Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

HESLB YAWAKUMBUSHA WAAJIRI KUZINGATIA SHERIA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewakumbusha waajiri nchini kote kuzingatia matakwa ya Sheria ya bodi hiyo inayowataka kuwasilisha orodha ya majina ya waajiriwa ambao ni wahitimu wa shahada au stashahada ili kuiwezesha Bodi kubaini wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Akizungumza na waandishi habari wakati wa wa hafla fupi ya kuwatambua baadhi ya waajiri wanaotimiza masharti ya Sheria ya HESLB, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo,Abdul-Razaq Badru amesema kuwa sheria hiyo inawataka waajiri kukata asilimia 15 ya mshahara ghafi wa mwajiriwa na kuwasilisha makato hayo kwa HESLB ndani ya siku 15 baada ya tarehe ya mwisho ya mwezi.

Amesema kuwatunuku ngao ni kutambua mchango wao katika kurejesha mikopo ili kuwasomesha watu wengine na kuwataka waajiri watekeleze sheria hiyo na kuongeza ufanisi wa shughuli za HESLB hususan katika urejeshwaji wa mikopo.

Taasisi zilizokabidhiwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PSPF), Benki ya NMB, Benki ya CRDB, Benki ya Stanbic, Deloitte Tanzania, Kampuni ya Sigara Tanzania, na Kamouni ya Coca Cola Kwanza. Kampuni nyingine ni Vodacom Tanzania, Nokia Solution Tanzania, Shule za Academic, Shule za Al-Hikma na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
 Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa HESLB Bw. Phidelis Joseph akizungumza na waandishi habari kuhusiana ufatilialiaji mkopo kwa walionufaika leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bw. Nzinyangwa Mchany (kulia) na Meneja Mawasiliano wa EWURA Bw. Titus Kaguo(katikati) wakionesha ngao ya utambuzi ya utambuzi walioyokabidhiwa leo (Jumatatu, Februari 19, 2018) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru (kushoto) kutambua mchango wa taasisi katika urejeshaji mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wafanyakazi wanufaika EWURA. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru (kushoto) akimkabidhi Mwakilishi wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Academic, Mariam Mtelesia ngao ya utambuzi wa ushirikiano wao katika kufanikisha kazi ya urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wanufaika ambao ni wafanyakazi katika taasisi yao.
Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo wa HESLB Bw. Phidelis Joseph akiongea leo (Jumatatu, Februari 19, 2018) jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwakabidhi waajiri ngao za utambuzi wa ushirikiano wao katika kufanikisha kazi ya urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wanufaika wafanyakazi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Muhimbili Yaanza Kutumia Teknolojia ya Kisasa Kutoa Majibu kwa Wagonjwa

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza majaribio ya utumiaji wa teknolojia ya kisasa katika Idara ya Radiolojia ili kuharakisha utoaji wa majibu ya wagonjwa ambao wanafika katika idara hiyo kwa ajili ya kupima vipimo mbalimbali ikiwemo MRI, CT-Scan, Utra Sound pamoja na X-ray.

 Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu maboresho ya utoaji wa huduma katika hospitali hiyo , Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Museru amesema kwa muda mrefu kumekua na changamoto ya utoaji wa majibu kwa wagonjwa kutokana na ripoti ya mgonjwa kupitia hatua kadhaa.
 Amefafanua kuwa teknolojia hiyo ambayo imewezeshwa na Chuo Kikuu cha Yale cha nchini Marekani itawawezesha wataalam kutoa majibu kwa wakati na haraka sanjari na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi hivyo kwenda kwenye ngazi za juu zaidi za huduma ya Raiolojia . 
 “Lengo letu ni kufanya majibu yatoke haraka na kuondokana na changamoto ya Daktari kutumia muda mrefu kuandika ripoti ya mgonjwa , kwani teknolojia hii ya kisasa inaondoa hatua karibu tatu ambazo zilimlazimu Daktari kuzipitia na hivyo mgonjwa kusubiri majibu kwa siku mbili hadi tatu hivyo kuanza kutumia mfumo huu ni hatua nzuri kwa hospitali na kwa wagonjwa, pia teknolojia hii itakapofanikiwa tutaipeleka pia katika Maabara yetu’’. Amesema Profesa Museru. 
 Akielezea kuhusu teknolojia hiyo Profesa Frank Minja ambaye ni mtaalam wa Radiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Yale , amesema mfumo huo unatafsiri kwa sauti majibu ya mgonjwa , huku ukichapa moja kwa moja majibu hayo na kisha kumfikia Daktari wakati huohuo. 
 “Mfumo huu unasaidia sana kutoa majibu kwa wakati, kuongeza tija katika utendaji kazi na hutumika sana nchini Marekani , mfumo huu unatumia vipaza sauti , na unahitaji Kompyuta yenye nguvu hivyo tumejikita zaidi katika kuongeza kumbukumbu kwenye Kompyuta zetu na ndio maana tumekuja na mtaalam wa IT ambaye anasaidia katika mfumo huu lakini pia anatoa elimu kwa wataala wa MNH ’’ amefafanua Profesa Minja. 
 Hospitali ya Taifa Muhimbili katika Idara ya Radiolojia kwa siku imekuwa ikihudumia wagonjwa zaidi ya 200, asilimia 20 hupima kipimo cha MRI, Asilimia 25 CT-Scan, asilimia 30 Plain X-Ray, asilimia 23 Utra Sound na asilimia 2 vipimo vingine.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital i ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari baada kupokea msaada wa teknolojia ya kurekodi majibu kwa wagonjwa. Teknolojia hiyo itasaidia wagonjwa kupata majibu kwa wakati kwani hakutakuwa na haja ya wataalamu kuandika majibu na badala yake itarekodi moja kwa moja.  Kulia ni Bwana Tarek  El- Shayal kutoka Taasisi ya Afya na Elimu ya nchini Marekani ambaye amewezesha kupatikana kwa teknolojia hiyo. Kushoto ni Mtaalamu wa Radiolojia, Profesa Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani.
 Baadhi ya wataalamu wa radiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani wakiwa kwenye mkutano huo. Wengine ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital i ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akimkabidhi zawadhi ya diary Bwana Tarek  El- Shayal kutoka Taasisi ya Afya na Elimu ya nchini Marekani.
Mtaalamu wa Radiolojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Frederick Lyimo akiwaeleza waandishi wa habari jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.

Rais wa FIFA kufanya majadiliano na waandishi wa habari za Michezo

$
0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Duniani (FIFA) Bw.Gianni Infantino atafanya mkutano wa majadiliano na vyombo vya habari kumi na mbili vya ndani ya nchi.
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika mkutano na wahariri wa habari za michezo uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
‘’Huu ni utaratibu wa viongozi wa FIFA kufanya mkutano wa mazungumzo na waandishi wa vyombo vya habari katika nchi wanazofanyia mikutano yao  ya kikazi kama ulivyo mkutano huu wanaotarajia kuufanya nchini Februari 22,mwaka huu,’’alisema Dkt. Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa Rais wa FIFA Bw. Gianni Infantino anatarajia kuwasili nchini alfajiri ya saa nane usiku kuamkia Februari, 22 2018 ambayo ndiyo siku ya mkutano na saa tatu asubuhi yake ataelekea ikulu kukutana na viongozi wakuu wa nchi.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw.Wilfred Kidau alitoa ufafanuzi kuhusu mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF kuwa umebeba ajenda mbalimbali  ikiwemo kujadili kuhusu Maendeleo ya Soka la Wanawake,Maendeleo ya Soka la Vijana,Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.
‘’Mkutano huu wa FIFA unatarajia kufanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam (JNICC) na ni sawa na kikao cha ndani ambacho kimelenga zaidi kujadili masuala ya maendeleo ya shirikisho hilo kwa ajili ya kuandaa agenda za mkutano mkuu wa FIFA wa dunia hivyo ombi kwa waandishi wa habari ni kuelewa dhana ya mkutano siyo kuwa wamenyimwa fursa bali huo ndiyo utaratibu’,’alisema Bw. Kidau.
Pamoja na hayo Bw.Kidau alifafanua kuwa miongoni mwa vyombo vitakavyopata fursa ya kushiriki majadiliano hayo baadhi yao watarusha mazungumzo hayo mubashara katika vyombo vyao hivyo wadau wengine wataweza kufuatilia tukio hilo moja kwa moja kupitia vyombo hivyo.
Halikadhalika Rais huyo wa FIFA anatarajia kuondoka nchini jioni mara baada ya kumaliza mkutano mwake na kushiriki chakula cha jioni.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi wa idadi ya waandishi watakaohitajika katika mkutano wakati wa mkutano wa  majadiliano na Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) Bw.Gianni Infantino utakaofanyika mnamo Februari 22, Mwaka huu na waandishi wa habari, katika mkutano wake na Wahariri wa Habari za Michezo (hawapo pichani) nchini leo jijini Dar es Salaam,Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Suzan Mlawi na Kulia ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidau
 Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw.Wilfred Kidau akitoa ufafanuzi kuhusu ajenda za mkutano wa Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) na CAF utakaofanyika nchini Februari 22,2018 katika mkutano na  Wahariri wa Habari za Michezo nchini  (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari kutoka Gazeti la Nipashe Bi Somoe Ng’itu akiuliza swali kuhusu utaratibu wa waandishi wa habari watakaofika Ikulu kuripoti tukio la Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) kukutana na viongozi wakuu wanchi, kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani ) leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wahariri wa habari za michezo nchini.

MAKAMU WA RAIS AWAHAKIKISHIA WANANCHI UPATIKANAJI WA DAWA ZA KUUWA WADUDU WAHARIBIFU WA PAMBA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Simiyu kuwa Serikali itamaliza kabisa tatizo la uhaba wa dawa za kuuwa wadudu waharibifu wa zao la pamba.
Mhe. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Busega kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Lamadi wakati akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Simiyu.
Amesema awamu ya kwanza ya dawa zimeshafika Simiyu kwa ajili ya kuwagawia wakulima wa pamba na akaahidi kuwa awamu ya pili ya kuleta dawa hizo inamalizika katika wiki inayoanza leo tarehe 19/02/2018, hivyo tatizo hilo litakuwa limekwisha.
“Ninajua kuna kiasi kikubwa cha dawa kinakuja Simiyu dawa itakuwa nyingi na wakulima wote watapata, hatuwezi kuacha nguvu zenu zipotee bure na kwa kuwa Simiyu ni mkoa wa Viwanda na ndiyo unazalisha pamba kwa wingi tutajenga viwanda vinavyotumia pamba, kwa maana hiyo hatuwezi kuiacha pamba iharibike” alisema.
Katika hatua nyingine Mhe.Makamu wa Rais wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Masanzakona baada kuweka  jiwe la msingi mradi wa maji wa Kiloleli amewahimiza wananchi kuchangia huduma za maji ili miradi ya maji iwe endelevu.
Amesema Serikali imedhamiria kumaliza kabisa tatizo la maji hapa nchini kwa kujenga miradi ya maji  hivyo ni vema wananchi wakaunga mkono juhudi za Serikali kwa kuchangia huduma za maji ili kusaidia miradi hiyo kujiendesha.
Akiwasilisha taarifa ya mradi wa Kiloleli kwa Makamu wa Rais, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Busega, Mohammed Said amesema mradi huo utagharimu jumla ya shilingi bilioni 1.6 mpaka kukamilika kwake mwezi Machi 2018  na utawahudumia wananchi wa vijiji vitatu vya Yitwimila B, Ihale na Ijitu.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Busega, Mbunge wa Busega Mhe. Raphael Chegeni amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa kwa wananchi wakati wa kampeni ya kuwapelekea mradi wa Maji wananchi wa kata ya Kiloleli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya kikazi ya siku nne(04) mkoani Simiyu, ambapo amepata fursa ya kuzungumza na wananchi pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Busega na Bariadi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Masanzakona leo wilayani Busega wakati wa ziara  yake wilayani humo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi Nyumba za Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika eneo la Nyaumata mjini Bariadi, wakati wa ziara yake wilayani humo, (kulia) Mkuu wa Mkoa huo , Mhe.Anthony Mtaka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Samia Suluhu Hassan (mwenye ushungi)  akikagua mradi wa maji wa Kiloleli wilayani Busega mara baada ya kuuwekea jiwe la msingi wakati wa ziara yake wilayani humo leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Samia Suluhu Hassan (kulia) akipewa maelezo na Meneja wa TBA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Likimaitare Naunga kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa huo mara baada ya kuuwekea jiwe la msingi leo Mjini Bariadi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Samia Suluhu Hassan (mwenye ushungi) akiweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Kiloleli wilayani Busega wakati wa ziara yake wilayani humo leo,(kushoto) Mbunge wa Busega, Mhe.Dkt.Raphael Chegeni.

MAMA SALMA KIKWETE AZITAKA MAMLAKA KUTOA HAKI KWA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete amezitaka mamlaka zinazojihusisha na utoaji haki, kuwasaidia wanawake kupata haki zao pindi wanapofungua mashauri ya kudai matunzo ya watoto. Amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la wanawake wanaolea watoto peke yao Single Mothers lililoandaliwa na kituo cha Radio cha Efm na Tv E.
Mama Salma amesema kuwa ni vyema wanaume kutambua majukumu yao ya kulea watoto kwani ni matakwa ya sheria watoto kulelewa na wazazi wote na sio kuwatelekeza  na kusema  watoto wanatakiwa kupata malezi mema  na ya upendo.
"Wanawake wanatekesa wanapotafuta haki zao  kutokana na unyonge na umasikini waliokuwa nao hivyo haki itendeke ili wanawake watembee kwa kujiamini katika nchi yao," amesema Mama Salma.
Aliongeza kuwa watoto wana haki ya kupata malezi mema kutoka kwa wazazi wote, elimu na afya ili kukua vizuri kiakili na kijamii.
"Ukiona wanawake wanatupa watoto jiulize kuna nini, bila tatizo hawawezi kutupa mtoto kwani anauma sana na ndio maana wengine wanapojifungua wanawaviringisha na kuwaweka mahali pazuri  akijua kwamba lazima watu watapita na kumuokota na kwamba atalelewa vizuri," alieleza.
Alisisitiza kuwa wanaume wanapaswa kutambua mazingira ya wake zao pindi wanapokuwa wajawazito na wawatunze, kuwathamini na kuwajali watoto.
Mama Salma alisema wasiwaachie malezi wanawake pekee kwani hakuna mtoto asiye na baba.
Pia alisema kuwa kampeni hiyo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi inayofanywa na Kituo cha Redio Efm na TV E inapaswa kuungwa mkono kwani ndio muelekeo wa Siku ya Wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8.
Naye, Mhariri wa kituo hicho cha redio, Scholastica Mazura alisema ni wakati wa kutoa elimu kwa vijana wanaoingia kwenye ndoa ili kupunguza idadi ya watoto wanaolelewa na mzazi mmoja. 
Alisema wanawake wengi wanaishi nje ya ndoa zao  kwa sababu mbalimbali na hivyo tatizo la malezi ya upande mmoja kuwa kubwa nchini.
Alieleza kuwa wanawake wamekata tamaa kwani wapo ambao wametelekezwa nao wanatelekeza watoto lakini wengine wanawalea kwa shida ili wapate malezi bora.
"Tuwacheke wanaume wanaokimbia majukumu yao na kuwaachia wanawake pekee kwa kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa kwani mnauwezo mkubwa wa kulea nasi tutawasaidia ili mjikwamue kiuchumi," alisema Mazura.
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete Akicheza na Wanawake waliojumuika katika Tamasha la Single Mothers lililoandaliwa na Efm Radio kwa kushirikia na Tv E
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wanawake walioshiriki Tamasha la Sinle mothers wakati anaingia ukumbini
 Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige akizungumza na kuwatia moyo wanawake hao na kusema pia hata yeye ni Single Mothers na bado maisha yanenda
 Mhariri wa kituo hicho cha redio Efm na Tv E, Scholastica Mazura akizungumza  na vijana wanaoingia kwenye ndoa ili kupunguza idadi ya watoto wanaolelewa na mzazi mmoja. 
 Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akipoke Zawadi kutoka kwa Meneja Tukio wa Efm na Tv E , Jesca Mwanyika.
 Mbunge wa Viti Maalum Rita Kabati akizungumza na wnawake wanaolea Watoto peke yao juu ya umuhimu wa kumtegeea Mungu hili kufanikiwa
 Waziri Mstaafu na Mbunge , Hawa Ghasia akieleza ugumu wa kulea mtoto peke yako na kuwatia moyo wanawake wote waliotelekezwa
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne na Mbunge wa kuteuliwa, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Efm Radio na Tv E ambao ni Single Mothers 

THE LAUNCH PAD YAWANOA VIJANA MABALIMBALI JUU YA MAHARIFA YA KAZI NA UJASILIAMALI

$
0
0
 Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw Makbel akizungumza juu ya mpango wa uanagenzi ulivyoweza kuwasaidia Vijana wengi kuingia katika sekta rasmi na kuweza kushindana na wasomi wengine ambao walipata ujuzi katika mfumo wa kawaida.
 Mwakilishi wa Tasisi ya Vijana Think Tank akizungumza namna Vijana wanavyotakiwa kufikiri zaidi hili waweze kujikwamua katika wimbi la kukosa ajira kwa kusema kuwa kila mwaka kundi la Vijana wasiokuwa na ajira wanavyoongezeka
 Mtaalamu wa Masula ya ushauri wa kujikwamua na ajira kutoka Shirika la kazi Duniani ILO, Comoro Mwenda akitoa somo ya namna vijana nini waweze kufanya hili kufikia malengo yao ya kuajiriwa au kujiajiri popote pale duniani
 Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Launch Pad Tanzania, Caroline Ndosi akizungumza wakati wa akiongoza Meza ya mjadal awakati wa kongamano la kuwajengea Vijana uwezo wa ujasiliamali na kuweza kuajirika katika Tasisi mbalimbali.
Sehemu ya Vijana kutoka sehemu mbalimbali ya Tanzania walioshiriki Kongamano la Kuongeza Maharifa ya ujasiliamali na kuajirika lililoandaliwa na Tasisi isiyo ya Kiserikali ya The Launch Pad

MASAUNI AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

$
0
0
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani  ya  Nchi. Lengo la baraza hilo ni kujadili utendaji na maendeleo ya kila idara katika kutimiza majukumu ya wizara. Kikao hicho kimefanyika  katika Ukumbi wa Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi Hamad  Masauni (watatu kulia), na  Naibu Katibu Balozi Hassan Simba Yahya (wanne kulia), wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Lengo la baraza hilo ni kujadili utendaji na maendeleo ya kila idara katika kutimiza majukumu ya wizara .Wengine ni  viongozi wa Chama cha Wafanyakazi  tawi la wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Thobias Andengenye, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala na Kamishna   wa Magereza anayeshughulikia  Utawala na Fedha, Gaston Sanga wakiimba  wimbo wa mshikamano wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, lengo la baraza hilo ni kujadili utendaji na maendeleo ya kila idara katika kutimiza majukumu ya wizara.Kikao hicho kimechofanyika katika Ukumbi wa Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akichangia hoja wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lengo la baraza hilo ni kujadili utendaji na maendeleo ya kila idara katika kutimiza majukumu ya wizara.Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.Wengine ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Thobias Andengenye(kushoto) na Kamishna wa Magereza anayeshughulikia  Utawala na Fedha, Gaston Sanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Thobias Andengenye,akichangia hoja wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lengo la baraza hilo ni kujadili utendaji na maendeleo ya kila idara katika kutimiza majukumu ya wizara.Kikao hicho kimechofanyika katika Ukumbi wa Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo.Wengine ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala na Kamishna   wa Magereza anayeshughulikia  Utawala na Fedha, Gaston Sanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, akichangia hoja wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MWANASHERIA WA MISUNGWI ASIMAMISHWA KAZI

$
0
0
*Ni baada ya  kuisababishia halmashauri hasara ya sh. milioni 279.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Alphonce Sebukoto na kuagiza achungunzwe na vyombo husika.
Amechukua hatua hiyo baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vema halmashauri hiyo na kuisababishia hasara ya sh. milioni 279.

Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Bw. Sebukoto leo (Jumatatu, Februari 19, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. 

“Mwanasheria utasimama kazi kuanzia leo na tuhuma zako zitachunguzwa kikamilifu na vyombo husika na uchunguzi ukibaini kama huna kosa utarudi kazini. Hatuta kuonea lakini hatuwezi kukuvumilia kwa utaratibu huo ulioufanya.”

Amesema mwanasheria huyo Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi aliidhinisha malipo ya sh.milioni 279 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Anthony Bahebe.

Waziri Mkuu amesema Bw. Bahebe aliishtaki halmashauri hiyo akidai kulipwa fedha kwa ajili ya kazi ya ukandarasi wa mradi wa maji Igenge uliojengwa na kampuni ya ukandarasi ya Seekevim. 

Amesema mradi huo ulianza 2014 na ulitakiwa ukamilike 2015. Mwanasheria huyo aliidhinisha malipo hayo wakati ambao tayari hati maalumu ya uwakilishi ilikuwa imekwisha tangu Desemba 2015.

“Mwanasheria amemlipa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kufanya kazi na Halmashauri baada ya kuifikisha Halmashauri yake Mahakamani. Amemlipa fedha wakati kazi yenyewe ilikuwa haijaisha na aliharakisha malipo hayo kipindi ambacho Mkurugenzi hayupo.”

Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi na matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesema fedha alizolipwa Bw. Bahebe zingeweza kutumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Awali, Waziri Mkuu alifungua mabweni ya watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Mitindo iliyoko wilayani Misungwi na kisha alikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 19, 2018.
Aliyekuwa Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Alphonce Sebukoto akiwa anamsikiliza waziri mkuu wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo.


SITA WAJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI

$
0
0
 Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akimkabidhi kadi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) Kata ya Mwalusembe, Abass Mjavile.
 Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akikabidhi bati 80 na mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa ofisi mbambali za chama cha mapinduzi kata ya Mwarusembe  zenye thamani y ash.milioni mbili.
 Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  wa Kata ya Mwarusembe  ambapo wanachama wapya sita walijiunga  na chama hicho kutoka Chama cha Wananchi (CUF).
 Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwakabidhi pikipiki kwa viongozi wa chama hicho kata ya Mwalusembe yenye thamani ya zaidi ya milioni mbili
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi  (CCM)  wa Kata ya Mwarusembe  wakisikiliza Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

FIFA: Mkutano wao hawataki Mtu zaidi ya viongozi wa TFF na Waandishi 10 tu

WCF YAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUMISHI WASIOCHANGIA MFUKO WA FIDIA

DKT. MATUZYA APIGWA 'FULL STOP' MIAKA MITATU KUJIHUSISHA NA UONGOZI WA VYAMA VYA MICHEZO

MAGAZETI YA JUMANNE LEO FEBRUARY 20,2018

MGIMWA ATOA BATI 590,MIFUKO YA SARUJI 220 UJENZI MADARASA KATA YA IHALIMBA

$
0
0
Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo likiwa kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi. 

Akizungumza na walimu wa kata hiyo mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.

“Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na walimu juu ya mambo aliyoyafanya kwenye kata hiyo kielimu ambapo ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kata ya Ihalimba
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na viongozi wa elimu ngazi ya wilaya kata na vijiji wakati wa mkutano baina ya viongozi hao na walimu wa shule za kata ya Ihalimba
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimkabidhi zawadi mmoja ya mwalimu aliyefanya vizuri darasani kwa kuongeza ufaulu 

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


TAKUKURU TANGA YAPOKEA TAARIFA 204 ZA VITENDO YA RUSHWA

$
0
0
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tanga (Takukuru) imepokea taarifa 204 za vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi wakizilalamikia idara mbalimbali za serikali na sekta binafsi.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2017.Alisema taarifa hizo ni ongezeko la taarifa 30 sawa na asilimia 17 ukilinganisha na kipindi cha miezi sita iliyopita ambapo taarifa zilizo pokelewa ni 174.

Aidha alisema katika taarifa hizo 52 zilihusu serikali za mitaa, ardhi/ mabaraza ya ardhi 33,vyama vya siasa 28,Polisi 23,Elimu 18,Mahakama 16,Afya 15,Kilimo 8,Tasaf 5,Bandari (TPA) 1,Maji 1,Ushirika 1,Uhamiaji 1,Tanesco 1 na Misitu 1.

Mkuu huyo alisema kati ya taarifa hizo 204 zilizopokelewa taarifa 92 zinaendelea kuchunguzwa wakati nyengine 66 uchunguzi wake ulikamilika na majalada kufungwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.Aliongeza kuwa taarifa 46 zilihamishwa kwenye idara nyengine kwa sababu zilikuwa zikihusiana na makosa chini ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2017.
Sehemu ya wanahabari mkoani Tanga wakifuatilia matukio katika mkutano huo.



TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA KANDA YA ZIWA, KUFANYIKA APRILI 1 UWANJA WA CCM KIRUMBA

$
0
0
Kampuni ya Msama Promotiosn Ltd inaandaa tamasha la Pasaka kanda ya ziwa likalofanyika mwanzoni mwa mwezi Aprili,litakalohusisha waimbaji wa nyimbo za injili mbalimbali hapa nchini,na kwamba litakuwa tamasha lile lile ambalo limekuwa likifanyika jijini Dar Es Salaam kwa miaka yote. 

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama amesema Tamasha la Pasaka Mwaka huu litafayika jijini Mwanza na mkoa wa Simiyu mnamo Aprili 1 na April 2 na baadaye kuendelea kwenye mikoa mingine. 

“Tamasha la pasaka safari hii linaanzia mkoani Mwanza na baadae mkoa wa Simiyu,na pia mikoa mingine,tamasha hilo kwa jiji la Mwanza litafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba, na baadae mkoani Simiyu katika uwanja wa Halmashauri mjini Bariadi’’,alisema Msama. 

Msama amesema kuwa tamasha hilo kwa Mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa,kwa maana ya eneo lakini mambo yote yaliyokuwa yikifanyika jijini Dar,yatahamia jijini Mwanza. 

Msama anawakaribisha wakazi wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake,kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia utukufu wa Mungu kwa njia ya kuimba kupitia waimbaji wa nyimbo za Injili . 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ,Alex Msama akizungumza mbele ya Waandishi wa habari,alipokuwa akieleza kuhusu mwanzo wa maandalizi ya tamasha la pasaka 2018,litakaloanzia kanda ya ziwa.

ALIKIBA, OMMY DIMPOZ, LAVALAVA, BEN POL, HARMONIZE NDANI YA MUONEKANO MPYA WA NYWELE

DAWASA,DAWASCO ZATAKIWA KUPELEKA HUDUMA ZA MAJI PEMBEZONI MWA JIJI LA DAR

$
0
0


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso (wa pili toka kulia) akiwa na katibu tawala wa Wilaya ya Temeke, Edward Mpogolo wakati wakipatiwa maelezo machache juu ya uharibifu wa miundo mbinu ya maji inayofanywa na wananchi wasio waaminifu wakati wa ziara ya Naibu huyo aliyoifanya katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kujionea miradi mbali mbali ya maji.


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso akiangalia moja ya mradi wa maji.


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Juma Aweso amezitaka mamlaka zinazohusika na usambazaji wa huduma ya maji safi na taka (DAWASA na DAWASCO) kuendelea kusambaza huduma pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.

Kauli hiyo ameitoa Februari 19, 2018 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake aliyoifanya katika manispaa ya Temeke na Ilala ili kuweza kujionea miradi mbali mbali iliyoanzishwa ili kuweza kuwafikia huduma ya maji kwa urahisi.

WAZIRI JAFO KUWAVALIA NJUGA WAWEKEZAJI WENYE MASHAMBA PORI AMBAYO HAWAKUYAENDELEZA

$
0
0
WAZIRI  wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi  Selemani Jafo amesema hawezi kuwavumilia hata kidogo baadhi ya wawekezaji ambao wamekuwa na tabia ya  kufanya  udang’anyifu kwa wananchi kutokana na kuchukua maeneo makubwa ya ardhi pasipo kuyaendeleza mpaka yanapelekea kuwa mashamba pori hivyo ameagiza yarudishwe katika mikono ya serikali za vijiji ili wananchi wenyewe waweze kuyaendeleza katika shughuli nyingine za kimaendeleo.

Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa wananchi wa kijiji cha Kimara Misale kilichopo kata ya Mafizi katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ambapo amekwenda kwa ajili ya kuweza kujionea  na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuweza kusikiliza changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa jimbo lake.

Amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la mashamba pori katika baadhi ya maeneo  ambayo kwa kipindi cha muda mrefu  yametelekezwa hivyo  ameahidi kulivalia njuga suala hilo kwa lengo la kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kurudishiwa maeneo yao ambayo yamechukuliwa na watu wachache ambao wameshindwa kabisa  kuyaendeleza kama inavyostahili.
 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha  kimara misale iliyopo kata ya Mafizi Wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbai mbai ya maendeleo na kuweza kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi ii kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani wakiwa katika mkutano wa adhara kumsikiliza Waziri jafo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kujionea miradi mbai mbali ya kimaendeleo inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na nguvu za wananchi wenyewe.(PICHA  ZOTE NA VICTOR MASANGU)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images