Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 216 | 217 | (Page 218) | 219 | 220 | .... | 3348 | newer

  0 0

   Baadhi ya washiriki wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar Afisi Kuu iliyofanyika katika ukumbi wa Afisi hiyo uliopo Jimkana Mjini Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar hapo kwenye ukumbi wa umoja huo Jimkana Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya Viongozi wa CCM walioshiriki futari ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hapo Jimkana. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
  ----------------
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameitahadharisha Jamii nchini kujiepusha na tabia za baadhi ya watu wanaotumia dini katika ushawishi wa kuhatarisha amani ya Nchi.
  Alisema uchezewaji wa amani hiyo endapo utavurugika watakaoumia na kupata shida na taabu ni wananchi waliowengi na kamwe hazitowagusa wale waliochangia ushawishi wa kuivuruga amani hiyo.
  Balozi Seif alitoa kauli hiyo nzito mara baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Afisi Kuu Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa Umoja huo uliopo hapo Jimkana Mjini Zanzibar.
  Alisema wananchi walio wengi wamekuwa wakishuhudia hotuba za uchochezi zilizokuwa zikitolewa katika baadhi ya misikiti na mmoja wa sheikh kutoka nje ya Zanzibar ambazo zinahatarisha amani ya Nchi.
  Aliwatahadharisha wananchi hasa Vijana kuacha kununua au kutumia kanda zilizorekodiwa hivi karibuni na mhadhiri huyo na kusambazwa katika maeneo mbali mbali nchini.
  “ Amekaanga mbuyu yeye na hivi sasa hayupo. Lakini hata Mama watoto wake hayupo, watoto wake hawapo na mama yake pia hayupo. Sasa kapanda chuki jamii inapaswa kujihadhari nayo chuki hiyo. Likitokea vurugu lolote lile tutakaoumia ni sisi na wala sio yeye aliyekaanga mbuyu hizo “. Alitahadharisha Balozi Seif.
  Alifahamisha kwamba Taifa limekuwa katika hali ya amani kwa kipindi kirefu sasa hali ambayo ni muhimu katika kustawisha ustawi wa  wananchi wote Mjini na Vijijini.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alikumbusha kwamba bila ya amani wananchi wasingepata fursa ya kuendelea na shughuli zao za kimaisha  za kila siku.
  Alisisitiza kwamba wananchi wakati wote wana wajibu wa  kukataa maovu sio katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani bali hata katika miezi mengine ya kawaida  ili waendelee kuishi kwa amani na upendo.
  Akitoa shukrani kwa niaba ya Umoja wa Vijana wa CCM Afisi Kuu Zanzibar Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alisema Zanzibar ina hazina kubwa  ya Uislamu.
  Alisema hazina hiyo ambayo nadra kupatikana katika baadhi ya Nchi haipaswi miongoni mwa waumini wakaichezea kwa kuwaalika mahadhiri wa nje ya Zanzibar kuja kufitinisha waumini.
  Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar alimpongeza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Sheni na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa kauli zao za kila wakati za kusisitiza umuhimu wa kuitunza  amani wakati wote.
  Vuai Ali Vuai alishauri na kuomba suala hili muhimu kwa ustawi wa Taifa hili lazima likaungwa mkono na vyombo vya Dola hapa Nchini.
   
  Na Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  4/8/2013.


  0 0

   Jaffar Sadiq, Age: 19Years 
  Missing since Tuesday 31th July last seen in Arusha. 
  If you have any information about this boy please contact family by these numbers 
  or nearest police station. 
   Left home with white shoes, blue jeans trouser and cream shirt only. 

  PLEASE HELP FINDING THIS YOUNG BOY

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton baada ya mazungumzo na kisha kushuhudia utiwaji saini mkataba wa maelewano kati ya serikali ya Tanzania na taasisi ya Clinton Foundation kusaidia maendeleo ya kilimo na afya nchini Ikulu jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma
   Gari aina la HIACE likisogea kumchukua Mhe Bill Clinto
  Mhe Bill Clinton akiingia kwenye gari baada ya kuhitimisha shughuli zake Ikulu huku mwenyeji wake akimwangalia. Hilo lilikuwa tukio la nadra kwa kiongozi kama huyo kutumia usafiri wa kawaida kama huo

  0 0


  0 0

   Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha na Mkurugenzi wa Taasisi ya Catherine Foundation, Catherine Magige akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya zawadi za Mkono wa Idd El Fitiri kwa yatima na wasio jiweza.
   Catherine (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi na wasimamizi pamoja na watoto wa kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha
   Watoto wa kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha walipata zawadi mbalimbali kwaajili ya siku Kuu ya Iddi.

  0 0
 • 08/04/13--14:44: ngoma azipendazo ankal
 • Ngoma ya 'Love Station' ya The Winners ilikuwa balaa enzi zetu...

  0 0

   Hawa ni wafanya biashara wa masoko ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakiwa katika kikao 

  -----------------------------------------------------------
  Na Nathan Mtega,Songea

  UMOJA  wa wafanyabiashara wa masoko ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma umeendelea kuulalamikia uongozi wa Manispaa ya Songea kwa kuongeza gharama za pango la vibanda na gharama za leseni za biashara kwa wafanyabiashra pamoja na utaratibu usioridhisha wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hali hiyo imepelekea wafanyabiashara hao kuazimia kugoma.

  Wakizungumza katika mkutano wa dharula wanachama zaidi ya themanini wa umoja huo wamesema hawakubaliani na utaratibu wa uendeshaji wa masoko yaliyopo ndani ya manispaa hiyo ikiwa ni pamoja na ogezeko la pango lililoamriwa na uongozi wa manispaa bila kuwashirikisha wafanyabiashara hao.

  Wamesema uwezo wa wafanyabiashara katika masoko ya Manispaa ya songea na mzunguko wa fedha uliopo hauendani na ongezeko hilo la kodi,ushuru na utaratibu wa kuwataka wafanyabiashara hao  kuomba tenda ya kuendelea kufanya biashara katika vibanda hivyo walivyokuwa wakifanyia biashara zao.

  Wakizungumza wafanyabiashara Christian Kayombo na Hamis Machaku katika mkutano huo wamesema kuwa utaratibu unaofanywa na uongozi wa Manispaa wa kuongeza pango la vibanda na kutangaza tenda kwa ajili ya vibanda hivyo ambavyo wao wamekuwa wakivitumia kwa mkataba wa muda  mrefu bila kushirikishwa kwenye maamuzi hayo mapya ni ishara ya unyanyasaji kwao na hawajatendewa haki kwa sababu walishaomba kupunguzwa kwa kodi pamoja na malipo ya leseni lakini kabla maombi hayo hayajafanyiwa kazi wanaletewa ongezeko la kodi.

   Wamesema kuwa ni vyema uongozi wa Manispaa ukaona umuhimu wa kuwashirikisha wafanyabiashara kwa kupitia viongozi wa umoja wao katika kutoa na kufikia maamuzi yanayowahusu badala ya uongozi huo kukaa na kuamua juu ya wafanyabiashara wakati ukijua hali za biashara katika Manispaa ya Songea na mzunguko wa fedha ulivyo.

  Aidha wafanyabiashara hao wametangaza kugoma siku ya jumanne 6 Agosti 2013  kwa muda usiojulikana kuendesha biashara ikiwa malalamiko hayo hayatafanyiwa kazi kwa sababu kumekuwepo na vitendo vingi vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa halmashauri dhidi ya wafanyabiashara na hususani wafanyabiashara wadogo .


  Akizungumza makamu mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara wa masoko ya Manispaa ya Songea Leornad Chiwangu alisema wafanyabiashara wameazimia kuanza mgomo huo siku ya Jumanne na utaendelea kwa muda usiojulikana ikiwa malalamiko na maombi yao hayatafanyiwa kazi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mipango Mkakati na Uhusiano wa Kibiashara wa benki ya TIB Jaffar Machano akimuonesha Kamishna wa Polisi Mkoa wa Dodoma baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wawekezaji waliokopeshwa na benki ya TIB waliopo ndani ya Banda la TIB.
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Gregory G Teu akiongozwa na Mkurugenzi wa Mipango Mkakati na Uhusiano wa Kibiashara wa benki ya TIB Jaffar Machano kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na TIB wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda hilo katika maonesho haya ya NaneNane.
  Mheshimiwa Mbunge wa Kondoa kusini Juma Nkamia akipata maelezo juu ya moja ya huduma zinazotolewa na benki ya TIB mara baada ya kutembelea banda la TIB katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea Mkoani Dodoma. Benki ya TIB ni mdhamini mkuu wa Maonesho haya.
  Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la TIB wakiwa katika darasa maalumu ndani ya banda hili kwa ajili ya kuwapatia wananchi maelezo ya jinsi gani ya kunufaika na huduma za kibenki na kuwaongezea ujuzi wa kibiashara. Madarasa haya hutolewa kila siku bandani hapo.

  0 0
 • 08/04/13--20:03: KUMBUKUMBU


 • 0 0

  Vazi NI DUKA LA NGUO, VIATU, VIPODOZI, NA FASHION ACCESSORIES.


  FIKA dukani  Vazi Ujipatie  mavazi  ya watoto yenye ubora wa uhakika  kutoka  Ulaya na marekani kwa bei za kawaida.

  Mavazi hayo ni kama vile; Suruali na kaptula Kali za Kadet, Mashati, Tshits, magauni  Sketi na blouse.

  Zaidi ya Nguo za Watoto!
  Dukani Vazi Utajipatia Vitu mbali mbali kama vile

  Make up za Sleek; Viatu; Tops na Blouse, Body Splash  na Lotions za Victoria’s Secret

  pamoja na

   vipodozi vya aina Mbalimbali


  KUONA BIDHAA MBALI MBALI ZINAZOPATIKANA VAZI na Maelekezo Kufika Dukani TEMBELEA blog WWW.vazitz.blogspot.com

  KUMBUKA! Vazi utapata bidhaa Zenye Ubora wa Uhakika kwa bei za Kawaida.

   DUKA LA Vazilipo barabara ya Mwai Kibaki   KATIKATI YA SHOPPERS PLAZA NA ZANTEL MAKAO MAKUU, DUKA LINATAZAMANA NA GHOROFA LA NHC, LILILOPO PEMBENI YA INTERNATIONAL COMMERCIAL BANK

  Kwa Mawasiliano piga 


  0658 286 555


  0 0

  Ige Moyaba

  Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” itatambulisha wanamuziki wapya pamoja na warembo watakaoshiriki Miss Ilala siku ya Iddi Pili Katika ukumbi wao wa Mango Garden, Kinondoni.
  Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka alisema jana kuwa onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na kudhaminiwa na Konyagi, Freddito Entertainment, Saluti5 na Twitter Pub.
  Alisema wanamuziki watakaotambulishwa siku hiyo maalum ni wanenguaji wapya, muimbaji Ige Moyaba ambaye alikuwa mwanamuziki wa bendi hiyo kabla kwenda Ufaransa kuendeleza kipaji chake.
   “Tumeamua kuleta wanenguaji wapya kabisa, wenye damu changa ili kuleta mapinduzi kwenye muziki wa dansi. Madansa wetu ni mabinti warembo, pia tuna  wanenguaji watanashati,” alisema Asha na kuongeza kuwa awameamua kubadilisha wanenguaji ili kuenda na wakati pamoja na soko la muziki.
  Kwa upande wa Ige Moyaba aliyetamba kwenye albamu ya ‘Mtu Pesa’katika mwaka wa 2004,  Asha alisema ameanda vitu vipya kuwapa mashabiki wa bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigino.
  “Kwa kweli hi siyo onyesho la kukosa kwani itakuwa ni zawadi yetu ya Idd kwa mashabiki wetu,” mkurugenzi huyo alisema.
  Mwezi uliyopita Twanga Pepeta walizindua albamu yao ya 10 lijulikanayo kana “Nyumbani ni Nyumbani”.
  Albamu zingine ambazo zitapigiwa siku hiyo ni Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari, Password, Mtaa Wa Kwanza, Mwana Dar es Salaam na Dunia Daraja.
  Naye mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga alisema kuwa warembo watakoshiriki kwenye shindano la kumtafuta Redds Miss Ilala pia watatambulishwa siku hiyo.

  0 0

   
   Kampuni ya Clouds Media Group mwishoni mwa wiki iliandaa Ftari ya pamoja kwa wafanyakazi wake na baadhi ya wadau mbalimbali,maeneo ya Sinza-jijini Dar Salaam.Pichani kushoto ni  Mkurugenzi wa vipindi na utafiti,Ruge Mutahaba pamoja na Meneja Vipi wa Clouds FM Sebastian Maganga wakiongoza wageni waalikwa mbalimbali kupata ftari.Pichani chini ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wadau wengine waalikwa wakijipakulia ftari safi kabisa.


  Sehemu ya Wadau wakiendelea kupata ftari.Picha na Jiachie Blog.

  0 0

   Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Mwezi wa Toba, Mwezi wa Ibada ya Funga na Visimamo vya Sunna kama Tarawehe ,Dhikri N.k. Ramadhani Hiyo inaelekea kuisha.Jee Kuisha kwa Mwezi wa Ramadhani Ndio Mwisho wa Ibada na Mambo Mema?

  Jee Kuisha kwa Mwezi wa Ramadhani Ndio Mwisho wa Ibada na Mambo Mema?

  JIBU
  HAPANA MAMBO MEMA NA IBADA  INATUBIDI/TUPASA TUENDELEE NAYO MILELE KWANI WAAJIBU WETU WANAADAMU NA NDIO LENGO KUU LA KUUMBWA KWETU WANAADAMU DUNIANI.

  ALIYEKUWA AKIIMUABUDU M/MUNGU KWA AJILI YA MWEZI WA RAMADHANI BASI JUA KWAMBA MWEZI WA RAMADHANI UMEKWISHA NA ALIYEKUWA AKIMUABUDU M/MUNGU KWA DHATI/UKWELI WA KUMUABUDU HUYU ANAJUA KUWA M/MUNGU DAIMA YUPO KATIKA KILA MIEZI NA KILA SIKU NA SI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI TU.

  Lengo kuu la Funga ni kuupata na kuufikia Ucha Mungu .
  Ikiwa Umeweza kujizuia na kula na kunywa na mengineyo Ndani ya Mwezi huu .
  Tuna Imani kwamba tunaweza kujizuia na Mengine katika Mabaya baki ya Miezi Mengine na hilo ndio lengo kuu.

  IANDAE SIKUKUU YA EID .

  Indae Sikukuu ya Eid kwa furaha zote Mshukuru M/Mungu kwa kukupa Uwezo wa Kufunga na ukaweza Funga kwani wengi katika sisi walitamani kuwa nasi katika funga ya Mwaka huu lakini kwa Uwezo wake M/Mungu hawakuweza kuitekeleza Ibada hiyo.

  Hivyo basi Tumshukuru Sana M/Mungu .
   Vaa vizuri , Kula Vizuri , Wanunulie watoto wako zawadi  , kuwa karibu na Familia yako , Wasaidie wasio na Uwezo , TOA ZAKKATUL FITRI KABLA YA SWALA YA EID na mengi katika Ratiba za kheri Ulizo zipanga.

  Tusirudi Nyuma katika Kufanya Mema na Mazuri Siri ya Mwisho wetu hapa Duniani Mola Ndiye ajue huenda hii ikawa Ndio Funga yetu ya Mwisho ikiwa ndio hivyo.

  M/Mungu Tunamuomba  atupokee waja wake tukiwa wasafi na wenye kufutiwa Dhambi zetu na kukubaliwa Maombi yetu.

  NDUGU ZANGU WAPENDWA TUSIRUDI NYUMA KIIBADA TUSONGE MBELE NA TUZIDISHE IBADA NA MEMA  ILI TUPATE RADHI ZAKE M/MUNGU DUNIANI NA KESHO AKHERA TUSIZIAME NYUMBA ZA IBADA  TUSIACHE KUWASAIDIA WASIO JIWEZA TUSIZIACHE TABIA NJEMA TULIZO KUWA NAZO KATIKA MWEZI HUU IKAWA TUMERUDI KATIKA MAKOSA AMBAYO HUENDA TUSIDIRIKI TOBA YAKE TENA.
   
  Miongoni Mwa Masharti ya Toba ya Kweli ambayo wanazuoni wametuongoza ni kutorejea katika Makosa ambayo tuliyo yatenda.
   
  Tujipange na kuhakikisha haturudi nyuma katika Mambo ya kheri ili kupata Radhi za Allah Subhanahu wataalllah.
   
  Nimalize kwa Dua Mola tunakuomba Tusamehe Waja wako , yapokee Maombi yetu , Tupe Upendo na Amani katika Nchi yetu ya TANZANIA , Usitu adhibu kwa makosa ya Wachache wetu , Wasamehe wazazi wetu walio tangulia Mbele ya haki na Ndugu zetu wote kwa Ujumla , tujaalie kuwa Miongoni wa Wajaa wako walio Udiriki Usiku wa Cheo LAYLATUL QADIR.
   
  Rehma na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na Amani.
   
  WABILAHI TAUFIQH
   
  NAWATAKIA EID MUBARAKA M/MUNGU AREJESHE FURAHA KWETU SOTE MILELE 
   
  Na : Ghalib Nassor Monero L Azhariy 
  Kijitonyama Ali Mauwa 
  Dar es salaam , Tanzania

  0 0

  Baadhi ya wabunge wa Bunge la Taiwan,wakioshana umwamba kwa kuchapana makonde jana baada ya kupishana kauli wakati wa mjadala wa kuhusu mpango wa kupiga kura ya maoni iliyoadhimia kuidhinisha umaliziwaji wa mradi wa nne wa Nyuklia katika kisiwa ambacho kinakaliwa na watu wapatao milioni 23.

  0 0

  Naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge akisalimiana na wafanyakazi wa mamlaka ya maji wilaya ya Same akiongozwa na mkuu wa wilaya hyo Dk. Herman Kapufi.
  Naibu waziri dK mahenge akitazama moja ya vilula kwa ajili ya maji katika kijiji cha Vunta wilayani Same.
  Naibu waziri Dk Binilith Mahenge akitembelea vyanzo vya maji pamoja na tanki la kuhifadhi maji katika kijiji cha Miombo wilani Same.
  Naibu wa ziri Dk Binilith Mahenge akitizama maendeleo ya ujenzi wa tanki la maji katika kijiji cha Miombo wilayani Same ambalo kukamilika kwake kutawezesha kuhifadhiwa maji kwa ajili ya wakazi wa kijiji hicho.Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi. 

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kiislam ya IRAN Mhe. Al-Akbar Hashemi Rafsanjani wakati Makamu wa Rais alipofika kwenye Makazi ya Rais huyo mjini Teheran Iran leo Ogast 05-2013, Makamu wa Rais yupo Nchini Iran kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo alieapishwa jana jioni.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kiislam ya IRAN Mhe. Al-Akbar Hashemi Rafsanjani wakati Makamu wa Rais alipofika kwenye Makazi ya Rais huyo mjini Teheran Iran leo Ogast 05-2013, Makamu wa Rais yupo Nchini Iran kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo alieapishwa jana jioni.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, kipata maelezo kutoka kwa maafisa wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya kiislam ya Iran alipotembelea makazi ya Rais Al-Akbar Hashemi Rafsanjani mjini Teherani Iran leo Ogast 05-2013. (Picha na OMR)

  0 0

  Hiyo habari ya gazeti la NIPASHE kuhusu elimu leo nimeisoma. Sioni kama ina tofauti yoyote na taarifa ya Wizara. Lakini haya ndiyo matokeo ya watendaji serikalini kujifanya miungu-watu. Hawataki kutoa ushirikiano kwa wanahabari. Kila wakipigiwa simu-wapo kwenye vikao-vikao havimaliziki. Matokeo yake ndiyo haya, wafumuliwe ndipo wajitokeze kutoa ufafanuzi ambao si lolote, si chochote.
  Kilichoandikwa na Nipashe wala hakina dosari yoyote, lakini kwa sababu Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ametaka aonekane yupo kazini, kazomoka na taarifa isiyo na mbele wala nyuma.  

   Dawa ya haya ni kuacha urasimu. Toeni habari pale mnapotakiwa. Msisingizie kwamba "Leo Jumapili, napumzika". Serikali haipumziki wala haiendi likizo. Kama kweli tunataka kuendelea, ni lazima urasimu huu wa kipuuzi uachwe serikalini.

  Manyerere
  Jamhuri

  0 0

  SAM_1063
  Mmoja wa Wahudumu  ndani ya banda la Konyagi,Bi.Matha Charles pichani kushoto akimuonesha mmoja wa wateja aliyetembelea banda hilo,kinywaji kipya cha kampuni hiyo kiitwacho Zanzi kwenye maonesho ya Nane yanayoendelea Njiro, jijini Arusha,ambapo watu mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kuyashuhudia maonseho hayo.SAM_1057Katika msimu huu wa sherehe za nane nane ,kampuni ya Event Planners &Consultants inawakaribisha katika banda la Tanzania Distilleries Limited linalojulikana kama JUMBA LA KONYAGI lililopo katika maonyesho ya nane nane Njiro,jijini Arusha.

  0 0

  Na Francis Godwin, Iringa
  WANAHARAKATI wa  maendeleo ya  watoto mkoani Iringa wametaka  kuwepo kwa sheria kali kwa  watu  wanaowatumia  watoto  wadogo katika  kusimamia  harusi, wakidai kuwa katika  siku za hivi karibuni umezuka  mtindo  wa baadhi ya  watu  wa kada  ya kawaida na  viongozi wa umma ,ambao  harusi zao zimekuwa  zikisimamiwa na  watoto ama kupambwa na  watoto jambo ambalo ni kinyume na mkataba  wa kimataifa  wa haki za  mtoto ,sheria  ya mtoto inayohusiana na maendeleo yake.  Hivyo  kutokana na sheria hiyo,  wanaharakati hao  wamesema,  ni vyema  kusimamia vema  sheria  hiyo  ili  kuwabana  wale wote  wanaotumia  watoto katika  kupamba harusi  zao kuwajibishwa .

  Sauti ya  wanaharakati hao  imepazwa  leo katika  warsha ya  siku mbili ya  malezi  na makuzi  ya  watoto  inayoendeshwa na asasi  zisizo  za kiserikali za TECDEN na CIC katika ukumbi wa maktaba ya mkoa  wa  Iringa.
   
  Wakichangia  katika  mada ya  Haki na mahitaji  ya mtoto   wanaharakati hao  wamesema  kuwa  watoto  wameendelea kunyanyasika katika jamii ikiwa ni pamoja na  baadhi ya  watu  kuwatumia  watoto hao kujipatia  fedha  za  kuendesha maisha  yao.
  Kwani  walisema  hivi  sasa  vituo  vya kulea yatima  vimeendelea kuongezeka  zaidi katika maeneo mbali mbali ya mkoa  wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa huku  kila anayeanzisha kituo  cha yatima amekuwa akitanguliza maslahi yake  mbele badala ya  kuwasaidia  watoto hao .
  "Hivi sasa wengi  wao wanaanzisha  vituo vya yatima kwa ajili ya kupata utajiri na kuishi maisha mazuri  wao na si  watoto na chimbuko la  kuanzisha  vituo  vya yatima  ni baada ya  kuona  waanzilishi waliotangulia wanamiliki magari ya  kifahari na  kujenga  majumba makubwa na ndio  sababu  wengi  wao  wamegeuza yatima  kama mradi  wao"

  Kwa  upande wake mwanasheria  wa kituo cha msaada kwa  wanawake na  watoto  mkoa  wa Iringa Bw Jackson Gaso  alishauri  kuwepo kwa adhabu kali  ikiwezekana kuhukumiwa jela maisha kwa  wale  wote ambao watakutwa na hatia katika makosa ya ubakaji kama  njia ya  kukomesha  vitendo  vya ubakaji kwa  watoto.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakati wa futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto) nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili.
   Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefua akimshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi kwa kuhudhuruia  futari aliyoaiandaa nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
   Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Alhad akiongoza dua kwa waalikwa waliohudhuyruia  futari aliyoaiandaa nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya  futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya  futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili. CHA NA IKULU

older | 1 | .... | 216 | 217 | (Page 218) | 219 | 220 | .... | 3348 | newer