Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Article 10


MKUU WA MKOA WA RUKWA STELLA MANYANYA AONANA NA WALIMU WA KIKE WA MANISPAA YA SUMBAWANGA LEO KUJADILI KERO ZAO MBALIMBALI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na walimu wa kike wa Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 02 Agosti 2013 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Lengo la mkutano huo likiwa kujadili kero mbalimbali za walimu pamoja na kuzitaftia ufumbuzi. Pamoja na kero mbalimbali zilizowasilishwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa maelekezo kwa Halmsahauri ya Manispaa kushughulikia kero zinazowezekana ikiwepo madai ya likizo na mengineyo. Kwa yale yaliyo nje ya uwezo wa Manispaa aliahidi kuyachukua na kuyafikisha panapohusika ili yaweze kutaftiwa ufumbuzi. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Kushoto ni Afsa Elimu Taaluma Mkoa wa Rukwa Bi Catherine Mashalla. 

 Katika kikao hicho walimu walitoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kufuta chama cha waalim (CWT) kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiwakata waalim mishahara kwa mda mrefu bila kuwa na msaada wowote kwao pindi wanapouhitaji. Mapendekezo mengine ni kupunguza idadi ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka tisa hivi sasa na kuwawekea masomo yatakayowawezesha kusoma na kuandika kuliko hivi sasa ambapo masomo ni mengi na huwachanganya watoto. Hata hivo Mkuu wa Mkoa aliweka bayana kuwa ni vyema chama hicho kikaona ni jinsi gani ya kuwanufaisha zaidi walimu kwa kujiwekea utaratibu wa kuwakopesha au kuwasaidia kwa njia nyingine kiuchumi.

Sehemu ya waalimu waliohudhuria katika Mkutano huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwashauri waalim kutokopa katika taasisi zisizo rasmi ambazo riba zake ni kubwa kupita kiasi. Alisema taasisi nyingi za namna hiyo zimechangia kufanya maisha ya walimu wengi kuwa magumu na badala ya kuwa msaada kwao inageuka na kuwa kero.

Mkuu wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Bi Witness Maeda akitoa kero mbalimbali wanazokabiliana nazo waalim ikiwepo uhaba madarasa, mabweni, bwalo na maabara chuoni hapo. Kwa ujumla kero zilizowasilishwa ziligusia mishahara hafifu ya walimu, uhaba na ubovu wa vyumba vya madarasa, kucheleweshewa madai yao ya mishahara na nauli (Salary Arears), kupandiswa madaraja na uhaba wa mafunzo ya mara kwa mara kuweza kukabiliana ni mabadiliko ya mitaala mipya. 
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa www.rukwareview.blogspot.com)

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KWA WANANCHI KWA MWEZI JULAI 2013

Balozi Kamala akutana na Mratibu wa Taasisi ya Ex-Change ya Ubelgiji

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimsikiliza Bibi Andrea Borgs Mratibu wa Taasisi ya Ex-Change ya Ubelgiji aliyemtembelea leo ofisini kwake Brussels. Taasisi ya Ex-Change imeomba Taasisi na Kampuni za Tanzania zinazohitaji ushauri katika masuala mbalimbali kutuma maombi. Taasisi hiyo inagharamia wataalamu hao kwenda na kurudi kutoka Tanzania. Taarifa zaidi zinapatikana www.ex-change.be. Mwaka 2013 Taasisi hiyo imetoa ushauri kwa Kampuni za Kitanzania 14. Kwa Afrika, walitoa ushauri kwa kampuni 207.

lugha Gongana au ndio Mwake???

mpigie Kura Feza Kessy aweze kubaki ndani ya Jumba la Big Brother

yale yaleeee....

$
0
0
Hii ni njia ya Upanga jijini Dar, ukiwa unaelekea Palm Beach kwa kupitia pale yalipo Makao Makuu ya Jeshi.kiukweli njia hii huwa na fujo sana wakati wa jioni, maana kila mmoja anajiona anaharaka kuliko wengine.Wazee wa Feva jitahidini kukatiza na huku ili kukomesha mambo haya.

BANDA LA JESHI LA MAGEREZA LANG'ARA MAONESHO YA NANENANE DODOMA

$
0
0
Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi wakiangalia Buti Ndefu ya ngozi(Long Boot)iliyotengenezwa maalum kwa ajili ya askari katika Kiwanda cha Jeshi la Magereza kilichopo Gereza Karanga, Moshi. Askari hao wametembelea Banda la Maonesho ya Nanenane la Jeshi la Magereza leo Agosti 02, 2013 lililopo Nzuguni, Dodoma ambapo wamepongeza ubora wa bidhaa mbalimbali zilizopo katika Banda la Jeshi la Magereza.

Na; Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Dodoma

Jeshi la Magereza Nchini katika kutekeleza jukumu lake la kuwalinda na kuwarekebisha wafungwa huwapatia pia mbinu na stadi za ufungaji bora ili waweze kuitumia katika Jamii zao pindi wamalizapo vifungo vyao.

Aina ya mifugo inayofugwa na Jeshi la Magereza ni ng'ombe wa nyama na maziwa, mbuzi wa kienyeji na wa maziwa, kondoo, nguruwe, sungula, simbilisi, kuku wa nyama, kuku wa mayai, bata wa weupe na wa kienyeji.

Mazao yatokanayo na mifugo kama nyama na maziwa hutumika kulisha wafungwa na ziada huuzwa kwa askari na Wananchi waishio jirani na mashamba hayo. Aidha mifugo hai huuzwa kwa Wananchi mbalimbali wanaohitaji kufuga na samadi hutumika kurutubisha ardhi ya Jeshi la Magereza kwa ajili ya Kilimo na ngozi huuzwa katika Viwanda vya ngozi hapa Nchini.

Akizungumzia baadhi ya Changamoto zinazoikabili Sekta ya Ufugaji Mifugo hapa nchini, Mtaalam wa Mifugo katika Banda la Maonesho ya Nanenane la Jeshi la Magereza, Stafu Sajini Charles Masuka alisema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na upatikanaji mdogo wa maji ambapo mabwabwa ya maji yaliyopo hayakidhi mahitaji ya wafugaji wengi hapa nchini hali inayowafanya wafugaji wengi kufuga kwa kuhamahama.

Pili, magonjwa ya milipuko ambayo yanatokomezwa kwa njia ya chanjo ambapo wafugaji wengi wamekuwa wakipata hasara kubwa kwani milipuko ya magonjwa ya mifugo inapotokea mifugo mingi hufa.

Changamoto nyingine ni wavamizi katika maeneo ya malisho hali ambayo inasababisha migogoro ya mara kwa mara ya kugombania maeneo ya malisho ya mifugo pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo husababisha ukame katika maeneo mbalimbali hivyo kukosekana kwa malisho ya kutosha kwa mifugo.

"Wito wangu kwa Serikali ni kuwa waandae mpango mahususi wa kuwachimbia wafugaji mabwabwa ya kutosha kwa ajili ya uvunaji wa maji ya mvua pamoja na kuandaa programu za chanjo ya mifugo kila mwaka ili kuyatokomeza magonjwa mbalimbali ya milipuko". Alisema Stafu Sajini Charles.

Miongoni mwa mashamba makubwa yanayofuga ng'ombe wa nyama na maziwa ni pamoja na Gereza Ubena - Pwani, Mbigiri- Morogoro, Mugumu - Mara, Kitengule - Kagera, Kingurungudwa na Kilwa - Lindi, Namajani - Mtwara, Majimaji - Ruvuma na King'ang'a - Dodoma. Aidha, Mikoa yote nchini kuna Magereza yanayofuga idadi ndogo ya ngo'mbe wa nyama na maziwa kwa ajili ya nyama ya kulishwa wafungwa, ziada huuziwa askari na raia.

BAADA YA KUFUNGUA KAMPUNI KUBWA AFRICA SWAHILI MEDIA MAREKANI MPIGANAJI DAVIS MOSHA "THE CEO" AMUITA SUGE KNIGHT KWA AJILI YA PROMO

$
0
0
    Alex Kassuwi akimpokea Mario Hugh knight Jr. aka Suge Knight alipokuwa anawasili kuitikia mwito wa "THE CEO" Davis Mosha. Ambapo walijadiliana jinsi ya kuikuza AFRICA SWAHILI MEDIA nchini Marekani. THE CEO alimuita Suge Knight kutokana na uzoefu wake katika branding na promotion. Suge ni mjasirialiamali na mwekezaji mkubwa, na ni muasisi na alikuwa CEO wa  Black Kapital Records na vilevile ni muasisi mwenza na CEO wa zamani wa Death Row Records. Amewapa mafanikio makubwa wasanii Tupac Shakur, Dr. Dre, Snoop Dogg aka Snoop Lion, Outlawz na Tha Dogg Pound. 
   Suge akiwasili kumuona "THE CEO" Davis Mosha under escort
  Suge Kabla ya kumuona THE CEO alitambulishwa kwanza kwa mtoto wa Davis Mosha, Edgar Mosha. Kulia ni Mayor wa L.A. Bwana Deo Temba.
 Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na THE CEO Suge alipata picha ya ukumbusho
  Mayor wa L.A. Deo Temba, Edgar Davis, Suge Knight na THE CEO Mpiganaji Davis Mosha wakiwa pamoja JW Marriott L.A. LIVE
Crew walioambatana na Suge Knight kuja kumuona "THE CEO" Davis Mosha kwa ajili ya Kuikuza AFRICA SWAHILI MEDIA Marekani.
Suge knight alipokuwa akiondoka baada ya kikao na Mpiganaji Davis Mosha THE CEO.
Picha na Africa Swahili Media

Hivi ndivyo Kansa ya Ngozi Ilivyomuharibu Mtoto wa Miaka 7....Baba yake aomba msaada kwa wasamaria wema (kunradhi kwa picha)

$
0
0
1
Mtoto Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.
2
“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.
“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi.

RAIS KIKWETE AAGANA NA BALOZI WA VIETNAM NCHINI

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Balozi wa Vietnam aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mhe Nguyen Duy Thien baada ya kuagana naye Ikulu jijini Dar es salaam jana.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga Balozi wa Vietnam aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mhe Nguyen Duy Thien  Ikulu jijini Dar es salaam jana. PICHA NA IKULU.

DK. SLAA AFUNGUA KONGAMANO LA UCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA JIJINI DAR

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa akifungua kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Chama cha Convervative cha Denmark, Rolf Aagaaro-Svenevosen na Katibu Mkuu wa chama wa vijana wa chama hicho, Nicholas Jansen.
 Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakinunua skafu, kofia za chama hicho wakati wa kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa akisalimiana na Katibu Mkuu wa chama hicho mrengo wa Vijana, wakati wa kongamano la Uchumi na Ajira kwa Vijana wa Tanzania lililofanyika leo katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Vijana wsakiwa katika kongamano hilo.
Katibu wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Deogratius Munishi akisisitiza jambo.

Mh. Gregory Teu aipongeza APRM kwa kusambaza nakala za Katiba

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu ameupongeza Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) kwa kugawa nakala za rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa Wananchi.

Naibu Waziri aliyasema hayo mara baada ya kutembelea banda la APRM kwenye maonesho yanayoendelea ya Nane Nane mjini Dodoma. Akizungumza mara baada ya kupatiwa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi za Wizara ya Mambo ya Nje zinazoshiriki Maonesho hayo za APRM Tanzania na AICC Arusha, Waziri huyo aliguswa baada ya kupatiwa nakala hiyo.

"Ni kazi nzui mnayoifanya hapa kama mnasaidia kugawa nakala hizi ili wananchi waweze kusoma na kufahamu kilichomo," alisema Naibu Waziri Teu.

Tangu yalipoanza maonesho hayo APRM Tanzania imekuwa ikigawa bure rasimu za Katiba kwa lengo la kuwapatia wananchi wengi fursa ya kusoma na kufahamu kilichomo katika rasimu hiyo ya kwa kwanza.

Akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Teu, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa APRM Tanzania, Bw. Hassan Abbas alisema APRM ilipokea nakala za kutosha kutoka Tume ya Marekebisho ya Katiba na imekuwa ikisaidia juhudi za Tume kuisambaza rasimu hiyo kwa wadau mbalimbali wa masuala ya utawala bora.

"Wananchi wengi waliofika hapa wamefurahi kupata nakala za rasimu. Wengi wamekiri kuwa hawakuwahi kuisoma au hata kufikiria kuwa ipo siku moja wataisoma nakala hiyo ya kwanza," alisema Bw. Abbas.

Kutokana na umuhimu wa rasimu na masuala ya Katiba Naibu Waziri Teu aliishauri APRM kutenga dawati maalum ili kuwaelimisha zaidi wananchi kuhusu Rasimu hiyo na masuala ya Katiba.

Nao wananchi mbalimbali waliohudhuria na kupata nakala hizo wameeleza kufurahishwa kwao na uamuzi wa Serikali kuruhusu maoni juu ya Katiba mpya. "Sjawahi katika maisha yangu kushiriki zoezi muhimu kama hili," alisema mkazi wa Dodoma aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Augustine na kuongeza.

"Serikali ihakikishe basi wananchi wote wanapata hii katiba mpya itakapokamilika kuliko ilivyokuwa kwa ile ya zamani (ya sasa) ambayo mimi hadi sasa sijabahatika kuiona."

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA SHINDANO LA TATU LA KUHIFADHI QUR'AN TUKUFU JIJINI DAR

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Sh. milioni 2, mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Juzuu 30, Abdulkarim Khamis, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa  washindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013. 
  Mtoto Maryam Nassor (8) akisoma moja ya haya iliyo katika kitabu cha Juzuu kwa kichwa, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Sh. milioni 1.5, mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Juzuu 20, Maryam Nassor (8), wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza za waumini wa dini ya Kiislamu, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Qur'an Tukufu, iliyofanyika jana usiku Agosti 2, 2013 katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam.
  Mtoto Maryam Nassor (8) akisoma moja ya haya iliyo katika kitabu cha Juzuu kwa kichwa, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013.
 Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislamu, waliohudhuria hafla hiyo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu, wakati wa hafla ya kuwakirimu wasindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku Julai, 2, 2013. Picha na OMR-

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

$
0
0
KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA LINDI INATANGAZA NAFASI YA MRATIBU WA KLABU.

SIFA ZA WAOMBAJI:
1.     AWE MTANZANIA MWENYE UMRI USIOPUNGUA MIAKA 25
2.     AWE NA ELIMU YA KIDATO CHA NNE AU ZAIDI
3.     AWE NA UWEZO WA KUTUMIA KOMPYUTA KWA UFASAHA
4.     MWENYE UWEZO WA KUUNGANISHA WADAU NA WANAHABARI
5.    AWE NA UWEZO WA KUBUNI NA KUTAYARISHA ANDIKO LA          MRADI  

MAOMBI YATUMWE KABLA YA MWEZI JULAI 30, 2013 KWA :

MWENYEKITI  LINDI PRESS CLUB  P.O.BOX 404-LINDI  
BARUA ZA MAOMBI ZIAMBATANISHWE NA VYETI VIVULI VYA ELIMU , CV NA MAJINA NA ANUANI ZA WADHAMINI WAWILI.  

KWA MAWASILIANO ZAIDI  FIKA KWENYE OFISI ZETU ZILIZOPO JENGO LA Y2K ZAMANI NOVELTY CINEMA MAKUTANO YA BARABARA YA KARUME NA ELIET MJINI LINDI AU PIGA SIMU NAMBA:0787176221  AU  0754052060  

Kuitwa Kwenye Usaili Madaktari, Wauguzi, Wakaguzi Wa Ndani, Maafisa Ugavi n.k

Simba yatoa sare ya 1-1 na Polisi Kombaini

$
0
0
 Mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki akimtoka mchezaji wa Polisi Kombaini, Magige Machango katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa  Polisi Kombaini, Admin Bantu akimtoka mshambuliaji wa  Simba, Abdulhalim Humud katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Mshambuliaji wa Simba Betram Mombeki akishangilia goli aliloifungia timu yake dhidi ya Polisi Kombaini katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
 Kikosi cha Simba
Kikosi cha Polisi Kombaini.

MAKUNDI MBALI MBALI MBALI YA VIJANA WA CCM MKOA WA MWANZA WASHIRIKI MJADALA WA KATIBA MPYA

$
0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa ufafanuzi wa CCM juu ya Rasimu ya Katiba mpya katika mkutano uliofanyika Mwanza leo na kuwakutanisha vijana wa makundi mbali mbali.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Stephen Wasira akifafanua juu ya mstakabali wa vijana katika mchakato wa Katiba mpya.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dk.Anthony Dialo akichangia mada juu ya umuhimu wa serikali mbili kwa Tanzania.
Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Mkoani Mwanza Sixbert Ruben akielezea umuhimu wa vijana wa Mwanza katika kushiriki kwa kwenye mchakato wa Katiba mpya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Martin Shigela akifafanua juu ya umuhimu wa vijana katika suala la  Katiba mpya
Sehemu ya Vijana walioshiriki katika  mjadala wa mchakato wa Katiba mpya uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo cha mafunzo Benki Kuu mkoani Mwanza ambapo vijana zaidi ya mia sita walihudhuria.

Nyota wa NBA Stephen Curry aendesha Clinic ya kikapu na kugawa vyandarua Jijini dar

$
0
0
Viongozi wa juu wa TBF Magesa, Maluwe na Msoffe wakiwa na NBA stars Stephen Curry na Hasheem Thabeet mara baada ya Wachezaji hao kuendesha clinic ya kikapu kwa Vijana 100 wa chini ya miaka 18 ... Katika kampung ya Nothing but Net ambapo Curry anagawa vyandarua ili kupitia vita Malaria.... Urey alikuja nchini katika ziara iliyoratibiwa na UN Foundation, US Embassy kwa kushirikiana na TBF, clinic hiyo ilisaidiwa na Cocacola, BBall Kitaa, Redcross na wadau wengi wa kikapu wa DSM.
Makamu wa Rais wa TBF Phares Magesa akiwa na viongozi wa UN Foundation, Redcross na mafias wengine waliombatana na Stephen Curry mara baada ya kuzindua kampeni ya kugawa vyandarua ili kupitia vita malaria ..... Kila kikapu Curry anachofunga anagawa vyandarua vitatu kupitia kampeni hiyo.

TSN, TCRA, AICC, TTCL, YARA WASHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE DODOMA 2013

$
0
0
 Kikosi kazi cha Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania Standard Newspapers (TSN) Limited ambacho kipo ndani ya viwanja vya Nzuguni katika Banda la Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo katika Maonesho ya siku ya Wakulima Nane Nane yaliyoanza Agosti Mosi na kutaraji kumalizika Agosti 8, 2013 kitaifa Mkoani Dodoma. Kushoto ni Afisa Masoko, Francis Kihinga akiwa na Afisa Mauzo na Masoko, Chikira Mgheni. TSN ndio wachapishaji na wasambazaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News, HABARILEO, HABARILEO Jumapili na SpotiLEO.
 Afisa Masoko wa TSN, Francis Kahinga akigawa majarida ya Elimika na Academy kwa wanafunzi walio tembelea banda la TSN. TSN ndio wachapishaji na wasambazaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News, HABARILEO, HABARILEO Jumapili na SpotiLEO.
 Kampuni Kongwe ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) nayo ipo katika Viwanja vya Nzuguni, kuelimisha umma juu ya huduma zake. Pichani ni Maofisa wa Kampuni hiyo Thomas Lemunge ambaye ni Afisa Biashara wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (katikati) akitoa elkimu kwa mwananchi huku Afisa Habari, Amanda Luhanga akifuatilia.
Ofisa Masoko na Utafiti wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Linda Nyanda, akiwapa maelezio wanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari ya Maria de-Mathias ya mjini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali za AICC walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wakulima nane nane katika Uwanja wa Nzuguni mjini Dodoma.
Ofisa Habari Mwandamizi na Itifaki wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Catherine Kilinda akiwapa maelezio wanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari ya Maria de-Mathias ya mjini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali za AICC walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wakulima nane nane katika Uwanja wa Nzuguni mjini Dodoma.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images