Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

DKT. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BODI YA UTALII (TTB)

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utaliii, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo Februari 20, 2018, amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Makao makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jijini Dar es Salaam na kuitaka kufanya kazi kwa kasi na ubunifu zaidi. 
 Akizungumza na viongozi wa Bodi hiyo, Dkt. kigwangalla amewataka kuongeza kasi zaidi katika kutangaza Utalii wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha studio ya kimataifa ya kutangaza vivutio vya Tanzania ndani na nje ya nchi kwa kutumia lugha mbalimbali za Kimataifa. 
 Aidha,amewataka kuharakisha zoezi la uwekaji wa mabango yanayotangaza Utalii wa Tanzania katika viwanja vya ndege hususani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam (JNIA). 
Amewataka pia kujikita zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuhakikisha inahuishwa mara kwa mara. 
 Pamoja na hayo, ameiagiza bodi hiyo, kushirikisha wadau mbalimbali wanaotoa huduma za Utalii ikiwemo madereva taxi na Marubani kwa kuwapa elimu ya kutangaza utambulisho wa Tanzania kupitia Utalii na vivutio vilivyopo. 
Akiwa katika ofisi hizo ndani ya jengo la Utalii House, alikagua ofisi mbalimbali za bodi hiyo pamoja na zile za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kupata maelezo ya shughuli zake kutoka wa maafisa wa Shirika hilo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Devotha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Devotha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.

Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na uongozi wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.


NAIBU WAZIRI DKT. NDUGULILE WAKATI AFUNGUA BARAZA LA WATOTO LA MKOA WA SHINYANGA

MHE BITEKO AWAHAKIKISHIA WANANCHI WALIOWAHI KUWA WAFANYAKAZI WA MGODI WA KIWIRA KULIPWA STAHIKI ZAO

$
0
0
Na Mathias Canal, Songwe
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amewahakikishia baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe na Wilaya ya Rungwe na Kyela Mkoani Mbeya kuwa serikali inamalizia mchakato wa uhakiki wa madeni yote ya wadai hivyo pindi itakapomaliza mchakato huo wadai wote watalipwa madeni yao.
Naibu Waziri, Mhe Biteko ametoa kauli hiyo leo 20 Februari 2018 akiwa Kijijini Kapeta, Kata ya Ikinga Wakati akizungumza na wananchi waliowahi kuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira waliosimamisha msafara wake wakati akiwa ziarani Mkoani Songwe na Mbeya kukagua shughuli za uchimbaji wa Madini.
Alisema kuwa wananchi hao ndio walioiweka serikali ya awamu ya tano madarakani hivyo serikali haina haiwezi kuwasahau ama kutosimamia haki yao bali wanapaswa kuwa wavumilivu wakati serikali inajiridhisha na madeni hayo kabla ya kuanza kulipa ili kuwa na uhakika na watu wanaostahili malipo hayo.
"Watumishi lazima tukubali kwamba madeni haya tumeyarithi hayakuwa ya serikali bali yalikuwa ya muwekezaji sasa ili serikali iweze kuyalipa ni lazima ijiridhishe isije ikaingia mkenge wa kulipa watu wasiostahili kwani madeni hayo ni makubwa na yanahitaji kujiridhisha" Alisema Mhe Biteko na Kuongeza kuwa: "Sisi serikalini tunalifanyia kazi jambo lenu na tumeshafanya kazi kwa kiasi kikubwa mpaka sasa ya kuona namna ya kuwalipa na ninataka niwahakikishie kuwa kila mwenye haki anayedai lazima atalipwa lakini mtuvumilie tumepita kwenye michakato mingi ya kuibiwa fedha kwa watu kupachika madeni ya watu wasiostahili kulipwa tena wengine walishafariki"

Mhe Biteko aliongeza kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli inatambua kuwa mgodi wa Kiwira na mradi wa uchimbaji makaa ya mawe wa Kabulo ni miradi ya kimkakati katika Wizara ya Madini hivyo inatambua umuhimu wake na tayari ipo mbioni kuanzisha tena uzalishaji katika mgodi huo ambao uzalishaji wake ulisimama tangu mwaka 2009.

Alisema kuwa wananchi wamesubiri kwa muda mrefu malipo yao lakini tatizo kubwa ilikuwa ni serikali kujiridhisha na kuanisha wanufaika wa madeni hayo hivyo serikali italimaliza jambo hilo na itabaki kuwa historia.

Alisisitiza kuwa katika maeneo mengi kulikuwa na changamoto mbalimbali lakini tayari serikali imezipatia ufumbuzi changamoto hizo na wananchi wanaona utofauti.

Akijibu maswali ya wananchi hao waliotaka kufahamu ni lini mradi huo utaanza uzalishaji, Mhe Biteko alisema kuwa ili mradi uweze kuanza zipo taratibu za kisheria ambazo lazima zifuatwe ili yasijejitokeza matatizo ya kisheria baadae hivyo zitakapomalizika haraka mradi huo utaanza uzalishaji na wananchi watajipatia ajira.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi waliowahi kuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira wakati akiwa ziarani Mkoani Songwe na Mbeya kukagua shughuli za uchimbaji wa Madini, Leo 20 Februari 2018. 
Baadhi ya wananchi waliowahi kuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko alipokuwa akizungumza jambo wakati akiwa ziarani Mkoani Songwe na Mbeya kukagua shughuli za uchimbaji wa Madini, Leo 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi waliowahi kuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira wakati akiwa ziarani Mkoani Songwe na Mbeya kukagua shughuli za uchimbaji wa Madini, Leo 20 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WazoHuru Blog

Taarifa kwa Umma toka TPDC kujibu hoja za Swala Oil and Gas kununua hisa za PAET

RUVUMA TV: RTO RUVUMA KUFANYA OPARESHENI YA MADEREVA WASIO NA SIFA

$
0
0
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mratibu Abeli Swai amewataka madereva pikipiki na magari mkoani ruvuma kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazotokea ambazo chanzo chake kikubwa zinasababishwa na matumizi mabaya ya barabara

THE LAUNCH PAD YATUMIA TASISI TATU KUWAELEZA VIJANA UMUHIMU WA NIDHAMU MAHAA PA KAZI

$
0
0
--
 Mkurugenzi na Mwanzilishi mwenza wa Tasisi ya Launch Pad Tanzania, Henry Kulaya, akizungumza na Vijana waliofika katika mafunzo ya siku mbili ya Ujasiliamali na Kuongeza Maarifa ya kuweza kuajirika katika tasisi mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Niajiri Platform, Lillian Madeje akizungumza na Vijana namna ya kuweza kuandaa Cv zao hili ziweze kuwasaidia kupata ajira kw aurais kupitia Mtnadao wake wa Niajiri Tanzania.
 Mkurugenzi ya Tasisi ya kuwezesha Vijana ya Empower Limited, Miranda Naiman akieleza namna tasisi yake ilivyojikita katika kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi katika kipindi hiki ambacho Dunia inapitia changamoto ya uhaba wa ajira.
  Mkurugenzi na Mwanzilishi mwenza wa Tasisi ya Launch Pad Tanzania,Carol Ndosi akichangia jambo katika mjadala wa kuongeza maharifa kwa vijana hili waweze kupata ajira kwa uraisi hili waweze kujikwamua kiuchumi
 Mmoja wa Vijana walioshiriki katika Kongamano hilo akieleza jambo juu ya umuhimu wa Vijana kuwa na Maadili kazini

Vijana walioshiriki kongamnao la Vijana Ujasiliamali na kuongeza maharifa hili waweze kuajirika katika mashirika mbalimbali lililoandaliwa na Tasisi ya The Launch Pad

MBUNGE WA LONGIDO,DK STEVEN KIRUSWA AAHIDI KUWATUMIA WANANCHI WOTE

$
0
0


Mbunge wa jimbo la Longido mkoa wa Arusha,Dk Steven Kiruswa akizungumza na wananchi mjini Longido katika sherehe aliyoindaa kuwashukuru kufuatia kuchaguliwa kwake mwezi uliopita. Ameahidi kuwatumikia wananchi wote bila kujali tofauti za kisiasa.

Mzee wa mila za jamii ya kimaasai,Kilorit Ngulupa(kushoto) akiwaombea baraka Mbunge wa jimbo la Longido mkoa wa Arusha,Dk Steven Kiruswa na mkewe wake, Agness Kiruswa.

Mbunge wa zamani wa jimbo la Longido mkoa wa Arusha,Lekule Laizer(kulia) akipokea zawadi ya blanketi kutoka kwa mbunge wa sasa, Dk Steven Kiruswa(kushoto) na mke wake,Agness Kiruswa wakati wa sherehe hiyo.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe hiyo.

Mbunge wa jimbo la Longido mkoa wa Arusha,Dk Steven Kiruswa(kulia) akizungumza jambo na Gavana wa Kaunti ya Kajiado nchini Kenya,Joseph Ole Lenku baada ya sherehe na kukubaliana kuongeza ushirikiano baina ya wananchi wanaoishi maeneo ya mpakani.

Mkuu wa mkoa wa Njombe,Christopher Ole Sendeka(kushoto) akipokea zawadi ya Mbuzi kutambua mchango wakati wa kampeni.

KIPINDI MAALUM CHA MAENDELEO YA UJENZI WA RELI NCHINI


Waziri Mwakyembe akutana na wasanii wa sanaa ya uchongaji kutatua changamoto ya umiliki wa eneo la Mwenge

$
0
0
Na Genofeva Matemu – WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa tasnia ya sanaa ya uchongaji haiwezi kuendelea kama mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge utaendelea kuchukua nafasi kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku hivyo kushindwa kujiinua kiuchumi na hata kushindwa kuchangia katika pato la taifa.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na wasanii wachongaji pamoja na wafanyabiasha wa kazi za sanaa ya uchongaji kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge ili kuweza kuweka mikakati ya kutatua changamoto hiyo iliyodumu kwa zaidi ya miaka 10.Waziri Mwakyembe amesema kuwa eneo la Mwenge lenye mgogoro lina uwezo mkubwa chini ya serikali ya awamu ya tano kupata pesa nzuri kutoka kwa wawekezaji na kubadilisha muonekano wake kutokana na eneo hilo kuwa na bidhaa nzuri zinazobuniwa na wasanii wachongaji hivo kuwa kivutio kikubwa kwa watalii kutoka mataifa mbalimbali.
“Tutarudi tena hapa kuja kutoa msimamo wa serikali ni upi ili tuweze kuendelea, hii ni serikali ya ya awamu ya tano haki lazima itendeke hiki sio kipindi cha wajanja wajanja kuchezea haki za wenzao” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe amewataka wasinii wachongaji  pamoja na wafanyabiashara wa kazi za sanaa ya uchongaji kuwa na umiliki wa pamoja na kutambuana kama watoto wa baba mmoja na mama mmoja ili kuweza kuiendeleza tasnia hiyo ya uchongaji kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Baraza la Sanaa la Taifa Bw. Godfrey Mngereza amesema kuwa lengo la kujadili sintofahamu ya eneo la Mwenge ni  pamoja na kurekebisha sintofahamu hiyo ili wasanii wachongaji pamoja na wafanyabiasha waweze kwenda kwa pamoja katika kujenga nchi hii kwani sanaa ni kazi, sanaa ni uchumi lakini pia sanaa inazalisha ajira.
Naye Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bw. Adrian Nyangamalle amesema kuwa nia kubwa ya shirikisho hilo ni kuifanya tasnia ya sanaa za ufundi kufika mahala ambapo italeta mchango unaokusudiwa kwa taifa na kubadilisha maisha ya wasanii na wadau wote wa tasnia hiyo na hili hayo yafikiwe ni lazima kuwe na amani ili kila mtu awe na uhuru wa kufanya kazi zake kwa nafasi.  
Aidha Bw. Nyangamalle amesema kuwa Shirikisho la Sanaa za Ufundi limeweza kupokea changamoto ya umiliki wa ardhi hiyo na kuwasilisha kwa wadau na serikali kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto hiyo.
 Katibu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bw. Adrian Nyangamalle
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na wasanii wa sanaa ya uchongaji pamoja na wafanya biashara wa kazi za uchongaji (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bw. Adrian Nyangamalle
 Mwenyekiti mstaafu Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) Bw. Focus Senya (kushoto) akitoa ufafanuzi wa mgogoro wa umiliki wa ardhi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa kikao kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) Bw. Isihaka Abdul akielezea historia ya umiliki wa ardhi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa kikao kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wajumbe wa chama cha Makonde Hand Craft Village Bw. Hamis Mhando (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wasanii wanaojishughulisha na sanaa ya uchongaji katika eneo la Mwenge wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujadili mgogoro wa umiliki wa eneo la Mwenge kati ya wachongaji na wafanya biashara wa bidhaa za uchongaji leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Genofeva Matemu - WHUSM

MICHUZI TV: MASOUD KIPANYA NDANI YA KIPINDI CHA DANGA CHEE NA SHAMSA DANGA

MAKATIBU MEZANI WA BUNGE WAPEWA MAFUNZO

$
0
0
   Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai akifungua mafunzo ya Makatibu mezani wa Bunge, Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo ya wiki moja yanatolewa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa pili wa kulijengea Bunge uwezo (LSP II). Kushoto kwa Katibu wa Bunge ni Spika Mstaafu wa Bunge, Mhe. Pius Msekwa ambaye ni mmojawapo wa watoa mada katika mafunzo hayo na Kulia kwa Katibu wa Bunge ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Bi. Nenelwa Wankanga.
 Spika Mstaafu wa Bunge Mhe. Pius Msekwa akizungumza wakati wa mafunzo ya Makatibu mezani wa Bunge. Mhe. Msekwa ni mmojawapo wa watoa mada katika mafunzo  hayo ya wiki moja yanatolewa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa pili wa kulijengea Bunge uwezo (LSP II).

c.       Mkurugenzi Mstaafu wa Shughuli za Bunge Ndg. Japhet Sagasii (aliyesimama) akitoa mada wakati wa mafunzo hayo ya Makatibu mezani wa Bunge. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mstaafu- Ofisi ya Bunge Ndg. Charles Mloka ambaye naye ni mtoa mada katika mafunzo hayo.
Spika Mstaafu wa Bunge Mhe. Pius Msekwa wa (pili toka kulia waliokaa), Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili toka kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Makatibu mezani wa Bunge maara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo Jijini Dar es Salaam.

Dakika 30 ZA Huzuni wakati ASLAY ALIVYOWALIZA WATU ESCAPE ONE

$
0
0
Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
Ilikuwa Usiku wa February 17 mwaka huu msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Aslay Isihaka alibadilisha historia ya muziki katika Maisha yake kwa kufanya shoo kubwa ya Mapenzi na Muimbaji Mwenzie Nandy ambae wameshirikiana katika nyimbo nyingi.
Licha ya usiku huo kufikiriwa kuwa wa nyimbo za Mahaba mambo yalikwenda tofauti kwa nusu saa nzima pale Aslaya alipopanda jukwaani na kibao cha “Angekuwepo” wimbo ambao aliumba kwa ajili ya kumkumbuka Mama yake Mzazi.
Aslay ambaye aliimba kisha kuishia kati na kwenda kumsogelea Mama Mzazi wa Nandy na kusema kuwa “natamani muda huu Mama yangu muda huu angekuwa hapa lakini sio mapenzi yangu...Natamani namimi ningekuwa kama Nandy naimba Mama yangu anaona. Hivyo nikuombe Mama Nandy kuanzia leo uwe mama yangu hili niweze kupata faraja kama anayopata mwanao” alisema Aslay.
Maneno yaliteka hisia za watu wengi na kumfanya Mama yake Nandy kuamka na kwenda kucheza na Aslay na kufanya watu wengi kuinuka kwenda kumwambia mwanamuziki huyo aendelee kuimba na kuacha kulia.
Aslay ambaye aliendelea kuimba wimbo huo huku akiwa amekaa chini kwa  huzuni na kutengeneza simanzi kubwa ndani ya ukumbi wa Escape One kwa zaidi ya Dk 30. Wengi walilengwa na machozi na kukubali kuwa Mama ni wa muhimu kuliko kitu chochote maishani.
 Aslay Isihaka akionyesha kidole juu kumshukuru Mungu kwa yote yaliyotekea katika maisha yake.
 Aslay akimuomba   Mama yake Nandy  kuwa Mama yake wa kumlea wakati anaimba wimbo wake angekuwepo
 Aslay akicheza na Mama yake Nandy  mara baada ya kukubali kuwa Mama Mlezi
 Mmoja wa Mashabiki wakinyamazisha Aslay asilie wakati anaimba wimbo angekuwepo
Mashabiki wa muziki wakiwa wamesimama kwa huzuni wakati Aslay akiimba wimbo huo

WALIMU WASTAAFU SONGEA WAASA VIJANA WAFANYE KAZI WA WALEDI

$
0
0
Walimu wastafu katika manispaa ya Songea wamewataka vijana kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuliboresha chama hicho kiweze kuwa imara na kuzaa matunda mema hayo wameyasema hayo wakati walipokabidhiwa fedha kiasi cha shilingi laki tatu na robaini kama sehemu ya mchango wao katika chama ch CWT. HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO FEBRUARY 21,2018

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 20.02.2018


SIKU SABA ALIZOTOA WAZIRI KIGWANGALLA ZAZAA MATUNDA.

$
0
0
Wiki chache zilizopita Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla alitoa siku saba kwa polisi kukamata watuhumiwa wa mauaji ya mwanaharakati dhidi ya mauaji tembo Wayne Lotter, pia alitaka nyumba zilizouzwa kinyemela huko Arusha zirudishwe na pia alitoa siku saba kwa wakurugenzi wa kampuni nne za uwindaji kukutana nae Dodoma.

Jana kwenye kipindi cha 360 Waziri Dk. Kigwangalla alitoa maelezo ya kina kuhusu maelekezo aliyotoa na pia kuelezea mikakati mbalimbali ya Wizara yake. Kuhusu mauaji ya Lotter alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa na kufikishwa mahakamani. Alimsifu IGP Sirro kwa ushirikiano na Wizara yake.

Alieleza kuwa Katiba inatambua Waziri kama sehemu ya Serikali na kwamba Polisi wapo ili kusaidia Serikali kutimiza malengo yake. Kuhusu nyumba za Arusha, alieleza kuwa ushahidi unaonyesha wazi kuwa waliotajwa walikuwa wamiliki wao binafsi au kupitia familia zao. Waziri Dk.Kigwangalla alieleza mkakati wa kufungua na kukuza utalii kusini mwa Tanzania.

Alieleza mradi wa regrow ambao utawezesha sekta ya kukua kusini mwa Tanzania. Pia alizung umzia umuhimu wa uhifadhi na kueleza kuwa mto Ruaha kwa sasa unakauka kwa siku 60 wakati wa kiangazi na malengo ni kurejesha hadi kukauka kwa siku 10 tu.

Kuhusu kutangaza vivutio, Waziri Dk.Kigwangalla alieleza mkakati wa kutangaza vivutio na pia uanzishwaji wa mwezi wa urithi ambao sio tu utaongeza vivutio vya utalii bali utaenzi tamaduni na mila za Kitanzania.

Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Pili

$
0
0
Picha/Makala na Josephat Lukaza.

Siku ya Leo tutaangalia Makundi mawili yaliyobaki katika makundi mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa, Siku zilizopita Katika makala ya Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Kwanzatuliweza kuangalia Makundi mawili ambayo ni Viral Infections pamoja na Bacterial Infections

Leo tutaangalia makundi mengine mawili ya mwisho ambapo tutapata nafasi ya kuangalia ni magonjwa gani yapo katika Makundi hayo mawili yaliyosalia.

Yes Let's Back to Class kama wasemavyo Wazungu, Leo tutaangalia Makundi Mengine Mawili ambayo ni Kama Ifuatavyo

1: Fungal Infections
Fungal infections ni magonjwa ambayo  husababishwa na fangasi magonjwa haya yanaathiri binadamu pamoja na mbwa japokuwa Mbwa hushambuliwa mara kumi zaidi ya binadamu kwa magonjwa yasababishwyo na fangasi. Magonjwa yasababishwayo na fangasi kwa Mbwa yanaweza kuleta madhara katika Macho, Ubongo, ngozi nk. Katika Kundi hili la magonjwa yasababishwayo na fangasi Ni kama vile .

Blastomycosis, Histoplasmosis,>>>>KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI AONDOKA DAR ES SALAAM KUELEKEA KAMPALA NCHINI UGANDA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda wakati akeielekea kwenye ndege yake tayari kwa safari ya kuelekea nchini Uganda kushiriki Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance  Mabeyo kabla ya kupanda ndege kuelekea nchini Uganda kushiriki Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala.

UPEPELEZI KESI YA MAUAJI MKURUGENZI PALMS BADO HAUJAKAMILIKA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, upelelezi wa kesi ya mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, Wayne Lotter (52) inayomkabikabili Meneja wa benki Khalid Mwinyi (33) bado haujakamikika.

Wakili wa Serikali, Adolf Mkini ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Wakili Mkini alidai kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ili kuona kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Kabla ya Wakili huyo kueleza hayo, mshtakiwa Rahma Almas aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa Mohammed Maganga anaumwa na yupo gerezani.

Washtakiwa wengine  katika kesi hiyo ni Rahma Almas maarufu kama Baby (37)  Mfanyabiashara na Mohammed Maganga mwenye (61) ambaye ni mchimba makaburi.

Kesi imeahirishwa hadi Machi 6,mwaka 2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la mauaji ambapo wanadaiwa, Agosti 16,mwaka 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie Kinondoni Dar es Salaam, ambapo walimuua Lotter.

WAMILIKI WA LESENI ZA MADINI WAASWA UONGEZAJI THAMANI YA MADINI

$
0
0
Na Mathias Canal, Mbeya

Wamiliki wa leseni za madini ya dhababu, vito na mengineyo kote nchini wametakiwa kuiga mfano wa Ndg Salim Jesa mmiliki wa kiwanda cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kinachojishughulisha na kukata, Kusaga na kuuza mawe kwa kufanya mchakato mzima mpaka bidhaa kukamilika hapa hapa nchini.

Kauli hiyo kwa wamiliki wa leseni za madini nchini imetolewa leo 20 Februari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya.

Alisema kuwa kiu ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ni kuona rasilimali za nchi zinaongezwa thamani zikiwa ndani ya nchi jambo ambalo linaakisi umakini wa utendaji na ulipaji kodi ya serikali pasina kukwepa ama kutorosha rasilimali madini yakiwa ghafi. 

Aliseama kuwa faida ya kuongeza thamani ya madini nchini ndio muarobaini wa sekta ya madini kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa hatimaye kufikia asilimia 10% kama ulivyo mpango wa wizara kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la Taifa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua mawe yaliyo katwa, Kusagwa na kuongezewa thamani katika kiwanda cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili katika kiwanda kinachoshughulika na kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Ndg Salim Jesa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Marmo E. Granite Mines (T) Ltd kuhusu usafirishaji wa mawe baada ya kuyaongezea thamani wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua utendaji kazi wa kiwanda cha kukata, Kusaga na kuuza mawe cha Marmo E. Granite Mines (T) Ltd wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya, Jana 20 Februari 2018.

Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images