ya ubunifu kwa kutumia sayansi na teknolojia ya kisasa kulingana na mazingira yanavyobadilika .
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia elimu msingi, Dk.Avemaria Semakafu wakati alipokuwa akizungumzia kongamano la Siku ya Wanawake lililoandaliwa na Mfuko wa  Ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF).
Dk.Semakafu amesema ni vyema wakajirudisha kwenye mazingira yetu ya kitanzania kwa kuwafanya wasichana kuwa wabunifu kuanzia ngazi ya familia na shuleni ili kupata wasichana viongozi.
Amefafanua Shule za Sekondari Ifunda, Tanga, Mtwara na Moshi ambazo tangu awali zilikuwa zikitoa mafunzo ya ufundi, zinaendelea na ukarabati na wanatarajia mwaka wa masomo 2018,19 kuanza kidato cha kwanza.
 Naibu Kiongozi  Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF), Joseph Manirakiza akizungumza juu ya  kongamano hilo ili kutoa fursa kwa watu kujifunza namna wanawake wamefanikiwa katika masuala ya ubunifu na kuleta maendeleo katika jamii inayoiwazunguka.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia elimu msingi, Dk Avemaria Semakafu  akizungumza katika kongamano la Siku ya Wanawake lililoandaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)

 Mmoja wa watu waliokuwa katika uchangiaji mada aliekuwa mrembo wa Miss Tanzania na kutwa taji la urembo wa Afrika Nancy Sumari akizungumza jambo wakati wa kongamano la Wanawake lililoandaliwa na mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)
 Wadau mbalimbali waliofika katika Kongamano la Wanawake lililoandaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)
 Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka shirika la Dot Tanzania, Ndimbuni Msongole akizungumza jambo juu ya ubunifu kaytika nyanja ya mawasiliano wakati wa Kongamano la Wanawake na ubunifu lililoandaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF). Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

MAKILAGI , MANYANYA WAWAFUNDA WANAWAKE WA DAR ES SALAAM UMUHIMU WA UJASILIMALI KATIKA UCHUMI WA VIWANDA

0
0
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa(UWT), Amina Makilagi akizungumza wakati wa Warsha ya Wanawake Wajasiliamali iliyoandaliwa na Uhuru Fm katika mahadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani
 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Warsha ya Ujasiliamali iliyoandaliwa na kituo cha Radio cha Uhuru Fm.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Radio cha Uhuru Fm, Angel Akilimali akizungumza kuwakaribisha  wanawake wajasiliamali kwenye warsha maalum iliyandaliwa kwa ajili yao
 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akikabidhi Cherehani kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Radio cha Uhuru Fm, Angel Akilimali kwa ajili ya Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Warsha ya Ujasiliamali iliyoandaliwa na kituo cha Radio cha Uhuru Fm.
 Mtangazaji wa kipindi Wanawake na ujasilimali cha Uhuru Fm akizungumza na Wanawake waliofika katika Warsha hiyo kujifunza mbinu mbalimbali.
 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya  na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa(UWT), Amina Makilagi  wakikagua bidhaa za Wajasiliamali waliofika katika Warsha iliyoandaliwa na Uhuru Fm.
 Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Warsha ya Ujasiliamali iliyoandaliwa na kituo cha Radio cha Uhuru Fm.

MAGAZETI YA IJUMAA LEO MARCH 9,2018

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ILIVYOADHIMISHWA MKOANI TABORA

0
0
Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete akimpongeza Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Tabora Munde Tambwe baada ya kupokea kiasi cha shilingi milioni moja kwaajili ya TIKA huku Mbunge huyo Munde Tambwe akiahidi mbele Mama Salma Kikwete kuchangia jumla ya mifuko Miambili ya Saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Mabweni katika Shule za Sekondari za kata manispaa ya Tabora na ujenzi wa uzio Kliniki ya Tabora mjini maarufu Town Clinic. 
Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete akizungumza katika maadhimisho hayo ambapo alisema kuna haja ya kuleta mabadiliko ya kisekta yatakayoharakisha maendeleo kwa Wanawake kupitia kujenga misingi imara ya kupata elimu bora itakayotoa fursa kwa Wanawake kuajiriwa na hata kujiajiri wenyewe. 
Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Tabora Munde Tambwe akizungumza katika Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake zilizofanyika kimkoa mkoani Tabora,katika maadhimisho hayo Munde aliwalipia Kadi za matibabu maarufu TIKA Wanawake wasio na uwezo Miamoja wanaoishi manispaa ya Tabora akiwa anakamilisha idadi kama hiyo kwa Wanawake wengine mia moja kwa kila Wilaya za mkoa wa Tabora ambazo ni wilaya saba. 
Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani mkoani Tabora ambapo Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi iliyofanyika viwanja vya Chipukizi mjini Tabora. 
Gwiji na Msanii mkongwe wa muziki wa Taarabu nchini Malkia Khadija Kopa akitumbuiza katika maadhimisho hayo mjini Tabora katika viwanja vya Chipukizi. 

NAIBU WAZIRI WA MAJI AMCHUKULIA HATUA MHANDISI ULANGA

0
0

 Naibu Waziri wa Majina Umwagiliaji, Jumaa Aweso akishuka mara baada ya kukagua tenki la mradi wa maji wa Gombe, wilayani Ulanga, mkoaniMorogoro.
   NaibuWaziriwaMajinaUmwagiliaji, JumaaAweso (kushoto)naMbungewaJimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga wa kiwa kwenye moja ya kichoteo cha maji cha mradi wa maji wa Gombe ambacho hakitoimaji.


  Naibu Waziri wa Majina Umwagiliaji, Jumaa  Aweso akiwa amebeba ndoo ya maji akiipeleka kwenye nyumba iliyopo katika Kijiji cha mara baada ya kuzindua mradi huo wavisima 27.
Naibu Waziri wa Majina Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Jumuiya yaWatumiaji Maji katika Kata yaLupiro, Wilaya ya Mahenge, mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amechukua hatua za kinidhamu kwa Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Interconsult kutokana na kutoridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji wa Gombe uliopo Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro.

Naibu Waziri ameagiza vyombo vya usalama kumkamata na kufanya uchunguzi kwenye mradi huo wa Gombe ambao umechelewa kukamilika licha ya asilimia kubwa ya fedha kuwa zimeshalipwa kwa mkandarasi, lakini pia unakosa thamani halisi ya fedha zilizotumika katika ujenzi wake.

Aweso alitoa maagizo hayo wakati alipokuwa ziarani katika Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro mara baada ya kupata taarifa ya kusuasua kwa mradi huo na wananchi wa Gombe kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu.

‘‘Katika taarifa nimeambiwa kuwa mradi unatoa maji, lakini nimekuja kuona na si kweli wakati wizara imetoa fedha. 

Kama Naibu Waziri wa Maji sitakubali kusikia fedha za miradi ya maji zinaliwa kila ninapoenda, naagiza Mhandisi Mshauri akamatwe na uchunguzi ufanyike na endapo itabainika amehujumu achukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wahandisi wote nchini’’, alisema Aweso. 

Amesema kuwa wizara itaandaa orodha ya majina ya wakandarasi wote waliohujumu miradi ya maji na kuikabidhi kwa Bodi ya Usajili ya Wakandarasi ili wafutiwe kabisa usajili na kutopewa kazi yoyote tena nchini endapo watathibitika kufanya hivyo.

Akiwa Ulanga Naibu Waziri Aweso amezindua ofisi ya maji ya Kata ya Lupiro, mradi wa maji wa visima 27 katika Kijiji cha Chikuti, ambacho ni moja ya vijiji vinavyonufaika na mradi huo na kukagua skimu ya umwagilaji ya Mnepa, iliyopo Kata ya Lupiro. 

MBUNGE WA TUNDURU KUSINI AKABIDHI PIKIPIKI 15 KWA MAKATIBU KATA.

0
0
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Daimu Mpakate amekabidhi pikipiki 15 zenye thamani ya shilingi milioni 23 kwa makatibu kata 15 wa chama hicho cha Mapinduzi kwa ajili ya shughuli za kichama na serikali katika jimbo hilo. 


WANAWAKE MSD WATOA MSAADA HOSPITALI YA TEMEKE NA MAKAO YA WATOTO YATIMA KURASINI DAR

0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela, akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima,  Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack)
  Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela, akimkabidhi msaada wa vyakula na vitu vingine Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa MSD, Neema Mosha.
Picha ya pamoja.
WANAWAKE Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani wametoa msaada wa vifaa vya kujifungulia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke pamoja na chakula kwa watoto wanaolelewa Makao ya Taifa Kurasini ya Watoto Yatima na Wenye Shida jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD,  Neema Mwela alisema kwao ni faraja kubwa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea wanawake wenzao katika hospitali hiyo pamoja na watoto hao.

"Sisi wanawake wa MSD tuliona ni vizuri tukasherehekea siku yetu pamoja na wakina mama waliopo katika hospitali hii pamoja na watoto wanaolelewa katika makao ya taifa ya Kurasini kwa ajili kula nao chakula cha mchana pamoja na kuwapa msaada wa chakula na vitu mbalimbali" alisema Mwela.

Mwela alisema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke waliweza kutoa Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) ambao umepunguzwa bei kutoka shilingi 40,000 mpaka shilinhi 21,000 na vifaa vingine vinavyohitajika kama sabuni na miswaki.

Akizungumzia watoto Yatima na wenye shida wanaolelewa katika makao ya Kurasini alisema ni jukumu la kila mmoja wetu kuwasaidia watoto hao badala ya kuiachia serikali pekee.

Alisema kazi ya malezi ya watoto hao ni kubwa mno hivyo kila mtu anapaswa kuwa na majukumu ya kuwalea kwani kumlea mtoto tangu akiwa mdogo hadi kufikia miaka 18 ni kazi kubwa.

Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange alisema katika makao hayo kuna watoto wanaosoma shule mbalimbali za msingi, sekondari na shule za awali na kuwa kama kuna mtu anayehitaji kumchukua mtoto wa kwenda kuishi naye taratibu zote zinaanzia ofisi za ustawi wa jamii zilizopo kwenye manispaa husika.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa MSD, Neema Mosha alisema waliguswa sherehe za siku ya wanawake duniani mwaka huu kuwatembelea wanawake wenzao waliopo wodi ya wazazi kwa ajili ya kujifungua pamoja na kula chakula na watoto Yatima na wale wenye shida waliopo Kurasini na kuwapa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vya matumizi ya shule.

Alisema fedha za kununulia mahitaji hayo zilichangwa na wao pamoja na wafanyakazi wanaume wa MSD na kuwa thamani ya fedha kwa ajili ya kununulia vitu hivyo ilikuwa ni shilingi milioni 3.5 wakati vifaa vya hospitalini viligharimu shilingi milioni 7.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima alishukuru kwa msaada huo nakuleza kuwa changamoto kubwa walionayo ni majengo ya hospitali hiyo kuwa machache kutokana na ongezeko la wagonjwa na uboreshaji wa miundombinu.

DC MSHAMA AWAASA WANAWAKE KUACHA KURUDISHANA NYUMA KIMAENDELEO NA FITNA

0
0
Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama.

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha.
MKUU wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,amewaasa wanawake kuacha tabia ya kurudishana nyuma kwenye maendeleo,fitna na kuwabeza wengine ambao wanakuwa na uwezo kiuchumi na uongozi .

Aidha amewataka wale wenye uwezo wa raslimali fedha kuthubutu kuanzisha viwanda vya kati na vikubwa ili kuikomboa jamii katika eneo la ajira.

Mshama amewasihi pia wanawake kuiunga mkono serikali ikiwa ni pamoja na kuisemea mazuri inayoyafanya ikiwemo kusimamia mafungu ya kuwezeshwa wanawake kupitia halmashauri nchini.

Mshama aliyasema hayo,Mwendapole katika maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyoadhimishwa na halmashauri ya Mji wa Kibaha.

Aliwaomba akinamama hao waungane mkono kwenye kila jambo ili kujiinua kimaisha.

"Unakuta tunabezana wenyewe ,mtu anauwezo mkubwa wa kufanya biashara ,anaongoza nyadhifa fulani lakini tunafanyiana fitna ,majungu na kukatishana tamaa" alisema Mshama.

Hata hivyo ,alielezea serikali ya awamu ya tano inaendelea kusimamia fedha zinazopaswa kuwezeshwa wanawake kwa asilimia nne ,vijana nne na wazee na walemavu asilimia mbili .

"Mjaribu kuwaelimisha wachache wasiotambua kazi kubwa inayofanywa na viongozi wetu waliopo madarakani " alisema Mshama.

Kuhusiana na changamoto wanayokabiliana nayo kundi hilo ikiwemo kukosa maeneo ya kuweka bidhaa na uhakika wa masoko,Mshama alisema atawasiliana na uongozi wa halmashauri ili iweze kutenga siku ya kuonyesha maonyesho ya bidhaa zao .

"Mfano kila mwisho wa mwezi tunapanga tupange biashara zetu pale Mailmoja ,lazima wateja watakuja kutoka ndani ya wilaya ,mkoa na nje ya Mkoa ,hii itaongeza tija kubwa kwenu"

"Sasa mnatakiwa mboreshe bidhaa zenu kwani kwenye ushindani wa soko ,kizuri chajiuza kibaya chajitembeza ," alibainisha Mshama.

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leah Lwanji alisema idara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wajasiriamali 751 ambapo kati yao Wanawake ni 480 .#

"Huduma ya usajili wa biashara ilitolewa na Brela kwa washiriki 24,"; Pia kongano za biashara zimeundwa kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali kufanya kazi zinazofanana na kupata fursa ya kueleza changamoto zao kama kongano" alisema Leah.

Leah alieleza mwaka 2016-2017 halmashauri ilitoa fedha kiasi cha sh.mil .173 kwa ajili ya mikopo kwa Wanawake na vijana  ,2017-2018 ilitoa mil.368 na July -Sept 2017 walitoa mil.100 kwa vikundi 50 vyenye wanachama 320.

Kwa upande wake ,diwani wa viti maalum Mji wa Kibaha ambae pia ni katibu wa jukwaa la uwezeshaji mkoani Pwani,Elina Mgonja alisisitiza umoja kwa akinamama utakaowezesha kuwa na sauti moja kupigania fursa za ujasiriamali .

Elina alieleza ,wamejipanga kuthubutu kuanzisha miradi mikubwa na kuboresha bidhaaa kwa kushikana mikono ili kujikwamua kiuchumi .

Airtel yashirikiana na Polisi kikosi cha usalama barabarani katika ukaguzi ya magari.

0
0
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeendeleza juhudi zake za kushirikiana na jeshi la Polisi Tanzania ambapo kwa sasa wameshirikiana na polisi kikosi cha barabarani kuitikia wito uliotolewa na Mkuu wa Kikosi cha Polisi Trafiki kuhahakisha kuwa magari yote yanakanguliwa na kuwekewa stika za usalama barabarani.

Kwenye zoezi hilo ambalo limefanyika kwenye makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, maofisa wa kukangua magari kutoka Kikosi cha barabarani walishirikiana na Kampuni ya Airtel kwenye kukagua magari ya kampuni hiyo pamoja na ya wafanyakazi.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Afisa Uhusiano na Matukio Airtel Tanzania Dagio Kaniki alisema kuwa usalama wa barabarani ni la kila mtu na ndio sababu kampuni ya Airtel imeendeleza ushirikiano wake na Polisi Kikosi cha barabarani kwenye kutimiza wito wa Kamishna wa Trafiki Tanzania la kuhakikisha kila chombo cha moto yakiwemo magari ya biashara, magari binafsi, bajaj pamoja na pikipiki zinakanguliwa na kubandikwa stika za usalama barabarani.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukishirikiana na Polisi kikosi cha barabarani kwenye matukio mengi. Ushirikiano huu umekuwa ni muhimu ili kupunguza ajali. Usalama wa barabarani ni jukumu la kila mtu na ndio sababu Airtel imekuwa mbele kuhakikisha hilo linafanyika, alisema Dagio.

Leo wakaguzi wa magari wameshiriki pamoja na wafanyakazi kukangua magari yao. Natoa shukrani kwa jeshi la polisi kitengo cha trafiki kwani kufika kwao hapa kumeweza kuokoa muda wa wafanyakazi wetu kwenda kufanya ukaguzi. Sisi Airtel tutaendelea kushirikiana na Polisi kuhakikisha elimu ya usalama barabarani linafikia kila mlengwa, aliongeza Dagio.

Dagio alitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa Airtel ya kuitikia wito wa ukaguzi wa magari ili kutimiza wajibu wa kila mtu. ‘Natoa rai pia kwa kile dereva ambaye kwa namna moja au nyingine anakuwa anaandikiwa faini za barabarani. Airtel Money ni suluhisho kwani ni rahisi kutumia kwa ajili ya kulipia gharama hizo.

TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MAJI ZATANGAZWA TENA.

0
0
Shirika lisilo la kiserikali la Shahidi wa Maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini na ne ya Tanzania kupitia programu yake ya Uhakika wa Maji, imetangaza kuongezwa muda wa uwasilishwaji wa machapisho na programu za redio na runinga kutoka kwa waandishi na vyombo vya habari ili kuwania tuzo za uandishi wa habari za maji.

Tuzo hizi, zilizinduliwa  na Shahidi wa Maji pamoja na washirika wake kwa mara ya kwanza mwezi Juni mwaka 2017, na kupewa jina la ‘Tuzo za Habari za Maji. Ili kushiriki katika tuzo hizi, waandishi watapaswa kuwasilisha kazi zao walizochapisha au walizorusha katika vyombo mbalimbali vya habari zinazohusu masuala mtambuka ya maji kama vile; usimamizi na utawala wa rasilimali maji, ukame, mafuriko, usambazaji maji, uchafuzi wa mito na vyanzo vya maji na kadhalika.
Vyombo vya habari pamoja na waandishi watakaoshinda tuzo hizi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, vifaa vya kuboresha ufanisi wa kazi kama vile kamera na kompyuta mpakato, kombe la tuzo pamoja na vyeti vya ushiriki, hii ikiwa na lengo la kuboresha uwajibikaji miongoni wa wadau wa sekta ya habari katika kuchapa na kusambaza habari zihusuzo maji ili kuleta mabadiliko chanya, endelevu na ya kudumu katika sekta ya maji na kuleta hali ya usalama na uhakika wa maji kwa watanzania wote.

Pia, makala/kazi a za washindi   zitapata fursa ya kurushwa kwenyetovuti zetu na kusambazwa katika vyomba mbalimbali vya habari na mitandao ya kimataifa kama vile: BBC, UK Guardian, Circle of Blue and Ooska News ambayo ni nafasi na fursa ya kipekee kwa waandishi na vyombo vya habari kusomwa zaidi na kutambuliwa kwa mchango wao katika kusaidia kuboresha sekta ya maji nchini.
Tuzo hizi zimeandaliwa mahsusi kwa waandishi na vyombo vya habari ambavyo vinatoa taarifa za masuala ya maji, kuchochea mabadiliko chanya katika uwajibikaji wa wadau wa sekta ya maji.  Shahidi wa Maji na washirika wake imejikita katika kufanya kazi kubadilisha namna ambavyo rasilimali maji inasimamiwa kwa manufaa ya wananchi wote, mazingira na uchumi wa nchi. Aidha, ili kufanikisha hayo shirika hilo na washirika wake wanafanya kazi kwa namna mbalimbali kama vile; Kusaidia jamii zenye uhitaji kuweza kutambua haki na wajibu walionao katika kuwezesha utekelezaji wa sheria zilizopo na kuwezesha jamii kufuatilia utatuzi wa matatizo ya usalama wa maji katika maeneo yao kwa watoa huduma ikiwemo serikali na sekta binafsi.
Mwisho wa uwasilishaji wa kazi za waandishi na vyombo vya habari umetajwa kuwa tarehe 31 mwezi Mei mwaka 2018.

NMB WATOA MSAADA WA VIFAA HOSPITAL YA WILAYA NAMTUMBO.

0
0
Bank ya NMB tawi la Namtumbo Mkoni Ruvuma imetoa msaada wa vifaa vya hospital ambavyo ni vitanda vya kujifungulia akina mama, vitanda vya kawaida, mashine za shinikizo ya damu na mashuka. Kaimu Meneja bank ya NMB kanda ya kusini Janeth Shango amesema huo ni mpango waliojiwekea NMB ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia sekta mbali mbali hapa
 nchini.


Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images