Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

DED UKEREWE APEWA SIKU TATU KUELEZA MATUMIZI YA SH. MIL. 350 ZA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Frank Bahati akijibu maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mkutano kati ya Waziri Mkuu na watumishi wa Halmashauri hiyo
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  madawati  ya madarasa ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Pius  Msekwa wilayani Ukerewe Februari 18, 2018. Wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mabweni mawili ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Pius Msekwa wilayani Ukerewe Februari 18, 2018. Wasita kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa wilayani Ukerewe
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijaza  maji katika ndoo ya Janet Magayi (kushoto) wakati alipozindua  mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa wilayani Ukerewe, akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati aeleze amepeleka wapi zaidi ya sh milioni 350 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali. 
Ametoa agizo hilo Jumapili Februari 18, 2018 wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. 
Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumia kuona fedha inazopeleka katika halmashauri hiyo kwa ajili ya kugharamia miradi na kulipa madai ya watumishi zinatumika kinyume na maelekezo. 
Amesema miongoni mwa fedha hizo ni sh. milioni 451.47 za miradi ya miradi ya maendeleo (CDG), ambapo zilizotumika ni sh. milioni 221.9 tu.” Namtaka Mkurugenzi na Muweka hazina wa Halmashauri hii Bw. Peter Molel tarehe 21 waje Mwanza wanieleze walikopeleka fedha hizo.” 
Waziri Mkuu amesema fedha zingine ni sh. milioni 50 za ziizotolewa na Serikali kwa ajili ya kulipa madai mbalimbali ya watumishi kama likizo ambapo zililipwa sh. milioni 13 na zingine hazijulikani zilipo. 
Pia Serikali ilitoa sh. milioni 65 za kugharamia mradi wa umwagiliaji wa Bugorola ambazo nazo hazijulikani zilipo pamoja na sh. milioni 84 zilizotolewa kwa ajili ya kulipa motisha kwa walimu ambapo zilizolipwa ni sh. milioni 60 tu. 
“Kama mlidhani Ukerewe ni sehemu ya kutafunia fedha za umma mmekosea kwa sababu Serikali haiwezi kuvumia haya, Mkurugenzi umeaminika na kupewa dhamana ya kusimamia rasilimali za umma lakini unafanya tofauti.”
Waziri Mkuu amesisitiza kwamba lazima viongozi hao wahakikishe fedha zinazopelekwa na Serikali katika Halmashauri zao zikiwemo za utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, uvuvi zinatumika kama ilivyoelekezwa na si vinginevyo. 
Pia Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza asimamie utendaji wa viongozi na watumishi katika  wilaya zote za mkoa huo na kisha kutoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, Bw. John Mongella. 
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo wasikubali kugawanywa kwa sababu ya maslahi ya watu ambayo hayana tija kwao na hata kwa wananchi wa wilaya hiyo.  
Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kubaini kuwepo kwa mgogoro kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Bahari pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. George Nyamaha ambao wamekuwa wakiwagawa watumishi. 
Amewataka viongozi hao kurekebisha tofauti zao kwa sababu mgogoro wao umesababisha watumishi kugawanyika, hivyo kuwaumiza wananchi wa wilaya ya Ukerewe kwa kushindwa kuwahudumia vizuri jambo ambalo halikubaliki.

Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Kwanza

$
0
0
Picha na Makala na Josephat Lukaza
- Dog Tips Tanzania
Mbwa ni mnyama kama wanyama wengine na pindi unapofikiria kufuga mbwa basi kwanza Jiulize Maswali yafuatayo. Moja Upo tayari kumuhudumia mbwa wako kwenye Chakula, Maradhi, Matibabu, Mafunzo na Kutoa Muda wako wa angalau kuanzia nusu saa  mpaka masaa mawili kwaajili ya kukaa nae, kucheza nae na uangalizi? 
Kama jibu ni HAPANA basi fahamu kuwa hujafikia hatua ya kufuga Mbwa ni heri uache maana vinginevyo yatakuwa mateso kwako na kwa mbwa mwenyewe. Mbwa anahitaji upendo kama ambavyo Binadamu tunavyowapenda binadamu wenzetu na hata kuwahudumia pale wanapokuwa wagonjwa basi na Mbwa ni hivyo hivyo unapoamua kufuga mbwa fahamu ya kuwa naye  ni mnyama kama mnyama mwingine ambapo akiumwa anahitaji matibabu. 
Leo tutaangalia Makundi mbalimbali ya Mangonjwa yanayoweza kumshambulia mbwa, mnyama anayekaribia uhusiano na mbwa, na hata binadamu pia.
Leo tutaangazia Makundi Mawili tu huku Makundi mengine yataangaziwa Katika post zetu zijazo kikubwa ni endelea kufuatilia post zetu kupitia Hapa DOG TIPS TANZANIA ili upate ufahamu na kuweza kutunza vizuri mbwa wako. Kuna aina nyingi ya magonjwa ya mbwa na magonjwa hayo tutayafahamu kupitia katika makundi haya mbalimbali. Makundi hayo Mawilin ni kama yafuatavyo:
1: VIRAL INFECTIONS
Viral infections ni magonjwa yanayosababishwa na virusi kutoka kwa mnyama mmoja kwenda kwa mnyama mwingine ambapo magonjwa haya yapo mahususi kwaajili ya mbwa na hata binadamu. Katika Kundi hili la Viral kwa mbwa kuna magonjwa kama vile Rabies (Kichaa cha Mbwa), Canine parvovirus ,Canine coronavirus, Canine distemper ,Canine influenza, Infectious canine hepatitis , Canine herpesvirus , Pseudorabies na Canine minute virus Haya ni baadhi tu ya magonjwa ambayo ni kwaajili ya mbwa lakini pia yapo ambayo yanaweza kumdhuru binadamu pia kama hatochukua tahadhari mapema. >>>  SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, ELIAS KWANDIKWA ATOA UFAFANUZI WA HOJA MBALIMBALI ZA WANANCHI WA MARAMA WILAYA YA MKINGA MKOANI TANGA

Taswa FC yang'ara Media Day ya DSTV

$
0
0
Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imewafundisha soka timu ya MultiChoice Tanzania (DSTV) baada ya kushinda katika mchezo maalum wa ‘Media Day’ uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam.
Taswa FC ilianza mchezo huo kwa ‘dharau’ na kujikuta ikipachikwa bao katika dakika ya tatu ya mchezo. Bao hilo liliwashtua timu hiyo ya waandishi wa habari na kusawazisha katika dakika 11 kupitia kwa Hare Temba baada ya pasi safi ya Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
Bao hilo liliwaduwaza DSTV iliyokuwa ikiongozwa na  Meneja Uhusiano wake, Johnson Mshana ambaye pamoja na kung’ara, walijikuta wakipachikwa bao la pili kupitia kwa Wilbert Molandi kufuatia mpira wa kona wa Majuto. DSTV ilisawazisha katika dakika za mwisho wa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili ilikuwa cha ‘kiama’ kwa DSTV baada ya kupachikwa bao la tatu na Majuto kufuatia mpira wa faulo nje ya eneo la hatari.
Baada ya bao hilo, DSTV walinyong’onyea na kupachikwa mabao matatu yaliyofungwa na Zahoro Mlanzi baada ya pasi safi  kutoka kwa Saidi Seif na Ibrahim “Maestro” Masoud.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana alisema kuwa  mbali ya matokeo hayo, lakini lengo lao limefanikiwa kwa kuweza kuwakutanisha waandishi wa habari za michezowa vyombo mbalimbali kwa kushirikiana na timu ya Taswa FC.
“Lengo la kukutana ni kufurahi pamoja ikiwa ni kucheza, kula na kunywa baada ya kazi kubwa ya kuendeleza gurudumu la maendeleo, waandishi wamekuwa na ushirikiano mzuri na sisi katika shughuli mbalimbali,” alisema Mshana.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary aliipongeza MultiChoice Tanzania kwa kuandaa halfa hiyo ambayo iliwakutanisha waandishi wa habari si chini ya 250.
“Ni faraja kwetu kujumuika hapa, mara ya kwanza tulikutana katika ukumbi wa Nyambizi na kujadiliana masuala mbalimbali, japo tulikuwa wachache, hapa wigo umeongezeka na tunaamini tutakuwa tukifanya hafla kama hizi mara kwa mara,nawashukuru sana,” alisema Majuto.
 Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC, katika picha ya pamoja na  timu ya MultiChoice Tanzania (DSTV) kabla ya mchezo wao maalum wa ‘Media Day’ uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
Mpambano kati ya Taswa FC na  MultiChoice Tanzania (DSTV) katika  mchezo wao maalum wa ‘Media Day’ uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.

daraja la kilombero mkoani morogoro lakamilika

$
0
0
Hali ya "Sanda Mkobani" ilivyokuwa wakati wa kuvuka mto Kilombero mkoani Morogoro kabla ya ujenzi wa daraja.
Ujenzi wa Daraja la Mto Kilombero uliopangwa kukamilika mwezi Februari 2017, sasa umekamilika kwa 100% na liko tayari kuzinduliwa.  Daraja hilo linalounganisha wilaya mbili za mkoa wa Morogoro (Ulanga na Kilombero) pamoja na Mkoa wa Ruvuma, litaokoa maisha ya wananchi wa wilaya hizo ambao katika kipindi chote cha mwaka walikuwa wakipata shida kuvuka mto huo huku shughuli za usafirishaji wa mazao ya mpunga, ufuta, mahindi, ufugaji na madini zitarahisishwa,  kuongeza pato na kukuza uchumi wa Taifa.Pia kukamilika kwa daraja la Mto Kilombero kutarahisisha usafiri kutoka Dar kwenda Songea – Ruvuma ambapo ni mbali mfupi sana kwa kupitia Mikumi-Ifakara-Mahenge mpaka Songea kuliko kupitia Iringa-Njombe mpaka Songea.

MAGAZETI YA JUMATATU LEO FEBRUARY 19,2018

MICHUZI TV USO KWA USO NA WAKUVANGA

MSAADA UNAHITAJIKA KWA KIJANA JONES MBWAMBO.

$
0
0
KIJANA JONES MBWAMBO ANASUMBULIWA NA TATIZO LA UVIMBE KATIKA UTI WA MGONGO AMBALO LIMESABABISHA KUPOOZA KWA MWILI WOTE. ANATAKIWA KUPELEKWA NCHINI INDIA KWA MATIBABU. 

GHARAMA ZA MATIBABU NI SHILINGI MILIONI 30,  TUNAOMBA MSAADA WAKO ILI KUWEZA KUFANIKISHA MATIBABU HAYO NA KUOKOA UHAI WAKE. UNAWEZA KUTUMA FEDHA ZA MATIBABU KWA MPESA: 0754295650 AU TIGO PESA: 0716913937 JINA LA MPOKEAJI NI JAINA MSUYA MAMA WA JONES. AKAUNTI YA BENKI NI 0112020233500. 

TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU ZA DHATI NA MUNGU AWABARIKI NA KUWAZIDISHIA PALE MTAKAPOTOA.

MARA WAHIMIZWA KUTOA USHIRIKIANO WAKATI WA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI

BARAZA LA MADIWANI NYASA LASITISHA MKATABA WAKALA WA MAJENGO TBA

$
0
0
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, limestisha mkataba na wakala wa majengo Tanzania (TBA) kuendelea na ujenzi wa ofisi za Halmashauri hiyo kutokana na kushindwa kumaliza kazi kwa wakati

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MAJI UKEREWE

$
0
0
*Awataka viongozi wa wilaya wahakikishe unakuwa endelevu.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Bwasa katika mji wa Nansio wilayani Ukerewe na kuuagiza uongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha maji hayo yanatoka wakati wote na mradi huo unakuwa endelevu.
Waziri Mkuu alizindua mradi huo jana (Jumapili, Februari 18, 2018) wakati akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Alisema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama nchini.

Baada ya kuzindua mradi huo, Waziri Mkuu alizungumza na wananchi wa mji wa Nansio kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Getrude Mongella, ambapo alisema mradi aliouzindua katika kijiji cha Bwasa ni sehemu ya mradi wa maji wa Kazilankanda utakaohudumia vijiji 13 vya wilaya hiyo.

Alisema mradi huo unagharimu shilingi bilioni saba na unatekelezwa katika vijiji vya Muhula, Mahande, Namasabo, Namagondo, Kazilankanda, Malegea, Igalla, Kigara, Lutare, Busunda, Bwasa, Buhima, Hamuyebe  na utahudumia wakazi  68,038 pindi utakapokamilika.

Mkataba wa Mradi huo ulisainiwa Machi 2013 na unatarajiwa kukamilika ifikapo April, 2018, ambapo hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 5.637 sawa na asilimia 78.26 tayari zimeshatumika na mradi umekamilika kwa asilimia 92 na tayari baadhi vijiji vimeanza kupata maji.

Waziri Mkuu alisema mkakati wa Serikali ni kuwahudumia wananchi kwa kutatua kero zinazowakabili ikiwemo ya upatikanaji wa maji, ambapo imedhamiria kuendelea kusambaza huduma hiyo hadi vijijini ili kuhakikisha vyote vinapata maji.

Waziri Mkuu alisema Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, inayolenga kuwaondolea wananchi tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Waziri Mkuu aliwaambia wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini  ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Bw. Estomihn Chang’ah apange siku maalumu kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hususani za ardhi na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu huyo wa wilaya leo saa 3.00 asubuhi akiwa na watumishi wa Idara ya Ardhi akutane na wananchi wote wenye malalamiko ya ardhi ili ashirikiane nao katika kuyapatia ufumbuzi. Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko mengi ya wananchi yahusuyo masuala ya ardhi yaliyowasilishwa kwake kupitia njia ya mabango.

Alisema kwa sababu ya kutotekeleza wajibu wao ipasavyo kumekuwa na kero na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hivyo kusababisha wananchi kuwasilisha kero na malalamiko hayo wakati wa ziara za viongozi wakuu wa nchi.

Awali, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bw. Luhaga Mpina aliwaomba wananchi hao kutunza rasilimali zilizopo ndani ya ziwa Victoria na kujiepusha na uvuvi haramu kwa sababu unatishia uwepo wa samaki ndani ya ziwa hilo.

Waziri huyo alisema iwapo vitendo vya uvuvi haramu vikiachwa bila ya kuzuiwa kuna uwezekano mkubwa wa samaki kutoweka ndani ya ziwa hilo baada ya miaka miwili. Alisema tayari Serikali inaendelea na operesheni ya kupambana na uvuvi haramu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 19, 2018.

TAXIFY YAZINDUA HUDUMA MPYA ‘TAXIFY BAJAJ’JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Taxify, ambayo imejitanua katika utoaji wa huduma zake barani Ulaya na Afrika, leo imetambulisha huduma yake mpya ya ‘Taxify Bajaj’ ambayo ni App maalum kwa ajili ya Usafiri wa Bajaj huku wakiichagua Dar es salaam kuwa jiji la kwanza katika uzinduzi wa huduma hii.

Kupitia uzinduzi wa huduma hiyo, Taxify sasa imepiga hatua zaidi katika jitihada zake za kupunguza msongamamo jijini Dar es Salaam, mara baada ya uzinduzi wa App yake maalum kwa ajili ya usafiri wa teksi miezi miwili iliyopita.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Maendeleo Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki, Shivachi Muleji alisema, ‘Taxify Bajaj’ ni App mpya ya Taxify jijini Dar es Salaam ambayo inaunganisha watumiaji wa usafiri wa Bajaji na madereva ndani ya dakika chache.

"Tunafurahi sana kuanzisha huduma hii kwa mara ya kwanza kabisa jijini Dar es Salaam pia ni tumaini letu kuwa huduma hii itapokelewa vyema. Tunaamini kwamba huduma hii inaendana na utamaduni wa wakazi wa jiji hili na kwamba itatoa urahisi wa watu kuchagua usafiri anaoutaka kwa gharama nafuu pindi mtu anapotaka kufanya safari zake za mjini”

Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya 'Taxify Bajaji' mwishoni mwa juma. Application hiyo ni maalum kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa Bajaj kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. Taxify sasa inapiga hatua nyingine katika kuleta suluhisho la usafiri hapa jijini, baada ya uzinduzi wa App yake kwa ajili ya magari miezi miwili iliyopita jijini Dar es salaam. Gharama za Taxify Bajaji kwa kipindi hiki zitakuwa kama ifuatavyo ya kuanzia TZS; Sh 750, TZS 350 kwa kila kilometa moja. TZS 75 kwa dakika huku bei ya kiwango cha chini ikiwa ni Shilingi 2000

Shivachi Muleji, Meneja Maendeleo wa Taxify, Kanda ya Afrika Mashariki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya 'Taxify Bajaji' mwishoni mwa juma. Application hiyo ni maalum kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa Bajaj kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. Taxify sasa inapiga hatua nyingine katika kuleta suluhisho la usafiri hapa jijini, baada ya uzinduzi wa App yake kwa ajili ya magari miezi miwili iliyopita jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka.
Fenelisti Simon Metumba, Dereva wa Usafiri wa Bajaji jijini Dar es salaam akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya 'Taxify Bajaji'. App maalum iliyozinduliwa na kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa Bajaj kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. Taxify sasa inapiga hatua nyingine katika kuleta suluhisho la usafiri jijini Dar es Salaam, baada ya uzinduzi wa App yake maalum kwa ajili ya magari miezi miwili iliyopita jijini Dar es salaam.

BINSLUM ATAKA MSHIKAMANO COASTAL UNION

$
0
0
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Klabu ya Coastal Union,Hafidhi Kidoh kulia akisalimiana na mwandishi wa gazeti la Majira Tanga Mashaka Mhando kwenye halfa hiyo ya kupongeza wachezaji iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga 

UONGOZI wa timu ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” umetakiwa kushikamana na kutoruhusu migogoro na makundi yasiyokuwa na tija kwani yanaweza kukwamisha ndoto zao za kupata mafanikio katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara. 

Lakini pia waaache vurugu na chokochoko iwapo wanataka kupata mafanikio huku wakitakiwa kuangalie wale wachache watakaopelekea hali hiyo wasiwaunge mkono kwa kuonyesheni mfano wamewachoka. 

Hayo yalibainishwa na Mfadhili wa timu hiyo,Nassoro Binslum wakati akizungumza kwenye ghafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo sambamba na utolewaji wa zawadi baada ya kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort 

Alisema tatizo kubwa ambalo limekuwa likirudisha nyuma mafanikio ya timu hiyo ni majungu,fitina na makundi ndani na nje ya timi hiyo hivyo ni bora viongozi,wapenzi ,wanachama wakabadilika na kuongeza mshikamano  
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Coastal Union baada ya kupanda daraja kucheza Ligi kuu msimu ujao katika halfa iliyofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort Mjini Tanga kushoto ni Mwenyekiti wa timu ya Coastal Union Steven Mguto na Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum 
Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hemed Aurora
Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Mfadhili wa timu hiyo Nassoro Binslum kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.

TRA YATAIFISHA TENA GARI,BIDHAA MPAKANI NAMANGA

$
0
0
Na: Veronica Kazimoto-Arusha

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa mara nyingine ndani ya wiki mbili imekamata na kutaifisha tani moja ya sukari, mafuta ya kupikia katoni 10 na gari lililotumika kusafirisha bidhaa hizo kutoka nchini Kenya kupitia njia za magendo mpakani Namanga mkoa wa Arusha.

Meneja Msaidizi wa Forodha mkoani hapo Edwin Iwato alisema bidhaa hizo zimekamatwa usiku wa kuamkia leo na ni mali ya mfanyabiashara Paul Swai, ambaye alitumia gari namba T 496 AFE Nissan Carravan mali ya Christian Nko ambalo limetaifishwa pamoja na bidhaa husika.

"Tumemkamata mfanyabiashara mwingine aitwae Paul Swai akiwa anaingiza nchini bidhaa kutoka Kenya kuelekea mkoani Arusha kupitia njia za magendo bila kibali wala kulipa ushuru wa Serikali", alisema Iwato.

Iwato amefafanua kuwa tani moja iliyokamatwa ambayo ni mifuko 20 ya sukari ina thamani ya shilingi 2,200,000 na mafuta ya kupikia ambayo ni kilogramu 12 yana thamani ya shilingi 520,000.

Mfanyabiashara huyo pamoja na dereva wa gari lililotaifishwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria ya Forodha na bidhaa hizo baada ya kukaguliwa na kugundulika kuwa zinafaa kwa matumizi ya binadamu zitagawiwa kwa taasisi mbalimbali za Serikali zenye uhitaji kwa mujibu na taratibu zilizowekwa na TRA.

Hii ni mara pili katika mwezi huu ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania imekamata na kutaifisha bidhaa mbalimbali zikitokea nchini Kenya kupitia njia za magendo mpakani Namanga mkoa wa Arusha.

NAIBU WAZIRI DK. NDUGULILE AZINDUA BARAZA LA WATOTO MKOA WA SHINYANGA,AKABIDHI OFISI,KOMPYUTA

$
0
0
Baraza hilo lenye wajumbe 12 likiwa na mwenyekiti,makamu mwenyekiti,katibu na mweka hazina na wajumbe sita mmoja kutoka kila halmashauri na watoto wawili wanaowakilisha watoto wenye ulemavu. 

Akizungumza wakati wa kuzindua baraza hilo, mjini Shinyanga, Dk. Ndugulile aliupongeza uongozi wa mkoa wa Shinyanga na kuutaka kuendelea kulea baraza hilo na mikoa mingine kuanzisha mabaraza ya watoto. 

“Wizara inaunga mkono kuanzishwa kwa baraza hili na tumetoa kompyuta moja itakayotumika kwa kazi za baraza,tunapenda kuona haki za watoto zinalindwa na ni wajibu wa kila mmoja kuwalinda watoto ili kuhakikisha haki zao hazivunjwi”,alieleza. 

“Naomba wajumbe wa baraza hili muwe mabalozi wa watoto wengine,heshimuni wazazi na walezi,nendeni shule na mjijenge katika maadili na tabia njema,msikae kimya, mpoona haki zenu zinavunjwa toeni taarifa,serikali ipo tuna sheria za kuwalinda”,aliongeza Dk. Ndugulile. 
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile leo Jumatatu Februari 19,2018 amezindua Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga na kukabidhi rasmi ofisi na kompyuta kwa ajili ya baraza hilo. 
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa kuzindua Baraza la Watoto mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Februari 19,2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.Kushoto ni ni Kamishina wa Ustawi wa Jamii Dk. Naftali Ngo'ndi ,kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Wawakilishi wa watoto wanaounda baraza la watoto mkoa wa Shinyanga wakimsilikiza Dk. Faustine Ndugulile. 
Dk. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza la watoto mkoa wa Shinyanga.Wa kwanza kulia aliyeinama ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Rashid Mfaume. 


TASAF YAOKOA WATOTO KATIKA KAZI ZA UCHIMBAJI MADINI MKOANI KATAVI.

$
0
0
Na estom sanga - katavi.

Tatizo lililokuwa linaukabili mkoa wa Katavi la watoto kutoka katika kaya maskini kuacha masomo na kutafuta vibarua kwenye migodi ya machimbo ya madini,limepungua kwa kiwango kikubwa baada ya kuanza kutekelezwa kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bibi. Lilian Charles Matinga amesema hayo mwishoni mwa wiki alipofungua Warsha ya Wandishi wa Habari wa mkoa wa Katavi juu ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini .

Bi.Matinga amesema kupungua kwa tatizo la ajira ya Watoto kumetokana na moja ya masharti ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaohimiza watoto kuhudhuria masomo kwa zaidi ya asilimia 80 kwa mwezi ili waweze kupata huduma za Mpango.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amesema walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, wameanza kuboresha maisha kwa kujenga nyumba za kudumu huku wengine wakijiongezea kipato kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo kama ufugaji wa kuku,bata, nguruwe na wengine kukuza shughuli za kilimo.

Ili miradi ya Walengwa hao wa TASAF iweze kupata mafanikio yanayotarajiwa ,Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza Wataalam wa ugani kuweka mipango ya kuwatembelea walengwa na kuona namna ya kuwasaidia kuboresha miradi wanayoianzisha.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Mtaalamu wa Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhura Mdungi amesema baada ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kufikia takribani miaka minne sasa , katika maeneo mengi ya utekelezaji wa Mpango ,walengwa wameboresha maisha yao huku kukuwa na mafanikio makubwa katika nyanja za elimu, afya na uanzishaji wa miradi midogo midogo ya kiuchumi. 
Mkuu wa wilaya ya Mpanda ,Bi.Lilian Charles Matinga (aliyesimama) akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya waandishi wa habari juu ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Katavi. Kulia kwake na Mtaalamu wa Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhurua Mdungi na kushoto kwake ni Mratibu wa TASAF wa mkoa wa Katavi .
Mtaalamu wa Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhura Mdungi (aliyesimama) akitoa mada kwenye warsha ya waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF mkoani Katavi.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa mkoa wa Katavi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Mpanda Bi. Lilian Charles Matinga (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha juu ya kuwajengea uelewa wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Moja ya nyumba zilizojengwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwa kutumia ruzuku wanayopata kutoka TASAF katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

WAAJIRI WANAOTUHUMIWA KUTOJISAJILI MFUKO WA FIDIA KORTINI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

WAAJIRI  wa kampuni nne tofauti wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini  Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa kadhaa yakiwemo ya kushindwa kujisajili na kuwasilisha taarifa za shughuli wanazozifanya kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi [WCF].

Washtakiwa hao, Malakkara Semis na Shafeek M. Purayil ni Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya SPASH  INTENATIONAL CO. LTD. Silas Shemdoe na Deusdedit Samwel Kibassa ambao ni  Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya ENCC CONSULTANTS.

Wengine ni Wakurugenzi Watendaji wa LASAR LOGISTIC, Abshir Farah Gure na Farhiya Hersiwarsame, wakati Mshtakiwa mwingine ni Josephat Alexander ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KAMANDA SECURITY GUARDS CO. LTD.

 Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao na waendesha mashtaka tofauti wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Emilly Kiria mbele ya Hakimu Mfawidhi Victoria Nongwa. Wanashtakiwa kinyume cha Kifungu  cha 71 (1) (a) na 71 (4) cha Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi Sura ya 263 marejeo ya mwaka 2015.

Akisoma mashtaka yanayomkabili Joseph inadaiwa  Januari, mwaka 2018 walishindwa kujisajili na kutoa taarifa muhimu za shughuli zake na za wafanyakazi kwa Ofisa aliyeteuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF.

Ilidaiwa Januari 11, mwaka 2018 mshtakiwa huyo alishindwa kutoa taarifa mihimu za waajiriwa wake ikiwamo majina na mishahara ya wafanyakazi.

Katika kesi ya jinai namba 33 ya mwaka 2018, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benson Mangowi  alidai washtakiwa  Malakhara Semis  na Shafeek Purayil  wa kampuni ya Spash International Co.Ltd  Desemba 25,mwaka 2017 walishindwa kusajili na kutoka taarifa muhimu za shughuli za kampuni kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF.
  Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni ya Spash International Co  Ltd  Shafeek Purayil (kulia) na Japhet Alexander  wa Kampuni ya Kamanda Security Guard Co. Ltd, wakipelekwa mahabusu ya Mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 2018 baada ya kusomewa mashtaka mawili ya jinai kwa kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), na kuwasilisha taarifa za shughuli za Makampuni wanayoyaongoza kwa Mfuko huo. Washtakiwa wakipatikana na hatia wanakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka mitano (5), jela au faini isiyozidi shilingi milioni hamsini au vyote kwa pamoja.
Shafeek Purayil(mbele) na Japhet Alexander wakitoka mahakamani baada ya kusomewa mashtaka na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Bibi Victoria Nongwa.  
Meneja Matekelezo (Compliance Manager),  wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Victor Luvena akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo. Alisema washtakiwa wengine Zaidi watapandishwa kizimbani Jumanne Februari 20, 2018 kwa makosa hayo hayo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAJALIWA ATEMBELEA SHULE YA MSINGI YA MITINDO INAYOLEA NA KUSOMESHA WATOTO WENYE UALBINO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto wakati alipotembelea shule  ya msingi ya Mitindo wilayani Misungwi  na kufungua bweni la wavulana katika shule hiyo ambayo pia inalea  na kusomesha watoto wenye ulemavu wa ngozi , Februari 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua bweni la wavulana katika shule ya msing ya Mitindo wilayani Misungwi, Februari 19, 2018.Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella na watatu kulia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga,
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mdawati katika madarasa ya shule ya msingi ya Mitindo wilayani Misungwi baada ya kufungua bweni la wavulana shuleni hapo Februari 19, 2018. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hyo, S. Mafie.
Wazri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mtoto Januari  wa Shule ya Msingi ya Mitindo wilayani Misungwi ambayo pia inawalea na kuwasomesha watoto wenye ulemavu wa ngozi , Februari 19, 2018. Mtoto huyo siku zote amesisitiza kwamba baada ya kumaliza masomo yake akiwa mtu mzima angependa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania .
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na  watoto alipotembelea Shule ya Msingi ya Mitindo ambayo pia inalea na kuwasomesha watoto  wenye ulemavu wa ngozi wilayani Misungwi Februari 19, 2018. Mheshimiwa Majaliwa pia alifungua bweni la wavulana shuleni hapo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ULEGA AZIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI WA MKURANGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega amefanya ziara katika vijiji vya Kise, Kibululu na Kiparang'anda (B) Kata ya Kiparang'nda ili kujua changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi na kuweza kuzishughulikia kupitia Halmashauri pamoja Ofisi yake.
Akizungumza na wananchi wa Vijiji hivyo amesema wakati wa sasa ni kufanya wa maendeleo ya kweli bila kuangalia itikadi za vyama.
 Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kise Kata ya Kiparang'nda kuhusu changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi hao.
 Mkazi wa Mkuranga, Selemani Mpambika akiuliza swali kwa kwa Naibu Waziri Mifugo na  Uvuvi, ambae ni mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega wakati wa mkutano huo.
 Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa jimbo la Mkuranga,, Abdallah Ulega (alieshika kikombe cha kahawa) akiwa sambamba na Wazee wa Mkuranga kwenye kijiwe cha kahawa akipata kikombe cha kahawa pamoja ambapo pia walibadilishana mawazo juu ya maendeleo ya wilaya yao.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKONI SIMIYU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa wa Simiyu kuhakikisha kila shule ya sekondari inayojengwa inajengwa ikiwa na maabara.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu ikiwa siku yake ya kwanza ya ziara ya siku tano mkoani humo.

Makamu wa Rais ambaye alianza ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji uliopo Kiloleli ambapo mradi huo ukikamilika utasaidia kupatikana kwa maji safi na salama kwa vijiji vitatu na utagharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 80%.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Kiloleli ambao utafaidisha vijiji vitatu, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt. Raphael Chegeni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Masanza Kona, Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu.
Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt. Raphaele Chegeni akizungumza mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kusalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi barabarani eneo la Nyashimo kumsalimia Makamu wa Rais ambaye ameanza ziara ya siku tano mkoani Simiyu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za Viongozi wa Mkoa katika eneo la Nyaumata, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images