Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live

Article 9

$
0
0
SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
WAZEE WA KAZI
TAARIFA YA ONGEZEKO LA BEI
MTATUWIA RADHI WATEJA WETU, IMEBIDI TUONGEZE BEI KIDOGO ZA NDEGE
HII IMETOKANA NA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA YA NDEGE
AIR CARGO TO DAR NOW £3.80
INCLUSIVE CLEARANCE
STILL THE CHEAPEST AND SIMPLY THE BEST!
WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
KUCHUKUA MZIGO WAKO DAR ES SALAAM 
MPIGIE AGENT WETU DAR; TORNADO LUKOSI TEL; 0713607116
MZIGO UNANDOKA KILA IJUMAA UNACHUKUA IJUMAA INAYOFUATA
FROM NOW ALL OUR CARGO GOES  WITH KENYA AIRWAYS! 
THIS MEANS A DIRECT FLIGHT TO NAIROBI/DAR EVERY WEEK 
THIS MEANS NO MORE DELAYS OR EXCUSES!
THIS MEANS BETTER SERVICE THAN BEFORE!

ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN TANZANIA
UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA KUCHUKUA ILALA DAR BILA KULIPA TENA

FLIGHTS EVERY WEEK

KWA WALE WANAOTAKA KUNUNUA VITU UK TUTUMIE EMAIL AU TUPIGIE
MINIMUM WEIGHT IS 40K HANDLING/ADMIN FEE £20
40' CONTAINER TO DAR/MOMBASA NOW £1,800
OUR AGENT IN DAR; TORNADO TEL; +255 713607116

Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

NORTHAMPTON AGENT,
MOSES MBAA,  TEL 07904773779
SUITE 15 NOTHAMPTON BUSINESS CENTRE, NOTHAMTON NN1 2JL

READING AGENT
GERALD LUSINGU,  TEL  07405571187
OXFORD AGENT
Peter & Robert.
Peter - 07932439714.
Robert- 07554425879.

HEAD OFFICE
HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

Makamu wa Rais Dk Bilal ahudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Iran

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislam ya IRAN alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Teheran leo Ogast 03-2013 kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Bw. Hassan Rouhan  Al-Quds  anaetarajiwa kuapishwa kesho baada ya kushinda kwenye uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Teheran leo Agosti 03-2013 kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Bw. Hassan Rouhan  Al-Quds  anaetarajiwa kuapishwa kesho baada ya kushinda kwenye uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mshauri Maalum wa Waziri wa Mambo ya nje wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislam ya IRAN bw. Mohammad Valulleh kwenye chumba maalum cha mapumziko VIP katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Teheran leo Ogast 03-2013 alipowasili Nchini Irani kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Bw. Hassan Rouhani Al-Quds anaetarajiwa kuapishwa kesho baaada ya kushinda kwenye Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni. (Picha na OMR).

masupa staa wa kimarekani wazidi kumiminika bongo, safari hii ni Bill Clinton, Jesse Eisenberg, Dakota Fanning na Brook Lopez

$
0
0

Rais Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinto ambaye yuko nchini kwa ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na taasisi yake ya Clinton Foundation katika nchi kadhaa za Afrika

Katika msafara wa Mhe Bill Clinton kuna mastaa kadhaa wa sinema basketball ambao wameongozana na Rais huyo mstaafu wa Marekani aliye katika ziara ya kikazi kukagua na kuendeleza kazi za maendeleo zinazofanywa barani Afrika na taaisis yake ya Clinton Foundation. Pichani juu kulia ni mcheza sinema nyota Dakota Fanning akiongea na mcheza sinema mwingine nyota Jesse Eisenberg na nyuma yao aliyekwenda juu ni mcheza basketball katika NBA Brook Lopez
 Jesse Eisenberg na Dakota Fanning wakishuhudia utiwaji saini wa mkataba wa maelewano kati ya Serikali ya Tanzania na tasisi ya Clinton Foundation Ikulu jijini Dar es salaam 
 Ankal akiwa na Jesse Eisenberg
Ankal akila pozi na Brook Lopez ambaye kenda hewani 
kama Hasheem Thabeet

BENKI YA KCB YATOA MSAADA WA VIFAA VYA WATOTO NJITI ZANZIBAR

$
0
0
 Meneja wa KCB  Bank Tawi la Stone Town mjini Zanzibar, Cosmas Mwankemwa akizungumza kwenye sherehe ya kukabidhi msaada wa vifaa vya kuhifadhia watoto wachanga ambao hawakutimia umri wa kuzaliwa "njiti" kwaajili ya hospitali ya Kivunge Zanzibar jana vikiwa na thamani ya sh.12 milion
 Meneja wa Benki ya KCB Tawi la stone Town Zanzibar, Cosmas Mwankemwa (kulia) akikabidhi vifaa vya kuhifadhia watoto wachanga ambao hawakutimia umri "njiti" kwa  Dk.Yussuf Haji,ikiwa ni dhamana ya hospitali ya Kivunge Zanzibar jana vikiwa na thamani ya sh.12 milioni.

JK AKUTANA NA BINGWA WA DUNIA WA KURUKA KAMBA HAMISI MOHAMED NA WENZAKE

$
0
0
Rais Jakaya  Kikwete akimpongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa  kunyakua ubingwa wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko Orlando, Marekani, mwezi uliopita. Kijana huyo, ambaye  awali alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo  Dar es Salaam, alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya Afrika Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu. Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha Dogodogo Centre

 Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia 
 Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani
 Hamisi Mohamed na wenzake wakionesha umahiri wao wa mchezo wa kuruka kamba ambao unazidi kupata umaarufu duniani kote
 Hamisi akionesha manjonjo yake Ikulu
 Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.
Rais Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote katika michezo ya kimataifa.

Mwenyekiti wa Sport  Training Centre (TSTF), Dennis Makoi amesema  kuwa walipotambua kuwa kijana huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. Alisema kuwa walipata mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili huyo  alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480 kutoka  timu 44 kutoka nchi 14 ambapo jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.

Amy Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania ili kuukuza  ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini kwao  na kuitangaza Tanzania.


Hamisi Mohamed alisema anashukuru kwa malezi aliyoyapata katika kituo hicho cha watoto yatima cha Dogodgo Centre na kwa msaada waliojitolea katika kukiendeleza kipaji chake.

HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI, 2013

$
0
0
Ndugu wananchi;

Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kwa mara nyingine tena kutekeleza utaratibu wetu huu mzuri tuliojiwekea wa Rais kuzungumza na taifa kila  mwisho wa mwezi.

Ndugu Wananchi;


Mwezi Julai, 2013 ulikuwa wa neema kubwa ya wageni kwa nchi yetu wakiwemo watu na viongozi mashuhuri duniani. Natoa shukrani nyingi kwa Watanzania wenzangu kwa jinsi tulivyowapokea wageni wetu zaidi ya 1,700.  Wamefurahi kuwepo kwao nchini na wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu.  Wageni wetu wamekuwa wa manufaa makubwa kwa nchi yetu.  Wamesaidia kuitangaza Tanzania duniani na kuendeleza fursa za kukuza utalii, biashara na uwekezaji nchini na kwingineko katika Afrika.


ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Mdau B.M. wa Washington DC ametweet ngoma hii ya Caiphus Semenya ya 'Angelina' na kutuomba tukumbuke enzi hizo

TAARIFA KAMILI YA JUMUIYA KUHUSU WATANZANIA WALIOVAMIWA UGIRIKI

$
0
0
Katika mitandao hivi karibuni zilionekana picha za watanzania wawili waliovamiwa na kupigwa  vibaya  Ugiriki.
Picha hizo hazikuwa na maelezo ya kutosha  na hatimae zilizusha maswali mengi yaliyokosa majibu muwafaka.
Jumuiya ya watanzania ugiriki baada ya kikao cha tume maalum inapenda kutoa  taarifa kamili ifuatayo:
1.   Waliovamiwa ni Makamu Mwenyekiti  bw. SALUM MSELEM  na Mhazina bw. SAID MOHAMED SAID  maarufu kwa jina la NURAMO(CHIDI)  NDUGU HAWA SI WAKIMBIZI, NI WATANZANIA HALISI.
2.   Mabwana hao walikuwa wanapita kwenye garden usiku  wa Jumatano 01/08/2013 kuelekea makwao,wakitokea  kwenye kikao muhimu ofisini .      Karibu na  garden hiyo kulikuwa na wezi waliokuwa wanajaribu kuvunja gari iliyokuwa imeegeshwa.Wezi hao walijishuku kama Salum  kawagundua wakamfuata kwa vitisho na kuanza kumpiga. Wakati huo lilitokea kundi lao jingine la watu wasiopungua  kumi wakaanza kumkimbiza Chidi ambaye alijitahidi kukimbia hadi  kufika chini ya nyumba anayoishi Salum(umbali wa mita 50)  huku akipiga kelele na hapo waliendelea kumpiga.Kelele za Chidi kwa bahati zilisikika na mke wa Salum  ambae nae alipiga kelele za kuomba msaada zilizowafanya  wakimbie na kumwacha Chidi akiwa hoi.
3.   Ndugu zetu tuliwafikisha hospitali  na tulitoa ripoti polisi  wanaoendelea na uchunguzi ambao hadi wakati huu tunapoandika maelezo haya HAKUNA TAARIFA ZOZOTE CHANYA  ZA KUWAKAMATA WAHUSIKA.
4.   Uongozi wa jumuiya unashindwa kutamka  kuwa wezi hawa wana uhusiano na kile kikundi maarufu kinachochukia na kuwavamia  wageni.Hatuna ushahidi.Bali tuna imani kubwa walikuwa ni vibaka toka nchi jirani.
5.   Tumeamua kuutaarifu ubalozi na vyombo vyote vya habari vilivyokuwa vimetumiwa taarifa za awali za tukio hili.
6.    Mwisho jumuiya yetu inatangaza bila kusita:                                         VIONGOZI WETU HAWAKUFANYA BAYA LOLOTE  LILILOSABABISHA WAVAMIWE NA KUPIGWA. TUPO PAMOJA NAO KWA HALI NA MALI.
Ahsanteni                                                                            
                                                                                                     Kny
TUME MAALUM YA JUMUIYA.
                                                                                              (Kayu Ligopora)  

KISOMO CHA KUMWOMBEA MAREHEMU SAID JETHA MWANAHANJI NA FUTARI YA PAMOJA DMV

$
0
0
kutoka kushoto ni Habiba na mwanae Mrs Mtalemwa, Farida na Asha katika picha ya pamoja Jumamosi Aug 3, 2013 wakati Farida na Habiba na familia zao waliposoma kisomo cha kumuombea marehemu baba yao Mzee Said Jetha Mwanahanji aliyefariki July 2011, Dar Es Salaam, Tanzania. Kisomo kilifanyika Silver Spring, Maryland na kuambatana na futari ya pamoja iliyoandaliwa na Farida Catering ambayo inamilikiwa na Farida.
Baada ya kisomo Ally Mussa (wapili toka kushoto mwenye mic) aliongoza swala ya magharibi kabla ya kufuturu iliyofanyika Silver Spring, Maryland
WanaDMV wakiendelea na swala ya magharibi.
Swala ikiendelea.
Juu na chini wakina mama wakiendelea na swala.
Swala ikiendelea baada ya kisomo cha marehemu mzee Said Jetha Mwanahanji
Kutoka kushoto ni Seif, Shekh Omar na Mpwa katika picha ya pamoja kabla ya kisomo kuanza.

FFU wa Ngoma Africa band kusherekea miaka 20 ya kuendeleza libeneke kwenye International African Festival Tubingen,Ujerumani

$
0
0
 Kamanda Ras Makunja akibeba boxi jukwaani

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" a.k.a FFU a.k.a Watoto wa Mbwa
yenye makao yake nchini ujerumani.Muzimu huo wa muziki "Ngoma Africa band,utasherekea miaka 20 tangu ianzishwe mwaka 1993 na kiongozi wake mwanamuziki Ebrahim Makunja almaarufu kamanda Ras Makunja wa FFU UGHAIBUNI.

Bendi hiyo yenye wapenzi,washabiki na wadau lukuki katika kila kona duniani itasherekea miaka 20 ndani ya International African Festival Tubingen 2013,katika viwanja vya Fest-platz huko Tubingen,Ujerumani,ambapo wapenzi wa bendi hiyo
wapewa siku mbili kuanzia tarehe 9 na 10.08.2013 kupata burudani ya bendi hiyo.

Ngoma Africa Band a.k.a FFU imetajwa kuwa ndio bendi ya kiafrika hiliyoweza kudumu kwa muda mrefu katika medani ya muziki barani ulaya,na kuweza kujizolea wapenzi na washabiki katika kila kona.
Washabiki na wadau wa bendi hiyo ndio wanao jigamba kuwa wanamiliki na kuipa nguvu bendi hiyo na kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja na wanamuziki wa bendi ni watumishi tu wanao watumikia washabiki na wapenzi wa Ngoma Africa.
Tunaitakia kila la heri Ngoma Africa band tusikose kuwasikiliza FFU at

HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA WANANCHI, TAREHE 31 JULAI, 2013

$
0
0
Ndugu wananchi;

Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kwa mara nyingine tena kutekeleza utaratibu wetu huu mzuri tuliojiwekea wa Rais kuzungumza na taifa kila  mwisho wa mwezi.

Ndugu Wananchi;


Mwezi Julai, 2013 ulikuwa wa neema kubwa ya wageni kwa nchi yetu wakiwemo watu na viongozi mashuhuri duniani. Natoa shukrani nyingi kwa Watanzania wenzangu kwa jinsi tulivyowapokea wageni wetu zaidi ya 1,700.  Wamefurahi kuwepo kwao nchini na wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu.  Wageni wetu wamekuwa wa manufaa makubwa kwa nchi yetu.  Wamesaidia kuitangaza Tanzania duniani na kuendeleza fursa za kukuza utalii, biashara na uwekezaji nchini na kwingineko katika Afrika.


BANDA LA NSSF LATIA FORA MAONESHO YA 8 8 KANDA YA MASHARIKI,VIWANJA VYA Mwalimu Julius Nyerere.

$
0
0
 Afisa Biashara mkoa wa Morogoro Lucas Mwaisaka akipata maelezo ya mfuko huo kutoaka kwa Afisa matekelezo wa NSSF mkoa wa Morogoro Christopher Msagati nyuma yake ni Afisa mwandamizi wa Mafao mkoa Morogoro Adolfide Mulokozi baada ya kuvutiwa na huduma zinazotolewa na mfuko huo uwanajani hapo.(picha na Joseph Malembeka).

wanafunzi watembelea banda la ofisi ya waziri mkuu kwenye maonesho ya nane nene dodoma

$
0
0
 Afisa Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ibrahim Hamidu akitoa maelezo kuhusu utendaji wa kazi za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maria De Matias ya Mkoani Dodoma, walipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya NaneNane yanayofanyika Kitaifa Viwanja vya Nzuguni Mkoani Dodoma.

 Mratibu Mwandamizi wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Edgar Senga akieleza shughuli za Uratibu wa Maafa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Maria De Matias ya Dodoma katika Maonesho ya NaneNane viwanja vya Nzuguni Mkoani Dodoma walipotembelea Banda la Waziri Mkuu leo.

Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Shedrack Kiteve akieleza kazi za Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maria De Matias ya Dodoma walipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya NaneNane yanayofanyika Kitaifa Nzuguni Mkoani Dodoma leo.

Waziri Mkuu Mhe Mizengo Kayanza Peter Pinda kuktana na watanzania London Jumanne Agosti 6, 2013

$
0
0
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania London unawakaribisha Watanzania wote watakaoweza kupata fursa kuja kuzungumza na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda hapo Ubalozini siku ya Jumanne (tarehe 6 Agosti 2013) kuanzia saa Kumi na Nusu alasiri (1630 hours au 04.30 p.m.).
Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Pinda anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi na ushirikishwaji wa Diaspora. Aidha atajibu maswali kutoka kwa wananchi hao.


IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, LONDON, JUMAPILI (4 AGOSTI 2013)

UZINDUZI WA CHAMA CHA WAZAZI WA WATOTO WENYE ULEMAVU WA MTINDIO WA UBONGO, AKILI NA VIUNGO TANZANIA.

$
0
0
                                 
UZINDUZI WA CHAMA CHA WAZAZI WA WATOTO WENYE ULEMAVU WA MTINDIO WA UBONGO, AKILI NA VIUNGO TANZANIA. (CHAWAUMAVITA) UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI AGOSTI 24’ 2013 KATIKA UKUMBI WA SABASABA AMBAPO MGENI RASMI ANATARAJIWA KUWA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE. 

DKT SHEIN AWAKARIBISHA BILL CLINTON NA BINTIYE CHELSEA ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na  Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,(katikati) aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake. Kushoto ni Chelsea Clinton,ni Mtoto wa Rais Mstaafu huyo wa Marekani
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na  Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar baada ya mazungumzo yao
 Mtoto wa  Rais Mstaafu wa Marekani Chelsea Clinton,akipiga mpira kama ishara ya kufungua mpambano wa Timu za wachezaji wa zamani katika sherehe za Ziara ya Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,kukagua miradi mbli mbali katika nchi za Afrika iliyo chini ya ufadhili wa Taasisi yake ya CLINTON FOUNDATION katika
uwanja wa Amaan leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mtoto wa Rais Mstaafu wa Marekani  Chelsea Clinton,baada ya kufungua mpambano wa Mpira wa Miguu kwa timu za Wachezaji wa Zamani uliofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium,(katikati) Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, na Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,wakipata maelezo kutoka kwa  Bruno Mnnen,wakati walipotembelea katika banda la utoaji wa huduma ya uchunguzi wa Damu ya Maleria pamoja na Vyandarua,(Clinton Health Access Initiative-CHAI) katika ziara yake Clinton kuangalia miradi mbali mbali katika Nchi za Afrika,(wapili kushoto) Mtoto wa  Rais Mstaafu wa Marekani Chelsea Clinton
Picha na Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar

kwaya ya IYF TOKA KOREA KUSINI wakiimba wimbo wa "Tanzania, Tanzania, nakupenda Tanzania" Ikulu, Dar es salaam

SONG RELEASE: Acha Umbea by Yvonne Mwale

$
0
0

Not a long time ago the sensational Afro-Jazz singer Yvonne Mwale launched her album 'Kalamatila' in Dar es Salaam and managed to draw a massive crowd of fans to the concerts she had in Tanzania. The Zambian born artist toured eight countries in Europe in 2010 and thereafter decided to settle in Tanzania to continue working on its musical career. The result was her second album 'Kalamatila' which at the same time marked the debut as a solo artist. The single and video 'Familia Yangu' got respectable airtime on East African stations.

Her popularity got another boost after the release of her collaboration with Fid Q. Their song 'Sihitaji Marafiki' became a super-hit all over East Africa and was leading radio and TV charts for weeks. Finally, the same song was nominated in two categories at the Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013.

As a thank you to all the East African Fans and their great support Yvonne decided to give away another song written in Swahili for free. The title 'Acha Umbea' says it all: Gossiping and talking behind people's backs are destructive. The message is direct and clear - gossipers are not welcome here! All fans can download the track here: http://www.reverbnation.com/yvonnemwale/song/18188029-acha-umbea

Since December Yvonne and her band are back on the road touring around the world. Early 2013 they toured her home country Zambia, playing there more than 20 shows an TV appearances and getting a massive media feedback. The Daily Mail wrote about her TV performance: "Yvonne Mwale was certainly out of this world, a textbook with all the instructions on how to perform live on stage. ... Full of emotion at times, she made use of that vast stage while at the same time, producing a vocal performance that was admirable in every sense." The government station ZNBC selected Yvonne Mwale to open the new year on TV with a live performance of her song 'Kalamatila', backed by her band of Tanzanian and Zambian musicians.

Right now Yvonne is back to Europe where she will start touring shortly and is in preparation of recording her third album in one of the major music studios in Germany. 

'Acha Umbea' can be downloaded for FREE from here: http://www.reverbnation.com/yvonnemwale/song/18188029-ac


ha-umbea


Yvonne Mwale on Facebook: http://www.facebook.com/YvonneMwaleMusic
Yvonne Mwale on YouTube: http://www.youtube.com/yvonnemwale

uzinduzi wa kitabu cha mashairi cha dada edna lyatuu hogan wafana

$
0
0
Hivi majuzi pale Southern Sun Hotel jijini Dar es salaam Dada yetu  Edna Lyatuu Hogan ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu huko Dublin nchini Ireland alizindua kitabu chake cha mashairi.
Kitabu hicho kinaitwa’ The bird that sings  my name’ Poems of the heart   by Edna Lyatuu Hogan

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi. Kulikuwepo na mabalozi mbalimbalia, wafanya biashara, na waheshimiwa na watu kutoka nyanza mbalimbali.
Jenerali Ulimwengu ambaye pia ametoa maoni katika kitabu hiki na alisaidia katika uhakiki alikuwepo katika shughuli  na alisoma shairi kutoko kwenye kitabu hicho iitwayo ‘A true friend’.

Kulikuwa na uigizaji wa mashairi kutoka kwa wanafunzi wa shule mbalimbali, mashairi yaliyotungwa na kuongozwa na dada Edna mwenyewe. Katika hafla hiyo kitabu hiki kilinadiwa kwa shilingi 170,000/= kwa kopi moja..

Dr Mengi alinunua kopi nyingi ambazo zitawezesha upatikanaji wa computers  kwa  shule 30 zenye thamani ya mamilioni ya pesa. Kompyuta hizo zitaambatana na huduma nyingine za Teknohama kwa shule hizo zitakazochaguliwa.


Kitabu hiki kinapatikana bookshop zote za NOVEL IDEA nchini  na TPH  bookshop pale Samora Avenue.



Kitabu kinafaa sana kwa watu wa umri wowote. Kwa wanafunzi kinafundisha ubunifu wa uandishi na pia mashairi kwa sababu yanalenga jamii yanaburudisha sana, alisema mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.

Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) kufungwa kesho

$
0
0
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Uamuzi wa kusogeza mbele umetokana kuchelewa kupata disc ya usajili msimu huu ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo hutolewa na kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili.
Kutokana na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha pingamizi kitakuwa kati ya Agosti 6 na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.
Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu. Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa hazijajaza nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa kuanzia Novemba 15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu.
Pia klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha usajili wao zinatakiwa kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya mazoezi, nakala za bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo yameelezwa kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom.

KAMISHNA RWIZA KUSIMAMIA MECHI YA CHAN
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Rwiza wa Tanzania kuwa kamishna wa mechi ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Rwiza atakuwa kamishna katika mechi ya kwanza ya raundi hiyo itakayohusisha mshindi wa mechi kati ya Msumbiji na Namibia dhidi ya Angola itakayochezwa kati ya Agosti 9 na 11 mwaka huu. Mechi hiyo itachezeshwa na refa Noram Matemera kutoka Zimbabwe.
Matemera atasaidiwa na Wazimbabwe wenzake Tapfumaney Mutengwa atakayekuwa mwamuzi msaidizi namba moja, Ncube Salani ambaye ni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ruzive Ruzive.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live




Latest Images