Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

HUDUMA YA TAXIFY BAJAJI YAWA NAFUU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Taxify imetangaza punguzo la asilimia 50 kwa bei ya bajaji zake jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuwavutia watumiaji wa huduma hiyo na kuwapa nafasi ya kutumia huduma zake.

Kampuni hiyo inayokuwa kwa kasi barani Ulaya na Afrika kupitia huduma zake mbalimbali za usafirishaji kwa kutumia teknolojia, imetangaza punguzo la asilimia 50 kuanzia Februari 28 kwa watumiaji wa Application yake ya ‘Taxify Bajaji’ ambapo wateja watalipa Shilingi 150 kwa kilometa na Shilingi 50 kwa dakika huku nauli ya kuanzia safari ikiwa Shilingi 300 kuanzia Jumatano Februari 28. Gharama ya nauli ya chini kabisa ikiwa Shilingi 1,000.

Wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya ya Usafir wa Bajaji kwa kutumia teknolojia wiki mbili zilizopita Taxify ilikuwa ikitoza malipo ya Shilingi 350 kwa kilomita, Shilingi 75 kwa kila dakika inayotumiwa katika safari, pamoja nauli ya chini ya shilingi 750.

"Punguzo la asilimia 50 kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam hususani kwa wale wote wanaopenda kutumia usafiri huu kwa safari fupi mjini ni hatua kubwa," alisema Remmy Eseka, Meneja Uendeshaji Taxify Tanzania.

Eseka alifafanua jinsi ambavyo watumiaji wa huduma hiyo watakavyokuwa wakilipa nauli zao pindi wanapofanya safari zao katika baadhi ya maeneo maarufu jijini Dar es Salaam baada ya kutolewa kwa ofa ya punguzo la asilimia 50. "Huduma mpya ya Taxify Bajaji itatoza Shilingi 1,400 tu kutoka Makumbusho kwenda Sinza, Shilingi 1,800 kutoka Ubungo kwenda Mwenge na Shilingi 2,500 kutoka Tangi Bovu kwenda Mlimani City" alisema Eseka.

Akijibu swali, kuhusu mabadiliko ya bei iwapo kama yatawaathiri madereva wa bajaji wanaofanya kazi hiyo jijini hapa. Eseka alisema, "Tutawafidia madereva kwa kuwapa bonasi ili kuhakikisha kipato chao kinabaki kuwa kizuri, hivyo hawataathirika na punguzo hili la bei."

Taxify imeendelea kuwa maarufu jijini Dar es Salaam ikiwa ni miezi mitatu tu sasa tangu kampuni hiyo tanzu ya Estonia izunduliwe jijini hapa, lakini hadi sasa imekwisha zindua huduma zake mbili jijini Dar es salaam ambazo zipo katika programu za usafiri za Kampuni hiyo, kitu ambacho ni kinawafanya waweze kuongoza katika ushindani na kuwa kampuni ya usafirishaji kwa mtandao inayopendwa katika soko na wateja wake. 

Pia bei za sasa za huduma ya Usafiri wa Taxi kupitia programu ya Taxify zina punguzo la asilimia 25, huku nauli kwa kilometa ikiwa ni Shilingi 560, Shilingi 110 kwa dakika na nauli ya kuanzia Safari ikiwa ni kiasi cha Shilingi 1,200 na bei ya chini ya Safari ikiwa ni Shilingi 3,000.

Watanzania wahimizwa kujiunga na mtandao wa mitaji

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora amewataka wafanyabiashara nchini kuhamasika kujiunga na mtandao wa mitaji ya ubia ili kuimarisha vitega uchumi vyao na pia kusaidia kuanzisha viwanda hapa nchini.

Profesa Kamuzora alisema hayo wakati akizindua Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network jijini Dar es salaam jana.Aidha Katibu Mkuu huyo amesema uzinduzi wa mtandao huo umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda,

Aliwataka wananchi kuacha uoga katika ushiriki wa kuwawezesha kuwepo kwa mitaji ya kutosha kwa ajili ya uimarishaji wa uwekezaji nchini Tanzania.Alisema serikali kwa sasa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazingira ya biashara na uwekezaji yanakuwa bora, ndio maana wameanzisha mchakato wa kutengeneza sera ya maendeleo ya viwanda hasa katika sekta binafsi.

Alisema ni vyema wenye viwanda na wananchi wengine kushiriki katika mchakato huo ili kufanikisha nia ya kuipeleka Tanzania katika nchi ya viwanda. Alisema kwa kuwa na sera sheria nyingi zitabadilika na hivyo kupunguza urasimu na pia vikwazo vya kuwezesha kazi katika masuala ya viwanda na biashara.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital ambapo amesema umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi akitoa neno la ufunguzi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora kutoa hotuba ya uzinduzi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi akibadilisha na mawazo na Afisa Mtendaji Mkuu wa DOB Equity, Brigit van Dijk-van de Reijt wakati wa hafla ya uzinduzi wa wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora (wa tatu kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) akifafanua jambo kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Wanaomsikiliza ni Muasisi wa Mtandao wa Tanzania Venture Capital, Bw. Salum Awadh (wa pili kushoto aliyesimama), Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kulia) pamoja Mkurugenzi wa Uwekezaji na Maendeleo ya Viwanda –TPSF, Edward Furaha (kulia).

DIWANI ACT WAZALENDO KATA YA GIHANDU,WILAYANI HANANG AJIUZULU,AJIUNGA CCM

$
0
0
Na Jumbe Ismailly -HANANG . 

ALIYEKUWA diwani wa kata ya Gihandu,wilayani Hanang,Mkoani Manyara kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo,Mathayo Samuhenda amejiuzulu udiwani wa kata hiyo na kujiunga na Chama Chama Mapinduzi (CCM)

Akitangaza azma yake hiyo ya kujiuzulu katika nafasi yake ya udiwani wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Gihandu,Samuhenda alisisitiza kwamba aliamua kujiuzulu na kuwaacha wapiga kura wake siyo kwa njia ya ukatili bali alifikia maamuzi hayo kwa lengo la kuwaunganisha wananchi wote wa kata hiyo.  

Aidha alifafanua kwamba katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa wananchi wa kata hiyo wana matatizo ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kutokana na wanasiasa kutumia mtaji huo kuomba kura.
“Inatosha wanasiasa sisi tutumie shida ya maji ili tuoate kura tuondoke,inatosha..na watu wa Gihandu nawaomba sana hiyo ikiletwa kama sehemu ya mnada mzuri tu wa mtu kujinadi mkataeni inatosha tumeumia vya kutosha.”alisisitiza Samuhenda. 

Hata hivyo diwani huyo aliyejiuzulu aliweka bayana kwamba umefika wakati sasa kwa wanasiasa kubadili ajenda za kupatia kura za Gihandu na isiwe upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwani hiyo sasa imekuwa ni kejeli

Akimpokea diwani huyo,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara,Simon Lulu alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoendeleza makundi licha ya kuwa hivi sasa siyo wakati wa kumpeni na badala yake aliwataka kuvunja makundi hayo na kusisitiza juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.
 Ni Mbunge wa Jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,DK.Mary Nagu (wa kwanza kutoka kushoto) akimpongeza aliyekuwa diwani wa Kata ya Gihandu,Mathayo Semuhenda mara baada ya kutangaza azma yake ya kujiunga na CCM.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara,Simon Lulu akipokea kadi ya Chama Cha ACT Wazalebdo kutoka kwa aliyekuwa diwani wa kata ya Gihandu,Mathayo Semuhenda.
 Aliyekuwa diwani wa kata ya Gihandu kwa tiketi ya ACT Wazalendo,MATHAYO SEMUHENDA akipokea kadi ya CCM baada ya kutangaza azma yake ya kujiunga na CCM.
 baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wa wilaya na Mkoa wa Manyara wakishiriki kikamilifu pamoja na wanachama wapya kula kiapo cha uadilifu baada ya kuwakabidhi kadi za chama wanachama wapya wa chama hicho.

BASF YAANZISHA KIWANDA CHA UZALISHAJI KEMIKALI ZA UJENZI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
-Uzalishaji utapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa usambazaji kwa wateja.
- Uzalishaji wa michanganyiko mbalimbali ya saruji utazingatia makubaliano ya ushuru.
- Kituo hicho kipya cha uzalishaji kitachochea huduma bora kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya BASF yenye ufumbuzi wa bidhaa bora.

Kampuni inayoongoza kwa utengenezaji wa kemikali duniani vilevile kemikali za ujenzi , imeanza kuwekeza madhubuti kwenye uzalishaji wa ndani na hivi leo imekabidhi kituo cha uzalishaji nchini Tanzania. Kiwanda hicho ambacho kitazalisha mchanganyiko wa saruji, kitatumika kupitia makubaliano maalum ya ushuru na kitatoa ufumbuzi wa kibunifu ili kuiwezesha BASF kukidhi mahitaji ya wateja.

Kutokana na kiwanda hicho kipya, kitengo cha kemikali na ujenzi BASF kitajiimarisha katika wigo wa kuwafikia wateja wake wengi zaidi na kukidhi mahitaji ya soko huku ikitoa ufumbuzi wa hali ya juu katika sekta ya ujenzi. "Uwekezaji huu ni hatua nyingine muhimu kwa BASF Afrika.

Ushiriki wetu katika bara la Afrika unaongezeka na jukumu kubwa muhimu linalotekelezwa na kitengo hichi ni kutazama zaidi kwenye nchi zenye mipango mizuri na fursa kubwa, kama vile Tanzania "alisema Michael Gotsche, ambaye ni Makamu wa Rais wa BASF Afrika.

Christian Geierhaas ambaye ni Makamu wa Rais wa kitengo cha kemikali za ujenzi Upande wa Mashariki ya Kati, Asia Magharibi, CIS & Afrika, alisema kuwa "Kuwekeza nchini Tanzania, kutaiwezesha kitengo hicho kuleta bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu na ufumbuzi zaidi kwa wateja wetu katika soko hili muhimu."

BITEKO AITAKA MIGODI KUBORESHA MAHUSIANO NA JAMII

$
0
0

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amezikumbusha Kampuni za Madini nchini kuhakikisha suala la mahusiano na jamii linapewa kipaumbele ili kuboresha utendaji wa shughuli zao.

Amesema hayo Machi 5, 2018 Mkoani Geita alipokutana na wawakilishi wa Kampuni ya OreCorp Tanzania Limited yenye Leseni ya Utafiti ambayo inatarajia kuanzisha shughuli za uchimbaji mkubwa wa dhahabu kwenye eneo la Nyanzaga, Wilayani Sengerema.

Katika mkutano huo uliofanyikia kwenye Ofisi za Madini, masuala mbalimbali ya shughuli za uchimbaji madini yalijadiliwa na msisitizo ukiwa kuhakikisha suala la uboreshaji wa mahusiano na jamii zinazozunguka miradi linapewa kipaumbele.

Biteko alisema uboreshaji wa mahusiano na jamii ni kwa faida ya kampuni kwani kufanya hivyo kutasaidia kuepuka migogoro isiyo ya lazima na hivyo kuboresha utendaji kazi na kuwa na uzalishaji wenye tija.

Aidha, awali kabla ya kukutana na kampuni hiyo, Biteko alikutana na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, Mhandisi Yahya Samamba na Afisa Madini Mkoa wa Geita, Mhandisi Ally Maganga.

Naibu Waziri Biteko atahitimisha ziara yake hapo baadaye leo hii Machi 6, 2018 kwa kutembelea machimbo ya dhahabu ya Nyang'wale na kuzungumza na wachimbaji kwenye machimbo hayo.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza wakati wa kikao na wawakilishi wa Kampuni ya OreCorp Tanzania Limited (hawapo pichani) walipokutana kwenye Ofisi za Afisa Madini Mkoa wa Geita.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (mbele katikati) akizungumza na wawakilishi wa Kampuni ya Ore Corp Tanzania Ltd.  
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akijadiliana jambo na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, Mhandisi Yahya Samamba (kulia). Kushoto ni Afisa Madini Mkoa wa Geita Mhandisi Ally Maganga.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akizungumza wakati wa kikao na Kampuni ya OreCorp (T) Ltd. Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, Mhandisi Yahya Samamba akifuatiwa na Makamu wa Rais Uwekezaji na Uendeshaji wa kampuni hiyo, Henk Diederichs.

MAMA WA MITINDO APEWA TUZO YA KUTAMBUA MCHANGO WAKE

$
0
0

Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii

ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo amepokea tuzo ya Lifetime achievement award kutoka kwa designers na models wa Tanzania.

Sherehe za kupewa tuzo hiyo zilifanyika Jumapili ya wiki iliyopita kwenye ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam ambapo tuzo hiyo pia amepewa kwa kutambua namna alivyokuwa mstari wa mbele kuandaa majukwaaa yanayotoa fursa wanamitindo kutangaza vipaji vyao.

Akizungumza baada ya kupewa tuzo hiyo ya kutambua mchango wake kwenye tasnia ya mitindo, Mama wa Mitindo pamoja na mambo mengine amewashukuru sana wanawe.

Amefafanua amewashukuru kwa sababu ya kumthamini na kuona kwamba alikuwa Mama asiechagua wa kumsaidia."Nitaendelea kuwa pamoja nanyi kwa kuhakikisha nawashauri hasa kuzingatia maadili mema katika mavazi na tasnia nzima,"amesema Mama wa Mitindo.

Wanamitindo na wabunifu wa mavazi waliondaa sherehe na tuzo hiyo wameongozwa na Martin Kadinda,Alabama King, Agusta Masaki, Nelson,Ommystlishy na Rukia Walele ambapo wamesema wamevutiwa na wataendelea kutambua mchango wa Mama Mitindo katika tasnia hiyo.
 ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo akiwa katika picha ya pamoha na designers na models wa Tanzania.
 ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo aakionesha tuzo ya Lifetime achievement award aliyopewa na designers na models wa Tanzania.
 ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo kwa pamoja akifurahia na designers na models wa Tanzania mara baada kukabidhiwa tuzo ya Lifetime achievement award 
  ASIA Idarus Khamsin maarufu kwa jina la Mama wa Mitindo akimshukuri mmoja wa Waandaji wa hafla hiyo Martin Kadinda

UPELELEZI KESI YA MAUAJI MKURUGENZI WA PALMS BADO HAUJAKAMILIKA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa, upelelezi wa kesi ya mauji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la Palms Foundation, Wayne Lotter inayowakabili watuhumiwa nane bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Adolf Mkini ameeleza hayo leo mapema mbele Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa. Upelelezi bado haujakamilika

Aidha Mahakama ilielezwa na mshtakiwa Rahma Almas  kuwa mshtakiwa Mohammed Maganga anaumwa na yuko gerezani.

Kutokana na taarifa hizo, kesi imeahirishwa hadi Machi 21, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kujua kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni, raia wa Burundi, Nduimana Jonas maarufu Mchungaji (40) Mkazi wa Kamenge Burundi, Godfrey Salamba (42) Mkazi wa Kinondoni Msisiri A. Innocent Kimaro (23) Mkazi wa Temeke Mikoroshini, Chambie Ally(32) Mkazi wa Kia/Boma na Ofisa wa Benki ya NBC, Robert Mwaipyana (31) Mkazi wa Temeke Mikoroshini.

Wengine ni  Meneja wa Benki ya Baclays Khalid Mwinyi (33) Mkazi wa Mikocheni B, Mfanyabiashara Rahma Almas (37) Mkazi wa Mbagala B na Mohammed   Maganga (61) mchimba makaburi.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ambapo katika shtaka la kwanza wanadaiwa kuwa kati ya Julai Mosi na Agosti 16,mwaka 2017 wakiwa ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania washtakiwa hao walikula njama ya kufanya mauaji ya Wayne Lotter.

Katika shtaka la pili, washtakiwa wanadaiwa Agosti 16, mwaka jana katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie Kinondoni Dar es Salaam,  walimuua Lotter.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika

TUCTA KUTUMIA KONGAMANO LA WANAWAKE KUJADILI CHANGAMOTO SEHEMU ZA KAZI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) limesema
litatumia kongamano la Siku ya wanawake linalotarajiwa kufanyika
kesho  kujadili nafasi ya mwanamke na namna ya kutatua changamoto
zinazowakabili maeneo ya kazi.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa TUCTA,
Rehema Ludaga amesema kongamano litafanyika jijini Dar es Salaam
ikiwa ni siku moja kabla ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani
ambayo ni Machi 8 ya kila mwaka.

"Tutatumia kongamano letu la Machi 7(kesho) kujadili mambo
mbalimbali yanayowakabili wanawake kwenye maeneo ya kazi na moja
ya mjadala utahusu namna ya kuangalia changamoto zilizopo na  nini
kifanyike kukabiliana nazo au kuziondoa kabisa"amesema Ludaga.

Kuhusu kauli mbiu ya mwaka huu kwenye maadhimisho ya siku ya
mwanamke duniani inasema hivi "Tathimini ya Unyanyasaji wa kijinsia
mahala pakazi".

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa TUCTA, Dk.Yahya Msigwa amesema
kila mwaka wanafanya kongamano ila kupata mawazo ya wanawake
kwa lengo la kuboresha mahali pakazi na mgeni rasmi kwenye
kongamano anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam
Sophia Mjema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Rehema Ludaga akizungumza kuhusiana na Kongamano siku ya wanawake, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa TUCTA, Dk. Yahya Msigwa akizungumza na kuhusiana na utaratibu wa TUCTA kuandaa kongamano la wanawake.

TCCIA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUJADILI FURSA ZA MAENDELE

$
0
0
Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA) mwezi huu imeandaa mkutano wa wanachama wake pamoja na wafanyabiashara kwa ujumla. Mkutano huu ambao umebatizwa jiina la TCCIA breakfast utajadili mambo kadhaa ikiwemo; Urahisishaji wa biashara za kimataifa kupitia Benki, Fursa zitokanazo na makubaliano kati ya TCCIA na Chemba ya China, Fursa katika biashara ya bomba la mafuta na pia uboreshaji wa mazingira ya biashara. 
Akizungumzia mkutano huo Afisa Mkuu wa TCCIA Gotfrid Muganda alisema " huu ni mwendelezo wa ujengaji uwezo na kuwapa fursa wanachama wake na wafanyabiashara wa Tanzania". Pia TCCIA inalenga kurahisisha ufanyaji wa biashara kati ya China na Tanzania unaolenga kuondoa kabisa utapeli ambao baadhi ya wafanyabiashara wanakumbana nao. Mwaka jana TCCIA ilifanya mikutano kama hiyo mingi kwa mafanikio.

Pia Leo hii Afisa Mtendaji Mkuu wa TCCIA Ndugu Muganda alikutana na mwambata wa ubalozi wa Algeria Nchini Tanzania na kuzungumzia ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria. Kupitia mkutano huo Ubalozi wa Algeria umetoa mwaliko wa maonyesho ya kibiashara Nchini Algeria yaitwayo Algeria International Fair mwezi wa tano Mwaka 2018. Mkutano wa breakfast umedhaminiwa na Azania Bank, Air Tanzania na Zurich Insurance

BENKI YA CRDB YATANUA MTANDAO WA MATAWI YAKE

$
0
0
Muonekano wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Mlandizi mkoani Pwani.
Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB tawi la Mlandizi wakipata huduma za kifedha katika tawi hilo.
Meneja wa Tawi jipya la Benki ya CRDB la Mlandizi mkoani Pwani, Twahibu Likungwala (kushoto), akitoa maelezo kwa mteja wa benki hiyo aliyefika tawini hapo jana namna anavyoweza kunufaika na akaunti maalum ya Wanawake (Malkia Akaunti).
Ufafanuzi kuhusu huduma za Kifedha katika Tawi la Mlandizi.
 Mteja wa Benki ya CRDB akipata ufafanuzi wa huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kutoka kwa Meneja wa Tawi jipya la Benki ya CRDB la Mlandizi mkoani Pwani, Twahibu Likungwalakwa (kulia).
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Cassian Nombo (katikati), akimuhudumia mmoja wa wateja waliofika katika tawi la Benki ya CRDB la Mlandizi mkoani Pwani kupata huduma za kifedha.

Wafanyakazi Wanawake wa Vodacom Tanzania Foundation, Doris Mollel Foundation waadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa msaada hospitali ya Muhimbili

$
0
0
Wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC na taasisi yake ya kuhudumia masuala ya jamii ya Vodacom Tanzania Foundation, leo wametembelea wodi ya wazazi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutoa vifaa mbalimbali ,ukiwa ni mwendelezo wake wa kutoa vifaa vya kuokoa zaidi ya watoto 260 wanaozaliwa kabla ya wakati kila mwaka nchini.

Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo na kutembelea wagonjwa, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia alisema “Tunayo furaha kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu kwa kutembelea hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutoa msaada katika wodi ya wazazi vitakavyowezesha kupunguza vifo vya watoto wachanga. Tutaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania za kuboresha sekta ya afya hususani kwa wanawake wajawazito na watoto wachanga”.

Vifaa tiba mbalimbali vya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) vilitolewa, baadhi ya vifaa hivyo ni vya kuwasadia watoto kupumua, kuongeza joto, kupima na kuratibu uzito kidijitali, pampasi na khanga, [oxygen concentrators, nebulizer machines, digital weigh scales, surfactants, infusion pumps and continuous positive airway machines, as well as Pampers and khangas].
 Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia (wa tatu kushoto) akikabidhi sehemu ya vifaa tiba maalum kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), kwa Dkt. Mariam Kalomo aliyemwakilisha mgeni rasmi naibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, jinsia na watoto, Dr Faustine Ndugulile. Wa pili kulia ni Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti, Doris Mollel.

Vodacom Tanzania Foundation inaelewa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wanawake nchini, wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua ndio maana imeamua kulivalia njuga changamoto zao na kuhakikisha vifo vya wanawake na watoto vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi vinapungua.

“Kusaidia kuboresha afya za wanawake na watoto na lishe bora ni moja ya malengo ya taasisi yetu ya Vodacom Tanzania Foundation. Tunaamini msaada mkubwa unatakiwa kunusuru maisha ya wanawake na watoto kutokana na changamoto mbalimbali zinazowazunguka, tunaamini msaada huu utafanikisha kuleta matokeo chanya ya kuboresha na kuokoa maisha ya watoto wachanga,”alisema Mworia.
Msaada huu ni mwendelezo wa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, kutoa vifaa vya kisasa vinavyowezesha kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) sambamba na miradi mingine inayolenga kuboresha afya ya uzazi na kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini, inayotekeleza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Baadhi ya miradi hiyo ni kuwasafirisha wanawake wenye ugonjwa wa Fistula hadi hospitali na kugharamia matibabu yao, kutoa jumbe za afya ya uzazi kwa wanawake wajawazito bure kupitia simu zao za mkononi za mtandao wa Vodacom sambamba na kuwawezesha wanawake wajawazito kuwahishwa katika vituo vya afya vyenye wataalamu wakati wanapokaribia kujifungua, kwa ajili ya kuokoa maisha yao na watoto wanaozaliwa.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

RAIS DK.SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA COMORO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Visiwa vya Comoro katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohammed Fakih Al Baadawy alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na  mgeni wake Balozi wa Visiwa vya Comoro katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mohammed Fakih Al Baadawy alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na  mgeni wake Balozi wa Visiwa vya Comoro katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mohammed Fakih Al Baadawy baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,(Picha na Ikulu)

KATIBU WA ORGANAZESHENI CCM ZANZIBAR AFANYA ZIARA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KATIBU wa  Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar ,Ndugu Bakari  Hamad Khamis amesema wanachama na watendaji wa CCM wanatakiwa kuandaa mipango endelevu ya kuhakikisha Chama kinashinda na kubaki madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Rai hiyo ameitoa katika ziara yake ya kujitambulisha kwa watendaji wa Chama na Jumuiya zake ambao ni wajumbe wa Sekreterieti za Wilaya na Majimbo ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, amesema Chama Cha Mapinduzi ili kishinde ni lazima maandalizi ya ushindi wake yaanze kwa sasa.

Alieleza kuwa pamoja na mambo mengine lengo la ziara hiyo ni kuwakumbusha watendaji hao majukumu yao ya msingi wanayotakiwa kuyafanyia kazi kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Amesema CCM ikiwa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa ni lazima ifanye kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi wote bila ya ubaguzi.

 WATENDAJI wa CCM Wilaya ya Kaskazini ‘A’ wakimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu wa Kamti Maalum ya NEC, Idara ya organazesheni CCM Zanzibar ndugu Bakari Hamad Khamis katika ziara ya kujitambulisha kwa Secretarieti ya CCM ngazi za majimbo na Wilaya.
 BAADHI ya wajumbe wa Sekreterieti za majimbo na Wilaya ya Kaskazini ‘A’ wakimlaki mgeni rasmi mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Wilaya iliyopo Gamba Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 KATIBU mwenezi CCM Wilaya kASKAZINI ''A'' Ali Chum Haji(kulia aliyesimama akizungumza), Katibu wa idara ya organazesheini CCM Zanzibar Bakar Hamad (katikati).
BAADHI ya wajumbe wa Sekreterieti za majimbo na Wilaya ya Kaskazini ‘A’ wakimlaki wakisikiliza na kufuatilia nasaha za mgeni rasmi.
  Katibu wa Kamti Maalum ya NEC, Idara ya organazesheni CCM Zanzibar ndugu Bakari Hamad Khamis akizungumza na watendaji hao katika ziara ya kujitambulisha kwa Secretarieti ya CCM ngazi za majimbo na Wilaya ya Kaskazini ‘’A’’.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JITIHADA ZA SERIKALI KUKUZA KILIMO ZALETA NEEMA LINDI

$
0
0
Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma

Wakulima Mkoani Lindi wamejipatia takribani bilioni 259 kwa kuuza mazao ya Biashara ikiwemo Korosho katika msimu uliopita baada ya Serikali kuweka msukumo na mazingira wezeshi katika uzalishaji na uuzaji mazao hayo.

Akizungumza katika Kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari-MAELEZO, Mkuu wa mkoa huo Bw. Godfrey Zambi amesema kuwa dhamira ya mkoa huo ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya bishara ambapo kwa msimu uliopita jumla ya kilo milioni 75 za korosho zilizalishwa.

“Mwaka 2017 Mkoa wa Lindi ulizalisha miche laki saba ya korosho na kuitawanya kwa wananchi wakati mwaka 2018 tumezalisha miche ya korosho milioni nne la laki tisa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza kilimo cha mazao ya biashara katika mkoa wetu”

Akifafanua kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo Zambi amebainisha kuwa ujenzi wa gati katika bandari ya Lindi umeklamilika kwa asilimia 90 na kiasi cha shilingi bilioni 1 na milioni 800 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huo.

Ujenzi wa gati hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa wananchi wa Mkoa huo.

“Katika kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na Afya bora Serikali imehakikisha kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ni wakuridhisha na unaendana na mahitaji ya Mkoa wetu hivyo tunaipongeza Serikali kwa hatua hii” amesisitiza Bw. Zambi.

Bw. Zambi ameongeza kuwa katika kuimarisha sekta ya afya, Mkoa huo umefanikiwa kupata watumishi watakaoziba pengo la wale walioondolewa katika utumishi wa umma kutokana na kuwa na vyeti  vya kughushi.

Akizungumzia ujenzi wa viwanda, Zambi amebainisha kuwa swala la kuanzisha viwanda 100 kila mkoa kwa upande wa Mkoa wa Lindi agizo hilo linatekelezwa  na kila Halmashauri  katika Mkoa huo.

Kwa upande wa umeme alibainisha kuwa  Vijiji 180 vimeshanufaika na mradi wa REA na awamu ya tatu zaidi ya Vijiji 175 vitanufaika ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kufikisha nishati ya  Umeme katika Vijiji  vyote nchini.

Aidha, kwa upande wa  upatikanaji wa huduma za maji  kwa wananchi wa Mkoa huo hasa Vijijini umefikia asilimia 53 ambapo kwa sasa Serikali inaendelea na juihudi za kutafuta mzabuni  wa kujenga miundo mbinu ya kusambazia maji katika mkoa huo.

Kipindi cha Tunatekeleza kinarushwa na Shirikika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Kuratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO kikiwashirikisha viongozi mbalimbali wa Serikali ambapo awamu hii ni Wakuu wa Mikoa yote.

MLINZI SUMA JKT AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA

$
0
0
Na Ripota Wetu, Mbeya
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema watu wasiojulikana wamemvamia mlinzi wa SUMA JKT Chewe Wilson(34) na kumsababisha kifo baada ya kumkata mapanga sehemu za kichwani na mguu na kisha kupora silaha yake akiwa lindoni.


Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mohamed Mpinga amesema kuwa jeshi hilo limeendelea na jitihada zake za kukabiliana na matukio ya uhalifu ambapo kwa siku kadhaa sasa limekuwa likiendelea kufanya msako kwenye maeneo mbalimbali.

Kamanda Mpinga amesema kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama, jeshi hilo limepata mafanikio makubwa katika kudhibiti wahalifu na matukio ya uhalifu mkoani Mbeya.

"Tumefanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukamata watuhumiwa mbalimbali wa uhalifu, silaha na vifaa mbalimbali vya kutengenezea silaha,"amesema.

MLINZI SUMA JKT AUAWA KIKATILI

Kamanda Mpinga amesema usiku wa kuamikia Februari 26 mwaka huu huko maeneo ya Kituo cha mafuta kiitwacho Manyanya kilichopo Uyole jijini Mbeya watu wasiofahamika majina walimvamia mlinzi wa SUMA JKT aitwaye Chewe Wilson mkazi wa Iduda.

"Mlinzi huyo akiwa lindoni katika kituo hicho alivamiwa na kisha kukatwa mapanga na silaha aliyokuwa nayo ikaporwa na watu hao na baada ya hapo wakatoroka nayo,"amesema Kamanda Mpinga.

Amefafanua mlinzi huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na majeraha aliyoyapata sehemu za kichwani.

Kamanda Mpinga amesema kutokana na tukio hilo Polisi walifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano ambao baada ya kuhojiwa wamekiri kuhusika na tukio hilo.

"Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria mara baada ya upelelezi kukamilika,"amesema.

WADAKWA WAKIWA NA  GOBORE

Kamanda Mpinga amesema wamefanya msako katika Kitongoji cha Kibaoni wilayani Chunya na kuwakamata watu wawili wakiwa na bunduki aina ya Shortgun iliyotengenezwa kienyeji na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengenezea bunduki.

Amewataja watuhumiwa hao ni Fadhili Mayega(60), na Mashaka Samuel(38), wote wakazi wa  Kambikatoto

Ameongeza baada ya watuhumiwa kupekuliwa walikutwa na bunduki hiyo na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengenezea bunduki aina ya shortgun za kienyeji ambavyo ni mMkono wa kuwekea risasi kwenye bunduki,  unga wa baruti wenye uzito wa gramu moja.

Pia mafuta ya kusafishia bunduki, risasi 25 zilizotengenezwa kienyeji, tupa 10, chuma kimoja cha kukatia risasi, tindo za kukatia mawe, vipande vya vyuma viwili, visu vitano, nyundo kubwa mbili, bisibisi moja, mguu wa Pedal ya baiskeli na triger mbili.

"Watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria mara tu baada ya upelelezi kukamilika,"amesema Kamanda Mpinga.

Ametoa mwito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha tamaa ya kupata mali kwa njia zisizo halali kwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa ajili ya kujipatia kipato.

BODI YA PAMBA YAONGEZA CHUPA MILIONI NNE ZA DAWA ZA KUUA WADUDU KATIKA PAMBA

$
0
0
Na Tiganya Vincent
Serikali kupitia Bodi ya Pamba nchini (TCB) imeongeza dawa zaidi za kukabiliana na wadudu waharibifu wa zao la pamba zenye thamani ya bilioni 16 ili kuwasaidia wakulima waweze kuokoa mazao yao shambani.

Kauli hiyo ilitolewa juzi mjini Igunga na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania(TCB) Marco Mtunga wakati wa kampeni ya kutoa elimu juu ya unyunyuziaji sahihi wa dawa za kuua wadudu katika pamba.

Alisema dawa hizo zitarajiwa kusambazwa kwa wakulima kuanzia wiki hii ili kuwawezesha kuoka pamba yao na hatimaye waweze kupata mavuno mengi yatakayowapatia mapato mengi.

Mtunga alisema  jumla ya chupa za dawa milioni 4 zitasambazwa katika maeneo yote yanayolima pamba haba nchini.

Alisema chupa hizo ni nyongeza katika chupa milioni 2.5 ambazo tayari zimemeshasambazwa kwa wakulima wa maeneo mbalimbali yanayolima pamba hapa nchini.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwataka wakulima wa pamba kuhakikisha wanazingatia ushauri wote ambao wataalamu kilimo na viongozi wanaowapa juu ya upigaji dawa ili mazao yao yawe na vitumba(matunda) vingi hasa kuanzia 20 na kuendelea ambavyo ndiyo vitawawezesha kupata kilo 1000 na kuendelea katika ekari moja.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa elimu kwa wakulima wa pamba juu ya unyunyuziaji sahihi wa dawa za wadudu waharibifu wa zao hilo  mjini Igunga.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Igunga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akiendesha kampeni matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu katika zao la pamba jana. Picha na Tiganya Vincent

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKONDA ATAKA FEDHA ZA MKOPO WA BARABARA ZITUMIKE KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii
MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameigizaa Bodi ya Barabara kuhakikisha fedha za  mkopo ambazo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara zinatumika ipasavyo

Amesema fedha hizo zinatakiwa kujenga barabara za kisasa na si  kutumika kwenye warsha, semina na safari za mafunzo nje ya nchi.

 Akizungumza leo, Makonda amesema Dar es salaam ina fedha za DMDP takribani Sh.bilioni 600 kwa ya kujenga barabara na mifereji lakini asilimia kubwa ya fedha hizo zimekuwa zikitumika kwenye semina na safari za nje ya nchi kujifunza namna ya usimamizi wa barabara.

"Jambo jambo linalosaabisha Serikali kulipa madeni kwa mirado ambavyo imekusudiwa," amesema Makonda.

 Pia Makonda  amegundua gharama ya kujenga barabara ya Kilometa moja kwa fedha ya DMDP ni sawa na gharama ya kujenga barabara ya TANROAD Kilometa 3, hivyo ameshauri kikao hicho kuangalia kwa umakini jambo hilo ili fedha hizo ziweze kuleta tija kwa wananchi kwa uwepo wa barabara zenye ubora.

Amesema kwa mwaka wa fedha wa 2018-2019 Mkoa wa Dar es salaam umetenga Sh.bilioni 289.3 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Wakala wa Barabara za Mijini na Vijini(TARURA),Tanroad na vyanzo  Wakala wa Barabara za Mjini na vya ndani vya halmashauri.

Ameongeza  hataki kuona w,ananchi wa Dar es Salaam wanateseka kutokana na ubovu wa barabara zenye mashimo na mahandaki.

Amesema hali hiyo husababisha hasara ya uharibifu wa vyombo vya usafiri na wakati mwingine ongezeko la msongamano wa magari.

"Nimeanza kuona nuru baada wakandarasi wa barabara za Dar es salaam kuanza kufuata taratibu kwa kutengeneza barabara za kisasa.Niwasihi TARURA m uwe wasimamizi wazuri wa ujenzi barabara kama wanavyofanya TANROAD ili tuwe na barabara zinazodumu muda mrefu," amesema Makonda.

MKUU  wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika leo jijini.

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema(kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori wakiwa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es Salaam 


Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(kushoto) pamoja na wajumbe wakingine wakiwa kwenye kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dar

MEYA MWITA APELEKA MAJI SAFI NA SALAMA PUGU, WANANCHI WAMPONGEZA

$
0
0
Na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya Dar
WANANCHI wa Kata ya Pugu, Mtaa wa Mustafa, wamempongeza Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita kwa kuwapelekea maji safi na salama huku wakibainishiwa ameweka historia ya kutatua changamoto hiyo.

Kata hiyo ambayo inadaiwa kuongoza kwa changamoto ya maji kwa kipindi kirefu, imejenga historia leo kupitia kwa Meya Mwita ambaye amepeleka maji na hivyo wananchi hao kuondokana na adha hiyo iliyodumu kwa kipindi kirefu.

Meya Mwita ameahidi pia kuongeza huduma hiyo kwenye maeneo ambayo yanachangamoto ya maji.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mtaa huo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mustafa Bahati Lusizi amemshukuru Meya Mwita kwa juhudi alizozionyesha  hadi kufanikisha kuwapatia huduma hiyo kwani kilikuwa ni kilio cha muda mrefu.

Amesema tangu kuingia kwa uongozi wake umekuwa wa mafanikio makubwa na kwamba waliomba kwa kipindi kifupi kupatiwa maji huduma hiyo na hivyo wameweza kutekelezewa kwa wakati walioahidiwa.

Amefafanua kwa sasa wananchi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama, nakuomba kufikishiwa kwa huduma hiyo maeneo mengine yenye changamoto hizo.

“ Kwaniaba ya wananchi wa mtaa huu, tunakupongeza Meya umefanya kazi kubwa, eneo hili linachangamoto ya maji, lakini kwa sasa itakuwa historia ,kwenye huu utawala wako tutakukumbuka kwa kutuondolea kero hii” amesema Lusizi.
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (mwenyesuti nyeusi) akitoa maelekezo kwa Diwani wa Kata ya Pugu Bonivesture Mphuru na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mustafa Bahati Lusizi leo alipotembelea kukagua mradi wa maji kwenye kata hiyo, ambapo kwa sasa wananchi hao wameanza kupata maji safi na Salama.
 Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akimtwisha Mwananchi ndoo ya maji leo, wanao shuhudia tukio hilo ni Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Mwenye suti nyeusi) akiwa na madiwani wa halmashauri ya jiji  leo walipotembelea kukagua mradi wa ujenzi wa barabara wa kilomita 0.7 kuingia katika Dampo la Pugu Kinyamwezi ambapo inajengwa kwa kiwango cha zege.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SIMBA YAANIKA MIKAKATI YA KUIBUKA NA USHINDI SHIDI YA AL MASRY

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

KUELEKEA mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry benchi la ufundi la Klabu ya Simba limeweka wazi mikakati yake ya kuhakikisha wanaondoka na ushindi kwenye mtanange huo muhimu.

Simba wanatarajia kucheza kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa kuanzia saa 12 jioni ukiwa ni mchezo wa pili wa kimataifa baada ya kuwatoa Gendamarie ya Djibout.

Akizungumzia mchezo huo leo jijini Dar es Salaam, Nahodha wa Simba John Raphael Bocco amesema wapo tayari kucheza vizuri na kwa bidii kesho dhidi ya Al Masry ili washinde.

 Kocha Mkuu, Mfaransa, Pierre Lechantre amesema baada ya maandalizi mazuri, vijana wake wapo tayari kwa mchezo wa kesho.

Hats hivyo Bocco amesisitiza anafahamu utakuwa mchezo mgumu kwa sababu Al Masry ni timu nzuri kwa rekodi zake na matokeo yake ya nyuma.

Pia Bocco amesema hata Simba ni timu nzuri na iona rekodi nzuri pia kwenye michuano ya Afrika, hivyo mchezo wa kesho utakuwa wa ushindani mkubwa.

Bocco amewaomba wapenzi wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kesho kuishangilia timu yao ili iweze kupata ushindi nyumbani.   

Baada ya mchezo wa kesho, timu hizo zitarudiana siku 10 baadaye mjini Cairo, Misri na mshindi wa jumla ataingia kwenye mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi kwa kucheza na moja ya timu zilizotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu zinazoingia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho hupatiwa dola za Kimarekani 150,000 zaidi ya Sh.mlioni 300 ambazo huongezeka kulingana na matokeo zaidi kuanzia hatua hiyo.

Bingwa wa Kombe la Shirikisho hupata Dola za Kimarekani 625,000 zaidi ya Sh. bilioni 1.5, mshindi wa Pili wakati mshindi wa pili wa Kundi hupata dola 239,000 sawa na wa tatu wakati mshindi wa nne hupata dola 150,000.

MKURUGENZI ATOA POLE KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA MBAGALA RANGI TATU

$
0
0
 MKURUGENZI wa Halmashauri wa Temeke jijini Dar es Salaam, Nassib Mmbagga ametoa pole kwa wafanyabiashara wa soko la Mbagala Rangi tatu  ambao wamepoteza mali zao baada ya kuungua kwa soko hilo.

Soko hilo ambalo lilikuwa na wafanya biashara zaidi ya 500 lilianza kuteketea usiku wa kumkia leo.

Akizungumza leo,Mkurugenzi  amesema Halmashauri imepanga kukutana na wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara katika soko hilo.

Amesema lengo ni  kuangalia ni jinsi gani halmashauri itawasaidia
   Vibanda vilivyokuwa vinamilikiwa na wafanyabiashara wa Soko la Mbagala Rangi Tatu vikiwa vimeteketea kwa moto.
 Baadhi ya wananchi wakiwa eneo la tukio
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images