Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA JUMATANO LEO MARCH 7,2018


LUKUVI AELEZA MABORESHO YALIYOFANYIKA KATIKA SEKTA YA ARDHI

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi ametaja maboresho kadhaa yaliyofanyika katika Wizara ya Ardhi.
Mhe. Lukuvi aliyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
Akieleza Maendeleo yanayofanyika sasa katika eneo la Urasimishaji; Mhe Lukuvi alieleza kuwa zoezi la Urasimishaji sasa linaendelea kwa kasi, na kutolea mfano wa Jiji la Mwanza kuwa zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa. Alisema; “Mpaka sasa viwanja 35,000 vimeshapimwa na Hati 12,000 kutolewa  katika wilaya za Ilemela na Nyamagana.  
Mhe. Lukuvi alisema baadhi ya maeneo mengine ambayo yamefanya zoezi la Urasimishaji kwa kiwango cha kuridhisha ni pamoja na Kimara na Makongo ambapo Wananchi wenyewe wamekuwa wahusika wakuu katika kuhakikisha kuwa wamezingatia miongozo waliopewa na Wizara kufanikisha zoezi hilo, ikiwepo kuzingatia kuainisha miundombinu muhimu kama  njia za barabara, maji , umeme n.k.
Akiendelea kufafanua jinsi eneo la Upimaji wa viwanja lilivyoboreshwa. Mhe. Waziri ameeleza kuwa sasa kuna kampuni 48 za upimaji ambazo zimesajiliwa na kuidhinishwa na Wizara, na zinazoendelea  sasa na kufanya upimaji wa viwanja katika maeneo mbalimbali nchini.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akionyesha muonekano wa Hati ya Kielektroniki inavyotarajiwa kuwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere; Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akionyesha moja ya ramani za Mipango Miji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku na msaidizi wake walipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS MAGUFULI ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA DK.KABURU

0
0
 Aliyekuwa  mbunge  wa  kigoma  mjini, mbunge  wa  bunge la  Africa  Mashariki na Mwenyekiti mstaafu  wa  CCM mkoa  wa  Kigoma,  Dr  Amani Walid Kabourou enzi za uhai wake

WAZIRI MWIJAGE AFANYA ZIARA KIBAHA

0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage jana tarehe 6 Machi, 2018 amekabidhi eneo lenye ukubwa wa hekari 200 kwa mkandarasi SUMA JKT ambaye atakuwa na kazi ya kufanya leveling kwa ajili ya ujenzi wa sheds kwa Viwanda Vikubwa na vya kati. 
Katika eneo hilo la TAMCO Kibaha vitajengwa Viwanda vya nguo, Viwanda vya madawa ya binadamu na Wanyama, Viwanda vya kuunganisha magari na mitambo kama matrekta, ili kuongeza ajira kwa watanzania.

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA BAJETI YA MWAKA 2018/2019

0
0
Na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii
BARAZA  la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia mkutano wake maalum limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida  na mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019.

Ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatarajiwa kukusanya na kupokea Sh. 242,185,292,987.00 ambapo Sh. 209,436,308,079.00 sawa na asilimia 86.5 ni ruzuku kutoka Serikali kuu.

Wakati Sh. 686,380,000.00  sawa na asilimia 0.3 ni mchango wa jamii na  Sh. 32,062,704,908.00 sawa na asilimia  13.2 ni mapato ya ndani ya manispaa.

Akizungumza mbele ya Madiwani wa Manispaa hiyo katika kikao hicho jana, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta amesema kati ya fedha hizo zilizopitishwa, Sh. 120,326,705,873.00 ni matumizi ya kawaida ambayo ni sawa na asilimia 49.7 ya bajeti yote.

Amesema Sh. 121,858,587,114.00 ni fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 50.3 ya bajeti.

 Meya Sitta ameeleza kuwa atika fedha hizo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatarajia kukusanya Sh. 32,749,084,908.00 kutoka vyanzo vyake vya ndani.

"Sh. 16,392,166,400.00 zitatumika kwa matumizi ya kawaida na Sh. 16,356,913,508.00 zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo na  fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu ni Sh. 209,436,208,079.00 zitakazojumuisha Sh. 105,501,668,606.00 kwa  ajili ya miradi ya maendeleo," amesema.

Sitta amefafanua mishahara ya watumishi kutokana na mapato ya ndani ni Sh. 906,498,855.00 na mishahara kutokana na ruzuku ya Serikali Kuu ni Sh. 99,590,270,811.00.

Hivyo inafanya jumla ya Sh. 100,496,769,666.00 fedha kwa matumizi mengineyo ni Sh. 15,485,667,545.00 kutoka vyanzo vya ndani na Sh.4,344,268,662.00 kutoka ruzuku ya Serikali kuu na kufanya jumla ya matumizi mengineyo kuwa ni shilingi 19,829,936,207.00.

"Ili kufikia mafanikio yaliyokusudiwa Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni itaimarisha mahusiano mazuri kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wadau wengine itaendelea kujenga uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma  zilizo bora.

" Madiwani na  wenyeviti wa Serikali ya Mitaa nao  watakuwa mstari wa mbele katika kusimamia  shughuli za wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,"amesema.

Aidha mpango wa matumizi nabajeti ya mwaka 2018/2019 ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2015-2020.

Hivyo matokeo ya utekelezaji wa  mpango na bajeti yameelekezwa katika kujibu matarajio ya watu ambayo ni utatuzi wa  kero zao pamoja na maisha bora kwa kila mtanzania,"amesema Sitta.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sitta akizungumza mbele ya Madiwani wa Manispaa hiyo  katika mkutano maalumu wa Baraza leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Madiwani wakimsiliza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

MWILI WA DK. AMANI KABURU KUSAFIRISHWA KESHO KIGOMA

0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

MWILI wa aliyekuwa Mbunge  wa  Kigoma  Mjini, Mbunge  wa  Bunge la  Afrika  Mashariki na Mwenyekiti mstaafu  wa  Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Kigoma Dk.Amani Walid Kaburu ambaye amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili unatarajiwa kusafirishwa kesho.

Taarifa zilizotufikia zinaeleza mwili wa Dk.Kaburu utasafirishwa kwenda mkoani Kigoma kwa ajili ya kuupumzisha kwenye nyumba yake ya milele.

Dk.Kaburu kabla ya kufikwa na umauti alikuwa Hospitali ya Muhimbili ambapo alifikishwa kwa ajili ya matibabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili(kiharusi).

Kwa sasa msiba upo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati taratibu nyingine zikiendelea kabla ya kuelekea Kigoma.Michuzi Blogu itaendelea kutoa taarifa za msiba huo kadri zinavyotufikia.

HISTORIA FUPI YA DK.KABURU

Dk. Kaburu alizaliwa 23 Mei mwaka 1949 na enzi za uhai wake amefanya shughuli mbalimbali za ujenzi wa nchi na amekuwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi na hasa kwenye vyama vya siasa nchini.

Enzi za uhai wake Dk. Kaburu amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema na akiwa kwenye nafasi hiyo alifanya kazi kubwa ya kuuimarisha upinzani na hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).

Ambapo uongozi wake kwenye nafasi hiyo alifanikiwa kushawishi wananchi wengi wa Mkoa wa Kigoma kujiunga Chadema.Hata hivyo Septemba mwaka 2006 alijiunga na CCM na Oktoba mwaka 2012 akawa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma.

Pia Dk. Kaburu enzi za uhai wake amewahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki kuanzia Juni 5 mwaka 2007 hadi Juni 4 mwaka 2012.

UHIFADHI WA KUMBUKUMBU YA HISTORIA YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA KUWAVUTIA WADAU

0
0
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Popou (kushoto) alipotembelea katika ofisi za kukumbumbu ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika na kuona namna Urusi ilivyochangia katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimuonyesha Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Popou (kushoto) pikipiki iliyotolewa na Urusi (Soviet Union) ili iweze kutumiwa wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika alipotembelea katika ofisi za kukumbumbu ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika na kuona namna Urusi ilivyochangia katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimuonyesha mazingira ya ofisi za kukumbumbu ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Popou (wapili kushoto) alipotembelea katika ofisi hizo kuona namna Urusi ilivyochangia katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ujio wa Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Popou (kushoto) alipotembelea katika ofisi hizo kuona namna Urusi ilivyochangia katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Mwakilishi wa UNDP nchini, Bibi. Natalie BOUCLY (kushoto) alipotembelea katika ofisi za kuhifadhi urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam na kujadili namna ambavyo UNDP itasaidiana na wizara katika kuhifadhi historia hiyo kwa manufaa ya vizazi vijavyo. 
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimshukuru Mwakilishi wa UNDP nchini, Bibi. Natalie BOUCLY (kulia) baada ya kutembelea ofisi za kuhifadhi urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam na kujadili namna ambavyo UNDP itasaidiana na wizara katika kuhifadhi historia hiyo kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Picha na: Genofeva Matemu -WHUSM

KAMPUNI YAMPA BAISKELI MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA ILI ATIMIZE NDOTO YAKE

0
0
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya D&G Export Company Ltd inayojishughulisha na ununuzi wa mazao na utunzaji wa korosho wilayani Tunduru na Liwale imeamua kumsaidia baiskeli ya magurudumu matatu mwanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Kichangani Shaibu Mpoto.

Mwanafunzi huyo alishindwa kuendelea na masomo yake baada ya kupata ugonjwa  wa kupooza miguu, miaka minne iliyopita jambo ambalo lilimfanya kuwa na wakati mgumu kuendelea na masomo lakini  kupatikana kwa baiskeli hiyo kutarudisha ndoto zake kielimu.

Shaibu alipatwa na tatizo la kupooza mwaka 2014 akiwa darasa la tatu na alilazimika kukaa nyumbani bila kujua hatma yake.Hivyo Kampuni hiyo kupitia Mkurugenzi wake Geofrey Kalamba imeamua kutoa msaada wa baiskeli hiyo yenye thamani ya Sh.320,000.

Akizungumzia zaidi leo kuhusu msaada huo, Kalamba amesema ametoa baiskeli hiyo ili kumsaidia Shaibu kuhudhuria masomo na hatimaye aweze kutimiza ndoto zake.

"Niliguswa sana baada ya kuona amebebwa mgongoni na bibi yake akipelekwa shuleni licha ya umri wa Shaibu kuwa mkubwa.Hivyo nilisema lazima nimsaidie baiskeli ili kumrahisisha anapotaka kwenda shuleni na maeneo mengine,"amesema.

Kwa upande wake Shaibu amesema ameshukuru kwa kupata msaada huo na kueleza ndoto za kupata elimu zitatimia kwani alishakata tamaa lakini sasa anauhakika atatimiza alichokusudia kwenye elimu.

"Nashukuru sana kwa msaada huu wa baiskeli, itanisaidia kwenda na kurudi shuleni na kwenda katika maeneo mengine bila kuhitaji kubebwa na mtu.Kila siku nilikuwa na mhurumia bibi yangu ambaye alilazimika kunibeba  kunipeleka shule na kunirudisha nyumbani,namuomba Mungu ampe maisha marefu bibi yangu na  aliyenipa baiskeli,"amesema Shaibu.

Kwa upande wake mlezi wa Shaibu ambaye ni bibi yake Fatma Kaluma amesema kwa sasa atapumzika kumbeba Shaibu kila siku asubuhi na jioni na atapata muda wa kufanya kazi za kujiongezea kipato kwa kuwa awali alishindwa kupata nafasi hiyo kutokana na tatizo la mjukuu 
wake.

Amewaomba wasamaria wema kuendelea kumsaidia mjukuu wake, kwani bado anahitaji vifaa vya shule ikiwemo daftari,vitabu na hata sare za shule ili mjukuu wake aweze kutimiza ndoto za kupata elimu.
 Mkurugenzi wa kampuni ya D&G Export Company Ltd, Geofrey Kalamba (kushoto) akimkabidhi baiskeli ya magurudumu matatu kwa mlezi wa mwanafunzi, Shaibu Mpoto anayesoma darasa la 7 shule ya msingi Kichangani Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ili iweze kumsaidia kwenda shuleni.


UWT YAWAGEUKIA WADAIWA SUGU BENKI YA WANAWAKE

0
0
*Yataka waliokopa warejeshe mkopo haraka, wakishindwa wachukuliwe hatua

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT)kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Gaudentia Kabaka  amewataka wateja wanaodaiwa na Benki ya Wanawake Tanzania(TWB), kuhakikisha wanalipa marejesho yao ya mikopo mara moja na ikiwezekana ndani ya siku saba.

Akizungumza leo katika Makao makuu ya UWT  Dar es Salaam, Kabaka amesema UWT inaungana na taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya wanawake  Tanzania (TWB) Beng'i Iasa ya  kutaka wadaiwa sugu wa benki hiyo walipe marejesho ya mikopo ndani ya siku saba.

"Sisi umoja wa Wanawake Tanzania, na wanawake wote kwa ujumla nchini hatutakubali na hatuko tayari kabisa kuona watu wachache wakiwemo hata wanawake wenzetu wakitumia benki hii kwa kujinufaisha wao wenyewe.Waliochukua mkopo wahakikishe wanalipa ili wengine nao wakope,". alisema.

Ameongeza UWT wanapenda kuona mikopo hiyo inarejeshwa kwa wakati na kufafanua TWB ndiyo benki pekee inayoweza kumkopesha mama mjasiriamali mdogo.Pia ni miongoni mwa benki tatu tu zilizopo duniani ambazo ni maalum kwa ajili ya wanawake.Mbali ya hii ya hapa kwetu ya TWB, moja ipo Pakistan na nyingine India.

"UWT tunatoa rai kwa wakopaji wote na tunatoa tamko, hao ambao wamekopeshwa na hawajarudisha mikopo kwa wakati wachukuliwe hatua za haraka na stahiki ikiwemo kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha wanalipa mikopo yao yote kwa manufaa na uhai wa benki yetu na kwa manufaa ya wanawake wote nchini.

"Wadaiwa sugu ni 7065 ambao ni wengi sana hasa kutokana na fedha wanayoihodhi ambazo ni kiasi cha Sh. bilioni 6.79. Tungependa kuona mikopo hii inarejeshwa kwa wakati.Tunaendelea kufuatilia na tunatamani tungepata hiyo orodha ya hao wadaiwa sugu," amesema Kabaka.

Ameongeza kuwepo kwa benki hiyo ni maombi na kilio cha muda mrefu cha wanawake nchini tangu uhuru kupitia Jumuiya ya CCM kuzaliwa. Ni kilio cha Kina bibi Titi Mohammed na mama Sophia Kawawa wakati wa uhai wao wakiwa wenyeviti wa UWT kwa nyakati  tofauti na kilio cha wenyeviti wengine waliofuata hadi sasa.

"Napenda kuwaambia jambo hili  kama Mwenyekiti wa UWT nalifuatilia kwa karibu sana kwa kuwa ni miongoni mwa maagizo yaliyotolewa na Mwenyekiti wetu, Rais Dk.John Magufuli wakati wa Mkutano wetu Mkuu uliofanyika Desemba 8, 2017 mjini Dodoma", amesema.

Amesema uongozi mpya wa UWT umekaa na benki ya wanawake kuangalia namna gani benki itawafikia wanawake wengi na kwa riba nafuu zaidi. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) kupitia CCM, Gaudentia Kabaka (katikati) akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuunga mkono taarifa ya Benki ya Wanawake Tanzania(TWB) inayotaka wadaiwa sugu wa benki hiyo kulipa mkopo ndani ya siku saba.Wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu UWT, Amina Makilagi na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Bara Eva Kiwhele. (Picha na Said Mwishehe)

BARCLAYS LAUNCHES A NEW AFRICA MARKETS INDEX IN THE CONTINENT

0
0
A survey of the stock markets of 17 African countries by Barclays Africa Group has rated Tanzania’s financial markets 11th overall with a score of 44% in the continent ahead of the likes Morocco (42 %,) Ivory Coast (41%) and Egypt (39%). South Africa with a score of 92% was ranked first. 

The Africa Financial Markets Index (AFMI) advocates for the expansion and deepening of financial markets across the continent. The Index measures six pillars namely: depth and breadth per instrument or product that can be traded; access to foreign exchange; market transparency, tax and regulations; macro economic opportunity; legality and enforceability. The index measured and tracked 40 indicators across the six pillars.

“The Index provides countries with valuable insights and tools to improve the state of their financial markets,” said Abdi Mohamed, Managing Director, Barclays Bank Tanzania. “By broadening and deepening their understanding of the requirements of local and international investors, Africa’s leaders can develop robust markets – a prime condition for sustainable, inclusive growth,” he added.

Tanzania scored second highest ranking in East Africa in Market transparency, tax and regulatory environment pillar, ahead of Uganda, Kenya, Ghana and Morocco. It outpaced some Western African peers in the market depth pillar, which focussed on areas such as the range of financial products, currencies and hedging options available and capacity of local investors’ parameters. 
 Corporate executives jointly display the just-launched the Barclays Africa Financial Markets Index in Dar es Salaam yesterday. From right are Barclays Bank Tanzania (BBT) Managing Director, Abdi Mohamed, BBT Director for Corporate and Investment Banking, Esther Maruma, Dar es Salaam Stock Exchange Chief Executive Officer, Moremi Marwa, Barclays Head of Africa Trading, Corporate and Investment Banking, George Asante and Barclays Africa Chief Economist and Head of Research, Jeff Gable. 
Barclays Bank Tanzania (BBT) Managing Director, Abdi Mohamed (left), and a Bank of Tanzania (BoT) Acting Director Financial Markets,  Emmanuel Akaro, exchange views during the official launch of Barclays Africa Financial Markets Index in Dar es Salaam today.

PROF. MBARAWA AWATAKA WATENDAJI KUTUMIA HEKIMA KUONGOZA

0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa , akikata utepe kuzindua rasmi taarifa ya Klaimatolojia ya mwaka 2017, wakati alipofungua baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), linalofanyika Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Agnes Kijazi.
 Wajumbe wa Mkutano wa baraza la Wafanyakazi  wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa baraza hilo mkoani Dodoma.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Nchini (TMA), Dkt. Agness Kijazi mara baada ya ufunguzi wa  baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo Mkoani Dodoma.
 Afisa Utumishi Mkuu aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Sekta ya Uchukuzi, Banaga Katabazi, akitoa shukrani mara baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) kufungua baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), linalofanyika Mkoani Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali Hewa Nchini (TMA), mara baada ya kulifungua Mkoani Dodoma.

CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA (TPSC) KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA JIMBO LA PUNTLAND NCHINI SOMALIA

0
0
Wataalamu waandamizi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), wapo nchini Somalia kwa ajili ya kazi ya kuandaa mafunzo ya kuboresha utumishi wa umma katika Jimbo la Puntland nchini Somalia. 

Kazi hiyo inafanyika kwa ushirikiano kati ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania na Chuo Kikuu cha Taifa cha Puntland kilichopo Jimbo la Puntland nchini Somalia. Mkuu wa Chuo Dkt Henry Mambo alisema kwamba watumishi hao waliondoka nchini tarehe 3 mwezi Machi mwaka huu na wanatarajia kurejea chini tarehe 11 mwezi huu. Dkt Mambo alisema mafunzo hayo yanafanyika ikiwani ushirikiano kati ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania na Chuo kikuu cha Taifa cha Puntland kilichopo Jimbo la Puntland nchini Somalia. 

Alifafanua kuwa ushirikiano huo ni matokeo ya hati ya makubaliano iliyosainiwa mwezi Mei, 2017 Makao Makuu ya Chuo cha Utumishi wa Umma Jijini Dar es Salaam na wakuu wa vyuo hivyo viwili, Dr. Henry Mambo ambaye ni Mkuu wa TPSC na Bw. Mohamud Hamid Mohamed ambaye ni Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa cha Puntland. Makubaliano hayo yalishuhudiwa na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki na Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Puntland Mh. Abdirahman Ahmed Abdulle. 

Kwa mujibu wa makubaliano hayo Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kitashirikiana na Chuo Kikuu cha Puntland kuandaa na kuendesha mafunzo mbalimbali ya muda mfupi na mrefu ili kuwajengea uwezo watumishi wa umma wa Puntland. Maeneo yaliyopewa kipaumbele katika uandaaji wa mafunzo ni pamoja na;Rasilimali watu (Human Resources Management), Utawala wa Fedha (Financial Management), Masuala ya Manunuzi (Procurement Management), 

Mengine ni Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Mipango, Tathmini na Ufuatiliaji, (Planning, Monitoring and Evaluation), Sera,Tafiti pamoja na Utunzaji wa Kumbukumbu. Mpango huo wa Puntland unafadhiliwa na Benki ya Dunia ambao unatarajiwa kufadhili zoezi zima la uandaaji wa mafunzo hayo. 
Aliyekuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki (wa Pili Kulia) na Waziri wa Kazi,Vijana na Michezo wa Puntland Abdurahman Ahmed Abdulle wakisaini mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa kuboresha sekta ya utumishi wa umma jimboni Puntland ambapo serikali kupitia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) itaendesha mafunzo hayo kwa kushiriakana na Chuo Kikuu cha Puntland. Kulia Mkuu wa TPSC Dk. Henry Mambo. 

Wafanyakazi TBL walivyoshiriki Kilimanjaro Marathon 2018

0
0
Wafanyakazi TBL walivyoshiriki Kilimanjaro Marathon 2018
Idadi kubwa ya wafanyakazi kutoka kampuni ya TBL Group wameshiriki mbio za Kili Marathon zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.Mashindano haya maarufu duniani yanadhaminiwa na kampuni hiyo kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premier Lager.
Mwaka huu TBL Group imekuja na ajenda ya kuwezesha na kuhamasisha  upandaji mti katika maeneo yanayozunguka mlima Kilimanjaro ili kulinda mazingira,ambapo kwa kushirikiana na taasisi  ya Kilimanjaro Project, inatarajia kupanda miti 100,000.
Uhamasishaji wa mradi huu umeanza kutekelezwa wakati wa mashindano ya Kili Marathon yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. 
 Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group wakipongezana baada ya kumalizika mashindano ya Kili Marathon
Moja ya vibanda  vyenye vipeperushi vya kampeni ya kupanda miti na maelezo vilivyokuwa  vimewekwa mitaa mbalimbali ya mji wa Moshi
 

TWB yadai mikopo sugu yenye thamani ya Tsh.bilioni 7.9 toka kwa wateja 7,065

0
0
Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) katika hatua zake za  kutaka kuimarisha mtaji wake na kufanya kazi zake kwa ufanisi imewataka wateja wake 7,065 wenye mikopo sugu yenye thamani Tsh. bilioni 7.9, kulipa mikopo hiyo ndani ya siku saba vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Bi. Beng’i Issa alisema benki imeanza kuchukua hatua za kuimarisha mtaji wake kwa kuwataka wateja wake wenye madeni sugu kulipa madeni yao ndani ya siku hizo vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa. 

“Moja ya mambo yanayokwamisha  kuimarika kwa mtaji na kupanua huduma za kibenki ni kuwepo kwa mikopo sugu,” sasa tunawataka wateja wetu wenye mikopo sugu kulipa bila shuruti vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa, aliongeza kusema,Bi Issa ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Alisema hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha mtaji wa benki unaimrika na itasaidia kutoa huduma za kibenki kwa ufanisi. Wakopaji wengi wamepitiliza siku 90 za urejeshaji madeni ya mikopo yao na hiyo kinyume na utaratibu wa mikataba waliyokubaliana na benki wakati wanakopa.
Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Wanawake (TWB), Bi. Beng’i Issa akisisitiza jambo wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya benki hiyo ilivyojipanga kuimarisha mtaji wake kwa kuwataka wateja wake wenye madeni sugu kulipa madeni yao ya mikopo, wa pili kulia ni Mjumbe wa Bodi hiyo, Bw. Oswald Mutaitina, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Japhet Justine na wa pili kushoto ni Mjumbe wa Bodi hiyo Bw. Ramadhani Saidi. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Madini ni mali ya Watanzania sio wawekezaji wa kigeni: Biteko

0
0
Na Mathias Canal, Geita
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli tangu ianze utendaji wake imejipambanua wazi kuwa rasilimali zote za nchi ikiwemo madini ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa hivyo ni Mali ya watanzania wenyewe sio wawekezaji wa kigeni.


Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusisitiza kuwa katika rasilimali Madini Taifa halipaswi kukurupuka kuyachimba kwa kuwa uwezo wa kitaaluma na kiteknolojia kuwezesha kuyachimba na kuyafaidi kama Taifa ulikuwa mdogo kwa mantiki hiyo, Baba wa Taifa akaenda mbali zaidi kwa kuagiza madini yasichimbwe hadi hapo Taifa litakapokuwa na uwezo wa kuyachimba ili watanzania waweze kunufaika ipasavyo.


Hayo yamebainishwa na Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko Leo 6 Machi 2018 wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama akiwa katika ziara ya kikazi Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita.


Mhe Biteko alisema kuwa Mwalimu kwa wakati huo alijua fika kuwa Tanzani a ikifungua milango ya kuchimba madini bila Taifa  kujenga uwezo imara wa kufanikisha lengo hilo ipasavyo, wataalamu na wafanyabiashara au wale wanaoitwa wawekezaji kutoka nje, ilimradi wanazo fedha nyingi; watalilalia Taifa na kuwadanganya watanzania na hatimaye kuweza kufaidika zaidi kutokana na rasilimali madini.
Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya watendaji katika Wilaya ya Nyang'wale mara baada ya kuzuru wilayani Nang'wale akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018.
Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Nyang'wale iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hivyo Mhe Hamim Gwiyama ikimsikiliza kwa makini Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018.
Naibu waziri Wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (aliyesimama) akielezea mikakati ya wizara hiyo wakati alipozuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita Leo 6 Machi 2018, Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale Mhe Hussein Nassor Amari Kasu, na Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mhe Hamim Gwiyama.


RAIA WA ZAMBIA, WENZAKE KORTINI KWA KWA TUHUMA ZA UTAKATISHAJI FEDHA

0
0
 Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

RAIA wa Zambia na wenzake sita wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kula njama, wizi na utakatishaji wa fedha.

Hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo na Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Wakili wa Serikali mwandamizi Mutalemwa Kishenyi imewataja watuhumiwa hao ni Kirby Ng'andu, Meneja uendeshaji wa kampuni ya Zambia Cargo and Logistic, Robert Christopher na Wakala wa usafirishaji, Isihaka Ngubi, Cathbert Mlugu mlinzi, Mrisho Mindu, Karani Giften John na Maulid Said.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi imedaiwa, kati ya Januari 26 na Februari 2 mwaka huu, huko katika kampuni ya Zambia Cargo and Logistics iliyopo Dar es Salaam,washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Imeendelea kudaiwa, siku na mahali hapo, washtakiwa hao  waliiba katoni 700 za korosho zilizobanguliwa  zenye thamani ya USD 54180 ambazo ni sawa na Sh.120,563,909,53, mali ya Barabara Trading Tanzania Ltd.

Wakili Mwanaamina amedai  kuwa, siku na mahali hapo, watuhumiwa hao wote pia walijihusisha na muamala unaohusiana na katoni hizo 700 za korosho zenye thamani hiyo ya fedha huku wakijua kuwa, mali hiyo ni zao lililotokana na kosa la wizi.

Hata hivyo, washtakiwa wote wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kuwa shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana, wakili Kishenyi amedai kuwa, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho kutwa, Machi 9 mwaka huu.

KUYEKO AWAONYA WENYEVITI KUTOCHUKUA FEDHA ZA WANANCHI WANAOHITAJI HUDUMA

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MEYA wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Charles Kuyeko amewataka wenyeviti wa Serikali za mitaa wilayani humo kuacha kuwatoza fedha wananchi  wanaofika katika ofisi zao kupata huduma kwani kufanya hivyo tafsiri yake ni rushwa.

Meya Kuyeko amesema hayo leo asubuhi alipokuwa akifungua ofisi mpya ya Serikali ya mtaa wa Mtakuja iliyopo katika kata  Vingunguti Ilala jijini ambapo amesisitiza umuhimu wa viongozi wa ngazi mbalimbali kutoa huduma kwa wananchi bila kuomba fedha.

"Utekelezaji wa majukumu ya ofisini, ninaomba tusiombe rushwa wananchi wanaohitaji huduma.Viongozi endeleeni kushirikiana na wananchi ili kazi ziendelee.Nishauri wananchi msikae na vitu moyoni, mnapaswa kupaza sauti kwa jambo lolote ili lipatiwe ufumbuzi,"amesema Kuyeko.

Kwa upande wa Diwani  wa Kata ya Vingunguti na Naibu Meya wa Manispaa hiyo , Omary Kumbilamoto amemshukuru Meya kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo ambayo italeta tija kwa wananchi waishio maeneo hayo kwani kabla ya hapo walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma kwa Mwenyekiti.

Aidha amemshukuru  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo kwani kupitia Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini( TARURA) amekubali kuifanyia matengenezo barabara ya Vingunguti kwa Mnyamani.

Amefafanua barabara hiyo imechimbika na hivyo kuwa na mashimo mengi kiasi cha kuifanya kutopitika kwa urahisi na hivyo kusababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na msongamano mkubwa wa magari yanayosababishwa na ubovu wa barabara.

Pia amemuonya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtakuja asigeuze ofisi hiyo mpya ya Serikali ya mtaa kuwa mahabusu kwa kunyanyasa wananchi wasiokuwa na hatia,hivyo watu wote watakaokamatwa wapelekwe kwenye vyombo vya kisheria.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akifungua ofisi mpya ya Serikali ya Mtaa wa Mtakuja kata ya Vingunguti ambayo imejengwa kwa gharama za Halmashauri hili kuweza kuleta huduma jirani na Wananchi.kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Omary Kumbilamoto akishuhudia uzinduzi huo.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza na wakazi wa Vingunguti kuhusu umuhimu wa ofisi hiyo na kusisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutoa taarifa za rushwa wanazoombwa na Viongozi.
 Diwani wa Kata ya Vingunguti  na Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Omary Kumbilamoto akitoa nasaha zake kwa wakazi wa Vingunguti mara baada ya uzinduzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mtakuja.
 Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mtakuja inavyoonekana kwa nje, mara baada ya kujengwa  na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa gharama ya Shilingi Milioni 45 .
Sehemu ya Wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa ofisi ya Serikali  ya Mtaa wa Mtakuja ambayo imejengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

MAVUNDE: WAAJIRI WASIOFUATA SHERIA YA UAJIRI KUENDELEA KUKIONA CHAMOTO

AZAM FC, MWADUI HAPATOSHI KESHO CHAMAZI

0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii

KLABU Bingwa Afrika Mashariki na kati AzamFC inatarajia kuwakaribisha wachimba madini wa Shinyanga Mwadui FC katika michuano inayoendelea ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. 

Mtanange huo utakao ni wa ushindani kwa kila timu kutaka kupata ushindi utafanyika kesho saa moja usiku na mchezo utachezwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Azam FC wanatafuta alama 3 ili kuwakaribia Mabingwa watetezi Tanzania Bara  Yanga  wenye alama 40 wakiwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.

Wakati Azam FC wakiwa nyuma kwa alama 35 na wapo nafasi ya tatu huku wakiongozwa na  vinara wa Ligi hiyo wekundu wa Msimbazi Simba  wakiwa na alama 46.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema kikosi kipo vizuri na wamejipanga kuchukua alama tatu wakiwa nyumbani.

"Tumeandaa timu vizuri na mwalimu  amepata muda wa kutosha wa kuandaa vijana  vizuri kuelekea mchezo huo na wachezaji wote walifanya mazoezi ya pamoja.

"Isipokuwa tutaendelea kumkosa mchezaji wetu katika mchezo wa kesho Yakubu Mohamed ambaye ni majeruhi"amesema Jaffary na kuongeza wanataka kubaki na alama tatu  kama ambavyo walizipata walipocheza na Singida United,"amesema Jaffary.

MWENYEKITI UVCCM PWANI ATOA NENO KWA VIJANA

0
0
Na Elisa Shunda, Kibiti
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Makwiro amewataka vijana wa mkoa huo kutojihusisha na mambo ambayo hayana tija kwa Taifa huku pia akipokea wanachama wapya 60 ambao wameamua kujiuna na umoja huo mkoani Pwani.

Wanachama hao wamejiunga leo wakati wa ziara yake ambayo aliongoza na wajumbe wa baraza kuu la UVCCM Mkoa wa Pwani  wakati anazungmza na wajumbe wa baraza la wilayani Kibiti.

Akizungumza baada ya kuwapokea vijana hao, Mwenyekiti Charangwa Makwiro amewatahadharisha vijana hao kutokubeba ajenda ambazo hawazielewi kwa undani wake kwa kuwaeleza wasifanye jambo ambalo halina faida kwao wala kwa Taifa.

"Serikali ya Awamu ya Tano na Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais Magufuli ana imani kubwa na  vijana,unapokuwa kijana wa CCM unapaswa kuwa mzalendo,uwe na adabu na heshim.Kataa rushwa na kubwa zaidi tufanye kazi kwa bidii.

"Linapotokea jambo tusishabikie pasipo kuelewa undani wa jambo hilo kwani hakuna kitu kibaya kama watu wasioitakia mema nchi yetu kutaka kukuingizia wewe kijana katika ajenda zao ambazo wewe huzifahamu kwa ajili ya kuharibu amani,"amesema.

Makwiro amewakumbusha vijana kutambua wao ndo nguvu na jeuri ya CCM katika kufanikisha mambo yote yanayopaswa kufanyika katika chama hicho na kueleza kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka ujao.

"Tuhakikishe tunajiandaa kwenye uchaguzi huo mapema na vijana mnayo nafasi ya kuwania nafasi za uongozi kwenye Serikali za mitaa.Hivyo ni jukumu letu vijana wa CCM kuanza kujipanga mapema ili tushinde kwa kishindo,"ameongeza.

Pia amekumbusha umuhimu wa vijana kuchangamkia fursa ya mikopo na kwamba Serikali kutoa fedha mikopo kwa vijana wote ili kufanya shughuli za kimaendeleo na kuwashauri vijana kutengeneza vikundi ili kufanya ujasiriamali.

"Itapendeza pia kama mtakuwa na CV(wasifu) zenye maelezo yao ya taaluma na vipaji mlivyonavyo na kuziwasilisha katika ofisi ya wilya ya umoja huo wa vijana ili hata nafasi za kazi zikitokea wilayani na kwingineko itakuwa rahisi kupata ajira serikalini na maeneo mengine,"amesema.

Makwiro amewaahidi vijana wilayani Kibiti kuwa kwa kumchagua yeye kuwa Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani pamoja na wajumbe wa baraza kuu la mkoa huo atahakikisha anatumia rasirimali zake binafsi, akili zake kuhakikisha jumuiya hiyo ya vijana inatatua baadhi ya changamoto za vijana hao,"amesema.

Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao amesema yupo bega kwa bega na Makwiro ili kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa umoja huo taifa, Kheri James kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa baraza la wilaya hiyo, Mwenyekiti UVCCM wa Kibiti,Juma Ndaluke amesema wamepokea maelekezo yote kutoka kwa viongozi hao wa Mkoa na ameahidi kuyatekeleza kwa jinsi watakavyojaliwa huku akisisitiza yeye na  wajumbe wake hawatowaangusha katika uboreshaji wa utendaji kazi wa umoja huo wa vijana.
  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa wa Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti,Juma Ndaluke. Picha zote na Elisa Shunda
   Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti, Juma Ndaluke (wa pili kulia) kadi 200 na kanuni 100 kwa baada ya kuzungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa wa Mkoa wa Pwani ,Ramadhan Mlao.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti, Juma Ndaluke akizungumza katika mkutano huo. 
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akimkabidhi Yusuph Kimbe (kulia) kadi ya Umoja wa Vijana baada ya kujiunga.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images