Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

DR MPOKI AWATAKA WATU KUACHA KUPOTOSHA JUU YA TIBA YA USINGIZI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

 Katibu Mkuu wa Wizara Afya, Jinsia , Wazee na Watoto Dk . Mpoki Lusubisya amesema taaluma ya tiba ya usingizi ni moja ya kiungo muhimu katika matibabu hasa upasuaji katika hospitali zetu.

Dk Mpoki Amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano kwa wataalamu wa dawa za usingizi kwa hospitali zote zilizopo ukanda wa pwani.

"Kumekuwa na dhana tofauti juu ya tiba ya usingizi kiasi cha watu kuiita ni nusu kaputi jambo ambalo limekuwa likipotosha na kuogopesha wagonjwa hivyo naomba niwaambie kuwa tiba ya usingizi sio nusu kaputi bali ni dawa ya kuzoofisha mishipa"amesema Dk Mpoki.

Amesema kuwa watu wanatakiwa kuwa waelewa zaidi kuwa tiba ya usingizi ni dawa muhimu sana katika kuhakikisha kuwa tiba za upasuaji zinafanikiwa 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku tano ya  awamu ya nne kwa wataalamu wa dawa za usingizi katika hospitali zilizopo katika ukanda wa pwani 
 Mratibu wa Mafunzo ya Wataalamu wa dawa za Usingizi kutoka Tasisi ya Mifupa (MOI), Karima Khalid akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa wataalamu wa dawa za usingizi
 Wataalamu wa Dawa za usingizi wakifatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na wataalamu wa dawa hizo
Wataalamu wa Dawa za usingizi wakifatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa

GATI YA LINDI YAKAMILIKA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA) kwa kukamilisha ujenzi wa gati ya Lindi na kuwataka kutafuta masoko ili bandari hiyo iweze kunufaisha Serikali na wananchi wa Mkoa huo.
Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati hiyo mkoani Lindi ambapo amesema mradi umekamilika kwa asilimia 92 na kukamilika kwa gati hiyo kutarahisisha biashara na kukuza uchumi kwa wananchi kwani meli kubwa zitaanza kutia nanga katika bandari hiyo.
“Napenda kuwapongeza sana TPA kwa kazi kubwa mliyoifanya kukamilisha mradi huu, ni wakati sasa mkatafute masoko ili mpate faida na kurahisisha usafirishaji kati ya mkoa huu na visiwa vinavyozunguka” amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa ameongeza kuwa pamoja na kukamilisha mradi huo TPA itunze miundombinu hiyo na kuifanyia ukarabati wa mara kwa mara ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka, amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa, kuwa Mamlaka itazingatia maelekezo yake na kuahidi kusimamia sehemu ndogo iliyobaki ili iweze kukamilika kwa wakati na viwango vilivyokubaliwa.
Mhandisi Mattaka ameongeza kuwa ujenzi wa gati hiyo imegharimu kiasi cha shilingi zaidi ya bilioni 3 na fedha hizo zimefadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hatua nyingine Waziri Profesa Mbarawa, amesema Kivuko kwa ajili ya Lindi na Kitunda kitawasili mapema katikati ya wiki ili kianze kutoa huduma kwa wakazi wa mkoa huo.
Aidha ameauagiza uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kuhakikisha wanatafuta fedha na kujenga majengo ya abiria kwa upande wa Lindi na Kitunda ili kupunguza changamoto inayowakabilia abiria hasa nyakati za mvua.

Naye Mkandarasi wa Kampuni ya Hematec, Emmanuel Lyimo amesema mpaka sasa ujenzi uko kwenye hatua za mwisho na ambapo ndani ya siku chache mradi huo utakamilika na kukabidhiwa kwa ajili kuanza kutoa huduma.
Waziri Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku mbili kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Bandari na Vivuko.


Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na

Mawasiliano, Kitengo aha Mawasiliano Serikalini.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA, Eng Karim Mattaka, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), kuhusu hatua za ujenzi wa gati ya Lindi, wakati Waziri huyo alipotembelea mradi kukagua maendeleo yake.
 Muonekano wa Gati mpya ya Bandari ya Lindi ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia zaidi ya  90. Gati hiyo imegharimu kiasi zaidi ya shilingi bilioni 3 ikiwa ni fedha za Serikali kwa asilimia 100.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akipanda kwenye boti kuelelekea katika eneo la Kitunda mkoani Lindi, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani humo. Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wakazi wa Mkoani humo kuwa kivuko hicho kitawasili na kuanza kutoa huduma mwishoni mwa wiki hii.
 Muonekano wa hatua ilipofikia Gati ya kuegeshea kivuko katika eneo la Kitunda Mkoani Lindi. Ujenzi wa Gati hiyo umefikia asilimia zaidi ya 90 na imejengwa kwa fedha za Serikali.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akishiriki katika kuchanganya zege katika ujenzi wa barabara ya maegesho ya kivuko Mkoani Lindi, alipokagua maendeleo ya ujenzi wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akiongea na wakazi wa Mkoani Lindi, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi maegesho ya Kivuko. Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wakazi hao kuwa kivuko kitawasili katikatia ya wiki na kuanza kazi mwishoni mwa wiki.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Mdahalo Wakuwania Uongozi wa Urais Jumuiya ya Watanzania DMV, Marekani

$
0
0
Huu ni Mdahalo wa Sehemu ya kwanza kati ya mbili zijazo, wa kugombania kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Urais kupitia Jumuiya ya Watanzania waishio DMV, ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi, Siku ya Jumamosi March 3, 2018 katika ukumbi wa Indiana Springs Terrance Local Park Sliver Spring Maryland Nchini Marekani.

AHMED ALBAITY AWASILI NA KUPOKELEWA BEIJING- CHINA

$
0
0
 Hatimaye yule mtanzania aliyesaidiwa kupata ufadhili wa matibabu na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amewasili leo hii majira ya saa 9:20 alasiri katika Uwanja wa kimataifa wa Beijing Capital. Mtanzania huyo aitwaye Ahmed Albaity alipokekewa na Maafisa waandamizi wa ubalozi pamoja na watanzania waishio hapa jijini Beijing na kusindikizwa kwenye hospitali ya kimataifa ya Puhua.

Ndugu Ahmed Albaity  ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo ambalo limedumu kwa takribani miaka kumi na moja akiwa kitandani,tayari ameanza kupatiwa  Matibabu  katika hatua za  awali  mara tu baada ya kuwasili hospitalini hapo.

Mapema akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi wakitanzania Wanaosoma na kuishi nchini humo Bw. Remidius Emmanuel ambaye pia ni Katibu Mkuu Shirikisho hilo amesema wao kama watanzania wanaosoma na kuishi katika Taifa la China  wameshiriki kumpokea Mtanzania mwenzao (Ndugu. Ahmed Albaity )  na kwamba  kwa kipindi chote ambacho atakuwepo hapa Beijing China wataendelea kutoa Ushirikiano na kumjulia hali wakati wote.

 "Tunamshukuru Mwenyezi MUNGU amemuongoza Bw.Ahmed kufika salama hapa Beijing, Tumeshuhudia watanzania wakimsindikiza   uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na  kuongozwa na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda, huu ni upendo wa kipekee, na sisi tumeguswa na kuwiwa kumpokea tukiongozwa na Maafisa waandamizi wa Ubalozi wetu hapa China" Alisema Bw. Remidius.

Kwa upande wake ndugu Ahmed Albaity ameushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini China pamoja na uwakilishi wa Watanzania wanaosoma na kuishi nchini humo kwa moyo wao wa upendo na namna walivyoweza kumpokea yeye na ujumbe alioambatana nao.

Bw.Michael Semindu moja kati watanzania wanaosoma nchini humo aliyeshiriki mapokezi hayo  alimhakikishia Ndugu Ahmed Ushirikiano kwa kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu jijini Beijing "Nimefurahi kuungana na Maafisa wa Ubalozi pamoja na watanzania wenzangu kumpokea mwenzetu, tunamuahidi ushirikiano kwa kipindi chote atakachoendelea kupata matibabu  nchini China"  Alisema Bw. Michael

Shilingi Trilioni 1 Zatengwa Kulipa Madeni Mbalimbali Mwaka wa Fedha 2017/2018

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Serikali imetenga jumla ya shilingi Trilioni 1 mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali ya watoa huduma, wazabuni na watumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameeleza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa miradi na ahadi mbalimbali za Serikali.
"Kati ya shilingi Trilioni 1 zilizotengwa kulipia madeni kwa mwaka huu wa fedha, shilingi Bilioni 896.3 zimeshalipwa kwa watoa huduma, wazabuni na watumishi wa Serikali," alisema Dkt. Abbasi.

Amesema hesabu hiyo inajumuisha shilingi Bilioni 43 ambazo zimelipwa Februari, 2018 ikiwa ni malimbikizo ya wafanyakazi  wa sekta ya Umma. 
"Madeni mengine uhakiki unaendelea na yataendelea kulipwa siku zijazo na tutawajulisha," alifafanua Dkt. Abbasi.

Vile vile amesema, Serikali katika kuwaondolea adha ya usafiri kwa wananchi wa maziwa makuu likiwemo Ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria. Kwa upande wa Ziwa Victoria,  mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini mkataba na kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwezi huu kwa ajili utengenezaji wa meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tani 400.

Kwa upande wa Ziwa Tanganyika zabuni kwa ajili ya utengenezaji wa meli mpya ya abiria na mizigo itatangazwa mwezi huu. Meli hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo na italeta mapinduzi makubwa katika usafiri ziwani hilo.

Aidha Dkt. Abbasi amesema Julai mwaka huu nchi itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo Boeing Dreamliner na ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa, Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi kote nchini.

UFARANSA YAIPONGEZA TANZANIA KWA KUPAMBANA NA RUSHWA

$
0
0
SERIKALI ya Ufaransa imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa mapambano dhidi ya rushwa na inaamini fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali zitatumika kama ilivyokusudiwa.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumatatu, Machi 05, 2018) na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Bw. Frederic Clavier alipomtembelea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.alozi Clavier amesema Ufaransa imeridhishwa na mapambano ya rushwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wataendelea kushirikiana nayo katika uboreshaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Pia Balozi huyo amesema Septemba mwaka huu wanatarajia kufungua ofisi ya Shirika la Kimataifa la Misada ya Maendeleo la Ufaransa (AFD) jijini Dar es Salaam ili kurahisisha utoaji wa huduma. Kwa sasa ofisi za AFD zipo Nairobi nchini Kenya.Shirika hilo limekuwa likishirikiana na Serikali, katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo na ya maji safi na maji taka kwenye mikoa ya Simiyu, Mwanza, Musoma na Morogoro.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka kipaumbele katika uwajibikaji na kupambana na rushwa ili kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi zinatumika vizuri pamoja na wananchi kupata haki.

Amesema mapambano dhidi ya rushwa yataiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda, uwekezaji, kilimo na utalii, hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Ufaransa ili waje kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda, kilimo, madini na miundombinu mbalimbali.

Pia Waziri Mkuu amesema Serikali itashirikiana na Ufaransa katika kuandaa mikutano mbalimbali itakayowakutanisha wadau wa sekta binafsi kutoka nchi zote mbili ili kuwapa mbinu za namna ya kukuza uchumi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Machi 5, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Machi 5, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier (katikati), kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Machi 5, 2018, kushoto ni mwakilishi mkazi wa Nchi ya Ufaransa, Emanuel Baudran. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Dkt. Magufuli atoa kibali cha kuendelezwa ujenzi wa msikiti wa Sumbawanga, serikali ya mkoa wa Rukwa yachangia Milioni 5.7 kuumalizia

$
0
0

Uongozi wa Waislamu Mkoani Rukwa umepokea kwa furaha mchango wa Shilingi Milioni 5.7 uliotolewa na uongozi wa serikali ya Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo katika kikao cha maridhiano juu ya ujenzi wa msikiti uliosimama kwa muda.


Fedha hizo zilizochangwa zilijumuisha ahadi, fedha taslimu pamoja na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa kwa umoja wa viongozi wa serikali kuonesha mshikamano uliopo kati ya serikali na wananchi bilaya kujali itikadi, dini wala rangi huku Mh. Wangabo akichangia milioni 1.5.

Kabla ya maridhiano hayo Mh. Wangabo alitoa salamu za rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya kuuendeleza msikiti huo na kunukuu kuwa Mheshimiwa Rais ametoa kibali cha kuuendeleza msikiti hio na yupo tayari kuweka jiwe la msingi ama kuuzindua msikiti huo.

“Mh. Rais ameniagiza niseme yafuatayo kuwa ametoa kibali cha kuendelea kujenga msikiti huu ahdi umalizike, ameyafikiria mambo mengi sana mpaka kuja kufikia maamuzi haya, ili yalete muskabali wa maridhiano, ilete amani, ilete utulivu, mshikamano, maoelewano na umoja ili Rukwa yetu iweze kusonga mbele kama kitu kimoja., la pili alisema kuwa yupo tayari kuweka jiwe la msingi ama la kuzindua msikiti huu,”

Kwa kuongezea hilo Mh. Wangabo aliuomba uongozi wa uislamu mkoa kuendelea kushirikiana na kudumiasha amani na kuhakikisha wanajenga Rukwa moja isiyoyumbishwa na tofauti yoyote kwani ushirikiano huo umekuwa wa muda mrefu hovyo asingependa pawepo na tofauti.

Pia alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kuhakikisha vikwazo vyote vianondolewa na kumtaka kamishna wa ardhi nyanda za juu kusini kufanya haraka kupitisha kibali ili msikiti huo upatiwe hati.
Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa mkoa wa Rukwa Rashid Akilimali amesifu maamuzi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli na kukubali ombi lake la kutaka kuja kuweka jiwe la msingi ama kuuzindua msikiti huo na kuwa waislamu wataendelea kuungana nae na kumuombea amalize vipindi vyake salama.
“Mh. Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya waislamu wa mkoa wa Rukwa kwanza tunatoa shukrani za dhati kwa Mh.Rais wa nchi Mh. Dk. John Magufuli, nimeamini kama alivyosema kuwa yeye ni msikivu na yeye anatuomba kila siku tumuombee dua na sisi mwisho wa khotuba yetu kila ijumaa tunadua huwa tunaiomba, Eee Mola wetu linda amani ya nchi yetu na uwalinde viongozi wetu,” Shekh Akilimali alimalizia.
Uongozi wa mkoa wa Rukwa uliowajumuisha kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa halmashauri, Mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sumbawanga pamoja na kaimu Kamishna wa Ardhi nyanda za juu kusini.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo akitoa salamu za Rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya waislamu kukubaliwa kuendelea na ujenzi wa Msikiti.
 Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Rashid Akilimali akiwasihi waislamu wanedelee kumuunga mkono Rais Dk. John Pombe Magufuli na kumshukuru kwa kuwaruhusu kuendelea na ujenzi wa msikiti. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (kulia) akiepeana Mikono na  Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Sheikh Rashid Akilimali baada ya maridhiano ya ujenzi wa Msikiti.
  Msikiti ulioruhusiwa kuendelea kujengwa.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MBEYA YETU TV: POLISI MBEYA WANASA WASHUKIWA WA MAUAJI


MICHUZI TV: 'NDOTO'na mwanamuziki Sister Fey

Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari mjini Dodoma

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt Abdallah Possi akutana na watanzania waishio nchini humo

VOA Swahili: Duniani Leo 5th March 2018

CHIRWA, KAMOSOKU KAMILI GADO KUWAVAA WABOTSWANA KESHO

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba kikosi chao kimejiandaa vyema kuwakabili Township Rollers ya Botswana hapo kesho katika mchezo wao wa klabu bingwa barani Afrika utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia mishale ya saa 10 na nusu jioni.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charles Boniphace Mkwasa amesema kwamba hali ya wachezaji iko vizuri kwa ajili ya pambano hilo na jambo la faraja ni kurejea kwa baadhi ya wachezaji wao ambao awali walikuwa majeruhi akiwemo Obrey Chirwa na Thabani Kamusoko.

Mkwasa alisema kwamba kuelekea katika mchezo huo itategemea na mipango ya mwalimu kama ataweza kuwajumuisha wachezaji hao ambao walikuwa majeruhi katika pambano hilo linalotaraji kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Aidha alisema kwamba licha ya kurejea kwa wachezaji Donald Ngoma, Amisi Tambwe na Vicent Andrew katika kikosi ila bado hawapo katika mipango ya mwalimu kwa ajili ya mechi ya kesho hivyo huenda wakatumika katika mechi ya marudiano itakayochezwa nchini Botswana.

Hata hivyo Mkwasa alisema kwamba wataingia katika mchezo huo kwa tahadhari kubwa kwa kuwa wanakutana na timu ngumu iliyo bora kwenye mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Townshio Rollers utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

NHIF, Waratibu wajadili uboreshaji wa huduma zake

$
0
0
Na Grace Michael, Morogoro

 KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu kupitia Mfumo wa Bima ya Afya, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekutana na waratibu wake kutoka halmashauri zote nchini kwa lengo la kujipanga kuwafikia wananchi wengi zaidi pamoja na uboreshaji wa huduma kwa wanachama. 

Akifungua kikao kazi hicho cha siku mbili, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alisema kuwa ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Serikali ya Viwanda ni lazima Mfuko kwa kushirikiana na wadau wake kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanafikiwa kwa kujiunga na Mfuko ili kuwa na uhakika wa huduma za matibabu. 

“Ili kufikia lengo la Nchi ya Viwanda ambalo Rais wetu amelianzisha, ni lazima tuhakikishe wananchi wote wanakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wanapopatwa na magonjwa na ndio maana tumeamua kabisa tukutane kwa pamoja ili tukubaliane namna bora ya kuwafikia lakini pia kuboresha na kuimarisha huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma,” alisema Bw. Konga. 

Kikao hicho pia kina lengo la kupata mrejesho wa pande zote mbili kuhusu maboresho mbalimbali yaliyofanyika ndani ya Mfuko na kujadili kwa pamoja mambo yanayohitaji kuboreshwa kwa lengo la kuongeza wigo na kutoa huduma bora. Mkurugenzi Mkuu pia alisisitiza juu ya kukabiliana na tatizo la udanganyifu ambalo limekuwa likifanywa na baadhi ya watoa huduma wasiokuwa waaminifu hali inayorudisha nyuma jitihada kubwa za Mfuko za kuimarisha Mfuko. 

Alisema kuwa kwa upande wa Mfuko, umeanzisha mifumo mbalimbali ya TEHAMA ambayo inatumika katika kubana mianya ya udanganyifu kwenye utumiaji wa huduma na uwasilishaji wa madai ya watoa huduma hivyo akawaomba waratibu hao kutoa ushirikiano mkubwa katika suala hili kwa lengo la kulinda uhai wa Mfuko. 

Kwa upande wa waratibu wamesema kuwa mkutano huo ni fursa kubwa kwao kupata taarifa mbalimbali za maboresho yaliyofanywa na kujengeana uwezo wa ushawishi kwa wananchi kujiunga na huduma za Mfuko.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Bernad Konga akifungua kikao kazi kilichohusisha Waratibu wa Mfuko kutoka Halmashauri zote nchini mjini Morogoro.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw. Bernard Konga akifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa katikati ni Meneja wa NHIF, Mkoa wa Morogoro Bi. Agnes Chaki na Kushoto ni Mkurugenzi wa 
Utawala na Rasilimali Watu Bw. Charles Lengeju.
 Waratibu wa Mfuko wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wawezeshaji

MAGAZETI YA JUMANNE LEO MARCH 6,2018


BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 05.03.2018

CHIRWA,KAMOSOKU KAMILI GADO KUWAVAA WABOTSWANA KESHO

$
0
0


Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba kikosi chao kimejiandaa vyema kuwakabili Township Rollers ya Botswana hapo kesho katika mchezo wao wa klabu bingwa barani Afrika utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia mishale ya saa 10 na nusu jioni.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charles Boniphace Mkwasa amesema kwamba hali ya wachezaji iko vizuri kwa ajili ya pambano hilo na jambo la faraja ni kurejea kwa baadhi ya wachezaji wao ambao awali walikuwa majeruhi akiwemo Obrey Chirwa na Thabani Kamusoko.

Mkwasa alisema kwamba kuelekea katika mchezo huo itategemea na mipango ya mwalimu kama ataweza kuwajumuisha wachezaji hao ambao walikuwa majeruhi katika pambano hilo linalotaraji kuwa na ushindani wa hali ya juu.
Aidha alisema kwamba licha ya kurejea kwa wachezaji Donald Ngoma, Amisi Tambwe na Vicent Andrew katika kikosi ila bado hawapo katika mipango ya mwalimu kwa ajili ya mechi ya kesho hivyo huenda wakatumika katika mechi ya marudiano itakayochezwa nchini Botswana.

Hata hivyo Mkwasa alisema kwamba wataingia katika mchezo huo kwa tahadhari kubwa kwa kuwa wanakutana na timu ngumu iliyo bora kwenye mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Townshio Rollers utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

NAMNA YA KUOMBA HATIMILIKI YA ARDHI YA KIMILA.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub

1.     HATIMILIKI  YA KIMILA NI IPI.
Hati  ya ardhi  ya kimila ni nyaraka  ya umiliki wa ardhi ambayo  inatoa utambuzi maalum wa umiliki wa ardhi. Hizi ni sawa  na hati miliki zile mnazozijua ambazo hutolewa kwa ardhi za mijini japo ipo tofauti kidogo. Moja ya tofauti  ya hati ya kimila na hatimiliki za mijini ni kuwa hizi husimamia ardhi mijini wakati hizi nyingine husimamia ardhi za vijijini.
2.      HATI YA KIMILA HUTOLEWA NA NANI.
Hati  ya umiliki wa  ardhi ya kimila  hutolewa na baraza la ardhi la kijiji( land village council). Kila kijiji  kinalo baraza hili. Pia baraza hili ndilo linalowajibika kwa masuala ya kila siku ya ardhi ya kijiji. Kwa hiyo maombi  yote ya kuomba ardhi au hati ya kimila yataelekezwa baraza hili.
                    KUSOMA ZAIDI NENDA: sheriayakub.blogspot.com

Barclays Bank launches a study skills programme for UDSM students.

$
0
0
24 Barclays Scholarship recipients from UDSM to take part in a training program to equip them with much needed skills.

Dar es Salaam, Saturday 3 March 2018, Barclays Bank Tanzania Ltd has today launched the Elevate Programme for students from the University of Dar es Salaam –UDSM. The event was held at the University of Dar es Salaam Business School (UDBS).

Speaking during the launch of the program, Barclays Bank Tanzania Ltd Citizenship Manager, Hellen Siria said that the Elevate Program is an award-winning international education company which has been training students to use the best-practice study skills for the last 16 years.

‘Elevate equips students with skills they need to succeed in school and beyond. It also trains teachers and parents/ guardians to ensure best-practice study behaviors are reinforced across the classroom and at home. The Elevate program works with more than 2,500 schools and 500,000 students each year and here in UDSM we are targeting 24 students’, said Siria.

Siria added that they use three steps in identifying students to engage. She named the student needs assessment which includes conducting an online audit of students,’ use of independent learning skills and student engagements which guarantee a high level of engagement to maximize skill uptake and challenge negative perceptions of study skills.

The elevate program will help students increase self-efficacy which fosters independent learning, increase student efficiency, motivation levels across the year, improve the caliber of student graduating from university and in addition will achieve a sustained behavior shift in students study habits and equip students with essential academic and non-academic skills that can assist with tertiary education and the transition into the work place.

“Our aim is to change learning behavior and inspire students to achieve their goals which for many would lead in breaking the poverty cycle”. She continued “The elevate program will improve academic performances of students and it will also help offer employments to students to deliver the program for a second year”.

The Elevate program is currently working with 150 South African Schools and 25 universities with scholarships in African countries. In addition, the Elevate program has conducted workshops to more than 25,000 students and presented three conferences for over 100 teachers across South Africa. 

Barclays Bank Tanzania Citizenship Manager, Hellen Siria (second left), talking to some University of Dar es Salaam (UDSM) students, during the official launch of elevate study skills progamme organized for 24 Barclays scholarship recipients at UDSM to equip them with needed skills in school and beyond. A brief occasion was held at the University’s Business School (UDBS) premises, in Dar es Salaam last Saturday. The Elevate Program is an international education company which has been training students to use the best-practice study skills and currently working with 150 South African Schools and 25 universities with scholarships in African countries. 
Elevate Education facilitator, Phehello Makgoe (left), giving a presentation on study and life skills to some University of Dar es Salaam (UDSM) students, during the official launch of elevate study skills progamme, organized by Barclays Bank Tanzania to 24 Barclays scholarship recipients at UDSM to equip them with needed skills in school and beyond. A brief occasion was held at the University’s Business School (UDBS) premises, in Dar es Salaam last Saturday.
Some UDSM students, lecturers, elevate and Barclay’s officials posing for a souvenir photograph after the launching of elevate education programme AT University of Dar es Salaam Business School premises in Dar es Salaam (UDBS) last Saturday. 

WILAYA YA UBUNGO MWENYEJI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8, 2018

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images