Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

WAZIRI KALEMANI ASHIRIKI MAKABIDHIANO YA SOKO LA SAMAKI, UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA, CHATO

$
0
0
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani leo tarehe 14 Februari, 2018 ameshiriki makabidhiano ya Soko la Kimataifa la Samaki la Kasenda lililojengwa chini ya ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya Dola za Marekani 148,146. Aidha, Waziri Kalemani ameshiriki utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Japan na Tanzania kwa ajili ya ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilomita moja ya Muganza kwa gharama ya Dola za Marekani 90,645.
Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida (kulia) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato, Joel Hari (kushoto) mara baada ya kusaini mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Japan kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Muganza kwenye uzinduzi huo. Katikati anayeshuhudia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida akisoma hotuba katika uzinduzi huo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akisisitiza jambo katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akielezea mafanikio ya mkoa wake katika uzinduzi huo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kushoto, waliosimama mbele) Balozi wa Japan Nchini, Masaharu Yoshida ( wa n ne kushoto, waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Geita mara baada ya uzinduzi wa Soko la Kimataifa la Samaki la Kasenda.


TAASISI YA ALBINISM AWARENESS NA UBALOZI WA KUWAIT WATOA MISAADA KWA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
 Kaimu Balozi wa Kuwait nchini,  Mohamed Al-Amiri akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuikabidhi Shule ya Msingi ya Jeshi la uokovu vifaa vya walemavu wa viungo na ngozi pembeni yake mwasisi wa Jumuiya ya Albinism Awareness Foundation Suleiman Magoma, Mwalimu wa shule Bi. Flourina Milinga na Afisa elimu taaluma Mkoa Bw. Fortunatus Kagoro
 Mwasisi wa Jumuiya ya Albinism Awareness Foundation, Suleiman Magoma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea vifaa vya walemavu wa viungo na ngozi vyenye thamani ya shilingi milioni 30 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya nchi ya Kuwait,pembeni yake aliyevaa kanzu ni Kaimu Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Mohamed Al-Amiri
Kaimu Balozi wa Kuwait nchini, Mohamed Al-Amiri awakabidhi wanafunzi walemavu wa Shule ya Msingi ya Wokovu viti vya matairi,pembeni yake mwasisi wa Albinism Awareness Foundation Suleiman Magoma na Mkurugenzi qa shule Thomas Sinana.

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA BUCHOSA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la Hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Mwanza Februari 15, 2018 .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na kulia ni Mbunge wa Buchosa na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MADIWANI WA BUCHOSA WAMKATAA MKURUGENZI WAO MBELE YA WAZIRI MKUU

$
0
0
MADIWANI wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Cyprian Luanda baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Wametoa ombi hilo leo (Alhamisi, Februari 15, 2018) katika kikao cha Waziri Mkuu na watumishi Halmashauri ya Buchosa akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

Waziri Mkuu baada ya kupokea ombi hilo alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella kwenda katika halmashauri hiyo na kufanya kikao cha pamoja kati ya Madiwani, Mkurugenzi na watumishi ili kubaini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

Awali, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, ambapo ujenzi wake hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 10.55.Pia Waziri Mkuu amezindua madarasa manne ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Secondari ya Nyehunge wilayani Sengerema na kuwata wanafunzi wasome kwa bidii.

Waziri Mkuu amesema wanafunzi hao wanatakiwa wasome sana kwa sababu Rais Dkt. John Magufuli amewaondolea wazazi michango ya hovyo ili wao wapate fursa ya kusoma.

Pia amewasisitiza walimu wasijiingize katika masuala ya michango ili wajikite na masuala ya taaluma. Kama kuna michango kutoka mtu mmoja mmoja, vikundi au Taasisi yote sasa itafikishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri.
Amesema awali wanafunzi walikuwa wanatumika kama njia ya kutengeneza fedha, ambapo wazazi au walezi wanaposhindwa kutoa michango hiyo watoto wao walikuwa wanarudishwa nyumbani. Waziri Mkuu amesema kila mwezi Serikali inapeleka moja kwa moja shuleni sh. bilioni 20.8 kwa ajili ya kugharamia Elimumsingi bila malipo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, FEBRUARI 15, 2018.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Cyprian Luanda ambaye madiwani wa Halmashauri  hiyo walimwambia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  aondoke nae . 

MAGAZETI YA IJUMAA LEO FEBRUARY 16,2018

introducing Papii Kocha - Waambie (Official Video)

Rais Magufuli kuwaapisha Dkt. Slaa na Mhe. Mboweto kuwa Mabalozi


WATENDAJI WA SERIKALI,WANANCHI WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KULETA MAENDELEO

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti amewataka watendaji wa Serikali na wananchi kushirikiana katika shughuli za maendeleo katika ukusanyaji wa mapato na kufanya kazi.

Lengo ni kuboresha huduma za kijamii katika Wilaya hiyo na kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.Mwito huo aliutoa juzi katika chakula cha pamoja na wazee wa Wilaya ya Buhigwe ,Watumishi wa serikali, viongozi wa dini na chama pamoja na kuhamasisha shughuli za maendeleo.

Ambapo aliwataka kila mwananchi mmoja mmoja, kwa makundi na kwa ujumla wao kuweka mikakati ya pamoja ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu, afya, miundombinu na jinsi ya kupatikana haki za wazee.

Mkuu huyo aliwataka watendaji wa Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi wote ndani ya Wilaya kusaidia jitihada za kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato."Lengo ni kuwezesha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa mafanikio makubwa ambapo mapato hayo yatasaidia vijiji ambavyo havina zahanati vipate huduma hiyo kutokana na mapato hayo," amesema.

 MKUU wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza na Baadhi ya Watendaji wa Serikali na wananchi kushirikiana katika shughuli za maendeleo katika ukusanyaji wa mapato na kufanya kazi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TRA KUWAFUTIA LESENI MAWAKALA WA FORODHA WADANGANYIFU

$
0
0

Na Rachel Mkundai, Tunduma
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere ametishia kuwafutia leseni mawakala wa forodha wanaofanya udanganyifu katika kadhia za wateja wao wanazoziwasilisha katika ofisi za TRA pindi wanapotoa au kuingiza mizigo nchini kwani hizo ni njama za kuwepa kodi.
Bw. Kichere ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na mawakala wa forodha wanaofanya shughuli zao katika mpaka wa Tanzania na Zambia uliopo katika mji mdogo wa Tunduma mkoani Songwe akiwa katika ziara yake kutembelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
Kamishna Kichere amesema kumekuwepo na baadhi ya mawakala wa forodha ambao huwasilisha nyaraka zenye taarifa za uwongo au zinazoonesha idadi pungufu ya bidhaa zilizopo kwenye mizigo tofauti na uhalisia.
“Kusema ukweli sitawavumilia maajenti (mawakala) ambao watakuwa wanaongepea serikali, nitafuta leseni zao, tukiwakamata mnaenda kubumba bumba nyaraka zenye ankara za uwongo, nitafuta leseni” alisisitiza Kamishna mkuu wa TRA.
Hali kadhalika, Kichere amewataka mawakala wa forodha hao kushirikiana na maafisa wa TRA kwa kutoa taarifa sahihi za kadhia za wateja wao ili waweze kukadiriwa kodi stahiki wanayotakiwa kulipa na kuilipa kodi hiyo kwa hiyari kwa kuwa wote ni watanzania wanaoshirikiana kujenga taifa moja.
Nao mawakala wa forodha katika mpaka wa tunduma wameufurahia ujio wa kamishna mkuu na kuahidi kushirikiana na maafisa wa TRA kwa kuwa taasisi hiyo ni kiungo muhimu kati yao na wateja wao.

SERIKALI KULIPA FIDIA WANANCHI UJENZI WA BANDARI ZA ZIWA NYASA

$
0
0

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga shilingi milioni 358 kwa ajili ya kulipa fidia nyumba na ardhi za wananchi waishio mwambao wa Ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari za Ziwa hilo

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake aliyoifanya ya kukagua bandari za Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Manda iliyopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi bandari ya Itungi iliyopo wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya.

Katik ziara hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Msese amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania imetenga fedha hizo kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wa maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa waliojitolea maeneo yao ili kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari zilizopo ndani ya Ziwa Nyasa kuanzia bandari ya Lipingu iliyopo Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe hadi bandari ya Matema iiyopo wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka kwenye boti katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya
Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Sese (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) wakati wa ziara yake kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe. Deo Ngalawa na wa kwanza kushoto ni Katibu wa Mhe. Nditiye Mhandisi Hamza Faiswary.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeketi) akisimikwa kuwa Chifu wa kitongoji cha Ihiiga kilichopo kwenye kijiji cha Nkwimbili, kata ya Lupingu, Wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe ikiwa ishara ya pongezi kwa kiongozi wa kitaifa kufika hapo tangu mwaka 1979 katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mzee Thadei Otmari Ngalawa na aliyevaa miwani ni Diwani wa Kata ya Lupingu Mhe. Skanda Mwinuka.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nsele kilichopo kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa Mzee Kolimba akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya

MAHAKAMA YAANZA UJENZI WA MAHAKAMA TATU MKOANI GEITA

$
0
0
Na Lydia Churi-Geita.

Katika kutekeleza dhamira yake ya kuboresha huduma za Mahakama na kusogeza huduma hizo karibu zaidi na wananchi, Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imeanza rasmi ujenzi wa majengo matatu ya Mahakama katika mkoa wa Geita pamoja na wilaya zake za Bukombe na Chato.

Ujenzi wa Mahakama hizi ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2015/16 hadi 2019/2020) wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ambao ulianza kutekelezwa rasmi mwaka 2015. Miradi hii kwa pamoja inalenga kuboresha huduma na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Mahakama imeanza ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mkoa wa Geita ambalo litajumuisha pia na Mahakama ya wilaya ya Geita. Majengo mengine yanayojengwa ni ya Mahakama za wilaya za Bukombe na Chato.

Majengo haya yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita kutoka sasa na yanajengwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu na ya muda mfupi iitwayo Moladi ambapo kampuni ya Moladi Tanzania ndiyo imepewa dhamana ya kujenga majengo hayo. Jumla ya majengo ya Mahakama za Mkoa, wilaya na Mwanzo sita tayari yameshajengwa kwa kutumia teknolojia ya Moladi katika jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.
Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita na Mahakama ya Wilaya Geita likiwa katika hatua za awali za ujenzi
Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Bukombe likiwa katika hatua za awali za ujenzi wake katika mji mdogo wa Ushirombo wilayani Bukombe
Jengo la Mahakama ya wilaya ya Chato likiwa katika hatua ya Msingi. Majengo haya yote yanajengwa kwa Teknolojia ya Gharama nafuu na ya muda mfupi iitwayo Moladi na yanajengwa na Kampuni ya Moladi Tanzania. Ujenzi wake unatarajiwa kutumia muda wa miezi sita.

KWANDIKWA ATOA MAELEKEZO KWA WATENDAJI WA TBA, TEMESA NA TANROAD

ZANZIBAR YAKABIDHIWA CHETI CHA KIMATAIFA CHA UBORA WA KUTOA HUDUMA

$
0
0

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 15.02.2018

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA umekabidhiwa rasmi Cheti cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma cha kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015.

Cheti hicho cha ubora ni kielelezo cha taasisi ya ZFDA juu ya kusimamia misingi imara ya kuhakiki ubora wa huduma katika kiwango cha kimataifa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Cheti hicho Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amesema mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa vitendo wa azma ya serikali inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya hususan upatikanaji chakula, dawa na Vifaa tiba.

Amesema kunahitajika ubunifu na jitihada za makusudi za kila mfanyakazi wa ZFDA kuhakikisha Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba ni bora na salama kwa afya za wananchi.Amefahamisha kuwa mafanikio hayo yaliyopatikana yawe chachu ya kuongeza ufanisi kiutendaji ili kufikia dira iliyowekwa.

“Mkifikia dira dira hiyo itakuwa mmetekeleza kikamilifu jukumu mllopewa na Serikali la kulinda afya ya jamii.Serikali inaaamini mnao uwezo wa kuwa taasisi bora ya udhibiti Afrika na Duniani kwani hakuna kizuizi cha kufikia dira hiyo” Alisema Waziri Kombo.Aliitaka menejimenti ya ZFDA kuimarisha udhibiti wa uingizaji wa Chakula, Dawa na Vipodozi nchini kiholela ili kulinda afya za Wazanzibari.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo katikati akizungumza mara baada ya kupokea Cheti cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma cha kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015 katika hafla iliyofanyika Ofisi za ZFDA Mombasa mjini Zanzibar.

MAGAZETINI, FEBRUARI 16, 2018: TEKNOLOJIA BORA YAIPA TANZANIA TUZO TENA


LIQUI MOLY YAJIVUNIA KUWAPATIA WATANZANIA BIDHAA ZENYE UBORA

$
0
0
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Liqui Moil Tanzania, Faraja Mkinga akizungumza Mbele ya Wanahabari kuhusiana na Uzinduzi wa bidhaa zao nchini Tanzania,mapema jana jijini Dar Es Salaam.Mkinga alisema kuwa kampuni yao inajisikia fahari kubwa kuwapatia Watanzania bidhaa zenye ubora wakati Taifa likijipanga kuelekea katika uchumi wa kati.

 ''Tanzania imeingia katika mapinduzi makubwa kwenye sekta ya magari na mitambo kwa kuanza kutumia Oili na vilainishi bora na halisi vya kampuni ya Liqui Moly yenye makao yake makuu nchini Ujerumani'',alisema Mkinga. 

Kuhusu kampuni hiyo, Mkinga amesema ilianzishwa mwaka 1957 nchini Ujerumani na inatengeneza bidhaa zaidi ya 4,000 ambazo zinazosambazwa katika nchi zaidi ya 130 duniani na kwa mara ya kwanza sasa zimeanza kupatikana nchini Tanzania kupitia mawakala wao.Pichani kulia ni Mtaalamu wa Mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Liqui Moly Tanzania,Nyanzige Nyabero na kushoto ni Mtaalamu kitengo cha Ufundi Harry Hartkorn.
MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya Liqui Moil Tanzania, Faraja Mkinga akiwaonesha Waandishi wa habari moja ya bidhaa yao mara baada ya kuzindua bidhaa zao mbalimbali nchini Tanzania,mapema jana jijini Dar Es Salaam.MKinga alisema kuwa “Kuna vilainishi vya magari madogo, magari ya usafirishaaji, meli, majenereta, pikipiki, ndege na mashine mbalimbali za viwandani''. 

Pia tuna mpango wa kuhakikisha tunakuwa na mawakala kwa ajili ya bidhaa zetu maeneo mbalimbali nchini Tanzania,” alisema Mkinga. Amewataja baadhi ya mawakala hao ni Jaffary Car Wash( Mikocheni), Fishcrab Auto Care (Kinondoni) , Top Gear (Kinondoni) , 0-60 (Kinondoni) na TFL Garage (Mikocheni) na wote wapo jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Mauzo na Masoko kutoka kampuni ya Liqui Moly Tanzania,Nyanzige Nyabero akizungumza mapema jana mbele ya Wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa bidhaa zao za Liqui Moly nchini Tanzania.
Baadhi ya Wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa bidhaa za kampuni hiyo ya Liqui Moly nchini Tanzania.
Baadhi ya Wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakifautilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa bidhaa za kampuni hiyo ya Liqui Moly nchini Tanzania.
Sehemu ya meza kuu wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo mara baada ya bidhaa za kampuni hiyo kuzinduliwa rasmi nchini Tanzania

PROF. MBARAWA ATOA MIEZI 9 KWA MKANDARASI NYAZA ROADS WORKS

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works kukamilisha ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 kwa kiwango cha lami ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.

Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo na kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Kisorya na kusema kuwa usanifu wa barabara na madaraja katika barabara hiyo umewasilishwa sasa ni jukumu la mkandarasi kuendelea na ujenzi kwa kasi na kwa viwango vya ubora.

“Serikali ina nia njema kwa wananchi wa wilaya ya Bunda na mkoa wa Mara sasa tunaijenga barabara hii na mwishon mwa mwaka mtaanza kunufaika nayo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo utarahisisha mawasiliano na kupunguza gharama za shughuli za usafirishaji wa samaki, mazao na abiria, uboreshaji makazi na kukuza uchumi kwa maeneo yaliyo kando ya barabara.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kisorya, wilaya ya Bunda alipokutana nao baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani humo, mkoani Mara.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Kangi Lugola, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati wa ukaguzi wa barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Bulamba-Kisorya yenye urefu wa KM 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilayani Bunda, mkoani Mara.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Makutano-Sanzate yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 54. Barabara hiyo inajengwa na wakandarasi wazawa M/S Mbutu JV.

WATENDAJI TENGENI MUDA WA KUWAHUDUMIA WANANCHI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji na wakuu wa idara mbalimbali kuhakikisha wanatenga muda na kwenda vijijini kuwahudumia wananchi.Amesema wananchi hususani waishio maeneo ya vijijini wanachangamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kupatiwa ufumbuzi na watendaji hao.

Aliyasema hayo jana (Alhamisi, Februari 15, 2018) alipozungumza kwa nyakati tofauti na watumishi na wananchi katika kata ya Nyehunge na Ibisabageni wilayani Sengerema akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza.

Alisema Serikali imedhamiria kwa dhati kuwatumikia kwa lengo la kuwaondolea kero mbalimbali zinazowakabili, hivyo hakuna sababu ya watendaji kukaa maofisini.“Watumishi wanawajibu wa kuwafuata wananchi katika maeneo yao hasa vijijini kwa sababu si kila mwananchi anauwezo wa kufuata huduma katika ofisi zenu na atakayeshindwa kufanya hivyo hatutomvumilia.”

Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali inawawezesha watumishi wake kwa kuwapatia vitendea kazi kama usafiri ili waweze kuwahudumia wananchi ipasavyo.Alisema kwa sababu ya kutotekeleza wajibu wao ipasavyo kumekuwa na kero na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hivyo kusababisha wananchi kuwasilisha kero na malalamiko hayo wakati wa ziara za viongozi wakuu.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwataka wananchi wanaofanya kazi katika kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao ya nafaka cha Doto Alex Posho Meel kuwa waaminifu.Waziri Mkuu alisema wafanyakazi hao wanatakiwa wawe waaminifu na wafanye kazi kwa bidii ili kukiwezesha kiwanda hicho kuendelea na uzalishaji.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, FEBRUARI 16, 201
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda kidogo cha Dotto Posho Mill, Bw. Alexander Dotto (kushoto) kuhusu unga na Mchele unaozalishwa na kiwanda hicho kilichopo eneo la Bukara, Sengerema Februari 15, 2018. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Miongella.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Sengerema baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kusaga nafaka na kukoboa mpunga cha Dotto Posho Mill kilichopo eneo la Bukara, Sengerema Februari 15, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Buchosa wakati alipoingia kwenye uwanja wa michezo wa Nyehunge wilayani Sengerema kuhutubia mkutano wa hadhara Februari 15, 2018.

Waziri Mwakyembe Akutana Na Wajumbe Bodi Ya Filamu,atemebela Studio Zinazoandaa Kazi Za Filamu,Muziki

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema (kulia) moja ya kompyuta mpakato kuashiria makabidhiano ya vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa kwa ajili ya kuimarisha majukumu ya Bodi ya Filamu alipofanya ziara katika ofisi za Bodi na kukutana na wajumbe wa Bodi ya Filamu jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Jasons Televisheni (JTV) Bw. Sanstus Mtsimbe (kulia) alipotembelea studio za televisheni hiyo kuangalia namna kazi za filamu zinavyoandaliwa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Bw. Silvester Sengerema
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Studio za Wanene Bw. Darsh Pandit (wapili kushoto) baada ya kuangalia baadhi ya kazi zilizoandaliwa na studio hizo wakati wa ziara yake kutembelea studio mbalimbali zinazojishughulisha na uandaaji wa kazi za filamu na muziki jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) kiandika maoni yake katika kitabu cha wageni baada ya kutemblea studio za Wanene zilizopo Mwenge wakati wa ziara yake kutembelea studio mbalimbali zinazojishughulisha na uandaaji wa kazi za filamu na muziki jana Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo na kushoto ni Mkurugenzi wa Studio za Wanene Bw. Darsh Pandit.

RAIS DKT MAGUFULI AWAAPISHA DKT WILBROD SLAA NA MUHIDIN MBOWETO KUWA MABALOZI WETU SWEDEN NA NIGERIA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Muhidin Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Wilbrod Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiashuhudia Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa wakila kiapo cha maadili ya viongozi baada ya kula kiapo kuwa mabalozi katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Mohamed aliyeungana na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama kushuhudia kuapishwa kwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Bw. Rogers Sianga pamoja na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofika kushuhudia kuapishwa kwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidin Mboweto na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam asubuhi leo Februari 16, 2018 .
PICHA NA IKULU

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images