Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA MISUNGWI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea na kukagua kiwanda cha kusindika nyama cha Kampuni ya Chobo Investment kilichpo wilayani Misungwi chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 600 mbuzi na kondoo 920 kwa siku.
Alitembelea kiwanda hicho kinachomilikiwa na wazawa jana (Jumatatu, Februari 19, 2018) wakati akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Alisema amefarijika na uwekezaji huo.

Alisema uwekezaji wa aina hiyo ulikuwa unasubiriwa sana nchini kwa sababu unakwenda kupunguza tatizo la wafugaji kutokuwa na soko la uhakika wa mifugo yao, hivyo Serikali itamuunga mkono ili kiwanda hicho kiwe endelevu.

Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza sera ya uchumi wa viwanda na inahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika viwanda mbalimbali, ambapo aliipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda

Akizungumzia kuhusu changamoto ya kutokuwa na maeneo ya kunenepeshea na kulisha mifugo yao, Waziri Mkuu alisema tayari alishamuagiza Waziri wa Mifugo Bw. Luhaga Mpina kushughulikia suala hilo na kwamba litapatiwa ufumbuzi.

Pia Waziri Mkuu aliwataka watumishi waliojiriwa katika kiwanda hicho wafanye kazi kwa bidii, wawe waaminifu na waadilifu.

Awali, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bw. John Chobo alisema kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji, hivyo kinategemea maji ya kisima au ya kuletwa na boza kutoka Mwanza mjini jambo ambalo linachangia katika kuongeza gharama za uzalishaji.

Baada ya kutoa malalamiko hayo Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga  kushughulikia suala hilo na ahakikishe kiwanda hicho kinapata maji. Kiwanda hicho kipo umbali wa kilomita nne kutoka Ziwa Victoria.

Akizungumzia kuhusu changamoto ya eneo la kulishia na kunenepeshea ng’ombe Bw. Chobo alisema kampuni yake iliomba kupatiwa eneo kutoka kwa Serikali tangu mwaka 2014 karibu na kiwanda hicho lakini hadi sasa hawajapatiwa.

Kiwanda hicho kinauza bidhaa zake ndani na nje ya nchi. Nchi hizo ni Oman, China, Canada na Misri. Baadhi ya wanunuzi hao kutoka Omani ni Bw. Tahir Al Hashim na kutoka China ni Bw. Kingsong Shao walisema nyama inayochakatwa kiwandani hapo ni nzuri na ina ubora wa kimataifa.

Pia kiwanda hicho kinasambaza nyama katika migodi yote mikubwa nchini ambayo awali ilikuwa inaagiza nyama kutoka nje ya nchi, hivyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho aliiomba Serikali kuwasaidia katika kulinda soko la ndani.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 20, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitaza uchakataji wa nyama ya ng’omba wakati alipotembelea kiwanda cha nyama cha Tanbeef kinachomilikiwa na kampuni ya Chobo Investments Company katika eneo la usagara wilayani Misungwi Februari 19, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyama ya ng’ombe na mbuzi iliyofungashwa kitalaamu tayari kwa kuuzwa ndani na nje ya nchi wakati alipotembelea kiwanda cha nyama cha Tanbeef kinachomilikiwa na kampuni ya Chobo Investments Company katika eneo la usagara wilayani Misungwi Februari 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewataka makandarasi wazawa wa kampuni ya Samota, Anam na Jossam JV wanaojenga barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 kwa kiwango cha lami wahakikishe wanakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa muda uliowekwa.

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo katika kijiji cha Motomoto, Wilaya ya Urambo mkoani Tabora alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mtandao wa barabara mkoani humo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo.

“Nataka nione kazi za ujenzi zinafanyika kwa haraka, kwani uzoefu unaonesha baadhi ya makandarasi wazawa wamekuwa na kasi ndogo, hivyo mjipange vizuri ili barabara ikamilike kwa wakati”, amesema Prof. Mbarawa.

Amesema kuwa nia ya Serikali ni kuwajengea makandarasi wazawa uwezo ili waweze kutekeleza miradi mikubwa mingine ya ujenzi hapa nchini lakini haitasita kuwanyima kazi hizo kama miradi hiyo itacheleweshwa, haitakidhi viwango vinavyohitajika na kama hawataonekana eneo la kazi kwa kipindi kirefu.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na uongozi wa Wilaya ya Urambo, alipokutana nao katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
 Mbunge wa jimbo la Urambo, Mhe. Magreth Sitta, akimshukuru Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), kwa kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 inayojengwa kwa kiwago cha lami, mkoani Tabora.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu hatua za mradi wa ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 na kusisitiza nia ya Serikali ya kuwajengea uwezo wakandarasi wazawa ili waweze kutekeleza miradi ya ujenzi hapa nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, na uongozi wa wilaya ya Tabora wakipita juu ya daraja la Wala lenye urefu wa mita 34 katika barabara ya Tabora-Pangale yenye urefu wa KM 30, katika ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo, mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AHITIMISHA ZIARA WILAYANI MISUNGWI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiakata utepe wakati alipoweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mbarika – Misasi katika  kijiji cha Manawa  wilayani Misungwi, Februari 19, 2018. Wapili kulia  ni mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga na wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa  wa Mwanza, John Mongella. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mbarika- Misasi katika kijiji cha Manawa wilayani Misungwi Februari 19, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella na wapili kulia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kiwanga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua  madarasa yanayojengwa kwa nguvu za wananchi katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi Februari 19, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, wapili kulia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga na watatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubi mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi, Februari 19, 2018. 
  Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Misungwi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamayinza, Februari 19, 2018.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadahara kijijini  hapo,  Februari 19, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la pamba lenye ukubwa w hekari 6 la  Bw. Muhoja Ngole (kulia kwa Waziri Mkuu) katika kijiji cha Mondo wilayani Misungwi, Februari 19, 2018.

TAARIFA MATOKEO YA UCHUNGUZI KUHUSUKAULI YA ASKOFU ZACHARY KAKOBE.

Wateja wa Airtel wajishindia smartphone kwenye promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti

$
0
0
Wateja wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania wameendelea kujishindia zawadi mbali mbali kwenye promosheni inayoendelea ya SHINDA NA SMATIKA  Intaneti.

Kwenye droo ya leo ambayo imefanyika jijini Dar es Salaam, wateja ishirini wamejishindia simu mpya za smartphones pamoja na modem za kisasa huku wengine 3,000 wakijishindia 1GB bando ya intaneti

Akiongea wakati wa droo hiyo, Meneja Uhusiano Jackson Mmbando Airtel Tanzania amesema kuwa kampuni ya Airtel bado inaendelea kutoa zawadi mbali mbali zikiwemo simu za smartphones pamoja na moden huku kila siku wateja 1,000 wakijishindia bando ya 1GB.

Mpaka sasa kuna zaidi ya wateja elfu ishirini ambao wamejishindia simu aina ya smartphones na modem huku wengine 14,000 wakishinda bando ya intaneti ya 1GB. Promosheni yetu ni kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu na kwa hivyo kuingia kwenye droo mteja haitaji kujisajili. Kila mtu anatika kufanya ni kununua bando ya intaneti kwa kupiga 149*99# kisha kuchangua 5 Yatosha Smatika Intaneti halafu nunua bando ya siku, wiki au ya mwezi na kuingia kwenye droo, alisema Mmbando

Washindi wetu wamekuwa wakitoka sehemu mbali mbali hapa nchini. Kwa mfano washindi wa smartphones wametokea mikoa ya Mtwara, Zanzibar, Mwanza na wengine Dar es Salaam.

Promosheni hiyo ya siku 30 inatarajia kufikia tamati mwanzoni mwa mwezi ujao huku bando ya 30,000 GB zikiwa zimetolewa kwa wateja 1,000 kila siku.
 Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiwasiliana na moja ya washindi wakati wakuchezesha droo ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ambapo washindi 3000 na wengine simu za smartphone na modem. 
 Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando na Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah Hemedy wakiangalia moja ya namba ya washindi wakati wakuchezesha droo ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ambapo washindi 3000 na wengine simu za smartphone na modem.

MAKATIBU WAKUU WA WIZARA MBALIMBALI KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA UGANDA

$
0
0
Makatibu  Wakuu na Wataalam wa Wizara mbalimbali kutoka nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan ya Kusini wamekutana nchini Uganda ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya hiyo. 

Katika kikao kilichofanyika  Kampala nchini Uganda, Makatibu Wakuu hao na wataalam walijadili ripoti kuhusu  masuala ya Biashara, Fedha, Ushuru, Siasa, Miundombinu na Afya iliyokabidhiwa katika kikao cha Mawaziri wa Jumuiya hiyo kilichofanyika kuanzia tarehe 19 na kitahitimishwa tarehe 21 Februari, 2018.

Wizara kutoka Tanzania zilizohudhuria kikao hicho ni Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,  Wizara ya Katiba na Sheria, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Afya, Wazee Jinsia na Watoto na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar.
Wizara ya Nishati  iliwakilishwa na Katibu Mkuu, Dkt Hamis Mwinyimvua aliyeambatana na Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga,  Mjiolojia Mkuu, Adam Zuberi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Edith Mwanje ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao cha Makatibu Wakuu na Watalaam kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akizungumza katika kikao hicho.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza kulia waliokaa) akiwa katika kikao cha Makatibu Wakuu na Wataalam ambao wamehudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Uganda wa pili kulia  ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju, wa tatu kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Stephen Mbundi katika Wizara ya Mambo ya Nje, wa nne kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga.
 Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wataalam kutoka Nchi wanachama husika na Wajumbe mbalimbali wakijadili ripoti itakayotumika katika Mkutano wa 35 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri ambao unafanyika tarehe 19– 21 Februari, 2018 mjini Kampala nchini Uganda.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, Shomar O. Shomar (mbele), Kaimu Kamishna Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (mstari wa nyuma, kushoto) Mtalaam kutoka Wizara ya Nishati, Adam Zuberi na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Clarence Ichwekeleza wakiwa katika kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Mbundi wakifuatilia mada katika kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

ASKOFU KAKOBE AKUTWA AMETUNZA FEDHA NYINGI KWENYE NDOO NA MAJAB

$
0
0
Ni baada ya TRA kuchunguza Kanisa Full Gospel Bible fellowship

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) uchunguzi ambao wameufanya kwenye Kanisa la Askofu wa Kanisa Full Gospel Bible fellowship, Zakaria Kakobe wamebaini kuwa kanisa hilo linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na majaba.

Wamesema kitendo hicho ni kinyume na taratibu za utunzaji wa fedha lakini pia uwekaji na utoaji wa fedha nyingi kutoka benki haushiriki vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika huku ikibainika pia amekuwa mkwapaji wa kodi .

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema baada ya kufanya uchunguzi wamebaini mbali ya kuwa anatunza fedha nyingi kwenye ndoo na majaba , pia wamebaini hana akaunti yeyote nchini katika benki isipokuwa ni msimamizi wa akaunti ya Kanisa yenye fedha zaidi ya sh.bilioni nane.

Amesema katika uchunguzi huo wamebaini kuwa Kanisa limekwepa kodi ya zaidi ya Sh.bilioni 20 lakini amelipa baada ya kufanyika kwa uchunguzi huo wa TRA,

Pia uchunguzi wa TRA umebaini kuna kampuni ya watoto wa Askofu Kakobe kukwepa kodi ya zaidi ya Sh.milioni 37 ambazo ziliweza kulipwa na watoto hao.“Utaratibu wa utunzaji wa fedha za Kanisa kwenye ndoo na majaba ni kinyume cha utaratibu wa utunzaji fedha.Pia utoaji wa fedha nyingi katika akaunti haushirikishi vyombo vya ulinzi kwa ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika,”amesema Kichere

Hata hivyo, amesema safari za Askofu huyo za nje zinahusisha yeye na mkewe tu na kuhoji kwanini wengine hawasafiri katika safari hizo.Ikiwa pamoja na Kanisa hilo kushindwa kutengeneza hesabu za mapato na matumizi ya fedha jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya katiba na usimamizi wa fedha.

Ameeleza kwenye uchunguzi wa TRA umebaini kwamba fedha za Kanisa ndizo ambazo zimetumika kujenga nyumba ya mkewe Askofu Kakobe kwa jina lake kinyume na taratibu za Kanisa.

“TRA inatoa mwito kwa taasisi za dini nchini ambazo zinajihusisha na shughuli zozote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu za kod.Pia taasisi za dini zifuate katiba zao pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumiz,”amesema.

NAIBU WAZIRI WA MAJI :FIKISHENI HUDUMA YA MAJI PEMBEZONI MWA JIJI LA DAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameziagiza DAWASA na DAWASCO kuhakikisha zinafikisha huduma ya maji kwenye maeneo yaliyo pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, ambapo kuna uhaba mkubwa wa maji pamoja na kuwa na wakazi wengi zaidi na si kujikita katikati ya jiji hilo tu.
Naibu Waziri Aweso ametoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kikazi katika Wilaya ya Temeke kujionea uhalisia wa utekelezaji wa miradi ya maji, wilaya ambayo imekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na huduma hafifu ya majisafi  na salama.
Aweso amesema kuwa kuna haja ya DAWASA na DAWASCO kuimarisha huduma ya maji kwenye maeneo ya pembezoni mwa jiji kama Temeke, Kigamboni, Ukonga, Mbagala na Segerea ili kukidhi mahitaji makubwa ya maji kwa wakazi wengi wanaoishi maeneo hayo.
''Fanyeni utaratibu wa kukarabati miradi ya zamani kama hatua ya kwanza na ya haraka ya kuwapatia wananchi maji, wakati mkiendelea kutekeleza miradi mipya na mikubwa ambayo utekelezaji wake utachukua muda mrefu. Mmejikita sana katikati ya jiji, ambapo kwa sasa huduma hiyo imeimarika kwa kiasi kikubwa. Umefika wakati wa kuwekeza maeneo ya pembezoni kwa sasa, na wakazi hawa nao wafurahie huduma ya maji ya uhakika'', aliagiza Naibu Waziri Aweso.
Aidha, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji alitoa onyo kwa manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam kutowapa kazi wakandarasi wasio na uwezo. Pia, kuchukua hatua stahiki kwa wakandarasi wote wanaosuasua katika utekelezaji wa miradi, huku akiwahakikishia wakandarasi wote kulipwa fedha zao kwa wakati ili wasikwame katika utekelezaji wa miradi hiyo.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu walipokuwa kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala Kuu kujionea upatikanaji wa huduma ya maji katika shule hiyo.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akikagua mradi wa maji wa KIWICA uliopo Kijichi, Mbagala.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Usambazaji Majisafi DAWASCO, Mhandisi Aaron Joseph (mwenye miwani) eneo la Kijichi Mbagala.

GSM YAMPATA MSHINDI WA KWENDA HONG KONG

$
0
0
Meneja Masoko wa GSM Farida  Rubanza akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mshindi wa shidano la Disney ,Consolata Mlebusi mkazi wa Mbezi Beach  ambapo ataenda mapumziko.
Mwakilishi wa wateja aliyezungusha gurudumu hilo na kuokota ticket ya mshindi Edward Laurent Kapwapwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupatika mshindi wa shindano hilo.

Mshindi wa shidano la Disney lililokuwa linaendeshwa na kampuni ya Maduka ya GSM leo limefikia mwisho baada ya leo kuchezeshwa droo na kupata mshindi ambaye ataenda mapumziko huko Hong Kong.

Akizungumza wakati wa uchezeshaji shidano hilo Meneja Masoko wa GSM Farida  Rubanza amemtangaza mshindi wa shidano hilo kwa ni Consolata Mlebusi mkazi wa Mbezi Beach , mshindi huyo  amepatikana baada ya ticket yake kuokotwa baada ya kuzungushwa kwa gurudumu lenye Mamia ya ticket.

Aidha amewataka wateja wa maduka ya GSM kuendelea kutumia huduma zao kwa kuwa zina ubora .
Kwaupande wake  Mwakilishi wa wateja aliyezungusha gurudumu hilo na kuokota ticket ya mshindi Edward Laurent Kapwapwa, ameishukuru kampuni ya GSM kwa kuendesha shindano hilo kwa uwazi.

"Mimi nimekuja kununua vitu hapa dukani nimetoka Mtwara nimekuja hapa Dar es Salaam kwa kazi zangu nimeitwa tu na wameniomba  niokote ticket, kwanza huyu mshindi hata simfahamu, kwakweli nimeona shindano hili ni la haki na kweli  nawaomba watu wote na wateja wa GSM  kuendelea  kutumia bidhaa zao hata mimi hapa nimekuja kununua bidhaa zao" Alisema

Mshindi huyo atawasili muda wowote kufahamishwa taratibu za safari yake  amabapo kwa mujibu GSG anatakiwa kusafiri yeye na familia yake jumla wawe wanne, shindano hilo limedumu kwa muda wa miezi miwili Lilianza December 2017 hadi February 4,na leo kuchezeshwa droo.

WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

WAKURUGNZI Watendaji saba wa kampuni tano za jijini Dar es Salaam wanatarajia kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 23 na Machi 12, mwaka huu.

Imeelezwa Wakurugenzi hao ambao walitakiwa kusomewa mashtaka yao leo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ni, lakini ilishindikana kwa kuwa hawakuwepo ni Omari Mgwaya na Nelson Rubagumisa wa kampuni ya Panacom Solution Co.Ltd, Issa Lupigila wa kampuni ya Upame Co.Ltd na  Osca Chongola wa kampuni ya Nolc Engineering Company, 

Wengine ni,Petronia Mrosso na Fritz Masanjo wa Kampuni ya Skyscape International Co.Ltd, na Josephat Mwita wa kampuni ya Tan Geo Info Consult,

Washtakiwa  hao wanakabiliwa na kesi za jinai namba 38, 31, 37, 39 na 32 zote za mwaka 2018, 

Katika kesi inayomkabili Osca, Wakili wa Serikali Dereck Mukabatunzi alidai kesi ilipangwa kwa ajili ya mshtakiwa hiyo kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Wakili wa mshtakiwa,Hassan Kihangio aliieleza mahakama kuwa mteja wake ni mgonjwa, anamatatizo katika pingili za uti wa mgongo, yupo hospitali amepewa mapumziko akaomba apangiwe tarehe nyingine ili afike asomewe mashtaka.

Kutokana na suala la ugonjwa upande wa mashtaka haukuwa na pingamizi na Hakimu Nongwa amahirisha kesi hiyo hadi Machi 12, 2018.

Naye Wakili wa Serikali Emmil Kilia aliyetakiwa kumsomea mashtaka Issa Lupagila alidai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa mashtaka yanayomkabili lakini hawakuweza kumpata ili wampatie wito wa mahakama afike mahakamani hivyo wakaomba hati nyingine ya mwito.

Kilia amedai wanaendelea kumtafuta baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa aliamuru wapewe hati ya wito na kesi imeahirishwa hadi Machi 12,2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama atakuwa amepatikana ama la.

Katika kesi inayomkabili Joseph Mwita, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benson Mangowi alieleza mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo hawajaweza kumpata hivyo aliiomba mahakama itoe hati ya wito ili waweze kumpata na kumsomea mashtaka yanayomkabili.

Kesi imeahirishwa hadi Machi 12,mwaka 2018.

Katika kesi inayomkabili Omari Mgwaya na Nelson Rubagumisa, Wakili wa Serikali,Emma Msofe aliieleza Mahakama  washtakiwa hao hawajaweza kuwapata ili kuwapatia hati ya wito wa mahakama.

Hivyo aliiomba wapatie hati ya mwito nyingine ili waweze kuwapatia washtakiwa hao wafike mahakamani kusomewa mashtaka yanayowakabili.Kesi imeahirishwa hadi Machi 12,mwaka 2018.

Katika kesi inayowakabili, Petronia Mrosso na Fritz Masanjo, Wakili was Serikali, Dereck Mukabatunzi alieleza washtakiwa walipokea hati ya mwito wa mahakama ila wapo nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 23, mwaka 2018 ambapo washtakiwa hao watasomewa mashtaka yanayowakabili.

AZAM FC, KMC KUMENYANA CHAMAZI

$
0
0
Na Agness Francis Globu ya jamii 
Mabingwa Afrika Mashariki na kati AzamFc watashuka dimbani kufuana na  timu ya  KMC FC  katika kuwania Kombe ya FA hukuwa wakiwa wenyeji wa kikosi hicho. 

AzamFC watakuwa wageni dhidi ya timu hiyo katika Uwanja wa Azam Complex ambapo KMC watautumia uwanja huo kama wa nyumbani, ikiwa mchezo huo utapigwa saa moja jioni. 

Akizungumza Ofisa Habari wa AzamFc Jaffary Iddy Maganga katika ofisi zao Mzizi Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa timu imesharejea nyumbani kutokea Mkoani Iringa ambapo walikuwa na mchezo wao dhidi ya Lipuli waliotoka sare bila kufungana. 

Aidha amesema kikosi kimeshaingia kambini na kimeshaanza mazoezi  katika kuelekea mtanange huo dhidi ya KMC. 

"Mchezo ni mgumu unajitahid juhudi za hali ya juu ukizingatia  kikosi hicho ni kizuri na itakuwa lazima mmoja atoke ili kuelekea Mchuano wa Robo Fainali kombe la FA," amesema Maganga.

Hata hivyo,wachezaji wa AzamFC walikuwa majeruhi karibuni wote wako fiti isipokuwa Kiungo mkabaji Himidi Mau Mkami. 

"Tutaendelea kumkosa Himid Mau takribani kwa wiki 3 kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ambapo Daktari amesema kuwa ana uvimbe uliovilia damu kwenye goti lake,"amesema Jaffary Maganga.
Afisa Habari wa AzamFc Jaffary Iddy Maganga, akizungumza na waandishi wa habari  leo katika Ofisi zao Jijini Dar es Salaam kuhusu mchezo wao dhidi ya KMC utaorindima pale Azam Complex Chamazi siku ya Jumamosi tarehe 24 majira ya sa 1 Usiku ambapo watakuwa wageni wa mchezo huo.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI MEATU MKOANI SIMIYU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kwenye ujenzi wa mradi wa bwawa la maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo la Mwanjolo wilayani Meatu mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa bwawa la maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo la Mwanjolo wilayani Meatu mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandishi Isack Kamwelwe akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa bwawa la maji Mwanjolo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasalimia wananchi wa Mwanjolo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bwawa la Maji Mwanjolo, Meatu. (picha na ofisi ya Makamu wa Rais)

BENKI YA EQUITY YAZINDUA HUDUMA YA EAZZYBANKING KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WAO BILA STRESS

$
0
0
 Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.
BENKI ya Equity imezindua huduma za kibenki kwa njia ya mtandao  ambapo wateja wao sasa watapata huduma mahali popote kupitia  simu za mkononi, tablets na kompyuta za mezani na mpakato.

Huduma hizo watazipata kupitia Eazzy Banking kwa kufanya miamala  kirahisi iwe usiku au mchana, wakiwa nyumbani, au ofisini na kubwa zaidi sasa watakuwa na nafasi ya kuokoa muda na gharama.

Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Eazzy Banking,  Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Joseph Iha amesema kuwa huduma  hizo mpya zitatoa fursa kwa wateja kufanya miala mahali popote.

"Huduma za Eazzy Banking zitaambana na EazzyBanking App, app ya  kimataifa ya masuala ya kifedha inayounganisha huduma za laini za simu na kuwawezesha wateja kutuma fedha na pia kufanya malipo kupitia simu zao popote walipo na wakati wowote.

"EazzyBanking ni rahisi kuianzisha na hutoa huduma za kipekee kama  kutuma fedha kwenda akaunti za benki au mitandao ya simu, kuomba na kulipia mikopo , kulipia bili(ankara) na aina ya huduma za malipo," amesema Iha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity, Joseph Iha akizungumza na wageni waalikwa na wanahabari waliofika katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja kufanya miamala yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa.
Wateja walihudhuria uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayotolewa na benki ya Equity jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Joseph Iha akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali mara baada ya uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja kufanya miamala yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa. Pembeni ni wakurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo ikiongozwa na Simbeye.

NAIBU WAZIRI MHANDISI STELLA MANYANYA AFANYA ZIARA MKOANI ARUSHA

$
0
0
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya, akifungua rasmi kongamano la kimataifa la Asali (CESO) likiwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa asali nchi.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (wa pili kutoka kulia) akishiriki kongamano la kimataifa (CESO) la kujadili changamoto katika uzalishaji wa asali nchini, limefanyika katika ukumbi wa Mount Meru Hotel, Arusha tarehe 19/2/2018.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya, akimsikiliza Mhandisi Mkuu wa Utafiti kutoka Shirika la Usanifu Mitambo (TEMDO) akifungua rasmi kongandugu Patrick Kivanda.
Wafanyakazi wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya, alipotembelea kiwanda cha SUNFLAG.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya, akiangalia nguo mbalimbali zinazotengezwa na kiwanda cha SUNFLAG cha jijini Arusha, pembeni ni Mtenaji mkuu wa Kiwanda ndugu Ajay Shah.

BEI ZA MATUNDA SOKO LA MABIBO KWA SIKU YA LEO

$
0
0
Fatilia bei za matunda mbalimbali katika masoko ya jiji la Dar es Salaam kwa kuanzia Soko la Mabibo .
 Baadhi ya wanunuzi na wauzaji katika soko hilo wakiwa katika pilikapilika sehemu ya ushushaji ndizi katika mikoa mbalimbali.
 Bei ya Ndizi inauzwa katika sokoni hapo inauzwa kati ya Sh.15000 hadi Sh.25000 kwa mkungu.
 Bei ya Parachichi ni kati ya Sh.200 hadi Sh.700.
 Bei ya Passion kwa kilogram moja ni sh. 2000. 
 Bei ya tikiti kati ya sh. 1000 hadi 3000 katika soko la Mabibo.
 Bei ya Boga ni sh. 1500 hadi sh.3500 katika soko la Mabibo jijini Dar es Salaam.
 Bei ya Embe ni Sh.600 hadi 700 katika soko la Mabibo.
Bei ya Ndizi Mbivu inauzwa kati ya Sh. 100 hadi Sh.150.

Taarifa hizi zimeandaliwa na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

IDARA YA UHAMIAJI YAWABAINI WAFANYAKAZI 37 KWA KUKOSA VIBALI VYA KUFANYA KAZI NCHINI KATIKA CHUO CHA KAMPALA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii 
IDARA ya Uhamiaji nchini imefanya operesheni katika Chuo Kikuu cha Kampala (Kampala International University - KIU) kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar es salaam na kubaini uwepo wa wafanyakazi 37 wanaofanya kazi bila kuwa na kibali maalumu. 
Akizungumza na Michuzi Blog leo, Msemaji wa Idara hiyo, Bw. Ally Mtanda amesema kuwa baada ya kuwabaini wafanyakazi hao wanaofanya kazi kinyume na utaratibu idara hiyo imechukua maelezo kutoka kwa kila mfanyakazi na amesema baada ya uchunguzi kukamilika wengine wanaweza kwenda mahakamani na kwa wengine taratibu zingine za kiuhamiaji zitaendelea. 
Amesema kuwa kwa sasa wanachukua maelezo ili kuweza kujiridhisha juu ya kuwepo kwa na kafanya kazi nchini hapa. Bw. Mtanda amesema kuwa operesheni hiyo ni endelevu katika kubaini wahamiaji haramu na wanaoishi na kufanya kazi bila vibali nchini.

RC MORO AUNDA TIMU YA VYOMBO VYA DOLA ILI KUHAKIKI MAJINA YA WAKAZI WALIOLIPWA FEDHA ZA FIDIA KUPISHA MRADI WA BWAWA LA KIDUNDA ILI KUBAINI HARUFU YA MALIPO ‘HEWA’

$
0
0
Na John Nditi, Globu ya Jamii Morogoro
MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ameunda timu maalumu inayojumuisha  vyombo vya ulinzi na usalama itakayoshirikiana na wataalamu wa uthamini  wa Serikali na wenyeviti wa vitongoji vya vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , halmashauri ya wilaya ya Morogoro   ili kuhakiki  upya majina  ya  waliolipwa  fedha za fidia na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya  kupisha ujenzi wa mradi  wa  bawawa la Kidunda .
Mkuu wa mkoa amelazimika kuunda timu hiyo baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi wa vijiji hivyo   wakati wa mkutano  wa  hadhara uliofanyika katika kijiji cha Bwila Chini  na kuhudhiriwa na mamia ya wananchi wa vijiji hivyo.
Dk Kebwe alisema  , ameiunda timu hiyo  licha ya pande zote kueleza kwa udani namna zoezi la uhakiki na uthamini wa  makazi ya watu wa vitongoji vinane  vya vijiji hivyo  kuelezwa kuwa zoezi hili lilifanyika  kwa uwazi ulioshirikisha  wenyeviti wao wa vitongoji na malipo kufanyika baada ya taratibu zote za kisheria kufuatwa.
Kwa nyakati  tofauti  baadhi ya wananchi waliopewa furasa ya kuuliza maswali wakidai kuwa wapo baadhi ya watu wamelipwa fedha za fidia  wakati zi  wakazi wa vitongoji vya vijiji hivyo  wakiwa hawana nyumba wala mashamba .
“ Nimelazimika niunde  timu  ya baadhi ya wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama  itakayoshirikiana na wataalam na viongozi wa serikali za vitongoji kuhakiki majina yote kwa ajili ya kujiridhisha  ili kubaini  endapo madai  ya  wananchi  yanaukweli ama laa   na yakiwa na  ukweli hatua za kisheria zitachukuliwa  kwa wahusika” alisema Dk Kebwe.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kushoto)  akifungua kikao cha kusikiliza kero za  wananchi  wa vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , halmashauri ya wilaya ya Morogoro  wakati wakiwasilisha changamoto mbalimbali  zikiwemo za malipo ya   fedha za fidia  kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)  kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi  wa  bawawa la Kidunda
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kushoto)  akiwasiliza kero za  wananchi  wa vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , halmashauri ya wilaya ya Morogoro  wakati wakiwasiisha changamoto mbalimbali  zikiwemo za malipo ya   fedha za fidia  kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)  kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi  wa  bawawa la Kidunda

 Sehemu ya wananchi  wa vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , halmashauri ya wilaya ya Morogoro  wakimsikiliza mkuu mkoa  huo Dk Kebwe Stephen Kebwe ( hayupo pichani)  wakati akitoa majawabu ya changamoto mbalimbali  zikiwemo za malipo ya  fedha za fidia  kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)  kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi  wa  bawawa la Kidunda 
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Kibena Kingo ( aliyesimama meza kuu) akitoa maenezo ya ufafanuzi  mbele ya mkuu  wa mkoa  huo Dk Kebwe Stephen Kebwe  ( hauonekani pichani) kabla ya kusikiliza changamoto za   wananchi  wa vijiji vya Bwila Chini na Kiburumo , kata ya Selembala , iliyopo kwenye halmashauri hiyo.
Mkazi wa kijiji cha  Bwila Chini kata ya Selembala halmashauri ya wilaya ya Morogoro akitoa kero yake kwa mkuu mkoa  wa Morogoro Dk Kebwe Stephen Kebwe ( hayupo pichani)   wakati wa mkutano wake wa kusikilkiza changamoto mbalimbali  za wananchi wa vijiji viwili cha Bwila Chini na Kiburumo ambao wamelipwa   fedha za fidia  kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)  ili  kupisha ujenzi wa mradi  wa bawawa la Kidunda. Picha na John Nditi. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

UNNewsKiswahili: Kuzaliwa CAR, Pakistan na Afghanistan ni tiketi ya kifo- Ripoti

FIFA WAONGEZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA KWA TANZANIA, MZUNGUKO WA NNE WA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUANZA KESHO

$
0
0

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA limeongeza tiketi kwa Tanzania kwaajili ya fainali za kombe la Dunia zitakazochezwa Russia mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TFF, shabiki yeyote anayetaka kwenda kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia awasiliane na idara ya mashindano ya TFF kwa utaratibu wa namna ya kupata tiketi hizo.
Taarifa imesema Ngwe hii ya pili ya tiketi za Kombe la Dunia imefunguliwa Februari 15, 2018 na itafungwa Machi 12, 2018. Ikumbukwe awali FIFA walitoa tiketi 290 kwa Tanzania ili kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia kabla ya zoezi hilo kufungwa mwezi Januari na sasa imefunguliwa ngwe nyingine ya tiketi hizo.
Wakati huo huo, TFF imetangaza kwamba hatua ya mzunguko wa Nne (4) wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam inatarajia kuanza kesho Jumatano Februari 21, 2018. 
Taarifa imebainisha kwamba kwenye Uwanja wa Sabasaba Njombe kutakuwa na mchezo mmoja utakaowakutanisha mwenyeji Njombe Mji atakayecheza dhidi ya Mbao FC kutoka Mwanza saa 10 jioni. 
 Mechi nyingine za Kombe la Shirikisho la Azam zitaendelea Jumamosi Februari 24,wakati Singida United watakapowakaribisha Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Namfua saa 10 jioni na KMC watawaalika Azam FC saa 1 usiku Azam Complex. 
 Jumapili Februari 25, 2018 Buseresere watakuwa uwanja wa Nyamagana Mwanza saa 8 mchana kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro,Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam saa 10 jioni wakati Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania saa 1 usiku Azam Complex Chamazi. 
Jumatatu Februari 26, 2018 kutachezwa mechi mbili Kiluvya United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko atembelea mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira

$
0
0

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi na watumishi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe na Kyela Mkoani Mbeya katika ukumbi wa ofisi za Mgodi wa Kiwira zilizopo katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Leo Februari 2018.
 Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili mgodini
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua hali ya mitambo tangu kusimamishwa kwa uzalishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mwaka 2009 katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Leo Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua hali ya magari tangu kusimamishwa kwa uzalishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mwaka 2009 Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Leo Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, WazoHuru Blog
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images